Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

UTARATIBU UNAOTUMIKA KUTOA VIBALI VYA UJENZI WA MAJENGO :1.

KIBALI CHA UJENZI


Kulingana na Sheria ya Serikali za Mitaa Na. 8 ya mwaka 1982.
Sheria ya Mipango Miji na Majengo Mijini si ruhusa kwa mtu yeyote
kujenga au kuanza kujenga jengo bila :i.
ii.
iii.
iv.

2.

Kutuma maombi kwa mamlaka ya Mji kwa kupata ridhaa ya awali


(Planning Consent)
Majengo makubwa kuwe na ramani (Outline scheme designs)
Kuwasilisha michoro ya jengo na kumbukumbu husika za kiwanja.
Kupata kibali kwa maandishi kinachoitwa Kibali cha Ujenzi.

KIBALI CHA AWALI


(Planning Consent);
Inashauriwa kupata kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi.
Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (Outline plan) kwa
utaratibu unaotakiwa ukionyesha aina ya ujenzi atakaokusudia kufanya ili
aweze kupata ridhaa ya kuendelea na hatua za kuandaa michoro ya mwisho.
FAIDA:
Kuokoa muda na gharama, iwapo michoro ya mwisho itaonekana kuwa na
dosari za kitaalam ambazo zitahitaji kufanyiwa marekebisho.
Kuwa na uhakika kuhusu mahitaji muhimu ya kuzingatiwa wakati
michoro inaandaliwa.

3.

JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA UJENZI


Baada ya michoro kukamilika, iwasilishwe ikiwa kwenye majadala kwa
namna ambayo inaweza kufunguliwa na kusomeka. Michoro hiyo iwasilishwe
kama ifuatavyo:

4.

Seti tatu za michoro ya jengo (Architectural drawings)


Seti mbili za michoro ya vyuma) structural drawings) kwa majengo ya
ghorofa.

MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI


Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:

Jengo litakavyokuwa (Plan) Sections, elevations, Foundation and roof


Plan).
Namba ya eneo la kiwanja kilipo,Jina la Kampuni na anwani ya
Kampuni iliosanifu jengo husika.
Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
1

Ujazo wa kiwanja (Plot coverage)


Uwiano(Plot ratio)
Urefu wa jengo (height)
Matumizi yanayokusudiwa Idadi ya maegesho yatakayokuwepo
Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks) na
Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo. Barabara inayopitia
mbele ya kiwanja na mshale unaoonyesha Kaskazini.

5.

VIAMBATANISHO

6.

Fomu moja ya maombi iliyojazwa kwa usahihi.


Hati ya kumiliki kiwanja au barua ya toleo au leseni ya Makazi
Kumbukumbu nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo,
makabidhiano n.k.
Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo
Mabadiliko ya matumizi ya ardhi.

HATUA ZINAZOFUATWA KATIKA KUSHUGHULIKIA MAOMBI YA KIBALI


Zifuatazo ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuchunguza michoro hiyo:
Kuwasilisha michoro na kulipa gharama za uchunguzi(scrutiny fee).

Uhakiki wa miliki

Kukaguliwa usanifu wa michoro

Kukaguliwa kiwanja kinachokusudiwa kuendelezwa

Uchunguzi wa upimaji kiwanja

Uchunguzi wa matumizi ya jengo na uwiano

Uchunguzi wa Maafisa Afya

Uchunguzi wa Mipango ya uondoaji majitaka

Uchunguzi wa tahadhali za moto

Uchunguzi wa athari za mazingira (EIA)

Uchunguzi wa uimara wa jengo (Structural Drawings)

Kuandaliwa kwa maombi yaliokamilisha taratibu hizi na kupelekwa


kwenye Kamati ya Ujenzi ambayo wajumbe wake ni Madiwani

Hatimaye kuandika na kutoa kibali

7.

FAIDA ZA KUJENGA NYUMBA IKIWA NA KIBALI CHA UJENZI


Kuishi kwenye nyumba ambayo imethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama

Kuwa na mazingira bora kwa kuwa na mji ulipangwa

Kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kutokea iwapo ujenzi


umefanyika bila kibali kiwa ni pamoja na kushitakiwa mahakakani,
kuvunjiwa na kulipa gharama za uvunjaji.

You might also like