Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 32

MAKALA 1

Kutoka meza ya Mkuu wa Wilaya


Wilaya ya Ilala tunatambua kuwa
maendeleo ya elimu, afya, maji, usafi,
utunzaji wa mazingira, Miundombinu n.k.
yataletwa na sisi wenyewe. Wadau wetu wa
maendeleo watatusaidia kufikia shabaha
ya malengo yetu kwa haraka. Tutaendelea
kutekeleza malengo yaliyoainishwa
katika mpango wa maendeleo wa miaka
mitano, Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu
wa mwaka 2010, Malengo ya Maendeleo
ya Milenia na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2000-2025.

Tunajenga uwezo wetu wa kujiletea maendeleo. Manispaa ambayo ipo kwa ajili ya
kuunganisha wananchi na wadau wengine; ikusanye mapato yake kwa kiwango cha kutosha.
Baada ya kukusanya matumizi yafanyike kwa uadilifu na weledi ili kupata thamani ya fedha.

Wananchi wetu wanatakiwa kuelewa mipango yetu yote na waimiliki. Wasione mipango
hii ni ya viongozi au kikundi cha watu kwa msingi huu tuwashirikishe kuibua miradi
au mipango yetu ya maendeleo. Waelewe sababu za kutoa kipaumbele kwa shughuli
yoyote itakayoamuliwa kutekelezwa. Utaratibu huu utasaidia kuondoa malalamiko
kutoka kwa wananchi wetu; miradi itakuwa mahitaji ya wananchi na wataimiliki.

Mpango wa matokeo makubwa sasa unatupa uelewa mzuri wa kutekeleza malengo


yetu. Kulingana na mazingira yetu, tunaweza kuongeza sekta za Usafi wa Mazingira na
Biashara ndogo ndogo. Tukipata matokeo makubwa katika sekta za mapato, elimu, maji,
miundombinu, nishati, usafi wa mazingira na biashara ndogo ndogo ni mwanzo mzuri.

Mafanikio ya maendeleo Ilala yatategemea ushirikiano na uwajibikaji wa uongozi na


watendaji wote. Viongozi jukumu lao ni kuamua mambo gani sahihi ya kutekeleza na
kutatua changamoto sugu. Watendaji jukumu lao ni kutekeleza mambo yaliyoamuliwa
kwa usahihi na ufanisi.

Wito wangu kwa wote ni tujenge ushirikiano na uwajibikaji kuleta maendeleo Wilaya yetu
ya Ilala. Ni lazima mchango wetu wa kukabiliana na changamoto za elimu, afya, maji
safi, maji taka, miundombinu, biashara holela, uchafu na uharibifu wa mazingira, makazi
holela, matumizi ya madawa ya kulevya, ukosefu wa ajira, ombaomba n.k. matokeo
yake yaonekane, changamoto zote tunazijua hivyo jukumu letu ni kuzipatia suluhu sasa.

Mhe. Raymond H. Mushi


Mkuu wa Wilaya ya Ilala

Sauti ya Ilala
2 MAKALA

Yaliyomo

w a 6
asa
Ukur

Bonnah education
trust fund mkombozi
wa Elimu
Uku
rasa
wa 2
4
Sofia Kavishe: Kila
aina ya ufugaji uko
kwangu
a 12
s a w
ur a
Uk
Usafi wa Mazingira
ni Jukumu letu sote,
tuwajibike
Sauti ya Ilala
MAKALA
HABARI 3
Mnazi Mkinda wazinduliwa rasmi Ilala
Na Lucy Semindu-Ilala mkono kwa kuratibu mpango wa Mnazi Mkinda ili kukuza
elimu na vipaji vya wanafunzi wa Shule za Msingi za

M nazi Mkinda ni Mpango maalum unaolenga


kuongeza mahudhurio na kisha ufaulu wa wanafunzi
katika shule za msingi katika Manispaa ya Ilala.
Manispaa ya Ilala.

Kwa upande wake Afisa Elimu Shule za Msingi Bi


Mpango huo unasimamiwa na Idara ya Elimu ya Msingi Elizabeth Thomas alisema kuwa Idara yake imeona ni
katika Manispaa ya Ilala chini ya Afisa Elimu wa Idara ya vyema wakaanzisha Tamasha la Mnazi Mkinda ambalo
Msingi Bi. Elizabeth Thomas kwa kushirikiana na wadau linatokana na minazi michanga ambayo imefananishwa
mbalimbali. na mtoto ambaye yupo shuleni anayehitaji kulelewa na
kuboreshwa kitaaluma na kama ana kipaji kinastahili
Katika uzinduzi wa Mpango huo, Mstahiki Meya wa kuibuliwa na kuboreshwa kwa manufaa ya mwanafunzi
Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa amesema wakati sasa mwenyewe na Taifa kwa ujumla.
umefika wa kuboresha Elimu kwa maendeleo ya nchi
yetu na kwamba mpango wa Mnazi Mkinda ni mpango Alifafanua kuwa mpango umelenga kuibua vipaji
utakaoleta matokeo makubwa sasa maarufu (BRN) kwani vya watoto mashuleni na inawafanya wanafunzi hao
wanafunzi wataweza kufahamu kuandika, kusoma na kujitambua, kujiamini na kujitegemea.
kuhesabu huku wakijitambua, kujiamini na kujitegemea
na pia utasaidia kuibua vipaji mbalimbali vya wanafunzi. Alisema wanatambua kuna baadhi ya watoto hawajui
kusoma, kuandika na kuhesabu na kwamba kupitia mpango
Aidha, Mhe. Silaa amesisitiza kuwa wakati umefika wa Mnazi Mkinda itawezesha hasa wale wanafunzi
sasa kwa asasi mbalimbali
kuhusishwa na maendeleo
ya elimu na kwamba ipo haja
vifaa vya kufundishia, vitabu
na taaluma vikaboreshwa ili
kuleta matokeo makubwa
sasa.

Alisema kuwa mchango


wake utakuwa mpaka kufikia
mwisho wa mwaka huu
kupitia mpango aliouanzisha
hivi karibuni ujulikanao kwa
jina la Dawati ni Elimu
kila mwanafunzi katika
Manispaa ya Ilala akalie
dawati.

Awali akitoa utambulisho wa


Mnazi Mkinda Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Mhe. Zuberi Samataba akihutubia
Insiders Tanzania Bw. walimu wanafunzi na wazazi siku ya uzinduzi wa tamasha la mmazi mkinda
Haroun Kinega, alisema, lilofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja. (Picha na David Langa)
Insiders ni washauri katika
kuzindua mpango mkakati wa
Minazi Mikinda kupitia ushirikiano wa wadau na Serikali ambao walikuwa watoro kubaki shuleni kusoma huku
ujulikanao (PPP) Private Public Partneship ). Alifafanua vipaji vyao katika michezo vikaibuliwa na kuendelezwa
kwamba mpango wa Mnazi Mkinda ni kupata matokeo mpaka kufikia kiwango kizuri cha kusoma, kuandika na
makubwa sasa katika sekta ya elimu. kuhesabu. Mpango wa (BRN) Umeanzishwa na Serikali
katika sekta mbali mbali lengo ni kuiwezeshaTanzania
Aidha, Bw. Kinega alisema wao kama wadau wameguswa kufikia moja ya nchi yenye Uchumi wa kati Duniani.
na mpango ulioanzisha Manisapa ya Ilala kupitia idara ya
Elimu ya Msingi na hivyo wameona ni vyema waunge

Sauti ya Ilala
4 MAKALA
Bonnah education trust fund mkombozi
wa Elimu
Na Lucy Semindu Ilala wadau wana nafasi kubwa ya kuchangia maendeleo
kwa kushirikiana na Serikali. Alishukuru wote

E limu ni jambo la msingi kwa kila mtu, ili nchi


yeyote duniani iweze kufikia hatua kubwa ya
maendeleo Amesema Mh.Bonna Kalua Diwani, wa
wanaomuunga mkono Mhe. Bonnah Kalua kwa
jitihada zake za kuchangisha fedha kwa ajili ya
kusomesha wanafunzi 100 watakaokosa ada ya
Kata ya Kipawa. Mh. Kalua ameliona hilo ndio maana masomo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2014.
akaamua kuanzisha mfuko wa Bonnah Education Trust Alisisitiza kwamba pamoja na kwamba Serikali ina
Fund kwa ajili ya kuweza kushiriki kikamilifu kwa changamoto nyingi kama ujenzi wa barabara, kilimo
kushirikiana na Serikali ili Kuleta maendeleo katika ,afya na elimu huku kukiwa na wazazi ambao watoto
sekta ya elimu kwa kuhakikisha watoto ambao wazazi\ wao wamefaulu kwenda kidato cha kwanza lakini
walezi wao wameshindwa kuwasomesha katika elimu wanashindwa kuwapeleka kwa kukosa ada.
ya sekondari kwa kukosa ada, sare za shule , na vitabu
waweze kupata elimu hiyo sawa na watoto wengine. Alisema ni vyema ndoto ya watoto hao ya kupata
elimu isikatishwe Je tuwaache wasiendelee na
Hilo ndilo jambo la Msingi litakalofanywa na mfuko masomo alihoji Mhe. Silaa. Alisema hatua hii ya
Bonnah Education Trust Fund iliyozinduliwa katika kusomesha watoto hao ni ya kimaendeleo kwani
viwanja vya mnazi mmoja. Mpango huo ulizinduliwa unaweza ukawa na madawati, madarasa lakini
na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya ukakosa wanafunzi ambao wanatakiwa wapewe
Ilala Mhe. Jerry Silaa ambapo aliwashukuru watu wote elimu lakini wanashindwa kupata elimu hiyo kwa
waliofika katika shughuli hiyo muhimu ya kampeni sababu ya changamoto za wazazi wao.
maaluum ya kuchangisha fedha za kusomesha watoto
katika Manispaa ya Ilala kwa ngazi ya elimu ya Awali Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Milton
sekondari ijulikanayo kama elimu mwanzo mwisho Makongoro Mahanga ambaye ni Mbunge wa Jimbo la
ambayo ilijumlisha pia uonyeshaji wa mavazi mitaani Segerea aliishukuru Kampuni ya Tigo kwa kukubali
(Street fashion show). kushirikiana na Bonnah Education Trust fund kwa
ajili ya kuweza kuchangia fedha kwa ajili ya ya
Mhe Silaa alisema wakati umefika tutambue
Inaendelea Uk 7

Kutoka kushoto
zi na Ajira,
ni Naibu Waziri wa Ka Kalua,
Kipawa Mhe. Bonnah
Ma ko ng oro Ma ha ng a, Diwani wa Kata ya Wi laya ya
Mhe. aa na Mkuu wa
e Shisael, Meya Jerry Sil
paa ya Ilala kwenye picha
za Tig o Bi Wo ind
Meneja wa huduma ozi waandamizi wa Manis
shi pa mo ja na vio ng
Ilala Mh.Raymond Mu nafunzi wa shule ya sekondari
Mvuti.
. Picha kulia: Wa
ya pamoja siku ya tamasha hilo
Sauti ya Ilala
MAKALA 5
Bonnah education trust fund...
Kutoka Uk. 6 vyema wadau wengine wakajitokeza kwa ajili ya
kusomesha wanafunzi waliokosa fursa ya kulipiwa jambo hili muhimu.
ada ya sekondari. Aliyataka makampuni mengine
yaige mfano huo kwa kusaidia sekta za kijamii. Akifunga shughuli hiyo iliyoambatana na maonesho
ya mavazi ya Mwanamitindo mashuhuri Tanzania
Kwa upande wake Meneja wa huduma wa Tigo Bi. Asia Idarius, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.
Bi Woinde Shisael alisema kuwa Tigo imepanga Raymond Mushi alisema Serikali inazo changamoto
kusomesha wanafuzi 42 ili kuunga mkono kwa dhati nyingi zinazohitaji juhudi za kila mmoja wetu.
mpango huo ulioanzishwa na Bonnah Education .
Trust Fund. Aidha, Bi Woinde alisema kuwa tangu Alisisitiza kwamba yeye ataunga mkono Kiongozi
kuanzishwa kwake mwaka 1993, Tigo inatambua yeyote ambaye ana mpango wa kutatua changamoto
jukumu lake la kusaidia katika sekta mbalimbali za Serikali. Aliwataka Madiwani wengine wajitokeze
ikiwemo ujasiriamali, TEHAMA na Elimu na kwamba kutatua changamoto zilizopo na kwamba changamoto
Tigo inatambua umuhimu wa kuwajibika katika jamii haziwezi kutatuliwa na mtu mmoja peke yake. Sekta
na hii ni moja sehemu ya mikakati ya Tigo. ya elimu ni moja ya sekta ambayo ikiangaliwa na
kutekelezwa kwa dhati itasaidia Serikali kufikia
Alitoa rai kwa makampuni mengine kuchangia kwa matokeo makubwa sasa yaani BRN na kuiwezesha
ajili ya ada na vifaa vya shule na kwamba Serikali Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.
peke yake haiwezi kutatua changamoto zilizopo, ni

Kata ya Buguruni kujenga


stendi ya kisasa ya daladala
Na Charles Chale-UDSM ni biashara inahitaji miundombinu iliyo bora ili kuwasaidia

K ata ya Buguruni katika Manispaa ya Ilala ipo katika


mchakato wa ujenzi wa miradi miwili ya maendeleo
ambayo ni stendi mpya kwa ajili ya daladala na mtaro
wakazi wa kata hiyo.

Kwa mujibu wa Mhe. Lufungulo, Mradi huo wa ujenzi wa


ikiwa ni katika harakati zake za kuboresha mazingira na stendi hiyo unategemewa kutumia fedha za Halmashauri
maendeleo ya Kata hiyo. ya wilaya ya Ilala hivyo kuwataka wananchi kutunza kituo
hicho ambacho hata hivyo ujenzi wake bado haujaanza.
Akizungumzia ujenzi wa stendi hiyo mpya katika
mahojiano na jarida la Sauti ya Ilala, Diwani wa Kata hiyo Hivi sasa jiji la Dar es salaam linatatizo kubwa linalotukabili
Mhe. Magina Lufungulo alisema kuwa tatizo la ubovu ni foleni za magari, hivyo tuna imani mradi huu ukimalizika
wa stendi linasababisha kutokea kwa foleni ambayo utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo hili kwa sababu
inawachelewesha wakazi wa kata hiyo kufika maofisini kata yetu ina wakazi wengi mno hivyo tunausubiri mradi
pamoja na shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa. huu kwa hamualisema mmoja wa wakazi wa Buguruni
ambaye pia ni dereva wa daladala.
Kutokuwepo kwa stendi maalum katika Kata hii
kumekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi katika utekelezaji Akizungumzia mradi wa ujenzi wa mtaro wa maji machafu,
wa shughuli mbalimbali, tunaamini ujenzi huu utakapoanza Mhe. Lufungulo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya
na kukamilika utasaidia kupunguza msongamano wa Mipango miji alisema miradi yote ya ujenzi imepangwa
magari na kukuza pato la wananchi pamoja na Manispaa kwenda sambamba katika kata hiyo.
yetu alisema Diwani.
Mradi huu utaenda sambamba na mradi mwingine wa
Aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi huu umekuja wakati ujenzi wa mtaro wa maji machafu ambao utasaidia katika
muafaka kwa sababu Kata ya Buguruni inakua kwa kasi kudumisha usafi wakati wa mvua. Mradi huu unadhaminiwa
kubwa sana na moja ya shughuli muhimu katika Kata hiyo na Benki ya Dunia
Sauti ya Ilala
6 MAKALA
Manispaa ya Ilala yakamilisha ujenzi nyumba za walimu
Na Michael Noel-UoI

K atika kuhakikisha
kuwa Manispaa
ya Ilala inapiga hatua
katika sekta ya elimu,
Ofisi ya Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala
imesaidia kukamilisha
ujenzi wa nyumba
nne za walimu katika
Kata ya Kiwalani huku
mojawapo ya nyumba
hizo ikijengwa shule
ya msingi Kigilagila na
kukabidhiwa walimu wa
shule hiyo pamoja na
kuezeka upya vyumba
10 vya madarasa.
Naibu Katibu Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Ndg.
Akielezea ujenzi wa
Ibrahim Nassib, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa nyumba tano za walimu
nyumba hizo kwenye
Kata ya Kiwalani zilizojengwa na Manispaa ya Ilala. Kulia ni Afisa Mtendaji
Mahafali ya darasa la
saba shule ya msingi
Kata ya Kiwalani Ndg. Adeltus Kazinduki (Picha na Michael Noel)
Kigilagila, Afisa
Mtendaji (WEO) wa hivyo kuendana na kauli mbiu isemayo Big Results Now
Kata ya Kiwalani, Ndg. Adeltus Kazinduki, amesema (Matokeo Makubwa Sasa), ilisema sehemu ya risala
kuwa, ujenzi ulianza mwaka 2005 kwa fedha za Wizara hiyo.
ya Elimu kupitia kwa Afisa Elimu wa Manispaa ya Ilala
lakini hazikutosha, hata pale wazazi walipochangishana Walimu hao wameendelea kumshukuru Mkurugenzi wa
pia hazikutosha. Manispaa ya Ilala kwa kuthamini maendeleo ya elimu
kwa kuwasaidia kuezeka upya vyumba vya madarasa
Nyumba hizo zilizogharimu kiasi cha Tsh. 53,970,300, 10 ambavyo bati zake zilishachakaa sana, na ujenzi
kwa mujibu wa Kazinduki, mwaka 2012 Kamati ya wa nyumba nne za walimu katika Kata ya Kiwalani
Maendeleo ya Kata (WDC) ikaazimia kuzimalizia, ambapo mojawapo ikiwa ni ya shule hiyo, sambamba
Shukrani kwa Mkurugenzi wa Manispaa kwa kusikia na vyumba vinne vya madarasa ambavyo kwa sasa
kilio chetu na hatimae kukamilisha ujenzi huo mwezi ujenzi umesimama kutokana na kukosekana fedha za
Juni mwaka huu alisema Kazinduki. kuvimalizia.

Nao wanafunzi wa shule hiyo katika wimbo wao maalumu Akitoa nasaha kwenye mahafali yaliyoandaliwa shuleni
wa shukrani, wametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa hapo, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Manispaa ya Ilala na kamati ya maendeleo ya Kata Tanzania, Ndg. Ibrahim Nassibu, amewaasa walimu,
kwa mchango mkubwa wa kuweza kukamilisha ujenzi wazazi na wanafunzi juu ya maadili mema na kuongeza
wa nyumba hizo na kuahidi kushirikiana na walimu kuwa elimu ya msingi waliyoipata iwe chachu ya
kuzitunza. muendelezo wa elimu ya juu ili kujiletea maendeleo.

Katika Risala yao, walimu wa shule hiyo wameishukuru Aidha, Nassibu ameipongeza Manispaa ya Ilala na
Serikali kwa kutambua umuhimu wa elimu na kuiwezesha Kamati ya maendeleo ya Kata ya Kiwalani kwa kujenga
kwa vitabu vya masomo mbalimbali.Tunaishukuru nyumba hizo za walimu na kuahidi ushirikiano kwenye
ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa utaratibu mzuri
unaofanywa wa kutuletea vitabu vya kiada na ziada, Inaendelea Uk. 11
utaratibu huu utawasaidia wanafunzi na walimu na
Sauti ya Ilala
MAKALA 7
Gongo la mboto wageuza taka kuwa mali
Na David Langa Katika kituo hiki watu zaidi ya 200 wamepata ajira

K atika jiji la Dar es Salaam suala la takataka ni kwa namna mbalimbali ambapo taka zinazofikishwa
changamoto kubwa sana kwani pamoja na jiti- kwenye kituo hiki hutenganishwa na kisha kurejeshwa
hada kubwa zinazofanywa na Serikali na idara zote kwenye matumizi kwa njia tofauti.
zinazohusika lakini bado kuna taka nyingi sana zina-
zobaki bila kuzolewa nakupelekwa sehemu zinazo- Hapa taka kama vile Plastiki hukusanywa pamoja na
husika. kisha kuuzwa kwa wenye viwanda kwa ajili ya kutu-
mika kuzalishia tena bidhaa za Plastiki. Pia taka za
Inakadiriwa kuwa Manispaa ya Ilala pekee inazalisha chupa, vyuma na karatasi pia hukusanywa pamoja na
takribani tani 1100 za taka ngumu kwa siku ambapo baadaye kuuzwa kwenye viwanda vilivyopo ndani ya
kati ya hizo ni tani 550 tu ndizo huzolewa kwa ushiri- Jiji la Dar es Salaam.
kiano wa Manispaa na wakandarasi mbalimbali wali-
opewa tenda ndani ya Manispaa. Zipo pia taka zinazotokana na vyakula na mimea ya
aina mbalimbali kama vile maganda ya viazi, ndizi
Taka hizi zinapozolewa toka sehemu mbalimbali za na mabaki ya vyakula. Taka za aina hii zimekuwa
jiji hupelekwa katika dampo la Pugu-Kinyamwezi mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Gongo la Mboto,
ambalo linasimamiwa kwa ushirikiano na mamlaka kwani zinatenganishwa na kisha kutumika kutengen-
ya jiji la Dar es Salaam. eza mbolea ya mboji ambayo ni rafiki wa mazingira.

Hata hivyo pamoja na kuwepo kwa dampo hilo la- Mbolea hii hutumika kukuzia mazao ya aina mbalim-
kini pia kuna changamoto mbalimbali kutokana na bali ikiwa ni pamoja na Bustani za mboga na maua
maeneo hayo ya dampo kukaliwa na watu, hivyo ku- ambapo watu hufika katika kituo hiki na kununua
sababisha kero kubwa kwa wakazi wa maeneo yote mbolea kwa ajili ya matumizi yao.
yanayo lizunguka dampo.
Inaendelea Uk. 11
Maeneo yanayoathirika zaidi
ni pamoja na eneo lote la Kata
yaUkonga, maeneo ya Gongo la
mboto, Pugu, Pugu-Kinyamwe-
zi, Majohe na Kipawa mpya.

Kwa Kuliona hili uongozi wa


kata ya Gongo la Mboto kwa
kushirikiana na Diwani wa Kata
hiyo Mh. Jerry Silaa ambaye pia
ni Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala kwa pamoja waliamua
kuanzisha kituo cha kukusanya
taka na kisha kuzitenganisha ka-
tika mafungu mbalimbali kuto-
kana na aina ya taka husika.

Kituo hiki kinajulikana kama


Kituo cha kutumia tena taka Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Terezya Hoviza wa
(KIKUTA) kilichopo eneo la Vi- pili kushoto akipata maelekezo ya namna ya utendaji ndani ya kituo
wanja vya Kampala Gongo la cha KIKUTA alipokitembelea. Wa tatu kushoto (mwenye miwani) ni
mboto ambacho kimekuwa msaa- Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ambaye pia ni
da mkubwa kwa wakazi wa eneo Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto. (Picha na David Langa)
hilo na maeneo jirani.
Sauti ya Ilala
8 MAKALA
Sheria za Maegesho zapunguza foleni barabarani
Na Michael Noel-UoI

K uwekwa kwa
sheria ndogon-
dogo za matumizi ya
Mzunguko wa sanamu ya askari katikati Manispaa (kushoto) na
sehemu ya kuegesha magari husaidia kupunguza msongamano wa
maeneo ya bara-
bara za katikati ya
Jiji yanaegeshwa
magari katika maeneo
barabara Manispaa
ya Ilala, kumesaidia yaliyoruhusiwa tu
kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa magari kwa ajili ya maegesho ya magari.
barabarani hali iliyopelekea barabara nyingi za kuingia Kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria ma-
mjini na za mitaa kuwa wazi na hivyo kuruhusu magari dereva wa magari yanayoegeshwa katika maeneo ya-
kupishana bila kikwazo. nayokatazwa kuegeshwa magari.
Kuhakikisha kwamba hakuna biashara zinazofanyika
Magari mengi yalikuwa yakipaki maegesho yasiyo rasmi katika maeneo ya barabara na bakaa za barabara na
kandokando ya barabara na hivyo kusababisha ufinyu wa kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wataka-
barabara na kusababisha foleni zisizokuwa za lazima. She- okaidi.
ria hizi zimesaidia kwa kiasi fulani kupunguza adha hiyo.
Kuhakikisha kwamba hakuna shughuli za uoshaji wa
magari katika maeneo ya barabara, bakaa za barabara
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala baada ya kugundua
na maeneo mengine yasiyoruhusiwa katikati ya Jiji na
tatizo hili, wakawapa mkataba kampuni za TAMBAZA na
kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaokai-
MWAMKINGA, AUCTION MART & GENERAL BRO-
di.
KERS, ili kusimamia utekelezaji wa sheria hizi na ukamata-
ji wa magari yaliyopaki katika maeneo yasiyo rasmi. Kuhakikisha kwamba maeneo ya barabara hayatumiki
kama maegesho ya kudumu ya magari mabovu au
Ni dhahiri kwamba lengo la sheria hizi ni kuielimisha jamii gereji bubu.
na madereva wa magari juu ya matumizi sahihi ya barabara
ili kuondokana na msongamano wa magari unaosababish- Kuhakikisha kwamba hakuna vifaa vya ujenzi
wa na baadhi ya madereva kuegesha magari yao kiholela vinawekwa katika barabara na bakaa za katikati ya Jiji
pembezoni mwa barabara na kuifanya kuwa finyu na ma- na shughuli nyingine zozote zenye kuchafua mazin-
tokeo yake kusababisha foleni. gira ya barabara.

MADHUMUNI MAKUU YA SHERIA HIZI: Kuhakikisha kwamba magari ya mizigo hayapaki ka-
Kuwaelimisha watumiaji wa barabara pamoja na mad- tika maeneo ya barabara isipokua kwa ajili ya kupakia
ereva wa magari kuhusu maeneo yanayostahili kuege- na kupakua tu na kwa muda mfupi usiozidi dakika 15.
sha magari na yasiyoruhusiwa kuegesha magari. Pamoja na mambo mengine, utekelezaji wa zoezi hili
Kuweka alama za kuonyesha maeneo ya barabara utafungua barabara nyingi katikati ya jiji hivyo ni muhimu
yanayoruhusiwa kuegesha magari na maeneo yasiy- kwa Manispaa ya Ilala kuzisimamia ipasavyo kupitia
oruhusiwa kuegesha magari kwa kufuata mwongozo mawakala waliyoidhinishwa pamoja na kutoa elimu kwa
kutoka kwa Mhandisi wa Manispaa ya Ilala. umma kuhusiana na sheria hizo.
Kuhakikisha kwamba magari yanayoegeshwa katika

Sauti ya Ilala
MAKALA 9
Gongo la mboto wageuza taka kuwa mali
Kutoka Uk. 9 kuwavutia wawekezaji kuja miaka miwili ijayo kuanzia sasa,
kuwekeza katika kituo hiki na lengo kuu ikiwa ni kuwajengea
Katika kituo hiki upo pia mradi kutoa elimu kwa wakazi wa Gongo uwezo wakazi wa eneo hili ili hapo
wakuzalisha umeme kwa kutumia la Mboto na maeneo ya jirani. baadaye waweze kujisimamia na
taka-vimiminika (Biogas) ambapo kisha kituo kujiendesha kwa faida.
taka laini kama vile kinyesi cha Kituo hiki kimepata ufadhili
wanyama hutumika kuzalisha kutoka nchini Ujerumani Mwakilishi wa BODRA Bi.
umeme wakutosha kutumika chini ya Shirika la BORDA Larissa Duma anasema wao wapo
katika eneo lote la mradi kwa (Bremen Overseas Research and nchini kwa ajili ya kuhakikisha
kuwashia taa na pia upo mpango Development Association) ambao wanawawezesha Watanzania
wakuzalisha umeme zaidi kwa ajili kwa kushirikiana na uongozi wa kujisimamia katika kutunza
ya kuendeshea mitambo ambayo Manispaa ya Ilala inayoongozwa mazingira na kuwa na mazingira
kwa sasa mitambo hii hutegemea na Mstahiki Meya Jerry Silaa endelevu na rafiki kwa viumbe
zaidi nguvu za mikono. wameweza kusimamia ukusanyaji vyote.
wa taka pamoja na kutoa elimu
Hali hii imeweza kubadilisha kwa wakazi wa Gongo la mboto Pamoja na Tanzania BORDA pia
dhana nzima ya taka kuwa kitu na maeneo ya jirani. inafanya kazi katika nchi zilizo
kisichohitajika kwa jamii nzima katika jumuiya ya maendeleo ya
kiasi kwamba hatua hii imeweza Shirika la BORDA linatazamiwa nchi zilizo kusini mwa Afrika
kuwepo katika kituo hiki kwa yaani SADC.

Manispaa ya Ilala yakamilisha ujenzi nyumba za walimu


Kutoka Uk. 8 Mzambarauni na vyumba vya
ujenzi wa madarasa manne watakaotumia nyumba hizo madarasa 16 ambapo kwa hatua
unaoendelea kwa kuchangia milioni kushirikiana na walinzi wa shuleni ya awali imeshakamilisha
moja. hapo kuhakikisha usalama wao na vyumba nane.
mali zao.
Katika hatua nyingine, Afisa
Mtendaji wa Kata hiyo, ameelezea Ujenzi wa nyumba hizo umeenda
changamoto zilizojitokeza na sambamba na ujenzi
kusema kuwa, baadhi ya wananchi wa Ofisi ya Walimu
wenye nia mbaya kwa kutokujali Shule ya Msingi
wamekuwa wakitoa matofali
na kuta na kuiba madirisha
hali iliyopelekea usumbufu
mkubwa, na kuongeza kuwa
wasimamizi wa mradi huo
alikuwa yeye, walimu wakuu
katika Kata ya Kiwalani, Mwl
E. Shekwavi, Mwl Adam
Salida, na Watendaji wa
Mitaa.

Kwa upande wake Mwalimu


Mkuu wa shule hiyo, Mwl Verian Nyumba ya mwalimu Shule ya Mzambarauni(Picha na David Langa
Mfugale, ametoa wito kwa walimu

Sauti ya Ilala
10 MAKALA
Usafi wa Mazingira ni Jukumu letu sote, tuwajibike
Na Michael Noel-UoI kikubwa jitihada za usafi wa mazingira.

M aisha ya Binadamu yanategemea kwa kiasi Jukumu la usafi wa mazingira siyo la Serikali pekee,
kikubwa mazingira ya mahali tunapoishi na tu- bali kila mwananchi anapaswa kuhakikisha anawa-
napofanyia shughuli zetu mbali mbali, kwani mazin- jibika kuyatunza. Ili kufanikisha hili, viongozi wa
gira safi huleta afya bora kwa kupunguza milipuko ya Serikali za Mitaa lazima washirikishwe katika op-
magonjwa na kujenga jamii imara yenye afya na ari eresheni mbalimbali za utunzaji mazingira ili kuwapa
ya kufanya kazi za kijamii na kiuchumi. uwezo wa kusimamia na kukampeni zoezi hili kuan-
zia ngazi ya mtaa yaani nyumba kwa nyumba katika
Wakati Mataifa mengi duniani yakihaha kukabil- maeneo husika.
iana na uharibifu wa tabaka la anga yaani O-zone
layer inayosababishwa kwa kiasi kikubwa na shu- Kasi ya ongezeko la watu wanaoingia na kutoka wak-
ghuli za viwanda, na kusababisha mabadiliko ya tabia iwemo wafanyabiashara ndogo ndogo katika Manis-
nchi na kuleta athari kubwa kwa viumbe hai kama paa ya Ilala, imeleta changamoto katika idadi na ufan-
vile ongezeko la ukame, magonjwa, mafuliko na isi wa vitendea kazi vya kusafisha na kubebea taka
kadhalika, hali kadhalika hatua kali zaidi zinapaswa hasa ikizingatiwa taka nyingi zinaonekana maeneo ya
kuchukuliwa kukabiliana na uchafuzi wa mazingira jirani na masoko.
katika makazi ya watu kunakosababishwa na utupaji
holela wa takataka hasa katika maeneo ya masoko na Tuboreshe mazingira kwa afya zetu, tunza mazingira
madampo yasiyo rasmi katika mitaa na pembezoni nayo yakutunze.Tushirikiane, kwa pamoja tunaweza.
mwa barabara za katikati ya jiji.

Uchafuzi wa mazingira unach-


angia kwa kiasi kikubwa
kusambaa kwa magonjwa
kama vile, kipindupindu, ma-
gonjwa ya kuhara, malaria,
TB na mengine, ambayo
husababisha vifo na kupun-
gua kwa nguvu kazi ya taifa
na kushuka kwa uzalishaji.
Kama wananchi wa kawaida
watafikishiwa elimu ya utun-
zaji wa mazingira Environ-
mental Education, na Serika-
li kuwawekea miundombinu
mizuri na kuwajengea uwezo
wa kuhifadhi taka mahali sa-
hihi pamoja na kuzisimamia
sheria za mazingira, ni imani Gari la kubebea taka, Manispaa ya Ilala
yangu kuwa tatizo hili litakuwa historia.

Katika utunzaji wa mazingira, Manispaa ya Ilala im-


epiga hatua tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma. Ili
kuhakikisha inakabiliana na changamoto hii, hivi kar-
ibuni imebuni mradi wa kusindika taka kuwa mbolea
ujulikanao kama KIKUTA (Kituo cha Kutumia tena
Taka) Gongolamboto, hali itakayosaidia kwa kiasi

Sauti ya Ilala
MAKALA 11
Mpango wa Anuani za Makazi na
Postkodi una lengo la kuinufaisha nchi
Na Lucy Semindu

H ayo yamesemwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya


Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete katika uzinduzi wa mpango wa Anuani
na Postkodi uliofanyika katika viwanja vya Kar-
imjee Jijini Dar es salaam.

Katika hotuba ya uzinduzi, Rais Kikwete alise-


ma kuwa mpango huu ni utekelezaji wa Sera ya
Taifa ya Posta ya mwaka 2003. Alifafanua kuwa
mpango huu wa Anuani na Postkodi utawezesha
watu kufikika kirahisi kule waliko kwani katika
mpango huu nyumba zitapewa namba na mitaa
kutambulika kwa majina, hivyo barua zitaweza
kuwafikia watu majumbani kwao wanakoishi ki-
rahisi zaidi.

Aidha, alisema kuwa mpango huu umekwisha


anza Mwaka 2009 katika Mkoa wa Arusha kati-
ka Kata nane na Mkoa wa Dodoma mwaka 2011
katika Kata nane pia. Alitaja manufaa ya mpango Rais Dk. Jakaya Kikwete akikabidhiwa anuani ya makazi na Waziri
huu ni pamoja na mtu kuweza kutambulika ma- wa Ardhi na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka wakati wa uzinduzi
hali alipo au anapoishi, utarahisisha upatikanaji wa Anuani za Makazi (postikodi) iliyofanyika katika viwanja vya
wa huduma mbalimbali kirahisi, itasaidia katika Karimjee jijini Dar es Salaam.
shughuli za kimaendeleo mfano upatikanaji wa
mikopo, itakuwa rahisi kwa wafanyabiashara kabla ya uhuru kulikuwepo majina ya mitaa lakini baada
kujulikana walipo na hivyo kurahisisha shughuli za kibi- ya Uhuru tulisahau kuendelea kuipa majina mitaa. Maeneo
ashara. yote yaliyopimwa yapewe majina ya mitaa yake alisisi-
tiza.
Alitoa mfano wa sasa nchini Tanzania teknolojia ya mawa-
siliano imekua sana kiasi cha watu kuweza kupokea pesa Sanjari na hilo Rais Kikwete amezitaka Halmashauri zote,
kupitia simu zao za mikononi. Alibainisha kuwa mizigo Manispaa na Majiji kutunga sheria ya kulinda vibao vya ma-
siyo rahisi kuisafirisha kupitia simu za mikononi hivyo ni jina na mitaa. Alisema waharibifu wadhibitiwe na kwamba
lazima ipelekwe mahali kwa anuani kamili. Alisema shu- elimu kwa umma ni jambo muhimu sana litakalorahisisha
ghuli za kiuchumi zitarahisishwa kutokana na mpango huu utekelezaji wa mpango huu.
wa anuani na postkodi.
Pia alizitaka wizara husika zitenge fedha za kutosha kufani-
Aidha, Rais Kikwete alisema ni vyema tujipe muda wa kisha mpango huu muhimu kwa Taifa.
kufanya kazi hiyo, pamoja na kuandaa rasilimali watu na Awali , Waziri wa Sayansi na Mawasiliano Prof. Makame
fedha. Aliziagiza Halmashauri zote ikiwemo, Halmashauri Mbarawa alimweleza Rais kuwa mpango wa anuani za
za Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni kuanza kuipa makazi na postikodi ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya
majina mitaa mahali ambapo makazi yapo kwenye viwanja Taifa ya posta ambapo Wizara iliiagiza TCRA kutekeleza
vilivyopimwa kwani suala hili halihitaji pesa. mpango huu na suala la uwekaji wa majina ya mitaa na
namba zimepewa Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali
Alisema Halmashauri kupitia Madiwani na Kamati za za Mitaa.
maendeleo za Kata zinaweza zikakaa na kupitisha majina
ya mitaa ambayo bado hayajapewa majina. Alitoa mfano Mpango huu unatokana na Azimio la Dunia la kuwepo kwa
wa viwanja vya Tegeta vimepimwa lakini mitaa yake haina anuani na postikodi katika nchi zote ambapo Mhe. Anna
majina Ni vyema mitaa yote iliyo mahali kulipopimwa Kajumulo Tibaijuka Waziri wa Ardhi na Makazi ameteuli-
ipewe majina haraka katika kipindi cha wiki mbili kwani wa kuwa Balozi wa dunia wa mpango huo.
inawezekana kufanya hivyo alisisitiza Mh. Rais. Alisema
Sauti ya Ilala
12 MAKALA
Sekta ya ulinzi yakua kwa kasi nchini Tanzania
Na Lucy Semindu

U linzi ni jambo la msingi ili


nchi yoyote iweze kuendelea
na kufanya shughuli za maendeleo
kwa ustawi wa nchi husika. Ulinzi
ukitetereka basi amani katika nchi
hutoweka na kupelekea nchi hiyo
kupata changamoto mbalimbali kwa
kukosekana kwa ulinzi madhubuti.
Bila shaka Tanzania ni moja ya nchi
zilizopo Afrika ya Mashariki am-
bapo ulinzi na usalama umeimarika
kwa kiasi kikubwa.

Hii inatokana na jitihada za Serikali


kwa kuweza kushirikisha wadau
mbalimbali katika suala la ulinzi
na usalama. Ulinzi unaimarishwa
kwa kutumia Jeshi la ulinzi, Jeshi la
Polisi, Mgambo, Makampuni ya ul-
inzi na sasa Ulinzi shirikishi jamii.
Wafanyakazi wa kampuni ya Swift Security Team Ltd
Swift Security Team limited ni
moja ya makampuni binafsi
ambayo yamepiga hatua kubwa
katika suala la ulinzi na usala-
ma. Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo Bw. Jacob Kissi
alifanya mahojiano na Sauti ya
Ilala akaeleza historia ya kam-
puni yake toka kuanzishwa hadi
kufikia mafanikio ya sasa.

Bw. Kissi alisema kampuni


yake ilianzishwa mwaka 2007
na kwamba alipata uzoefu wa
masuala ya ulinzi kutoka kwa
KK Security ambapo alifanya
kazi kwa miaka minne na ndipo
alipopata wazo la kuanzisha
kampuni yake ya Swift Security
Team limited.

Aidha, Bw. Kissi alisema kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Swift Security Team limited
wakati wanaanza hawakuwa na wa- Bw. Jacob Kissi akifanya mahojiano na Sauti ya Ilala. (Picha Na
teja wengi lakini siku hadi siku wateja David Langa)
waliendelea kuongezeka kutokana na
kuwepo kwa uwajibikaji na utendaji
bora walionao. Kwani wameweza kufanya kazi kwa Inaendelea Uk. 15
ufanisi bila kuwa na matukio ya kiuhalifu na malindo

Sauti ya Ilala
MAKALA 13
Sekta ya ulinzi yakua kwa kasi...
Kutoka Uk. 14 yamekuwa salama kiasi cha kuzidisha imani kwa wa-
teja wao. Hii inatokana na mfumo bora wa mawasiliano
waliojiwekea baina ya wateja na kampuni pamoja na
maaskari kwa masaa 24.

Pamoja na mafanikio hayo Bw. Kissi alieleza changa-


moto mbalimbali ambazo Swift imekuwa ikizikabili
ikiwemo kuwepo kwa wateja ambao wanahitaji ma-
lindo yalindwe na silaha za moto (bunduki). Alieleza
mara nyingi wahalifu wanakuwa na silaha zenye uwezo
mkubwa kuliko silaha wanazoruhusiwa kuwa nazo. Pia
alitaja changamoto nyingine ni ushindani mkubwa wa
masoko hali inayoonyesha kukua kwa sekta ya ulinzi
binafsi.

Bw Kissi alitoa wito kwa Serikali badala ya kuchoma


silaha za moto zinazokamatwa kutoka sehemu mbali
mbali , ingeweka utaratibu mzuri chini ya Jeshi la Polisi
ili silaha hizo zimilikishwe upya kwa makampuni bin-
afsi ikizingatiwa makampuni binafsi ya ulinzi hayana
uwezo wa kuwa na silaha zinazotosheleza mahitaji.

Pia Bw. Kissi ameitaka Jamii iendelee kuamini sekta


binafsi za ulinzi kwani toka zimeanzishwa zimeonesha
kufanya kazi kwa mafanikio kwa kusaidia kuzuia ma-
tukio mbalimbali ya kiuhalifu.

Sekta ya ulinzi binafsi ni sekta inayokua kwa kasi nchini


kwani inakadiriwa kuwa na ajira zinazozidi 50,000. Ni
Sekta inayopaswa kupewa mtazamo mpya kwani inau-
wezo wa kuajiri na kuimarisha suala la ulinzi na usala-
ma.Makao makuu ya Swift Security Team limited yapo
Ilala Sharifu Shamba No 128 block B.

Ilala Sharifu Shamba No 128 block B


Sauti ya Ilala
14 MAKALA
Ujasiriamali na ukombozi wa maisha kwa vijana
Na Gladness Malimi Afisa Habari Mushi na Albert Kimario.
-Halmashauri ya Mkuranga
Joshua G. Traders, duka hili lilianzishwa mwaka 2000

K atika Dunia ya sasa yenye maendeleo ya sayansi kwa kuuza vyombo vya nyumbani peke yake, huku
na teknolojia, sekta ya biashara inakua kwa kasi likiwa na mtaji wa kiasi cha Shilingi za Kitanzania
zaidi hapa nchini na duniani kote kwa ujumla, huku Laki Sita (600,000/=). Mwaka 2002, duka la Joshua
vijana wengi wakitumia fursa zilizopo kujikwamua G. Traders lilianzisha pia biashara ya kuuza mabegi,
kimaisha. ikiwa ni sehemu ya faida iliyotokana na duka la awali
la uuzaji wa vyombo vya nyumbani.
Vijana hao wamekua wakitumia fursa za kujipatia
mikopo midogo na mikubwa kutoka katika asasi za Ni kweli haba na haba hujaza kibaba hadi kufikia
kiserikali na binafsi,na hata kukopeshana wao kwa mwaka 2013 kampuni ya Joshua G. Traders ikika-
wao kutoka katika vikundi vidogo vidogo vya
kuweka na kukopa (SACCOS) vyenye riba iliyo
na unafuu, ili waweze kujipatia mitaji ya bi-
ashara.

Fursa nyingine iliyopo ni kuhudhuria semina


na mafunzo yanayohusu ujasiriamali, ili kupata
ufahamu mkubwa wa uendeshaji na usimamizi
wa biashara.

Mfanya kazi wa Joshua G. Traders akionyesha


moja ya mabegi yanayopatikana dukani hapo.

diriwa kufikia kiasi cha Shilingi za Kitanzania


Milion 3.

Mpaka kufikia mwaka 2013, duka la Joshua G.


Traders limeweza kujitanua na kujihusisha na
usafirishaji wa mizigo kwenda mikoani na hata nje ya
Katika mtaa wa Lumumba jijini Dar-es-Salaam mipaka ya Tanzania.
mkabala na Chalize auto spare naliona duka kubwa
linalouza mabegi kimtazamo linanivutia na kunifanya Ni mbinu zipi zinazotumiwa na Joshua G.
niingie ndani ya duka hili, Traders katika kuleta mvuto wa biashara
kwa wateja?
Ndipo nakutana na Mfanyabiashara anaitwa Estomihi
Lema anayemiliki duka linaloitwa Joshua G. Traders,
duka hili linauzwa mabegi na vyombo vya nyumbani, Mmiliki wa duka la Joshua G. Traders, bwana
huku likiwa na Wafanyakazi wawili ambao ni Noel
Inaendelea Uk. 17
Sauti ya Ilala
MAKALA 15
Ujasiriamali na ukombozi wa maisha...
pango.
Kutoka Uk. 16 Gharama kubwa za kodi ya biashara (T.R.A)
Estomili Lema, anabainisha siri za mafanikio ya duka Kuchelewa kulipa mishahara ya Wafanyakazi,
lake: ambapo muda mwengine hushusha morali ya kazi
Kauli nzuri wakati wa kuongea na kukosekana ufanisi.
na wateja, Wafanyakazi wangu Kuwa mvumilivu kwenye Una ushauri gani kwa Wa-
wamekua ni wakarimu kwa wa- kazi wakati wote wa bi- fanyabiashara wengine?
teja wanaokuja kununua bidhaa ashara ikiwa ni pamoja Hapa Bwana Estomili Lema,
kwetu na hata wale wanaokuja na kuheshimu kila mtu anashauri yafuatayo:
kuulizia bidhaa kwetu, huku unayekutananaye kwenye Uvumilivu katika bi-
wakitumia lugha nzuri zenye ashara ni jambo muhimu
ushawishi kwa wateja wetu.
kazi hakuna shortcut ya mno, maana kuna wakati bid-
kufanya ili kumfanya mtu haa zinakosa soko, siku nzi-
Pia, kwa upande wa bei ya bid- atoke kimaisha ma unaweza usiuze bidhaa
haa, duka la Joshua G. Traders hata moja, sasa ukikosa uvu-
milivu unaweza ukashindwa
biashara.
Kujiamini napo ni sehemu ya mafanikio ya bi-
ashara, Mjasiriamali watakiwa usiogope kujaribu
jambo (risk taker)
Kuiheshimu kazi kwa kuwajibika,nidhamu na ku-
jituma
Unawahimiza nini Wananchi?

Mmiliki wa duka la Joshua
G. Traders, bwa-
na Es-

limeweka bei zilizo na unafuu kwa wateja


wake, bei isiwe kubwa sana au ndogo
sana, bei ya kumridhisha mteja

Kuwa mvumilivu kwenye kazi wakati


wote wa biashara ikiwa ni pamoja na
kuheshimu kila mtu unayekutananaye
kwenye kazi hakuna shortcut ya kufanya
ili umfanya mtu atoke kimaisha bwana
Estomihi Lema alisisitiza
tomili Lema, anawakaribisha Wananchi wote kwenda
Ni changamoto zipi wanazokabiliana nazo Joshua G.
kupata bidhaa mbalimbali za maofisini na nyumbani,
Traders katika kuendesha biashara yao?
kama vile mabegi na vyombo vya nyumbani.
Bwana Estomili Lema, anabainisha changamoto wa-
nazokabiliana nazo:
Gharama kubwa za ulipaji wa pango, mfano mwa-
ka 2004 tulikua kwenye hatari ya kupokonywa

Sauti ya Ilala
16 MAKALA

Habari kat

1 2

3 4
2 Rais Dk. Jakaya Kikwete akiteta na jambo Meya wa
Manispaa ya Ilala Mhe. Jerry Silaa katika siku ya
maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa na walemavu.

3 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi


(kutoka kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.
Sofia Mjema, Mama Salma Kikwete na Meya wa
Manispaa ya Ilala Mhe. Jerry Silaa katika mazoezi
kabla ya kuanza ziara ya kuhamasisha Dawati ni
Elimu.

4 Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Huduma za


Jamii wa Manispaa ya Ilala katika picha ya pamoja

5 na Watendaji na Viongozi wa Jiji la Mwanza, wakati


wa ziara ya kamati hiyo Jijini Mwanza. (Picha na
Tabu Shaibu)

1 Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa 5 Wanafunzi wa shule mbalimbali wakifanya mazoezi
(katikati), Afisa Elimu Misingi Bibi Elizabeth Thomas kabla ya kuanza ziara ya kuhamasisha Dawati ni
(kulia) na Mkururugenzi Mkuu wa Kampuni ya Elimu chini ya Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe.
Isiders Tanzania Bw. Haruni Kinega (Kushoto) Jerry Silaa.
katika kikao na waandishi wa habari

Sauti ya Ilala
MAKALA 17
atika picha Picha na David Langa

6 7

8 9
7 Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala.(katikati) Mhe. Angelina
malembeka(Uchumi na Huduma za jamii), (kushoto)
Mhe. Lufungulo Magina(Mipango Miji na Mazingira),
(kulia) Mhe. Sultan Salim (Ujenzi) wakiwasilisha taarifa
za Kamati zao katika Baraza la Madiwani. (Picha na
David Langa)

8 Daktari bingwa wa watoto Dk. Andrew wa Hospitali


ya Amana akiwatembeza wadau wa afya waliofika
kutembelea Hospitali hiyo na kukabidhi vifaa vya
hospitali.

10 9 Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Jerry Silaa


akipokea mashine maalum ya kuhifadhia watoto
waliozaliwa kabla ya wakati (incubator ) toka kwa
Sujata Jaffey wa kampuni ya PKF.
6 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge 10 Watumishi wa Idara ya Afya Manispaa ya Ilala
wakicheza ngoma ya Mganda kwenye wakinyunyiza dawa ya kuuwa mazalia ya mbu
uzinduzi wa Tamasha la Mnazi Mkinda katika Bonde la Jagwani

Sauti ya Ilala
18 MAKALA
Serikali ya awamu ya nne yatekeleza
ahadi za ilani ya uchaguzi kwa vitendo
Barabara ya mradi wa usafiri uendao haraka awamu ya kwanza wazinduliwa.
Ujenzi wa daraja la Kigamboni ambalo ni la kisasa na kipekee Afrika Mashariki
na Kati wazinduliwa rasmi.
Na Lucy Semindu Dar es Salaam

S erikali ya awamu ya nne imetekeleza


ahadi ilizotoa kwenye ilani ya uchaguzi.
Hayo yamedhihirishwa kwa vitendo pale
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alipozindua mi-
radi mikubwa itakayoondoa adha ya usafiri
kwa wananchi hususan wakazi wa Jiji la Dar
es salaam. Miradi hiyo ni barabara ya mradi
wa usafiri uendao haraka awamu ya kwanza
na Ujenzi wa daraja la Kigamboni.

Itakumbukwa kuwa tangu kuzinduliwa


kwa Barabara ya mradi wa usafiri uendao
haraka uliofanyika Septemba 2012, katika
viwanja vya Jangwani na Mhe. Rais Dk. Ja-
kaya Mrisho Kikwete. Mradi huo umeende-
Rais Dk. Jakaya Kikwete akitazama mfano wa daraja
lea kuwa tumaini kubwa kwa wakazi wa Mkoa wa
Dar es salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam la Kigamboni
Mhe. Sadick wakati wa uzinduzi wa barabara
ya mabasi yaendayo kasi alibainisha kuwa ki-
tendo cha Serikali kuamua kujenga barabara
hiyo ni kithibitisho cha utekelezaji wa Ilani
ya uchaguzi ya CCM kwa vitendo.

Mradi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka


unakadiriwa kugharimu Bilioni 225.62 za Ki-
tanzania ambapo ni Mkopo kutoka Benki ya
Dunia. Wakati wa uzinduzi Mhe. Rais alisema
ameridhika na maendeleo ya ujenzi wa bara-
bara hiyo na alitaka kuwepo na usimamizi wa
kutosha na kuhakikisha barabara inajengwa
kwa viwango vilivyokusudiwa.Kwa sasa kasi
ya ujenzi wa barabara hiyo ni wa kuridhisha
na ni matumaini ya wakazi wa Dar es Salaam
kuwa adha ya usafiri katika jiji hilo linakaribia
kufika tamati.
Barabara ya Morogoro inayoendelea kujengwa kwa
Ni wazi kuwa ufumbuzi wa changamoto ya usafiri magari yanayoenda haraka
katika Mkoa wa Dar es Salaa ni kujengwa kwa
barabara ya mabasi yaendayo haraka na baadaye wakati mmoja na kupunguza adha ya usafiri katika
kuwepo mabasi makubwa yatachukua watu wengi kwa Inaendelea Uk. 20
Sauti ya Ilala
MAKALA 19
Serikali ya awamu ya nne...
Kutoka Uk. 20
mkoa wa Dar es salaam. Faida nyingine
ya mradi huu ni kupunguza msonga-
mano ambao ni changamoto ya kitaifa,
kijamii na kiuchumi kwani muda ambao
ungetumika kwa shughuli za uzalishaji
mali unapotea wakati watu wakihangai-
ka kutafuta usafiri.

Barabara ya mabasi yaendayo haraka


inajengwa kwa kutumia wakandarasi
mbalimbali wakiwemo , Ms Beijing,
Strabag kutoka Ujerumani , Civil En-
gineering Construction Company na
Spencon. Kwa mujibu wa Dk. Magu-
fuli mradi huu ulikusudia kutoa ajira Mchoro wa barabara ya magari yaendayo haraka

barabara za juu fly-overs katika eneo la Ubungo.

Sanjari na tukio hilo Dar es Salaam ilishuhudia


uzinduzi wa kihistoria wa Daraja la Kigamboni lil-
iozinduliwa tarehe 20 Septemba, 2012, na Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete. Ambapo Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadick ali-
ishukuru Serikali kwa kutatua changamoto za wa-
nanchi ikiwemo utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi
na kwamba karibuni ahadi zote zimetekelezwa
ikiwemo ujenzi wa daraja la Kigamboni.

Daraja la Kigamboni linajengwa na Shirika la Hi-


fadhi ya Jamii la (NSSF) lililo chini ya Wizara
ya Kazi na Ajira. Mhe. Gaudensia Kabaka am-
baye ni Waziri wa Kazi na Ajira alieleza manu-
faa yatakayopatikana na kuwepo kwa ujenzi wa
Daraja la Kimara linalojengwa katika barabara ya daraja la Kigamboni ni pamoja na ; kuunganisha
Morogoro kwa magari yanayoenda haraka mji mpya wa Kigamboni na Jiji la Dar es slaam,
kusaidia jamii kiuchumi ,kupunguza adha ya us-
kwa watu 650,000 na tayari watu wengi wamefaidika afiri kwa wakazi kwani magari makubwa hushindwa
kupata ajira katika mradi huu. kutumia kivuko na kulazimika kuzunguka masafa
marefu kupitia mbagala, kongowe na kutokea kigam-
Kama ilivyoelezwa na Mkurugenzi wa Tanroads, boni, matumizi ya daraja yataondoa msongamano wa
Mhandisi Parick Mfugale ujenzi wa awamu ya kwan- kusubiri kivuko,kurahisisha usafiri kutoka katika eneo
za wa barabara ya usafiri uendao haraka utajengwa moja kwenda lingine.
ikiwa na upana wa mita saba njia mbili kila upande.
Barabara hii itajengwa kuanzia; Kimara Ubungo kupi- Waziri wa Ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli alikwi-
tia morogoro Road mpaka Kivukoni, Magomeni hadi sha eleza kuwa ujenzi wa Daraja hilo linalogharimu
Moroco na Ubungo Jangwani mpaka Kariakoo. San- shilingi
jari na hilo Tanzania kwa mara ya kwanza itakuwa na Inaendelea Uk. 22
Sauti ya Ilala
20 MAKALA
Serikali ya awamu ya nne...
Kutoka Uk. 21
bilioni 214.6 linajengwa kwa kutumia Mkandarasi
China Railway Construction Group, litakuwa la kisasa
alifafanua kuwa daraja hilo litakuwa na nguzo ndefu
na litashikiliwa na nyaya maalum (cables) na kwamba
litakuwa kivutio cha pekee Afrika Mashariki na Kati .

Katika uzinduzi huo Mhe. Rais Dk. Jakaya Kikwete


alisema barabara ni mishipa ya fahamu ya ustawi wa
uchumi na kwamba ujenzi wa barabara na madaraja
una faida kubwa kiuchumi na kijamii. Alisema Bara-
bara zimeongezeka lakini magari yameongezeka pia
kutokana na hali ya uchumi wa watu kuongezeka na
hivyo magari yamekuwa mengi pia. Hivyo Barabara za
mzunguko (ring roads) ni suluhisho la kuondoa mson-
gamano. Alisema hatutaki kusutwa kwa kutoa ahadi
zisizotimizwa kuzinduliwa kwa ujenzi wa daraja la
Kigamboni ni kielelezo kuwa tumeweza .

Usafi wa mazingira Uzingatiwe

Maafisa mazingira wasaidizi wa Manispaa ya Ilala wakiwa katika picha ya


pamoja kabla ya kuanza ukaguzi wa mazingira. (Picha na Hatibu Jumbe)

Sauti ya Ilala
MAKALA 21
Kamati yahimiza uzingatiaji wa Sheria za Mipangomiji
Na Kassim Nyaki ifafanua.
Katika ziara ya kamati hiyo iliyotembelea pia sekta

H almashauri ya Manispaa ya Ilala kupitia


kamati ya Madiwani inayosimamia Mipan-
gomiji, Maliasili na Mazingira imetoa wito kwa
ya Viwanda, wajumbe wa kamati hiyo wametoa agi-
zo kwa wenye viwanda katika Manispaa hiyo kuhak-
ikisha wanafuata sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja
wananchi wa Manispaa hiyo kuzingatia sheria za mi- na utunzaji wa mazingira, usafi katika maeneo yao ya
pango miji ikiwa ni pamoja na kutobadilisha matumizi kazi pamoja na kuwapatia watumishi wao vitendea
ya maeneo yao bila kupata kibali kutoka Manispaa hiyo. kazi vitakavyosaidia kujikinga na maradhi mbalimbali.

Mwenyekiti wa kamati ya Mipangomiji katika Halmashauri Wakiwa katika ziara ya kutembelea viwanda vya maeneo
ya Manisipaa ya Ilala, Mhe. Magina Lufungulo, amesema ya Kiwalani na Buguruni wajumbe wa kamati hiyo Mhe.
kuwa, wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakibadilisha Abdulkarim Masamaki na Mhe.Gharib Riyami wame-
matumizi ya maeneo yao bila kufuata taratibu zilizowekwa washauri wamiliki wa viwanda hivyo kwamba pamoja na
kisheria juu ya kuomba vibali vya kubadili matumizi kwamba wamekuwa na msaada mkubwa hasa katika suala
ya makazi au biashara kutoka mamlaka zinazohusika. la ajira kwa wananchi na kusaidia katika huduma za jamii,
kuna umuhimu wa kuwajali wafanyakazi wa viwanda hivyo
Mhe. Lufungulo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bugu- ikiwa ni pamoja na kuwanunulia vitendea kazi kama sare,
runi ameliambia Sauti ya Ilala kuwa kamati yao inafanya gloves, mabuti na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.
kazi kubwa kwa kushirikiana na watumishi mbalimbali Wamiliki wa viwanda mmesaidia serikali katika suala la
wa Halmashauri hiyo ili kuhakikisha suala la mipangomiji ajira kwa vijana wetu, lakini msijali uzalishaji wenu zaidi
linazingatiwa, hali itakayosaidia upangaji wa mipango ya kuliko afya za wafanyakazi, ni vizuri na wao wakafurahia
maendeleo ya wananchi na kukuza pato la Halmashauri kazi kwa kuwaboreshea mazingira, isiwe wanawazalishia
ninyi mnanufaika wao wanabaki na hali ngumu baada ya
kumaliza mi-
kataba yao ya
kazi, alieleza
Mhe. Riyami.

Wakati huo-
huo, kamati
hiyo imeshauri
maombi ya
kubadilisha
matumizi ya
uwanja eneo
la Kimanga
kuwa soko ya-
tazamwe upya
kwa kushiriki-
sha wataalamu
wa Mipango-
miji kutoka
chuo kikuu
kabla ya kamati
hiyo kuridhia.

Ni muhimu majengo kama haya yazingatie sheria za mipango miji Akitoa tath-
imini ya
ziara hiyo
Kamati yetu imedhamiria kufanya kazi kwa kushirikiana mwenyekiti wa kamati hiyo amebainisha kuwa kamati
na wataalam mbalimbali wa Halmashauri yetu ili kuhak- yao imejipanga vizuri kuhakikisha inatekeleza maju-
ikisha utaratibu wa mipango miji unapangwa na kusaidia kumu kwa kushirikiana na kamati ya ujenzi katika Hal-
uboreshaji wa mapato ya Halmashauri, hali itakayosaid- mashauri ya Ilala ili kuhakikisha sheria za Mipangomiji
ia uboreshaji wa huduma za jamii kwa wananchi, al- zinafuatwa na kuimarisha maendeleo ya Manispaa hiyo.
Sauti ya Ilala
22 MAKALA
Sofia Kavishe: Kila aina ya ufugaji uko kwangu
Na David Langa wa mambapo tulikuwa tunawauzia majirani zetu.

M ama Sofia Peter Kavishe mkazi wa Ukonga


Mwembe Madafu anaeleza jinsi alivyonufaika
na Ufugaji na Kilimo tangu alipoanza mwaka 1982
Baada ya hapo Mama Kavishe aliongeza shughuli
zake za ufugaji kwa kuongeza idadi ya ngoombe,
mbuzi, kuku wa mayai na nyama, kondoo, bata, ngu-
akiwa mkoani Kilimanjaro ambapo alikuwa akifuga ruwe na samaki ambapo mpaka sasa ana aina mbali
ngombe wa maziwa pamoja na kuku wa kienyeji. mbali za wanyama zaidi ya 200 wanaofugwa kwa
kutumia ufugaji wa kisasa.

Hapa nina zaidi ya Nguruwe 120, ngombe 20,


mbuzi 20 pamoja na kondoo. Hivi karibuni nimeanza
ufugaji wa samaki ambapo nimepandikiza vifaranga

3300 katika bwawa lililopo


karibu na nyumba yangu;
2
Mama Kavishe anasema ufu-
gaji wa Samaki ni rahisi kuliko
aina yoyote ya ufugaji kwani nguvu
kazi inayohitajika ni ndogo ukilinganisha na aina
nyingine ya ufugaji.Anasema samaki hawahitaji
kuhudumiwa mara kwa mara kama ngombe au
kuku kwani ukishawapandikiza unasubiri tu maele-
kezo ya wataalamu ili kuhakikisha samaki wana-
Inaendelea Uk. 25

nilihamia jijini Dar es Salaam mwaka 1993 nikiwa


na ngombe wawili tu ambapo kazi hiyo nilikuwa nai-
1 Mama Sofia Kavishe akihojiwa na Sauti
ya Ilala kuhusu miradi yake
fanya mimi mwenyewe kwa kushirikiana na watoto
wangu baada ya kutoka shule 2 Mradi wa mbuzi

Anasema mara ya kwanza watoto wangu walikuwa


wanaona kama ni adhabu kuhudumia wanyama lakini 3 Mradi wa kuku na bata
kadri siku zilivyokuwa zikienda waliipenda kwani
waligundua kuwa walikuwa wakipata matumizi yao
yote kutokana na mifugo hiyo baada ya kuuza mazi- 4 Biashara ya samaki

Sauti ya Ilala
MAKALA 23
Kila aina ya ufugaji...
Kutoka Uk. 24
Wito kwa Akina Mama.
kuwa salama.
Mama Kavishe anawashauri wakina
Mafanikio mama kuto-
Mama Kavishe anasema amefanikiwa
kuwasomesha watoto wake wote ndani
na nje ya nchi kupitia ufugaji na pia
amefanikiwa kujenga nyumba ya kuishi
na zingine tatu za kupangisha na kumu-
ingizia kipato cha kila mwezi.

Pia kupitia mifugo napata mahitaji yangu


yote ya kila siku kuanzia chakula na ku-
weza kuwalipa wafanyakazi wanaonisaidia
katika shughuli zangu za ufugaji, anasema
mama Kavishe. Na pale ninapouza mifugo
naweka akiba kwa ajili ya familia yangu
ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika ujenzi
wa nyumba. kaa kusubiri ku-
ruwe saidiwa na waume
radi wa ngu
Changamoto zao M kwani kazi ya ufugaji
Changamoto kubwa inayotukabili sisi wafugaji ni ni ra- hisi na inaweza kufan-
soko la uhakika kwani wakati mwingine nakosa soko y i k a katika eneo dogo katika makazi wanayoishi.
Anasema ufugaji unafaida kubwa sana
tofauti na watu wanavyofikiri kwani un-
akupatia maahitaji yako ya kila siku en-
dapo utajituma kufanya kazi kwa ufanisi.
Wito kwa Serikali.

Mama Kavishe anaomba serikali ku-


wawezesha wafugaji wadogo wadogo kwa
kuwapatia mikopo yenye riba nafuu kwani
kwa sasa wanategemea mikopo inayotole-
wana na Mabenki ambayo masharti yake ni
magumu na pia riba inayotozwa ni kubwa
kiasi cha kutokuwa na manufaa kwa wafu-
gaji wadogo wadogo.

Pia anaiomba Serikali kuwa na sera inay-


olinda soko la ndani la bidhaa ya mifugo
kwani mpaka sasa hoteli kubwa hapa nch-
Bwawa la samaki ini zinaingiza bidhaa kama maziwa, nyama
la uhakika la maziwa kiasi cha
kufanya maziwa yaharibike. na mayai toka nje ya nchi hali inayowakwamisha
Changamoto nyingine ni pale wanyama wanapokufa wafugaji. Nashangaa kusikia wenye hoteli wanain-
kutokana na magonjwa mbali mbali ikiwa ni pamoja giza mayai toka nchi za nje wakati walaji kwenye ho-
na kula mifuko ya plastiki iliyozagaa mitaa yote hali teli hizi ni sisi watanzania; anasema mama Kavishe.
inayoturudisha nyuma.

Sauti ya Ilala
24 MAKALA
BRN kuiwezesha Ilala kuongeza mapato ya ardhi, majengo
Na Michael Noel- UoI

H almashauri ya Manispaa ya Ilala imeweka


mpango mkakati wa kuongeza mapato yake
kupitia kodi ya ardhi na majengo katika mpan-
Makusanyo ya kodi ya Ardhi yanatarajiwa
kuongezeka kutoka 8.1 bilioni mwaka 2013/14 hadi
kufikia 16.8 bilioni mwaka 2015/16. Kinachotaki-
go wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now wa ni kufanya kazi kwa pamoja (teamwork) kwa
(BRN), ili kuondokana na utegemezi kutoka Seri- uwazi na kubadili sheria ya kodi za Serikali za mi-
kali kuu. taa kupitia TAMISEMI ili kuziwezesha Halmashauri
kuongeza kipato chao, aliongeza Mkandi.
Hayo yalielezwa hivi karibuni na Mkuu wa wilaya
ya Ilala Mhe. Raymond Mushi pamoja na viongozi Kuna njia rahisi na fupi inayotumia rasili-
waandamizi wa Manispaa hiyo katika semina ele- mali kidogo kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
kezi kwa viongozi watendaji wa Serikali za Mitaa alisisitizaAidha, Mkandi alibainisha kuwa, kiasi
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee, Posta. cha Shilingi 8,434.5 milioni hazikusanywi kutoka-
na na mpangilio mbovu wa majengo. Naye Abel
Akifungua semina hiyo Mhe. Mushi alisema, Mwasunguti akitoa ufafanuzi wa Uthamini wa
Serikali imeweka sekta sita za kipaumbele am- Ardhi na Majengo, ,ameelezea kuwepo kwa idadi
bazo ni Nishati na gesi asilia, Kilimo, Maji, Elimu, kubwa ya majengo ambayo hayalipiwi kodi kuto-
Uchukuzi, na Ukusanyaji mapato, hivyo akatoa kana na kutosajiliwa.
wito kwa kila kata kuhakikisha inatilia mkazo uku-
sanyaji mapato ya kodi ya majengo kwa kuonesha Kuna zaidi ya majengo 400,000 hayajaingizwa ka-
ushirikiano wa kutathimini (Mass valuation) ardhi tika mfumo huu, hivyo ni lazima yaingizwe katika
na majengo ya wakazi wao. mfumo ili kuleta Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
alisisitiza Mwasunguti.
Akitoa mada kwenye semina hiyo kuhusu Mfumo
wa Maabara ya mapato na viashiria vya matokeo
makubwa sasa (BRN)
kwa kukusanya mapato
ya vyanzo vya Mamlaka
ya Serikali za Mitaa Bw.
Shomari Mkandi kutoka
Presidential Delivery
Bereau (PDB) amesema
kodi ya ardhi inach-
angia kiasi kikubwa cha
mapato ya vyanzo vya
ndani vya Halmashauri
za majiji mengi ikiwemo
Mwanza, Mbeya, na Dar
es salaam.

Kiashiria cha msingi,


kwa mujibu wa Mkandi
ni kuongeza mapato ya
kodi za majengo kuto-
ka shilingi 16.7 bilioni Mwenyekiti wa mipango miji wa Manispaa ya
mwaka 2012/13 hadi 25.3 bilioni mwaka 2013/14. Ilala Mhe. Sultan Salim akikagua moja ya jengo
Aliongeza kuwa, 32.9 bilioni mwaka 2014/15 na linalojengwa katika Manispaa ya Ilala. (Picha David
42.8 bilioni katika mwaka 2015/16 kinatarajiwa Langa)
kukusanywa kupitia kodi ya majengo.
Inaendelea Uk. 33
Sauti ya Ilala
MAKALA 25
Mwenge wa Uhuru Dira ya maendeleo Ilala
Na Hashim Jumbe

S iku ya 22 ya mwezi wa Oktoba, mwaka


1959, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere, wakati aki-
hutubia Baraza la Kutunga Sheria (LEGI-
CO) wakati huo, kama Mwenyekiti (Rais)
wa TANU na Mjumbe wa LEGICO, alise-
ma: Sisi (Watanganyika), tunataka kuu-
washa mwenge na kuuweka juu ya Mlima
Kilimanjaro umulike hata nje ya mipaka
yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna
matumaini, upendo pale ambapo pana
chuki,heshima ambapo pamejaa dharau

Miaka miwili baadae, usiku wa kuam-


kia tarehe 9-12-1961, Meja Alexander
Gwebe Nyirenda, akaipandisha bendera
ya Uhuru na kuuweka Mwenge wa Uhu- Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi, akipokea
ru juu ya Mlima Kilimanjaro, na historia Mwenge wa Uhuru kutoka kwa wakimbiza Mwenge, kulia
mpya ya Watanganyika ikaandikwa, Tan- Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Jerry Silaa
ganyika mpya iliyo huru, yenye amani, wakati wa mbio za Mwenge huo Manispaa ya Ilala hivi
upendo,matumaini na yenye heshima ika- karibuni.(Michael Noel)
zaliwa, ni jambo jema, lenye faraja na fu-
kwa kila mwaka, mbio za Mwenge wa Uhuru huwa
raha sana kua sehemu ya historia ya nchi uipendayo
na kauli mbiu ambazo huchaguliwa kila mwaka
au hata kuhadithiwa au kuisoma historia ya nchi hii
kutokana na vipaumbele vya kimaendeleo ya Man-
ya watu waliozoea kuishi katika misingi ya amani na
ispaa, zikihusishwa na uzinduzi wa miradi ya maen-
upendo, huku wakiendelea kurithi kauli ya Sisi wote
deleo katika kila maeneo upitapo Mwenge wa Uhu-
ni wamoja
ru, huku mbio hizo zikiambatana na ujumbe wa
matumaini,upendo,amani na heshima.
Muasisi wa harakati hizi, leo hii hatunae tena Duniani,
mwili wake umelala kwenye ardhi ya kijiji chake
Siku ya 5 ya mwezi Septemba, mwaka huu wa 2013,
huko Butiama, fikra,falsafa, maono na mawazo yake
wakati Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond
yamebaki nasi Duniani, ingawa nachelea kusema
Mushi akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru, kwenye vi-
zidumu fikra za Mwenyekiti, lakini kwa muda huu
wanja vya shule ya msingi Msimbazi, Kiongozi wa
nitasema kivuli cha Mwalimu bado kinaishi nasi.
Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Juma
Ali Simai, alianza kwa kusifu mapokezi makubwa
Ni zaidi ya miaka 50 sasa, tangu Mwenge wa Uhu-
waliyoyapata, huku akijiaminisha kwa kuwasifu pia
ru uwashwe kwa mara ya kwanza, mbio za Mwenge
viongozi na watendaji wa Manispaa ya Ilala, Waswa-
wa Uhuru hufanyika kila mwaka katika maeneo
hi wanamsemo wao usemao nyota njema huoneka-
mbalimbali nchini, mbio hizi huanza eneo moja na
na asubuhi ama kwa hakika nyota ya Ilala ilianza
kupokelewa katika maeneo mengine, huku zikihama-
kungara tangu Mwenge ulipowasili viwanja vya
sisha ushiriki katika miradi ya maendeleo pamoja na
mapokezi ya Mwenge, shule ya msingi Msimbazi.
kuhamasisha amani na umoja.
Katika Halmashauri ambayo ni kioo cha Halmashau-
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, imekuwa mstari
ri nyingine nchini Tanzania, au mfano wa kuigwa
wa mbele katika kufanikisha mbio za Mwenge wa
na Halmashauri nyingine, utahitaji viongozi wenye
Uhuru kila mwaka, huku ikijitahidi kujihakikishia
haiba
kua kinara wa mbio hizo kwa Manispaa nyengine Inaendelea Uk. 30
Sauti ya Ilala
26 MAKALA

Vivutio vilivyo Ma

1 Ikulu ya Rais
2 Soko la samaki feri

3 Mwl Julius. Nyerere


International Airport
4 Bustani ya Posta

5 Bandari ya Dar es Salaam Maktaba kuuu Ya Taifa 6

Sauti ya Ilala
MAKALA 27
Manispaa ya llala

7 Hyatt Regency Dar es Salaam

Dar es Salaam Serena Hotel 8

9 Mwenge wa Uhuru 10
Sanamu ya mpiga ngoma

11 12
Benki Kuu Soko la Kariakoo

Sauti ya Ilala
28 MAKALA
Mwenge wa Uhuru Dira ya...
Kutoka Uk.27
Shilingi 264,362,893
na mvuto wa kiuongozi kama Mheshimiwa Mstahiki
Ujenzi wa zahanati Kipawa, iliyopo Kata ya Kipawa,
Meya wa Ilala, Jerry Silaa na Mkurugenzi wa Manis-
wenye thamani ya Shilingi 139,637,000
paa ya Ilala, Bwana Maganga katika kuibua, kuisimamia
na kuiendeleza miradi
ya kimaendeleo kwa
Wananchi wa Ilala.

Utayari na kujitolea ac-


countability and com-
mitiment ndiyo nguzo
muhimu za msingi wa
maendeleo ya Manis-
paa ya Ilala, Viongozi
na Watendaji wame-
kuwa chachu katika
kugundua miradi ya ki-
maendeleo, kuisimamia
na kuitekeleza katika
wakati muafaka, na hii
ndiyo tofauti ya huku
kwetu Ilala na Man-
ispaa nyengine katika
utendaji, ingawa Wa-
toto wa Mjini husema Maabara ya Shule ya Sekondari Msimbazi, iliyozinduliwa na mbio za Mwenge
kua namba moja kwa wa Uhuru. (Picha na Michael Noel)
muda inawezekana, la-
kini kuwa namba moja
siku zote haiwezekani, sisi tunaamini Ilala itaendelea
Ujenzi wa barabara ya lami Kinyerezi, yenye urefu
kua namba moja siku zote, tunajivunia kufanya kazi na
wa kilomita 1.2, Kata ya Kinyerezi, wenye thamani ya
viongozi wawajibikaji, na Ilala imezaliwa kushinda siku
Shilingi 460,000,000
zote, na kwa nini tusishinde?
Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata, Kata ya
Kivule, wenye thamani ya Shilingi 110,870,204
Mwenge wa Uhuru, ulikimbizwa katika maeneo tisa
Usafishaji wa mazingira, Kata ya Gongo la Mboto,
yenye miradi ya kimaendeleo, iliyosimamiwa na Man-
wenye thamani ya Shilingi 50,000,000
ispaa ya Ilala, huku ikigharimu jumla ya Shilingi
Uelimishaji Rika juu ya Ukimwi, Dawa za kulevya
1,203,929,097.
na Mazingira, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
Kitaifa Bw. Ally Sumai alizindua vikundi viwili vilivy-
Miradi ya kimaendeleo, iliyosimamiwa na Manispaa na
opo Vingunguti, kimoja kinachotoa Elimu ya Mad-
kupitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru, ilikuwa ni ya
hara ya Ukimwi cha IDINEPHA VICOBA, thamani ya
kimaendeleo ya kijamii, nayo ni kama ifuatavyo:
Shilingi 28,000,000, na kikundi cha pili ni Vingunguti
Ujenzi wa Maabara shule ya Sekondari Msimbazi,
Youth, kinachojihusisha na Uelimishaji Rika na Madhara
wenye thamani ya Shilingi 58,900,000
ya Utumiaji wa dawa za kulevya, thamani ya Shilingi
Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Walimu Shule ya Msingi
15,000,000
Mzambarauni, iliyopo Kata ya Ukonga, wenye thamani
ya Shilingi 34,900,000
Mwenge wa Uhuru ulikesha katika viwanja vya shule
Ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi Zimbili,
ya msingi Majani ya Chai, huku vikundi vya burudani
iliyopo Kata ya Kinyerezi, wenye thamani ya Shilingi
ya muziki na uchekeshaji vikitumbuiza.
42,259,000
Mungu Ibariki Ilala yetu, Mungu wabariki viongozi
Ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari
wetu, Mungu ibariki nchi yetu.
Migombani, iliyopo Kata ya Segerea, wenye thamani ya

Sauti ya Ilala
MAKALA 29
Ilala na harakati za kuboresha, kukuza uvuvi
wa aina zote kuanzia wadogo.
Afisa uvuvi wa Manispaa ya Il-
ala Bw Msongo Songoro anasema,
Wapo wavuvi wachache wanaoji-
husisha na aina hii ya uvuvi ambapo
wanaopatikana na kosa adhabu kali
huchukuliwa dhidi yao ikiwa ni
pamoja na faini na kunyanganywa
kabisa leseni ya uvuvi

Hata hivyo Bw. Songoro anase-


ma wanakabiliwa na changamoto
kubwa katika kukabiliana na hili
tatizo kutokana na kuwa wapo wa-
vuvi wanaotoka nje ya Manispaa
ya Ilala kutokana na kuwa Bahari
ya Hindi inamilikiwa na Wilaya zi-
Afisa Uvuvi Manispaa ya Ilala Bw. Msongo Songoro (wa pili kusho- patazo 16 ambapo ndani ya bahari
to) akipata maelekezo ya kiutendaji toka kwa timu yake ya Sensa ya hakuna mipaka inayotenganisha
Uvuvi. (Picha na David Langa) Wilaya moja na nyingine hivyo
inakuwa vigumu kuwadhibiti
ya kitakwimu Idara ya uvuvi ka- kutokana na wahusika kukimbia
Na David Langa tika manispaa ya Ilala inatarajia na kurudi kwenye Wilaya zao.

W ilaya ya Ilala ni miongoni


mwa wilaya 16 za Ukanda
wa pwani. Katika sensa ya uvuvi
kujua idadi kamili ya wavuvi ka-
tika eneo lote la utawala linalomi-
likiwa na Manispaa, aina ya zana
Bw. Songoro anasema kuwa
wameanzisha ushirikiano na Wilaya
za karibu kama vile Temeke, Kilwa,
ya mwaka 2009 Wilaya ya Ilala za uvuvi zinazotumika kama vile Kinondoni, Bagamoyo na Pan-
ilikuwa na Mwalo mmoja, vyombo boti, nyavu na ndoano zinazotumi- gani lengo kuu likiwa ni kudhibiti
vya uvuvi vipatavyo 222, Wavuvi wa na wavuvi wetu ili kuweza ku- uvuvi haramu ambao ni hatari kwa
1,331, na zana za uvuvi 1,570. baini ufanisi wa zana hizo, changa- maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo, Sensa ya uvuvi moto pamoja na faida na hasara Bw. Songoro alisema kuwa, wa-
iliyoanza rasmi tarehe 15 Sep- zinazowakumba wavuvi katika takapokamilisha Sensa hii itakuwa
temba mwaka huu inatarajiwa ukanda huu wa Bahari ya Hindi. ni rahisi kwao kujua changamoto
kutoa picha halisi ya hali ya Kwa siku za hivi karibuni kume- mbali mbali zinazowakabili wavu-
uvuvi na wavuvi katika ukanda kuwepo na tetesi na malalamiko vi na sekta ya uvuvi kwa ujumla ili
wa pwani mwa Bahari ya Hindi. ya wadau wa uvuvi ya kuwepo kupanga namna ya kuwahudumia
Sensa hii inafanywa na watumishi baadhi ya wavuvi wanaojihusi- na kuwapatia ulinzi wa kutosha
wa idara ya uvuvi katika Manispaa sha na uvuvi haramu ambao una- pale wanapokabiliana na mazingira
ya Ilala kwa kushirikiana na Wiz- hatarisha mazingira yote ya uvuvi magumu katika maeneo yao ya kazi.
ara ya Mifugo na Uvuvi ambapo kuanzia kwa wavuvi, wafanyabi- Katika kufanikisha hili, wanawa-
Sensa ya mwisho ilifanywa miaka ashara wa Samaki na walaji pia. shirikisha wavuvi wenyewe ili kila
minne iliyopita hivyo inatarajiwa Uvuvi haramu unahusisha ma- mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake
kuwepo na mabadiliko makubwa tumizi ya mabomu katika uvuvi, na pia kutoa taarifa pale wanapoona
ya kitakwimu kutokana na baadhi sumu ya kuua samaki ndani ya ba- mazingira hatarishi ndani ya bahari.
ya wavuvi kuhamia Wilaya ya Il- hari na zana zilizopigwa marufuku Ilala ni eneo linalopakana na
ala, kuingizwa kwa vyombo vipya kama vile Kokoro (nyavu yenye Bahari ya Hindi hivyo kuwa
vya uvuvi au kuharibika kwa baa- tundu ndogo ndogo) ambayo si sehemu muhimu katika sek-
dhi ya vyombo na zana za uvuvi. rafiki katika mzingira ya uvuvi ta ya uvuvi nchini na hasa ku-
Katika kufanikisha Sensa hii kutokana na kukamata samaki wepo kwa soko la samaki Feri.
Sauti ya Ilala
30 MAKALA
Mama Salma Kikwete aongoza
matembezi ya kuchangia madawati
Silaa: Dawati ni Elimu
Lengo: kuhamasisha jamii kuhusu tatizo la madawati na hivyo jamii kuguswa
kwa kushiriki kumaliza changamoto ya madawati.
Na Lucy Semindu elimu ili iweze kuleta mafaniko chanya changamoto

M adawati ni nyenzo muhimu sana katika kufanik- ya madawati haina budi kutatuliwa na hivyo kusaidia
isha maendeleo ya sekta ya elimu nchini kwani kuleta mazingira bora elimu na kuinua kiwango cha
wanafunzi wanapokalia madawati hujenga mazingira elimu kwa wanafunzi wa Halmashauri ya Manispaa
bora ya kusoma hivyo huwawezesha kufuatilia vyema ya Ilala.
masomo na kupelekea kuwa na matokeo mazuri dar-
asani. Hii inaiwezesha nchi yeyote kupata rasilimali Dawati ni Elimu ni mpango ulioanzishwa na kubu-
watu watakaochangia kwa kiasi kikubwa maendeleo niwa na Mhe. Jerry Silaa kupitia Mayors Ball am-
ya nchi. bapo Meya hukutana na wadau mbalimbali kujadili
maendeleo ya Halmashauri ya Ilala na namna wadau
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala hao wanaweza kuchangia kuchochea miradi mbalim-
Mhe. Jerry Silaa ni miongoni mwa viongozi nchini bali ya maendeleo ikiwemo ya sekta ya elimu.
Tanzania wenye mtazamo chanya wa kufanikisha
maendeleo ya nchi yetu kupitia sekta mbalimbali Matembezi ya kuhamasisha jamii kuchangia kwa ajili
ikiwemo sekta ya Elimu. ya madawati yalifanyika hivi karibuni ambapo Mgeni
Kwa upande wake Mhe. Jerry Silaa ameona sekta ya rasmi alikuwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Inaendelea Uk. 35

Mama Salma Kikwete (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Meya wa Manispaa ya Ilala
Mh. Jerry Silaa wakiwa katika katika matembezi ya kuhamasisha Dawati ni Elimu. (Picha na David Langa)

Sauti ya Ilala
MAKALA 31
BRN kuiwezesha Ilala kuongeza mapato ya ardhi, majengo
Kutoka Uk. 26 ia mjadala huo walilalamika juu ya ushirikishwaji
hafifu wa wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mi-
Wakieleza njia za ulipaji kodi hiyo, Pascal Ka- taa na kudai kuwa wao ndiyo wanawafahamu wa-
bunduguru na George Haule kutoka Mamlaka ya miliki wa ardhi na majengo kwenye maeneo husika.
Mapato Tanzania (TRA), wameelezea kuwa hu-
fanyika kupitia Benki, M-PESA, Airtel Money, na Akisoma maazimio hayo, Mohamed S. Mwar-
NMB Mobile, na kuongeza kuwa majukumu ya izo kutoka Sekretarieti ya Manispaa ya Ilala,
TRA ni kutathimini, kukadiria, kukusanya pamo- amesema kuwa wajumbe wote wameafiki maaz-
ja na kutoa na kusambaza hati za madai (Bills). imio manne na kuyataja kuwa, Mosi, Suala
Kazi nyingine ni kuhasibu kodi ya majengo na ku- la kutambua na kubainisha majengo yanayo-
toa namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN). paswa kulipiwa kodi yafanywe kwa kushirikisha
ngazi ya mtaa, Pili, Halmashauri ya Manispaa
Fedha hizo hutumika kuipatia Serikali mapato, na TRA wakae kwa pamoja kuweza kupata ul-
kulinda viwanda vidogo vidogo vya ndani ya nchi, inganifu wa taarifa za walipa kodi za majengo.
kufanya mgawanyo sawa wa mapato, kuzuia ma-
tumizi ya bidhaa hatarishi ikiwa na kufanikisha Tatu, Halmashauri iandae taarifa ya kina kuhusu
kujenga miradi ambayo inachochea maendeleo leseni za makazi, na Wathamini wa Manispaa
kama barabara, umeme n.k alielezea Haule. waandae taarifa ya kina na iwasilishwe tena
katika ngazi zote. Hatua hii inachukuliwa kwa
Katika mafunzo hayo, wajumbe wengi waliochang- lengo la kuzijengea uwezo Serikali za Mitaa.

Baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kikao cha Baraza hilo kilichozinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera,
(Kulia) Ndg. Mwendahasara Maganga ( Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala )(Picha na Lucy Semindu)

Sauti ya Ilala
32 MAKALA
Manispaa yakamilisha usajili wa Katiba ya michezo
Na Kassim Nyaki
undwa Manispaa za Ilala, Kinondoni na Te-

O fisi ya Michezo na Utamaduni katika Halmashau- meke kila Halmashauri ilianza kujitegemea.
ri ya Manispaa ya Ilala imekamilisha mchakato
wa kuandaa na kusajili katiba yao ikiwa ni katika har- Kwa mujibu wa Bw. Mpelembwa wadhamini wa
akati za kutekeleza agizo la serikali juu ya ushiriki wa michezo ya Manispaa ya Ilala watakuwa ni Mkuruge-
michezo kwa watumishi mahala pa kazi pamoja na zi, Afisa Utumishi mkuu pamoja na Mweka Hazina
ile ya mashindano ya mamlaka ya wakishirikiana na ofisi yao
serikali za mitaa (SHIMISEMITA) Tayari tupo katika hatua ikiwa ni katika hatua ya
nzuri, uundwaji wa kati- kuongeza msukumo juu ya
Akizungumza na Sauti ya Ilala Afisa utekelezaji wa programu ya
Utamaduni wa Manispaa hiyo Bw. ba ya michezo ya manis- michezo kwa kila mwaka.
Claud Mpelembwa alieleza kuwa paa yetu umekamilika na Pamoja na kuwashiriki-
ofisi yao imeshakamilisha usajili sha watendaji hawa wakuu
wa Katiba ya michezo kwa Man-
tunamshukuru Mkurugenzi pia tutawaomba Wakuu
ispaa hiyo ili kuhakikisha michezo wetu kutuunga mkono kati- wa Idara waunge mkono
mbalimbali inaanzishwa kuanzia ka utekelezaji wa agizo hili, juhudi hizi kwa kutenga
mwakani ikiwa ni hatua za utekele- bajeti ya michezo kwa timu
zaji wa maagizo ya Baraza la
Michezo la Taifa (BMT) juu ya
uundwaji wa vilabu na agizo
lililotolewa na serikali kuu-
fanya michezo na ushiriki wa
mamlaka za Serikali za Mitaa.

Tayari tupo katika hatua nzuri,


uundwaji wa Katiba ya mich-
ezo ya Manispaa yetu umeka-
milika na tunamshukuru Mku-
rugenzi wetu kutuunga mkono
katika utekelezaji wa agizo hili,
tunaamini kuanzia mwakani
Manispaa ya Ilala kupitia Idara
zake itaanza kushiriki michezo
mbalimbali hali itakayosaidia
kujenga uhusiano baina ya
wafanyakazi na kujenga afya
zao, alifafanua Mpelembwa. Kiwanja cha michezo cha Karume
zao ili tu-
Aliongeza kuwa baada ya kukamilisha uundwaji wa weze kuzind-
Katiba ya klabu ya Halmashauri hiyo hatua itakayofua- ua mashindano ndani ya Manispaa na
ta ni uundwaji wa uongozi wa klabu hiyo utakaoweze- tunaamini hali hii italeta hamasa hata kwa watu-
sha kuratibu shughuli mbalimbali za michezo ndani mishi wenyewe na kuiletea sifa Halmashauri yetu
ya Halmashauri pamoja na mashindano ya mamlaka
ya Serikali za Mitaa ambayo hufanyika kila mwaka. Aidha, Afisa Utamaduni huyo amebainisha kuwa baada
ya mipango yote kukamilika ofisi yao iko mbioni kupeleka
Kabla ya kuandaa katiba kwa vilabu katika ombi rasmi kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ilikuona
Manispaa jijini Dar es salaam, Jiji hilo li- uwezekano wa kuwa na timu ya Madiwani kama mhimi-
likuwa likiundwa na timu moja iliyojulikana li muhimu ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
kama Jiji Sport club ambapo baada ya ku-

Sauti ya Ilala

You might also like