Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

TANZANIA TUNA MIGODI YA THAMANI KULIKO DHAHABU NA GESI

SEHEMU YA KWANZA
Unapoutazama ulimwengu kiuchumi, unagawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni
nchi tajiri, nchi za kipato cha kati na nchi za kipato cha chini (high-income, middleincome and low-income countries). Ninapenda kutumia vigezo vya kipato kutofautisha
makundi haya kuliko kile cha "nchi maskini na nchi tajiri" kwa kuwa sio kweli kwamba nchi zote
zenye kipato cha chini ni maskini na zote zenye kipato cha juu ni tajiri. Utajiri na umaskini wa
nchi ni zaidi ya kuzalisha mali zinazohesabika kama mapato. Huu ni msimamo wangu na sio
lazima ukubaliane na kanuni na tafsi za wachumi wabobezi au wanasiasa. Nyingi ya nchi
zinazoitwa tajiri, zimepata utajiri huo kwa kupora mali kutoka nchi zinazoitwa maskini kwa hila
na ujanjaujanja wa aina nyingi wanaoulinda na mifumo na kisheria zinazoitwa za kimataifa.
Mara nyingine, wanalazimisha nchi zenye rasilimali zijitungie na kujiwekea sheria mbovu
zinazawapa wao uhalali wa kuja kupora huku mukiwatazama na kuwapigia makofi kwa jina la
uwekezaji.

Tofauti kubwa kati ya nchi za kipato cha juu na zile za kipato cha chini inaweza kutazamwa
zaidi katika tofauti ta maendeleo ya kiviwanda na tafiti za sayansi na kiteknolojia (elimu). Nchi
tajiri zimepiga hatua kubwa katika tafiti za kisayansi na hivyo kuwa na maendeleo makubwa ya
kiteknologia na viwanda na kupelekea kuwa wazalishaji wa bidhaa nyingi, ambazo mwisho wa
siku, soko lake kubwa ni nchi zisizo na uwezo huo (za pato dogo). Siyo hivyo tu, bali
maendeleo haya ya kisayansi na teknolojia yamewafanya kupiga hatu kubwa ya ujenzi wa
miundombinu ya kila aina yenye kuboresha hali za maisha ya watu wao, kujitafutia kipato,
pamoja na uhakika na ubora wa huduma za kijamii (afya, elimu, maji, nishati, usafiri, nk).
Wataalam wa
kiuchumi
wanatushauri
kwamba, ili nchi iweze kuendelea, pamoja na
mambo mengine ni lazima iweze kuwa na
viwanda angalau vidogo na vya kiwango cha
kati ambavyo vitaweza kubadilisha malighafi
zinazopatikana katika nchi husika kuwa
bidhaa zinazotumika. Mfano mzuri ni
viwanda vinavyoweza kusindika vyakula na
vinywaji vya matunda; kutengeneza mavazi
kutokana na pamba; kutengeneza viatu na

bidhaa zitokanazo na ngozi, nk. Historia ya


uchumi wa dunia hasa ndani ya miaka 30
iliyopita imjenga tofauti kubwa sana kati ya
nchi za kipato cha juu na cha chini na
kuzifanya nchi za kundi la pili kuwa na wakati
mgumu sana wa kuendelea kiviwanda kama
njia kuu ya kupiga hatua za maendeleo.
Kuna maelezo mengi ya kwa nini hali hii
imekuwepo lakini ushahidi ni mkubwa
kwamba nchi zilizoendelea kiviwanda na

teknologia zimekua sababu kubwa ya


kuzifanya nchi maskini kushindwa kupiga
hatua. Kuna mifumo mingi ya kifedha,
kiuchumi, kibiashara, uwekezaji na kisiasa
ambayo imezifanya nchi maskini zisisogee
na hivyo kuendelea kuwa wanyonge mbele
ya nchi tajiri. Naomba nisiingie ndani sana
katika hili maana kuna maelezo mengi,
magumu na sababu zingine zinaleta
maumivu ya kihisia.

Mifumo hii ya uchumi unaondeshwa na kuamuliwa na nchi tajiri ni mgumu sana kuuvunja au
kuupindua kwani waliouweka wamejenda misingi mikubwa sana yenye nguvu katika kila
nyanja ya maisha. Kwa mfano, nchi zenye nguvu ya kiuchumi, zimeingiza baadhi ya dhana na
kuzifanya kuwa vigezo vya kimataifa (international standards) ambazo nchi maskini ikivikeuka
zinajikuta katika hali ngumu. Mojawapo ya vigezo hivyo ni msisitizo wa misingi ya kiutawala wa
kidemokrasia; zinazoitwa haki za binadamu; mahusiano ya kibiashara; na mengine.
Kinachoumiza zaidi ni ukweli kwamba, vigezo hivi vyote vinaungwa na wenye uwezo kwa
kuzingatia maslahi yao na kisha nchi maskini zinalazimishwa kuzikumbatia na kuzilinda
kisheria bila kujali misingi na tamadunia zao ambazo zinatofautina na anaowaletea taratibu
hizo. Mambo haya yameiweka nchi maskini katika wakati mgumu na kujikuta zimejiingiza
kwenye mikataba mibaya na mahusiano mabovu ya kibiashara. Haya yamepelekea kuendelea
kuua uwezo wao wa kujitegemea na wakati huohuo kushuhudia utajiri na rasimaliza za nchi
zao kuchotwa na kuwaacha wakiwa hawana chochote cha kuwanufaisha kwa muda mrefu.
Tanzania inahusika sana katika hili na mifano ni mingi ya jinsi tulivyoumizwa na
tunavyoendelea kuumizwa na mifumo hii.
Tufanyaje?
Serikali yoyote makini inayoangalia hali ya kiuchumi ya wananchi wake na taifa kwa ujumla na
kuwa wakweli bila uyeyushaji wa kisiasa, ni lazima ikubali ukweli kwamba hawawezi
kufurukuta kirahisi katika mazingira haya na ni lazima wajiuli ze swali la pili: tunafanyaje? Je,
tuna mbadala?
Ili kutoendelea kuwa wahanga wa mifumo kandamizi ya uchumi wa kidunia inayozinyima nchi
maskini kuendelea, ni lazima zirudi kwenye msingi (drawing board) na kuangalia ubunifu
mbadala wa kujikwamua kwenye umaskini. Hili ni lazima lifanyike kwa umakini mkubwa sana
ili kuona ni maeneo gani kika mazingira yetu twaweza kuyatumia kujikwamua na kubadili hali
za maisha yetu bila kuhitaji msaada wa mtu au nchi nyingine. Sio hivyo tu, bali tuweze kufanya
hivyo huku tukiwapa wanyonyaji nafasi ndogo sana ya kutuingilia na tutumie rasilimali zetu
tulizonazo ikiwa ni pamoja na wataalamu wetu tuliowandaa sisi wenyewe. Tukiweza hilo,
tutakua na uwezo hata wa kujenga mahusiano sahihi na nchi zingine yenye usawa katika aina
ya ushirika tunaojenga kuliko huu wa sasa.
Nchi makini zilizopitia mazingira haya ya uonevu wa kiuchumi, zimetumia njia hizi na
zinafanikiwa sana. Miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na China, India, Korea ya Kusini na
Brazili. Kwa mfano, kwa kutambua umuhimu wa ushindani wa kimataifa na kujiandaa vuma
kupambana na washindani (maadui!!) wa kiuchumi, China inapeleka raia wake zaidi ya milioni

ishirini (20,000,000) kila mwaka kusoma kingereza nje ya nchi yao. Sio hivyo tu, ukienda vyuo
vikuu vya nchi za Ulaya zinzosifika kwa elimu bora, utashangaa na wingi wa wanafunzi wa
shahada za uzamili na uzamivu toka chini za Asia na hasa China. Nimeshuhudia baadhi ya
programu za uzamivu (hasa biashara na uhandisi) kwenye baadhi ya vyuo, vikiwa havina hata
mwanafunzi mmoja wa nchi husika na badala yake ina mamia ya wanafunzi toka China. Vijana
hawa wanapomaliza, hawatafuti kuzamia kubaki ulaya, bali wanarudi kwenye nchi zao
kupeleka ujuzi huu na kushindana kikamilifu.

Nchi ya Korea Kusini ambao uchumi wao unatisha kwa kutegemea viwanda hasa eneo la vifaa
vya kielkroniki, kila mwaka linapeleka mami ya vijana kufanya shahada za uzamivu (PhD)
katika vyuo bora kabisa duniani Marekani na Ulaya. Vijana hawa wanasomeshwa kwenye
vyuo hivi kwa gharama kubwa ya serikali zao kwa lengo la kupeleka ujuzi sahihi wa ushindani
kujenga nchi yao.
Nchi ya India, pamoja na maeneo mengi ya
uazalishaji yakiongozwa na kilimo cha
kisasa, imewekeza katika biashara ya tiba
(medical
tourism)
kwa
kuhakikisha
imesomesha wataalamu bora; kutengeneza
madawa; kujenga hospitali za kisasa; na
kutengeneza vifaa bora vya tiba. Ndio
maana imekua kimbilio la tiba na inavuna
mabilioni ya fedha toka karibu nchi zote za
kiafrika kwa idadi kubwa ya wagonjwa
wanaopelekwa kupata tiba kila mwaka.
Huduma hii sio tu kwamba imeipa India
umaarufu na kuongeza kipato cha moja
kwa moja, bali imetengeza wingi wa ajira na
mapato yatokanayo na huduma zingine
zitakazohitajika na watu wanaofuata tiba.
Nchi zingine zinazoona mbali kama vile

Omani na Dubai, zimeanza kuwekeza


kwenye eneo hili la tiba pamoja na kwamba
wanafanya vizuri sana kwenye maeneo
mengi ya uzalishaji. Wamegundua kwamba
katika dunia ya kisasa, tiba sio huduma tu
bali ni biashara na uwekezaji unaolipa kwa
uhakika.

Sina haja ya kueleza ni kwa jinsi gani Brazil wametumia mpira wa miguu (football) kama
uwekezaji usiohitaji mtaalamu wala msaada toka nje na ni kwa jinsi gani umpira
umeitambulisha nchi hii katika uso wa dunia na kuwa ajira ya muhim na njia ya mapato kwa
wengi. Mifano ni mingi ya jinsi nchi zinazoibukia zinafanya hivyo kwa ubunifu unaokwepa
utegemezi wa nchi tajiri na kutumia ubunifu wao. Hata hivyo ngoja nijirudi kwa ninachotaka
kusema kuhusu nchi yangu pendwa ya Tanzania.
Tuanzie wapi?
Serikali yetu kwa muda mrefu sasa imekua na mipango na mikakati mingi ya kujikwamua
kwenye umaskini na kuijengea nchi uwezo wa kujitegemea. Mipango na mikakati hii ni mizuri
tu na inaonesha nia njema kabisa ndani ya mioyo na mawazo ya waliyoiandaa. Hata hivyo
tukubali kwamba mingi ya mikakati hii haijaleta matokeo tarajiwa. Kuna ambayo imekufa kabla
ya utekelezaji wake; kuna ambayo imekua ni mifuko iliyotoboka ya kupoteza mabilioni ya
fedha; kuna ambayo inasonga kwa kujikangoja; na kuna michache inaleta mafanikio
yanayotia moyo. Nisingependa kuwa msemaji wa serikali katika makala hii kuelezea ni miradi
na mikakati ipi imefanikiwa au imesindwa kuleta mafaniko. Sina ujasiri wa kufanya hivyo kwa
sasa hasa ukizingatia ni kipindi cha kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu.
Pamoja na mikakati iliyoko, ambayo mingi inaendeshwa na nchi tajiri kwa namna mbalimbali
(inategemea ufadhili wao; tau tunaiga wanachofanya wao; au unategemea ushauri na
utaalamu wao; au wanatulazimisha kuitekeleza kwa malengo yao); ninaamini kuna vitu
hatujavitazama kama rasilimali na kama tumefanya hivyo hatujavuka toka kwenye mtazamo
kwenda kwenye vitendo. Katika makala hii, nataka nizungumzie maeneo matatu au manne
ambayo ninashawishika tuna uwezo mkubwa sana wa kuyafanyia kazi, kuyaendeleza na
kuyatumia kuboresha hali ya maishayetu. Makuzi na uzoefu niliopitia umenifundisha
kutodharau mambo madogo na kutotamani mambo makubwa wakati madogo yamenishinda
au sijafanikiwa kuyatekeleza. Kwa minajili hi yo, naamini katika dhana ya kukua, kuendelea na
kufanikiwa hatua kwa hatua ili kuwa na maendeleo endelevu kwa mtu binafsi, jumuiya ya
watu, na taifa pia. Historia ya watu na nchi nyingi zilizofanikiwa zinaonesha na kulithibitisha
hilo. Siamini sana katika mafanikio ya kushtukiza, kusaidiwa, kuoteshwa, au ya miujiza isiyo
na maelezo maana yana madhara yake. Hivyo ninataka nizungumzie maeneo matatu ambayo
kwa udogo wake yanaweza kubadili mwelekeo wa baadhi ya mambo na kuleta maendeleo ya
kichumi ya mtu mmoja mmoja na taifa, na kulijengea taifa letu sifa za kipekee kama zile
tunazozifuata kwenye nchi nyingine.
Maeneo hayo sio mageni na nitakua muongo nikisema naleta uvumbuzi au ugunduzi mpya.
Ninachotaka kufanya ni kuyaelezea katika mtazamo unaweza kumfanya angalau mtu mmoja
kuyatazama kiuchumi/uzalishaji-mali, badala ya kuyatazama tu kwa mazoea kama huduma za
kijamii. Sababu ya kufanya hivyo unajengwa katika msingi wa kwamba nchi yetu iko katika
mazingira yenye fursa za kipekee (strategic position and opportunities) ukilinganisha na nchi
nyingi zinazotuzunguka. Hivyo, tunaweza kutumia fursa hizo kujijenga sisi wenyewe na
kuwafanya wengine watuone kama kimbilio lao kwenye baadhi ya mambo hivyo kutuletea
mapato kwa watachokifuata kwetu.
Endelea kunisoma kwenye makala itakayofuata.
Mwalimu MM ni mhadhiri katika kitengo cha Sayansi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na mtafiti wa mifumo ya TEHAMA katika Huduma za afya (Health Informatics). Unaweza
kuwasiliana naye kupitia mmmwalimu@gmail.com

You might also like