Taarifa - Wanafunzi 2348 Washinda Rufaa Za Mikopo Ya Heslb

You might also like

Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 1

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA

JUU

WANAFUNZI 2,348 WASHINDA KATIKA RUFAA ZAO ZA MIKOPO


YA ELIMU YA JUU

1.0 UTANGULIZI

Taratibu za upangaji na utoaji mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,zinatoa


fursa kwa waombaji ambao ama hawakupata mikopo au wamepata kiwango
cha mikopo wanachoona hakikidhi mahitaji, kukata rufaa. Kwa mujibu wa
taratibu zilizopo, waombaji hupewa siku tisini (90) kuanzia mwanzo wa
mwaka wa masomo kuwasilisha rufaa zao. Rufaa hizo huwasilishwa kwa njia
ya mtandao na vielelezo/viambatisho huwasilishwa kupitia madawati maalum
ya mikopo vyuoni. Katika mwaka wa masomo 2016/17, zoezi la kupokea
rufaa lilianza rasmi tarehe 1 Novemba, 2016 na kuhitimishwa tarehe 31
Januari, 2017.

2.0 MATOKEO YA RUFAA

Katika kipindi cha kati ya tarehe 1 Novemba, 2016 na 31 Januari, 2017 jumla
ya rufaa 20,020 ziliwasilishwa kwa njia ya mtandao. Kati ya hizo, jumla ya
fomu za rufaa 17,020 zilipokelewa kutoka vyuoni zikiwa na viambatisho
muhimu. Mapitio ya rufaa zilizowasilishwa yalifanywa kwa fomu zote
zilizopokelewa na matokeo ya rufaa hizo (zilizoshinda) kwa makundi ni kama
ifuatavyo: Walemavu 61; Yatima 57; Wenye mzazi mmoja 570; Familia zenye
kipato duni 1,169 na Waliosomeshwa na wahisani 491.

3.0 HITIMISHO

Bodi ya Mikopo tayari imetuma vyuoni majina ya wanafunzi walioshinda rufaa


zao na inaendelea kukamilisha malipo ya mikopo yao. Aidha, Bodi inapenda
kuwataarifu waombaji na umma kwa ujumla kuwa zoezi hili limefungwa rasmi
hadi hapo litakapotangazwa tena katika mwaka ujao wa masomo.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
28 Februari, 2017

You might also like