Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

TAARIFA KWA WATEJA

NA UMMA KWA UJUMLA

Tunapenda kuwataarifu wateja na umma kwa ujumla kuwa matawi yetu yatafungwa siku ya
Jumatano tarehe 09 Desemba 2015 kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Uhuru.
Pia tunafuraha kuwataarifu kuwa matawi yetu yote yanayofanya kazi siku za Jumapili na sikukuu,
yataendelea kufanya kazi siku ya tarehe 09 Desemba 2015,
matawi hayo ni:

NMB Wami
NMB Tandika
NMB Tegeta
NMB Kenyatta
NMB Kariakoo

NMB Mwanjelwa
NMB Mlimani City
NMB Arusha Market
NMB Nelson Mandela
NMB Ifakara

Matawi haya yatafunguliwa kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 8:00 Mchana isipokuwa tawi la
NMB Mlimani City ambalo litafunguliwa kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 10:00 Jioni.
Ili kuhakikisha kuwa tunaendelea kukupatia huduma bora katika siku ambayo matawi yetu yote
yatafungwa, njia mbadala za kutoa huduma kwa wateja kama ATM, NMB Mobile, Internet Banking
n.k zitaendelea kufanya kazi kama kawaida kwa saa 24.
Kituo chetu cha huduma kwa wateja kitakuwa wazi kuanzia saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00
usiku. Hivyo unaweza kuwasiliana nasi kwa kupiga simu ya bure kupitia namba 0800 11 22 33 kwa
msaada zaidi.
Imetolewa na Menejimenti ya NMB
Vigezo na masharti kuzingatiwa.

You might also like