Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 2

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
ikulucommpress@googlemail.co
m
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENTS OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA
ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amewateua wakuu wa wilaya wapya 13 na kuwahamisha vituo vya kazi
wengine saba.
Wakuu wa wilaya 13 walioteuliwa ni Shaaban Athuman Ntanambe ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mkoa wa Kagera; Thabisa Mwalapwa ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara; Richard Kasesera ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Ruth Msafiri ambaye anakuwa
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma na Abdallah Njwayo ambaye anakuwa
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Wakuu wa Wilaya wengine wapya ni Asumpta Mshama ambaye anakuwa Mkuu
wa Wilaya ya Wangingombe, Mkoa wa Njombe; Mohammed Mussa Utaly ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma; Dauda Yasin ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe; Honorata Chitanda ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera; Vita Kawawa ambaye anakuwa
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga na Christopher Ngubyagai ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida.
Wakuu wengine wapya ni Hawa Nghumbi ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya
ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga na Mrisho Gambo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya
ya Uvinza, Mkoa wa Kigoma.
Wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili Nkurlu ambaye
anatoka Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda Wilaya ya Arusha, Mkoa wa Arusha;

Wilson E Nkambaku ambaye anahamishiwa Arumeru, Mkoa wa Arusha kutoka


Kishapu, Mkoa wa Shinyanga; Francis Miti ambaye anahama Wilaya ya Hanang, Mkoa
wa Manyara kwenda Monduli, Mkoa wa Arusha na Jowika Kasunga ambaye anahamia
Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa kutoka Monduli .
Wengine waliohamishwa ni Muhingo Rweyemamu kutoka Wilaya ya Makete,
Mkoa wa Njombe kwenda Wilaya ya Morogoro; Hadija Nyembo ambaye anahamia
Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Tabora kutoka Uvinza, Mkoa wa Kigoma na Benson
Mpyesya ambaye anahamia Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma kutoka Kahama.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
04 Oktoba, 2015

You might also like