Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 17

HABARI

HabariZA
za
NISHATI
nishati&MADINI
&madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Toleo
No.145
51
Toleo No.

Limesambazwa
kwa Taasisi
naTaasisi
Idarana
zote
MEM
, 2015 11 - 17, 2016
Limesambazwa
kwa
Idara
zote MEM Tarehe - 23-29 JanuariNovemba

Wabunge

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

MRAMBA ARIDHISHWA NA KASI


UJENZI MRADI WA UMEME KINYEREZI II

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

Somahabari Uk.2

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania


(TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia), akiongozana na
Meneja Mradi wa ujenzi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen Manda
kufanya ziara katika eneo litakapojengwa mitambo ya umeme.

Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli,


Mafanikio Sekta za Nishati, Madini

Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini, anayeshughulikia
Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini anayeshughulikia
Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,


Mhandisi Felchesmi
Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa
REA, Dk. Lutengano
Mwakahesya

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

>>>
UK. 10

Ofisi ya M awasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali


kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na Madini
Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
kwa
ajili ya News Bullettin
Jarida laGhorofa
Wizarya
a Tano
ya Nishati
au Fika hii
Ofisina
ya Mawasiliano
(MEM) na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Novemba 11 - 17, 2016

MHANDISI MRAMBA

ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI


MRADI WA UMEME KINYEREZI II

kwenye mazungumzo na watu


wa TANROADS na mamlaka
nyingine kuhusu utaratibu wa
kusafirisha mitambo hiyo kutoka
bandarini kuileta hapa, alifafanua
Mhandisi Manda.
Akielezea zaidi kuhusu
manufaa ya mradi huo pindi
utakapokamilika, Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO,
Mhandisi Felchesmi Mramba
alisema, TANESCO iliwaahidi
watanzania kuwa kwa kushirikiana
na Serikali itaendelea kuboresha
miundombinu ya umeme ikiwa
ni pamoja na kuzalisha umeme
mwingi zaidi ili hatimaye uende
sambamba na malengo ya serikali
ya Awamu ya Tano ambayo
imedhamiria kujenga nchi ya
viwanda.
Nia ya Mheshimiwa Rais
ya kujenga nchi ya viwanda
itafanikiwa kwa vile sasa umeme
mwingi na wa uhakika utapatikana
ili kuhudumia viwanda vilivyopo
na vipya vinavyoendelea
kujengwa.Alihitimisha Mhandisi
Mramba.
Ujenzi wa msingi wa
Tenki la kuhifadhia maji
(raw water tank) katika
eneo la Kinyerezi jijini
Dar es Salaam.

Na Grace Kisyombe,
TANESCO

kurugenzi
Mtendaji wa
Shirika la Umeme
Tanzania
(TANESCO),
Mhandisi Felchesmi Mramba
ameeleza kuridhishwa na kasi ya
ujenzi wa mradi wa umeme wa
gesi wa Kinyerezi II utakaozalisha
umeme wa Megawati 240
unaotekelezwa na Shirika hilo jijini
Dares Salaam.
Mradi huo ulizinduliwa Machi
2016 na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt.
John Pombe Magufuli, kwa kuweka
jiwe la msingi ambapo eneo hilo
lilikuwa pori na kazi ya kusafisha
eneo ili kuanza ujenzi ilianza miezi
minane iliyopita.
Kwa wale waliokuwepo siku
Mheshimiwa Rais anaweka jiwe
la msingi la ujenzi wa mradi huu,
mtakumbuka kuwa eneo lote hili
lilikuwa pori, napenda niwapongeze
wahandisi na mafundi wote
mnaotekeleza ujenzi huu kwa
kazi nzuri na kasi ya kuridhisha.
Alipongeza Mhandisi Mramba,
ambaye alitembelea eneo hilo
mwishoni mwa wiki kukagua
maendeleo ya ujenzi wake.
Wahandisi wa TANESCO
wakishirikiana na wenzao kutoka

kampuni ya SUMITOMO
CORPORATION NA TOSHIBA
za Japan na washauri wa mradi
Lahmeyer International ya
Humburg nchini Ujerumani, ndio
wanaojenga mitambo hiyo ambapo
mradi unatekelezwa kwa fedha za
walipa kodi wa Tanzania na Japan.
Akitoa taarifa ya maendeleo
ya ujenzi huo, Meneja Mradi,
Mhandisi Stephen Manda alisema

kuwa mradi huo unahusisha ujenzi


wa msingi wa kitalu namba moja
(Foundation Works Block I) na ujenzi
wa msingi wa tenki la kuhifadhia maji
(raw water tank).
Kazi inaendelea vizuri napenda
kukujulisha kuwa baadhi ya vifaa
muhimu vimekwishawasili na
tunachosubiri pengine kufikia mwezi
Januari 2017 ni kuwasili kwa mashine
zenyewe (Turbines), hivi sasa tuko

Kazi ya kuhamisha kifusi


ikiendelea katika eneo
la Kinyerezi jijini Dar es
Salaam.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Novemba 11 - 17, 2016

PETROLEUM EXPLORATION IN
OFFSHORE TANZANIA

TAHARIRI

On 2nd November 2016, TPDC, BG/Shell and the Consortium spudded


Kitatange-1 well in Block-1, offshore Tanzania. The well is located in water
depths of 2318m at the Indian Ocean about 60km from the shore. The well
will be drilled to a total depth (TD) of 4186m subsurface, targeting Basal
Tertiary (Paleocene_ turbidities).

Tumetekeleza!
Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Nishati
na Madini imeweka Mikakati yenye kuendana na Dira ya
Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 inayoelekeza nchi kuingia
katika uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025. Ili kufikia malengo
hayo, Serikali imeweka kipaumbele katika uchumi wa viwanda.
Katika uchumi wa viwanda, Nishati ya uhakika inahitajika
ili kuwezesha Wawekezaji zaidi kutoka ndani na nje ya nchi
kuwekeza nchini . Mara baada ya kugundulika kiasi kikubwa
cha gesi nchini kinachofikia futi za ujazo takribani trilioni 57.2,
ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu Serikali ya Awamu
ya Tano iingie madarakani kampuni kubwa kutoka ndani na nje
ya nchi zimeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa Viwanda
vya Gesi Kimiminika na mbolea katika mikoa ya Lindi na
Mtwara.
Miongoni mwa uwekezaji huo ni mradi wa ujenzi wa
kiwanda cha kusindika gesi kimiminika (Liquefied Natural Gas;
LNG), unaotarajiwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 30
sawa na zaidi ya shilingi trilioni 65 za kitanzania unatarajiwa
kuanza mara moja baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria.
Kampuni zitakazohusika na ujenzi wa kiwanda hicho ni
pamoja na Statoil ya Norway, Exxonmobil ya Marekani, Shell
ya Uholanzi, BG na Ophir za Uingereza na Pavillion ya
Singapore.
Manufaa yatakayopatikana kutokana na mradi wa ujenzi wa
kiwanda hicho ni pamoja na ajira zaidi ya 10,000 zitakazotolewa
wakati wa ujenzi wa mradi na ajira nyingine zaidi ya 8,000
zitatolewa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda
hicho. Pia mradi huo utachochea ujenzi wa viwanda vingine
vidogo vidogo kwa ajili ya bidhaa zitakazouzwa katika kiwanda
cha LNG, ujenzi wa vituo vya biashara, ununuzi wa bidhaa
kutoka kwa wananchi waishio karibu na kiwanda hicho na hivyo
kuchangia ukuaji wa uchumi
Pia uwekezaji mwingine ni ujenzi wa kiwanda kikubwa
cha mbolea katika eneo la Msanga Mkuu mkoani Mtwara,
ambapo Serikali itashirikiana na kampuni ya Helm kutoka nchini
Ujerumani.
Kiwanda cha mbolea kinachotarajiwa kujengwa, kitahitaji
gesi kiasi cha futi za ujazo trilioni 0.8 kwa kipindi cha miaka 20
ambapo Serikali imejipanga katika kuhakikisha kuwa gesi ya
kutosha inazalishwa ili kuendana na mahitaji ya kiwanda hicho
pamoja na matumizi mengine ya majumbani.
Katika maandalizi ya ujenzi wa kiwanda hicho, Serikali
imetenga eneo la Msanga Mkuu lililopo Mtwara lenye ukubwa
wa hekta 400 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho ambapo
eneo hili limeshalipiwa fidia pamoja na Halmashauri ya Mtwara
kuboresha miundombinu ya barabara kwa kuweka lami kutoka
Mtwara Mjini hadi eneo la kiwanda tayari kwa kukabidhiwa kwa
mwekezaji kwa ajili ya ujenzi.
Aidha, Serikali inatarajia kujenga kiwanda kingine cha
mbolea katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi ambapo kitatumia
gesi asilia. Kiwanda hicho kitakachojengwa kwa ubia kati ya
Tanzania na nchi za Denmark, Ujerumani na Pakistani kitakuwa
na uwezo wa kuzalisha tani 3,800 za mbolea kwa siku.
Tunapongeza juhudi zinazofanywa na Serikali na tunawaasa
wananchi hususan waliopo katika mikoa ya Lindi na Mtwara
kujiandaa na fursa za uwekezaji zitakazojitokeza ili kuwa sehemu
ya uchumi wa gesi nchini.

KITATANGE: All wells in Block 1 are


named after fishes, other wells in the Block
include Mkizi, Jodari, Chaza andMzia.

NOBLE GLOBE TROTTER II DRILLING SHIP


KWA HABARI PIGA SIMU
kitengo cha mawasiliano

TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Bodi ya uhariri
Msanifu: Lucas Gordon
Waandishi: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson
Mwase, Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,
Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

Five
Pillars of
Reforms
increase efficiency
Quality delivery
of goods/service
satisfAction of
the client
satisfaction of
business partners
satisfAction of
shareholders

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Novemba 11 - 17, 2016

Dkt. Pallangyo aeleza mikakati


ya Serikali kuzalisha Umeme
Teresia Mhagama na
Mohamed Saif

li kukidhi mahitaji ya umeme


na nchi kuwa ya viwanda kama
ilivyoainishwa katika Dira ya
Maendeleo ya mwaka 2025,
Serikali imeamua kutekeleza
miradi mbalimbali ya umeme.
Hayo yamesemwa na Naibu
Katibu Mkuu anayeshughulikia
Nishati, Wizara ya Nishati na Madini
Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo
wakati akifungua Kongamano
lililofanyika jijini Dar es Salaam
likihusu Ufunguaji wa Milango ya
Uwekezaji katika Sekta ya Nishati ili

kuongeza upatikanaji wa nishati hiyo


nchini.
Alitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa
ni ya kufua umeme ikiwemo upanuzi
wa mradi wa Kinyerezi I (MW
185) na Mradi wa kufua umeme wa
Kinyerezi II (MW 240).
Miradi mingine tunayotekeleza
ni ya usambazaji umeme ikiwemo
njia ya Iringa Shinyanga yenye
msongo wa kV 400, Arusha Singida
yenye msongo wa kV400, na Dar es
Salaam- Chalinze Tanga Arusha
wa msongo wa kV 400, aliongeza
Mhandisi Pallangyo.
Alisema kuwa kwa sasa kiasi cha
umeme kilichopo kwenye gridi ya

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati,Wizara ya Nishati na Madini


Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akifungua rasmi Kongamano la Ufunguaji
wa Milango ya Uwekezaji katika Sekta ya Nishati Tanzania.

Washiriki wa Kongamano kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia


majadiliano. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia
Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, katikati ni Mhandisi Neema Rushema
akifuatiwa na Mhandisi Ahmed Chinemba.

Taifa ni megawati 1,357.69 ambapo


umeme unaotokana na chanzo cha
maji unachangia asilimia 41.7%, gesi
asilia 44.7%, mafuta mazito 12.8% na
tungamotaka 0.8%.
Aliongeza kuwa umeme
unaopatikana nje ya gridi ni megawati
82.28 na kwamba mpaka sasa
asilimia 40 ya wananchi nchini ndiyo
wanaopata huduma ya umeme.
Alisema kuwa miradi ya umeme
vijijini inayotekelezwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) imechangia
kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya
wananchi wanaotumia umeme na
kuongeza kuwa mahitaji ya umeme
nchini yanakadiriwa kukua kwa

asilimia 10 hadi 15 kwa mwaka.


Aidha, alisema kuwa ili kutimiza
lengo la kuwa nchi ya viwanda ifikapo
mwaka 2025, Serikali imelenga
kuongeza uzalishaji wa umeme hadi
kufikia megawati 5000 ifikapo 2020 na
megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.
Sasa ili kutimiza lengo hilo la
kuwa na megawati 10,000 ifikapo
2025 inahitajika kuwa na mtaji
mkubwa ili kuweza kutekeleza miradi
mbalimbali kama ya usambazaji na
usafirishaji umeme hivyo ni muhimu
kwa Serikali kushirikiana na Sekta
binafsi katika kutekeleza hayo,
alisema Mhandisi Pallangyo.
Kongamano hilo liliandaliwa na
Wakala wa Bima ya Biashara Barani
Afrika (ATI) na kuhudhuriwa na
wawekezaji mbalimbali kutoka ndani
na nje ya nchi, Taasisi za Kimataifa,
Wizara na Taasisi mbalimbali za
Serikali ambapo masuala mbalimbali
kuhusu Nishati yalijadiliwa.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano wakifuatilia Majadiliano.

Washiriki wa Kongamano wakiendelea na majadiliano. Wa kwanza


kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), Mhandisi Decklan Mhaiki akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima NyamoHanga akifuatiwa na Mwakilishi kutoka Nedbank Afrika Kusini, Michael
Creighton.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati,
Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi
Juliana Pallangyo (wa tatu kutoka kulia) katika
picha ya pamoja na waandaaji wa Kongamano.
Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
ATI na Kamishna wa Bima Tanzania, Israel
Kamuzora akifuatiwa na Mwenyekiti wa
Bodi ya Nishati Vijijini, Dkt. Gideon Kaunda,
Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Bima ya
Biashara Barani Afrika (ATI), George Otieno
na wa kwanza kutoka kushoto ni Kamishna
Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme,
Mhandisi Innocent Luoga.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Novemba 11 - 17, 2016

PROF. MUHONGO, afanya kikao na Bodi


TPDC, Balozi wa Uingereza na Marekani

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika picha


ya pamoja na Naibu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser mara
baada ya kumaliza mazungumzo yao wakati Naibu Balozi huyo
alipomtembelea ofisini kwake jijini
Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

aziri wa Nishati na
Madini, Profesa
Sospeter Muhongo
hivi karibuni
alikutana na Bodi na
Menejimenti ya Shirika la Maendeleo
ya Petroli Tanzania (TPDC), katika
kikao kilichochadili maendeleo ya
utekelezaji wa miradi inayosimamiwa
na shirika hilo ikiwemo Mradi wa
Kusindika Gesi Asilia, (LNG) na
Mradi wa Bomba la Kusafirisha
Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki
(EACOP) kutoka Hoima nchini
Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Katika kikao hicho Prof. Muhongo
aliitaka Bodi na Menejimenti hiyo
kuongeza kasi katika utekelezaji wa
miradi husika kutokana na manufaa ya
miradi hiyo kwa Maendeleo ya Taifa.
Mbali na Bodi na Menejimenti ya
TPDC, kikao hicho pia kilihudhuriwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Prof. Justin Ntalikwa,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, anayeshughulikia
Madini, Prof. James Mdoe na baadhi
ya Watendaji kutoka Wizara ya Nishati
na Madini.
Aidha, wakati huo huo, Waziri
Muhongo pia alikutana na Balozi wa
Uingereza nchini Sarah Cooke ambapo
walijadili masuala kadhaa kuhusu sekta
ya nishati ikiwemo chanzo cha Nishati
Jadidifu.
Pia, Waziri Muhongo alikutana
na Naibu Balozi wa Marekani nchini
Virginia Blaser ambapo walijadili
masuala kadhaa kuhusu Sekta ya
Nishati.

Sehemu ya Wajumbe wa Bodi ya TPDC, Menejimenti na baadhi ya


Watendaji wa Wizara wakifuatilia kikao baina yao na Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Sehemu ya Menejimenti ya
TPDC wakifuatilia kikao baina
yao na Waziri wa Nishati
na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo (hayupo pichani).

Waziri wa Nishati na Madini,


Prof. Sospeter Muhongo akiwa
katika picha ya pamoja na
Balozi wa Uingereza nchini
Sarah Cooke (wa pili kushoto)
na ujumbe uliofuatana na
Balozi huo.

Waziri wa Nishati na Madini,


Prof. Sospeter Muhongo (wa
pili kulia) akizungumza na
Balozi wa Uingereza nchini
Sarah Cooken (wa tatu
kushoto) na ujumbe wake
walipomtembelea leo ofisini
kwake Jijijini Dar es Salaam.
Kulia ni Kamishna Msaidizi
wa Nishati anayeshughulikia
umeme, Mhandisi Innocent
Luoga.

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Novemba 11 - 17, 2016

Watalaam Tanzania wajifunza


Uendelezaji Jotoardhi, JAPAN
Na mwandishi wetu,
JAPAN

hiyo ni kwamba katika uzalishaji


umeme utokanao na Jotoardhi
tunatakiwa kuanza na uzalishaji
wa megawati chache na kuendelea
ataalam kutoka
kuongeza kiwango kadri uzalishaji
Wizara ya Nishati
unavyoendelea, ilisema taarifa ya
na Madini,
Wataalam.
Kampuni ya
Mbali na mafunzo hayo, ujumbe
Uendelezaji
huo pia ulikutana na viongozi wa
Jotoardhi Tanzania (TGDC), na
juu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST),
Japan (MOFA); Wizara ya Uchumi,
wakiongozwa na Naibu Katibu
Viwanda na Biashara (METI)
Mkuu wa Wizara ya Nishati na
pamoja na Shirika la Ushirikiano wa
Madini, Profesa James Mdoe tarehe
Kimataifa la Japan (JICA).
16-26 Oktoba, 2016, walishiriki
Ziara hiyo iliyoratibiwa na
katika ziara ya mafunzo nchini Japan kampuni ya Japan External Trade
kuhusu Nishati ya Jotoardhi.
(JETRO) kwa kushirikiana na
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni
Kampuni ya TOSHIBA za nchini
kujifunza masuala ya uendelezaji
Japan ilihusisha pia kutembelea
wa Jotoardhi, kutafuta msaada
Makao Makuu ya TOSHIBA
wa kifedha na kiufundi kwa ajili ya
yaliyoko Kawasaki, Japan External
kuendeleza mradi wa Nishati ya
Trade (JETRO), Earthquake
Jotoardhi katika eneo la Ziwa Ngozi
Laboratory Japan University, West
pamoja na kujifunza teknolojia ya
Japan Engineering Company (West
uendelezeji wa nishati ya Jotoardhi
JEC).
ikiwemo matumizi ya moja kwa
Maeneo mengine
moja.
yaliyotembelewa ni pamoja na
Ziara hiyo imekuwa na mafanikio Kiwanda cha TOSHIBA, mtambo
makubwa kwa kuwa Serikali ya Japan wa Geo-portable Geothermal
kupitia Taasisi zake zimeonesha
Power Plant wa megawati 2 ulioko
nia na utayari wa kutoa msaada
Waita Japan, mtambo wa kuzalisha
wa kiufundi na kifedha kwa ajili ya
umeme wa Jotoardhi wa megawati
kuendeleza Mradi wa Ziwa Ngozi.
25 ulioko Hokaido na makumbusho
ya kampuni ya Sayansi ya Toshiba
Somo ambalo wajumbe
yaliyoko Kawasaki.
wameweza kujifunza katika ziara

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini,


Profesa James Mdoe (kulia) akiwa na Mwakilishi wa Kampuni ya JETRO nchini
Japan

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia


Madini, Prof. James Mdoe (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na Balozi
wa Tanzania nchini Japani, Mathias Chikawe (wa pili kushoto) wakifuatilia
jambo katika Ubalozi wa Tanzania nchini Japan wakati ujumbe wa Tanzania
ulipotembelea nchini humo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia


Madini Prof. James Mdoe (wa kwanza kushoto waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania katika ziara hiyo. Balozi wa
Tanzania nchini humo, Mathias Chikawe (katikati) na Wawakilishi wa
kampuni za JETRO na TOSHIBA.
Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi
Innocent Luoga (wa pili kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao baina ya
Ujumbe wa Tanzania na mwakilishi wa kampuni ya JETRO.
Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya
Nishati na Madini
anayeshughulikia
Madini, Prof. James
Mdoe (wa tatu kulia)
akipata maelezo
kutoka kwa wasimamizi
wa Mtambo wa
kuzalisha umeme
utokanao na Nishati
ya Jotoardhi wakati wa
ziara yao nchini Japan.

Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi


Innocent Luoga, (wa pili kushoto) akimweleza jambo Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe (kushoto kwake)
walipotemebelea Mtambo wa kuzalisha umeme wa megawati 2 Waita,
nchini Japan.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Novemba 11 - 17, 2016

KAMPUNI YA CHINA
GEZHOUBA GROUP
Kaimu Kamishna Msaidizi
wa Nishati anayeshughulikia
Maendeleo ya Nishati, Juma
Mkobya ( wa kwanza kushoto)
akizungumza wakati wa
kikao chake na Wawakilishi
wa Kampuni ya China
Gezhouba Group Company
Ltd (CGGC). Kampuni
hiyo inayojishughulisha na
uendelezaji wa Nishati ya
umeme ikiwemo uzalishaji
wa umeme kwa kutumia
teknolojia mbalimbali, illikutana
na Wizara ili kubaini fursa
za uwekezaji zilizopo katika
sekta hiyo.Wengine katika
picha ni wataalam kutoka
Wizara ya Nishati na Madini.

Naibu Meneja wa kampuni ya China Gezhouba Group Company Ltd


(CGGC) Feng Jun (wa tatu kulia), akizungumza jambo wakati wa kikao
hicho.
Wawakilishi wa
Kampuni ya
China Gezhouba
Group Company
Ltd (CGGC)
wakifuatilia
majadiliano
na Wataalam
wa Wizara
ya Nishati na
Madini.

Wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kikao baina


yao na Kampuni ya China Gezhouba Group Company Ltd (CGGC).

Habari za nishati/madini

Novemba 11 - 17, 2016

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

PBPA yatakiwa kuhamasisha


Wazawa kwenye Zabuni za Mafuta
Katibu Mkuu
wa Wizara
ya Nishati na
Madini, Profesa
Justin Ntalikwa
(mbele)
akiongoza
kikao
kilichoshirikisha
Bodi na
watendaji
kutoka Wakala
wa Uagizaji
Mafuta kwa
Pamoja (PBPA)
hivi karibuni
jijini Dar es
Salaam.

Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam

wa shughuli zake, kuzifanyia kazi


pamoja na kuwahamasisha katika
ushiriki wa zabuni ya uagizaji wa
bidhaa ya mafuta kwa pamoja.
atibu Mkuu wa Wizara
Awali akielezea kuhusu shughuli
ya Nishati na Madini, za Wakala huo, Kaimu Mkurugenzi
Profesa Justin Ntalikwa wa PBPA, Kedron Mbwilo
ameutaka Wakala
alisema kabla ya kuanzishwa
wa Uagizaji Mafuta
Wakala huo, majukumu ya
kwa Pamoja (PBPA) kuhamasisha
usimamizi wa uagizaji wa mafuta
kampuni za ndani katika ushiriki
kwa pamoja yalikuwa chini ya
wa zabuni ya uagizaji wa bidhaa ya kampuni binafsi ya Petroleum
mafuta kwa pamoja.
Importation Coordinator Limited
Profesa Ntalikwa aliyasema hayo PICL iliyokuwa imeanzishwa
alipofanya ziara katika Wakala
na kampuni za mafuta na
huo hivi karibuni lengo likiwa ni
kuandikishwa BRELA
kufahamu maendeleo ya shughuli
Alisema majukumu makuu ya
za Wakala pamoja na changamoto Wakala ni pamoja na kusimamia
zake.
mahitaji ya mafuta kwa nchi na
Aliielekeza PBPA kukaa kikao
kuhakikisha kuwa mafuta yanaletwa
cha pamoja na kampuni za ndani
ili kukidhi mahitaji hayo. Majukumu
zinazojihusisha na usambazaji wa
mengine ni pamoja na kuhakikisha
mafuta ili kubaini changamoto
kuwa mafuta yananunuliwa kwa
njia yenye ufanisi.
zinazowakabili katika uendeshaji

Sehemu ya Wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa


Pamoja (PBPA) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (hayupo
pichani).

Sehemu ya watendaji kutoka Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja


(PBPA) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani).

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta


kwa Pamoja (PBPA), Kedron Mbwilo (kushoto) akielezea
majukumu ya Wakala huo kwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (hayupo
pichani). Kulia ni Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na
Madini Mhandisi Yahya Samamba.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Novemba 11 - 17, 2016

JIFUNZE KUHUSU TETEMEKO LA ARDHI (2)


Na Samwel Mtuwa-GST

ya majanga kama hayo, watu


huchelewa kuchukua uamuzi wa
haraka kujinusuru kwani huwa
etemeko la ardhi au kwa
bado wanajiuliza kwamba wafanye
jina lingine linafahamika
nini. Hivyo mazoezi ya mara kwa
kwa jina la zilizala ni
mara ya jinsi ya kuchukua tahadhari
mishtuko ya ghafla ya
ardhi. Inatokea mara kwa humfanya mtu kufanya uamuzi wa
haraka pindi tukio linapotokea.
mara, lakini mara nyingi ni hafifu
Pili; wananchi pia wanashauriwa
mno, na inapimwa na mitambo ya
kujenga nyumba bora na imara kwa
wataalamu.
kuzingatia viwango halisi vya ujenzi,
Tetemeko kubwa laweza
kuweka misingi imara wakati wa
kusababisha uharibifu mkubwa na
ujenzi, kupata ushauri wa kitaalamu
vifo, hasa kutokana na majengo
wa aina ya majengo yanayofaa
yanayoanguka.
Katika makala iliyopita tulijifunza kujengwa katika eneo husika
kulingana na ardhi ya mahali hapo,
juu ya maana , sababu, pamoja na
kuepuka ujenzi wa nyumba katika
athari au madhara yake kwa jamii ,
miinuko mikali yenye kuambatana
makala hii tunajifunza zaidi juu ya
na mawe/ miamba na kuepuka
mambo muhimu ya kuzingatia ili
kuepukana na madhara ya tetemeko ujenzi wa makazi katika maeneo tete
yenye mipasuko ya miamba (faults)
la ardhi.
na uwezekano mkubwa wa kutokea
Kabla ya tukio, elimu ya
matetemeko.
tahadhari inapaswa itolewe ili kila
Tatu ,wakati wa tukio la tetemeko
mmoja aelewe nini cha kufanya,
la ardhi, unashauriwa kukaa mahali
linapotokea tetemeko la ardhi ikiwa
ni pamoja na kupata mafunzo kutoka salama kama vile sehemu ya wazi
isiyo na majengo marefu, miti mirefu
kwa watu wa msalaba mwekundu
na miinuko mikali ya ardhi. Watu
kuhusu namna ya kuhudumia
majeruhi ama waathirika; na pia jeshi wanashauriwa kukaa nje ya nyumba
la zimamoto ili kupata elimu kuhusu katika sehemu za uwazi.
Nne ,endapo tetemeko
namna ya kutumia kizimamoto.
litakukuta ukiwa ndani ya nyumba,
Elimu na mafunzo hayo,
unashauriwa ukae chini ya uvungu
yatasaidia kuwaweka watu katika
wa meza imara, ama kusimama
hali ya tahadhari; na hii itasaidia
kupunguza taharuki wakati wa tukio, kwenye makutano ya kuta na pia
ukae mbali na madirisha na makabati
kwa vile watakuwa sasa wanajua
ya vitabu, vyombo au fenicha ili
namna ya kuchukua tahadhari kwa
kuepuka kuangukiwa na vitu hivyo.
namna mbalimbali.
Tano, unashauriwa usitembee
Mosi, kufanya mazoezi ya
umbali mrefu kwa lengo la kutafuta
kuchukua tahadhari hizo mara
mahali salama kwa sababu tetemeko
kwa mara ili kujizoesha, kwani
la ardhi, hutokea ghafla na huchukua
mara nyingi wakati wa matukio
muda mfupi. Takwimu zinaonesha

kwamba watu wanaotaharuki na


kukimbia ovyo wakati wa tukio la
tetemeko ndio hupata madhara ama
kuumia.
Sita; salimisha macho yako kwa
kuinamisha kichwa chini chako
wakati wa tukio.
Saba, baki mahali salama hadi
hapo mitetemo itakapomalizika na
kisha ujikague kuona kama hujaumia
na ndipo utoe msaada kwa wengine
ambao watakuwa wameumia. Sita;
ondoka mahali ulipo kwa uangalifu,
kuepuka vitu ambavyo vitakuwa
vimedondoka na kuvunjika kwani
vinaweza kukudhuru.
Nane; jiandae kisaikolojia kwa
mitetemo itakayofuata baada ya
mtetemo mkuu.
Tetemeko kuu huwa mara nyingi
linafuatiwa na mitetemo mingi
midogo midogo. Nane; kumbuka
kuwa matukio ya matetemeko
ya ardhi, huweza kuambatana na
moto hivyo jihadhari na matukio
ya moto, kwa vile tetemeko la ardhi
linaweza kusababisha kupasuka kwa
mabomba ya gesi au kukatika kwa
nyaya za umeme ama kuharibika
kwa vifaa vinavyotumia umeme na
kusababisha hitilafu ya umeme.
Tisa; kama uko nje ya jengo
wakati tetemeko linatokea,
unashauriwa kubaki nje, simama
mahali pa wazi na uwe mbali na
majengo, miti mikubwa, nguzo
na nyaya za umeme na ujikinge
kichwani kadri inavyowezekana
kwani paa za nyumba, miti, nguzo
na nyaya za umeme vinaweza
kudondoka na kuleta madhara.
Kumi; endapo utakuwa
unaendesha chombo cha moto

wakati wa tukio la tetemeko la ardhi,


unashauriwa usimame kwa uangalifu
sehemu salama na usubiri hadi
mitetemo imalizike, ndipo uendelee
na safari yako kwani tetemeko
linaweza kusababisha barabara au
madaraja kukatika.
Kumi na moja; endapo utakuwa
kwenye maeneo ya miinuko au
milima, uwe mwangalifu ili kuepuka
kuporomokewa na mawe au
kuangukiwa na miti.
Kumi na mbili; baada ya
mitetemo kumalizika, endapo
itakulazimu kuondoka mahali ulipo
ukiwa katika jengo refu, unashauriwa
kutumia ngazi badala ya lifti au
kipandishi.
Baada ya tukio: Mosi,wananchi
wanashauriwa baada ya tukio,
kuzima umeme katika majengo ili
kuepuka kutokea kwa hitilafu ya
umeme, kwani mitetemo huenda
ikaendelea tena.
Pili; kukagua majengo kwa
uangalifu ili kuhakikisha kama
hayakupata madhara kama vile
nyufa n.k, na kwamba yanaweza
kuendelea kutumika na kama ikibidi,
basi unashauriwa kuwaita wataalamu
wa majengo ili wayafanyie ukaguzi.
Tatu; endapo utaangukiwa na
vitu vizito, usijaribu kutumia nguvu
nyingi ili kujinasua kwani hujui
vitu hivyo vina uzito kiasi gani,
omba msaada kwa kuita kwa sauti,
lakini usifanye hivyo mara nyingi
ili usipoteze nguvu nyingi mwilini
maana hujui ni lini utaokolewa.
Nne; toa msaada unaowezekana
kwa watu walioathirika na tetemeko
na utoe taarifa kwa vyombo
vinavyohusika na uokoaji.

10

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Novemba 11 - 17, 2016

Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli,


Mafanikio Sekta za Nishati, Madini

ovemba 5, 2016, Serikali


ya Awamu ya Tano chini
ya uongozi wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli ilifikisha kipindi cha
mwaka mmoja wa Utawala wake
tangu ilipoingia madarakani, mnamo
tarehe 5 Novemba, 2015.
Yapo mambo mengi yamefanyika
ndani ya kipindi cha mwaka mmoja
kupitia sekta mbalimbali nchini. Kwa
upande wa Wizara ya Nishati na
Madini, Serikali imeendelea kutekeleza
shughuli mbalimbali za sekta kama
ilivyopangwa katika Bajeti ya Wizara
kwa mwaka wa Fedha 2016/17.
Ndani ya kipindi cha mwaka
mmoja tumeshuhudia mafanikio
kadhaa kupitia sekta za Nishati na
Madini, mafanikio ambayo yanalenga
katika kuchangia maendeleo na ukuaji
uchumi wa taifa letu kwa kuzingatia
mchango wa sekta husika.
Miongoni mwa mafanikio
katika Sekta ya Nishati ni pamoja
na; Kuongezeka kwa uzalishaji
wa umeme nchini katika vyanzo
vilivyounganishwa kwenye Gridi ya
Taifa kufikia GWh 5,006.50 katika
kipindi cha mwezi Januari hadi
Septemba, 2016, ikilinganishwa na
GWh 4,560.61 kwa kipindi kama
hicho mwaka 2015. Pia, uzalishaji
umeme kwa kutumia gesi asilia
umeongezeka kutoka wastani wa

Megawati 328 hadi kufikia Megawati


593 kutokana na kukamilika kwa
bomba la gesi asilia kutoka Mtwara
hadi Dar es Salaam.
Aidha, kumekuwa na ongezeko
la Watanzania wanaopata Huduma
ya umeme nchini kutoka asilimia 36
mwezi Oktoba, 2015 hadi asilimia
51 mwezi Oktoba, 2016. Ongezeko
hilo limetokana na juhudi za Serikali
za kusambaza umeme nchini kupitia
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
na Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO). Ukiacha ongezeko
la wanaopata huduma hiyo, wateja
wapya 234,383 waliunganishiwa
umeme kwa kipindi cha kuanzia
Oktoba, 2015 hadi Septemba, 2016
sawa na ongezeko la asilimia 14.68.
Pia, ipo miradi kadhaa ya
kusafirisha umeme inayoendelea
kutekelezwa na Serikali katika maeneo
mbalimbali nchini, miongoni mwake ni
Mradi wa Kusafirisha Umeme kutoka
Iringa hadi Shinyanga wenye Msongo
wa kilovoti (400) ambao umekamilika
kwa asilimia 97, katika sehemu Tatu
(lots) za: Iringa-Dodoma asilimia
100; Singida-Shinyanga asilimia 100;;
Dodoma-Singida asilimia 89; na vituo
vya kupozea umeme katika maeneo
ya Iringa na Shinyanga asilimia 100.
Mradi unatarajiwa kuzinduliwa na
Rais Magufuli mwezi Novemba, 2016.
Vilevile, tayari Serikali imeanza
utekelezaji wa Mradi wa Kinyerezi - II

MW 240 baada ya Jiwe la msingi


la mradi huu kuwekwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli tarehe 16 Machi, 2016.
Mitambo hiyo itatumia teknolojia ya
Combined Cycle na itatumia gesi asilia
kuzalisha umeme.
Ukiachana na mengi
yaliyotekelezwa katika Sekta ya Nishati,
Yapo pia mafanikio yaliyotekelezwa
katika Sekta ya Madini yakiwemo;
Uanzishwaji wa Migodi ya Uchimbaji
wa Kati, ambapo katika kipindi
cha Oktoba, 2015 na Oktoba, 2016
Mgodi wa CATA Mining ambao ni
wa uchimbaji wa kati wa madini ya
dhahabu ulianzishwa mkoani Mara
katika Wilaya ya Musoma Vijijini.
Mgodi huo unamilikiwa na Mwekezaji
Mtanzania kwa ubia na Mwekezaji wa
kigeni.
Mnada wa madini ya vito, hususan
Tanzanite ulifanyika kuanzia tarehe
09 hadi 12 Agosti, 2016 Jijini Arusha,
ambapo madini yenye thamani ya
Dola za Marekani 3,448,050, sawa
na Shilingi bilioni 7.56 yaliuzwa na
kuwezesha Serikali kukusanya Dola za
Marekani 150,491.06, sawa na Shilingi
milioni 331 ikiwa ni mrabaha na vibali
mbalimbali.
Halikadhalika, Wizara imeendelea
kuboresha huduma za utoaji leseni za
madini kupitia mfumo wa huduma
za leseni kwa njia ya mtandao (Online

Mining Cadastre Transactional Portal


(OMCTP)). Katika kipindi cha mwezi
Oktoba, 2015 mpaka Oktoba, 2016
jumla ya leseni 6,015 zimetolewa kwa
kutumia mfumo wa OMCTP. Mfumo
huo wa OMCTP unawasaidia wateja
kupata taarifa za leseni zao kila wakati
kupitia njia ya ujumbe mfupi wa simu
(SMS) na njia ya barua pepe.
Aidha, kupitia Mradi wa Ubia wa
TanzaniteOne, uzalishaji wa Tanzanite
umeongezeka, ambapo kwa kipindi
cha kuanzia mwezi Februari hadi
Septemba, 2016, jumla ya kilogramu
1,348.48 za tanzanite zilizalishwa.
Aidha, mauzo ya tanzanite pia
yameendelea kuongezeka, ambapo
kati ya Januari hadi Agosti, 2016
jumla ya kilo 2,406.98 za Tanzanite
zimeuzwa kupitia minada ya wazi na
kuingiza jumla ya Dola za Marekani
milioni 7.35. Yapo mafanikio mengi
yaliyopatikana kwa kipindi cha mwaka
mmoja wa Rais Magufuli madarakani,
yaliyoainishwa ni baadhi tu.
Kutokana na mafanikio hayo
yaliyotajwa na mengine mengi
yaliyopatikana ambayo yana mchango
wa moja kwa moja na ukuaji uchumi
wa nchi yetu, Watanzania hatuna budi
kuendelea kushirikiana na Serikali
katika utekelezaji wa mipango na
programu mbalimbali zilizopangwa
ili hatimaye kuweza kufika katika
Tanzania Tunayoitaka kupitia Sekta za
Nishati na Madini.

u
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati)
akikata utepe wakati wa kuweka jiwe la msingi
la mradi wa Kinyerezi II MW 240 jijini Dar es
Salaam tarehe 16 Machi, 2016

Baadhi ya mitambo ya umeme katika


kituo cha kupoza na kusambaza umeme
kilichopo mkoani Singida. Hiki ni moja ya kituo
kilichoboreshwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji
wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya
kusafirisha umeme ya msongo wa kV 400
kutoka Iringa hadi Shinyanga (Backbone).

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Novemba 11 - 17, 2016

11

MAONESHO YA KIMATAIFA YA
VITO KUFANYIKA MEI 2017

Mwenyekiti wa Kamati ya Chama cha Wafanyabiashara wa Madini


Tanzania (TAMIDA) Peter Pereira (wa kwanza kushoto - mbele),
akiongoza kikao cha Kamati ya Maonesho kilichojadili maboresho ya
Tovuti ya AGF hivi karibuni jijini Arusha.Wengine katika picho ni Kaimu
Kamishna Msaidizi wa Nishati na Madini Kanda ya Kaskazini, Adam
Juma (wa pili kushoto mbele) pamoja na wajumbe wa kamati ya
AGF kutoka kwenye Taasisi za Serikali na wajumbe wa TAMIDA

Na Rhoda James

aonesho ya Tano
ya Kimataifa
ya Vito ya
Arusha (AGF)
yanatarajiwa
kufanyika, kuanzia tarehe 3 hadi 5,
Mei 2017.
Maonesho hayo ambayo
hufanyika kila mwaka jijini Arusha
na kuwakutanisha Wafanyabiasha
wa Madini na Vito na Wadau
mbalimbali wa madini yatafanyika
katika Hoteli ya Mount Meru jijini
Arusha.
Hayo yameelezwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya Maonesho ya Vito
kutoka upande wa Chama cha
Wafanyabiashara wa Madini
Tanzania (TAMIDA) Peter Pereira
wakati wa kikao cha kamati ya
maandalizi kilichofanyika hivi
karibuni jijini Arusha.
Pereira alisema kuwa, lengo la
Maonesho hayo ya Kimataifa ni

kukutanisha wadau mbalimbali


ndani na nje ya nchi na kutoa fursa
ya kutanua masoko ya madini ya
vito inchini.
Aliongeza kuwa, Maonesho
hayo yameendelea kuboreshwa
na sasa yanajumuisha Masonara
na Wachimbaji wa Madini,
Wafanyabiashara wa Madini ya
Vito wa ndani na nje, Wanunuzi wa
Madini wa ndani na nje, pamoja
na Wataalam wenye uzoefu wa
shughuli za madini ya vito.
Aidha katika kikao hicho,
Kamati hiyo iliazimia kuwa
Makamishana Wasaidizi wa Madini
wa Kanda zote washiriki kwenye
vikao vya maandalizi ili kujadili
namna ya kufanya minada ya ndani
ili kukusanya madini ya kutosha
kwa ajili ya maonesho yajayo ya
AGF.
Maonesho hayo huratibiwa
na Wizara ya Nishati na Madini
kwa kushirikiana na Chama cha
Wafanyabiashara wa Madini
Tanzania (TAMIDA)

Wajumbe wa TAMIDA na Taasisi za Serikali wakisikiliza mada


iliyokuwa ikiwasilishwa na mjumbe (hayupo pichani) wakati wa kikao
hicho.

12

Habari za nishati/madini

Novemba 11 - 17, 2016

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Mwaka mmoja wa Dkt. Magufuli


Viwanda vikubwa kujengwa, Lindi, Mtwara
Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam

erikali ya Awamu ya
Tano kupitia Wizara ya
Nishati na Madini imeweka
mikakati yenye kuendana
na Dira ya Maendeleo ya
Taifa ya Mwaka 2025 inayoelekeza
nchi kuingia katika uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025. Ili kufikia
malengo hayo, Serikali imeweka
kipaumbele katika uchumi wa
viwanda.
Katika uchumi wa viwanda,
nishati ya uhakika inahitajika ili
kukaribisha Wawekezaji zaidi kutoka
ndani na nje ya nchi. Mara baada
ya kugundulika kiasi kikubwa cha
gesi nchini kinachokadiriwa futi za
ujazo takribani trilioni 57.2, ndani
ya mwaka mmoja tangu Serikali ya
Awamu ya tano kuingia madarakani
makampuni makubwa kutoka ndani
na nje ya nchi wameanza kuonesha
nia ya kuwekeza katika ujenzi wa
viwanda vya gesi kimiminika na
mbolea katika mikoa ya Lindi na
Mtwara.
Akielezea ujenzi wa kiwanda
cha kusindika gesi kimiminika
(Liquefied Natural Gas; LNG),
unaotarajiwa kugharimu Dola za
Marekani Bilioni 30 sawa na zaidi
ya shilingi trilioni 65 za kitanzania,
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo anasema
kuwa ujenzi unatarajiwa kuanza
mara moja baada ya kukamilika
kwa taratibu za kisheria.
Anataja kampuni zitakazohusika

na ujenzi wa kiwanda hicho kuwa


ni pamoja na Statoil ya Norway,
Exxonmobil ya Marekani, Shell
ya Uholanzi, BG na Ophir
za Uingereza na Pavillion ya
Singapore.
Akielezea manufaa ya mradi
wa ujenzi wa kiwanda hicho, Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dk.
Medard Kalemani anaeleza kuwa
ajira 10,000 zitatolewa wakati wa
ujenzi wa mradi na ajira nyingine
8,000 zitatolewa mara baada ya
kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda
hicho.
Manufaa mengine ya mradi huo
ni pamoja na ujenzi wa viwanda
vingine vidogo vidogo kwa ajili ya
bidhaa zitakazouzwa katika kiwanda
cha LNG, ujenzi wa vituo vya
biashara, ununuzi wa bidhaa kutoka
kwa wananchi waishio karibu na
kiwanda hicho na hivyo kuchangia
ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia
kodi.
Pia, huduma za jamii
zitaboreshwa katika mkoa wa
Lindi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
miundombinu kama vile barabara,
umeme, hospitali za kisasa anasema
Dk. Kalemani.
Akielezea hatua iliyofikiwa
ya maandalizi ya mradi huo, Dk.
Kalemani anasema, katika hatua
ya awali itaundwa timu ya kufanya
majadiliano ya namna nchi ya
Tanzania itakavyonufaika na mradi
huo kuanzia kwa mwananchi
mmoja mmoja, taifa, washirika na
mataifa mengine.
>>Inatoka Uk. 13

Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha


Madimba, Sultan Pwaga (kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa
(kulia) hukusu mikakati inayofanywa na kiwanda hicho katika
kuhakikisha kuwa gesi ya uhakika inapatikana.

Meneja Mkazi wa Kampuni ya Statoil Tanzania, ystein Michelsen


(wa tatu kutoka kushoto) akielezea maendeleo ya shughuli za
utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini kupitia kampuni
yake.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani


(kushoto) akifungua Kongamano lililokutanisha Wadau mbalimbali
kwa ajili ya kujadili taarifa juu ya ushirikishwaji wa Wazawa
kwenye mradi mkubwa wa kiwanda cha kusindika gesi kimiminika
kinachotarajiwa kujengwa huko mkoani Lindi, lililofanyika tarehe
29 Septemba, 2016 jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya kiwanda cha kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kama


kinavyoonekana pichani.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Novemba 11 - 17, 2016

13

Mwaka mmoja wa Dkt. Magufuli


Viwanda vikubwa kujengwa, Lindi, Mtwara
>>Inatoka Uk. 12
Tunataka kuhakikisha kuwa
kila mwananchi anashirikishwa
katika mradi huu kulingana na
uwezo wake na ndio maana
kama Serikali tumeanza
kwa kupeleka wanafunzi wa
kitanzania wanaofanya vizuri
katika masomo ya sayansi
kusomea kozi za mafuta na gesi
ili waweze kuajiriwa katika mradi
huu.anasisitiza Dk. Kalemani.
Akielezea ujenzi wa
kiwanda kikubwa cha mbolea
kinachotarajiwa kujengwa
katika eneo la Msanga Mkuu
mkoani Mtwara, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na
Madini, Profesa Justin Ntalikwa
anasema kuwa serikali inatarajia
kushirikiana na kampuni ya
Helm kutoka nchini Ujerumani.
Ili kuhakikisha kuwa suala

hilo la viwanda linatekelezwa


hivi karibuni Profesa Ntalikwa
alifanya ziara ya siku Tatu
mkoani Mtwara kutembelea
maeneo ambayo gesi inazalishwa
na kujiridhisha iwapo
itatosha katika uendeshaji wa
kiwanda kikubwa cha mbolea
kinachotarajiwa kujengwa.
Anaeleza kuwa, kiwanda
cha mbolea kinachotarajiwa
kujengwa, kitahitaji gesi kiasi
cha futi za ujazo trilioni 0.8 kwa
kipindi cha miaka 20 na kusisitiza
kuwa serikali imejipanga katika
kuhakikisha kuwa gesi ya
kutosha inazalishwa ili kuendana
na mahitaji ya kiwanda hicho
pamoja na matumizi mengine ya
majumbani.
Akielezea maandalizi ya
ujenzi wa kiwanda hicho,
Profesa Ntalikwa anafafanua

kuwa, Serikali imetenga eneo la


Msanga Mkuu lililopo Mtwara
lenye ukubwa wa hekta 400
kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda
hicho na kuongeza kuwa eneo
hili limeshalipiwa fidia pamoja
na halmashauri ya Mtwara
kuboresha miundombinu ya
barabara kwa kuweka lami
kutoka Mtwara Mjini hadi
eneo la kiwanda tayari kwa
kukabidhiwa kwa mwekezaji
kwa ajili ya ujenzi.
Pia Serikali inatarajia
kujenga kiwanda kingine cha
mbolea katika wilaya ya Kilwa
mkoani Lindi ambapo kitatumia
gesi asilia. Kiwanda hicho
kitakachojengwa kwa ubia kati ya
Tanzania na nchi za Denmark,
Ujerumani na Pakistani
kitakuwa na uwezo wa kuzalisha
tani 3,800 za mbolea kwa siku.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa


Sospeter Muhongo akielezea miradi ya
ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi
kimiminika (LNG), na viwanda vya mbolea
katika mikoa ya Lindi na Mtwara hivi
karibuni ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

PROFESA NTALIKWA AITAKA TMAA


KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU MADINI
Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam

atibu Mkuu wa Wizara


ya Nishati na Madini,
Profesa Justin Ntalikwa
ameutaka Wakala wa
Ukaguzi wa Madini
Nchini (TMAA) kutoa elimu zaidi

kwa umma kuhusu shughuli za


ukaguzi wa madini zinazofanywa na
Wakala kwenye migodi.
Profesa Ntalikwa aliyasema hayo
alipofanya ziara katika Wakala huo
hivi karibuni lengo likiwa ni kufahamu
maendeleo pamoja na changamoto
unazokumbana nazo katika shughuli
zake.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa


akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisi za Wakala wa
Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa, Umma umekuwa


na mtizamo hasi juu ya Sekta
ya Madini kwa kudhani kuwa
kumekuwepo na udanganyifu juu ya
kiasi cha madini yanayozalishwa na
kusafirishwa nje ya nchi jambo ambalo
si sahihi.
Mnatakiwa kutumia mikakati
mbalimbali ikiwa ni pamoja na vipindi

na Makala kwenye vyombo vya habari


kuelezea jinsi Wakala unavyosimamia
uzalishaji wa madini migodini hadi
usafirishaji nje ya nchi, alisema
Profesa Ntalikwa.
Aidha aliitaka TMAA kushirikiana
na Bodi yake ambaye ndio mshauri
mkuu ili kuleta matokeo bora kwenye
utendaji kazi wa Wakala huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa


(mbele) akizungumza na watendaji na watumishi wa Wakala wa Ukaguzi wa
Madini Tanzania (TMAA) hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

14

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Novemba 11 - 17, 2016

ZIARA YA PROF.
NTALIKWA REA
Kutoka kushoto ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Profesa Justin Ntalikwa,
Kamishna Msaidizi wa Nishati
anayeshughulikia Umeme,
Mhandisi Innocent Luoga, na
Mhandisi Yahya Samamba
kutoka Wizara ya Nishati na
Madini wakifuatilia maelezo
yaliyokuwa yanatolewa na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) Mhandisi Gissima
Nyamo-Hanga (hayupo
pichani) hivi karibuni jijini Dar
es Salaam.

Sehemu ya Watendaji kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA)


wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani).
Katibu Mkuu
wa Wizara
ya Nishati na
Madini, Profesa
Justin Ntalikwa
(katikati,
waliosimama
mbele) akiwa
katika picha
ya pamoja
na watendaji
wa Wakala
wa Nishati
Vijijini (REA),
alipofanya ziara
katika Wakala
huo hivi karibuni
jijini Dar es
Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi


Gissima Nyamo-Hanga akielezea mipango ya REA katika usambazaji
wa umeme vijijini.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Novemba 11 - 17, 2016

15

BUSINESS PERSPECTIVE

Email: salum.mnuna@gmail.com

By Salum Mnuna

Salum Mnuna is MBA, Certified PPP specialist based in Dar es Salaam


Can be reached via email salum.mnuna@gmail.com The views in the article are
solely based on the knowledge of the author and should not be associated with his
employer.

Putting Political Sales proposition HAPA KAZI TU to Work, Make It an action item to

achieve Institution targetsmanagement and the art of getting things done

n 4th November 2016


President of United
Republic of Tanzania
His Excellence Dr.
John Pombe Magufuli
for the first time ever since last year
general election, called for a meeting
with Journalists and used the event
to address the nation through
questions and answers session that
was televised live. Couple of days
before the event day, the occasion
was well advertised by couple of
TV stations in the country to raise
awareness to the much-awaited
moments since he has assumed
highest power in the country. The
ads really cached my attentions and
raised my enthusiasms and desire
not dare miss to hear the statesman
addressing the group of journalists
for the first time since he got into
power. On the occasion day, I took
my time to watch the statesman
response to some of the toughest
questions posed to him by brilliance
packed editors in the state house
event room. My curiosity paid off,
watching a statesman response to
the questions with a patriotic tone
and unbent truth that I have not
experienced for a quite some time in
my adulthood since 80s when I was
little boy.
You look into the President
body language when synchronizing
his words to his facial and body
response and you could tell it, he
meant what he was saying. One
year gone and gone so fast. Mr
President said this job is tough
and sometime takes him to bed
late, you could feel it for him, the
fatigue, anger and I could not
stop imagining the magnitude of
the job that he is undertaking to
tackle unprecedented past event on
corruptions, inefficiency and general
civil service unwelcome catastrophic
behaviors in service delivery. His

address got me thinking and


reminded of the line from the late
Baba wa Taifa past address on a
president value and characteristics,
who when he speaks of corruption
and you look into his face, you
understand that he meant what he
says. For the minute I thought may
be Mwalimu meant this person and
he must be smiling in heaven now
if that is the case. Well, I do not
want to get into that topic, but my
intention purely meant to underline
on current leadership honest
ambition in building the nation to
prosperity for all.
Instilling the work value
The President five years
leadership agenda is famously
defined by slogan hapa Kazi
tu which clearly define work and
nothing else but work as priority in
the long journey to fulfil his election
promise and build a nation with
different mindset in either wealth
creation or work for just a survival
and earning a living. The president
on the move walking the talk, his
call for people to join the ride to
rebuild our country to leave up to
its true potentials regardless of our
political ideology, party affiliation,
tribe or religious background is
nothing but an interest call for every
country person to support. On the
Private investment, he has indicated
his willingness and desire to support
responsible private businesses
that create value to the society as
opposed to dubious and crooks
business practices in the country. He
has iterated with strong tone that he
does not wish to see irresponsible
businesses grows by stealing instead
of creating value to the society. This
ideas needs to synchronize amongst
business community and public
institutions supporting business
community. Work is a lifetime

responsibilities for any grown up


responsible individuals. I do not see
HAPA KAZI TU to be as an
event based slogan but a powerful
lifetime responsibility.
Hapa Kazi tu living a reality
Being a civil service servant, I
thought for a minute what does
this address actual mean to me
and the institution I serve. Is there
anyway, I can translate this speech
to a productive tangible action
and influence my responsibilities?
Well, I could not come up with
immediately better suggestions but
think what HAPA KAZI TU
means in absolute terms, especially
for the people who directly serve
below it. My thought triggered me
to revisit my institution target that
I will be happy to open up and
welcome some debates amongst my
readers and colleagues on what this
really means for the success of entire
fifth government and its affiliates
in building the industrial economy,
employment, sustainable growth
and responsible private investments.
Taking an example of the
Ministry of energy that is tasked
to bring Electricity to about 5000
MW by year 2020 from the current
1500 MW and help it to fuel the
ambitions industrial economy plan.
The Ministry has been supported
by substantive development budget
allocation to accelerate energy
development implementations.
The presence of Electricity (Market
Re-Organization and Promotion
of Competition) regulation 2016,
that provide guide and a legal
platform for an ambitious reform
Programme in its Electricity
Supply Industry (ESI) to attract
investments and remedy capacity
shortages. The regulation will stir
private sector participation in the
electricity subsector by re organize

electricity market and promoting


competition in Electricity supply
chain and boost energy security
at large. With presence of legal
tool, strong leadership, controls
and discipline to public service
topped with individuals ownership,
compliance and eagerness targets
seems to be within reach inside five
years term. Budget and Technology
limitations has always been a
constraint for public development
investments before PPP laws came
into existence. The presence of
Public Private Partnership (PPP)
laws and structured responsible
independent Power Producer
(IPP) procedures create conducive
environment to attract private
partners to participate, address
technology, and budget constraints
issues. Competitive PPP, IPP and
Renewable energy bidding processes
provide the implementation road
map. These processes need not be
static but to continuing evolving to
accommodate changes triggered by
ever-changing investment appetites,
markets and environment.
Peoples behavior like Witch
hunting and finger pointing
which comes centrally in public
service delivery, need to be wiped
out through proper controls and
predictable governance structure.
The need to introduce and
cementing new working culture
of continues improvement from
the previous attempt within
departments and units is of
paramount importance for general
productivity improvement. With
half of such an approach, HAPA
KAZI TU will come out to be the
best social marketing slogan that
turned out to be an action item and
a living reality in country efforts to
bring about economic liberations to
the People of Tanzania.

16

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Novemba 11 - 17, 2016

WAKALA WA JIOLOJIA TANZANIA (GST)

Geological Survey of Tanzania, Kikuyu Avenue, S.L.P 903, Dodoma, TANZANIA. Simu: +255 26 2323020 Nukushi: +255
26 2323020, Barua pepe:madini.do@gst.go.tz, Tovuti:http//www. gst.go.tz, portal:http//www.gmis-tanzania.com

MWAKA MMOJA WA RAIS DK. JOHN MAGUFULI MADARAKANI


Mtendaji Mkuu, Menejimenti na wafanyakazi wa
Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wanaungana na
Watanzania wote kumpongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli,
kwa kutimiza mwaka mmoja madarakani kwa
mafanikio makubwa.
TAARIFA FUPI YA MAFANIKIO YA GST KWA
KIPINDI CHA MWAKA MMOJA CHA UTAWALA WA
SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

iv. Kufanya utati wa jio-sayansi (jiolojia, jiokemia na


jiozikia) katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuchora
ramani (ramani namba 3) za kuainisha kuwepo kwa
madini mbalimbali ili kuhamasisha uwekezaji kwenye
maeneo ya Nachingwea, Ruangwa na Masasi (Mineral
investment promotion map of Nachingwea Ruangwa
Masasi Block)
Ramani Na3: ya Jiolojia ya Nachingwea-Masasi
block.

Katika kipindi cha Mwaka Mmoja cha


Utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano (5)
inayoongozwa na Rais Dr. John Pombe
Joseph Magufuli, Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST) imeweza kutekeleza
majukumu
mengi
kwa
mafanikio
makubwa. Baadhi ya mafanikio hayo ni
kama ifuatavyo:- ikiwa ni pamoja na
i. Kufanya utati wa jiokemia katika
Mikoa wa Mbeya na Songwe
na kuchora ramani za jiokemia
zinazoonesha uwingi wa dhahabu na
metali mbalimbali kwenye miamba.
Ramani hizi zitasaidia katika zoezi la
utafutaji Madini katika mikoa hiyo.

madini
maeneo
Tanzania

ii. Kufanya utati na kuchora


ramani za jiokemia za nchi nzima
zinazoonesha wingi wa metali
mbalimbali (k.m. dhahabu, shaba,
chuma, nikeli, bati n.k.) kwenye
miamba (Country Wide MultElement Geochemical Maps)
Ramani Na. 1:
Ramani
inayoonesha uwingi wa
ya
shaba
katika
mbalimbali
nchini

v.
Utati wa jiosayansi kwa ajili ya kutathimini
wingi wa mashapo katika maeneo yaliyotengwa kwa
wachimbali wadogo ili kuwaongezea tija na ufanisi
wachimbali hao.
Maeneo yaliyofanyiwa utati huo ni pamoja na LondoniSambaru, Misaki, Mpambaa, Kirandotaa na Sekenke
Mkoani Singida; Mvomero Mkoani Morogoro, Handeni,
Kilindi Mkoani Tanga; Mererani, Dongobesh, Mkoani
Manyara; Itumbi na Sangambi Mkoani Mbeya, D-reef,
Kapanda, Ibindi Mkoani Katavi; Katente, Nganzo,
Kerezia na Mgusu Mkoani Geita; Nyamongo na
Buhemba Mkoani Mara na Kyerwa Mkoani Kagera.
Aidha, wakati wa ughani huo mafunzo mbalimbali
(utati, uchimbaji na uchenjuaji salama) yalitolewa
kwa wachimbaji wadogo zaidi 2500 na vijarida vya
kuwaelimisha viligawiwa. Vijarida hivyo ni pamoja
mwongozo kwa wachimbaji wadogo kuhusu utati,
uchimbaji na uchenjuaji salama na wenye tija.
Uchorongaji ili kubaini uwingi wa mashapo umeanza
katika maeneo ya Katente na Nganzo kwa lengo la
kubaini uwingi wa dhahabu (Resource estimates) na
madini mengine yaliyopo.

iii. Kufanya utati na kuchora ramani inayoonesha


viwango vya pH (pH values) (Ramani Namba 2) kwenye
udongo kwa nchi nzima Ramani hiyo inaonesha
maeneo yenye pH ndogo na kubwa ambayo ni mikoa ya
Mbeya, Njombe, Dodoma-Singida, Manyara, Arusha,
Shinyanga na Kigoma. Kutokana na hali hiyo GST
inaandaa programu ya utati wa namna ya kurekebisha
pH katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kwa kutumia
miamba ili yafae kwa kilimo.
Ramani Na.2: Ramani inayoonesha viwango vya pH
nchini Tanzania

vi. Utati wa kubaini chanzo cha tetemeko la ardhi


lililotokea Mkoani Kagera tarehe 10/09/2016 na athari
zake. Utati huo unaonyesha kuwa tetemeko hilo
limetokana na kuteleza kwa mapande ya miamba
kwenye mipasuko ya ardhi kwenye bonde la ufa katika
kina kirefu chini ya ardhi takribani kilometa 36. Aidha,
mafunzo kwa wananchi ya jinsi ya kujikinga na madhara
ya matetemeko pamoja na namna ya kuimarisha ujenzi
wa nyumba na miundombinu mingine yanaendelea
kutolewa mkoani Kagera.
vii. Kuanzishwa kwa mfumo wa kusambaza na kuuza
takwimu, taarifa na ramani za jiosayansi kwa njia ya
eletroniki umetengenezwa (online data sales portal) ili
kuwarahisishia wadau popote walipo duniani waweze
kupata taarifa pale wanapozihitaji. Anwani ya online
data sales portal hiyo ni http://www.gst-datashop.com/

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Novemba 11 - 17, 2016

17

You might also like