Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 32

1

JIVUNIE KISWAHILI
UAMILIAJI LUGHA SARUFI MAJUMUI NA UAMILIAJI LUGHA YA PILI.
Makala haya yataangalia maana ya sarufi majumui, masuala ya msingi yanayohusu
maarifa ya lugha, sifa za sarufi majumui, sarufi majumui na uamiliaji lugha ya pili na
mwisho tathmini. Kwa mujibu wa Chomsky (1976:29) kama alivyonukuliwa na Ellis
(1996:430) sarufi majumui ni mfumo wa kanuni na sheria ambazo ni msingi wa lugha
za binadamu (tafsiri yangu). Muasisi wa nadharia hii ni Noam Chomsky. Msingi wa
nadharia hii ni kwamba binadamu anapozaliwa anakuwa na maarifa asilia ambayo
humsaidia katika ujifunzaji lugha; mambo ya ndani na nje ambao husaidia katika
uamiliaji wa lugha. Maarifa haya hupatikana pale tu binadamu anapozaliwa kwani
huwa na kifaa cha uamiliaji lugha ambacho kinakuwa na kanuni majumui na kanuni
badilifu ambazo hukutana na tajiriba (uwezo wa jamii katika lugha) na kusababisha
uamiliajli lugha kutokea. Waamiliaji wa lugha ya kwanza huwa na maarifa asilia
ambayo huwawezesha kuiamili lugha yao kwa kutumia maarifa hayo. Hivyo maarifa
hayo yanaamshwa na tajiriba ambayo mjifunzaji anaikuta katika jamii iliyomzunguka
na hatimaye kukutana na maarifa asilia katika kifaa cha uamiliaji lugha hatimaye
kuzalisha sarufi mahsusi ya lugha husika. Waamiliaji wa lugha ya pili wanakuwa na
lugha ya kwanza ambapo sifa za sarufi majumui bado humwezesha kuamili lugha ya
pili, kwani kanuni badilifu na kanuni majumui zilizojengwa kwa misingi ya lugha ya
kwanza hutumika katika kuamilia lugha ya pili. Hivyo kwa mujibu wa nadharia ya
sarufi majumui inamsaidia mjifunzaji katika kuamili lugha ya pili. Wataalam
mbalimbali wameweza kujadili juu ya uwezo wa sarufi majumui wa kuwa kifaa
weazeshi cha kujifunza lugha ya pili, kuna wataalam wanaokubali na wanaokataa
mchango huo. Kama Flyn (1984-1987) anavyoelezea kama alivyonukuliwa na Ellis
(1996:453) kifaa cha uamiliaji lugha ya kwanza kitahusika na mchakato wa ujifunzaji
lugha ya pili. Akaendelea kusema kanuni badilifu za lugha ya kwanza na lugha ya pili
zikiwa sawa ujifunzaji utakuwa rahisi kwa sababu mjifunzaji wa lugha ya pili ana
uwezo wa kuhusisha miundo wakati kanuni hizo zikitofautiana kati ya lugha ya

kwanza na lugha ya pili ni vigumu kujifunza. Flyin yeye anaunga mkono juu ya
sarufi majumui kuwa kifaa wezeshi katika ujifunzaji wa lugha ya pili. Kwani
anaamini bado maarifa ambayo mjifunzaji wa lugha ya kwanza anayoyatumia katika
ujifunzaji wa lugha hiyo, ndiyo yale yale anayoyatumia mjifunzaji wa lugha ya pili.
Hata hivyo Clahsen na Muysken (1986-1991) kama walivyonukuliwa na Ellis
(1996:454) wanasema uamiliaji wa lugha ya pili ni tofauti na uamiliaji lugha ya
kwanza muamiliaji lugha ya kwanza huwa na kifaa wezeshi cha uamiliaji lugha
wakati wa lugha ya pili hutumia mbinu za lugha ya kwanza katika kujifunza lugha ya
pili wanaendelea kusema muamiliaji lugha ya pili huhitaji nadharia ya isimu wakati
wajifunzaji lugha ya pili huhitaji naharia tambuzi. Hata hivyo sarufi majumui
imeangaliwa katika mitazamo tofautitofauti, hivyo kuonesha ubora lakini pia
mapungufu yake katika ufundishaji wa lugha: Kwa kuwa na sarufi majumui tunaona
kuwa sifa za lugha huingiliana, hivyo mwingiliano wa lugha ya kwanza na ya pili
unaweza kumwezesha muamiliaji lugha ya pili pale miundo ya lugha ya kwanza na
lugha ya pili itafanana na hata ikitofautiana mjifunzaji anakuwa na uwezo wa
kujiundia miundo yake itakayomsaidia katika ujifunzaji wake kwa kutumia sifa
majumui za lugha. Flynn (1984;1987) kama alivyonukuliwa na Ellis(1996;453)
anaeleza kuwa kifaa cha uamiliaji lugha ya kwanza kinaweza kutumika katika
uamiliaji wa lugha ya pili. Kama kanuni badilifu za lugha ya kwanza na ya pili
zinauhusiano hurahisisha ujifunzaji. Hivyo yeye anakubali kabisa kuwa sarufi
majumui ni kifaa wezeshi katika ujifunzaji wa lugha ya pili, anaamini sifa za
mjifunzaji wa lugha ya kwanza ndizo ambazo anakuwa nazo mjifunzaji wa lugha ya
pili. Aidha Ellis (1994:461) anaeleza ubora wa sarufi majumui kuwa imetoa msingi
wa uibukaji wa nadharia zingine za ujifunzaji lugha baada ya kuegemea kwenye
maarifa asilia anayozaliwa nayo binadamu. Pia imeweza kueleza sifa majumui za
lugha mbalimbali za ulimwengu kwa ufupi, hivyo kusababisha sifa za lugha
kueleweka kwa urahisi kwa wajifunzaji wa lugha ya pili. Kwa mujibu wa Ellis
(1994:458) udhaifu huu unajidhihirisha katika maeneo kadhaa, kiini cha sarufi
majumui yenyewe, pia mbinu zilizotumika kukusanyia data. Hivyo inaonekana kuwa

kuna tatizo katika mbinu za ufundishaji na namna ya ufundishaji wa lugha ya pili.


Nadharia ya sarufi majumui haikuonyesha namna gani mjifunzaji anapata ujuzi wa
kutumia maarifa asilia aliyozaliwa nayo lakini pia mbinu iliyotumia katika
ukusanyaji wa data ni ile mbinu ya kukusanya data isiyo ya vipindi maalum. Hivyo
kupelekea data zake kutoweza aminika. Vilevile clahsen na Muysken (1986),
Meisel(1991) kama walivyonukuliwa na Ellis (1996;454) muamiliaji wa lugha ya pili
atakuwa tofauti na muamiliaji wa lugha ya kwanza kwa sababu kifaa cha uamiliji
lugha kipo tu kwa mtu anayejifunza lugha ya kwanza na yule anayejifunza lugha ya
pili huweza kusaidiwa na maarifa/mbinu mbalimbali ya ufundishaji na mazingira.
Hivyo hawa wanaona kuwa safuri majumui si kifaa wezeshi katika ujifunzaji wa
lugha ya pili. Kuibuka kwa nadharia zingine kunaonesha udhaifu wa nadharia ya
sarufi majumui, mfano Fabisz, N.[1] Anaelezea nadharia ya uzawa iliyoasisiwa na
Andersen ambayo inasisitiza juu ya urithishaji wa lugha, pia nadharia ya
utamadunishi iliyoasisiwa na John Schumann (1978)inayosisitiza jinsi utamaduni wa
jamii ulivyo na mchango mkubwa katika ujifunzaji lugha kwani lugha huendana na
utamaduni mfano ni vigumu kujifunza lugha ya kiingereza kwa mswahili kwasababu
tunatofautiana katika utamaduni hata kama utajua kiingereza hautafanana na
mwingereza mzawa kwa kuwa yeye atatumia miundo ya lugha hiyo akihusisha na
utamaduni wake. Hivyo katika kujifunza lugha sarufi majumui sio kifaa wezeshi
pekee cha uamiliaji lugha pekee ambacho hutumika bali kuna vitu kama mazingira,
motisha na urudiaji wa mara kwa mara humpelekea muamiliaji lugha ya pili
kujifunza lugha ingawa kuna utofauti wa uamiliaji kuna wengine huchukua muda
mrefu na wengine muda mfupi, si lazima waamiliaji wa lugha ya pili wawe na sarufi
majumui inayofanana, hivyo tofauti zao wakati mwingine haziepukiki. Kama ubora
na udhaifu wa sarufi majumui unavyojidhihirisha, hii inaonesha kuwa sarufi majumui
peke yake haitoshi kumfanya mjifunzaji wa lugha aweze kuamili lugha ya pili vizuri,
hivyo walimu wanashauriwa kutumia nadharia changamani katika ufundishaji wao
wa lugha ya pili ili kumwezesha mjifunzaji wa lugha ya pili kuamili lugha hiyo
vizuri. Kimsingi sarufi majumui inajidhihirisha kuwa ni kifaa wezeshi katika

ujifunzaji wa lugha ya pili licha ya kuwa na udhaifu wake, haipelekei kuiondoa


katika hali ya uwezeshi katika ujifunzaji wa lugha ya pili, kwani sifa majumui
zinazopatikana katika lugha mbali kwa kiasi kikubwa zinawasaidia wajifunzaji
kujifunza lugha ya pili, mfano wajifunzaji wanapogundua miundo ya lugha na
uundaji wa misamiati unaolingana itawawia rahisi katika ujifunzaji wao. Lakini hata
ikitofautiana sarufi majumui imefafanua namna ambavyo mjifunzaji huyu ataweza
kujiundia sarufi yake ambayo itakuwa imejengeka kwa misingi ya lugha ya kwanza.
Kuna umuhimu wa kuwa na mazingira bora ya ujifunzaji ambapo mawasiliano
yanapewa msisitizo mkubwa katika nadharia mbalimbali, hivyo walimu hawana budi
kujenga mazingira hayo kwa wanafunzi wao ili waweze kujifunza lugha ya pili kwa
usahihi. Ikiwa ni pamoja na kubadilisha mazingira ya darasa kuwa mazingira rafiki
kwa mwanafunzi ambapo mawasiliano ndiyo kiini cha ujifunzaji. Nadharia ya sarufi
majumui imeonekana ina mchango mkubwa katika tendo la ujifunzaji, lakini haitoshi
kusema ndiyo nadharia pekee ambayo inapaswa kutumiwa na walimu katika
ufundishaji wao kwani pia imeonekana kuwa na udhaifu, hivyo nadharia zingine
kama za utamadunishi, uzawa na urithishaji ni muhimu kuzipa umuhimu pia ili tendo
zima la kujifunza liweze fanyika, lakini pia cha msingi ni kujua wajifunzaji hawawezi
kuwa na uwelewa wa aina moja hata kama haya yote yatatimia, hivyo
kinachoangaliwa ni kufikia ile hali ya kawaida katika matumizi ya lugha, ambapo
kila mjifunzaji anatarajiwa afikie.
ISTILAHI
External approach - mkabala wa nje
Intuition - ujuzi
Internal approach - mkabala wa ndani
Parameter - kanuni badilifu
Principles - kanuni majumui
Prompted - Papo hapo
Universal grammar - sarufi majumui

MAREJEO Ellis, R. (1994), Second Language Acquisition, USA: Oxford University


Press Fabisz, N. ANALYSIS OF KRASHENS THEORY OF SECOND
LANGUAGEACQUISITION,http://webspace.webring.com/people/ap/panandrew/sla
.html,

FONOLOJIA YA KISWAHILI UTANGULIZI USULI WA TAALUMA YA


FONOLOJIA
Neno fonolojia linatokana na maneno mawili ya Kigiriki phone-sauti za kusemwa na
logos- taaluma/mtalaa. Masimulizi yanadai kuwa taaluma hii ilianza zamani sana kati
ya mwaka 460 kabla ya Masihia huko India ya kale, ambapo mtu aliyeitwa Panini, na
ambaye huaminika kuwa ni baba wa isimu aliandika kuhusu fonolojia ya Kisansikriti
katika matini aliyoiita Shiva Sutras. Ni katika andiko hili ndipo alipobainisha kuwepo
kwa dhana ambazo leo hii hujulikana kama fonimu, mofimu na mzizi. Baada ya
andiko hilo, habari za taaluma ya fonolojia ni kama zilipotea kabisa katika uwanja wa
isimu hadi ilipofika karne ya 19 ambapo wanaisimu wengine waliibuka na
kuzungumzia upya masuala ya fonolojia. Miongoni mwa wanaisimu wa mwanzo
wanaotajwa kujihusisha na fonolojia ni Mpolandi "Jan Baudouin de Courtenay" ,
(pamoja na mwanafunzi wake wa zamani "Mikoaj Kruszewski" alipobuni neno
fonimu mnamo mwaka 1876, na kazi yake, ijapokuwa hairejelewi sana, inachukuliwa
kuwa ni mwanzo wa fonolojia mamboleo. Mwanaisimu huyu si tu alishughulikia
nadharia ya fonimu, bali pia vighairi vya kifonetiki (ambavyo leo huitwa alofoni na
mofofonolojia). Maandishi ya Panini (Sarufi ya Kisanskriti) pamoja na Jan Baudouin
de Courtenay yalikuja kuwa na athari kubwa kwa anayeaminika kuwa baba wa
nadharia ya Umuundo Mamboleo, Ferdinand de Saussure, ambaye pia alikuwa ni
profesa wa Sansikriti. Wanaisimu wote hawa walikuwa wanajaribu kulinganisha sauti
za lugha za Asia Mashariki na za Ulaya, lengo lao likiwa ni kujua mizizi ya lugha
zilizoitwa India-Ulaya. Kutokana na mkabala huo, katika kipindi hicho isimu ilikuwa
Isimu-linganishi tu. Kutokana na tafiti zao hizo waliweza kupata maneno yenye sauti
na maana zilizolingana, kufanana au kukaribiana. Utafiti huo uliweza kugundua jamii
mbili za lugha ambazo ni jamii ya lugha za Kirumi na jamii ya lugha za Kijerumani.
Baadhi ya wanaisimu mahususi kabisa wanaokumbukwa kuchangia katika maendeleo
ya fonolojia ni pamoja na: (i) Jan Baudouin de Courtenay (1845-1929) Kama

ilivyoelezwa hapo awali, huyu ni mwanaisimu aliyebuni dhana za foni na fonimu.


Katika nadharia yake, alidai kuwa sauti za mwanadamu ni za aina mbilifoni na
fonimu. Alisema kuwa foni ni sauti za kutamkwa tu lakini fonimu ni sauti za lugha.
Hata hivyo, de Courtenay hakutumia istilahi za foni na fonimu (kama zinavyotajwa
sasa) bali alitumia istilahi za anthrophonicsfoni na psychophonicsfonimu. Yeye
alidai kuwa foni zipo karibu sana na taaluma ya kumuelewa binadamu pamoja na
alasauti zake ambazo kwa hakika hutofautiana sana na za wanyama wengine. Na
kuhusu fonimu, alidai kuwa zinahusu kumwelewa binadamu pamoja na akili zake na
namna anavyofikiri katika akili yake. Alidai kuwa, mara nyingi, binadamu hupokea
kinachotamkwa na kufasiliwa. (ii) Ferdinand de Saussure (1887-1913) Ni
mwanaisimu wa Kiswisi anayejulikana kama baba wa isimu kutokana na mchango
wake alioutoa katika taaluma hii. Yeye anakumbukwa zaidi kutokana na uwezo wake
wa kutofautisha dhana alizoziita languemfumo wa lugha mahsusi na parole
matamshi ya mzungumzaji wa lugha husika. Langage hufafanuliwa kuwa ni uwezo
alionao mzungumzaji wa lugha mahususi wa kuzungumza na kuelewa matamshi ya
mzungumzaji mwingine wa lugha hiyohiyo. Ni sehemu ya lugha inayowakilisha
maarifa kati ya sauti na alama. Ni mfumo wa alama kwa maana ya kiufundi tu. Dai
lake la msingi ni kuwa alama inategemea vitu viwilikitaja na kitajwahivyo ili
mawasiliano yafanyike, mfumo wa ishara lazima ufahamike na ukubaliwe na
wanajamii wote. Kwa upande wa parole, anadai kuwa ni matendo uneni. Ni namna
lugha inavyotamkwa katika hali halisi na mtu mmoja mmoja. Dhana ya parole
inalingana na dhana ya performance (utendi) ya Noam Chomsky. Katika lugha,
parole ni matamshi tofauti ya sauti mojaalofoni. Wanaisimu wanaonekana
kukubaliana na madai ya Saussure kwakuwa inaelekea kuthibitika kuwa hakuna
uhusiano wa moja kwa moja kati ya kitaja na kitajwa [alama (lugha) na
kinachowakilishwa (masilugha)], bali makubaliano baina ya wazungumzaji wa lugha
moja husika ndiyo hutawala. (iii) Nikolai Trubetzkoy (1890-1939) Ni miongoni mwa
waanzilishi wa taaluma ya fonolojia akichota mizizi ya taaluma ya isimu kutoka
katika Skuli ya Prague. Mwanaisimu huyu aliandika misingi ya fonolojia kwa

kutumia maarifa yaliyoibuliwa na Ferdinand de Saussure. Ni mtaalamu wa kwanza


kufasili dhana ya fonimu. Aliandika vitabu vingi kwa lugha ya Kijerumani, miongoni
mwake ni Grundzge der Phonologie (Principles of Phonology, 1939), ambapo ni
katika kitabu hicho ndimo alimotoa fasili ya fonimu pamoja na kubainisha tofauti
baina ya fonetiki na fonolojia. (iv) Noam Chomsky (1928-) Huyu ni mwanaisimu wa
Kimarekani anayevuma sana kwa mchango wake katika taaluma ya isimu kwa
ujumla. Dhana za competence (umilisi) na perfomance (utendi) zimemfanya awe
maarufu ulimwenguni. Dhana hizi zinaelezea tofauti baina ya maarifa na udhihirishaji
wa maarifa hayo ya mtumiaji wa lugha. Katika fonolojia, Chomsky anakumbukwa
kwa ufafanuzi wake wa dhana ya fonimu kwa mtazamo wa kisaikolojia.
Anapochunguza dhana hii, hudai kuwa fonimu ni tukio la kisaikolojia, hivyo fonimu
zimo kichwani mwa mzungumzaji wa lugha. (v) Daniel Jones (1881-1967) Ni
mwanafonetiki kinara na maarufu kabisa katika nusu ya kwanza ya karne ya ishirini.
Ni Mwingereza msomi ambaye alikuwa na shahada ya kwanza ya hisabati na shahada
ya mahiri ya sheria, shahada ambazo hata hivyo, hakuwahi kuzitumia. Baadae,
alisomea lugha na kuhitimu shahada ya uzamivu. Daniel Jones alifunzwa fonetiki na
maprofesa mbalimbali, japokuwa aliathiriwa zaidi na Paul Passy na Henry Sweet.
Hamu yake kuu ilikua kwenye nadharia ya fonetiki. Anafahamika zaidi kwa
ufafanuzi wa dhana ya fonimu kwa mtazamo wa kifonetiki (ufafanuzi wake
tutauchunguza katika sehemu ya mitazamo ya dhana ya fonimu).
FONETIKI NA FONOLOJIA
Fasili ya taaluma ya fonolojia haiwezi kukamilika, na pengine kueleweka, iwapo
hakuna linalosemwa kuhusiana na taaluma ya fonetiki. Hali hii inatokana na ukweli
kuwa kuna uhusiano wa kinasaba kati ya fonolojia na fonetiki. Massamba na
wenzake (2004:5) wananeneleza ukweli huu kwamba: fonetiki na fonolojia ni
matawi mawili tofauti ya isimu lakini yenye kuhusiana sana. Uhusiano wa matawi
haya unatokana na ukweli kwamba yote mawili yanajihusisha na uchunguzi na
uchambuzi unaohusu sauti za lugha za binadamu. Kutokana na ukweli huu, jitihada

za kufasili dhana ya fonolojia inaelekea kuwa nyepesi, dhana hizi mbili


zinapofasiliwa kwa mlinganyo.
Tuanze na fonetiki:
FONETIKI NI NINI?
Fonetiki ni tawi la isimu linalochunguza sauti za kutamkwa na binadamu ambazo
huweza kutumika katika lugha asilia. Massamba na wenzake (kama hapo juu)
wanafasili fonetiki kuwa ni tawi la isimu linalohusika na uchunguzi na uchambuzi wa
taratibu za utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji, na ufasili wa sauti za lugha za
binadamu kwa ujumla. Wanasisitiza kwamba, kinachochunguzwa katika fonetiki ni
[maumbo] mbalimbali ya sauti zinazoweza kutolewa na alasuti za binadamu (yaani
sauti za binadamu zinazotamkwa tu). Kipashio cha msingi cha uchambuzi wa
kifonetiki ni foni. Foni ni sauti yoyote inayotamkwa na binadamu na inayoweza
kutumika katika lugha fulani. Hivyo basi, foni ni nyingi sana na hazina maana
yoyote. Wanafonetiki hudai kuwa foni zimo katika bohari la sauti (dhana dhahania)
ambalo kila lugha huchota sauti chache tu ambazo hutumika katika lugha mahususi.
Sauti chache zinazoteuliwa na lugha mahususi kutoka katika bohari la sauti huitwa
fonimu. Matawi ya Fonetiki: Kuna mitazamo miwili tofauti kuhusiana na matawi ya
fonetiki. Mtazamo wa kwanza ni unaodai kuwepo matawi matatu; na mtazamo wa
pili ni unaodai kuwepo matawi manne. Mtazamo wa kuwepo matawi matatu unataja
fonetiki matamshi, fonetiki akustika, na fonetiki masikizi. Mtazamo wa kuwepo
matawi manne (kama Massamba na wenzake (kama hapo juu), pamoja na matawi
tuliyokwisha yataja, wanongezea tawi fonetiki tibamatamshi. Fonetiki matamshi
huchunguza jinsi sauti za lugha zinavyotamkwa kwa kutumia alasauti. Hususani,
huchunguza namna na mahali pa kutamkia sauti husika. Fonetiki akustika
huchunguza jinsi mawimbi ya sauti yanavyosafiri kutoka katika kinywa cha mtamkaji
hadi kufika katika sikio la msikilizaji. Fonetiki masikizi hujihusisha na mchakato wa
ufasili wa sauti za lugha, hususani uhusiano uliopo baina ya neva za sikio na za
ubongo. Na fonetiki tibamatamshi ni tawi jipya lililozuka mwanzoni mwa karne hii,
ambalo huchunguza matatizo ya utamkaji ambayo binadamu huweza kuzaliwa nayo

10

au kuyapata baada ya kuzaliwa. Ni tawi linalojaribu kutumia mbinu za kitabibu


kuchunguza matatizo na kutafuta namna ya kuyatatua.
FONOLOJIA NI NINI?
Fonolojia ni taaluma ya isimu inayochunguza mifumo ya sauti za kutamkwa
zinazotumika katika lugha asilia mahususi za binadamu. Inapolinganishwa na
fonetiki, inasisitizwa kuwa fonolojia ni tawi la isimu linalochunguza mifumo ya sauti
za lugha mahususi tu, kama vile sauti za Kiswahili, Kiingereza, Kigogo, n.k. Hata
hivyo, wapo wanaisimu wanaoelekea kukubaliana kuwa kuna fonetiki ya lugha
mahususi pia, na kuna fonolojia ya jumla, na fonetiki ya lugha mahususi. Mathalani,
Massamba (1996) licha ya kufasili fonolojia kuwa ni taaluma ya isimu
inayochunguza mfumo wa sauti za lugha mahususi, anaenda mbele zaidi na kudai
kuwa fonolojia inaweza kuchunguza sauti kwa ujumla wake bila kuzihusisha na
lugha mahususi. Akmajian na wenzake (2001), nao wanadokeza msimamo kama wa
Massamba wanapodai kwamba fonolojia inaweza kuchunguzwa kwa mitazamo
miwili tofauti. Kwanza, fonolojia kama tawi dogo la isimu linalochunguza mfumo na
ruwaza za sauti za lugha mahususi ya binadamu; na pili, fonolojia kama sehemu ya
nadharia ya jumla ya lugha ya binadamu inayohusika na tabia za jumla za mfumo wa
sauti za lugha asilia za binadamu. Katika mhadhara huu, hata hivyo, tutakuwa
wafuasi wa mtazamo unaoona kuwa fonolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia
mfumo wa sauti za lugha mahususi, hivyo tuna, kwa mfano, fonolojia ya Kiswahili,
fonolojia ya Kiingereza, fonolojia ya Kiha, fonolojia ya Kihehe, na fonolojia ya
Kibena. Kipashio cha msingi cha fonolojia ni fonimu.
FONIMU:
Ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachoweza kubadili maana ya neno.
Hivyo basi, fonimu ina maana, kwakuwa inaweza kubadili maana ya neno
inapobadilishwa nafasi katika neno husika. Foni chache zilizoteuliwa kutoka katika
bohari la sauti ili zitumike kwenye mfumo wa sauti za lugha mahususi ndiyo fonimu.

11

Hivyo, fonimu ni chache ikilinganishwa na foni. Idadi ya fonimu za lugha


hutofautiana kati ya lugha moja na nyingine. Mathalani, Kiarabu kina fonimu ishirini
na nane (28), Kiswahili kina fonimu thelathini (30), Kifaransa kina fonimu thelathini
na tatu (33), na Kiingereza kina fonimu arobaini na nne (44). Sauti ambayo huweza
kubadilishwa nafasi yake katika neno lakini maana ikabaki ileile huitwa alofoni.
Alofoni ni kipashio cha kifonolojia kinachotaja hali ambapo fonimu moja hutamkwa
na kuandikwa tofautitofauti bila kubadili maana ya neno. Mfano: Fedha na feza Sasa
na thatha Heri na kheri Kwa kifupi, alofoni ni matamshi tofautitofauti ya fonimu
(sauti) moja.
MITAZAMO YA DHANA YA FONIMU
Juhudi za kufasili dhana ya fonimu zilizofanywa na wanaisimu mbalimbali zimezua
mitazamo mbalimbali ya namna ya kuchambua dhana hii. Hadi sasa, mitazamo
mitatu ifuatayo ndiyo hujulikana zaidi. Fonimu ni Tukio la Kisaikolojia Huu ni
mtazamo uliokuzwa na kutetewa na wanasarufi geuzi-zalishi, mwanzilishi wake
akiwa ni Noam Chomksy. Kwa mujibu wa mtazamo huu, fonimu ni dhana iliyo
katika akili ya mzungumzaji wa lugha. Mtazamo huu unadai kuwa kila mzungumzaji
wa lugha ana maarifa bubu ya idadi na jinsi ya kutamka fonimu za lugha yake.
Chomsky anayaita maarifa haya kuwa ni umilisi (competence). Anadai kuwa maarifa
haya ya fonimu hufanana kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wazungumzaji wa lugha
moja husika. Kinachotofautiana ni jinsi ya kudhihirisha (kutamka) fonimu hizo, yaani
utendi (perfomance). Chomsky anabainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa
kuhitilafiana baina ya umilisi na utendi kutokana na matatizo mbalimbali ambayo
mzungumzaji hukabiliana nayo. Matatizo hayo ni kama vile uchovu, ulemavu wa
viungo vya matamshi (alasauti za lugha), athari za mazingira, ulevi, na maradhi.
Hivyo, kutokana na hali hii, fonimu hubaki kuwa tukio la kiakili, yaani kisaikolojia
tu. Fonimu ni Tukio la Kifonetiki Wafuasi wa mtazamo huu wanaongozwa na Daniel
Jones.

Daniel

Jones

..........................Inaendelea

anaiona

fonimu

kuwa

ni

[umbo]

halisi.

12

13

MOFOFONEMIKI YA KISWAHILI
Katika mada hii tumeangalia fasili ya mofofonemiki kwa mujibu wa wataalam
mbalimbali, kisha tukaangalia kwa ufupi historia ya nadharia ya mofofonemiki na
katika kiini cha mada tumejadili sababu zilizopelekea kuibuka kwa nadharia ya
mofofonemiki. Kwa kuanza na fasili ya mofofonemiki kwa mujibu wa mtandao wa
Wikipedia wanafafanua mofofonemiki kuwa ni tawi la isimu linalojishughulisha na
mwingiliano wa michakato ya kimofolojia na kifonolojia au kifonetiki. Pia
hujishughulisha na mabadiliko ya sauti yanayotokea katika mofimu wakati
zinapoungana kuunda maneno. (Tafsiri yetu). fasili hii ina mapungufu fulani kwani,
mofofonemiki haijishughulishi na michakato yote ya kifonolojia na kimofolojia bali
ni baadhi tu ya michakato hiyo ambayo ilishindwa kufafanuliwa kwa kutumia data za
kifonolojia au kifonetiki peke yake. The New Oxford American Dictionary
inafafanua kwamba, mofofonolojia/mofofonemiki ni tawi la isimu linalojishughulisha
na uwakilishi wa kifonolojia wa mofimu. Hivyo basi tunaweza kusema kuwa,
mofofonemiki ni tawi la isimu linaloshughulikia matumizi ya kimofolojia katika
kueleza baadhi ya tofauti za kifonolojia ambazo isingewezekana kuzielezea kwa
kutumia data za kifonetiki au kifonolojia peke yake. Baada ya kuangalia fasili ya
neno mofofonemiki ifuatayo ni historia fupi ya nadharia ya mofofonemiki. Kwa
mujibu wa Massamba (2010:82) akimrejelea Martnet (1965) anafafanua kwamba,
istilahi hii mofofonemiki/mofofonolojia ilipendekezwa kwa mara ya kwanza na N.S.
Trubetzkoy (1929). Trubetzkoy alitumia istilahi hii kwa maana ya tawi la isimu
ilinaloshughulikia matumizi ya mafolojia katika kuelezea baadhi ya tofauti za
kifonolojia ambazo isingewezekana kuzielezea kwa kutumia data za kifonolojia au
kifonetiki peke yake. Baada ya kuangalia historia fupi ya mofofonemiki yafuatayo ni
mambo yaliyosababisha kuibuka kwa nadharia ya mofofonemiki. Kuchunguza
ubadilikaji wa sauti ambao usingeweza kuelezwa kwa kutumia data za kifonolojia
peke yake. Baadhi yao wakapendekeza kuwapo kwa kiwango cha kimofofonemiki
pamoja na kipashio umbo kiini kama kiwakilishi cha mofimu, kwa hiyo

14

walipendekeza hivyo baada ya kushindwa kujua ipi ni alofoni ya fonimu ipi kwa
kutumia kigezo cha kifonetiki pekee Kwa mfano;
walishindwa kujua /k/ ni alofoni ya /c/ au /c/ ni alofoni ya /k/ Kwa mfano hata katika
lugha ya kurusi ruka = mkono runoj = a mkono Mzizi ni ruk na ru
Wanamofofonemiki walichunguza wakagundua kuwa katika mazingira fulani /k/
hubadilika kuwa // baada ya kufuatiwa na noj. Hivyo wakapendekeza umbo kiini
la maneno haya ni ruKa au runoj umbo kiini lake lilitambulika kama {K} au {}
Katika lugha ya Kiswahili kuna mabadiliko ya sauti yanayotokea katika baadhi ya
maneno baada ya sauti fulani kufuatiwa na kiambishi cha unominishaji (i) kwa mfano
katika maneno yafuatayo;
Fuata fuasi
Penda Penzi
Cheka Cheshi
Pika Pishi Pia
Wanamofofonemiki walichunguza ubadilishanaji huu wa sauti kwani walishindwa
kujua ipi ni alofoni ya fonimu ipi. Ndipo wakagundua kuwa katika mazingira fulani
/t/ hubadilika kuwa /s/ baada ya kufuatwa na mofimu ya unominishaji i pia sauti /d/
hubadilika na kuwa /z/ baada ya kufuatwa na mofimu ya unominishaji i Baada ya
kupendekeza umbo kiini maneno haya yakaandikwa kama ifuatavyo: kwa mfano
neno {fuaTa} umbo {T} likawa umbo kiini ambalo linawakilisha sauti zote mbili
yaani /t/ na /s/, pia neno {piKa} umbo kiini lake ni {K} ambalo linawakilisha sauti /k/
na // Kuchunguza mabadiliko ya sauti yanayotokea mofimu zinapoungana. Kwa
mfano;
katika lugha ya Kiswahili, U + ima wima I + etu yetu Mu + alimu Mwalimu U
+ imbo wimbo Vi + ake vyake Wanamofofonemiki wakagundua kuwa sauti fulani
huweza kuungana na kuunda sauti moja na kubadili umbo la neno. Chunguza
muundo wa kifonolojia wa mofimu katika lugha.

15

Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili; Mu + huni Mhuni Mu + gonjwa Mgonjwa


Mu + guu Mguu Mu + uguzi Muuguzi Mu + tu Mtu Wanamofofonemiki
wakagundua kwamba mofimu fulani huweza kuungana na mofimu nyingine na
kuunda umbo la neno. Kuchunguza ubadilishanaji wa sauti ambao una una uamilifu
wa kimofolojia lakini husababisha mabadiliko fulani ya kifonetiki.
Kwa mfano katika lugha ya kiingereza; Play + s [pleiz] Dog + s [dogz] Since
[sins]

Else

[els]

Place

[pleis]

Wanamofofonemiki

wakachunguza

kinachosababisha kuwepo na maumbo tofauti tofauti ya mofimu ya wingi. Kwa


mfano; /s/, /iz/, /z/ Wakagundua kuwa kuna mchakato zaidi ya ule wa kifonolojia
ambao ni wa kimofolojia unaosababisha umbo s kutamkwa /z/ au /iz/ au /s/
MAREJEO: The New Oxford American Dictionary. (2005), (2ndEdit), Oxford
University Press. New York.

16

KANUNI ZA UUNDAJI WA HOJAJI


Makala haya yanahusu kanuni za uandaaji wa hojaji. Katika kujadili mada hii
tumegawa kazi hii katika sehemu tatu muhimu, sehemu ya kwanza fasili ya hojaji
kulingana na wataalam mbalimbali, sehemu ya pili ni kiini cha swali ambapo
inaelezea kanuni muhimu za uundaji wa hojaji, hatimaye hitimisho. Kwa mujibu wa
Kothari C.R, (2004), uk 100, anafasili neno hojaji kuwa ni maswali yanayoandikwa
katika karatasi ili yaulizwe kwa mtafitiwa kwa lengo la kupata taarifa za tatizo la
utafiti. Nayo Kamusi ya Kiswahili sanifu (2004) TUKI uk 116, inasema kwamba
hojaji ni karatasi yenye maswali ya uchunguzi. Ni seti ya maswali mengi apewayo
mtu/watu kwa lengo la kupata taarifa juu ya jambo fulani (Macmillan Dictionary) [1]
Kutokana na fasili hizo hapo juu tunaweza kusema kuwa, hojaji ni maswali
yanayoandaliwa na mtafiti kwa lengo la kukusanya data kutoka kwa watafitiwa.
Hojaji hizo mtafiti anaweza kupeleka mwenyewe kwa mtafitiwa kwa njia ya mkono
au kwa njia ya posta ikiwa na kimbatanisho cha kumwomba mtafitiwa asome na
kuelewa maswali kisha ajibu maswali katika nafasi zilizoachwa wazi kwa matumizi
tu ya hojaji kisha kuyarudisha kwa mtafiti. Hojaji zinazopelekwa kwa njia ya mkono
husambazwa kwa haraka zaidi, na huwafikia watu wengi hususani wale
wanaomzunguka mtafiti. Faida yake ni rahisi kukusanya, pia zinachukua muda
mfupi, vilevile gharama zake ni ndogo, Faida ya kutumia njia ya posta ni pamoja na
kutumia gharama ndogo na husambazwa katika eneo kubwa kwa muda mfupi. Pia
mtafitiwa ana muda wa kutosha wa kuweza kutoa majibu kadri maswali
yalivyoulizwa. Pia mtafitiwa ambaye hawezi kuingiliwa kwa urahisi hii inaweza
kuwa njia nzuri ya kutumia. Licha ya njia hizo kuwa na faida pia zina hasara kama
zifuatazo; kwanza mara nyingi hojaji zinazorudi zikiwa zimejazwa ni chache. Hii ni
kutokana na mtafitiwa kutokuona umuhimu wa hojaji au kusongwa na majukumu au
maswali kutokueleweka. Pili inabagua maana inahitaji watu wanaojua kusoma na
kuandika, hojaji zinaweza kupotea zinapokuwa zinatumwa au kurudishwa. Ni
vigumu kuelewa kama majibu yatolewayo ni ya kwa kweli au ya uongo. Hata hivyo

17

njia hii ni ya taratibu mno kuliko njia zingine katika ukusanyaji wa data. Hojaji
zimegawanyika katika makundi makubwa mawili; kwanza hojaji funge na hojaji za
wazi (zisizo funge). Hojaji funge maswali yake yako wazi na yanaeleweka kwa
watafitiwa. Maswali yanayoulizwa yanakuwa sawa kwa watafitiwa wote, yanalenga
kutoa jibu moja tu. Mfano ndiyo au hapana, au ya kuchagua a,b,c,d. hayaruhusu
mtafitiwa kuweka hisia zake. Muundo wa maswali waweza kuwa funge.
Kwa mfano;
ANDIKA N KAMA JIBU NI NDIYO NA H KAMA JIBU NI HAPANA. AU
CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHII TU. Hojaji isiyo funge ni hojaji ambayo
inamruhusu mtafitiwa kutoa maelezo/kujieleza/au kutoa maoni ya ziada (kutoa
ufanuzi zaidi kadri ya uelewa wake kulingana na jinsi alivyoulizwa) Hojaji kama njia
ya ukusanyaji data ina kanuni muhimu za kuzingatiwa wakati wa kuiandaaa. Mtafiti
hana budi kuzingatia mambo yafuatayo;
kwanza; ajue TATIZO LA UTAFITI. Mtafiti akishajua tatizo la utafiti itamsaidia
kuandaa hojaji yake katika muundo unaotakiwa. Kwa mfano; atajua ni eneo gani
ataenda kufanyia utafiti wake, umri wa watafitiwa, jinsia na kiwango chao cha elimu.
Tatu izingatie usuli wa watafitiwa kama vile jina, umri jinsia, kabila na kiwango cha
elimu. Hii inasaidia mtatifi katika uchambuzi wa data kujua amehoji watu wa umri
gani na amehoji watu wa kiwango gani cha elimu. Pili ni mtiririko mzuri wa maswali;
ili kutengeneza/kuandaa hojaji nzuri na kupata majiu sahihi mtafiti lazima azingatie
mtiririko

mzuri

wa

uaandaaji

wa

maswali.

Mtiririko

mzuri

unaondoa

uvulivuli/ukakasi kwa mtafitiwa, hivyo basi maswali lazima yawe katika mtiririko
ufuatao; Kuanzia maswali mepesi kwenda maswali magumu, hii itampa moyo
mtafitiwa au kumvutia na kuonesha ushirikiano lakini pia yatamvutia na kumpa moyo
hivyo ataonesha ushirikiano au kupata hamasa ya kutaka kutoa majibu zaidi. Maswali
hayo yawe na uhusiano/ muwala. Maswali yafuatayo hayana budi kuekwa; maswali
yanayomtaka mtafitiwa kufikiri sana maswali yanayomhusu mtafitiwa, mfano una
watoto wangapi, mkewe yuko wapi, kwa nini huna mtoto? Maswali yanayohusiana

18

na mali za mtafitiwa, mfano je una magari mangapi? Au unalipwa kiasi gani kwa
siku? Maswali yanayofuata baada ya maswali ambayo hayana budi kuepukwa ni
maswali yanayohusiana na mada ya utafiti. Ambayo yanamtaka mtafitiwa kufikiri
kiundani ili kuweza kutoa majibu sahihi. Mfano, nafasi ya uchaguzi wa lugha ya
Kiswahili kama lugha ya kufundishia elimu ya juu. Maswali yalenge nini kinapelekea
Kiswahili kuteuliwa kuwa lugha ya kufundishia elimu ya juu. Au tatizo la utafiti ni
watoto wa mtaani. Kwa hiyo maswali yalenge sababu za kuwepo watoto wa mitaani.
Maswali magumu yaulizwe mwishoni. Hii ina faida kwa sababu, hata kama mtafitiwa
atashindwa kujibu kutokana na sababu mbalimbali maswali yale ya awali yatakuwa
yanatosha kutoa taarifa muhimu zinazohusu tatizo la utafiti. Pia mtiririko wa maswali
lazima uanze na maswali ya jumla kwenda maswali mahususi. Mtafitiwa hana budi
kuelewa kuwa majibu yaliyotolewa ni kwa ajili ya utafiti huo. jinsi/namna ya utungaji
wa maswali hayo; kutunga maswali katika mtiririko mzuri kwa kuanza na maswali
rahisi kwenda magumu lakini pia kwa kuzingatia maswali ya jumla kwenda maswali
mahususi. Maswali magumu yanaulizwa mwishoni. Maswali yanayotungwa yawe
wazi, yasiwe na upendeleo wa kijinsia au kisiasa au kidini. Maswali yazingatie
vigezo vifuatavyo; Maswali, yawe mafupi, yenye wazo moja, pia yawepo maswali ya
majibu mafupi ya ndiyo au hapana, ya kuchagua na yawepo maswali ya kutoa
maelezo. maswali yaeleweke/yawe sanifu maswali yaendane na uwezo wa kufikiri
wa mtafitiwa, mfano unasuka kwa mwaka mara ngapi? Swali hilo ni gumu kwa
maana hiyo lingeweza kuulizwa kuwa, kwa wiki unasuka mara ngapi? Hii itasaidia
kufikiria kwa haraka. Kanuni ya pili hojaji isiwe ndefu sana, na kila hojaji iwe na
lengo moja tu. Matokeo ya hojaji kuwa ndefu itamchosha mtafitiwa. Muhimu
maswali yasidokeze majiu. Kwa mfano Hivi wewe ndo Honest? Hapa hospitali
nasikia hakuna huduma nzuri ni kweli? Tatu izingatie usuli wa watafitiwa kama vile
jina, umri jinsia, kabila na kiwango cha elimu. Hii inasaidia mtatifi katika uchambuzi
wa data kujua amehoji watu wa umri gani na amehoji watu wa kiwango gani cha
elimu.

19

***namna/jinsi ya kutunga maswali, mtafiti lazima atambue kwamba kila swali


lazima liwe wazi vinginevyo mtafitiwa hataelewa swali linataka nini. Vilevile
maswali yasiwe na upendeleo wa kijinsia kwa mfano***
4. Maswali yazingatie vigezo vifuatavyo; yawe rahisi, na yenye wazo moja la msingi.
Maswali yaeleweke kirahisi. Maswali yaendane na uwezo wa kufikiri wa mtafitiwa
mfano unasuka kwa mwaka mara ngapi? Swali hilo ni gumu kwa maana hiyo
lingeweza kuulizwa kuwa kwa wiki unasuka mara ngapi? Hii itasaidia kufikiria kwa
haraka. Pamoja na hayo kuna miundo ya aina mbili ya utungaji wa maswali; maswali
yenye majibu ya kuchagua (funge) maswali yanayomruhusu mtafitiwa kujieleza (si
funge)
FAIDA YA MASWALI FUNGE
Kwanza ni rahisi kujibu, yanaeleweka kwa urahisi, mtafitiwa ana uwezo wa
kutofautisha swali moja na jingine.
HASARA:
Kwanza maswali hayo yanatoa majibu kwa mtafitiwa. Mfano Wahehe wanakula
mbwa? Andika ndiyo au hapana, pia huzuia nafasi ya mtafitiwa kujieleza zaidi kwa
jambo analolijua, pia hayako sahihi hasa pale ambapo yanakuwa magumu na hasa
mtafiti anahitaji majibu sahihi. Kutokana na udhaifu wa maswali funde, ndipo
maswali ya wazi yanapohitajika. Maswali ya wazi yanatungwa kwatika mazingira
ambayo yanatoa nafasi kwa mtafitiwa kutoa maelezo zaidi kwa kutumia
maneno/maelezo yake binafsi.
FAIDA YA MASWALI HURU
Huruhusu mtafitiwa kutoa maelezo mengi tena kwa maneno yake binafsi, mtafitiwa
huwa huru katika kujieleza,.

20

HASARA
Ni vigumu kukabiliana nayo, kwa maana kwamba inaibua ugumu wa kubaini majibu
sahihi ya swali lililoulizwa hii ni kwa sababu maelezo yanakuwa mengi. Pia
mtafitiwa anaweza akawa na mtizamo hasi kwa hiyo akajibu ndivyo sivyo. Kwa
hakika hojaji nzuri haina budi kutumia njia zote mbili yaani njia ya maswali funge na
njia ya maswali ya wazi. Kwani kwa kufanya hivyo unaweza kupata majibu ya ndiyo
au hapana kadri ya maswali yaliyoulizwa, lakini pia utapata maoni mbalimbali na
picha halisi kulingana na mtizamo wa mtafitiwa. Mtafiti lazima awe makini katika
maneno anayotumia katika kuaandaa maswali, maneno yawe na maana. Pia mtafiti
lazima atumie sentensi rahisi. Maneno ambayo ni magumu ambayo hayaeleweke,
istilahi za kitaalumaau na yenye maana zaidi ya moja lazima yaepukwe. Pia maneno
ambayo hayaendani na utamaduni wa jamii husika lazima yaepukwe Kimsingi utunzi
wa maswali na utumiaji wa maneno ni sanaa ambayo inahitaji mtu kujifunza.
MJENGO WA FASIHI SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI MJENGO WA
FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI. MJENGO WA FASIHI ANDISHI YA
KISWAHILI

21

22

SINTAKSIA HAIWEZI KUTENGANISHWA NA VITENGO VINGINE VYA


LUGHA.
Katika kujadili mada hii, kwanza tutatoa fasili ya sintaksia kwa mujibu wa wataalam
mbalimbali, fasili ya lugha, tutafafanua uhusiano uliopo kati ya sintaksia na vitengo
vingine vya lugha na mwisho tutatoa hitimisho juu ya mjadala wetu. Kwa mujibu wa
Massamba na wenzake (1999) Sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojihusishana
uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake.
Wanaendelea kusema, utanzu huu huchunguza sheria au kanuni zinazofuatwa katika
kuyapanga maneno ili yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika.
Pia Habwe na Karanja (2004) wanasema Sintaksia ni utanzu wa isimu
unaoshughulikia muundo wa sentensi na elementi nyingine zinazounda sentensi kama
vile kategoria za maneno, vikundi na vishazi. Kutokana na fasili hizi inaonekana
kuwa Massamaba na wenzake wamefafanua zaidi kwa kuonesha kuwa licha ya
kuzingatia kanuni na sheria za kupanga maneno lakini pia ni lazima maneno hayo
yawe na uhusiano. Kwa upande mwingine Habwe na Karanja wameshindwa kuelezea
suala hili, wao wanaona sintaksia inashughulika na muundo wa sentensi na vipashio
vyake. Kwa mantiki hii tunakubaliana na fasili ilyotolewa na Massamaba na wenzake
kuwa Sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa
maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake, kwa kuzingatia sheria na
kanuni za lugha husika ili kuleta mawasiliano. Katika fasili ya lugha, wataalam wengi
wanakubaliana kuwa lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii
kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao. Baadhi ya wataalam wanao kubaliana na
fasili hii ni Massamba na wenzake (Wameshatajwa). Kitengo kwa mujibu wa TUKI
(2004) ni mahali pateule palipotengwa kwa shughuli maalum. Tunaporejea katika
muktadha wa lugha tunaweza kusema kuwa vitengo vya lugha ni vipengele muhimu
vinavyounda maarifa ya lugha kwa ujumla. Kwa fasili hii, vipengele vinavyounda
maarifa ya lugha ni fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki. Kwa hiyo kutokana
na kwamba sintaksi pia ni kitengo mojawapo kinachounda maarifa ya lugha,

23

tunakubali kwamba, sintaksia haiwezi kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha


kutokana na uhusiano mkubwa uliopo baina ya vitengo hivi. Vitengo hivi hutegemena
na kuathiriana. Hivyo basi tunaweza kuonesha jinsi sintaksia isivyoweza
kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha yaani fonolojia, mofolojia na semantiki
kama ifuatavyo: Uhusiano baina ya fonolojia na sintaksia. Massamba na wenzake
(Wameshatajwa) wanafasili fonolojia kuwa ni uchambuzi wa mfumo wa sauti katika
lugha mahususi. Wanaendelea kusema ni jinsi ambavyo vitamkwa au sauti za lugha
zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha. Kwa hiyo tunaweza
kusema kuwa kuungana kwa vitamkwa ili kujenga maneno yanayokubalika katika
lugha fulani hutegemea mpangilio sahihi wa vitamkwa. Na kwa kuwa neno ni
kiwango cha msingi cha uchambuzi katika sintaksia basi fonolojia ina uhusiano wa
moja kwa moja na sintaksia. Mifano ifuatayo huthibitisha hoja hii:
Mfano 1.
Anapika. Hili ni neno lakini pia ni sentensi, hivyo huweza kuchanganuliwa
kifonolojia kama ifuatavyo: a|n|a|p|i|k|a|, mpangilio wa sauti umeunda neno
anapika.
Mfano 2.
a. baba. Limeundwa na (KIKI).
b. abab. Limeundwa na (IKIK).
Katika mfano 2a tunaona neno baba lina maana na limefuata kanuni na mpangilio
unaokubalika wakati mfano 2b neno abab halina maana katika lugha ya Kiswahili
kwa sababu halina mpangilio mzuri wa fonimu. Kwa mifano hii tunaona kwamba
hatuwezi kuwa na miundo mikubwa katika sentensi bila kuwa na mpangilio sahihi wa
sauti katika lugha. Kwa hiyo sintaksia haiwezi kukamilika bila fonolojia. Uhusiano
baina ya mofolojia na sintaksia. Mofolojia ni kitengo kingine cha lugha ambacho kwa
mujibu wa Rubanza (1996) ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha katika

24

kuunda maneno. Kutokana na fasili hii, kipashio cha msingi katika uchambuzi wa
kimofolojia ni neno ambalo ndilo hutumika kuunda darajia ya sintaksia. Vilevile
maumbo ya kimofolojia huathiri vipengele vingine vya kisintaksia, kwa mfano,
sentensi zifuatazo hufafanua zaidi:
1. Mtoto anacheza.
2. Watoto wanacheza. Katika mifano hii tunaona kwamba mofimu m- na wa- katika
upande wa kiima zimeathiri utokeaji wa mofimu a- na wa- katika upande wa kiarifu.
Pia kanuni za mfuatano na mpangilio wa mofimu au viambishi zikifuatwa huunda
maneno katika miundoya kisintaksia.
Mifano:
1. Alicheza = a-li-chez-a
2. Anaimba = a-na-imb-a
Kwa ujumla kipengele cha umoja na wingi katika maumbo ya kimofolojia ndicho
kinachoathiri umbo linalofuata jina na kuathiri muundo wa sentensi nzima.
Mifano:
1. Mwalimu alikuwa anafundisha.
2. Walimu walikuwa wanafundisha.
Tunaona katika mifano hii maumbo ya umoja na wingi ya maneno Mwalimu na
Walimu yameathiri mpangilio mzima wa sentensi. Uhusiano baina ya semantiki na
sintaksia. Habwe na Karanja wakimnukuu Richard na Wenzake (1985) wanasema
Semantiki ni stadi ya maana. Semantiki ni utanzu unaochunguza maana katika lugha
ya mwandamu. Wanaendelea kusema semantiki hutafiti maana za fonimu, mofimu,
maneno na tungo. Kwa hiyo kutokana na fasili hii maana hushughulikiwa katika
vitengo au viwango vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia, mofolojia na sintaksia.

25

Mifano:
a) Paka mweusi amepotea.
b) Mweusi paka amepotea.
c)Amepotea mweusi paka.
Katika mifano hii tunaona kwamba sentensi a) ina maana kutokana na kwamba
imefuata mpangilio sahihi wa maneno katika tungo na sentesi zilizobaki hazina
maana kutokana na sababu kwamba hazijafuata mpangilio ulio sahihi. Kwa mantiki
hii, kwa kuwa semantiki hushughulikia viwango vyote vya lugha, basi hushughulikia
pia kiwango cha sintaksia ambapo huangalia maana za tungo. Tungo yoyote ni lazima
ilete maana inayokubalika na wazungumzaji au watumiaji wa lugha husika, kama
itakuwa kinyume basi haitakuwa tungo bali ni orodha ya maneno tu. Mfano: Mtoto
anacheza mpira uwanjani. Mtoto uwanjani mpira anacheza. Tukiangalia mifano hii
tutagundua kwamba katika sentensi ya kwanza mpangilio wake wa vipashio unaleta
maana lakini sentensi ya pili haina maana kutokana na kuwa na mpangilio mbaya wa
maneno. Kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa sintaksia haiwezi
kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha kwa kuwa kuna uhusiano wa moja kwa
moja baina ya vipengele hivi vya lugha na kwa hiyo hutegemeana kati ya kipengele
kimoja na kingine. Kwa mfano, huwezi kupata mofolojia (neno) bila kupitia ngazi ya
fonolojia na pia huwezi kuwa na ngazi ya sintaksia (sentensi/tungo) bila kupitia ngazi
ya fonolojia na mofolojia lakini vitengo vyote hivi hutawaliwa na kitengo cha
semantika ili kuleta mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji.
MAREJEO Habwe, J na P. Karanja (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi:
Phoenix Publishers Ltd. Massamba, D.P.B na wenzake (1999). Sarufi Miundo ya
Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo. Dar essalaam: TUKI. Rubanza, Y.I (1996).
Mofolojia ya Kiswahili. Dar es salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. TUKI

26

(2004).Kamusi

ya

Kiswahili

Sanifu.

Dar

es

salaam:

TUKI.

27

KIAMBISHI TAMATI NI
Makala haya yatashughulikia ufupisho wa makala ya Swahili forum iliyohaririwa na
rose marie beck, Thomas gelder na wemer graefner katika uchambuzi wa kiambishi
tamati cha mahali ni, tathmini na mwisho hitimisho. Makala haya yanahusu asili na
usambaaji wa kiambishi tamati cha mahali ni. Karibu lugha zote za kibantu kuna
ngeli tatu za mahali zenye viambishi pa, ku, mu, kwa mfano katika lugha ya kisangu
viambishi hivi vya mahali hujitokeza pia katika maneno ya mu-khati, pa-khati, na kukhati. Kwa upande wa lugha ya kiswahili mofimu hizi yaani pa, ku, mu hutumika
kama viwakilishi vionyeshi kwa mfano hapa, huku na humu na vilevile hufanya kazi
kama viwakilishi vimilikishi. Kwa mfano kwetu, kwao na mwao. Dai hili limetolewa
na Beck na wenzake (1994). Swali la msingi, kama viambishi vya mahali
vinavyojitokeza katika ngeli hizo, kiambishi ni- hakipo, kiambishi hiki kimetoka
wapi?

NADHARIA YA UDENGUZI

NADHARIA YA UDENGUZI

KATIKA

UJITOKEZAJI WA WAHUSIKA WA TAMTHILIYA ZA KISWAHILI.


Wahusika ni kitu muhimu katika kazi yoyote ya kifasihi, kwani ndio wanaosukuma
mbele kazi ya kifasihi. Wataalamu mbalimbali wamezungumzia kwa namna tofauti
maana na ujitokezaji wa wahusika wa kazi ya fasihi. Hii ni taka enzi za Ugiriki ya
kale hadi katika fasihi ya kiswahili. Mulokozi (1996) anasema hadithi ya tamthilia
husonga mbele kwa njia ya vitendo na mazungumzo ya wahusika. Hivyo anaonesha
bila wahusika hata mazungumzo hayatakuwepo. Brecht (1898-1956) aliibua kanuni
ya ukengeushi ambayo aliitumia kukengeuka kanuni za Kiaristotle. Moja kati ya
ukengeushi wake ulikuwa ni katika kipengele cha wahusika. Ambapo kwa Aristotle
mhusika mkuu katika Tanzia alikuwa ni lazima atoke tabaka la juu, lakini kwa Brecht
haikuwa lazima kwa mhusika kutoka tabaka la juu. Lengo la Brecht lilikuwa
kuonesha kuwa hata tabaka la chini linaweza kuleta mabadiliko katika jamii.
Kanuni/dhana hii ya Brecht inalandana na nadharia ya udenguzi/ujenguzi. Udenguzi

28

ni nadharia ya kihakiki iliyoanzishwa na mwanafalsafa wa Kifaransa Jacques Darrida


(1973), ambapo anasema ujuzi na maarifa si vitu vinavyoweza kueleweka moja kwa
moja, katika matini yoyote ile ujuzi hutumika katika kuunda matini hiyo, kwa kuwa
ujuzi si kitu kinachoweza kueleweka moja kwa moja hupelekea kuonekana kwamba
ujuzi na maarifa kuwa ni kitu kisichoshikika yaani chenye utelezi. Hivyo hata tafsiri
ya matini kwa wahakiki haiwezi kuelezwa kwa namna moja, kila mtu ataieleza kwa
namna yake hii ina maana kwamba, maana zinaweza zikaendana au zikapingana.
Miller (1976) anasema udenguzi ni juhudi ya kufikia nguvu na uwezo wa matini
kama chombo kinachoweza kujifafanua. Rorty (1995) anasema udenguzi ni ukiushi
wa kaida wa matini, ukiushi huu utokeapo kwa amara ya kwanza huonekana kama ni
usaliti, lakini utokeaji wa ukiushi si ajali bali hukusudia kufikisha ujumbe
uliokusudiwa. Maelezo hayo ya Rorty yanatupa picha halisi ya mabadiliko
yanayoweza kutokea katika uundaji wa matini. Mfano uundaji wa mashairi ya
Kiswahili hapo mwanzo ulikuwa ukifuata urari wa vina na mizani lakini baadaye
yakaibuka mashairi ya kisasa ambapo wanajadi waliona kuwa ni usaliti wa ushairi wa
Kiswahili. Vilevile maelezo hayo yanatupa mwanga wa kuelewa kuwa katika matini
udenguzi utokeapo unakuwa na lengo la kujifafanua zaidi. Kutokana na maelezo
hayo ndipo Wafula na Njogu (2007) waliposema kwamba kutokana na udenguzi
hakuna toleo la mwisho la kazi ya fasihi. Hii ndio inayofanya wahakiki kutoa fasili
tofauti tofauti za jambo moja fasili hizo zaweza kufanana au kutofautiana. Kwa hiyo
udenguzi unaweza kuboresha matini au kuumba upya kwa lengo la kukidhi upya
mahitaji ya jamii kama ilivyokuwa kwa nadharia ya ukengeushi ya Brecht. Nadharia
hii tutaitumia kuhakiki ujiotokezaji wa wahusika katika tamthiliya za Kiswahili.
Semzaba (1997) anasema Wahusika ni tabia zinazopambanua mhusika mmoja na
mwingine. Wahusika ndio nyenzo muhimu inayosababisha mtiririko wa matukio.
Mhusika huonyeshwa na mwandishi kwa maneno pamoja na matendo. Kwa kuwa
tamthilia ni utungo ulioandikwa wahusika hutofautiana kwa mambo manne; kwa
mujibu wa Semzaba.

29

(i) Maumbile kama vile jinsia, umri, tambo, rangi nk. Pia hutofautiana dini, kiuchumi
nk.
(ii) Wahusika wasiobadilika (bapa) wanaobadilika (duara)
(iii) Wahusika ishara
(iv) Wahusika wafaili: Hujenga wahusika wakuu. Mulokozi (1996) Ametaja aina za
wahusika wa tamthilia; kuna wahusika wakuu:
(i) Mbabe /nguli
(ii) Mkinzani
(iii) Muwi (muovi)
Wahusika wadogo:
(i) Mfoili
(ii) Msimamizi
(iii) Chizi Wahusika hawa walioorodheshwa ni kutokana na uanishaji wa tamthilia za
kimagharibi. Tamthilia kwa upande wa fasihi ya Kiswahili zilifuata baadae, hivyo
ujitokezaji wa wahusika ukawa tofauti hasa baada ya kuingiza Uafrika (upya) katika
sanaa hizi. Hata kama aina ya mhusika ni ile ya Kimagharibi (Mfano msimulizi wa
chizi) lakini ujitokezaji wake ukaanza kuwa wa Kiafrika zaidi hapa ndipo tukaona
udenguzi unatokea, udenguzi huu hautokei kama ajali bali umelenga kuboresha na
kuhifanya tamthilia iendane na mazingira halisi ya fasihi ya Kiswahili, Katika
tamthilia ya Mkutano wa Pili wa Ndege ujitokezaji wa wahusika kiudenguzi ni katika
matumizi ya wahusika wa kifasihi simulizi. Mwandishi ametumia wahusika wa
kifasihi simulizi ambao ni ndege na wanyama, katika tamthilia. Mfano katika (uk.14
15) mwandishi anasema: Tausi: enyi wa mashariki Poleeni Ogeleeni Chiriku: ko ko
likoo! ooooh! Magharibi sisahau Wahusika hawa (ndege na wanyama) hutumiwa
sana katika fasihi simulizi, hivyo mwandishi amedengua ujitokezaji wa wahusika si
binadamu pekee katika tamthilia za Kiswahili kuna wahusika wasio binadamu. Pia
katika tamthilia ya Jogoo Kijijini na Ngano ya Jadi ujitokezaji wa wahusika
kiudenguzi ni katika matumizi ya wahusika wa kifasihi simulizi. Mwandishi
amemtumia mhusika Joka akaliita sesota, kiishara kuwakilisha ukoloni na jinsi

30

ukoloni huu ulivyokomaa, akalipa joka hilo vichwa sabini, kuonyesha kiasi gani
unavyoziathiri nchi za Kiafrika. Mfano: Katika (uk.21) mwandishi anasema Kwani
Likuwa tabia makini Killa mwaka ukibaini Joka hushuka kijijini Kuchukua mali na
binti mwema mmoja. Matumizi ya joka ni udenguzi. Pia katika tamthilia ya Nguzo
Mama, ujitokezaji wa wahusika kiudenguzi ni kupitia mhusika Chizi. Chizi kama
inavyoaminika katika jamii ni mtu asiyeweza kuongea neno la maana, lakini katika
tamthilia hii mwandishi amemtumia mhusika huyu na kumwonyesha akieleza kitu
cha msingi na muhimu. Mwandishi anasema: Chizi: Nani anapendeza? Waoneni watu
hawa Hawapendi demokrasia Nikisema yote mie Wananiita mie chizi Chizi mie au
nyie (uk. 29 31) Pia katika tamthilia hiyo hiyo ya Nguzo Mama ujitokezaji wa
wahusika kiudenguzi ni katika majina ya wahusika. Mwandishi amewapa wahusika
wake majina kwa kuanzia na Bi Moja Bi Nane. nk. Majina hayo yote huashiria
uhusika na kifasihi simulizi, kwa kuwa katika hadithi nyingi za Kifasihi simulizi,
huanza hivi. Hapa zamani za kale, palikuwa na baba mmoja na mama mmoja.
Hivyo mwandishi huyu ametumia majina ya kiidadi au kinamba ambayo ni majina
pia ya wahusika wa kifasihi simulizi katika tamthiliya ya Heshima Yangu ujitokezaji
wa wahusika kiudenguzi umejitokeza kupitia mhusika Mzee Issa. Mhusika huyo
anadai heshima ambayo yeye mwenyewe hajailinda heshima hiyo kwa kuzaa nje ya
ndoa na kuificha siri hiyo ya kuwa na mtoto nje ya ndoa yake. Mzee Issa alimkataa
Salum toka akiwa tumboni mwa mama yake, na kisa kutomjua baba yake hadi
ukubwani alipotaka kumuoa Rukia, ndipo anapoambiwa kuwa ni dada yake.
Mwandishi anaonyesha kuwa kuheshimiwa si kwa vile una umri mkubwa tu bali pia
matendo yako yanaweza kukuvunjia heshima hata kama una umri mkubwa.
Mwandishi anasema: Rukia (anasogea mbali na nyumba, anawaza kwa huzuni).
Heshima yangu, heshima yangu (Kimya kwa muda) Ni heshima gani ipatikanayo
katika kumkatalia Salum kijana mzuri, mwenye tabia nzuri na moyo wa imani, eti
kwa sababu ni mwana haramu? Ni kosa.....(uk. 10) Pia katika tamthiliya ya
Mashetani ujitokezaji wa wahusika kiudenguzi unajitokeza kupitia wahusika wake
Juma na Kitaru. Mwandishi katika tamthilia hii amedengua ujitokezaji wao kutoka

31

kufikia hali ya kuwa na majina yao ya Juma na Kitaru hadi kwenye uhusika wa
kishetani na kibinadamu. Mwandishi ameonesha udenguzi wa wahusika kwani si hali
ya kawaida kwa wahusika kuchorwa hivyo, Mfano:- Muhusika katika tamthilia
akichorwa kama baba, basi atakuwa baba hadi mwisho wa tamthilia hiyo. Pia katika
tamthiliya ya Kivuli Kinaishi ujitokezaji wa uhusika kiudenguzi unajitokeza kupitia
mhusika Bi Kirembwe, ambaye ni mhusika mwanamke lakini amechorwa kitofauti na
wahusika wengine wanawake wanavyochorwa katika baadhi ya kazi za Fasihi.
Mhusika huyu amechorwa kama mtawala na mwenye amri na sauti yakuwatisha hadi
wanaume. Hii ni tofauti kwa uchoraji wa wahusika wa kike katika tamthilia nyingi,
ambazo huwachora katika daraja la chini, duni na kukandamizwa. Mfano Martha
katika tamthiliya ya Kwenye Ukingo wa Thim, amechorwa ni mwanamke
anayekwenda na wakati lakini anakandamizwa na mfumo mzima wa jamii yake kwa
kuonyeshwa akipokonywa mali zote baada ya mume wake kufariki. Pia katika
tamthiliya ya Aliyeonja Pepo ujitokezaji wa uhusika kiudenguzi ni katika matumizi
ya wahusika wakifikirika au wa kiimani, ijapokuwa suala hili limejitokeza pia katika
riwaya za Kusadikika na Kufikirika lakini katika tamthilia hizi mwandishi
amekwenda mbali zaidi kwa kutumia usawiri wa pepo na uhusika wa kiimani zaidi
kuwakilisha mambo yaliyopo au yanayotendeka duniani na si nchi ya kidhahania
kama alivyofanya Shaaban Robert katika riwaya zake za Kufikirika na Kusadikika.
Mwandishi wa aliyeonja pepo ametumia wahusika kama malaika Ziraili, Sirafili,
Jaburili na wengine ambao huamini ni malaika au pepo kuwakilisha mambo
mbalimbali yanayotendeka duniani. Mfano: Mwandishi anasema: Ziraili: Wapi?
Jiburili: Huko ambako wewe bado hajajishughulisha nako Huko...........(uk.3). Katika
tamthiliya ya Lina Ubani ujitokezaji wa wahusika kiudenguzi ni kupitia mhusika Bibi
ambaye anajitokeza mwanzo kabisa mwa tamthilia kwa kuimba. Jambo ambalo ni
udenguzi wa kimuundo wa ujenzi wa tamthilia kwa kufuata misingi ya Kiaristotle,
ambao kimuundo anasisitiza wimbo katika tamthilia uwe mwishoni na si mwanzoni
mwa tamthilia kama alivyofanya mwandishi Penina Mhando katika tamthilia hii
katika ukurasa wa kwanza, mwandishi anatuonesha mhusika Bibi amekaa analia kwa

32

kuimba na kuombeleza. Bibi: Ingoma ili sikuidaha doo ae Woidoo ae ya Nime


mwitunda dya mele do Pia katika tamthiliya hiyo hiyo ya Lina Ubani ujitokezaji wa
uhusika

kiudenguzi

unajitokeza

kupitia

mhusika

Mwanahego.

Mwandishi

amemchora mhusika huyo kama mlevi lakini anaongea na kubishana na sauti mambo
yenye maana, tofauti na walevi walivyozoeleka katika jamii, kwamba ni watu
wasioweza kuchangia au kuongea mambo ya msingi katika jamii. Mwandishi
anasema; Mwanahego: Umoja na mke wamo mnajifunika wote shuka moja
Mwanahego na wewe tutakutana wapi ndipo tuwe na umoja....... wewe juu ya kilima,
mimi bondeni.....(Uk.46). Pia katika tamthiliya ya Morani ujitokezaji wa wahusika
kiudenguzi umejitokeza kupitia mhusika Jalia ambao ni mhusika wa kike ambaye
mwandishi amedengua kwa kuonyesha asishiriki bega kwa bega na katika kampeni
za kuwakamata wahujumu uchumi Jalia anashirikiana na mwenzake katika kampeni
hiyo na kuonyesha msimamo wa hali ya juu, na ushupavu wa wanawake katika
ukurasa wa 17 mwandishi anasema: Jalia: Na njia ya kuuzima moto ni kuwasha
moto; moto mkali zaidi. Hivyo ndiyo hatua kamili. Kwa kuhitimisha nadharia ya
Udenguzi na mawazo ya Brecht katika kuwachora wahusika yanalenga katika kuleta
upya

wa

fikra

kwa

watazamaji

na

wasomaji

wa

tamthilia.

You might also like