Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 3

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

17/09/2015
BENKI YA POSTA TANZANIA (TPB) YAKAMILISHA UJENZI WA
KITUO CHA AFYA UNGI MSUKA, KONDE.
Leo, tarehe 17 Septemba 2015, Benki ya Posta Tanzania (TPB)
inakabidhi rasmi mradi wa kituo cha Afya cha Ungi, Ungi Shehia
ya Msuka Mashariki Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini
Pemba, kituo ambacho Benki hiyo imedhamini ukamilishaji wake.
Kituo hicho cha afya kinatarajiwa kusaidia wananchi takriban elfu
tano wanaoishi kijijini hapo, ambao wamekuwa wakitembea
mwendo mrefu kuzifuata huduma hizo kwenye vijiji vya jirani.
Akiongea kwenye makabidhiano ya Kituo hicho Afisa Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba Moshingi alisema
benki yake inadhamiria kuendelea kuisaidia jamii kuondokana na
changamoto mbalimbali za kijamii, hususan huduma ya afya kwa
mama na mtoto.
Mara baada ya kupata maombi ya kumalizia ujenzi wa kituo hiki
cha Ungi kutoka Jumuiya ya Maendeleo Jimbo la Konde, tulichukua

uamuzi wa haraka wa kusaidia, kwa kuelewa umuhimu wa afya


kwa wananchi. Juhudi zetu hizi hazitaishia hapa, tunaahidi
kuendelea

kushirikiana

nanyi ili kuhakikisha kuwa huduma

zinazotolewa hapa zinawanufaisha wananchi wote kwa ajumla,


alisema Moshingi.
Akizindua jengo hili, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamo wa
Kwanza wa Raisi Mhe. Mohammed Aboud Mohammed aliishukuru
Benki ya Posta kwa msaada huo na kuipongeza kwa kuijali jamii.
Alisema kuwa taasisi zote zinazotoa huduma ni muhimu zitambue
kuwa

bila

wananchi

huduma

wanazozitoa

haziwezi

kuwa

endelevu, hivyo akazitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa Benki


ya Posta ya kuwajali wananchi wanaotumia huduma zao. Pia
aliwasihi wanakijiji wa Msuka kukitumia vizuri kituo hicho kwa
kukitunza.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Maendeleo Jimbo la Konde ambao
ndio watekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ungi
ndugu Ismail.. Aliishukuru TPB kwa msaada huo mkubwa
walioutoa na kuahidi kuwa watatumia na kutunza kituo hicho cha

afya ambacho wanaamini kitakuwa mkombozi kwa wananchi wa


Kijiji hicho cha Msuka na maeneo jirani.

You might also like