Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AFUNGUA KITUO CHA TAALUMA

YA UHASIBU (NBAA) BUNJU


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, ameiagiza Bodi ya Taifa ya Wa hasibu na
Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) kuwachukulia hatua wale wote wanaoitia
doa taaluma hiyo kwa kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.
Maagizo hayo yametolewa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt.Mpango, wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC)
uliokwenda sambamba na ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa wahasibu
unaojumuisha wadau kutoka nchi za Afrika Mashariki, katika eneo la Bunju, nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
AmesemakuwaIdadi ya Wahasibu wenye sifa inazidi kuongezeka na hivyo
kuisaidia Serikali, japo kuwa Serikali hairidhiki kuona wanataaluma wa Uhasibu
na Ukaguzi wa hesabu (CPA) wanaongezeka huku vitendo vya ubadhilifu wa fedha
za Umma na ufisadi vikiendelea kuripotiwa.
Wapo hata wahasibu wanaotumia taaluma yao vibaya, wanaowawezesha
wafanyabiashara kukwepa kodi, wanachakachua vitabu vya taarifa za fedha na
kufanya ufisadi kwa njia ya kalamu na kompyuta jambo ambalo halikubaliki hata
kidogo Aliongeza Dkt. Mpango
Amesema kuwa machozi ya masikini wa Tanzania yatawafuata mafisadi hadi
kaburini lakini serikali ya Awamu ya Tano haitasubiri hao mafisadi wafe,
itawatumbua na wala hakuna mzaha na kwamba tayari mahakama ya mafisadi
imeanza kazi na itawashughulikia.
Aidha, WazirihuyowaFedhana Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewaasa
wanataaluma wa uhasibu na ukaguzi wa hesabukuitumia taaluma yao kuisaidia
Serikali katika hatua yake ya kuelekea katika uchumi wa kati unaotegemea
viwanda kwa kuwa taaluma hiyo inaumuhimu mkubwa.

Kwaupande
wake
MkurugenziMtendajiwaBodiyaTaifayaWahasibunaWakaguziwaHesabu, Bw. Pius
Manenoamesemakuwa,Kituo hicho kilichozinduliwa cha APC hadi kumalizika,
kitagharimu Sh. Bilioni 35 ambapo mpaka sasa fedha zilizotumika ni takribani Sh.
Bilioni 31.5.
Gharama halisi za ujenzi wa kituo hicho zilikuwa Bilioni 14 lakini kutokana na
mzabuni wa ujenzi kuchelewesha ujenzi ndio maana kumekuwa na Ongezeko la
kiasi hicho cha fedha aliongeza Bw. Maneno.
Ujenzi wa kituo hicho ambao uko katika eneo lenye ukubwa wa takribani ekari 14
umehusisha ujenzi wa Kumbi za mikutano zinazochukua zaidi ya watu 1600,
viwanja vya michezo na vyumba vya kisasa 108 vya kulala wageni.
Bw. Maneno amesema kuwa kujengwa kwa kituo hicho kutaifanya Bodi hiyo
kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa kikitumika kukodi kumbi za kufanyia
na kusahisha mitihani ya Bodi (NBAA).
Amezitaja faida zingine kuwa ni kuboreshwa kwa mazingira ya kitaaluma na
wanataaluma wa uhasibu pamoja nakuimarika kwa utawala bora na kuwa chachu
ya uchumi wa viwanda, kwa kuwa Kituo hicho, kinatoa elimu bora
itakayowawezesha wahitimu kuingia kwenye ushindani ndani ya nchi za Afrika
Mashariki na Duniani kwa ujumla.
Ujenzi wa Kituo hicho umedhaminiwa na serikali kupitia mkopo kutoka Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii-NSSF, Bodi ya Uhasibu-NBAA na Mbia mwenza wa kituo hicho,
Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Serikali-GEPF.
Mwisho

You might also like