Professional Documents
Culture Documents
Maelezo Tabloid
Maelezo Tabloid
NCHI YETU
TANZANIA
Wasiliana nasi kwa Na:0222110585 au Tembelea Blog yetu kwa anuani: www.tanzaniangovernment.blogspot.com
Tanzania
Kunufaika
na Mradi
wa Bomba
la Mafuta
KUONGEZA MAPATO
UK.4
Na Daudi Manongi
humo.
Inaendelea UK.3
.7
UK
Inaendelea UK.2
Hatimaye Serikali
kuhamia Dodoma
Inatoka Uk.1
HAPA KAZI TU
na upatikanaji wa dawa na
vifaa tiba kwa wakati na
kwa gharama nafuu, hivyo
nawaomba mlitumie duka
hili, alisema Majaliwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa MSD,
Laurean Bwanakunu
anasema kuanzishwa kwa
duka hilo kutaongeza upatikanaji wa dawa na vifaa
tiba kwa gharama nafuu
, hivyo kuondoa usumbufu kwa wagonjwa wa
kwenda kuzitafuta katika
maeneo ya mbali na kwa
bei kubwa.
Nitoe mfano wa tofauti
wa bei za dawa kati ya
maduka yetu na mengine,
dawa ya sindano ya diclofenac tunauza sh. 250
huku mitaani ni sh. 1,000
hadi 1,500 , ampliclox
dozi moja MSD sh. 1,500
mtaani sh. 3,500 na Ciprofloxacin MSD sh. 100
na mtaani sh. 500 hadi
1,000, anasema Bwanakunu.
Mkurugenzi huyo anasema lengo la maduka hayo
si kuuza dawa reja reja,
nia yao ni kuziuzia hospi
tali, vituo vya afya na Zahanati ili wagonjwa wanapokwenda huko kupatiwa
huduma wapate dawa kwa
wakati.
Duka hilo ni la sita kufunguliwa tangu Mhe.
Rais Dkt. John Magufuli
alipotoa agizo kwa MSD
kufungua duka la dawa
ndani ya Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, ambapo mengine yako katika
mikoa ya Mwanza (Sekou
Toure), Arusha (Mount
Meru), Mbeya (karibu
na hospitali ya mkoa) na
Geita (Hospitali ya Wilaya
ya Chato).
Bohari ya Dawa ndiyo
taasisi pekee inayonunua,
kutunza na kusambaza
dawa na vifaa tiba vya
Serikali. MSD inazo kanda
za Mbeya, Iringa, Moshi,
Dodoma, Mtwara, Tabora,
Mwanza na Dar es Salaam. Pia ina vituo viwili
vya mauzo vya Muleba na
Tanga.
Tanzania
Kunufaika
na Mradi
wa Bomba la
Mafuta
HAPA KAZI TU
Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Edwin Ngonyani
alisema kuwa ndege hizo ambazo zinatarajiwa kununuliwa
zitatumia anga la Tanzania
ambapo hivi sasa anga hilo
linatumiwa na ndege zinazotoka nje ya Afrika, hivyo
upatikanaji wa ndege hizo
utasaidia kutoa fursa kutua
kwenye anga za nchi jirani.
Muda si mrefu tutapata
ndege mbili mpya, mwakani
tutaongeza nyingine mbili,
Serikali imejipanga kufufua
Shirika la Ndege na kubadilisha mfumo wa uendeshaji ili
liweze kujiendesha lenyewe
alisema Mhandisi Ngonyani.
Kwa mujibu wa Msemaji wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, (Mawasiliano) William Budoya ,
amesema kuwa msukumo
wa kununua ndege hizo ni
jambo la muda mrefu kuanzia
Serikali ya Awamu wa Nne
2005-2015,na katika kuendeleza utekelezaji wa juhudi hizo
Serikali ya Awamu ya Tano
imetoa msisitizo na kulipa
kipaumbele suala hilo.
Aidha, Afisa Mawasiliano
huyo amesema kuwa ndege
zitakazonunuliwa ni aina ya
Bombadier kutoka kampuni
ya Bombadier Inc ya nchini
Canada.
Serikali ilichagua kampuni
ya Bombadier Inc kwa sababu iliainisha mchanganuo
wa biashara ambao ulishauri
kuanza na ndege ndogo, kwa
kuangalia soko la ndani baadaye ndege zinaweza kuongezwa kwa kuangalia soko la
kimataifa.
Aliongeza kwa ndege hizo zinatarajia kufika nchini ifikapo
mwezi Septemba mwaka huu,
na kwa kuanzia zitaanza kutoa
huduma kwa safari za ndani
ya nchi.
Aidha alisema kuwa Serikali
imemteua mshauri mwelekezi
ambaye ataweka manejimenti
imara katika uendeshaji ikiwa
ni pamoja na kuajiri wafanyakazi walio na weledi na
wenye utayari wa kufanya kazi
kwufanisi.
akiongea kuhusu sababu
za kuchagua aina hiyo
ya ndege Katibu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Ndg.
Leordard Chamuriho alisema kuwa serikali ilichagua
ndege hizo kwasabu za kiuchumi,kiufanisi na uwezo
wa kumudu mazingira ya
Tanzania.
Shirika la ndege la Tanzania (ATC) lilianzishwa
mwezi Machi, 1977 chini
ya sheria ya Mashirika ya
Umma ya mwaka 1969 na
baada ya kuvunjwa kwa
lililokuwa Shirika la ndege
la Afrika Mashariki.
Katika kutekeleza sera ya
ubinafsishaji na ushirikishwaji wa sekta binafsi katika
uendeshaji wa Mashirika
ya Umma ya mwaka 2002,
Shirika la ndege la Tanzania (ATC) liliundwa upya
huku Serikali ikimiliki
asilimia 49 ya hisa zake
kwa Shirika la ndege la Afrika Kusini hatua ambayo
ilipelekea kuundwa upya
kwa kampuni ya ndege
Tanzania (ATCL).
Pamoja na kuwepo kwa
kampuni ya ndege ya
ATCL, kwa sasa kuna kampuni binafsi zinazojihusisha na huduma za usafiri
wa anga nchini na nje ya
nchi.Kampuni hizo ni Precision Air, Fastjet, Auric na
Coastal Air.
Akizungumzia mpango wa
Serikali wa kukabiliana na
changamoto ambazo zimekuwa zikiikabili kampuni
ya ATCL , Budoya alisema
kuwa mshauri mwelekezi
aliyeteuliwa na Serikali atatayarisha mpango
madhubuti wa kibiashara
utakaoifanya kampuni ya
ATCL kujiendesha kwa
faida na kuweza kuteka
soko la ndani na nje ya
nchi.
HAPA KAZI TU
HAPA KAZI TU
unge la Jamhuri ya
Muungano Tanzania
lilipitisha Muswada wa
Marekebisho ya Sheria
ya Manunuzi ya Umma
wa Mwaka 2016, ambayo
yanalenga kuziba mianya
ya rushwa, kuongeza uwazi
katika matumizi ya fedha
za umma, kuongeza kasi na
uwajibikaji.
Muswada huo umelenga
kuwa na Sheria ambayo
itahakikisha fedha za umma
zinatumika kwa usahihi
kulingana na thamani ya
bidhaa kwenye soko badala
ya kuwa kichaka na fedha
hizo kutumika kinyume na
malengo yaliyokusudiwa.
Hatua hiyo ya Bunge hilo
inafutia dhamira ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli
wakati akizindua Bunge la
11 la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania mjini Dodoma
mwezi Novemba mwaka
jana ambapo alionyesha
baadhi ya kasoro alizoziona
katika Sheria ya Manunuzi
ya mwaka 2011.
Moja ya maeneo aliyoyaona Rais Magufuli ni kuwepo na usimamizi hafifu
katika manunuzi ya umma
ambao uliruhusu mianya
ya rushwa kwa huduma
mbalimbali zilizotolewa
kwa Serikali kwa kuwa
zilikuwa hazilingani na
thamani halisi za fedha za
umma.
Kulingana na hali ya mau-
ghuli zinazogharimiwa na
fedha za umma, anapaswa
kuhakikisha asilimia 60 ya
wafanyakazi wa kampuni
yake ni Watanzania alisema Dkt. Mpango.
Aidha, marekebisho ya
Sheria hiyo yanaitaka Serikali kusimamia na kuhakikisha watumishi wa umma
ambao hawastahili kupewa
magari, watumie magari
yao binafsi, na wale ambao
wanastahili wakopeshwe
magari na Serikali na kupewa posho kidogo kwa ajili
ya mafuta na matengenezo.
Hatua hiyo itasaidia kuipunguzia gharama Serikali katika uendeshaji wa
shughuli zake za kila siku
na kujikita katika kutoa
huduma kwa wananchi
katika sekta mbalimbali.
Kwa upande wa Kamati ya
Bunge ya Bajeti, akiwasilisha maoni ya kamati hiyo,
Mwenyekiti wa Kamati,
Hawa Ghasia amesema
kuwa wajumbe wa kamati
yake wamekubaliana na
Marekebisho ya Muswada
wa Sheria ya Ununuzi wa
Umma wa mwaka 2016.
Kamati imekubaliana na
Serikali kufanya manunuzi
kwa kuzingatia thamani ya
fedha kwa bidhaa, ikiwamo manunuzi ya magari
ambapo muswada huu
unaonesha kuwa inawezekana kupunguza gharama
za Serikali kwa kufuata
thamani ya fedha alisema
Mwenyekiti huyo.
Aidha, Kamati hiyo imeis-
HAPA KAZI TU
erikali ya Awamu
ya Tano tangu iingie madarakani
mwishoni mwa mwaka
jana imechukua jitihada
mbalimabli za ujenzi na
uboreshaji wa barabara
mbalimbali katika Jiji la
Dar es Salaam ili kupunguza kero za foleni katika
Jiji hilo.
Jitihada hizo zimelenga
upanuzi , ukarabati , ujenzi
wa barabara za juu kwa juu
katika baadhi ya makutano ya Jiji la Dar es Salaam
kwa lengo la kuhakikisha
wananchi , wafanyakazi na
wasafirishaji wa ndani na
nje ya Tanzania wanafika
kwa wakati maeneo yao ya
kazi.
Katika kuonyesha kuwa
Serikali hii imekusudia
kuondoa kero hiyo katika
Jiji la Dar es Salaam, mapema mwaka huu ,Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli aliweka
jiwe la msingi la Mradi wa
Ujenzi wa barabara ya juu
(Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la
TAZARA.
Akihutubia katika tukio
inaendelea uk.7
inatoka uk.6
Muhimbili.
Vilevile tarehe 23 Novemba,
2015 aliyekuwa Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
alitembelea Hospitali hiyo ili
kuhakikisha utekelezaji wa agizo
la Rais Magufuli la kununua
vitanda na magodoro yake kwa
ajili ya wagonjwa waliokuwa
wanalala chini.
Hivi karibuni Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto, Ummy Mwalimu
alipokuwa akiwasilisha Makadirio ya mapato na matumizi kwa
mwaka wa fedha 2016/2017
amesema kuwa Serikali ina
mpango wa kuboresha hospitali
za rufaa, maalumu za kanda na
Hospital ya Taifa ya Muhimbili(MNH) ambayo kwa sasa
itaanza kutoa huduma ya kupandikiza figo.
Muhimbili itaanzisha huduma mpya ya upandikizaji figo
na upandikizaji wa cochle kwa
wagonjwa ambao ni viziwi ili
kupanua wigo wa kutoa huduma
kwa wagonjwa binafsi na viongozi wa kitaifa alisema Mwalimu.
Alibainisha kuwa maboresho
hayo kwa upande wa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili ni pamoja
na kuongeza idadi ya vitanda
vya wagonjwa wenye kuhitaji
uangalizi maalumu (ICU) kutoka
21 hadi vitanda 75.
Pia itanunua vifaa tiba vya
upasuaji na kuongeza vyumba
vya upasuaji kutoka 13 vya sasa
hadi 18 na kupanua huduma
ya kusafisha figo kwa kuongeza
vitanda kutoka 15 hadi vitanda
50 na kuanza kusafisha figo kwa
wagonjwa wenye Virusi vya
Ukimwi na Virusi vya ini.
HAPA KAZI TU
Neema watumiaji
wa reli ya kati yaja
Na Frank Shija
wa kipindi kirefu
huduma ya usafiri wa
treni kupitia Reli ya Kati
(Central Line Railway)
imekuwa msaada mkubwa
kwa wananchi wa mkoa wa
Kigoma na maeneo ya Kanda ya ziwa na nchi za jirani
zikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Historia inaonesha kuwa
Reli wa Kati kama inavyojulikana sasa ilijengwa kati
ya mwaka 1905 hadi 1914
wakati huo ikiitwa Reli
ya Tanganyika kwa kuwa
ilikuwa ikielekea Mkoani
Kigoma ambako Ziwa Tanganyika linapatikana.
Kutokana na umuhimu
wake katika kukuza uchumi
kupitia usafirishaji bidhaa
na huduma mbalimbali
ndani na nje ya Tanzania, Katika mwaka wa
fedha 2016/2017 Serikali
imeamua kuja na mpango kabambe wa kuifanyia
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangala (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mionzi cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Flora Lwakatare
kuhusu mashine mpya ya CT-Scan alipofanya ziara katika hospitali hiyo.
maboresho miundombinu ya reli hiyo ili iweze
kwenda na wakati na kasi
ya ukuaji wa uchumi wa
Tanzania.
Mpango huo unahusisha
ujenzi wa mtandao wa Reli
mpya ya Kati katika Viwango vya Kimataifa (Standard
Gauge 80) ili kuendana
kasi ya ongezeko la mizigo.
HAPA KAZI TU
Anasema hatua hiyo inawezesha kuanza kwa kazi
ya upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu
za pamoja kuanza kuanisha
mahitaji halisi ya ujenzi
wa mradi huo na kuongeza
kwamba ujenzi wake umekuja katika wakati muafaka
kwa kuwa reli iliyopo sasa
ya Kiwango cha meter
Gauge haina uwezo mkubwa wa kubeba mizigo mingi
hata baada ya kufanyiwa
ukarabati.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Ilala Mh.
Idd Azzan Madawati yaliyotolewa na Ofisi ya bunge
Na Lilian Lundo
kosefu wa madawati
kwa shule za Msingi na
Sekondari ni tatizo ambalo limekuwepo nchini kwa
takribani nusu karne ambapo
wanafunzi wengi wamekuwa
wakisoma wakiwa wamekaa
walioandikishwa mwaka
2015 ambapo jumla ya wanafunzi 1,282,100.
Ongezeko hilo la wanafunzi
lilipelekea Mhe. Rais kutoa
agizo kwa wakuu wa mikoa
aliowateua kwa kuwapa
miezi mitatu kuanzia siku
aliyowaapisha Aprili 15
inaendelea uk.9
HAPA KAZI TU
TAHARIRI
BODI YA UHARIRI
HAPA KAZI TU
HAPA KAZI TU
ais wa Jamuhuri
ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt
John Pombe Joseph Magufuli anastaili kupongezwa
kwa kuwa mstari wa mbele
kuhamasisha na kutekeleza
kwa vitendo kampeni ya
kitaifa ya usafi wa mazingira.
Kampeni hiyo inamtaka
kila mwananchi kushiriki kikamilifu kusafisha
mazingira yanayomzunguka kwa kuwa mlinzi na
mwangalizi wa mazingira
katika maeneo anayoishi,
maeneo ya Biashara, ofisi
za Taasisi, Wizara, Mashirika, vituo vya kutolea
huduma za kijamii kama
shule, hospitali, masoko na
vyanzo vya maji ili kudhibiti athari za uchafuzi wa
mazingira na magonjwa
ya milipuko.
Ili kuhakikisha kampeni hiyo inadumu
na kuwa endelevu,
Desemba 23 mwaka
2015, Serikali kupitia Naibu Waziri
wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais
Muungano na
Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina iliitangaza
na kuirasimisha Siku ya
Jumamosi ya kila mwisho
wa mwezi kuwa siku ya
usafi wa mazingira kitaifa.
Mhe. Mpina alitangaza
kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
ya viongozi na watendaji
wanaopuuza kusimamia
shughuli za usafi katika
maeneo yao pia wananchi
wanaoshindwa kutekeleza
agizo hilo katika maeneo
wanayoishi.
Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dar
es Salaam, Enezaeli Ayo
anaeleza kuwa suala la
usafi wa mazingira katika
jiji hilo limepokewa na
kupewa uzito unaostahili
kuanzia ngazi ya Mkoa,
Manispaa, Halmashauri,
vijiji, kata, mtaa hadi kaya.
Wananchi wameonyesha
ushirikiano mkubwa katika
kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi
kuanzia saa moja hadi saa
nne asubuhi ambayo sasa
imeyafanya mazingira
kuoneakana safi anasema
Ayo.
Anasema Halmashauri
aguzi
wa usafi
katika manispaa na kutoa ushauri pale
panapohitajika juu ya
masuala ya usafi kuanzia ngazi ya mtaa mpaka
wilaya.
Takwimu zinaonyesha
kuwa zaidi ya asilimia 70
ya magonjwa yanayoibuka
mara kwa mara nchini
yanahusiana na uchafuzi
wa maji na mazingira,
hivyo hali mbaya ya usafi
wa mazingira inaathiri
watu kiafya, kiuchumi na
kijamii.
Uchafu uliokithiri katika jiji la Dar es Salaa na
mikoa mingine hadi kufikia Juni 26 2016 umesababisha vifo vya watu 344
na wengine 22,185 waliugua ugonjwa huo tangu
kuripotiwa kwake nchini
Agosti 26 ,2015.
Aidha, katika Hotuba
ya Mapitio na mwelekeo
wa kazi za Serikali na
makadirio ya mapato na
matumizi ya fedha za ofisi
2016/2017, Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa aliwataka
viongozi na watendaji
wote wa Wizara, Mashirika, Taasisi za umma na
Sekta binafsi, Mikoa,
Wilaya na Halmashauri
zote nchini pamoja na
watendaji wa mitaa, kata,
vijiji, vitongoji na wakuu
wa kaya, kusimamia usafi
wa mazingira katika maeneo yao.
Napenda kuwahimiza na
kuwasihi wananchi wote
kudumisha utamaduni
na tabia nzuri ya kuhakikisha kuwa maeneo yenu
yanakuwa safi
wakati wote ili kuboresha afya zenu na kuleta
maendeleo endelevu
nchini, alisema Waziri
Mkuu.
Kwa upande wake Mkuu
wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda
amewataka wananchi wa
Mkoa wa Dar es Salaam
na mikoa mingine nchini
kujijengea utamaduni wa
kufanya usafi kila siku
ili waweze kujiepusha
na magonjwa. Alisisitiza
kuwa suala la usafi ni endelevu na wamejipamba
ipasavyo kuhakikisha jiji
la Dar es Salaam linakuwa
mfano wa kuigwa katika
suala zima la usafi.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee
na Watoto imemtunuku
Rais Dkt. John Pombe
Pombe
Joseph
Magufuli aliamua
kubadilisha
namna ya kuadhimisha Siku ya Uhuru
wa Tanzania Bara kwa
kuwataka watanzania wote
kushiriki katika kufanya
usafi ili kuondokana na
magonjwa kama kipindupindu ambayo husababishwa na uchafu.
Alisema siku hiyo itumike
kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi
(Uhuru na Kazi) katika
Taifa na kuwataka Watanzania waitumie siku hiyo
kwa kufanya usafi katika
sehemu mbalimbali kama
vile, hospitalini, maofisini, sokoni, viwandani na
usafi wa miji yao katika
kutimiza dhana ya Uhuru
na Kazi kwa vitendo.
Ni aibu kwa nchi yetu
kuendelea kuwa na
ugonjwa wa kipindupingu
katika maeneo mbalimbali wakati watanzania
wangeweza kuepukana na
ugonjwa huu kwa kujituma wenyewe kwa kufanya
usafi kwenye maeneo yao
Dkt. Magufuli.
India kuwekeza
Katika Sekta ya
Viwanda nchini
Na Immaculate Makilika
aadhi ya Mikoa na
Wilaya zimeanza kutenga maeneo
maalum kwa ajili shughuli
za uanzishwaji wa viwanda
vidogo kwa lengo la kuwaunganisha wazalishaji wadogo
wadogo ili waweze kuzalisha
bidhaa zilizo na ubora na
hatimaye wachagie katika
ujenzi wa uchumi wa nchi.
Hatua hiyo inalenga kuanzisha mitaa ya viwanda na
sehemu maalum za masoko
kwa ajili ya wajasiriamali
wadogo wakiwemo machinga na mama lishe ambapo
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji itawajibika
kutoa ushauri wa kitaalamu
utawasaidia wananchi kuunzisha viwanja hivyo.
Hadi hivi sasa, tayari Halmashauri kutoka mikoa
ya Arusha, Geita, Mbeya ,
Mwanza , Dar es Salaam na
Katavi zimetenga maeneo
kwa ajili ya kujenga mitaa ya
Viwanda vidogo vidogo kwa
ajili ya wajasiliamali wadogo
Ujenzi wa viwanda hivyo una
lengo la kuifanya Tanzania
kuwa na viwanda vitakavyoifanya iwe na uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025.
Juhudi hizo za Serikali zimechochewa na ziara ya siku
mbili ya Waziri Mkuu wa
India Mhe. Narendra Modi
ambapo nchi hizo zilisaini
mkataba wa pamoja kati ya
Shirika la Viwanda Vidogo
India (NSIC) na Shirika la
Viwanda Vidogo Tanzania
(SIDO) kwa ajili ya ushirikiano utakaowasaidia wajasiliamali wadogo na wakati.
Mkataba huo unatarajiwa
kuiwezesha SIDO kubadilishana uzoefu na NSIC, kufanya utafiti, kushauri kuhusu
miradi na sera ya uendeshaji
wa viwanda vidogo vidogo.
Hii yote ikiwa ni katika
kuanzisha vituo vya atamizi
(incubators) ambapo kupitia
atamizi hizo, wananchi watapatiwa mafunzo ya uzalishaji
wa bidhaa na mafunzo ya
biashara yatakayowawezesha
kuanzisha biashara zao za
viwanda vidogo vya uzalishaji.
Aidha, atamizi hizo zitawasaidia wabunifu kunufaika
na mafunzo na teknolojia
ya India. Mpango ambao
unadhamiria kutafuta ubia
kwenye sekta ya viwanda
inaendelea Uk.12
10
Inatoka Uk.10
Aidha, kampuni za
vidogo pamoja na uratibu wa
Shapoorji Pallonji na
maonesho ya viwanda hivyo.
Kamal Industries, zinajenKuhusu hatua ya Shirika la
ga mtambo wa kuzalisha
Viwanda Vidogo la nchini
umeme kwa kutumia gesi
India kushirikiana na SIDO,
wa MW 250 katika eneo
Rais Magufuli amesema
la Zinga, Mkoani Pwani.
itaisaidia Tanzania kufukia
Uwekezaji huo, unalenga
azma ya kuwa nchi ya uchukuzalisha umeme utakaotumi wa kati unaoongozwa na Uanzishwaji wa viwanda
mika katika eneo la viwanviwanda ifikapo mwaka 2025. hivyo hapa nchini utasaidia da la Kamal Industries na
bidhaa kama pikipiki, bajaji umeme mwingine utauzwa
Eneo jingine ambalo nchi
hizo zinakusudia kushirikiana na trekta kuzalishwa na
kwenye gridi ya Taifa na
kuuzwa kwa bei ya nafuu
katika sekta ya viwanda ni
baadaye kwenye maeneo
pamoja na kuanzisha Viwan- pamoja na kutengeza ajira mengine ya viwanda huko
kwa watanzania na Serikali Bagamoyo na kwa wanada vya kutengeneza dawa
itajipatia kodi.hapa nchini. nchi wa Mkoa wa Pwani.
za binadamu zitakazotibu
magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria, figo na kisukari. Katika sekta ya nishati,
Mahusiano yaliyopo kati
Kampuni ya Bajaj ya InViwanda vingine ni vile vya
ya Tanzania na India
dia, imeeleza nia yake ya
kutengeneza vifaa tiba viyamechukua muelekeo
kufanya uwekezaji mkub- mpya, ambapo makampuni
takavyotumika katika hoswa katika sekta ya mafuta kadhaa ya India yakitarapitali mbalimbali nchini,
nchini kwa kujenga kinu
uanzishwaji wake utasaidjiwa kuanzishwa ndani ya
cha kusafirishia mafuta,
ia kupunguza gharama ya
miaka michache ijayo amtayari kuna mawasiliano
kununua vifaa hivyo nje ya
bapo chini ya mpango huu,
nchi ambavyo vinaigharimu yanaendelea baina ya Shiri- Tanzania itakuwa kitovu
ka la Maendeleo ya Petroli cha viwanda vya India.
Serikali fedha nyingi.
Tanzania (TPDC) na KamAkizungumza, wakati wa
ziara hiyo Waziri Mkuu huyo puni ya Bajaj Group kuhusiana na uwekezaji huo.
wa India alikubali ombi la
11
HAPA KAZI TU
HAPA KAZI TU
inamungu ni kijana
aliye kuwa na bidii
sana shuleni, ndoto
yake ilikuwa awe rubani
pindi akimaliza masomo
yake ya taaluma hiyo. Kwa
bahati mbaya kwa kijana
huyo, wazazi wake walikosa ada ya kumsomesha,
hivyo akaishia darasa la
nne na ndoto yake ikaishia
hapo.
Kwa sasa ni mtoto wa
mitaani, inasikitisha, Je?
Binamangu angekuwa
anasoma kipindi hiki cha
Serikali ya Awamu ya Tano
ndoto yake ingezimika
au ingetimia! Bila shaka
ingetimia kwani Serikali
hii imeamua kutoa Elimu
ya Msingi bure.
Kati ya mambo ya
kupongezwa na kuungwa
mkono kwa Serikali hii ni
hili suala la ELIMU BURE.
Hakika Rais John Pombe
Joseph Magufuli na Serikali yake anawajali wananchi na hasa wa kipato cha
chini ambao ndio wengi.
Ni ukweli usiopingika
kuwa kutoa elimu kuanzia
awali, msingi hadi sekondari ni jambo la kushukuru
sana na litafanya vipaji
vingi watoto wanatoka
katika familia zilizo na
uwezo duni wa kipato
viweze kuibuka kwani
wazazi hawatashindwa
kuwapeleka watoto wao
shule kwa kisingizio cha
kukosa ada.
ri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), George
Simbachawene anasema kuwa serikali ilivyojipanga kugharamia
elimu ya msingi, SERIKALI inapeleka Sh
bilioni 18.77 kila mwezi
kwa ajili ya kugharimia
elimu bure kwa shule za
msingi na sekondari.
Simbachawene
anabainisha kuwa katika mpango huo, Serikali itagharimia gharama
zote za mtihani wa
kidato cha nne kwa
wanafunzi wote, tofauti
na miaka yote ambapo
wanafunzi hutozwa
gharama za mitihani.
Anasema fedha hizo
zitatolewa moja kwa
moja na Serikali kupia Baraza la Mitihani
(NECTA).
Majukumu ya Serikali
kuhusu utoaji elimu
bila malipo yameelezwa
katika waraka wa elimu
namba 6 wa mwaka
2015, Serikali itabeba
jukumu hili. Kutokana
na kuwabana mafisadi
tumeweza kupata fedha
za kutosha,anasisitiza
Simbachawene.
Kwa mujibu wa Waziri
huyo, Serikali inatoa
ruzuku ya uendeshaji
wa shule Sh 10,000 kwa
mwanafunzi wa shule
ya msingi na Sh 25,000
kwa mwanafunzi wa
sekondari kila mwaka.
Simbachawene anaongeza kuwa Serikali
itatoa fedha kwa ajili ya
fidia ya ada Sh 20,000
kwa kila mwanafunzi
wa shule ya kutwa na
Sh 70,000 kwa mwanafunzi wa sekondari kwa
mwaka.
Ama kweli Serikali ya
Awamu ya Tano imeonyesha dhamira ya
dhati ya kumkomboa
mwanachi hasa wa
kipato cha chini. Elimu
Kwanza na maendeleo
yanafuata. Hii inadhihirisha kuwa Serikali
hii imezidi kutambua
kuwa Elimu ni Ufunguo wa Maisha na ndio
maana suala la elimu
limepewa kipaumbele
na kuingizwa kwenye
mradi wa matokeo
makubwa sasa (BRN)
12
iongozi wengi wa
nchi hii walipata elimu yao ya
sekondari katika shule
ambazo ni kongwe. Shule
hizi zimechakaa kimiundombinu hivyo kuhitaji
ukarabati mkubwa.
Kwa kutambua umuhimu
na mchango wa shule hizo,
hasa za sekondari, Serikali
ya Awamu ya Tano imeamua kuzikarabati ili ziwe
na miundombinu bora kwa
ajili ya ya kuweka mazingira mazuri ya kusomea kwa
kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Ni dhahiri wanafunzi
pamoja na walimu wanahitaji mazingira mazuri
ya kujifunzia na kufundishia ili waweze kutimiza
malengo yao kulingana
na hatua mbalimbali wanazopitia kupata elimu.
Wakati wa vikao vya Bunge
la kumi na moja la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,
Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo
ya Ufundi Profesa Joyce
Ndalichako alisema moja
kati ya mkakati wa Wizara
yake ni kuzikarabati shule
kongwe nchini kutokana na
uchakavu wa miundombinu
hali inayosababisha utoaji
wa huduma ya elimu katika
shule hizo kutoridhisha
kama ilivyokuwa hapo awali.
Kauli hiyo aliirejea tena
siku ya maadhimisho ya
elimu Tanzania kwa kuweka bayana Uzinduzi wa
Mpango maalumu wa miaka
miwili unahusisha ukarabati wa shule kongwe 88 za
sekondari za serikali nchini.
Mazingira ya kufundishia
na kujifunzia yana mchango
mkubwa katika kuinua
ubora wa Elimu katika
ngazi zote kwani unamfanya
mwanafunzi na mwalimu
kuwa katika mazingira rafiki
ya kutimiza majukumu yao
13
HAPA KAZI TU
HAPA KAZI TU
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Magufuli wakiwasalimia na baadhi ya Watanzania waliojitokeza wakati
Bw. Narendra alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga
Ndugu Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini
kuelekea Nzega Mkoani Tabora
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli Rais Dkt. John Magufuli akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi
akisalimiana na Baadhi ya Wazee wakati kwenye kituo cha kulea wazee cha rasmi wa Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam
Nkaseka ambapo alitoa misaada ya Chakula, Mavazi pamoja na Vifaa vya
Malazi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Jakaya Mrisho Kik- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, Mwakilishi Mkazi
akisalimiana na Mwakilishi maalum wa Masuala ya Maji kutoka Shiri- wete akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Bi Tonia Kandiero, Waziri
ka la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Katiba ya Jamhuri ya wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
na Rais Mstaafu wa Kenya Mhe. Mwai Kibaki wakati wa Ufunguzi wa Muungano wa Tanzania na Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Daraja la Rusumo
linalounganisha nchi za Rwanda na Tanzania.
Maadhimisho ya Sita wa Wiki ya Maji ya Afrika.
14
15
anzania ni
miongoni mwa
nchi zilizobarikiwa kuwa na rasilimali
nyingi zikiwemo madini, mbuga za wanyama,
mlima Kilimanjaro,
misitu, ardhi yenye rutuba, maziwa na bahari.
Baadhi ya mazao ya
rasilimali hizo huweza
kusaidia katika shughuli
za uzalishaji kwenye
viwanda.
Kwa kutambua umuhimu
wa rasilimali
hizo, Serikali
ya Awamu ya
Tano chini ya
uongozi wa Rais
Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli imejikita
katika kufufua
sekta ya viwanda ili Tanzania
iwe miongoni mwa nchi
zenye uchumi
wa kati ifikapo
mwaka 2020.
Jitihada hizi
za Serikali ya
Awamu ya
Tano zinalenga kufanikisha kile
ambacho kiliwahi
kuwepo na kupotea
baada ya ubinafsishaji
katika miaka ya 90.
Ikumbukwe kuwa
Tanzania ilikuwa na
viwanda vingi ambavyo
vilishindwa kuzalisha na kubinafsishwa
kwa baadhi ya watu
ambao nao walishindwa kuviendeleza.
Tanzania imekuwa na
viwanda vya nguo kama
vile Mwatex, Mutex,
Kilitex, Sungura Textile,Tanganyika Packers na UFI ambavyo
baadhi yao vimebaki
kama magofu kwani
havizalishi chochote.
Rais Magufuli ameonyesha kutofurahishwa
na hali ya nchi kuwa na
rasilimali nyingi lakini
hazitumiki ipasavyo
kuchangia uchumi
wa Taifa hasa kupitia
viwanda akitolea mfano wa uwepo Bahari
ya Hindi toka Tanga
hadi Mtwara lakini
hakuna hata kiwanda
kimoja cha samaki.
Hali hii ndio inaleta
NSSF wamekusudia
kujenga kiwanda cha
sukari mkoani Morogoro
na hivi sasa wako kwenye
hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo.
NSSF tayari wameanza
kufanya utafiti wa awali
(Preliminary Studies)
kuhusu namna watakavyoanzisha kiwanda
hicho ambacho kinatarajiwa kupunguza uhaba
wa sukari na kutoa ajira
kwa vijana hapa nchini.
Shirika hilo pia limepanga
HAPA KAZI TU
po majadiliano baina ya
Mfuko na Shirika la Taifa la
Maendeleo (NDC) yamefanyika na tayari rasimu ya
upembuzi imewasilishwa.
Lengo ni kujenga kinu
cha kuyeyushia chuma
(foundry) ili kiwanda
kiweze kuzalisha vipuri
na mashine mbalimbali
za uzalishaji zitakazouzwa
katika soko la ndani na
nje. Tayari Menejimenti ya
Mfuko imetembelea kiwanda Julai 16 mwaka huu ili
kupata uelewa wa kiwanda
na changamoto zinazokikabili. Pamoja na ujenzi
wa kinu hicho, mfuko
unakusudia kutoa fedha za
uendeshaji (working Capital) anasema Msangi.
Mbali ya kuwekeza katika Kiwanda cha Vipuri
cha Kilimanjaro, mfuko
huo una nia ya kuwekeza
kwa pamoja na Benki ya
Maendeleo ya TIB katika kiwanda cha nyama
kinachojengwa Ruvu.
Kwa mujibu wa Bw. Msangi mfuko huo utaendelea
kushirikiana na NDC na
TIB ili kuweza kubaini
fursa nyingine kwa ajili ya
uanzishwaji au uendelezaji
wa viwanda mbalimbali.
Nao Mfuko wa Pensheni wa PSPF unaendelea
kuwekeza kwenye kilimo na
viwanda maeneo ambayo
yanachangia kuongeza ajira
na kukuza pato la nchi.
Maeneo hayo ni pamoja
na kiwanda cha nguo cha
21st Century cha Morogoro na kiwanda cha saruji
Tanga (Tanga Cement),
Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) na Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL).
Katika mikakati yao ya sasa
PSPF wameainisha maeneo
mapya ya kuwekeza ambayo ni kwenye viwanda
vya pamba, chuma, ngozi,
magadi na ukanda maalum
wa uwekezaji (EPZA).
Mikakati hii ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
ikitekelezwa vyema chini ya usimamizi thabiti
itasaidia kuinua uchumi
wa nchi na pia kuchochea maendeleo ya sekta
nyingine ikiwemo kuboresha maisha ya watanzania
na taifa kwa ujumla.
16
HAPA KAZI TU
Raymond Mushumbusi
kushiriki mashindano ya
Olimpiki kwa mwaka 2016
yanayofanyika Jijini Rio
dejaneiro nchini Brazil.
Mhe. Anastazia Wambura
amesema kuwa wadau
wa michezo wamekuwa
wakishirikiana na Serikali
sio katika suala la michezo
pekee hata katika habari
na Sanaa na amewapongeza kampuni ya vingamuzi
ya Multichoice Tanzania
(DSTV) na Bodi ya Utalii
Mhe. Anastazia.
Aidha amewataka wawakilishi wa Olimpiki kutumia fursa hii ya wadau
wa michezo waliojitokeza
kuwaunga mkono ikiwemo
Bodi ya Utalii kutangaza
utalii wa Tanzania kwa
mataifa mengine watakayo
kutana nayo katika mashindano ya Olimpiki nchini
Brazil.
Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Multichoice
Tanzania Bw.Maharage
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi
bendera katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil
katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016.
erikali imefanikwa
kukamata jumla ya
bidhaa za filamu na
muziki 94,000 ambapo
93,529 ni za wasanii wa nje
zilizoingia nchini kinyume
na sheria huku bidhaa
273 za wasanii wa ndani
zikiwa hazina stampu ya
ushuru wa bidhaa kutoka Taasisi ya Mapato
Tanzania(TRA) zikiwa
ni takwimu za awali.
Hayo yamejiri kufuatia
zoezi la kushtukiza lililofanywa na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Nnauye leo katika
soko la Kariakoo jijini
Dar es Salaam na kuahidi kwamba zoezi hilo
litafanyika nchi nzima.
Aidha aliongeza kuwa
mpaka sasa takribani
maduka 42 yamekaguliwa
na kukamata mitambo 19
ya kufyatua kazi za wasanii
(duplicators),printer 8
za Cd/Dvd,dvd writers
31,komputa 3,ups 7 kutoka
kampuni ya Aguster.
Hatua hii ni ya mwanzo
kwa kuwaonyesha Watanzania kuwa agizo la Rais
wa awamu ya Tano Mhe.
Dkt.John Pombe Magufuli la kulipa kodi na
kununua bidhaa halisi
kwa kutoa risiti linasimamiwa ipasavyo, alisema Mhe. Nnauye.
Mhe.Nnauye aliongeza kuwa wauzaji wengi
wa bidhaa za filamu na
muziki wamekiuka sheria zinazosimamiwa
na tasnia ya Filamu na
muziki ikiwemo sheria
ya Filamu na Michezo
ya kuigiza na.4 ya mwka
1976 inayosimamiwa na
Bodi ya Filamu Tanzania.
Chande ameishukuru
Serikali kwa kuwapa fursa
ya kushirikiana na timu ya
Olimpiki kuitangaza michezo na kuitangaza Tanzania kimataifa na kuahidi
kuendelea kushirikiana na
Serikali katika kuendeleza
michezo nchini.
Tumieni fursa
ya Uwanja wa
Taifa.
Na Lilian Lundo
Gazeti hili hutolewa na Idara ya Habari (MAELEZO) S.L.P 8031 Dar Es Salaam.
17