Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

MAKALA

By Mary Richard (Advocate)

Tanzania Women Lawyers Association

MAADHIMISHO YA NNE YA UMOJA WA MATAIFA KWA WIKI YA


USALAMA BARABARANI (UN ROAD SAFETY WEEK)

Madhara yatokanayo na ajali za barabarani yamemeendelea kuwa sababu


namba tisa katika kusababisha vifo vya watu wengi zaidi duniani ambapo
inakadiriwa zaidi ya watu milioni 1.24 hufa kila mwaka kutokana na ajali
za barabarani.Wakati huo huo watu zaidi ya milioni 50 wamebaki na
majeraha makubwa na aidha ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizi
kwa mwaka.

Wakati nchi za uchumi au kipato cha chini na cha kati hasa zilizopo kusini
mwa jangwa la Sahara zimeendelea kuchangia nusu ya idadi ya vifo
milioni 1.24 kwa mwaka ilhali nchi hizi zina namba ndogo zaidi ya vyombo
vya moto vya usafiri vilivyosajiwa.

Mwaka huu tarehe 8 hadi 14 Mei Watanzaia kama sehemu ya nchi


wanachama wa Umoja wa Mataifa tunaendelea kushuhudia maadhimisho
ya nne ya wiki ya usalama barabarani ambapo kauli mbiu ni udhibiti wa
mwendo kasi kwa vyombo vya vya usafiri.Tafiti zimeendelea kuonesha
kuwa mwendo kasi umechangia zaidi ya moja ya tatu ya ajali za
barabarani katika nchi tajiri, na hadi nusu ya ajali katika nchi za kipato
cha chini na cha kati ambapo madhara yaliyotokana na ajali ambazo
sababu zilikuwa ni mwendokasi ni vifo.

Katika kupambana na kidhibiti mwendokasi Umoja wa Mataifa


umeendelea kushauri nchi wanachama kuweka mikakati katika kujenga
au kuimarisha miundo mbinu ya barabara ikiwa ni pamoja na samani za
barabara zenye kupunguza mwendo kasi kadri inavyofaa kulingana na
aina za barabara, kudhibiti mwendo kasi kulingana na barabara husika,
kuweka usimamizi madhubuti wa sheria za barabarani zinazohusu
mwendokasi, kuweka vifaa vya kisasa vya kudhibiti mwendo katika
magari na kuendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara juu ya
athari za mwendokasi.

Aidha juhudi za Umoja wa mataifa kukabiliana na tatizo la ajali za


barabarani na madhara yatokanoayo na ajali zimekuwepo kwa miongo
kadhaa sasa, lakini tunaweza kuziona juhudi za maksudi tangu mwaka
2011 ambapo Umoja wa Mataifa kwa mamlaka ya Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa ulipitisha azimio la Mpango wa Muongo mmjoja 2011-2020
(Decade of Action) katika kuokoa maisha ya watu milioni tano kutokana na
vifo vya ajali na aidha kuzuia majeraha kwa zaidi ya watu milioni hamsini,
kwa kifupi mpango huu ulijielekeza katika kupunguza angalau nusu na
vifo na majeraha yatoakanayo na ajali za barabarani katika kipinidi cha
muongo mmoja yaani 2011 hadi 2020.

Mpango huu ulitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua juu ya
usiamamizi wa ajenda ya usalama barabarani, usalama wa barabara na
uchukuzi ,usalama wa vyombo vya moto, usalama wa watumiaji wa
barabara na huduma stahiki kwa majeruhi wa ajali za barabarani.

Kadhalika katika Mpango wa malengo ya maendeleo endelevu


(Sustainable Development Goals) nchi wanachama wa Umoja wa Matiafa
wameendelea kujiwekea mipango mikakati na viashiria katika
kutengeneza ajenda na sera za kipaumbele katika miaka kumi na mitano
ijayo yaani 2015 hadi 2030.Mpango wa Maendeleo endelevu
umejiendeleza kutokana na Mpango wa Maendeleo wa Milenia ambao nchi
wanachama wa Umoja wa Mataifa walijiwekea mwaka 2000 kulelekea
2015.
Katika Mpango wa Malengo ya Maendeleo endelevu swala la usalama
barabarani limeendelea kujitokeza kama ajenda ya peke yake katika lengo
namba tatu linallojielekekeza katika kuhakikisha kukua kwa ustawi na
ubora wa afya na maisha kwa watu wa rika zote ambapo katika moja ya
malengo mahsusi chini ya lengo kuu ni kupunguza nusu ya idadi ya vifo
na na majeruhi watokanao na ajali za barabarani.Hivyo madhara ya ajali
za barabarani yamepata kipaumbele sawa na vipaumbele vingine kama
kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto pamoja na UKIMWI.

Aidha lengo namba kumi na moja katika Mpango wa Malengo ya


Maenedeleo Endelevu ni kuwa na miji na makazi salama.Lengo mahsusi
likiwa kufikia 2030 kuhakikisha upatikanaji wa usafiri na mifumo ya usafiri
salama, hasa katika kuimarisha usafiri wa umma na kutoa kipaumbele
kwa makundi maalum na watu walio na mahitaji maalum wakiwemo
wazee, watu wenye ulemavu, watoto na wanawake.

Katika maadhimisho haya Tanzania kama sehemu ya Jumuiya ya Kimataifa


tuanayo fursa ya kutathimini juhudi zetu katika kukabiliana na ajali za
barabarani pamoja na madhara yake.Aidha kutathimini juhudi na hatua
amabazo kama Taifa tumechukua na ikiwa zimashabihiana na maazimio ya
Kimataifa ambapo na sisi kama sehemu ya maazimio hayo tuanyo sababu na
wajibu wa kujitathimini .

Katika kipindi cha mwaka 2016 Jeshi la Polisi limeripoti vifo 3256 na majeruhi
8958.Katika ajali zilizopelekea vifo na majeruhi vyombo vya usafiri binafsi na
pikipiki vimechukua asilimia 48% ya ajali zote ukilinganisha na vyombo
vingine ambavyo ni magari ya abiria,baiskeli na magari ya mizigo.

Unapolinganisha takwimu hizi na zile za mwaka 2013 ambapo vifo vilikuwa


4002 na mwaka 2014 vifo vilikuwa 3760 aidha majeruhi mwaka 2013
walikuwa 20,689 na 2014 majeruhi 14530 utaona kumekuwepo na
kupungua kwa kiasi ajali za barabaani na madhara yalipolekea vifo au
majeruhi.Hizi ni takwimu za Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani.

Aidha tumeendelea kushuhudia mikakati mabalimbali ya Jeshi la Polisi


kitengo cha Usalama Barabarani chini ya maongozi mazuri ya Baraza la Taifa
la Usalama Barabarani katika kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua
kwa kiasi kikubwa au kutokomezwa kabisa.Wadau mabalimbali zikiwemo
asasi za kiraia nazo zimeendelea kutoa mchango mkubwa wa elimu kwa
watumiaji wa barabara na kushawishi marejeo ya sheria na sera za usalama
barabarani katika kuziwezesha kukabiliana na changamoto hii iliyoendelea
kugharimu uhai wa Watanzania wengi.Chama cha Wanawake Wanasheria
Tanzania (TAWLA) kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Chama cha
Wanasheria wa Tanganyika(TLS), Chama cha Waandishi wa Habari wanawake
(TAWMA), Jukwaa la haki za mtoto (TCRF), Mabalozi wa Usalama Barabarani
(RSA),Chama cha wenye ulemavu (SHIVYAWATA), Safe Speed foundation,
Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanwake (WLAC),Chama cha Wamiliki wa
Mabasi pamoja na watu binafsi walio na uzoefu na nia njema juu ya agenda
ya usalama barabarani wameendelea kwa pamoja kushawishi mabadiliko ya
sheria na sera ya Usalama barabarani, ili kushabihiana na sheria nyingine
zinazohusiana na usafirishaji pia kukabilina na mianya katika sheria ambayo
kwa kiasi kikubwa imeendela kuwa sababu ya ajali ya barabarani.

Kadhalika tumeendelea kuona juhudi za serikali katika kuboresha


miundombinu ya barabara na njia nyinginezo za uchukuzi ambazo mwitikio
wake utakuwa ni katika kuwa na usafirishaji salama wa watu na mali
zao.Ujenzi wa barabara maalumu kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka katika
jiji la Dar es Salaam na moja ya hatua stahiki katika kuhakikisha tunakuwa na
usafirishaji salama.Hii ni kwa sababu aina ya barabara hii maalumu
inapunguza kwa kiasi kikubwa uwezekeno wa ajali kutokana na kutoingiliana
na vyombo vingine vya usafiri barabarabani.

Pamoja na mafanikio haya ni muhimu bado kujielekeza katika tathmini ya


mipango ya jumuiya ya Kimataifa hasa tukizingatia bado kama Taifa
tumeendelea kushuhudia maisha yakipotea kwa ajali za barabarani ,
ulemavu wa kudumu ukitesa wengi, pato kubwa la Tiafa katika sekta ya afya
likijilelekeza katika kukabililiana na madhara yatokanayo na ajali.

Mpango wa muongo mmoja wa Umoja wa Mataifa ulizitaka nchi


wananachama wa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua juu ya usiamamizi wa
ajenda ya usalama barabarani, usalama wa barabara na uchukuzi ,usalama
wa vyombo vya moto, usalama wa watumiaji wa barabara na huduma stahiki
kwa majeruhi wa ajali za barabarani.

Juhudi zinazoendelea zinaweza kuzaa matunda zaidi ikiwa kama Taifa


tutakuwa na usimamizi endelevu wa ajenda ya usalama barabarani unaotilia
maanani mbinu ya kuhusisha wadau wote, kuimarisha sheria husika na
utekeklezaji wa sheria kulingana na wakati wa dunia ya leo , kuboresha
huduma za majeruhi wa ajali na tiba ya mwili baada ya ajali.

Kama kauli mbiu ya maadhimisho haya mwaka huu kama nchi eneo la
kudhibiti mwendokasi ndani ya sheria, katika usimamizi wa sheria na
miundombinu bado tuna kazi ya kufanya.Takwimu za Jeshi la Polisi za mwaka
2016 zinaonesha vyombo vya usafiri binafsi na pikipiki vimechangia asilimia
48% ya ajali za barabarani. Ni vizuri kufahamu kuwa magari binafsi
yameendelela kusimamiwa na Sheria ya Usalama Barabarani yaani The Road
Traffic Act, Cap 168 [R.E.2002] Sheria hii imeendelea kwa kiasi fulani
kuruhusu mwendo usio na kikiomo katika maeneo yasiyo na makazi wala
vibao vya kulelekeza mwendo na katika mazingira haya magari binafsi
yameendlea kujikuta kuingia katika ajali. Kadhalika hata maeneo ambayo
vibao vianelekeza kiwango cha mwendo kasi bado katika saa ambazo askari
wa usalama barabarani hawapo barabarani madereva wameendelea kuvunja
sheria ilhali mhanga wa kwanaza wa madhara ya ajali hizi ni wale waliomo
katika chombo husika.

Madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda pamoja na juhudi kadhaa za


kuwaelimisha na kuwasimamia wameendelea kuendesha vyombo hivi kwa
mwendo mkali na pasipo kuzingatia alama za barabarani na hata taa za
barabarani.Sheria tajwa pia imeendela kuwa na mapungufu kadhaa juu ya
usimamizi wa mwedo kasi na maeneo mengine mengine katika usimamizi wa
pikipiki au bodaboda.

Ni wakati sahihi sasa kwa Serikali yetu kujumuisha juhudi za kupunguza ajali
au kuziondoa kwa kurekebisha mianya iliyopo katika sheria mama ya
Usalama barabarani ili ishabihiane na sheria nyingine zianazosimamia
usafirishaji kwa njia ya barabara nchini.Aidha ni wakati sahihi sasa wa Taifa
kuwa na mpango utakaoshughulikia usimamizi endelevu wa ajenda ya
usalama barabarani, kuangalia ubora wa vyombo vya usafirishaji
vinavyoingizwa nchini, kujumuisha elimu ya utumiaji salama wa barabara
katika mitaala yetu ya elimu na kuhakikisha usanifu na ujenzi wa
miundombinu yetu inazingatia ujenzi wa miundo mbinu salama kwa rika zote
kulingana na maeneo husika.

You might also like