Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 7

Madhara yatokanayo na ajali za barabarani

yamemeendelea kuwa sababu namba tisa katika


kusababisha vifo vya watu wengi zaidi duniani ambapo
inakadiriwa zaidi ya watu milioni 1.24 hufa kila mwaka
kutokana na ajali za barabarani.Wakati huo huo watu
zaidi ya milioni 50 wamebaki na majeraha makubwa na
aidha ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizi kwa
mwaka.

Wakati nchi za uchumi au kipato cha chini na cha kati


hasa zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara zimeendelea
kuchangia nusu ya idadi ya vifo milioni 1.24 kwa mwaka
ilhali nchi hizi zina namba ndogo zaidi ya vyombo vya
moto vya usafiri vilivyosajiwa.

Mwaka huu tarehe 8 hadi 14 Mei Watanzaia kama


sehemu ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa
tunaendelea kushuhudia maadhimisho ya nne ya wiki ya
usalama barabarani ambapo kauli mbiu ni udhibiti wa
mwendo kasi kwa vyombo vya vya usafiri.Tafiti
zimeendelea kuonesha kuwa mwendo kasi umechangia
zaidi ya moja ya tatu ya ajali za barabarani katika nchi
tajiri, na hadi nusu ya ajali katika nchi za kipato cha
chini na cha kati ambapo madhara yaliyotokana na ajali
ambazo sababu zilikuwa ni mwendokasi ni vifo.

Katika kupambana na kidhibiti mwendokasi Umoja wa


Mataifa umeendelea kushauri nchi wanachama kuweka
mikakati katika kujenga au kuimarisha miundo mbinu
ya barabara ikiwa ni pamoja na samani za barabara
zenye kupunguza mwendo kasi kadri inavyofaa
kulingana na aina za barabara, kudhibiti mwendo kasi
kulingana na barabara husika, kuweka usimamizi
madhubuti wa sheria za barabarani zinazohusu
mwendokasi, kuweka vifaa vya kisasa vya kudhibiti
mwendo katika magari na kuendelea kutoa elimu kwa
watumiaji wa barabara juu ya athari za mwendokasi.

Aidha juhudi za Umoja wa mataifa kukabiliana na tatizo


la ajali za barabarani na madhara yatokanoayo na ajali
zimekuwepo kwa miongo kadhaa sasa, lakini tunaweza
kuziona juhudi za maksudi tangu mwaka 2011 ambapo
Umoja wa Mataifa kwa mamlaka ya Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa ulipitisha azimio la Mpango wa Muongo
mmjoja 2011-2020 (Decade of Action) katika kuokoa
maisha ya watu milioni tano kutokana na vifo vya ajali
na aidha kuzuia majeraha kwa zaidi ya watu milioni
hamsini, kwa kifupi mpango huu ulijielekeza katika
kupunguza angalau nusu na vifo na majeraha
yatoakanayo na ajali za barabarani katika kipinidi cha
muongo mmoja yaani 2011 hadi 2020.

Mpango huu ulitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa


kuchukua hatua juu ya usiamamizi wa ajenda ya
usalama barabarani, usalama wa barabara na
uchukuzi ,usalama wa vyombo vya moto, usalama wa
watumiaji wa barabara na huduma stahiki kwa majeruhi
wa ajali za barabarani.

Kadhalika katika Mpango wa malengo ya maendeleo


endelevu (Sustainable Development Goals) nchi
wanachama wa Umoja wa Matiafa wameendelea
kujiwekea mipango mikakati na viashiria katika
kutengeneza ajenda na sera za kipaumbele katika
miaka kumi na mitano ijayo yaani 2015 hadi
2030.Mpango wa Maendeleo endelevu umejiendeleza
kutokana na Mpango wa Maendeleo wa Milenia ambao
nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walijiwekea
mwaka 2000 kulelekea 2015.

Katika Mpango wa Malengo ya Maendeleo endelevu


swala la usalama barabarani limeendelea kujitokeza
kama ajenda ya peke yake katika lengo namba tatu
linallojielekekeza katika kuhakikisha kukua kwa ustawi
na ubora wa afya na maisha kwa watu wa rika zote
ambapo katika moja ya malengo mahsusi chini ya lengo
kuu ni kupunguza nusu ya idadi ya vifo na na majeruhi
watokanao na ajali za barabarani.Hivyo madhara ya
ajali za barabarani yamepata kipaumbele sawa na
vipaumbele vingine kama kupunguza vifo vya mama
wajawazito na watoto pamoja na UKIMWI.

Aidha lengo namba kumi na moja katika Mpango wa


Malengo ya Maenedeleo Endelevu ni kuwa na miji na
makazi salama.Lengo mahsusi likiwa kufikia 2030
kuhakikisha upatikanaji wa usafiri na mifumo ya usafiri
salama, hasa katika kuimarisha usafiri wa umma na
kutoa kipaumbele kwa makundi maalum na watu walio
na mahitaji maalum wakiwemo wazee, watu wenye
ulemavu, watoto na wanawake.

Katika maadhimisho haya Tanzania kama sehemu ya


Jumuiya ya Kimataifa tuanayo fursa ya kutathimini juhudi
zetu katika kukabiliana na ajali za barabarani pamoja na
madhara yake.Aidha kutathimini juhudi na hatua amabazo
kama Taifa tumechukua na ikiwa zimashabihiana na
maazimio ya Kimataifa ambapo na sisi kama sehemu ya
maazimio hayo tuanyo sababu na wajibu wa kujitathimini .

Katika kipindi cha mwaka 2016 Jeshi la Polisi limeripoti


vifo 3256 na majeruhi 8958.Katika ajali zilizopelekea vifo
na majeruhi vyombo vya usafiri binafsi na pikipiki
vimechukua asilimia 48% ya ajali zote ukilinganisha na
vyombo vingine ambavyo ni magari ya abiria,baiskeli na
magari ya mizigo.

Unapolinganisha takwimu hizi na zile za mwaka 2013


ambapo vifo vilikuwa 4002 na mwaka 2014 vifo vilikuwa
3760 aidha majeruhi mwaka 2013 walikuwa 20,689 na
2014 majeruhi 14530 utaona kumekuwepo na kupungua
kwa kiasi ajali za barabaani na madhara yalipolekea vifo
au majeruhi.Hizi ni takwimu za Jeshi la Polisi kitengo cha
Usalama barabarani.

Aidha tumeendelea kushuhudia mikakati mabalimbali ya


Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani chini ya
maongozi mazuri ya Baraza la Taifa la Usalama Barabarani
katika kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua kwa
kiasi kikubwa au kutokomezwa kabisa.Wadau mabalimbali
zikiwemo asasi za kiraia nazo zimeendelea kutoa mchango
mkubwa wa elimu kwa watumiaji wa barabara na
kushawishi marejeo ya sheria na sera za usalama
barabarani katika kuziwezesha kukabiliana na
changamoto hii iliyoendelea kugharimu uhai wa
Watanzania wengi.Chama cha Wanawake Wanasheria
Tanzania (TAWLA) kwa kushirikiana na wadau wengine
ikiwemo Chama cha Wanasheria wa Tanganyika(TLS),
Chama cha Waandishi wa Habari wanawake (TAWMA),
Jukwaa la haki za mtoto (TCRF), Mabalozi wa Usalama
Barabarani (RSA),Chama cha wenye ulemavu
(SHIVYAWATA), Safe Speed foundation, Kituo cha Msaada
wa Sheria kwa Wanwake (WLAC),Chama cha Wamiliki wa
Mabasi pamoja na watu binafsi walio na uzoefu na nia
njema juu ya agenda ya usalama barabarani wameendelea
kwa pamoja kushawishi mabadiliko ya sheria na sera ya
Usalama barabarani, ili kushabihiana na sheria nyingine
zinazohusiana na usafirishaji pia kukabilina na mianya
katika sheria ambayo kwa kiasi kikubwa imeendela kuwa
sababu ya ajali ya barabarani.

Kadhalika tumeendelea kuona juhudi za serikali katika


kuboresha miundombinu ya barabara na njia nyinginezo
za uchukuzi ambazo mwitikio wake utakuwa ni katika
kuwa na usafirishaji salama wa watu na mali zao.Ujenzi
wa barabara maalumu kwa ajili ya mabasi yaendayo
haraka katika jiji la Dar es Salaam na moja ya hatua
stahiki katika kuhakikisha tunakuwa na usafirishaji
salama.Hii ni kwa sababu aina ya barabara hii maalumu
inapunguza kwa kiasi kikubwa uwezekeno wa ajali
kutokana na kutoingiliana na vyombo vingine vya usafiri
barabarabani.

Pamoja na mafanikio haya ni muhimu bado kujielekeza


katika tathmini ya mipango ya jumuiya ya Kimataifa hasa
tukizingatia bado kama Taifa tumeendelea kushuhudia
maisha yakipotea kwa ajali za barabarani , ulemavu wa
kudumu ukitesa wengi, pato kubwa la Tiafa katika sekta
ya afya likijilelekeza katika kukabililiana na madhara
yatokanayo na ajali.

Mpango wa muongo mmoja wa Umoja wa Mataifa ulizitaka


nchi wananachama wa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua
juu ya usiamamizi wa ajenda ya usalama barabarani,
usalama wa barabara na uchukuzi ,usalama wa vyombo
vya moto, usalama wa watumiaji wa barabara na huduma
stahiki kwa majeruhi wa ajali za barabarani.

Juhudi zinazoendelea zinaweza kuzaa matunda zaidi ikiwa


kama Taifa tutakuwa na usimamizi endelevu wa ajenda ya
usalama barabarani unaotilia maanani mbinu ya
kuhusisha wadau wote, kuimarisha sheria husika na
utekeklezaji wa sheria kulingana na wakati wa dunia ya
leo , kuboresha huduma za majeruhi wa ajali na tiba ya
mwili baada ya ajali.

Kama kauli mbiu ya maadhimisho haya mwaka huu kama


nchi eneo la kudhibiti mwendokasi ndani ya sheria, katika
usimamizi wa sheria na miundombinu bado tuna kazi ya
kufanya.Takwimu za Jeshi la Polisi za mwaka 2016
zinaonesha vyombo vya usafiri binafsi na pikipiki
vimechangia asilimia 48% ya ajali za barabarani. Ni vizuri
kufahamu kuwa magari binafsi yameendelela kusimamiwa
na Sheria ya Usalama Barabarani yaani The Road Traffic
Act, Cap 168 [R.E.2002] Sheria hii imeendelea kwa kiasi
fulani kuruhusu mwendo usio na kikiomo katika maeneo
yasiyo na makazi wala vibao vya kulelekeza mwendo na
katika mazingira haya magari binafsi yameendlea kujikuta
kuingia katika ajali. Kadhalika hata maeneo ambayo vibao
vianelekeza kiwango cha mwendo kasi bado katika saa
ambazo askari wa usalama barabarani hawapo barabarani
madereva wameendelea kuvunja sheria ilhali mhanga wa
kwanaza wa madhara ya ajali hizi ni wale waliomo katika
chombo husika.

Madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda pamoja na


juhudi kadhaa za kuwaelimisha na kuwasimamia
wameendelea kuendesha vyombo hivi kwa mwendo mkali
na pasipo kuzingatia alama za barabarani na hata taa za
barabarani.Sheria tajwa pia imeendela kuwa na
mapungufu kadhaa juu ya usimamizi wa mwedo kasi na
maeneo mengine mengine katika usimamizi wa pikipiki au
bodaboda.

Ni wakati sahihi sasa kwa Serikali yetu kujumuisha juhudi


za kupunguza ajali au kuziondoa kwa kurekebisha mianya
iliyopo katika sheria mama ya Usalama barabarani ili
ishabihiane na sheria nyingine zianazosimamia usafirishaji
kwa njia ya barabara nchini.Aidha ni wakati sahihi sasa wa
Taifa kuwa na mpango utakaoshughulikia usimamizi
endelevu wa ajenda ya usalama barabarani, kuangalia
ubora wa vyombo vya usafirishaji vinavyoingizwa nchini,
kujumuisha elimu ya utumiaji salama wa barabara katika
mitaala yetu ya elimu na kuhakikisha usanifu na ujenzi wa
miundombinu yetu inazingatia ujenzi wa miundo mbinu
salama kwa rika zote kulingana na maeneo husika.

You might also like