Imaan Newspaper Issue 81

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 19

TIF yatafuta Mil.

100 kusaidia waathirika wa tetemeko

ISSN 5618 - N0. 81


20 DHUL HIJA, 1437

ALHAMISI

SEPTEMBA 22 - 28, 2016

Bei: Sh800/KSH80/Ush1,200/-

Uk.7

HUWATOA WATU GIZANI

Al-Azhar yakanusha uvumi dhidi ya Answar


UK 7

IMETHIBITIKA!

Iran iliilaumu sana


Saudi Arabia kwa
uzembe wa vifo
769 mwaka jana na
hata kudai kuwa
tukio hilo ni mauaji
yaliyopangwa na
Saudi Arabia. Kwa
mujibu wa Ayatollah
Ali Khamenei, Saudia
ni wauaji wa mahujaji.

Vurugu Hijja huletwa


na mahujaji wa Kishia

Waislamu wayakana makundi


potofu yanayovuruga amani

UK 5

Ulevi, zinaa
vinavyodumaza
elimu Tanzania
UK 14

Wanne wasilimu msikiti wa Mtoro


UK 3

Na.
1
2
3
4
5
6
7
8

MJI
DAR ES SwalaAM
ZANZIBAR
TANGA
MOROGORO
MTWARA
ARUSHA
DODOMA
MBEYA

ALFAJR
11:20
11:19
11:21
11:31
11:27
11:27
11:32
11:48

HABARI / TANGAZO
DHUHUR
6:27
6:27
6:31
6:36
6:28
6:40
6:40
6:52

ASR
09:48
09:49
09:54
09:57
09:46
10:04
10:02
10:12

MAGHARIB
12:19
12:20
12:26
12:26
12:13
12:39
12:33
12:41

ISHA
1:28
1:31
1:37
1:37
1:24
1:49
1:44
1:52

Na.
9
10
11
12
13
14
15

MJI
KIGOMA
MWANZA
KAGERA
TABORA
SHINYANGA
SINGIDA
IRINGA

ALFAJR
11:56
11:39
11:43
11:44
11:40
11:37
11:41

DHUHUR
7:06
6:53
6:58
6:53
6:52
6:46
6:44

ASR
10:28
10:17
10:23
10:15
10:16
10:09
10:04

TIF yachinja
ngombe 150,
mbuzi 1600
Idi el Hajj
NASSORO ABEID,
MOROGORO

AASISI ya The Islamic


Foundation (TIF) ya mjini Morogoro imeshiriki
katika kulinda matukufu
ya dini ya Kiislamu kwa kuchinja mbuzi 1600 na ngombe
150 na kugawa katika mikoa
mbali mbali hapa nchini katika
sikukuu hii ya Idi-el-Hajj.
Mkuu wa Idara ya Ulinganiaji wa taasisi hiyo, Shekh Ismail
Kundya, amesema kuwa lengo
la kuchinja ni kutekeleza ibada
ya Sunnah iliyokokotezwa ya
kuchinja siku ya Idi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ma-

fundisho Uislamu.
Sheikh Kundya alisema taasisi yake iligawa vichinjo hivyo
kwa wahitaji. Alisema, katika
mkoa wa Morogoro, vichinjwa
hivyo viligawiwa katika ofisi
kuu ya TIF ambapo wakazi
kadhaa wa mkoa huo walijitokeza kupata msaada huo wa
nyama.
Licha ya makao makuu ya
TIF, shughuli ya kuchinja na
kugawa nyama pia iliendelea
katika misikiti mbalimbali
hapa hapa mkoani Mogororo,
alisema Sheikh Kundya.
Sadaka hiyo ilitolewa na taasisi zifuatazo: Dar Al Ber Society ya Dubai (UAE), Sharjah In-

aumini wa Dini Tukufu


ya Kiislamu wametakiwa kuishi kwa kufuata
taratibu kwa mujibu
wa kitabu kitakatifu cha Quran

na Mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehema na amani ya


Allah iwe juu yake) ili wafanikiwe akhera na duniani.
Nasaha hizo zimetolewa na
Ustadh Ally Mussa katika hutba
ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Haq uliopo Mtaa wa

ISHA
2:11
2:02
2:09
1:57
2:00
1:51
1:439

Uchinjaji wa
mbuzi 1600 na
ngombe 150
uliofanywa na
TIF na kugawiwa
katika mikoa
mbali mbali
hapa nchini
katika sikukuu
hii ya Idi-el-Hajj.

ternational Charity, Sharjah


(UAE), Emirates Red Crescent
- Abu Dhabi (UAE), Sheikh Eid
Charity - Doha (Qatar).
Nyingine ni RAF - Doha
(Qatar), Sheikh Zayed Bin Sultan Al Nahyan Foundation Abu Dhabi (UAE) na Sheikh

Khalifah Bin Zayed Al Nahyan


Foundation - Abu Dhabi
(UAE).
Kwa upande wao, baadhi ya
maimamu wa misikiti mbalimbali na waumini wa dini ya Kiislamu waliipongeza TIF kwa
kutekeleza ibada hiyo ya kuch-

Waislamu wahimizwa kufuata Quran


NA IBRAHIMU HAJJ,
MOROGORO

MAGHARIB
01:01
12:52
12:58
12:47
12:49
12:40
12:32

Karume mjini Morogoro.


Ustadh Ally alibainisha
kwamba ili kubarikiwa kimaisha, ni wajibu kwa Muislamu
kufuata maamrisho ya Allah
Mtukufu na kujiepusha na
makatazo yake.
Ustadh Mussa alinukuu

andiko la Kitabu Kitakatifu cha


Quran linalosema: Na lau kuwa
watu wa miji wangeliamini na
wakamchamngu, kwa yakini
tungeliwafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi.
Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale

inja na kufanikisha ugawaji wa


nyama kwa Waislamu.
Nao baadhi ya wanachi wa
mkoa wa Morogoro walisema
TIF ni mfano bora wa kuigwa
na kuzitaka taasisi nyingine
ndani na nje ya mkoa wa Morogoro kufuata mwendo huo.
waliyo kuwa wakiyachuma..
(Quran, 7:96). Aidha, Ustadh
Ally amewatahadharisha waumini wa Kiislamu kujiepusha na
miamala ya riba katika biashara
zao na wawe wenye kuridhika
kwa kile walichopewa na Allah
Taala. Katika hatua nyingine,
Ustadh Ally aliwahimiza waumini kujifunza na kuisoma dini
yao ili waweze kufuata maamrisho ya Mwenyzi Mungu na kujiepusha na makatazo yake.

Tazama Sayari ya Imaan kila siku


saa 3 kamili usiku kupitia TV Imaan

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

HABARI

IMETHIBITIKA!
Vurugu Hijja
huletwa na
mahujaji
wa Kishia
NA MWANDISHI WETU

ijja ya mwaka huu 1437 Hijriyya imemalizika yapata wiki moja iliyopita pasina
tukio lolote baya kwa mahujaji ukiacha
wale waliofariki kwa matatizo ya kiafya.
Kwa mujibu wa mahujaji mbali mbali waliorejea nchini kutoka Makka, ibada hiyo ya Hijja
ilitawaliwa na utulivu mkubwa tofauti na miaka
mingine. Mbali na kuimarika kwa huduma na
taratibu za Hijja, kuna jambo moja kubwa limedhihiri. Ilibidi mahujaji wajiulize, hivi kuna nini
kimepungua mwaka huu? Ikabainika kwamba
ni kukosekana kwa mahujaji kutoka Iran, taifa
la Kishia lenye msuguano na Saudi Arabia wa
kiitikadi na kisiasa.
Miaka mingi tangu kufanyika kwa Mapinduzi ya Kishia ya Iran mwaka 1979, Iran ilipanga kutumia ibada ya Hijja kama jukwaa la kisiasa, jambo ambalo lilipingwa na Saudi Arabia.
Matokeo yake ni kutokea kwa vurugu na hata
mauaji katika mji wa Makka mara kadhaa zikianzishwa na harakati za mahujaji wa Iran waliolazimisha kufanya maandamano na mara nyingine wakijipenyeza na silaha na kusababisha
makabiliano na polisi wa Saudi Arabia.
Mwaka jana lilitokea tukio la mkanyagano
katika eneo la Jamaraati, mkanyagano uliosababishwa na makundi mawili ya mahujaji yaliyokuwa yakienda pande mbili tofauti kukutana
na kusababisha vifo vya watu wengi.
Idadi ya vifo ilifikia 769 kwa mujbu wa taarifa
rasmi za Saudi Arabia huku wengi wao wakiwa
mahujaji wa nchi ya Iran ambayo ilidai waliofariki ni zaidi ya 2,000.
Kama kawaida yake, Iran iliilaumu sana
Saudi Arabia kwa uzembe na hata kudai kuwa
tukio hilo ni mauaji yaliyopangwa na Saudi Arabia. Kwa mujibu wa Ayatollah Ali Khamenei,
Saudia ni wauaji wa mahujaji.
Alhamdulillahi ukweli umebainika. Mleta
vurugu na msababisha matukio ya mkanyagano kama lile la mwaka jana amejulikana. Mwaka huu mahujaji wa Iran walisusia kwenda Hijja
kwa kutokuridhika na hatua zilizochukuliwa na
Saudi Arabia kudhibiti mienendo ya mahujaji.
Matokeo yake ndiyo haya. Hijja imefanyika
na kumalizika kwa amani na utulivu mkubwa
kiasi haijawahi kutokea. Ni wazi kwamba mahujaji wa Iran ndiyo chanzo cha vurugu katika
Hijja.

Wa-Iran waenda Hijja Karbala


Mahujaji wa Iran wapatao 64,000 waliokuwa waende Hijja Makka mwaka huu wengi
wao wameishia kwenda kufanya Hijja ya
Kishia huko Karbala nchini Iraq.
Kwa mujibu wa Adel Al-Mussawi, Msimamizi Mkuu wa Kaburi la Hussein ibn Ali
mjini Karbala, idadi kubwa ya mahujaji wa
Kishia wanatarajiwa kutembelea mji huo
mtakatifu kwa Mashia mwaka huu.
Tunategemea idadi ya mahujaji kufikia
milioni moja na asilimia 75 kati yao ni kutoka
Iran, alisema Al-Mussawi. Si wote waliopanga
kwenda Hijja Makka walikwenda Karbala
badala ya Makka. Kwa mujibu wa mashia, kuzuru kaburi la Imamu INAENDELEA UK 7

Wanawake Shamsia Dodoma

kujenga hospitali Tsh. Bil 4


NA JASMINE SHAMWEPU,
DODOMA

AASISI ya Wanawake wa Kiislamu ya Shamsia mkoani Dodoma


inatarajia kutumia Sh. Bilioni
nne kujenga hospitali ya kisasa
mkoani hapa itakayosaidia kuboresha
huduma za afya kwa wanawake na
watoto.
Mwenyekiti wa Shamsia, Nuru
Jabiri ametangaza habari hiyo nzuri
kwa wakazi wa Dodoma katika hafla
ya kutoa msaada wa chakula kwa
wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa mkoani hapa.
Nuru alisema kuwa hospitali hiyo
kubwa na ya kisasa itakayojengwa
eneo la Njedengwa Manispaa ya Dodoma kuanzia Desemba mwaka huu
itakuwa ni maalumu kwa kutoa huduma ya afya ya uzazi na watoto
Pia Nuru na kutaja lengo la ujenzi
wa hospitali kuwapa wanawake uhuru wa kueleza matatizo yao pindi wanapokuwa wanaumwa kwa kuwawekea madaktari wanawake.
Tutakuwa na madaktari wanawake wenye uwezo ili kuwasaidia
akinamama wenye matatizo ya afya
ya uzazi kujieleza vizuri kwa wanawake wenzao tofauti, kinyume na
inavyokuwa kwa madakatari wa
kiume, alisema Nuru.
Pia alisema katika hospitali hiyo
watakuwa na Kituo cha Mafunzo ya
Wauguzi na Wakunga ili kusaidia
juhudi za serikali za kuongeza watumishi wa kada hizo.
Taasisi ya Shamsia ( jina rasmi:

LENGO LA UJENZI
WA HOSPITALI
KUWAPA
WANAWAKE
UHURU WA
KUELEZA
MATATIZO
YAO PINDI
WANAPOKUWA
WANAUMWA KWA
KUWAWEKEA
MADAKTARI
WANAWAKE

Shamsia Women Group) inajihusisha


na masuala ya kijamii hususan afya,
kuwasaidia kiafya waathirika wa

ugonjwa wa Ukimwi, wajane pamoja,


wanafunzi hususan wa sekondari na
watu waishio katika mazingira magumu.
Kwa upande wa wajane, wanawake
wa Shamsia wamekuwa wakiwasaidia wanawake hao waliopoteza waume
zao kwa mitaji ya kufanya biashara.
Biashara ndogo kama kuuza
mbogamboga na matunda na kupika
vitafunwa zimesaidia sana akinamama wajane hadi baadhi yao kufanikiwa kujikimu na kujikwamua kimaisha, Nuru alisema.
Aidha, Nuru alitoa wito kwa jamii
kuwa na moyo wa kujitolea na siyo
kuendekeza mambo ya anasa huku
wakishindwa kusaidia wagonjwa na
watu wengine wenye mahitaji maalumu.

Wakimama wanne wasilimu msikiti wa Mtoro


Yumo mama wa maombezi kanisa la Pentekoste
NA MUGINI SINGIRA

liyekuwa mama wa
maombezi katika kanisa la Pentekoste banana, jijini Dar es Salaam, Sophia Kenani na
Wakina mama wengine
watatu kutoka sehemu na
madhebebu tofauti ya Kikirsto wamesilimu na kuingia Dini Tukufu ya Kiislamu.
Wakielezea sababu zilizopelekea kuchukua uamuzi
huo, wote walisema wamevutika na ujumbe na mafundisho ya Uislamu. Sophia
(49) alisema amependa kuingia katika Uislamu kwa hiyari yake na hakuna mtu
yeyote aliyemlazimisha kuchukua uamuzi huo.
Sophia alisema miezi
minne nyuma akiwa Mkristu zilimjia ndoto na mawazo
ya kubadili dini na kuingia

katika Uislamu. Sophia alisema mara kadhaa mtu aliyevaa kanzu nyeupe alimjia
ndotoni na kumwambia
kuwa yeye (sophia) ni mtu
msafi na hivyo anafaa sana
kuwa Muislamu.
Baada ya kutokewa na
hali hiyo mara kwa mara, alisitisha kwenda Kanisani
kwa kipindi cha takribani
miezi minne mpaka alipofikia uamuzi wa kusilimu.
Zaidi, Sophia alisema
wakati alipokuwa Mkristo
akiabudu alisoma mpaka
kufikia ngazi ya uchungaji
na alikuwa akishikilia nyadhifa mbalimbali ikiwa ni
pamoja na mama wa
maombezi, (mtu anayetembea akiwashuhudia watu)
na mwalimu wa watoto.
Mimi ni mtu mzima
mwenye akili timamu na
sasa nina miaka 49. Nimesil-

imu kwa hiyari yangu wala


sijalazimishwa na mtu yeyote na huko nilikotoka kwenye
Ukristo nilisomea uchungaji
na niliokoka mwaka 2002,
alisema Sophia Naye Najma
Vitalisi aliyekuwa akijulikana kwa jina la Emelda Emily
alisema alisilimu baada ya
kuvutiwa na ujumbe wa Kiislamu aliokuwa akiusikia
ukitolewa mara kwa mara
Msikiti wa Mtoro kupitia vipaza sauti wakati akiwa mahali anapofanyia biashara
karibu na msikiti huo.
Nimependa peke yangu
kuingia katika Uislamu
hakuna mtu yeyote aliyenilazimisha ila tu mawaidha
yanayokuwa yanatolewa
msikitini ndiyo yalinivutia
hususan wakati wa mwezi
mliokuwa mkifunga, aliema
akimaanisha Ramadhani.
Katibu wa Waumini Wa-

nawake wa Msikiti wa
Mtoro, Saida Saidi Kimpinga, ambaye ndiye aliyewasilimisha alielezea furaha yake
na kuwakaribisha wanawake
hao katika Uislamu huku
akisema idadi hiyo ya watu
wanne wakina mama kusilimu kwa siku mmoja ni mara
ya kwanza kwa msikiti huo.
Mwenyezi Mungu kawafungulia kutambua haki
hakuna mtu aliyelinganiwa
na uongozi wa hapa msikitini labda huyo dada anayefanya hapo biashara zake
ndiye katueleza mwenyewe
kuwa yeye huwa anasikia
mawaidha ndiyo yaliyomkinaisha kuupenda Uislamu,
alisema dada Saida.
Aidha, Saida alisema uongozi wa msikiti wa Mtoro
umeshawapa vyeti vya wanawake waliosilimu na uongozi wa wanawake wanashirikiana kuhakikisha wanapata walimu kuwafundisha
wakina mama hao Uislamu.

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

TUJIKUMBUSHE

NA ABU AMEENAH BILAL PHILIPS

IJUE HISTORIA YA MADHEHEBU (21)


ufundishwaji wa fiq-hi lingalishi
kimfumo.

Kuibuka kwa Taqliid


(kufuata madhehebu
kibubusa)

Toleo lililopita tulianza kuielezea hatua ya tano katika historia ya


madhehebu. Wiki hii tutaanza kuelezea kuhusu kuandikwa kwa Fiqhi za madhehebu na kuingia hatua ya sita ya historia ya madhehebu. Sasa Endelea. ..
Kuandikwa kwa Fiq-hi
Katika kipindi cha utawala wa
Banii Abbas, mfumo maalum wa
kuandika vitabu vya Fiq-hi uliibuka.
Mfumo huu ukawa ndiyo kipimo na
ndiyo uliobakia ukitumika hadi leo.
Masuala mbali mbali yaliwekwa
kwenye kundi chini ya kichwa kimoja cha habari na kichwa hicho
cha habari kuwekwa katika sura
(Chapters au Milango) mbali mbali,
kila moja ikielezea suala fulani kutokamana na Sharia.
Hata hivyo, milango ikawekewa
mfumo fulani. Mwandishi angeweza kuanzia na nguzo nne za Uislamu
baada ya nguzo ya imani kwani
nguzo ya imani inakuwa imeshashughulikiwa katika vitabu vya
Aqiida (Itikadi).
Baada ya kushughulikia kanuni
za Kisharia na masuala yahusuyo
tohara, Swala, Swaumu, Zaka na
Hijja, waandishi waliendelea na
mambo ya ndoa na talaka kisha hukumu za biashara na hatimaye
Adaab au maadili.
Katika kushughulikia moja katika masuala haya, mwandishi yeyote
kutoka madhehebu yeyote hutaja
ushahidi mbali mbali uliotumiwa
na madhehebu yake huku akipinga
hoja za madhehebu zingine.

Muhtasari
Mosi, Madhehebu nyingi zilizoibuka katika kipindi cha mwanzoni
zilitoweka na kubakia madhehebu
nne kuu. Pili, Madhehebu zilifikia
ukomo wa uundwaji wake kimfumo
katika kipindi hiki. Tatu, ijtihadi
(kufanya juhudi kutoa ufumbuzi wa
masuala) nje ya madhehebu iliachwa na ijtihadi ya kimadhehebu

ikachukua nafasi. Nne, Fiq-hi linganishi iliibuka lakini ilitumika sana


kwa ajili ya kuendeleza fikra za kimadhehebu.

Hatua ya Sita: Kudumaa


na kufifia
Hatua hii inakienea kipindi cha
takriban karne sita hivi kuanzia
kutekwa na kuharibiwa kwa mji wa
Baghdad mwaka 655 Hijriyya sawa
na 1258 miladiyya na kuuawa kwa
mfalme wa mwisho wa utawala wa
Banii Abbas, Al-Mutaswim Billahi
na kumalizikia katikati ya karne ya
19 miladiyya.
Kipindi hiki pia kinawakilisha
kuibuka kwa dola ya Waturuki (The
Ottoman Empire) iliyoanzishwa
mwaka 698 Hijriyya (sawa na 1299
Miladiya) na kiongozi Mturuki Uthman wa Kwanza hadi kuporomoka
kwake kutokana na mashambulizi
ya wakoloni wa Ulaya.
Hali ya madhehebu iliyokuweko
kipindi hiki ni ile ya Taqliid (yaani
kufuata madhehebu kibubusa) na
mifarakano. Mwenendo huu wa
kumaliza nguvu za umma ulitokana
na kufungwa kwa mlango w ijtihad
za aina zote na kuibuka kwa madhehebu kama makundi yanayofanana
na yale ya imani za kidini (setcs).
Kuandikwa kwa Fiq-hi katika
kipindi hiki kulikuwa kwa ajili ya
kutoa maoni (sherh) juu ya kazi zilizoandikwa miaka iliyopita na ilikuwa kwa lengo la kuienzi madhehebu husika.
Kwa hiyo, ule uhai wa mabadiliko ya ki- fiq-hi kulingana na mahitaji ya zama husika ukapotea na hukumu nyingi zikapitwa na wakati na
kutokutumika kama zilivyokuwa.

Ili kuziba ombwe hili la kisharia,


sheria za kutungwa na binadamu za
kizungu zikaanza kidogo kidogo kuchukua nafasi ya sheria za Fiq-hi
ambazo zilionekana kutokwenda
na wakati.
Baadhi ya wanamageuzi Waislamu walijaribu kupambana na wimbi hili la mabadiliko wakihimiza
kurejelewa kwa Sheria za Kiislamu
na utakasifu wake. Hata hivyo,
ikhtilafu na mifarakano ya kimadhehebu imeendelea hadi zama hizi
pamoja na kuongezeka kwa

QIBLA
(MAQAAMAT)
MBALI MBALI
ZILIWEKWA
KUZUNGUKA
AL-KAABA,
MOJA KWA
AJILI YA IMAMU
KUTOKA
MADHEHEBU
HIZO NNE.
WAKATI
WA SWALA
ULIPOWADIA,
IMAMU WA
MADHEHEBU
MOJAWAPO
ALIONGOZA
SWALA KWA
AJILI YA
WAFUASI WAKE

Wanawazuoni wa zama hizi


waliachana na ijtihadi zote na wakatoa fat-wa kwa kauli ya wengi ambayo ilikusudia kuufunga mlango
wa ijtihadi moja kwa moja.
Walitoa sababu kwamba masuala yote yanayowezekana kutokea
yameshashughulikiwa na kwamba
kwa sababu hiyo hakukuwa na hitajio la Ijtihaadi.(Tazama Muhammad Hussein Ad-dhahbiy, Assharia al-Islaamiyyah, uk. 12).
Kutokana na hatua hiyo (ya kufunga mlango wa ijtihaadi), mtazamo mpya wa madhehebu ukaibuka
nao ni kwamba ili Uislamu wa mtu
uwe sahihi, ni lazima afuate mojawapo kati ya madhehebu nne (za
Ahlu Sunnah wal Jamaa).
Kadiri muda ulivyopita, mtazamo huu ukabobea katika akili za
watu na hata miongoni mwa
maulamaa wa fiq-hi. Kwa hiyo dini
ya Uislamu ikafungika katika wigo
wa madhehebu hizo nne tu: Hanafi,
Maliki, Shafi na Hambali.
Madhehebu hizi nne zikachukuliwa kama ufahamu wa Uislamu uliofunuliwa kutoka kwa Allah. Zote
zilchukuliwa kuwa sahihi, sawa na
zenye kuwakilisha Uislamu wa kweli pamoja na kwamba kulikuwa na
tofauti nyingi kati yao.
Kwa hakika katika kipindi hiki,
kulikuwa na wanawazuoni ambao
walizitafsiri hadithi kwa namna ya
kuthibitisha kwamba Mtume Muhammad mwenyewe (rehema na
amani ya Allah ziwe juu yake) alitabiri kutokea kwa maimamu na
madhehebu zao.
Kwa sababu hiyo, ijtihada yoyote
ile nje ya madhehebu hizi kuu nne
zilichukuliwa kama kuchupa mipaka (heretical) na yeyote aliyekataa
kufuata madhehebu hizi alichukuliwa kama Murtad (aliyetoka katika
Uislamu).
Wanawazuoni wenye msimamo
mkali wa kipindi hiki walikwenda
mbali zaidi haki kufikia kutoa fatwa kwamba mtu yeyote aliyehama
kutoka madhehebu moja kwenda
nyingine alistahiki kuadhibiwa kwa
mujibu wa Qadhi atakavyoona.
Vilevile, ilitolewa fat-wa katika
madhehebu ya Hanafi ikikataza
ndoa kati ya mfuasi wa madhehebu
ya Hanafi na Shafi (Tazama Swafat
Swalaat N-nabiy, Muhammad Nasriddiyn Al-Albaniy, uk 51).
Hata nguzo ya pili ya Uislamu
yaani swala, haikusalimika na faraka za kimadhehebu. Wafuasi wa
madhehebu mbali mbali wakaanza
kukataa kuswali nyuma ya maimamu wa madhehebu nyingine.
Hili lilipelekea kujengwa kwa qibla (Maqaamaat) tofauti katika
misikiti iliyo katika jamii ambazo
kulikuwa na wafuasi wa madhehebu zaidi ya moja.
Misikiti ya aina hii bado inaweza
kuonekana hivi sasa katika maeneo

ya Syria ambapo Waislamu wa huko


ni wafuasi wa aidha madhehebu ya
Hanafi au Shafi.
Hata msikiti mtakatifu wa Makka, Masjidul al-Haraam - ambao ni
kiwakilshi cha umoja wa Waislamu
na ndiyo Qibla chao, uliathirika.
Qibla (Maqaamat) mbali mbali
ziliwekwa kuzunguka Al-Kaaba,
moja kwa ajili ya imamu kutoka
madhehebu hizo nne. Wakati wa
swala ulipowadia, imamu wa madhehebu mojawapo aliongoza swala
kwa ajili ya wafuasi wake.
Kisha imamu kutoka madhehbu
nyingine angewaongoza wafuasi wa
madhehbu hiyo (kutoka katika
Maqaam yao) na hivyo hivyo hadi
madhehebu zote zimalize kuswali.
Ni jambo la kustaajabisha
kwamba Maqaamati mbali mbali
kwa ajili ya medhehebu zilibakia
kuzunguka Al-Kaaba hadi robo ya
kwanza ya karne ya 14 Miladiyya
pale Mfalme Abdulaziz ibn Suud na
jeshi lake walipoiteka Makka mwezi
Oktoba mwaka 1924.
Ni yeye ndiye aliyewaunganisha
Waislamu kuswali nyuma ya imamu mmoja katika Al-Kaaba bila kujali imamu anatoka madhehebu
gani na maamuma ni mfuasi wa
madhehebu gani.

Tanbihi
Kitendo hiki cha utawala wa
Saudi Arabia kuondosha umadhehebuu uliowagubika Waislamu na
kuwaunganisha waswali nyuma ya
imamu mmoja katika Al-Kaaba ni
katika mambo yaliyowachukiza
baadhi ya Waislamu. Makka wakati
huo ilikuwa chini ya mtawala
(Amiri) Sharifu Hussein bin Ali.
Abdulaziz ibn Suud ndiye aliondosha utawala wa Masharifu Makka.
Kupigwa vita kukubwa kwa ukoo
wa Ibn Saud unaotawala Saudi Arabia kutoka kwa waijiitao Masharifu
na Mashia ni kutokana na kuuteka
mji wa Makka na kurejesha Uislamu usiotambua madhehebu kama
dini ndani ya dini ya Kiislamu.
Hussein ibn Ali alikuwa ndiye
mtawala wa mwisho wa ukoo wa
Hashim (Bani Haashim) kutawala
Makka. Kwa kuwa alikuwa akiheshimika sana duniani kote, utawala
wa ukoo wa Ibn Suud ulianza na kuchukiwa na washabiki wa umadhehebu.
Utawala huo uliunga mkono
harakati za kuurejesha Uislamu katika hali yake ya kutokushabikia
madhehebu zilizoongozwa na
Sheikh Muhammad ibn AbdilWahhab (Allah amrehemu).
Chuki ilyoelekezwa dhidi ya ukoo
wa Ibn Suud ikamwelekea pia
Sheikh Muhammad ibn AbdilWahhab ambaye alikuwa mwanachuoni mfuasi wa madhehebu ya
Imam Ahmad ibn Hambal (Allah
amrehemu).
Huu ndio ukawa mwanzo wa
kile kinachoitwa harakati dhidi ya
Uwahabi yaani harakati dhidi ya
fikra za Muhammad ibn AbdilWahhab, harakati ambazo zinashadidiwa na maadui wa Uislamu, washirikina na watu wa bida.
Itaendelea Inshaa-Allah.

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

Waislamu wayakana
makundi potofu
yanayovuruga amani
NA.IBRAHIMU HAJJ, MOROGORO

AISLAMU nchini wametakiwa


kulinda amani ili kupata utulivu
wa kujiletea maendeleo katika
miradi yao mbalimbali sambamba na kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, Waislamu wametakiwa kujiepusha na tabia ya kuleta ushabiki katika Uislamu na wameshauriwa kuwa na hamasa
ya kujifunza elimu ya dini ili waweze kuepukana na mitego ya kuingia katika makundi
potofu yanayojinasibisha na Uislamu.
Nasaha hizo zilitolewa na Mkuu wa
Kituo cha Dini cha Kiislamu cha Al-Azhar
Al-Shariif kilichopo maeneo ya Changombe
jijini Dar es Salaam, Sheikh Said Awadh
Abdul Adhiim katika kongamano la kidini
lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu
cha Kiislamu (MUM) kilichopo Mjini Morogoro.
Sheikh Said Awadh alisema makongamano ya Kiislamu ni muhimu ili kufundisha umuhimu wa kushikamana na dini kwa
kufuata miongozo sahihi iliyomo katika
kitabu cha Mwenyezi Mungu Quran Tuku-

Mkuu wa
Kituo cha
Dini cha
Kiislamu
cha
Al-Azhar
Al-Shariif,
Sheikh Said
Awadh
Abdul
Adhiim

MAKONGAMANO YA
KIISLAMU NI MUHIMU
ILI KUFUNDISHA
UMUHIMU WA
KUSHIKAMANA NA
DINI KWA KUFUATA
MIONGOZO SAHIHI
ILIYOMO KATIKA
KITABU CHA
MWENYEZI MUNGU
QURAN TUKUFU
fu pamoja na mafundisho ya Mtume Muhammad (rehema na amani ya Allah iwe
juu yake).
Kwa upande wake, mgeni rasmi katika
kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe aliwahimiza
waumini waliohudhuria kushikamana
pamoja na kufanya kazi kwa bidii sambamba na kuhakikisha wanailinda amani ya
nchi. Naye, Shekh Mkuu wa Mkoa wa Mo-

rogoro, Abdallah Mkangambe, aliwatahadharisha Waumini kutotoa mwanya kwa


maadui kupenyeza chuki zitakazopelekea
vita vya wenyewe kwa wenyewe na kutoweka kwa amani.
Kituo cha Dini cha Kiislamu cha Al

Azhar Shariif ni miongoni mwa vituo vya


dini vilivyokuwa mstari wa mbele katika
kuandaa makongamano ya kidini katika
mikoa mbali mbali nchini Tanzania kwa
lengo la kuhamasisha mshikamano na kutoa mafundisho sahihi ya Uislamu.

Afyais natural source of sweet drinking


water from underground stream which is
blended with essential minerals to support
and aid perfect metabolism.

WATERCOM LIMITED
P.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area Temeke,DareSwalaam, Tanzania. www.watercomtz.com, Email:info@watercomtz.com

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

HUTOLEWA NA KUCHAPISHWA

TAHARIRI / NASAHA

The Islamic Foundation, P.O. Box 6011 Morogoro, Tanzania, E-mail: imaanmedia3@gmail.com
CHUMBA CHA HABARI: 0652 777 969 AFISA MASOKO: 0785 500 502
TOVUTI: www.islamicftz.org

Tuungane kuwasaidia wahanga tetemeko la ardhi

usaidiana katika wema ni


moja ya alama za imani
ya muislam.Zaidi ni
kwamba, kuwafanyia
wema na ihsani waja wa Mwenyezi Mungu ndiko kunakopandikiza mapenzi, furaha na utangamano miongoni mwa makundi
ya watu.
Dini tukufu ya kiislam inawataka waumini wake kuwa mstari
wa mbele katika kutatua shida za
makundi mbalimbali ya kijamii.
Sambamba na hilo, Allah ameahidi kumpa maisha bora ya duniani na akhera muislam mwenye
kumuondolea tabu na uzito mtu
aliyefikwa na shida na misukosu-

sukumo katika kuiga


una ushawishi mkubwa
kwenye ujenzi wa tabia
na mienendo ya watu.
Katika mazingira ya kawaida
mtu huiga tabia njema au mbaya
kupitia mazingira anayoishi au
vivutio vinavyomzunguka.
Kimantiki, tabia kwa mwanadamu ni kama vazi, na wakati
mwingine huchukuliwa kuwa
ndiyo kipimo cha utu. Kwa kulitambua hilo, Mwenyezi Mungu
amewatuma Mitume na Manabii
ulimwenguni ili waje kuifunza
jamii adabu na tabia njema.
Umma wa Kiislamu umebahatika kulelewa katika misingi ya
viwili hivyo. Allah Taala anatuambia: Hakika nyinyi mnacho
kiigizo chema kwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu kwa anayemtaraji Mwenyezi Mungu na Siku
ya Mwisho (Quran, 33:21).
Pia, katika hadithi Mtume (rehema na amani ya Allah zimfikie)
amesema: Nimetumwa kukamilisha tabia njema (Ahmad).
Tunapotafakari kwa kina juu
ya kauli hizi tunagundua kuwa,
hakuna pambo nadhifu kwa
Muislamu isipokuwa tabia njema.
Na tabia njema iliyo na maana
pana zaidi, ambayo kila Muislamu anatakiwa kuwa nayo, ni
kuepuka kufanya mambo machafu na maovu. Sababu ni
kwamba, kinachoupa nguvu na
kuupandisha daraja Uislamu
kutoka kuwa nadharia hadi
utekelezaji, ni hoja ya kuwepo
kwa tabia njema na mifano elekevu kutoka kwa waja wema waliotangulia.
Mahujaji wanaweza kuwa
kielelezo na mfano wa kuigwa na
jamii kutokana na kudhihirisha
kwao dhana ya Ucha Mungu na
tabia njema wakati wote wa ibada ya Hijja.
Walifanya hivyo kwa lengo la
kutafuta radhi za Mola wao mlezi. Naamini hata wale ambao katika maisha yao ya kawaida
hawakuwa na ada ya kuswali
nyakati za usiku (Qiyamu llayli),
katika Hijja walipata wasaa wa
kuswali usiku.
Swali la kujiuliza ni je, baada
ya kukamilisha ibada ya Hijja na

ko. Kutoka kwa Swahaba Abu


Hurayra (Allah amuwie radhi),
Mtume (Rehema na amani ya Allah zimfikie) amesema:Yeyote
yule anaemsaidia muhitaji Allah
atamsaidia haja zake hapa duniani na akhera(Muslim).
Taasisi ya The Islamic foundation (TIF) yenye makao yake
makuu mjini Morogoro imeliona
hilo.Kupitia Mwenyekiti wake wa
kitengo cha maafa Ndugu Ahmed
Bawazir, TIF imewaomba watanzania kufanya hima katika kuwasaidia wahanga wa tetemeko la
ardhi lililotokea hivi karibuni
huko mkoani Kagera.
Kwa mujibu wa Bawazir kwa

sasa TIF inaendelea na kampeni


inayofahamika kama Changia
shilingi 10,000 kutoka kwa wafadhili 10,000 ambayo lengo lake
ni kukusanya kiasi cha shilingi
Milioni 100 ili ziwasaidie wahanga waliofikwa na maafa hayo.
Utekelezaji wa kampeni za
aina hii ni moja tu ya kazi za taasisi za dini ambazo bila shaka zipo
kwa ajili ya utoaji huduma za kiroho kwa waumini wake, lakini
pia kusaidia miradi mbalimbali
ya maendeleo ya kidini na kijamii.
Kwa hakika TIF inafanya jambo jema, lenye maslahi na wanadam.Ifahamike kuwa, kitendo

cha kuwasaidia viumbe wa


Mwenyezi Mungu ni katika
mambo yanayomfanya mja kufikia kilele cha utukufu na wema.
Katika Quran Allah Taala
anasema:Hamtoufikia wema
mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda, na chochote mnachokitoa, basi Mwenyezi Mungu hakika anakijua (3:92).
Tunatambua kuwa, nyoyo za
wanadamu zimeumbwa katika
maumbile ya kumpenda mwenye
kuzitendea wema na kumchukia
mwenye kuzitendea uovu na
ubaya.Na kwa vile mja ni
mtumwa wa ihsani, tunatumai
kampeni hii itakuwa mkombozi

NASAHA ZA WIKI
YUSUPH AMIN

Mahujaji onesheni athari ya

Hijja kupitia tabia njema

kwa wale wote walioathirika na


j a n g a h i l i . Wa s w a h i l i
wanasema:Kidole kimoja hakivunji chawa.Kutokana na ukweli
huo,tunazikumbusha taasisi
mbalimbali za dini ndani na nje
ya nchi, waislamu na wananchi
kwa ujumla kushirikiana kwa
pamoja katika kuwasaidia kwa
hali na mali watanzania hawa.
Allah Taala ameahidi malipo
bora kwa mwenye kuyafanya
haya kama anavyobainisha: Na
wote wana daraja mbalimbali
kutokana na yale waliyoyatenda.
Na Mola wako Mlezi si mwenye
kughafilika na yale wanayo yatenda (6:132).

katika kuhifadhi, kulinda na kuimarisha mawasiliano na Mola


wako wakati wa Hijja, pia unapaswa kuendelea na hali hiyo
baada ya Hijja.

Hijja na funzo la usamehevu


Suala la kusameheana linapaswa kupewa kipaumbele na
waumini kwa kuwa lina faida nyingi kidini, kijamii na kiafya.
Inaelezwa kwamba, nguvu ya
msamaha ni nyundo inayobomoa
masikitiko, hasira, machungu ya
moyoni na hali ya kutaka kulipiza
kisasi.
Vile vile, msamaha ni mlango
wa furaha na utulivu, na pia ni
chemchem ya kustawisha furaha
na amani baina ya wanajamii.
Kwa hakika hizi ndizo zilikuwa sera na malengo ya
Mtume (rehema na amani ya Allah zimfikie) pamoja na Maswahaba (Allah awe radhi nao) hadi
wakaweza kusimamisha dini katika maisha yao binafsi na jamii
kwa ujumla.
Muhimu kwetu, ni kuandaa
mipango maridhawa ya kuutekeleza Uislamu kivitendo.
Tukifanya hivyo tutakuwa tumetekeleza sehemu ya majukumu
yetu ya kila siku.

Je, unatatizika kupata


mifano mizuri ya kuiga?.

kurejea kwenye miji yao, ni kwa


kiwango gani Mahujaji hawa
wataweza kufikia kilele cha tabia
njema na maadili ya dini?.
Jibu la msingi la swali hili
litasalia katika kuwataka Mahujaji kuwa na ari ya kujijengea
misingi imara ya kitabia na kujiweka mbali na matendo mabaya
ili wawe mfano wa kuigwa na
wengine.
Lakini Allah Taala anasema:
Basi mkifanya wema, mnazifanyia wema nafsi zenu, na mki-

f a ny a u b ay a , m n a j i f a ny i a
wenyewe (Quran,17:7).
Hakuna asiyefahamu kuwa,
ulinganiaji ni jukumu la umma,
na kila Muislamu atahesabiwa
kwa kutotenda majukumu yake
binafsi ya kiibada na kijamii.
Mtume kwa upande wake aliweza kuwaonesha Maswahaba
mfano mwema wa tabia nao
wakimfuata na kumuiga katika
matendo na kauli.
Changamoto kubwa tuliyonayo Waislamu wa sasa, ni

kuyafanya mawaidha kama njia


kuu ya ulinganiaji huku tukisahau kwamba njia bora na imara
ya kuwalingania watu ni adabu,
heshima na matendo yetu mema.
Hii ni sawa na kusema: Ulinganiaji bora ni matendo mema.
Sina shaka juu ya ibada ya Hijja kuwa moja ya nembo muhimu
zinazoutambulisha Uislamu na
kwa sababu hiyo si jambo linalotarajiwa kwa Muislamu hasa aliyehiji kuishi kinyume na matakwa ya dini. Kama ulijitahidi

Kama jawabu ni ndiyo, basi


isome na uielewe Quran, Sunnah
ya Mtume sambamba na vitabu
vya kihistoria yani Tareikh. Ukifanya hivyo, utaweza kuchota mifano ya maisha bora kutoka kwa
Manabii na wengineo katika waja
wema waliopita (Salafi).
Kwa hakika hawa ni walimu
sahihi wa masomo ya imani,
maadili na maisha hivyo ukiwasoma barabara wataweza kukuokoa kutoka kwenye dimbwi la
maisha ya kijahili, upotevu na
dhulma. Kadhalika, Mahujaji
wanapaswa kuwa walimu bora
wa masomo haya ili kuifanya
jamii iishi katika hali ya utu na
u s t a a r a b u . Tu n a m u o m b a
Mwenyezi Mungu atujaalie kuwa
miongoni mwa wanaoutekeleza Uislamu kivitendo kwa ukamilifu wake.Aamiin!

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

Vurugu Hijja huletwa na mahujaji wa Kishia


INATOKA UK 3
Hussein ibn
Ali (Allah amridhie) ni moja ya wajibu wa kidini wa kila mwaka na
Mashia wengi hufanya hivyo.
Mwaka huu wakati wa siku ya
Arafa, Mashia walikuwa wakiihujumu Hijja kwa kudai kuwa kuzuru
Karbala siku ya Arafa ni jambo bora
kuliko kuzuru Makka. Na hiyo si
ajabu kwa sababu kwa mujibu wa
Mashia, ardhi ya Karbala ni tukufu
kuliko ardhi ya Makka.
Amepokea Al-hurr Al-Amily
kutoka kwa Jafar (Imam wa Sita
wa Kishia) alisema: Allah aliiumba

Karbala kabla ya kuiumba AlKaaba kwa miaka elfu 24 na akaitakasa na kuibariki na haijaacha
kuwa takatifu na yenye baraka kabla Allah hajaumba viumbe. (AtTahdhiib cha At-tuusiy, mjalada wa
6/72).
Na huyo huyo Al-Hurr Al-Amily
amesema katika upokezi mwingine
kutoka kwa Imam As-swaadiq:
Ardhi ya Al-Kaaba ilisema, nani
kama mimi na ilihali pamejengwa
juu yangu nyumba ya Allah juu ya
mgongo wangu, wananiijia watu
kutoka pande zote za mbali na

TIF yatafuta Mil.


100 kusaidia
waathirika wa
tetemeko
NA KASSIM LYIMO

AASISI ya The Islamic Foundation (TIF)


kupitia kamati yake ya maafa imeanzisha
kampeni ya kuchangisha shilingi Milioni
100 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Kampeni hiyo iliyopewa jina la Changia
10,000/- kwa wadhamini elfu kumi, inalenga
kuwapunguzia adha waathirika hao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya TIF,
Ahmed Bawazir, amesema kuwa licha ya kiwango
hicho cha 10,000/- kuwa kidogo, iwapo idadi ya
kutosha ya Watanzania
wa watachangia, lengo la
kukusanya milioni 100
litafikiwa kwani umoja ni
nguvu na utengano ni
udhaifu na kidole kimoja
kamwe hakivunji chawa.
Aidha, Mwenyekiti
huyo wa Kamati ya Maafa ya TIF alisema kila
Ahmed Bawazir
mwananchi anapaswa
kufahamu kuwa kuwachangia waathirika hao wa tetemeko la ardhi ni
kuendeleza umoja na ushirikiano miongoni mwa
Watanzania, bila kubaguana kwa misingi yeyote.
Tuna matumaini kwa uwezo wa Allah, Subhanahu Wataala, kiasi hicho cha fedha kitatimia
na tutaweza kuwafikishia walengwa kwa wakati,
alisema Bawazir na kuongeza: Sisemi kwamba
Taasisi ya The Islamic Foundation ina fedha nyingi, bali kutokana na kuaminiwa na Watanzania
wengi tumekuwa tukichangisha michango kama
hii na kuwafikishia walengwa na bila shaka safari
hii pia tutafanikisha, alisema Bawazir.
Nichukue fursa hii kuwahimiza Watanzania
wote kuunga mkono kampeni hii ya changia
10,000/- kwa wadhamini elfu kumi, yenye baraka
zote za serikali, kwa kutoa michango yao kupitia
namba zetu za kuchangia.
Bawazir alizitaja namba hizo kuwa ni Airtel
0785627284, Vodacom 0767627284 na Tigo
0713627284. Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mkuu wa TIF, Sheikh Ibrahim Twaha, alisema
kuwa suala la kuwachangia watu waliopatwa na
matatizo mbalimbali katika jamii limehimizwa
sana katika Uislamu. Katika hatua ya kuonesha,
watendaji wa Radio na Tv Imaan, wamekubali
kukatwa kiasi cha fedha katika mishahara yao ili
kungana na na Watanzania wengine kuwachangia waathirika wa tetemeko hilo.

nimefanywa mahali patakatifu pa


amani?
Allah akaishushia wahyi akisema: Nyamaza na utulizane. Ubora
wako si chochote kwa nilichoifadhilisha kwacho ardhi ya Karbala
ila ni kama sindano iliyochovywa
baharini na ikabeba maji.
Na kama si udongo wa Karbala,
nisingekufanya uwe na ubora wowote. Na kama si kwa yule niliyeidhaminii Karbala kwa ajili yake
nisingekuumba na nisingeumba
hicho unachojifakharisha kwacho,
basi nyamaza na utulizane.

Na kuwa kama mkia wenye


kunyenyekea dhalili mnyonge usiyejikweza wala kujitutumua juu ya
ardhi ya Karbala na kama usipofanya hivyo nitakufutilia mbali na
kukutumbukiza katika moto wa
Jehananu. (Wasaail As-Shiia,
mjalada wa 10/403).
Kwa hiyo, si ajabu kabisa mashia
wakaitukuza Karbala kuliko Makka na kumiminika huko kwa ajili ya
Hijja ya Kishia.
Ndiyo maana wakienda Makka,
Mashia huenda mahali ambapo
kwa itikadi yao siyo mahali patakat-

ifu kama Karbala hivyo kufikia hata


kuipaka kinyesi Al-Kaaba kama
walivyowahi kufanya huko nyuma.
Madai ya Iran ni kutaka Saudi
Arabia inyanganywe usimamizi wa
miji ya Makka na Madina kwa kisingizio kuwa hiyo ni miji ya Waislamu wote.
Lakin lengo lao kubwa wakifanikiwa kuidhibiti miji hiyo-na Allah
awadhallishe wasifanikiwe- ni hatimaye kuiuawa Hijja ili kuipa nguvu
Hijja yao ya Karbala kwa kuwa
huko ndiko patukufu kuliko Makka kama tulivyoona.

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

KUTOKA KATIKA QURAN NA SUNNAHH


SHEIKH TAWAKKAL JUMA

Misingi na matawi ya dini katika Uislamu


Sababu zinazopelekea makundi mbalimbali yasiungane katika Uislamu (9)
Mpenzi msomaji, Shia
wanaitakidi kuwa Maswahaba wengi,
isipokuwa wachache
sana, walikuwa
makafiri na wanafiki
walioritadi baada ya
kifo cha Mtume. Hili linasemwa wazi na
wengi wa wanazuoni
wa Kishia.
Vitabu vya Shia kikiwemo
kitabu cha Al-Kulayn vinasema
kuwa Swahaba waliritadi wakamkufuru Allah, wakarudi katika
ujahiliya, isipokuwa saba tu! Hii
ina maana kuwa waumini katika
Maswahaba baada ya Mtume kufa
walibaki saba tu. Hawa ni wachache mno.
Kwa nini basi hao walioritadi
wasiwavamie na kuwashambulia
hao wachache wanyonge, na kuwauwa wote? Na kwa nini basi
hawa walioritadi haikurudi
kwenye ukafiri na ujahiliya kama
walivyokuwa babu zao na baba
zao?
Mpenzi msomaji, Shia wanaamini kuwa Ali (Allah amridhie) ni bora kuliko mwanae Hussein, na iwapo hali iko hivyo ni
kwa nini hawamlilii kwa kukumbuka kuuawa kwake kama ambavyo wanalia kwa Hussein, nae
(Ali) aliuwawa kama alivyouwawa
Hussein (Allah amridhie)?
Vilevile, kwa nini Shia hawalii
kwa ajili ya Mtume Muhammad
(rehema na amani ya Allah
zimshukie) wakajitoa damu na
kutoa rambi rambi kwa ajili yake,
hali yeye ni Mtukufu zaidi ya wote
na hali yeye aliuwawa kwa kupewa
sumu na Mayahudi.
Kwa nini msiba wao huu wanauita Husayniyaati wasiunasibishe kwa Imamu wao wa kwanza
Ali na ukaitwa, Alawiyaati au
Mtume Muhammad (rehema na
amani ya Allah zimshukie) ukaitwa, Muhamadiyaati?
Kwa nini wanaunasibisha kwa
Hussein? Kwa nini hawafanyi
Husayniyaati aina nyingi au sehemu za kupokea rambi rambi,
wawe pia na Alawiyaati na Muhamadiyaati. Kwa nini hawafanyi
hivyo?
Mpenzi msomaji, Shia wanadai kuwa haikamiliki imani ya mtu
mpaka aamini katika uimamu wa
Ali na wanawe baada yake, na
kwamba asiyeamini hivyo amekufuru na anastahiki Jahanamu. Vitabu vya maimamu wa Kishia

vinadai hata kama mtu huyo


atashuhudia hapana Mola apasaye
Kuabudiwa kwa haki ila Allah na
Muhamad ni Mtume wake, akasimamisha Swala akatoa Zakka,
akafunga mwezi Ramadhani na
akahiji nyumba Tukufu -haitoshelezi mpaka aamini katika uimamu wa Ali na wanawe baada
yake. Hii ni Itikadi ya Shia.
Lakini kwa nini nguzo hii
kubwa haijabainishwa katika
Quran Tukufu - iwapo kweli asiyeamini katika uimamu hatanufaishwa na Shahada, Swala, Swaumu, Zakka wala Hijja. Kwa ukubwa na utukufu wa suala hili la uimamu, kwa nini halikutajwa katika Kitabu cha Allah wazi wazi na
ilihali Allah katika Quran Tukufu
ameweka wazi nguzo na wajibu
kama Swala Zakka, Swaumu na
Hijja?
Iweje Allah asibainishe hili hali
ameweka wazi katika Quran hata
baadhi ya yaliyoruhusiwa (Mubahaat) kama kuwinda? Ipo wapi
hiyo nguzo kubwa ya kuamini katika uimamu wa Ali (Allah amridhie)? Uko wapi uzito huu
mkubwa? Uimamu huo kwa nini
haujaletwa wazi katika Quran ikiwa una kiwango hiki cha utukufu na umuhimu katika dini ya Allah. Tunataka jawabu juu ya hili.
Mpenzi msomaji, kutokuwepo
kwa ushahidi huo ni sababu
kubwa inayowafanya Shia kudai
kuwa Quran imeondolewa baadhi ya Aya na imebadilishwa baadhi ya Aya wakati wa Abubakr na
Umar.
Kwa mfano wanapokea kwa
Abuu Jaafar kuwa aliulizwa kwa
nini Ali aliitwa Amirul Muumiinina? Naye alijibu: Allah ndiyo ali-

ATHARI NA
HADITHI ZA
KISHIA NI
NYINGI KATIKA
KUWATUSI
MASHEIKH
WAWILI
ABUBAKR NA
UMAR (ALLAH
AWARIDHIE)
NA KUDAI
KUWA WAO
WALIPONDOA
NA WALI
BADILISHA
KITABU CHA
ALLAH.
yemwita na hivi ndivyo alivyoshusha katika kitabu chake, Na pale
Mola wako alipowaleta katika wanadamu kutoka migongoni mwao
kizazi chao, na akawashuhudisha
juu ya nafsi zao, akawaambia je,
Mimi si Mola Mlezi wenu? Na ya
kuwa Muhammad ni Mtume
wangu na Ali ni Amiri wa Waumini. Hili ni limo katika usuul
Al-Kaafii (1:412).
Al-Kulayn naye alisema katika
tafsiri yake ya Aya: Basi wale waliomuamini yeye (Quran, 7:157)
yaani: Maimamu. Na wakamheshimu, na wakamsaidia, na
wakaifuata nuru iliyoteremshwa
pamoja naye; hao ndiyo wenye
kufanikiwa. (Quran, 7:157) yaani! ambao wamejiepusha na
kuabudu masanamu. Hii ni kauli

ya Al-Kulayni.
Kisha anasema Jibti na Twaghuti ni fulani na fulani. Hili limo
ndani ya Al-Kaafii ukurasa wa
429. Tazama katika kitabu cha AlKaafii hakutaja majina ya haya
Matwaghuti mawili kwa sababu
Al-Kulayn, (mwandishi wa kitabu
hicho) alikuwa wakati wa udhaifu
na unyonge.
Yeye, Muhammad bin Yakub
Al-Kulayni akasema: Fulani na
Fulani wakati ambapo Al-Majlisiy Sheikh wa dola ya Swafawiyah katika wakati wa nguvu na ulinzi alisema katika kitabu chake,
Bihaar-ul-Anwaar Juzuu 23
ukurasa wa 306, Muradi wa Fulani na Fulani ni Abubakr na
Umar(Allah awaridhie). Na hivi
ndivyo Al-Majlisiy alivyoona kuwa
Umar na Abubakr (Allah awaridhie) ni mashetani, (Allah
atukinge na upotofu huu.)
Imekuja katika tafsiri yake kwa
kauli ya Allah: Wala msifuate
nyayo za Shetani. Hakika yeye ni
adui yenu aliye dhahiri. (Quran,
2:168). Wamesema: Hatua za
shetani wallahi ni utawala wa fulani na fulani.
Na imepokewa kuwa Abuu
Abdillaahi amesema: Na mwenye
kumtii Allah na Mtume wake katika utawala wa Ali hakika huyo
amefuzu kufuzu kukubwa.
Amesema: Hivi ndivyo ilivyoshuka. Hili limo ndani ya Usuul-ulKaafi, juzuu ya kwanza ukurasa
wa 314.
Kadhalika imepokewa kutoka
kwa Abuu Abdillahi amesema: Jibrili alishuka kwa Muhamad na Ahli zake kwa aya hizi,
Enyi mliopewa kitabu aminini
yaliyoteremshwa kwa Ali ni nuru

iliyo wazi. Hili limo ndani ya Usuulul Kaafi Juzuu ya 7 ukurasa wa


66. Athari na hadithi za Kishia ni
nyingi katika kuwatusi Masheikh
wawili Abubakr na Umar (Allah
awaridhie) na kudai kuwa wao
walipondoa na walibadilisha kitabu cha Allah.
Hapa kuna swali au mushkeli
kwa Mashia wenye akili ili watafiti
ndani yake. Ikiwa Abubakr na
Umar (Allah awaridhie) wamepondoa Kitabu cha Allah katika
Aya hizi, basi kwa nini Ali (Allah
amridhie) hakuzinyoosha baada
ya kuwa Khalifa wa Waislamu
kwa kuweka wazi jambo hili.
Kwa nini hakusema wakati wa
ukhalifa wake hali akiwa mtawala
na nguvu zake, na baada ya kufa
Abubakr na Umar (Allah awaridhie). Kwa nini hakusema: Abubakr na Umar wamepondoa na
kuibadilisha Quran hii, na usawa
ni kadha wa kadha katika dini ya
Allah?
Kwanini hakuzirudisha Aya
hizi katika Quran kama zilivyoteremshwa? Hili ni wajibu kwake,
bali hili ni faradhi katika faradhi
zilizo juu yake kurudisha yaliyopondolewa na kubadilishwa katika aya za kitabu cha Allah baada
ya mauti ya Abubakr na Umar
(Allah awaridhie) ambao wamepondoa hiki kitabu kama wanavyoitakidi wanazuoni wa Shia. Kwa
nini hakufanya hivyo?
Mpenzi msomaji, mwanachuoni wa Kishia, Abul Faraj Al-Asfahany ametaja katika Maqaatil
Twaalibiyn ukurasa wa 88, 142 na
188 chapa ya Beiruti na Al-Arbaly
pia ametaja hivyo katika Kaashiful-Ghummah Juzuu 2 ukurasa
wa 66 na Majlisy katika, Jalaa-ulUyuun ukurasa wa 582 kuwa
Abubakr bin Ali bin Abi Twaalib
alikuwa ni miongoni mwa waliouawa katika mkasa wa Karbala.
Hawa wanazuoni watatu wa
Kishia wametaja katika vitabu
vyao kuwa Abubakr bin Ali bin
Abi Twaalib ni miongoni mwa
waliouwawa katika Karbala
pamoja na ndugu yake Hussein na
vile vile ameuawa pamoja na mtoto wa Hussein bin Ali ambae jina
lake ni Muhamad Al-Asghar aliyekuwa maarufu kwa kun-ya ya
Abubakr. Wote hao waliuawa
pamoja na Hussein.
Utata na Swali: Kwa nini wanazuoni wa Kishia wanaficha
jambo hili kwa wafuasi wao, wala
hawatilii mkazo isipokuwa kifo
cha Hussein? Je ni kwa kuwa
wana jina la Abubakr na wao daima wanatoa dalili ya ukafiri wa
Abubakr ? Umoja gani wa Sunni
na Shia?

Itaendelea

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

Al-Azhar yakanusha uvumi


dhidi ya Answar Sunnahh
Wafitini waumbuka mchana kweupe
Mahasidi wa Saudia aibu tupu
Wiki mbili
tu baada
ya Katibu
Mkuu wa
Idara ya
Utafiti wa
Kiislamu
wa Chuo
Kikuu cha
Kiislamu
cha AlAzhar nchini Misri,
Dkt. Muhyiddiyn Afify
kuilaani
Iran kwa
kuingiza
siasa katika mambo
ya Hijja,
chuo hicho
kimeendelea kukanusha uvumi dhidi ya
Answar
Sunnah.

Safari tamko limetolewa na


Makamu Mkuu wa Al-Azhar
Sharifu, Dkt. Abbas Shawmani
ambaye amenukuliwa na vyombo vya habari, akihoji: Kama
Saudia si miongoni mwa Ahlu
Sunnah Wal-jamaa, basi ni nani
SHEIKH MUHAMMAD ISSA
aliye katika Ahli Sunnah wal
Jamaa?
lakini alisisitiza Hakika hotuba yake
Dkt. Shawmani amesisitiza kwamba iliwatendea haki watu wote na ilikuwa
Al-Azhar Sharifu inatambua kuwa wazi na yenye kufahamika na kwamba
Saudia ni Dola ya Kiislamu muhimu na lawama kuhusu tamko la kongamano
kitovu cha Ahlu Sunnah wal Jamaa na hilo zisielekezwe kwa Al-Azhar.
kwamba ni upuuzi mtupu kudai kuwa
Pamoja na hayo Al-Azhar ilifanya
Saudia ambayo ni mlinzi wa miji miwili haraka kubainisha msimamo wake na
mitakatifu siyo Ahlu Sunnah wal Jamaa kuzuia masuala yasichupe mipaka amna kwamba hilo halipo katika fikra ya bapo mashekhe waliafikiana na sekrewanawazuoni wa Al-Azhar. Makamu tarieti ya kongamano na kuitaka kuruMkuu huyo wa Al-Azhar alikanusha dia maandiko ya tamko la mwisho ili
madai yaliyosambazwa kutoka konga- kuepuka malumbano na walikubali na
mano la Chechnya kwamba Saudia na marekebisho yakafanyika. Na wakati
madhehebu ya Answar Sunnah am- huo huo, chanzo kutoka chuo cha Albayo wapinzani wao huyaitwa Wahabi- Azhar Sharifu kilikanusha yaliyotamya si katika Ahlu Sunnah.
kwa kwa ulimi wa waliyemuita MwaKwa kuwa Saudia ni dola la Kiisla- na-Azhar Majhuul yaani Mwanamu muhimu sana tena katika kitovu Azhar asiyefahamika kupitia video ilicha Ahlu Sunnah wal Jamaa, litakapo- yoenea katika mtandao wa kijamii.
toka tamko lolote kutoka kwa yeyote
Katika video hiyo, mtu huyo alidai
yule kinyume na hivyo ni aibu juu ya kwamba eti Fadhwilat Sheikhul Azmtu huyo na si tamko la Al-Azhar, na Azhar, Dkt. Ahmad At-twayyib, mara
tamko hilo haliidhuru Saudia wala tu aliposhika ukuu wa chuo hicho alhaliiwajibikii Al-Azhar, aliongeza.
ianzisha Jopo la kupambana na WaNa katika kujibu tamko la Chechnya habiya katika Al-Azhar Sharifu. Chanlenye kughadhabisha, la ubabaishaji na zo hicho kilisema: Hakika kilichoko
mkanganyiko, Dkt. Shawmani aliweka katika video hiyo uzushi na uongo wa
wazi kwamba Sheikhul Al-Azhar hak- wazi kabisa na wala hauna msingi
wenda kushiriki kongamano hilo. Al- wowote wa ukweli na wala haustahiki
ieleza kwamba yeye alikwenda ziarani kujibiwa.
nchini Chechnya kwa mwaliko wa Rais
Chanzo hicho kikaongeza kusema
wa nchi hiyo, na kwamba Sheikhul Al- kwamba pamoja na hayo, watampeleAzhar pia hakuhuhduria kongamano kea Fadhwilat Sheikhul Al-zhar video
hilo lote isipokuwa kikao cha ufunguzi hiyo alipo katika mji aliozaliwa mkoani
pekee.
Al-Aqswar Kusini mwa Misri ili aone
Dkt. Shawmani alisema tuhuma zi- kama uzushi huo unastahiki kujibiwa.
nazoelekezwa kwa Al-Azhar zinanasiAkizungumzia kuhusu lengo la vidbishwa na hotuba ya Sheikhul Al-Azhar eo hiyo, chanzo hicho kilisema: Sidha-

Dkt Abbas Shawmani

ni kama kuna lengo jingine zaidi ya kufarakanisha kati ya wanawazuoni wa


umma lakini hilo haliwezi kutokea
kamwe. Kisha akasisitiza uzito wa mafungamano ya kihistoria yanayofungamanisha kati ya Al-Azhar Sharifu na
Saudi Arabia chini ya uongozi wenye
hekima wa Mtumishi wa Misikiti miwili mitakatifu, Mfalme Salman ibn
Abdilaziz.
Akasema Na anayoyatoa (Mfalme
Salman) katika msaada hayana mpaka
kwa Al-Azhar na taasisi zake zote kwa
lengo la kusambaza mafundisho sahihi
ya dini na kukabiliana na mawimbi ya
ufurutu dini na ugaidi.

Hebu tujadili:
Katika gazeti la Mizani toleo namba
212 la Septemba 9, 2016, paliandikwa
makala isiyo na jina la mwandishi chini
ya kichwa cha habari: Kongamano la
Maulamaa laukana Uwahabi-Ladai si
katika madhehebu ya Ahlu Sunnah.
Katika makala hiyo paliandikwa
hivi: Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Ahmad At-Tayyib alidaiwa kushiriki katika maamuzi ya kuwatoa Answar Sunnah kuwa si katika Ahlu Sunnah wal
Jamaa. Madai haya si mageni kwani ni
maarufu katika gazeti la Mizani kupitia
makala inayoandikwa na Mudir wa
Abudharr Muslim Mission, Dar es Salaam, ambayo ni kituo cha Mashia.
Alhamdulillahi, chuo cha Al-Azhar
Sharifu kimetoa msimamo wake
kwamba Saudi Arabia ni kitovu cha
Ahlu Sunnah wal Jamaa kama jibu kwa
wafitini hawa wa Kishia ambao daima
hawaishi njama za kuwagawa Ahlu
Sunnah wal Jamaa.
Mashia wanajua fika kwamba kama
Ahlu Sunnah wal Jamaa watabakia
kuwa Jamaaa yaani kundi moja kama
jina lao lilivyo, mikakati yao ya kuueneza Ushia katika nchi za Kisunni hauwezi kufanikiwa.

Nongwa za Mashia dhidi


ya Answar Sunnah
Nongwa za Mashia dhidi ya Answar
Sunnah ni za tangu zama za kale enzi

zile za Sheikhul Islaami Ibn Taymiyya


ambao wao humuita muasisi wa itikadi
za Uwahabi.
Ibn Taymiyya anajulikana kwa
mapambano yake dhidi ya mashia.
Miongoni mwa kauli za Ibn Taymiyya
kuhusu Mashia inayowafanya
wamchukie yeye ni hii hapa: Na
Raafidhwah yaani Mashia wana bida
kubwa kuliko Makhawaarij na wao wanawakufurisha wale ambao Makhawaarij hawakuwakufurisha kama vile
Abubakr na Umar.
Na wanatunga uongo dhidi ya
Mtume wa Allah na Maswahaba, uongo ambao hakupata kuutunga yeyote
mfano wake na Makhawaarij hawatungi uongo kama huo.
Na wao (Mashia) ni wenye kuwasaidia makafiri dhidi ya Waislamu
kwani tumeona Waislamu wanaposhambuliwa na adui kafiri wao
(Mashia) huwa pamoja naye dhidi ya
Waislamu kama ilivyokuwa kwa Genghizi Khan Mfalme wa Watartar
makafiri kwani Mashia walimsaidia
dhidi ya Waislamu.(Tazama Minhaaj
As-Sunnahh, mjalada 5/154).
Alipokuja Sheikhul Islami Muhammad ibn Abdil-Wahhab, ambaye kwa
jina lake ndiyo MASHIA huwaitwa
Answar Sunnah Wahabiya, akashika
mwenendo wa Ibn Taymiyya katika
kuwakabili Mashia.
Na Answar Sunnah yoyote, popote
pale alipo miongoni mwa wajibu wake
katika kuzinusuru Sunnah za Mtume
Muhammad (rehema na amani ziwe
juu yake) ni kukabiliana na itikadi
potofu za Kishia. Katika Ahlu Sunnah
wal Jamaa, hakuna watu walio mstari
wa mbele katika kukabiliana na Mashia
kama Answar Sunnah na ndiyo maana
utaona wabaya wa Mashia ni Answar
Sunnah.
Moja ya mbinu yao ya kuvunja nguvu ya Answar Sunnah ni kufarakanisha
baina yao na Ahlu Sunnah wal Jamaa
wenzao. Kwa hiyo tamko la kizandiki la
Grozny lililoshangiliwa sana na gazeti
la Mizani lilikubaliana na malengo na
mikakati ya Mashia.
Na kwa kuwa Saudi Arabia ni nchi
ya Kiislamu ya Ahlu Sunnah wal Jamaa
yenye msimamo wa Ki-Answar Sunnah, ndiyo utaona kila wakati Mashia
wanashambuliaa Saudi Arabia sambamba na Answar Sunnah.
Tamko la Dkt. Shawmani wa AlAzhar Sharifu limewaumbua maadui
wa Ahlu Sunnah wal Jamaa na porojo
yao ya kuwatoa Answar Sunnah katika
Ahlu Sunnah, ingawa pamoja na
ubainifu huu, kamwe watu hawa hawataacha kuwashambula ma-Answar
Sunnah na kuendelea kudai kuwa hao
siyo Ahlu Sunnah wal Jamaa.
Ni vema Masunni tukagundua
mkakati wa Mashia wa wagawe uwatawale. Wao huwatuhumu Answar Sunnah kwa kuwafarakanisha Waislamu
wakati wenye mwenendo huo ni
Mashia.
Al-Azhar imekiri wazi mchango wa
Saudi Arabia kwa Ahlu Sunnah na jinsi
ambavyo nchi hiyo inavyoisaidia AlAzhar Sharifu kama Masunni wenzao
na kwamba Saudi Arabia ni kitovu cha
Ahlu Sunnah wal Jamaa. Ukweli ndiyo
huo na unapaswa usemwe ili mwenye
moyo wa kuelewa aelewe, mwenye
masikio ya kusikia asikie na mwenye
macho ya kuona aone ingawa maadui
wa Ahlu Sunnah wal Jamaa watachukia.
Makala katika gazeti la Mizani, Mawahabi si Masunni Kamwe iliandikwa
na Mashia ingepaswa iwazindue
Masunni kwamba tangu lini Mashia
wakawasemea Masunni? Haya,
Masunni kupitia Chuo chao Kikuu
mashuhuri cha Al-Azhar Sharifu
wameshatoa fatwa kwamba, Ma-Answar Sunnah wao huwaita Mawahabi
ni Masunni kindakindaki.

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

10

11

Vipi umma uyakabili matukio ya ushindi na kushindwa?


SEIF RUGA

akika mtu mwenye tafakuri ya


ndani kabisa kuhusiana na
mwenendo wa umma wa Kiislamu tangu Alfajiri ya Uislamu
hadi zama zetu hizi za leo, ataona historia imesheheni matukio mengi ya
ushindi na vilevile matukio ya
kushindwa na kukandamizwa kwa
umma huu wa Kiislamu.
Kushindwa kwa umma kunajiri
pale ambapo umma unapokuwa
mbali na Muumba wake. Katika zama
zetu hizi umma unahitaji mtu atakayeurudishia hadhi yake iliyokuwa nao
wakati wa zama za Alfajiri ya Uislamu
na kuuweka katika njia iliyonyooka
kwa kupitia njia walizopitia watu
wema waliotangulia.
Allah Taala anasema: Hakika
Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko
kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao. (Quran, 7:11).
Umma wa Kiislamu una mfumo na
desturi yake katika namna ya kuyakabili matukio, aidha ya kupata nusura
au kushindwa.

Tukio la ushindi
Ikiwa ni kwa sura ya kwanza, yaani
kupata ushindi, hilo ni jambo la kushukuriwa, kumnyenyekea yule aliyeneemesha jambo hilo, naye si
mwingine bali ni Allah Taala. Ni yeye
Allah anayeunusuru umma wake dhidi adui zake. Hakika, La haula wala
kuwwa illa billahi..
Allah Taala anasema: Na
Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila
kuwa ni bishara kwenu, na ili nyoyo
zenu zipate kutua. Na msaada hautoki
isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka.. (Quran, 3:126).
Akikunusuruni Mwenyezi Mungu
hapana wa kukushindeni na akikutupeni ni nani basi baada yake
atakayekuwanusuru?(Quran,
3:160).
Yapaswa tufanye kama Mtume (rehema na amani za Allah ziwe juu yake)
alivyofanya wakati wa ufunguzi wa
mji wa Makka. Aliingia huku akinyenyekea na kumshukuru Mola wake
kwa kusoma suratul- fat-hi. Abdillahi
ibn Maghfal anasema: Nilimuona
Mtume wa Allah siku ya ufunguzi wa
mji wa Makka akiwa juu ya ngamia
huku akisoma suratul-fat-hi.

Tukio la kushindwa
Na ikiwa ni kwa sura yapili, yaani
tukio la kushindwa, basi yatupasa
kuthibiti na kujizatiti katika kulazimiana na mafundisho ya Uislamu kwa
kuyahubiri bila ya kubadilisha na hususan katika maudhui zinazohusiana
na mambo ya itikadi na kadhia zinazohusu umma wa Kiislamu, hasahasa
uwekaji msisitizo katika masuala yanayohusu mfumo wa kielimu (mitaala.).
Kushikamana na Uislamu na imani ndiyo njia pekee ya kupata nusura
ya uhakika kwani si lazima ushindi
siku zote upatikane kwa njia ya kupigana.
Allah Mtukufu anasema kumwambia Mtume wake(rehema na amani za
Allah ziwe juu yake) na Maswahaba
wake watukufu, baada ya kumalizika
vita vya Uhud ambavyo Waislamu
walishindwa: Makundi mawili mion-

MTU ANAYEIDURUSU VIZURI


SERA NA MWENENDO MZIMA
WA MTUME (REHEMA NA
AMANI ZA ALLAH ZIWE JUU
YAKE), ATANGAMUA NI JINSI
GANI MTUME ALIKABILIANA
NA MATUKIO KAMA HAYA,
NA NI JINSI GANI ALIKUWA
AKIWANASUA MASWAHABA
WAKE (ALLAH AWARIDHIE
WOTE) KUTOKA KATIKA KIPINDI
CHA SHIDA NA MATESO NA
KUWAPELEKA KATIKA HALI YA
FARAJA NA NUSURA.

KUSHIKAMANA
NA UISLAMU
NA IMANI
NDIYO NJIA
PEKEE YA
KUPATA
NUSURA YA
UHAKIKA
KWANI SI
LAZIMA
USHINDI
SIKU ZOTE
UPATIKANE
KWA NJIA YA
KUPIGANA
goni mwenu yakaingiwa na woga
kuwa watashindwa na hali Mwenyezi
Mungu ndiye Mlinzi wao, na waumini
wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.
(Qur-an, 3:122)
Basi msiregee na kutaka suluhu,
maana nyinyi ndiyo mtakaoshinda.
Na Mwenyezi Mungu yu pamoja
nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya
vitendo vyenu. (Quan, 47:36).
Na kwa upande mwingine, hakika
sisi tunashuhudia Waislamu wengi,
pindi umma wao unapopatwa na
matatizo ya kushindwa, kufeli katika
majambo - baadhi yao hunyongonyea
na kukata tamaa haraka au kushikwa
na ganzi, na midomo yao haiachi
kutaja matukio yaliosababisha
washindwe au kutaja matukio yaliyowahuzunisha, bila ya kuonesha dira
au njia mbadala itakayoleta tija na
ufumbuzi, utakaoutoa umma kutoka
katika lindi la udhalili na kushindwa.
Katika hali kama hiyo, wapo baadhi yao walio tayari kujiunga na madhehebu au mitazamo potofu, wakidhani kwamba kufanya hivyo ni njia
mbdala itakayowanasua na matatizo
au kuwatoa katika hali ya majonzi na
huzuni..
Mtu anayeidurusu vizuri sera na
mwenendo mzima wa Mtume (rehema na amani za Allah ziwe juu yake),
atangamua ni jinsi gani Mtume alikabiliana na matukio kama haya, na ni
jinsi gani alikuwa akiwanasua Maswahaba wake (Allah awaridhie wote)
kutoka katika kipindi cha shida na
mateso na kuwapeleka katika hali ya
faraja na nusura.
Ipo mifano mingi katika sira na
mwenendo wa Mtume (rehema na
amani za Allah ziwe juu yake) inayoakisi taswira hiyo.

Mifano katika sira ya


Mtume
Imepokewa kutoka kwa Khabbabu
bin al-Arrat (Allah amridhie) amesema: Tulishtaki kwa Mtume wa Allah
huku akiwa nguo yake ameiegemeza
katika kivuli cha Al-Kaaba tukamwambia, Hivi ni kwa nini
hutuombei kwa Allah Taala?!
Mtume akasema, Huko nyuma
watu waliokuwa kabla yenu ilifikia
hali mtu huchimbiwa shimo katika
ardhi, kisha hutumbukizwa ndani

3. Safari ya Mtume Taif

yake, halafu huletwa msumenu na kupasuliwa pande mbili kuanzia


kichwani mwake, yote hayo hayamfanyi aiache dini yake.
Aidha, mtu huyo huparurwa kwa
shanuo la chuma linalokwangua nyama na mifupa yake, yote hayo hayamfanye aikane dini yake, naapa kwa Allah yeye ndiye atakayeitimiza dini hii,
hadi ifikie hali mtu anayetembea kwa
mguu kutoka Sanaa hadi Hadharamauti haogopi tishio lolote isipokuwa
Allah Taala au mbwa mwitu kushambulia kondoo wake. Tatizo liliopo hapa
ni moja tu, nyinyi mna haraka na kiherehere. (Bukhari).
Ufafanuzi wa hadithi hii ya Mtume
Khabbabu(Allah amridhie) hakumuuliza Mtume (rehema na aman za
Allah ziwe juu yake) jambo la haramu,
bali alichotaka kutoka kwa Mtume ni
dua ya kunusuriwa kwa sababu ya
madhila na nakama wanazozipata
kutoka kwa washirikina wa Makka.
Pamoja na hivyo, tunamuona
Mtume anaghadhibika na uso wake
kuwa mwekundu. Hivi ni jambo gani
lililomfanya Mtume aghadhibike?
Kile ambacho kilimfanya Mtume akasirike-Allah Mtukufu ndiye mjuzi zaidi ni mambo mawili.
Mosi, ni hali ya uharaka aliyoiona
kutoka kwa Khabbab na wenzake (Allah awaridhie wote) kwa ushahidi wa
kauli ya Mtume mwisho wa hadithi:
Lakini nyinyi mna haraka. Pili, ni
kutegemea miujiza ambayo itapatikana kupitia dua ya Mtume (rehema na
amani za Allah ziwe juu yake).
Aidha, tunashuhudia kupitia hadithi hii Mtume akiwachorea ramani

Mji wa Baghdad
ukiwa
umeangamizwa
na majeshi
washirika
wakiongozwa na
Marekani.

Khabbab na wenzake kutoka katika


taswira ya hali ambayo wanaiishi
nayo ya mateso, mbinyo na madhila
na kuwapeleka katika taswira isiyolingana na hali yao hiyo ya kaumu ya
watu wa umma waliokuwa kabala
yetu, kiasi ambacho mtu huparurwa
kwa shanuo la chuma katika nyama
na mifupa ya mwili wake, lakini hilo
wala hilimfanyi mtu huyo aikane dini
yake, na hutupwa katika shimo kisha
hupasuliwa kwa msumeno, na hilo
pia halimfanyi aachane na dini yake.
Aidha, Mtume alimpeleka
Khabbab na wenzake katika taswira
nyingine, nayo ni dini hii kupata nusura, kiasi kwamba msafiri anayetembea kwa miguu ataweza kusafiri kutoka Sanaa hadi Hadharamauti-na ni
masafa marefu- hana shaka ya hofu
yoyote isipokuwa Allah Taala na
mbwa mwitu kushambulia kondoo
wake.
Lakini ili kufikia hali hiyo, subira
inahitajika na kujituma na wala hakuna shaka ya kwamba njia ya kupata
nusura na ithbati haikutandikwa
zulia la maua mazuri au kurashiwa na
uturi.
Tuchukulie kwamba Mtume (rehema na amani za Allah ziwe juu
yake) aliwaombea mabaya makafiri
wa ki- Quraishi wakaangamizwa
wote, kupitia dua ya Mtume na ushindi ukapatikana kwa wepesi kabisa,
na wala hakuna juhudi zozote zilizotolewa katika kufanikisha ushindi
huo, juhudi ambazo zinalingana na
thamani ya ushindi wenyewe au amani hiyo!
Ushindi wa aina hii ni haraka sana
kutoweka na kuondoka. Kwa kawaida

ushindi wowote unaokuja kwa wepesi


bila ya juhudi, mfano ushindi uliopatikana kwa njia ya kimiujiza ya dua ya
Mtume, hautathaminiwa na kupewa
uzito wake au kuenziwa ipasavyo.

Kisa cha Banii Israili


Ndugu yangu msomaji, hebu
chunguza kwa makini kisa cha Banii
Israili. Allah Taala alivyowahakikishia wao nusura kubwa nayo ni
kuangamia kwa adui yao mkubwa na
muovu Firauni, ambaye alikuwa akiwatesa kwa aina mbalimbali za adhabu kali,kama Allah Mtukufu anavyolithibitisha.
Hakika Firauni alitakabari katika
nchi na akawagawa wananchi
makundi mbalimbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na
akiwaacha watoto wao wanawake.
Hakika yeye alikuwa katika mafisadi.
Na tukataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe viongozi na kuwafanya
ni warithi. (Quran, 28:4).
Banii Israili walipatiwa nusura bila
juhudi juhudi yoyote, na haukupita
muda wakajisahahu na kumuasi Allaa Taala. Allah Taala aliwapasulia
wao bahari pande mbili, kila upande
mmoja ukawa kama mlima mkubwa.
Ili kuwanusuru na adui yao mkubwa
Firauni.
Tulimletea wahyi Musa tukamwambia, Piga bahari kwa fimbo
yako. Basi ikatengana na kila sehemu
ikawa kama mlima mkubwa.
(Quran, 26:63). Na Allah Mtukufu
akamwokoa Mtume Musa na wafuasi
wake, akawatengenezea wao katika

bahari njia kavu, wanayotembea kwa


miguu bila ya kuwa na hofu ya yule
anayewafutilia nyuma yao.
Allah amesema: Na tulimfunulia
Musa, Toka usiku na waja wangu, na
uwapigie njia kavu baharini. Usikhofu kukamatwa, wala usiogope.
(Quran, 20:77). Na baada ya Banu
Israili kuvuka bahari kwa salama,
huku Allah akimwangamiza adui yao
Firauni na jeshi lake na huku wao
wakitazama.
Tukawavusha baharini Wana wa
Israili, na Firauni na askari wake
wakawafuatia kwa dhuluma na uadui. Hata Firauni alipo kuwa anataka
kuzama akasema, Naamini kuwa
hapana Mungu ila yule waliye mwamini Wana wa Isarili, na mimi ni
miongoni mwa walionyenyekea
(Quran, 10:90).
Na baada ya muujiza huu mkubwa
na ushindi wa wazi na kabla ya miguu
yao haijakauka maji ya bahari, walimwambia Mtume wao (amani ya Allah iwe juu yake): Tujaalie na sisi
tuwe na Miungu kama wale walivyojifanyia Miungu.
Allah Taala anasema: Na tukawavusha baharini Wana wa Israili,
wakafika kwa watu wanaoabudu masanamu yao. Wakasema, Ewe Musa!
Hebu tufanyie na sisi miungu. Musa
akasema, Hakika nyinyi ni watu msio
jua kitu. (Quran, 7:138).
Hebu tazama jinsi Banii Israili
walivyoshindwa kuuthamini na kuuenzi ushindi mkubwa waliopatiwa na
Allah na kujisahau hadi wakataka
kwa Mtume wao (amani ya Allah iwe
juu yake) awape wao ruhusa ya kufanya ushirikina.

Mtume(rehema na amani za Allah


ziwe juu yake) alitoka kuelekea sehemu ya watu wa Taif kwa minajili ya
kuhubiri na kufikisha dini ya Allah
Taala. Lakini alipofika huko walimpokea kwa kuyapinga mahubiri yake,
na wakawahamasisha watu wapumbavu mongoni mwao na kuanza kumpiga Mtume kwa mawe hadi akaghumiwa na kuchanganyikiwa. Hakurudi
katika hali yake ya kawaida hadi alipofika katika eneo la Kaurnuthaalib.
Bi Aisha (Allah amridhie )alimuuliza Mtume(rehema na amani za Allah ziwe juu yake): Je ishawahi kupitia siku nzito kushinda siku ya vita vya
Uhudi? Mtume akamjibu: Hakika
hakuna siku nzito niliyokutana nayo,
kama siku ya Taifa, kwani nilifadhaika
na sikujitambua hadi eneo la Kaurnuthaalib, nikainua kichwa changu,
ghafla nikaona kiwingu kimenifunika.
Nikatazama na kumuona Malaika Jibrili akiita kwa kusema, Hakika
Allah amesikia kauli ya jamaa zako na
kitendo walichokufanyia. Allah amemtuma kwako Malaika anayesimamia masuala ya majabali na milima ili
umwamrishe utashi wako kuhusu kitendo kiovu walichokufanyia jamaa
zako.
Malaika anayesimamia majabali
na milima akaniita na kunisalimia.
Kisha akasema. Ewe Muhammad
huu ni utashi wako wewe, kama ungelitaka ningewafunika wao na milima hii miwili.
Mtume(rehema na amani za Allah
ziwe Bali matarajo yangu kwa Allah
watu hawa watazaa viumbe watakaomwabudu Allah bila ya kumshirikisha na kitu kingne. (Bukhari 992,
Muslim3352).
Lau wakati huo Mtume (rehema
na amani za Allah ziwe juu yake) angelibweteka, haraka haraka bila ya
hata kuchelewa angelimtaka Malaika
wa masuala ya milima ambaye wakati
huo alikuwa karibu naye kuwafunika
kwa majabali hayo mawili, lakini
Mtume ameakisi kwetu sisi mfano
mzuri katika subira na ufufuaji wa
roho ya matumaini, na akatufungulia
sisi nuru ya matarajio.

4. Hijra ya Mtume
Habari za kuhama kwa Mtume

(rehema na amani za Allah ziwe juu


yake) pamoja na Abuubakr Assidik
(Allah amaridhie) kutoka Makka na
kwenda Madina ziliwafikia makafiri
wa Ki- Quraishi wakatangaza zawadi
nono ya mtu atakayemsalimisha Muhammad mikononi mwao, au hata
kuonesha njia ya kukamatwa kwake
tu.
Mtu huyo angezawadiwa kitita cha
ngamia mia moja. Kwa kadari ya Allah Mtukufu, Suraka bin Malik aliijua
njia aliyoifuata Mtume na Abubakri.
Mtume akamwambia Suraka baada
ya kuwakaribia: Hivi unataraji siku
moja nawe uwe ni miongoni mwa
watu waliovaa vikuku -vito vya thamani vya Mfalme Kaizar?!
Mtume aliyasema maneno hayo
kumwambia Suraka mwenye uchu
wa kupata zawadi ya ngamia mia
moja, huku akiukimbia mji wa Makka
na nyuma yake akifukuzwa na
Makafiri wa Kiquraishi!!
Katika hali isiyo ya kawaida, katika
kipindi hicho kizito na chenye misukosuko anamsihi Suraka bin Malik
kumwachia na kumwahidi kuanguka
kwa ufalme wa Kaizar na himaya
yake kubwa sana kwa wakati huo.
Suraka bin Malik (Allah amridhie)
akamuuliza Mtume kwa mshangao
mkubwa: Himaya ya Mfalme Kaizar
bin Hurmuz?! Huyu Kaizar bin Hurmuz ninayemjua mimi?! Haikupitia
kabisa akilini mwa Suraka (Allah amridhie) kwamba atakuja kuyaona
mapambo ya thamani ya Mfalme Kaizar, sembuse kuja kuyavaa!

5. Vita ya Ahzab
Tukio la vita vya Ahzab ni tukio
huenda linaakisi vizuri hali tuliyokuwa nayo hivi sasa, wakati makundi
ya makafairi yalipojikusanya pamoja
dhidi ya Waislamu, na wakawazunguka Waislamu kama bangili izungukavyo mkono, kwa lengo la kumua
Mtume na kuongoa mzizi wa Uislamu na Waislamu,
Quran imeeleza kwa ufasaha tukio
hili, pale Allah Taala aliposema:
Hapo ndipo waumini walipojaribiwa
na wakatikiswa mtikisiko mkali. Na
waliposema wanafiki na wale wenye
maradhi katika nyoyo zao, Mwenyezi
Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu.
Na kundi moja katika miongoni
mwao lililoposema, Enyi watu wa

Yathrib! Hapana kukaa nyinyi! Rudini. Na kundi jingine miongoni mwao


likaomba ruhusa kwa Mtume kwa
kusema, Hakika nyumba zetu ni
tupu. Wala hazikuwa tupu. Hawakutaka ila kukimbia tu.
Na lau kuwa wangeliingiliwa kwa
pande zote, kisha wakatakiwa kufanya hiana, wangelifanya na wasingelisita ila kidogo tu. Na hakika walikwisha muahidi Mwenyezi Mungu kabla
yake kwamba hawatageuza migongo
yao. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni
yenye kuulizwa (Quran, 11-15).
Katika kipindi hicho kigumu
chenye kuogofya, ambacho macho
yalifadhaika na nyoyo zikakurubia
kufika katika shingo, tunashuhudia
Mtume (rehema na amani za Alah
ziwe juu yake) akitoa mafundisho ya
kimalezi kwa Maswahaba wake katika kujenga imani juu ya ahadi ambazo ameziahidi Allah Taala, na si
vingine ni kujenga roho ya matumaini
na kuacha suala la kukata tamaa, na
kuacha kuwapa makafiri na wanafiki
ushindi wa mapema. Katika vita vya
Ahzab katikati ya uchimbaji wa
handaki, Maswahaba (Allah awaridhie) walikutana na mwamba mgumu. Barrau bin Azib amesema:
Mtume wa Allah alituamuru tuchimbe handaki, wakati wa kuchimba
ukaibuka mwamba usiokubali kupenya sururu ndani yake.
Kufuatia hali hiyo tukamweleza
Mtume (rehema na amani za Allah
ziwe juu yake). Mtume wa Allah akafika na kuweka nguo yake, kisha
akashuka kwenye mwamba, akachukua sururu kisha akasema, Bismilillahi na akapiga pigo moja, likavunja thuluthi ya mwamba huo, na
akapiga tena pigo lingine, likamalizia
thuluthi iliyobakia.
Mtume akasema Allahu akbar,
sasa nimepewa funguo za kuifungua
miji ya Fursi. Naapa kwa Allah! Hakika mimi ninaiona miji na kasri nyeupe kutoka hapa nilipo.
Kisha akasema, Bismilillahi Na
akapiga pigo lingine, akaungoa
mwamba wote. Akasema Allahu akbar. Nimepewa funguo za Yemen.
Naapa kwa Allah! Hakika mimi
ninaona milango ya Sanaa kutoka
hapa nilipo. (Ahmad, Hadithi
17946).
Hebu tazama jinsi gani Mtume huwatoa Maswahaba wake (Allah
awaridhie) katika hali hiyo nzito na ya
dhoruba na taabu kubwa, na kuwapeleka katika hali ya faraja na matumaini makubwa. Hivi kuna darasa
gani lenye kutoa matumaini na faraja
kushinda hili la Mtume?! Na kuna
somo gani kubwa linalojenga imani
ya kupata ahadi za Allah na nusura
yake kuliko hili la Mtume?!
Na kupitia kisa hiki cha Handaki,
wakati mateso yaliposhitadi kwa
Mtume (rehema na amani za Allah
ziwe juu yake) pamoja na Maswahaba
wake, baadhi ya watu walipatwa na
unafiki na wakazungumza maneno ya
kuudhi.
Aidha, Mtume ikamfikia habari ya
Mayahudi wa Banu Kuraidha kuvunja ahadi waliokubaliana pamoja
naye. Alivyoiona hali hiyo ya mateso
na balaa kwa watu, ikawa anawahabarisha kauli za faraja ili kuwasogezea watu taswira ya kupata nusura.
Mtume (rehema na amani za Allah
ziwe juu yake) akasema: Naapa kwa
yule ambaye nafsi ya Muhammad ipo
mikononi mwake, shida na balaa hizi
zitawaondokeeni. Hakika mimi ninataraji kutufu katika Al-Kaaba hali
yakuwa nipo salama.

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

12

AFYA YAKO
PAZI MWINYIMVUA

Usiyoyajua kuhusu virutubisho kutoka katika vyakula


MOJA ya
sababu ya
udumavu
wa mwili
na akili
kwa watoto na magonjwa
sugu kwa
watu wazima ni upungufu au
wingi wa
virutubisho
mwilini.
Watu wakiwa na ufahamu wa
kutosha
kuhusu
virutubisho
na namna
vinavyofanya kazi
mwilini
wanaweza
kuitikia
wito wa
kupambana na
udumavu
na magonjwa
sugu duniani na
hasa hapa
nchini.

Nini virutubisho na mahitaji yake mwilini


Tunapokula vyakula tunapata vitu
vinavyoitwa virutubisho au viini- lishe,
ambavyo kwa lugha ya kigeni vinaitwa
nutrients. Virutubisho vikuu ni wanga,
mafuta, protini, vitamini na madini. Katika vyakula pia, tunapata vitu vingine
muhimu kifya kama vile maji, nyuzi lishe
(dietary fibers), vimengenyo (enzymes)
na aina mbalimbali za kemikali (phytochemicals).
Mwili wa binadamu unahitaji virutubisho kwa kazi kuu nne ili kuuwezesha
uwe hai na uwe na afya. Mosi, virutubisho
vinaunguzwa na kuupa mwili nishati.
Pili, virutubisho vinatumika kukuza
mwili kwa watoto, kujenga na kuukarabati mwili.
Tatu, virutubisho vinatumika kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi
mbalimbali. Nne, virutubisho vinauwezesha mwili kufanya kazi zake mbalimbali kama vile mawasiliano ya ndani ya
mwili ambapo kiungo kimoja kikiumia
mwili mzima unahisi maumivu.

Uzalishaji wa nishati
Chakula kikiwa tumboni katika aina
ya wanga, sukari, mafuta na kama ipo
haja ya protini huvunjwa vunjwa na
kupata vipande vidogo zaidi (glucose, fatty acids). Vipande hivyo vidogo vidogo
hufyonzwa kutoka katika utumbo na kupelekwa katika damu na hatimae katika
chembe hai (cells) zinaunguzwa na kuupa mwili nishati (energy).
Vipande hivyo vidogo vidogo kama
vipo vingi kuliko mahitaji ya mwili ya kuzalisha nishati, vinabadilishwa na kuwa
mafuta na hatimaye vinahifadhiwa mwilini kwa matumizi ya siku zijazo. Na hii
ndiyo sababu ya watu wanaokula chakula
kingi kuliko mahitaji ya mwili wanakuwa
na unene au uzito uliopitiliza.
Kwahiyo, ili mwili usiwe na akiba
kupita kiasi lazima kukipunguza chakula kilichohifadhiwa
kwa njia kama kufanya
mazoezi, kufanya kazi
za kutoka jasho
kama kulima kwa
jembe la jadi,
kula kiasi na
kufunga
swaumumara
k w a
mara.

Matumizi ya Protini
Virutubisho vya protini vinaweza kutumika kuzalisha nishati pale ambapo
mtu anapokula vyakula vya protini kuzidi
mahitaji ya kujenga na kukarabati mwili.
Pia, kama mtu hali chakula cha kutosha
aina ya protini, nyama za mwili wake hutumika huvunjwa vunjwa na kuunguzwa
ili kupata nishati.
Kama hali hiyo itatokea mwili wa mtu
huwa mwemba kuliko kawaida. Kwa watoto hali hiyo inaweza kupelekea udumavu wa mwili na akili.

Matumizi ya nishati
Nishati inayozalishwa baada ya virutubisho kuunguzwa mwilini inahitajika
kwa kazi kuu tatu. Kwanza, nishati huuwezesha mwili kupumua, kusaga chakula, kuwezeha mzunguko wa damu, kuleta
joto, na na mwili kufanya kazi nyingine
zinazotuwezesha kuwa hai.
Pili, nishati inauwezesha mwili kuviunganisha virutubisho vya aina mbalimbali kama protini ili kupata chembe
chembe hai, damu, majimaji (fluids),
kinga ya mwili (antibodies) na vitu
vingine.
Tatu, nishati huwezesha misuli kujikunja na kukunjuka na hivyo kuweza
mtu kutembea, kulima, kuandika, kuzungumza, kwenda haja ndogo na
kubwa, mama kujifungua, kufanya mazoezi, kujisomea, kupigana vita na kazi nyingine.
Watu wanahimizwa kula mlo kamili
wenye wanga, mafuta kiasi, matunda,
mboga za majani na maji safi na salama
ili kupata virutubisho vinavyohitajika na
miili. Matunda na mboga za majani zitaupa mwili vitamini, madini na nyuzi
lishe za kutosha.
Wasomaji wetu
Baadhi ya wasomaji wetu wa gazeti la
hili wanakabiliwa na tatizo la unene na
uzito uliopitiliza. Wanasema maisha yao
yapo hatarini kutokana na athari za unene na uzito uliopitiliza unaowakabili
kama vile kukosa usingizi, kuchoka

sana, kuwa na wasiwasi, kujiona wana


maumbo mabaya, kukabiliwa na shinikizo la damu na upungufu wa nguvu za
kiume au za kike.

Hospitali kwanza
Wale wote wenye uzito au unene kupita kiasi wanahimizwa kwenda hospitali
kwa ajili ya vipimo na ushauri zaidi wa
namna watakavyoweza kupunguza uzito
au unene bila ya kudhuru afya zao. Ni
hatari sana kununua dawa hata kama zitadaiwa kuwa ni za kiSunnah bila ya
kwanza kufika hospitali na kupimwa.
Matumizi ya dawa bila vipimo na ushauri
wa daktari unaweza kuharibu figo na viungo vingine.

Kazi za virutubisho vya


kujenga mwili
Virutubisho vinavyotumika kuujenga
na kuukarabati mwili ni protini, baadhi
ya aina za mafuta, maji na baadhi ya
madini kama vile chuma.
Virutubisho vya kujenga na kukarabati mwili vina kazi mbalimbali mwilini.
Kila binadamu anahitaji virutubisho
hivyo ili kutengeneza chembe chembe hai
mpya kama vile damu na mbegu za uzazi.
Pia, zinahitajika kutengeneza majimaji (mfano machozi) na sehemu zingine
za mwili. Utengenezaji wa vitu vipya
mwilini ni muhimu sana kwa sababu kila
siku kuna chembechembe hai zinakufa
na sehemu nyingine za mwili zinaharibika.
Kwa mfano, mtu akiugua ugonjwa wa
malaria, baadhi ya chembechembe hai
zake huharibiwa kabisa na ugonjwa huo.
Kwa hiyo, uzalishaji wa chembechembe
hai mpya na ukarabati wa mwili lazima
ufanyike.
Ukarabati na uzalishaji wa sehemu
mpya unahitaji virutubisho kama protini,
madini chuma, mafuta na vitu vingine.
Watoto wachanga na wale wanaokua wanahitaji virutubisho vya protini na vile
vingine ili waweze kukua vizuri.
Ukosefu wa virutubisho hivyo unasababisha watoto kudumaa na wengine
kuwa wazito kumudu masomo shuleni.
Pia, ukosefu wa virutubisho kama folic
acids unaweza kusababisha watoto kuzaliwa na vichwa
vikubwa vilivyojaa maji
na mgongo wazi.

Wajawazito
Kina

mama wajawazito wanahitaji virutubisho vya protini na vile vingine ili watoto
wao walio tumboni waweza kukua vizuri.
Vilevile, wajawazito wanahitaji virutubisho hivyo ili miili yao iweze kutengeneza mfuko wa uzazi (placenta), mafuta na
damu ya kutosha mwilini.
Mama mjamzito bila ya kuwa na
damu ya kutosha, wakati wa kujifungua
anaweza kupoteza maisha. Naye mama
anayenyonyesha anahitaji virutubisho
vya protini ili mwili uweze kutengeneza
maziwa ya kutosha. Bila ya hivyo, mtoto
atakuwa hashibi na kuweza kudumaa.

Virutubisho wezeshi
Muda wote mwili wa mwanadamu
unafanya kazi mbalimbali zikiwemo kusaga chakula, kuzalisha nishati, kusafirisha ujumbe kutoka kichwani kwenda viungo vya chini kupitia mishipa ya fahamu, kupumua, kujenga na kukarabati
mwili, kupambana na maradhi, yai la
mama kusafiri, mbegu za baba kusafiri na
kuweza kuingia ndani ya yai, kutoa uchafu kama mkojo, jasho na kinyesi.
Ili mwili uweze kufanya kazi zote hizo
unahitaji virutubisho vya kuwezesha kazi
kufanyika.
Virutubisho hivi vinahitajika katika
kiwango kidogo sana mwilini na kwa kimombo vinaitwa micronutrients. Virutubisho hivi ni vitamini na baadhi ya
madini.
Kwa mfano, mwili wa binadamu unahitaji aina mbalimbali za Vitamin B ili
kuwezesha kazi ya wanga aina ya glucose
kuunguzwa na hewa ya oxijeni (oxygen)
na kutoa nishati.
Watu wale vizuri
Watu wanahimizwa kula vyakula bora
vya aina mbalimbali na wasikose matunda na mboga za majani kila mlo ili kupata
virutubisho vya aina zote na kiasi cha kutosha.
Wito wa Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu kupitia Quran
Tukufu anawahimiza wanadamu kula
vya halali na vilivyo bora: Enyi watu kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala msifuate nyayo za shetani, bila
shaka yeye kwenu ni adui dhahiri (Quran,
2:168).
Enyi Mlioamini kuleni vizuri tulivyokuruzukuni, na Mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa mnamuabudu yeye peke
yake. (Quran: 2:172). Na kuleni katika
vile alivyokuruzukuni Mwenyezi Mungu
vilivyo vizuri na halali na Mcheni
Mwenyezi Mungu ambaye nyinyi
mnamwamini (Quran, 5: 88).

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

13

UCHUMI NA BIASHARA

ABUU MAYSARA

Kanuni za Biashara katika Uislamu (7)


Tunaendelea na miamala iliyoharamishwa katika Uislamu. Wiki iliyopita tuliangalia muamala
wa Muzaabanah na
uharamu wake.
Sasa endelea
2. Muamala wa Mulaamasah
Aina hii ya muamala iitwayo
Mulaamasah ni pale mtu anapokubali kuuza au kununua bidhaa kwa kuigusa tu (Al-lams)
pasina kuiangalia au kuikagua.
Na hii inaweza kuwa ni kutokana na bidhaa hiyo kufunikwa
au iko mahali pasipo na mwangaza wa kutosha kuiona na hivyo
kuigusa kunasimama badala ya
kuikagua kunakotakikana
kisharia. Sharia imeharamisha
muamala huu kwa sababu ya
madhara yatokanayo na mnunuzi kutokujua sifa za bidhaa anayonunua hivyo uwepo wa Algharar au utapeli jambo ambalo
limeharamshwa.
Mfano wa muamala huu ni
kama vile uuzaji wa nguo za mitumba ambapo muuzaji hushika
nguo akataja bei na na mtu
akikubaliana na bei hiyo basi
hutupiwa nguo hiyo na kutakiwa kuilipia huku akiwa hajaikagua kuona kama inamfaa au
hapana.
Kwa hiyo ni vema waislamu
wakaujua muamala huu wa Mulaamasah na uharamu wake
kisharia ili tusije kujipatia chumo la haramu kwa sababu kipato kitokanacho na muamal aha-

ramu na chenyewe ni haramu.


Imepokewa hadithi kutoka
kwa Abu Hurayrah (Allah amridhie) kwamba Mjumbe wa Allah (rehma na amani ziwe juu
yake) alisema Hakika Allah
amewaamrisha waumini yale
yale aliyowaamrisha Mitume.
Akasema Allah Taala Enyi
Mitume, kuleni miongoni mwa
vitu vizuri na tendeni mambo
mema. Na akasema Enyi mlioamini kuleni katika vizuri tulivy-

okuruzukuni.
Kisha akamtaja mtu ambaye
yuko katika safari, nywele zake
zikiwa zimetimka na mwili
umeenea vumbi huku akiinua
mikono yake mbinguni huku
akiomba Yaa Rabb! Yaa Rabb!
(Anaomba) na huku chakula
chake haramu, na mavazi yake
haramu na amekulia katika mzingira ya haramu, ni vipi atajibiwa? (Muslim, Na. 1015).
Kwa hiyo muislamu usisome

makala hii kama hadithi za


Abunuwas kwani hapa ndiko
kuliko na kufaulu kwetu au
kufeli kwetu kwa sababu kama
dua zetu hazikubaliwi basi sisi
tuna kheri gani?

3. Muamala wa Munaabadhah
Muamala huu ni muamala
wa kuuziana au kubadilishana
bidhaa pasina mnunuzi kuikagua wala muuzaji kuainisha sifa

za bidhaa kama tulivyoeleza katika kanunuzii za biashara.


Na inaingia katika muamala
huu kile kiitwacho kutupa fimbo ambapo mnunuzi hutupa
fimbo katika bidhaa kadhaa kwa
sharti kuwa atainunua kwa bei
kadhaa. Basi bidhaa yoyote ile
itakayofikiwa na fimbo iliyotupwa na mnunuzi au mfano wa
hayo hulazimika kuinunua kwa
bei iliyotajwa. Wakati mwingine
pande mbili hukubaliana kuuziana ardhi kwa kurusha fimbo
au mfano wa hivyo hadi pale
itakapoangukia kwa tahamni
fulani.
Basi mnunuzii hutupa fimbo
(au kitu kingine) na urefu kutoka pale aliporushia hadi ilipoangukia huwa eneo linalouzwa
kwa bei waliyokubaliana.
Mfano wa ,muamala huu ni
ule michezo ya tombola ambapo
watu hutoa viingilio na kisha
hutakiwa kurusha vitu kama
bangili kulenga bidhaa mbali
mbali zilizotawanywa uwanjani
kwa kubahatisha kisha wakipatia huchukua bidhaa hiyo.
Muamala huu ni aina katika
Al-gharar yaani udanganyifu
na muuzaji na mnunuzi wote
hupata madhambi. Na inaingia
katika hukmu hii kurusha vijiwe
nako ni kuweka sharti la kutimia
biashara baina ya watu wawil
kwa kutoa kijiwe kidogo badala
ya bidhaa.
Hakika biashara katika Uislamu ni lazima pande mbili zikamilishe masharti ya kuswihi biashara na kusiwe na upande
usiojua bidhaa inayouzwa wala
bei yake.
Na hapa nchini, miamala
kama hii ni mingi. Na upande
wa miamala ya biashara husuusan biashara za zama hizi nyingi
ni katika miamala haramu hivyo
waslamu tunapaswa kuwa na
tahadhari kubwa.
Itaendelea in shaaa Allah.

WASEMAVYO WANAZUONI WETU


Anasema Qurtubiy (Allah Amrehemu)
Allah awarehemu wema waliotangulia
kwani walisisiti za katika kumuusia kila
mwenye akili timamu kwa kusema:
Vyovyote uchezeavyo kitu, ole
wako kucheza na dini yako
(Al-Jamiu)

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

14
YUSUPH AMIN

Serikali
imekuwa
ikipambana
usiku na
mchana ili
kuhakikisha
kiwango cha
ufaulu kwa
wanafunzi wa
shule za msingi
na sekondari
kinaongezeka.
Kuonesha
uthubutu,
miaka ya
hivi karibuni
serikali kwa
kushirikiana
na wadau
mbalimbali
walifanikisha
ujenzi wa
maabara za
masomo ya
sayansi katika
shule zake za
sekondari nchi
nzima.

Na katika kumaliza tatizo la


uhaba wa madawati shuleni, serikali
kupitia kauli mbiu yake ya Hapa
kazi tu imefanikiwa kuhamasisha
wadau kuchangia na kupunguza
kama siyo kuondoa kabisa uhaba wa
madawati nchi nzima.
Binafsi nimekuwa nikifuatilia
mikakati mbalimbali ya serikali ya
kuinua kiwango cha ufaulu nchini
na na kugundua kwamba taifa
limeshindwa kuwadhibiti wanafunzi wanaohusika na kufanya vitendo
vya uasherati na ufuska ukiwemo ulevi wa pombe ijulikanayo kama viroba.
Ulevi ni janga kwa wanafunzi
wengi wa shule za sekondari nchini.
Licha ya madhara yake kiafya, ulevi
kwa wanafunzi limekuwa ni tatizo
sugu huku athari zake zikishuhudiwa kupitia matokeo ya wanafunzi
kwenye mitihani ya kitaifa ya darasa
la saba, kidato cha nne na sita.
Katika maeneo mbalimbali ya jiji
la Dar es Salaam, imethibitika kuwepo kwa wanafunzi wengi watoro
ambao huzurura mitaani wakicheza
kamari, kunywa pombe, kutafuna
miraa pamoja na kuvuta shishi na
bangi.
Pombe ndiyo mama wa maasi na
katika hasara zake ni kushuhudiwa
kwa matukio mengi ya mauaji,
ubakaji, matumizi ya dawa za
kulevya, uzinifu, wizi, utovu wa adabu na kadhalika.
Katika kuliangazia hili, Mtume
(rehema na amani ya Allah zimfikie)
amesema: Jiepusheni na ulevi, hakika ulevi ni mama wa maasi (maovu) (AnNasaai). Tena Mtume
akasema: Kila kinacholewesha ni
ulevi, na kila kinacholewesha ni haramu(Muslim).
Miaka saba iliyopita nilibahatika
kusoma elimu ya kidato cha tano na
sita kwenye shule moja ya jijini Dar

Ulevi, zinaa
vinavyodumaza
elimu Tanzania
es Salaam, na hapo nikajifunza mengi. Moja ya matukio ninayoyakumbuka sana ni maisha ya baadhi ya
wanafunzi shuleni hapo kutawaliwa
na tabia za ulevi na uasherati.
Hali hii ilitamalaki zaidi kila ilipofika mwishoni mwa wiki, na katika mwanzo na mwisho wa mihula
ambapo ilikuwa ni kawaida kwa wanafunzi kufanya hafla ya kurejea
shuleni maarufu kama back to
school party.
Nilichostaajabu zaidi ni kuwaona
wanafunzi wenzangu ambao wengi
wao walikuwa wamepanga kwenye
mabweni ya jirani na shule, kila
mmoja akiishi chumba kimoja na
mwanafunzi mwenzake wa kike
mithili ya mume na mke. Kwa hakika nilikuwa nikipata gagaziko la nafsi kila nilipoitafakari hali hii, lakini
kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu
nilifanikiwa kuhitimu kidato cha sita
pasi na kuathiriwa na mazingira.

Chimbuko la tatizo
Tukizungumzia malezi ya watoto,
tunazungumzia makuzi ya vijana
ambao ndiyo taifa la kesho. Katika
kile ninachoweza kukiita kujitia upofu wazazi wamekuwa wakiwapa

uhuru vijana wao kufanya kila wanachotaka tukidhani kuwa wao ni watu
wazima. Hali hii imesababisha kuwepo visa vingi vya utovu wa nidhamu kwa wanafunzi ambapo baadhi
yao wamekuwa wakijiingiza kwenye
vitendo vya kihuni. Rafiki yangu
mmoja ambaye ni mzee wa makamo
aliwahi kuniambia kuwa wakati akisoma malezi ilikuwa ni jukumu la
mzazi, mwalimu na jamii kwa ujumla.
Katika maelezo yake akanidokeza
kuwa walifanya hivyo kwa kutambua kuwa kuharibika tabia ya mwanafunzi mmoja athari zake husambaa kwa wengine kwa njia tofauti.
Aidha aliendelea kusema ni mbaya
kudhani katika jamii ni kundi fulani
tu la watu ndilo lenye wajibu wa
kusimamia malezi ya wanafunzi.
Kukosekana kwa utamaduni
huu wa malezi ya pamoja kulisababisha hata juhudi za wananchi za
kuwakamata wanafunzi wahuni na
kuwapeleka polisi kuishia patupu
kutokana na wanafunzi hawa kutopewa adhabu stahiki, alisema
Mzee huyo.
Ingawa hakuna utafiti wa kitaalamu unaobainisha chanzo cha wa-

nafunzi wengi kujiingiza kwenye


tabia za ufuska na uasherati, huenda
hali hii inasababishwa na malezi mabaya ya wazazi au walezi pamoja na
kusuhubiana na marafiki waovu.
Licha ya hivyo, wanafunzi ni lazima watambue ulevi si tabia inayowaathiri kimasomo peke yake bali
huathiri takribani kila kiungo cha
mwili.
Kama tatizo hili halitapatiwa
ufumbuzi wa haraka ni wazi taifa
litaingia kwenye hatari ya kukosa
wataalamu bora na wenye upeo,
jambo ambalo ni hatari katika nchi.
Kwa maneno mengine ni kushamiri
kwa tatizo hili kunaweza kuiathiri
sekta ya elimu na nyinginezo kama
vile uchumi na maendeleo.
Binafsi naamini kwamba hakuna
uwezekano wa mtumishi bora wa
umma akajengeka kupitia mazingira
ya ulevi, iwe nyumbani au shuleni.

Nchi nyingine zenye


tatizo hili
Tatizo hili la ulevi na uasherati
miongoni mwa wanafunzi si la Tanzania peke. Nchi nyingi duaniani
zimeathirika, hususan za Kiafrika.
Kwa mfano, duruzinaarifu kuwa,
katika nchi za Kenya na Afrika
Kusini, katika baadhi ya maeneo, ni
kawaida kumuona mwanafunzi wa
kike au kiume akivuta bangi na
kunywa pombe hadharani.
Kadhalika takwimu za miaka ya
karibuni zinaonesha kuwa, baadhi
ya wanafunzi wa shule za msingi
nchini Kenya na hushiriki vitendo
vya ufuska na uasherati ikiwemo zinaa tangu wakiwa na umri wa miaka
kumi.

Nafasi ya wazazi na walimu kwa wanafunzi


Shule zina kila sababu ya kupeleka walimu wa masomo ya dini
mashuleni ili kuwaelimisha vijana
juu ya madhara yanayoweza kusababishwa na ulevi pamoja na zinaa.
Naamini katika kufanya hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza
kama si kumaliza kabisa tatizo hili.
Nao wazazi na walezi walipoulizwa kuhusu kadhia hii walikiri
kuwepo kwa tatizo la kutozungumza
na vijana wao juu ya madhara ya
kunywa pombe na kuvuta bangi, hali
inayosababisha wanafunzi wengi
kudumu na hali hiyo bila kujua madhara yake.
Nilichokibaini ni wazazi wengi
kuona haya kuzungumza na vijana
wao kuhusu mustakbali wao kielimu, huku wengine wakisema hawafanyi hivyo kwa kuwa watoto wa
kizazi cha sasa siyo wasikivu. Hata
hivyo, baadhi ya vijana waliohojiwa
na gazeti hili walisema, wamekuwa
wakiusaka muda wa kuzungumza
na wazazi wao hasa wanaume ili kuzungumzia maisha yao ya baadae
bila mafanikio.
Kwa munasaba wa nafasi yetu
kama wazazi wa Kiislamu, tunalo jukumu la kuwalingania vijana juu ya
madhara ya ulevi, kamari na zinaa
kidunia na pia kesho akhera. Kufanya hivyo kunaweza kuwa ni kheri
kubwa ikizingatiwa kwamba, Shetani huyatumia maovu haya kama
kamba ya kumfungia mwanadamu
katika kumuasi Mwenyezi Mungu.
Allah Taala anasema ndani ya
Quran: Enyi mlioamini! Bila ya
shaka ulevi, na kamari, na kuabudu
masanamu, na kupiga ramli, (vyote
hivyo) ni uchafu katika kazi ya
Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili
mpate kufaulu. (Quran, 5:90).

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

MAKALA

15

Msahafu wa Imam

Ali ulikwenda wapi?


NA SHERALLY HUSSEIN SHERALLY

bali na hilo la Quran, pia tunasoma katika vitabu vya Mashia wakisema kuwa: Asiyeamini Uimamu wa Ali na watoto wake na wajukuu zake huyo ni kafiri, hata ikiwa anatamka Shahada, anaswali swala 5, anafunga swaumu ya Ramadhani, anatoa Zakka,
na anaenda kuhijji Makka. Yote hayo hayatamsaidia mtu huyo na mafikio yake ni
motoni kwa kuwa aliupinga uimamu.
Sasa, ndugu msomaji wa Makala hii,
hilo si dogo, kama Abdillahi Nasir anavyotaka kuwalaghai Waislamu kwenye kitabu
chake Shia na Quran - Majibu na Maelezo,
uk. 5. Nililotaka kulisema pale mwanzo wa
paragrafu hii ni kuwa Usunni hauwezi
ukawa sahihi na wakati huo huo Ushia nao
ukawa sahihi, kama vile ambavyo Uislamu
hauwezi ukawa dini sahihi na wakati huo
huo, ikawepo dini nyingine ambayo nayo
ikawa ni ya sawa na sahihi mbele ya Allah.
Nina maana ya kusema kuwa, Ushia
ukiwa ni itikadi sahihi basi Usunni lazima
uwe ni batili. Au, Usunni ukiwa ni itikadi
ya sawa na inayokubaliwa mbele ya Allah,
basi Ushia lazima uwe ni Batili. Haviwezi
vyote vikasimama na mtu akadai kuwa imani au itikadi zote mbili ni sahihi na ni safi
isipokuwa hitilafu zilizomo ni ndogo ndogo
tu!
Kwa maneno hayo, niwaombe
Masheikh zangu wote wenye kuifanya
Daawa hii, ya kuwalingania watu waje
kwenye dini na itikadi sahihi, wahakikishe
hili wanaliweka mbele katika kila mihadhara, minakasha, majadiliano, na kwenye
makala na mengineyo. Haiwezekani
Usunni uwe ni Uislamu na hapo hapo
Ushia nao uwe ni Uislamu.
Waingereza wana msemo usemao:
Two opposites, never converge. Waarabu
nao wana usemi; Adh-dhiddaani, laa yattafiqaani. Kiswahili chake ni Yakinzanayo, hayawafikiani. Kwa hiyo basi, kazi
yetu kwenye daawa hii iwe ni kuvunja nguzo za imani za Ushia. Kazi iwe ni kulivunja
sanamu la uimamu. Uimamu ukiporomoka, Ushia unakuwa kiwete.
Msijadiliane na Mashia kuhusu udhu.
Je! Tuoshe miguu au tupanguse.!? Msijadiliane na Mashia juu ya ubora wa Ali
dhidi ya Masahaba wengine! Mtapoteza
muda mwingi huko kwenye nukta hizo.
Mtachukua muda mrefu sana kutambua
nani kafiri na nani Muislamu kati ya Sunni
na Shia.
Muulize Shia ukikutana naye, ikiwa Uimamu wa Ali, uteuzi wake ni kutoka kwa
Allah Mtukufu, uteuzi ulioletwa duniani
na Jibril (amani imshukie), kisha uteuzi
huo ukatangazwa na Mtume Mtukufu
Muhammad (rehema na amani ya Allah
iwe juu yake), swali kwako ewe Shia Abubakr ndiye aliyekuwa wa kwanza kuivunja
amri hiyo kutoka kwa Allah, kwa itikadi
yenu, nyie Mashia, Je Abubakr mtamuitaje? Muumini au kafiri?
Kwa itikadi ya Mashia, kwa kuwa Abubakr aliipinga amri hiyo ya Uimamu wa
Ali, aliyeteuliwa na Allah Taala ni lazima
awe Kafiri. Endelea kumuuliza huyo Shia,
ikiwa hilo usemalo ni kweli, kwa muda wa
miaka 24 na miezi 9 , baada ya Mtume
wetu kufariki, Imamu Ali alikuwa akiswali
swala tano nyuma ya Imamu yupi?
Kumbuka, enzi hizo pale Madina,
msikiti ulikuwa mmoja tu, Waislamu wote
wa Madina wakiswali swala za jamaaa na
swala za Ijumaa hapo msikitini. Mpaka vipofu, waliamriwa wafike msikitini kuswali

swala za Jamaa, sikuambii aliye na macho.


Khalifa wa zama husika ndiye alikuwa
Imamu wa swala zote hizo. Wakati wa
ukhalifa wa Abubakr, yeye ndiye alikuwa
Imamu, wakati wa ukhalifa wa Umar Ibn
al-Khatwaabi, yeye Umar ndiye alikuwa
Imamu. Wakati wa Ukhalifa wa Uthmaan,
yeye ndiye alikuwa Imamu.
Toka afariki Mtume wetu (rehema na
amani ya Allah ziwe juu yake), zama za
Abubakr, zama za Ukhalifa wa Umar hadi
zama za Uthman, palipita miaka 24 na
miezi 9, ndipo Ali akawa Khalifa na hivyo
kuwa Imamu wa swala zote. Swali kwa
Mashia, kwa muda wote huo wa miaka 24
na miezi 9, Imamu Ali, Imamu Hassan,
Imamu Hussein; walikuwa wakiswali nyuma ya nani?
Kwa kuwa Abubakr, Umar na Uthman
walipinga uteuzi wa Imamu Ali na hivyo
kuidhulumu haki yake! Kumpiga na
kumjeruhi mke wa Ali! ambaye ni Binti
Rasuulillah, majeraha yaliyomfanya aharibu ujauzito na kusababisha kichanga kufa!,
mtoto wa Simba Wa Allah majeraha yaliyomfanya afariki dunia!!!
iweje tena, yule asifiwae kama - Asadullah (Simba wa Allah), Imamul Mashaariqi
Wal-Magharibi, aswali nyuma ya madhalimu, makafiri hawa!? Swala zake zote
kwa miaka hiyo 24 na miezi 9 pamoja na
swala za Imamu Hassan na Imamu Hussein zitaswihi vipi? Ikiwa watu hawa waliipinga amri ya Allah iliyotolewa pale
Ghadeer Khum, Uislamu wao utaswihi
vipi?
Kwa maswali hayo machache yaliyopo
hapo juu, inathibitika vizuri sana kuwa zile
simulizi za tukio la Ghadeer Khum, halikutokea, kama wanavyotaka lieleweke,
kwa maslahi ya dini yao. (It was-Ibn Sabaa
comedy). Ikiwa basi tukio hilo la Ghadeer
Khum ni la kughushi (Iranian Fiction),
basi na wasia wa Uimamu wa Ali nao
utakuwa ni jambo la kubuni.
Hapo ndipo Ushia unapo kufa kifo cha
mende. Kinyume chake, wakitaka kutetea
tukio la Ghadeer, ili Uimamu uthibiti, basi
wote waliokhalifu amri iliyotolewa
Ghadeer Khum, watakuwa wamekufuru!
Ikiwa itakuwa ni hivyo (kukufuru kwao
waliokhalifu), vipi tena Imamu Ali, Imamu
Hassan, Imamu Hussein, waswali nyuma
ya makafiri!?
Allah anawapa khizaya Mashia hapa
hapa duniani kwa kumzulia uongo Allah
Taala na kumzulia uongo Mtume (rehema
na amani ya Allah iwe juu yake). Hakuna
Shia yeyote anayeweza kutatua gogoro
hilo walilolizusha. Awali nilisema itikadi za
Sunni zikithibiti Ushia lazima uwe Batili.
Haiwezekani itikadi hizi, zinazo kinzana,
ati zote zikawa ni sahihi. Abadan, haiwezekani.

Msahafu wa Imamu Ali


Tumepata maelezo mafupi kuhusu
Msahafu Wa Fatima, katika makala ya
Sheikh Abuu Aymanah, wiki iliyopita. Iko
haja ya kuwaelezea Waislamu juu ya msahafu huo wa Fatima kwa kina zaidi. Namuombea Abuu Aymanah apate fursa ya
kutuelimisha zaidi kuhusu msahafu huo.
Kabla sijaendelea na maelezo yao
Mashia kuhusu- Msahafu wa Imamu Ali,
niseme kidogo kuhusu Msahafu wa Fatima. Tutaona hapa chini, muda si mrefu,
kuwa Mashia wana kubali kuwa Msahafu
wa Ali ni Quran. Pia wanakubali- Msahafu
wa Aisha ni Quran.
Pia wanakubali, msahafu wa Uthmani
ni Quran. Lakini ikija kwa msahafu ww

Fatima, huruka kama ngedere mitini, na


husema; msahafu wa Fatima si Quran bali
ni ule mkusanyiko wa makaratasi.
Tuwaulize hawa Marawaafidha, Mbona Nahjul-Balagha hamja ipa jina la- msahafu wa Nahjul-Balagha? Nacho si ni mkusanyiko wa makaratasi!? Mbona Al-Kaafi
hamja ipa jina la msahafu wa Al-Kaafi!?Kifo cha mende hicho- Ushia, (marigyo!)
hausimami hapo, lazima ufe.
Tuendelee, pamoja na maelezo hayo
mafupi, bado Mashia wote wanaamini na
kuukubali Msahafu wa Fatima kuwa upo.
Hakuna Shia hata mmoja anaelipinga hilo.
Ila wanachokisema, kwa Taqiyyah, ni kuwa
msahafu huo wa Fatima si Quran. Umeitwa Msahafu kwa sababu ni mkusanyiko
wa makaratasi.
Hebu tumsikilize, Abdillahi Nasir
anasema nini kuhusu Msahafu wa Fatima.
Katika ukurasa wa 18 wa kitabu chake:
Shia na Quran, chini ya Mlango, Msahafu
wa Fatima, anasema: Hili ni dai la saba la
Sheikh M. Al-Khatib - kwamba Shia wanamsahafu uitwao Msahafu wa Fatima, na
ambao ni tofauti na misahafu waliyonayo
Waislamu!-Na hilo ni kweli! Lakini neno
Msahafu hapo halina maana ya Quran
Nukta ya kwanza: Abdillahi Nasir, anakiri wazi kuwa Msahafu wa Fatima- upo!Tunawauliza Mashia, Msahafu wa Fatima
ulipatikana vipi? Hivi sasa uko wapi? Je!
Kuna Shia yeyote aliyewahi kuuona? Kama
Msahafu huo wa Fatima si Quran, bali ni
usia, mawaidha, utabiri, je! Mambo yote
hayo yalitoka kwa nani?
Hata wakijitetea kinafiki kuwa Msahafu
wa Fatima si Quran - lakini wanatuambia
Mashia kuwa ukubwa wa Msahafu wa Fatima ni mfano wa Quran yetu mara tatu.
Three times bigger than our present
Quran). Mawaidha hayo na usia (three
times bigger than our Quran) huo ulitoka
kwa nani?
Je! Ni kwa nini mawaidha hayo na usia
huo uwe ni kwa Fatima tu? Kama Baba
yake Fatima, Mtume (rehema na amani ya
Allah zimwendee) alirithisha msahafu
wake Fatima kwa wanae nao wakawarithisha watoto wao na wajukuu zao, hamuoni
kuwa hiyo ni dini ya kipekee iliyo wahusu
akina Fatima na wanawe na wajukuu tu?
Hamuoni kuwa nyie wafuasi wao mna dini
iliyo tofauti na Maimaamu wenu ?

Nukta ya Pili, Abdillahi Nasir anaukubali huo Msahafu wa Fatima kuwa upo.
Tabaan, ni wahyi kutoka kwa Allah. ni
kitabu (mkusanyiko wa makaratasi.) kilichoteremka baada ya Quran, kikiwa na
mafundisho, usia, utabiri wa mambo yatakayo kuja kutokea zama za mwisho wa
dunia. Kwa kifupi sana , huu ulikuwa ni
Wahyi kutoka kwa Allah, sub-haanahuu
wataAala.
Sasa kwa kuwa mlango wa wahyi
wameufungua Mashia katika dini yao,
(kwa Sunni, sisi Wahyi ulikoma mara tu
Mtume (rehema na amani ya Allah ziwe
juu yake) alipofariki dunia. Ndio maana
tunamuita Ahmad Mirza Qadiyani, kafiri.)
Tunawauliza Mashia, Ni lini mlango wa
wahyi ulifungwa?
Ghulam Ahmad Mirza Qadiyan, ambaye naye alidai kupata wahyi kutoka kwa
Allah, mtamkatalia vipi dai lake hilo ikiwa
nyie Mashia mnakubali kuwa wahyi uliendelea kushuka baada ya Mtume (rehema
na amani ya Allah zimwendee) kufariki?
Nukta ya Tatu: Kule kukubali kwao
Mashia kuwa kuliteremka kitabu baada ya
Mtume - (kwa hakika zaidi), kuliteremka
vitabu vingi baada ya Quran - kauli hii pekee inakutosha kukufanya uwe ni kafiri.
Kwa kukubali kwenu kuteremka msahafu wa Fatima, (ingawa si Quran, kwa Taqiyya yenu), ndiko kuliko wafanya Mashia
wenzenu; Imaamiya Ismaailiyya, kudai
kuwa Agha Khan aliteremshiwa wahyi na
kitabu (nao wanadai si Quran) kiitwacho
Jiinaan.
Nyie Mashia Ithna- Ashariyya mna
kitabu Msahafu wa Fatima (Wahyi kutoka
kwa Allah- Naudhubillah) na wao Mashia
Ismaailiyya Imaamiyya- wana kitabu- Jiinaan-(Wahyi kutoka kwa Allah- Nauudhubillah). Vipi hapo, mtakikubali kitabu
hicho?- (Hamkikubali, bali mnawaita hao
Mashia wenzenu kuwa ni makafiri). Ebwe!
Mlango wa wahyi mmeufungua nyie
wenyewe, sasa Ndugu zenu Mashia Ismailiyya, nao wanadai agha khan kapata
wahyi na kupewa kitabu- mnaruka kama
Ngedere. Mnawaita- Mashia Ismaailiyya
makafiri.
Yapo mengi sana, kwa leo tuachie hapo,
tutaendelea tena wiki ijayo, in shaa Allah,
kuelezea juu ya kitabu chao Mashia kiitwacho- msahafu wa Imamu Ali.

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

16
SEIF RUGA

atika makala iliyopita tulianza


kuangalia maafa yanayofarakanisha umma yakiwemo
watu kufuata matamanio ya
nafsi, kutoifuata haki na kuipindisha,
ubinafsi na umimi, kujenga dhana
mbaya kwa wengine na kupenda kukaribisha mijadala.
Katika nukta ya mwisho tulibainisha sifa za mtu mpenda mijadala ya
uhasama kwa nia ya kutaka kutiiwa.
Katika makala hii tunaendea na
maudhui hayo. (Sasa endelea..)
Ibin Qutaiba (Allah amrehemu)
amesema katika kubainsha hali waliyokuwa nayo wema waliotangulia,
Salafuswalihu (Allah awarehemu):
Walikuwa wenye mitazamo inayopishana katika ufahamu wa Fiq-hi
(sharia ya Kiislamu- kuhusu utukufu
fulani wa jambo, au ni jambo gani
lipo wazi zaidi ili lipate kutumiwa, na
ni jambo gani ambalo litawafaa watu.
Kwa kupitia mchakato huo, Allah
hunufaisha kupitia jambo hilo kwa
mtu aliyelisema na yule aliyelisikia.
Na mara nyingi kupishana kwao kimitazamo hutokea katika maeneo yaliojificha mno na yenye maana ya ndani sana. Lakini watu walipoanza tu
kuingia katika mijadala ya utangulizaji utashi wa nafsi, ndiyo wakaanza
kugawanyika.
Amri bin Qaisi amesema: Nilisema kumwambia Hakam bin Utbah,
Ni kitu gani kilichowafanya watu
wazame katika utashi wa nafsi? Akajibu, Ni kuendekeza mijadala ya ugomvi.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Qilaab, ambaye aliwadiriki baadhi ya
Maswahaba wa Mtume wa Allah (rehema na amani za Allah ziwe juu
yake): Msikae pamoja na watu
wenye mijadala ya uhasama. Ninahofia wasije wakawazamisha katika
upotevu wao, au kuwatatanisheni na
yale mnayoyajua. (Addarimiy).
Ikiwa ubishi na mijadala ya utangulizaji utashi wa nafsi na ukinzani
katika dini ni jambo baya, basi ubaya
huo unazidi mara mbili yake kwa
mtu anayefuata mkumbo wa watu
bila ya kuwa na elimu ya upambanuzi
na yule mwenye sifa ya ujinga .

Uhafidhina na
unganganizi wa jambo
Uhafidhina huu uwe ni wa kimtazamo wa kisiasa, kimadhehebu,
kikundi au kimakundi au uwe una
sura ya upetukaji mpaka kupenda au
kuchukia pindi unapoota mizizi ndani ya moyo wa mtu au akili yake huuzidi nguvu moyo na akili hiyo, na
mambo yote atakayofahamishwa
mtu mwenye maradhi ya aina hiyo
kuhusu dalili mbalimbali za
maandiko kutoka katika Quran na
Sunnah hawezi kuzikubali na kuzikiri.
Imamu Al-Mawrdiy (Allah amrehemu) amesema: Nilkuwa siku moja
na mtu mwenye uhafidhina (asiyetaka kubadilika kwa mujibu wa andiko
la Quran au hadithi ya Mtume) katika hafla fulani, ikawa mpinzani wake
ameleta hoja iliyo na mashiko ya ushahidi.
Jibu la mtu huyo lilikuwa hivi,
Hakika huu ushahidi aliouleta yeye
ni batili, na ni hoja dhaifu isiyokubalika, kwa sababu Sheikh wangu hajawahi hata siku moja kunielezea hoja
hiyo. Na kila ambacho Sheikh hakunifundisha basi hakina kheri ndani
yake.

Kufuata utashi kikwazo

cha kuufahamu Uislamu (2)


Yule bwana mtoa hoja yenye ushahidi wa nguvu akastaajabu na kunyamaza. Watu waliokuwepo katika hadhira
hiyo wakashangazwa na ujinga wa kiwango cha juu alioudhihirisha mtu huyo
muhafidhina. Wapo waliomdhihaki na
kumshanga, na pia wapo waliojilinda
kwa Allah na ujinga wa sampuli hiyo.
Miongoni mwa ujahili uliokubuhu,
ni baadhi ya taasisi na watu fulani kujipa
hatimiliki na kujivisha joho la umimi na
ubinafsi ya kwamba wao ndiyo peke yao
wenye haki ya kuuhudumia Uislamu na
Waislamu, wao ndiyo wenye fikra pevu
na busara zilizopea zinazotoa nuru ya
matumaini kila wakati.
Na ubaya wao unazidi maradufu pale
wanapojinasibisha na Ahlu Sunnah wal
Jamaa, huku kwa upande mwingine
wakishirikiana na watu au itikadi ya
watu wanao watusi na kuwavunjia heshima baadhi ya Maswahaba (Allah awaridhie wote) na wake zake Mtume (rehema na amani za Allah ziwe juu yake).
Mwanazuoni mahiri na mweledi katika taaluma ya sharia ya Kiislamu, Ibn
Taymiyya (Allah amrehemu) alisema
katika kuwaelezea maimamu wanne
maarufu katika madhehebu ya AhluSunnah wal Jamaa: Na Mwenye
kungangania rai au mtazamu wa imamu mmoja tu katika maimamu wanne,
na kutupilia mbali rai na mitazamo ya
maimmu wenginekatika ufahamu wa
kitabu cha Allah na Hadithi za Mtumehata kama mitazamo ya maimamu hao
imeafikiana na Quran na Sunnah za
Mtume (rehema na amani za Allah ziwe
juu yake) Mfano wake mtu huyo ni sawa
na yule aliyemkubali Swahaba mmoja
tu huku akiwananga wengine. Anakuwa
ni kama wale watu waliomkubali Ali bin
Abii Twalib (Allah amridhie) na
kuwakataa Maswahaba watatu waongofu (Allah awaridhie).
Tabia na mienendo kama hii ni ya
watu wenye kutanguliza matamanio ya

nafsi na mambo ya uzushi na ya bidaa


katika dini, na tabia hizi zimetajwa kuwa
ni mbaya kwa ushahidi wa Quran, hadithi na Ijmaa - makubaliano ya pamoja
ya wanazuoni wa Kiislamu.
Na watu wenye sifa za sampuli hii,
wapo nje kabisa ya sharia na mfumo
ambao Allah aliyetukuka na Mtume
wake (rehema na amani za Allah ziwe
juu yake) wamekuja nao.
Mtu ye yote atakayejifanya
kinganganizi na muhafidhina wa
kutetea rai au mtazamo wa imamu
mmoja tu, hata kama imamu huyo ameteleza katika kufahamu mafundisho ya
Allah Taala na Mtume wake, basi mtu
huyu hufanana na watu wenye sifa hizi,
sawasawa iwe rai hiyo ni ya Imamu Maliki, Shafi, Abuu Hanifa, Ahmad au
maimu wengine.
Sababu ya muhafidhina huyo
kungangania rai na mtazamo wa imamu mmoja tu si nyingine isipokuwa ni
ujahili na uchache wa elimu yake ya dini,
aidha ni ufinyu wa maarifa katika elimu
na ufahamu wa rai na mitazamo ya
maimamu wengine. Hivyo anakuwa jahili na dhalimu na Allah siku zote huamuru kuwa na elimu na uadilfu, na hukataza ujahili na dhuluma.
Vile vile Ibin Taymiyya ameendelea
kubainisha kuhusu maafa ya uhafidhina
na unganganizi wa kitaasisi au wa
kikundi kwa kusema: Msingi na malengo yoyote yale, ndiyo dira na madhumuni ya kikundi au taasisi ambayo mtu
anajiunga nayo.
Iwapo watu hao wamejumuika katika taasisi au kikundi fulani kwa misingi
ya kulinda na kutetea yale yote Allah
Taala na Mtume (rehema na amani za
Allah ziwe juu yake) wameyaamuru au
kuyakataza, bila ya kuzidisha jambo au
kupunguza, hakuna shaka yoyote watu
hao ni waumini, na wala hakuna tatizo
lolote juu ya mtazamo wa jina la taasisi
yao au kikundi chao, madhali

wameshikamana na muongozo wa
Quran na Sunnah ya Mtume.
Lakini iwapo watakuwa wamezidisha jambo katika dini au kupunguza mfano kumfanya rafiki na kumthamini
mtu anyeunga mkono kikundi au taasisi
yao, bila ya kujali mtu huyo yupo katika
haki au batili; na kumchukia yule ambaye hakubaliani na mitazamo ya kikundi au tasisi yao, bila ya kujali kuwa yupo
katika haki au batili - Bila ya shaka huu
ndiyo utengano na tofauti ambayo Allah
Taala na Mtume wake (rehema na amni
za Allah ziwe juu yake) wameusema
vibaya na kuukataza.
Hakika Allah Taala na Mtume wake
wameamrisha umoja na mshikamano,
na wamekataza utengano na tofauti, na
wameamrisha kusaidiana juu ya wema
na uchamungu, wamekataza kusaidiana
juu ya madhambi na kufanyiana uadui.
Sababu za nje zilizochochea farka
miongoni mwa Waislamu
Tulizozijadili zilikuwa sababu za ndani ya Waislamu ambazo huchochea
uhasama na utengano kwa jamii ya
Waislamu. Zifuatazo ni sababu za nje ya
wigo wa Waislamu ambazo zinazopelekea mifarakano kwa Waislamu.
Miongoni mwa sababu zinazoleta tofauti ni kukosekana mshikamano katika
safu ya umma wa Kislamu ni vita ya utamaduni na itikadi za dini nyingine.
Dini hizo zimeuchukulia Uislamu
kuwa ni adui yao namba moja katika
huu uso wa dunia, kuanzia katika upande wa kiitikadi na kiutamaduni. Vita
hii si ya leo wala ya jana bali ilianza tangu
dahari, tokea tu pale mbegu ya Uislamu
ilipodhihiri juu ya mgongo wa ardhi,
tangu pale Mtume (rehema na amani ya
Allah ziwe juu yake) alipoanza kulingania ibada ya Mwenyezi Mungu mmoja.
Hapa tutaangazia kwa muhatsari
baadhi ya harakati za mashirika ya kimisionari wa kinaswara zilizofanywa na
zinazoendelea kuratibiwa kwa juhudi
kubwa ili kuzalisha tofauti na mpagaranyiko miongoni mwa Waislamu.
Hakika Uislamu ulikuja kuunganisha baina ya watu wa pande mbalimbali
za Waarabu zilizokuwa zikizozana mara
kwa mara, na pia kuunganisha watu wa
kheri mingoni mwa viumbe.
Kwa mfano tunajua kuwa Swahaba
Bilali bin Rabah (Allah amridhie) mwadhini wa Mtume, asili yake ni mhabeshi
wa Ethopia upande wa bara la Afrika, na
Swahaba Suhaib (Allah amridhie) asili
yake ni Mrumi, Swahaba Salman (Allah
amridhie) asili yake ni Mfursi.
Naye Mohammad bin Ishak mwanazuoni wa kwanza kuandika katika fani
ya sira (historia) ya Mtume (rehema na
amani zaAllah ziwe juu yake),asili yake
ni ni Mfursi. Imamu Attwabariy Sheikh
wa wanahistoria wa Kiislamu na wanazuoni wa tafsiri ya Quran, asili yake ni
Mturuki.
Unapochunguza kwa makini vitabu
vinavyozungumzia wasifu wa wasomi na
wanazuoni maarufu wa Kiislamu na
uvumbuzi wao uliochangia kupatikana
fani na taaluma mbalimbali za kielimu,
utawakuta wengi wametoka maeneo tofauti ya kidunia.

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

MAKALA

17

MTUME
ALIPOMBASHIRIA
SUHAIB:
MAZINGATIO Biashara imekuwa na faida Abuu Yahya
MATUKIO YENYE

ZAHARANI BARAKA

aada ya Mtume (rehema


na amani ya Allah iwe juu
yake) kuamrisha Maswahaba wake kuhama kutoka Makka kwenda Madina, Swahaba Suhaib bin Sinan Ar-Rumi,
(Mungu amridhie) aliazimia kufanya hivyo lakini Maquraishi
walimzuia kutimiza azma yake
na wakamuwekea watu wa kumfuatilia kuhakikisha kuwa hahami.
Suhaib Ar-Rumi akafanya
mbinu ya kutoroka lakini walimkamata njiani. Wakamwambia Suhaib hatutokuacha ufanikiwe kutoka kwetu kwa nafsi
yako na mali yako. Ulikuja katika mji wa Makka ukiwa fukara,
ukatajirika.
Suhaib Ar-Rumi akawaambia: Mnaonaje ikiwa nitawaachia mali zangu mtaniacha
na njia yangu? Wakamwambia,
Ndiyo. Wakachukua mali zake
zote na wakamwacha akaendelea na hijra yake.
Suhaib (Allah awe radhi naye)
alipofika katika mji wa Quba,
Mtume (rehema na amani ya Allah iwe juu yake) akamuona na
kumpa habari njema kwa
kumwambia Biashara yako imekuwa ya faida Abuu Yahya.
(Twabaqaat Ibnu Saad)
Hili ni tukio ambalo linatupa
mfano hai wa namna ya kujitoa
kwa ajili ya dini ya Allah Mtukufu, kufadhilisha radhi za Allah
kuliko maslahi ya kidunia. Suhaybu Ar-Rumi alikuja katika
mji wa Makka hali ya kuwa ni
mtu fukara mno, akajishughuli-

sha ndani ya mji huo na baada ya


muda akawa ni mtu mwenye
mali nyingi na wasaa mzuri katika maisha yake.
Hata hivyo, hakuelemea katika raha ya maisha aliyoipata
baada ya dhiki. Kwa kawaida
mtu anapokuwa amepitia machungu ya dhiki kisha baadae Allah akamneemesha kwa mali nyingi, huwa muoga sana na
mwenye mipango mingi ya
kumshughulisha asije akarejea
tena kwenye hali ngumu kama
aliyokuwa nayo mwanzo.
Lakini kwa Suhaib, (Allah
awe radhi naye) halikuwa jambo
lenye kumshughulisha wala kubadilisha mwelekeo wa maisha
yake, bali yeye alifadhilisha
mapenzi makubwa aliyokuwa
nayo kwa Allah na Mtume wake,
akituonesha kuwa dunia ni kitu
dhalili ambacho hakipaswi kufadhilishwa mbele ya Allah na
Mtume wake.
Suhaib aliwaachia Maquraishi mali yake yote ili wamwache
aendelee na msafara wake wa
kuhama kutoka Makka kwenda
Madina ili apate kuungana na
Mtume (rehema na amani ya Allah iwe juu yake).
Allah Mtukufu alimfahamisha Mtume (rehema na amani ya

Allah juu yake) tukio hilo la kiimani alilolifanya Suhaib. Hata


Suhaib (Allah awe radhi naye)
alipofika Quba, Mtume alimpokea kwa furaha kubwa na
akampa bishara kuwa Allah amemkubalia kwa kumwambia:
Biashara yako imekuwa ya faida
Abuu Yahaya, kwa kurejea neno
hilo mara tatu.
Kutokana na msimamo huu
wa kiimani aliounesha Suhaib
Ar-Rumi, Allah akateremsha
Aya ambazo zitakuwa zikisomwa
siku zote ikiwa ni sifa na tukio la
kuigwa lilifanywa na huyu Swahaba Mtukufu (Allah awe radhi
naye): Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu;
na Mwenyezi Mungu ni Mpole
kwa waja wake (Quran, 2:207).
Wamesema Ibnu Abbas, Anas
n a S a i d i b n u l - Mu s a y y i b ,
Ikrimah pamoja na kundi la
watu wengine kuwa Aya hii iliteremka kwa Suhayb Ibnu Sinaani Ar-Rumi pale aliposilimu
katika mji wa Makka, akataka
kuhama watu wakamzuia kuhama na mali yake, akajikomboa
kwa kuwapa mali yake. Allah
akateremsha Aya hii (tafsiir Ibnu
Kathir).
Tukio hili ni moja tu ya ma-

HILI NI TUKIO AMBALO LINATUPA


MFANO HAI WA NAMNA YA KUJITOA
KWA AJILI YA DINI YA ALLAH
MTUKUFU, KUFADHILISHA RADHI ZA
ALLAH KULIKO MASLAHI YA KIDUNIA

tukio ya mifano ambayo linatuonesha jinsi Maswahaba wa


Mtume (rehema na amani ya Allah iwe juu yake) walivyokuwa
na imani madhubuti, imani isiyoyumba hata kwa kufanyiwa na
vitimbi vya makafiri, na isiyotetereka mbele ya mambo ya kilimwengu.
Kwa hali ya binadamu wa leo
aliyepitia katika dhiki kisha akapata faraja si jambo rahisi kuicha
mali yake yote kwa ajili ya
kuitetea imani yake na dini yake.
Hilo linapatikana kwa Maswahaba tu na wema wengine wenye
mapenzi ya kweli kwa Allah na
Mtume wake.
Kuna mambo mengi mno yanayoonesha udhaifu wa imani
kwa Waislamu wa zama zetu
ambao wao badala ya kutoa mali
zao kwa ajili ya dini wanaitumia
dini kuchuma mali. Wakati
mwingine wanachukua hata
mali za Waislamu ambazo watu
walizitoa wakfu kwa ajili ya kuitumikia dini na kuziuza kwa ajili
na kutumia fedha hizo kwa kutatua shida binafsi.
Kwa ajili ya dini Suhaib (Allah awe radhi naye) alipoteza
kila kitu akachagua imani yake
kwa kutafuta radhi za Allah.
Ama, baadhi ya Waislamu leo hii
wapo tayari kuiharibu dini,
kuchezea imani zao kwa ajili ya
kuipata dunia.
Hii ni mifano miwili tofauti
kati ya watu walioipa nyongo
dunia na vilivyomo kwa ajili ya
dini ya Allah na watu wallioipa
nyongo dini kwa ajili ya maslahi

ya kilimwengu.
Mtume (rehema na amani ya
Allah iwe juu yake) alimwambia
Suhaib Ar-Rumi : Biashara
yako imekuwa ya faida Abuu
Yahya. Lakini watu hawa, wallioipa nyongo dini kwa ajili ya
maslahi ya kilimwengu, inafaa
tuwaambie biashara yenu imekuwa ya hasara.
Kuna namna nyingi mno za
kufanya biashara ya aina hii aliyoifanya Swahaba huyu wa
Mtume, licha ya tofauti kubwa
itakayokuwepo kati yetu sisi na
yeye ya hali, mazingira na umadhubuti wa imani.
Bado tunayo nafasi ya kufanya biashara za namna hii kwa
sababu kuna kutoa na kuchukua,
lakini katika biashara hii unachokitoa kinaonekana lakini unachokichukua hakionekani bali
kinategemea imani yako na utakasifu wa nia kwani hicho kinapatikana kwa Allah Mtukufu.
Njia za kutoa katika kheri ni
nyingi, maeneo ya kutoa ni mengi ambayo tumehamasishwa
ndani ya Quran na katika Sunnah za Mtume (rehema na amani ya Allah ziwe juu yake).
Tutumie neema za mali alizotupa Allah ili tufanye biashara
yenye faida. Uzito wa tukio la
Suhaib haupo katika wingi wa
mali aliyoiacha kwa ajili ya Allah
tu bali upo katika nia na imani
aliyokuwa nayo na utayari wa
kulifanya jambo kwa kufadhilisha radhi za Allah na kuonesha
mapenzi ya dhati kwa Allah na
Mtume wake.

Mwanza
Arusha

Kigoma
Tabora

Moro
Dsm

Masafa ya Imaan FM
1
2
3
4
5
6

Daresalaam
Morogoro
Arusha
Mwanza
Kigoma
Tabora

104.5 Mhz
96.3 Mhz
90.8 Mhz
105.6 Mhz
92.5 Mhz
101.6 Mhz

7
8
9
10
11
12

Mbeya
Dodoma
Ruvuma
Mtwara
Zanzibar
Pemba

90.3 Mhz
102 Mhz
94.2 Mhz
90.9 Mhz
104.5 Mhz
104.5 Mhz

Mbeya
Ruvuma
Mtwara

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

18
SEIF RUGA

lah ziwe juu yake): Watu wa aina


tatu wameondoshewa wajibu juu
yao, mtoto mdogo hadi atakapo
balehe, mwenda wazimu hadi
itaporudi akili yake na mtu aliyelala
hadi atakapoamka. Aidha, kiapo
cha mlevi hakiswihi kwa kule
kuondokewa na akili.

Maana ya yamini
Neno yamini katika muktadha
wa lugha ya kiarabu, asili yake ni
mkono wa kulia kinyume cha
mkono wa kushoto. Sababu ya
yamini kuitwa kiapo kwamba
Waarabu waliapa kwa kushikana
mikono ya kulia kuonesha msisitizo wa kile walichokiazimia juu
yake. Kwa kuzingatia mazingira
hayo, kiapo kikaitwa yamini.
Ama yamini kwa kisharia ya
Kiislamu ni kuweka msisitizo katika jambo, kwa kutaja jina miongoni mwa majina ya Allah Taala au
sifa miongoni mwa sifa zake.

Jina linalostahiki kuapiwa ni la Allah pekee


au sifa yake

Kiapo katika Quran na


Sunnah
Asili ya uwepo wa yamini (kiapo) kisharia ni kauli yake Allah aliyetukuka: Na timizeni ahadi ya
Mwenyezi Mungu mnapoahidi,
wala msivunje viapo baada kuvithibitisha, ilihali mmekwisha
mfanya Mwenyezi Mungu ndiye
mdhamini wenu. Hakika
Mwenyezi Mungu anayajua muyatendayo. (Quran 16:91).
Mwenyezi Mungu hakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyoapa
kweli kweli kwa makusudio. Basi
kafara yake ni kuwalisha masikini
kumi kwa chakula cha wastani
mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha,aukumkomboamtumwa.
Asiyepata hayo, basi afunge siku
tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapoapa. (Quran, 5:89).
Na kwa upande wa Sunnah
(hadithi) ushahidi wa kiapo ni
kauli yake Mtume (rehema na amani za Allah ziwe juu yake) ...Na
hakika mimi inshaallah, nikiapa
juu ya jambo, kisha nikakuta kuna
kheri katika jambo hilo nililoliapia,
hukitengua kiapo changu kwa kutoa kafara, na huindea kheri
hiyo(Bukhari).
Na umma wa Kiislamu kwa
pamoja (Ijmai) umekubaliana juu
ya uwepo wa sharia ya yamini na
kuthibiti hukumu zake.

Uapaji wenye karaha


Kuapa ni katika jambo
liloruhusiwa na sharia, kwa dalili
na ushahidi tulizokwishazitaja
huko nyuma, na wala si jambo la
makruhu chukivu - isipokuwa
ukaraha unakuja pale mtu anapopetuka mpaka kwa kuapa mara
kwa mara.
Na hii ni kwa ushahidi wa kauli
yake Allah Taala: Wala usimtii
kila mwingi wa kuapa wa
kudharauliwa.(Quran, 68:10).
Hili ni karipio linalohukumu ukaraha wa kitendo chenyewe. Na
iwapo yamini kiapo- hakitakuwa
na sifa ya upetukaji mpaka,
itakuwa si jambo la makuruhu,
isipokuwa pale kiapo kitakapoambatana na jambo la karaha.

Uapaji katika jambo la


wajibu
Uapaji wa aina hii ni ule ambao
una lengo la kumuokoa mtu asiyekuwa na kosa kuuliwa au kupata
madhara.
Uthibitisho wa hilo ni hadithi ya
Suwaid bin Handhala amesema:
Tulifunga safari kwenda kwa
Mtume (rehema na amni za Allah
ziwe juu yake). Akiwa pamoja nasi,

Maana na utaratibu
wa yamini (kiapo)
katika Uislamu (1)
Wail bin Hujur, akatokezewa ghafla na adui yake, ikawa watu wanababaika kuhusu kuapa, mimi
nikaapa kwamba yeye ni ndugu
yangu, yule adui yake akamwachia.
Tulipofika kwa Mtume wa Allah (rehema na amani za Allah ziwe
juu yake) nikamuhabarisha tukio
hilo ya kwamba mimi nimeapa
kuwa Wail ni ndugu yangu.
Mtume akasema, Umesema kweli
Muislamu ni ndugu wa Muislamu
mwingine(Abuu Daudi).
Uapaji katika jambo la Sunnah
Uapaji huu unahusisha maslahi baina ya mahasimu wawili au
unaondosha chuki na mifundo katika moyo wa Muislamu kutoka
kwa hasimu wake, au unaondosha
shari. Uapaji wa aina hii ni Sunnah
kwa sababu kufanya jambo hili
kumesuniwa, na yamini kiapoina hukumu na kupelekea katika
hilo.

Uapaji katika jambo la


haramu
Uapaji huu ni wa uongo. Hakika Allah Taala ameukaripia uapaji
wa aina hii kwa kauli yake: Huwauoni wale waliofanya urafiki na
watu ambao Mwenyezi Mungu
amewakasirikia? Hao si katika

nyinyi,wala si katika wao. Na huapa kwa uongo,na hali kuwa wanajua. (Quran, 58:14).
Na kwa kuwa uongo dhati yake
ni jambo la haramu, na utakapokuwa uongo huo umeapiwa,
huzidi mardufu uharamu wake.
Hutokea wakati ikaruhusiwa
kuapa juu ya jambo la uongo. Hii
ni pale itakapobainika uongo ni
sababu ya kuokoa maisha ya mtu
asiyekuwa na kosa, kwa kutaka kuuliwa kwa njia ya dhuluma.
Mfano, mtu asiyekuwa na kosa,
alijificha katika nyumba ya mtu
ambaye anafahamu kwa yakini
kuwa yeye hana kosa. Pindi
dhalimu na mbaya wake akimuulizia kwa minajili ya kutaka kumuua, inaruhusiwa kisharia kukanusha uwepo wake katika njumba
hiyo. Ukanushaji huu ni wa uongo,
lakini kisharia unaruhusiwa, na
tena ni wajibu kufanya hivyo kwa
kuwa ndani yake kuna uokoaji wa
maisha ya mtu asiyekuwa na kosa.

Uapaji katika jambo la


makuruhu
Huu ni uapaji wa kufanya jambo la makuruhu au kuacha jambo
la Sunnah. Allah aliyetukuka
amaesema: Wala msifanye jina la

Mwenyezi Mungu katika viapo vyenye kuwa ni kisingizio cha kuacha


kufanya wema na kumchamungu
na kupatanisha baina ya watu. Na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye
Kusikia na Mwenye Kujua.
(Quran, 2:224)
Kwa maana msimjaalie Allah
Mtukufu ni kizuizi kati yenu na
amali za kheri,miongoni mwa kutenda wema, uchamungu na usuluhishi baina ya watu.
Aidha, uapaji mwingine wa
makuruhu ni kuapa katika kuuza
kitu au kununua, kwa kauli yake
Mtume (rehema na amaani za Allah ziwe juu yake): Uapaji katika
biashara unaipendezesha na kuifigalia bidhaa lakini huindoshea
baraka.(Bin Maja).

Sharti za Mwenye
kuapa
Mtu anayaeapa ni sharti awe
balehe, mwenye akili timamu,
mwanaume au mwanamke, na
awe na kusudio la kuapa. Vilevile,
muapaji aape kwa hiari yake bila
ya kulazimishwa. Kiapo) cha mtoto mdogo, mwenda wazimu na
mtu aliyelala hakiswihi.
Uthibitisho wa haya ni hadithi
ya Mtume (rehema na amni za Al-

Mtume (rehema na amani ya


Allah ziwe juu yake) amesema:
Zindukeni. Hakika Allah
amewakataza kuapa kwa kutumia
majina ya baba zenu. Yoyote yule
anayeapa, aape kwa jina la Allah au
kama si hivyo, basi
anyamaze.(Bukhari).
Wanazuoni wa Kiislamu wamekubaliana kwa pamoja (Ijmai) ya
kwamba kuapa kwa asiyekuwa Allah ni haramu, na wala hairuhusiwi. Mfano wake ni kama mtu
kuapa kwa kutumia majina ya
Malaika, Mitume, wazee, AlKaaba n.k.
Na katazo hili la kuapa kwa asiyekuwa Allah limekuja kwa zingatio kwamba mtu anapotaja kitu,
dhamira na kusudio lake ni
kukitukuza kitu hicho. Na hakika
anayestahiki kutukuzwa ni Allah
pekee.
Na yeyote anayeapa kwa kutaja
kitu kingine, anakuwa amekitukuza kitu hicho kama anavyomtukuza Allah aliyetukuka. Na jambo hili
haliruhusiwi kisharia, na kwa kuzingatia hilo ndiyo maana kitendo
hicho kimeitwa cha kishirikina,
kwa kuwa amekishirikisha kitu
kingine katika utukufu anaostahiki
Allah pekee aliyetukuka kwa kule
kukitaja wakati wa kuapa.
Na hilo linathibitishwa na hadithi ya Mtume (rehema na amani
za Allah ziwe juu yake isemayo:
Yeyote atakayeapa kwa kuacha
kumtaja Allah atakuwa amekufuru au amefanya kitendo cha ushirikina. (Tirmidhi).
Na ibara ya ukafiri na ushirikina
imetajwa katika hadithi hii ili
kuonesha ukaripiaji mkubwa juu
ya uzito wa suala lenyewe. Lakini
uhalisia ni kwamba ushirikina huu
uliotajwa hapa, haumtoi muhusika
wake katika Uislamu.
Rai hii ni kwa mujibu wa jopo la
wanazuoni wa Kiislamu. Pamoja
na hivyo, hakika uapaji wa asiyekuwa Allah Taala ni uasi,
mkubwa, kiasi Mtume(rehema na
mani za Allah ziwe juu yake) ameutaja kwa jina la ukafiri na ushirikina - hata kama wanazuoni
wamesema kuwa ni ushirikina
usiomtoa muhusika wake katika
Uislamu.

Viapo vya Quran


Ndani ya Quran, Kitabu Kitakatifu cha Allah Taala vimekuja
viapo mbalimbali kwa kutaja vitu
visivyokuwa Allah Taala.
Maelezo na ufafanuzi wa jibu la
swali hili ni kuwa mosi, katika uapaji huo kumeondoshwa jina la Allah ndani yake na imekadiriwa
hivi, Naapa kwa jina la Mola Mlezi
wa jua na mwangaza wake, kama
ilivyokuja katika kauli yake Taala
isemayo: Naapa kwa jua na
mwangaza wake (Quran, 91:1) na
mfano wa viapo vingine vilivyokuja
ndani ya Quran katika uapaji wa
kutaja majina ya viumbe.

20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016

19

WATOTO / MALEZI

ABUU RAMLA

Mbinu za kuwajengea watoto


haiba na hulka za Kiislamu
Ujengaji haiba na tabia nzuri kwa
watoto wa Kiislamu maana yake ni
kumwezesha mtoto awe wa kiume na
wa kike kuutambua Uislamu wake
kifikra, kiakili, kivitendo, kitabia, lengo la kuishi, mtazamo wake katika uzingatiaji wa matukio, mahusiano yake
na watu wengine, juhudi zake za kuuenzi na kuueneza Uislamu na udumishaji wa haki na kuiondosha batili.
Kwa fasili na taarifa fupi, tunaweza
kusema kujenga haiba ya Kiislamu
maana yake ni kumjenga na kumfunda mtoto awe mwema, kuanzia ndani
ya nafsi yake hadi kwa watu wengine,
kwa kipimo cha Uislamu.

shaji wa Mungu mmoja asiyekuwa na


mshirika katika utawala wake na uungu
wake, ambapo Aya ya pili inaelezea uwezo wake Allah na ukubwa wa ujuzi na
elimu yake.
Uwezo na ujuzi wa Allah ni mkubwa
kiasi ambacho lau kama jema au baya la
mja linakuwa dogo mno kama punje ya
Kharadali kisha punje hiyo ikawa imejificha katika sehemu madhubuti kama
vile katika mwamba au jabali, au sehemu yoyote ile katika mbingu na ardhi,
hakika Allah ataidhirisha punje hiyo.
Haiwezi punje hiyo ikajificha kwake, bali
ataijua na kuibainisha. Hakika Yeye ni
Mjuzi wa mambo yaliojificha .

Ujengaji haiba nzuri katika Quran

Wema unapaswa uanze


ndani ya nafsi ya mtu

Miongoni mwa ushahidi mzuri katika kuwajengea watoto wetu haiba


na tabia nzuri ni simulizi za Allah
kwetu kupitia nasaha na mawaidha
ya Luqman kwa mtoto wake, kwa
muundo na njia ya kumnasihi.
Hivyo inatakikana kwa wazazi na
walezi kutumia nasaha hizi katika kuwaidhi na kuwanasihi watoto wao
kwa kuwa ndani yake kuna mafunzo
makubwa ya Uislamu. Na hapa tutaja
miongoni mwa nasaha na mawaidha
ya Luqman ambayo ndani yake kuna
mafundisho ya tabia nzuri.
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu
katika utawala wake na uungu wake
Miongoni mwa nasaha za Luqmani ni kumpwekesha Allah Taala na
kumfanya mmoja katika utawala
wake na uungu wake.
Na Luqman alipomwambia
mwanawe kumpa mawaidha, Ewe
mwanangu!UsimshirikisheMwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina
bila ya shaka ni dhuluma iliyokubwa.
Ewe mwanagu! Kikiwapo kitu cha
uzito wa chembe ya Khardali, kikawa
ndani ya jabali au ndani ya ardhi, basi
Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika
Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa Yaliyofichika, Mwenye Khabari zote.
(Quran, 31:13-16).
Aya ya kwanza inafafanua upweke-

Na miongoni mwa nasaha za Luqman kwa mtoto wake, alimuamuru


mtoto wake kuwa mwema kwa kuanza
na nafsi yake, kisha kuwageukia watu
wengine. Na wema wenyewe ni utekelezaji wa ibada za Allah Taala, hususan
ibada ya swala.
Nasaha na wasia huu tunaupata
kupitia kauli yake Luqman pale alipomnasihi mtoto wake, kama Allah Taala alivyotusimilia ndani ya Quran: Ewe
mwanangu! Shika Swala, na amrisha
mema na kukataza maovu, na subiri kwa
yanayokupata. Hayo ni katika mambo ya
kuazimiwa. (Quran 31:17).
Wanazuoni wa fani ya tafsiri ya Quran
wamesema Luqman alipomkataza mtoto wake na ushirikina alimuogofya kuhusu ukubwa wa Elimu na Ujuzi wa Allah
Mtukufu, kisha akamuamrisha kutekeleza ibada ya Swala. Hii ina maana ya
kwamba ibada ya swala ilikuwepo kwa
watu waliokuwa kabla yetu, waliopewa
sharia na Allah, isipokuwa ilitofautiana
utekelezaji wake.
Allah aliyetukuka katika simulizi ya
wasia wa Luqman kwa mtoto wake
anasema iwapo utaitengeneza vizuri nafsi yako, kwa utekelezaji wa ibada za Allah
Taala, kwa kufanya hivyo utakuwa na
nafasi nzuri ya kujenga na kufanya mabadiliko ndani ya nafsi ya mwenzako,
kwa ni jukumu la Manabii na warithi

Miongoni
mwa
ushahidi
mzuri katika
kuwajengea
watoto wetu
haiba na
tabia nzuri ni
simulizi za
Allah kwetu
kupitia
nasaha na
mawaidha ya
Luqman kwa
mtoto wake,
kwa muundo
na njia ya
kumnasihi.

wao wanazuoni lilikuwa ni kuzijenga vizuri nafsi zao na za wenzao.


Hii ndiyo njia nzuri ya malezi inayoleta tija na mafanikio, na huu ndiyo
uhakika ambao anapaswa kuujua kila
baba, mlezi na mwalimu. Hakuna jambo
zuri la faraja kwa mzazi au mlezi kama
kumuona mtoto wake akiwa mwema na
mwenye maadili mazuri.
Kama watu wema waliotangulia walilijua hilo na kuwafunda watoto wao, bila
shaka katika zama zetu hizi inatakikana
kuzidisha maradufu yake kutokana na
kukithiri vikwazo na vishawishi vinavyozuia kufanikisha jambo hilo.
Katika zama zetu kuna lukuki ya vigingi vinavyobuniwa kwa minajili ya kumfanya mtoto wa Kiislamu asimtii Mola
wake.
Fitina na vishawishi vimetapakaa kila
mahala kuanzia katika majarida, magazeti, runinga, mitaala, barabarani na
njiani, hadi katika usikilizaji wa vigano
na hikaya fitina imetamalaki na inawamgojea watoto wa Kiislamu. Mtu
binafsi anaweza akaishinda fitina hii, lakini kuokoka kwa mtu mmoja peke yake
hakuleti tija mpaka atakapookoka yeye
na watoto wake pamoja na familia yake.
Allah aliyetukuka anasema: Na
waamrishe watu wako kuswali, na uendelee mwenyewe kwa hayo, sisi hatukuombi wewe riziki, bali sisi ndiyo tunakuruzuku. Na mwisho mwema ni kwa
mchamungu. (Quran 20:132).
Mtoto siku zote hufuata tabia ya baba
yake. Pindi mtoto anapomuona baba
yake akiswali, ni lazima na yeye atafuata
tabia na mwenendo wa baba yake. Ni
muhali na vigumu mzazi kutarajia mtoto
wake awe mwema hali ya kuwa yeye
yupo tafauti na wema huo.
Ni silka ya mtoto kujifunza kupitia
fikra na picha, na wala hawezi kutafautisha kati ya mzizi wa kitu na mtu. Yeye
siku zote baba yake ndiyo mtu mwenye
hadhi ya juu, na wala hawezi kutenganisha kwa kusema Uislamu una hadhi
kubwa sana isipokuwa dosari ipo upande
wa baba yangu.
Mtoto siku zote humtazama baba
yake kuwa ndiyo Uislamu, akifanya jam-

bo baya, fikra ya mtoto huliona zuri. Haiyumkiniki kutarajia mtoto wako awe
mwema, ikiwa wewe mwenyewe hukuvaa joho la wema.

Kujiepusha na sifa ya kiburi


na muenekano wake
Na katika wasia wa Luqman kwa
mtoto wake ni kumtaka awe na tabia
njema na kujieupusha na tabia mbaya
kwa sababu kujiepusha na tabia mbaya
kunapewa uzito zaidi kuliko kujipamba
na tabia nzuri na tukufu. Na kujiepusha
na tabia mbaya ni aina fulani ya kujipamba na tabia njema na tukufu.
Na miongoni mwa tabia ovu zaidi ni
mtu kujifanya mwapuza wa kutojua thamani ya nafsi yake, kiasi cha kuikabidhi
na kuiweka rehani katika lindi la machafu, ikwemo tabia ya kiburi.
Hili linajieleza kupitia simulizi ya Allah Taala katika wasia wa Luqman kwa
mtoto wake: Wala usiwabeuwe watu,
wala usitembee katika nchi kwa maringo.
hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila
anayejivuna na kujifaharisha. (Quran,
31:18).
Ubainifu wa Aya hii ni kwamba wakati Luqman alipomuamuru mtoto wake
kupitia wasia wake kwa kumweleza
kuwa wema ni lazima uanze ndani ya
nafsi yako, kisha ndiyo uitengenezi nafsi
ya mwenzako, alihofia kwa mtoto wake
mambo mawili.
Mosi, alihofia mtoto kujenga kiburi
kwa watu wengine, kwa kule kujiona
yeye ni msulihishaji wa tabia za wengine.
Pili, alihofia mtoto kujitengenezea mazingira ya ria ndani yake kutokana na kitendo cha kuitngeneza vizuri nafsi yake.
Ujengaji haiba nzuri kupitia Sunnah
Imamu Tirmidhi amepokea hadithi
kutoka kwa Ibn Abbas, (Allah amridhie)
amehadithia kuwa siku moja alikuwa
nyuma ya Mtume (rehema na amani za
Allah ziwe juu yake ) akasema: Ewe kijana, hakika mimi nitakufundisha
maneno yafuatayo, Mhifadhi Allah Taala
kwa kutekeleza amri zake na kujiepusha
na makatazo yake, naye Allah atakuhifadhi. Mhifadhi Allah utamkuta yupo uapande wako, na pindi utakapotaka
kuomba, basi muombe Allah, na ukihitaji msaada wa jambo la kidunia na
akhera, basi mtake msaada Allah.
Na jua kwamba lau umma wote ungelikusanyika upande wako ili upate
kukunufaisha, usingefanikiwa katika
hilo, ila lile ambalo Allah Taala ameshalithibitisha yeye mwenyewe. Na lau
kama watu wote watakusanyika dhidi
yako, juu ya kukudhuru wewe katika
jambo fulani, hawawezi kufanikiwa katika hilo, ila lile ambalo Allah Taala
mwenye ameshalithibitisha juu yako. Allah Taala ameshaweka makadirio yake
kwa viumbe.

Kanuni za
Biashara
katika
Uislamu
Uk 13
20 DHUL HIJA, 1437 ALHAMISI SEPTEMBA 22 - 28, 2016
NA MUGINI SINGIRA

imi ni mtu mzima


mwenye akili timamu sijawahi kuugua kichaa
hata siku mmoja tangu
utoto wangu na sasa nina miaka
49. Sijalazimishwa na mtu yeyote
kuingia katika Uislamu. Nimeingia mwenyewe kwa ridhaa yangu
baada ya kuipenda dini hii tukufu.
Hayo yalikuwa ni maneno ya
Sophia Kenani Samfundo, mwanamama aliyesilimu hivi karibuni
katika msikiti wa Mtoro.
Kauli ya Sophia inakubalina na
Aya Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake kitukufu cha Quran.
Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika dini, uongofu umekwisha pambanuka na upotofu, basi
anayemkataa shetani na akawamini Mwenyezi Mungu, bila shaka
yeye ameshika kishiko chenye nguvu kisichokuwa na kuvunjika, na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye
kusikia na mwenye kujua (Quran,
2:256)
Siku aliyosilimu Sophia hakuwa
peke yake. Wanawake wengine
watatu nao walijitokeza kusilimu
msikiti katika msikiti wa Mtoro,
ingawa kila mmoja alikuja kusilimu kivyake. Allahu Akbar.
Nilikutana na dada Sophia hivi
karibuni na kuzungumza naye na
kunielezea historia yake mpaka aliposilimu. Yeye ni mzaliwa wa
Mbeya. Aliolewa mwaka 1982 na
kubahatika kupata watoto wawili
lakini hata hivyo walifariki baada
ya kupata ajali ya gari wao pamoja
na mume wake, Innaa Lillaahi
Wainna Ilayhi Rrajiuun. Huo
ulikuwa ni mwaka 1992.
Mwanzo, Sophia alikuwa ni
muumini Kanisa wa Kikristo katika dhehebu la Roman Katoliki
hadi kubatizwa kwake. Aliabudu
katika kanisa hilo akiwa Ifakara
Mkoani Morogoro hadi baadae alipoamua kubadili kuhamia dhehebu la Pentekosite ambako alisomea dini hadi kupata uchungaji.
Sophia alinambia kipindi akiwa
mfuasi wa dhehebu la Roman Katoliki alijitahidi kusoma huku akifanya utafiti, hali iliyompelekea
kugundua kuwa Roman wanawanyima waumini wao uhuru wa
kusoma Biblia ili wasingundue
yaliyoandikwa ndani ya kitabu hicho. Ilikuwa ni viongozi pekee ambao walikuwa wakisoma Biblia.
Hali hiyo ilimpelekea kuamua
kuhama Roman Katoliki na kuanza kuabudu katika kanisa la kiPentekosti lililopo Banana Gongo
la Mboto jijini Dar es Salaam. Ni

SOPHIA
SAMFUNDO
Kutoka Ulokole hadi Uislamu

katika kanisa hilo ndipo alipoanza


kusoma mpaka kuwa mchungaji.
Sophia alisema amekuwa akishikilia nyadhifa mbalimbali kanisani kwake hapo ambako alikuwa
akiabudu hadi wiki iliyopita. Baadhi ya nyadhifa hizo ni pamoja na
kuwa Mama Kikundi cha
Maombezi, Mwalimu na Mlezi wa
watoto katika shule ya kanisa.

Kusilimu kwake
Akiwa anasali kanisa lake la
Pentekoste, siku moja Sophia alienda kusali na kawaida yake akiwa
kiongozi - Mama wa Maombezi na
Mlezi - alikuwa anakaa mlangoni
ili wasichana waliovaa sketi fupi
wakiingia anawapa sketi ndefu zinazoweza kustiri miili yao.
Jambo hilo halikumpendeza
Mchungaji Mkuu wa Kanisa ambaye alipinga utaratibu huo. Sophia
alisikitika kuona kuona Mchungaji
wake hataki watu wawe katika
mazingira ya kujihifadhi katika ki-

heshima badala yake akawa anataka waabudu huku wakiwa


wamevaa hizo nguo fupi.
Katika Uislamu Mwenyezi
Mungu ametaja suala hili aliposema: Ewe Mtume waambie wake
zako, na binti zako, na wanawake
wa Kiislamu (wengine waambie)
wajiteremshie uzuri nguo zao, kufanya hivyo kutapelekea upesi wa-

julikane (kuwa ni watu wa heshima


ili) wasiudhiwe, (na) Mwenyezi
Mungu ni Mwingi wa Kusamehe
na Mwingi wa Kurehemu.
(Quran, 33:59)
Sophia alisema kufuatia hali
hiyo ya Mchungaji Mkuu kutaka
watu waabudu wakiwa wamevaa
kama wako uchi ilipelekea kutokea
mgogoro na hivyo yeye kuamua

MWANZO, SOPHIA ALIKUWA NI


MUUMINI KANISA WA KIKRISTO
KATIKA DHEHEBU LA ROMAN
KATOLIKI HADI KUBATIZWA
KWAKE. ALIABUDU KATIKA
KANISA HILO AKIWA IFAKARA
MKOANI MOROGORO HADI BAADAE
ALIPOAMUA KUBADILI KUHAMIA
DHEHEBU LA PENTEKOSITE
AMBAKO ALISOMEA DINI HADI
KUPATA UCHUNGAJI

kuacha kwenda kanisani kwa miezi minne kuanzia April 24, 2016.
Tukilinganisha na mafunzo ya
Uislamu, Allah anasema: Bila
shaka dini (ya haki) mbele ya
Mwenyezi Mungu ni Uislamu na
waliopewa kitabu Mayahudi na
Manasara) hawakukhitalifiana ila
baada ya kuwajia ilimu, (Walikhitalifiana) kwa sababu ya uhasidi
uliokuwa baina yao, na
anayezikataa aya za Mwenyezi
Mungu ni mwepesi wa kuhisabu.
(Quran, 3:19)
Wakati huo wa miezi minne
ambayo hakuwa akienda kanisani,
Sophia alikuwa akifikiria juu ya
suala hilo huku akiwa ni mwenye
kukata tamaa. Kila alipojaribu
kupanga siku kwenda alijikuta
akiahirisha bila dharura yoyote ya
msingi.
Sophia anasema wakati alipokuwa bado Mkristo alikuwa alidadisi kuhusu Uislamu kwani
alikuwa akiishi na jamii ya Waislamu. Sophia aliwauliza watu waliokuwa akiishi nao mambo
mbalimbali ya Uislamu hadi wazo
la kuingia katika Uislamu lilimjia
kichwani.
Sophia alivutiwa na baada utaratibu na mienendo ya dini hii tukufu ya Uislamu hususan katika
mambo ambayo alikuwa akigombana na mchungaji wake, suala la
wasichana kwenda kuabudu wakiwa nusu uchi.
Sophia anasema ilifika wakati
akaanza kutolewa mtu usingizini
akimueleza kuwa yeye (Sophia) ni
mtu msafi na anafaa kuwa Muislamu na mara nyingine aliota anaenda msikitini huku akiongozwa na
mtu huyo aliyevaa kanzu. Huu
ulikuwa ni msumari wa mwisho.
Sophia hakuhitaji ishara zaidi
bali aliamua kushuhudia kuwa:
Hakika apasaye kuabudiwa kwa
haki ila Allah na Muhammad ni
Mtume wake. Hakika Mwenyezi
Mungu humzindua amtakaye na
kumuelekeza katika uongofu.
Karibu dada Sophia katika Uislamu.

HUTOLEWA NA KUCHAPISHWA na The Islamic Foundation, P.O. Box 6011 Morogoro, Tanzania E-mail: imaanmedia3@gmail.com

You might also like