Professional Documents
Culture Documents
Shilla
Shilla
AINA ZA ZANA
Katika uandaaji na utumiaji wa zana ,kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kama ifuatavyo;
Somo na mada, mwalimu anapaswa kuandaa zana zinazosadifu somo na mada husika , kwa
mfano; kama somo ni historia ,mwalimu anapaswa kuandaa zana kama vile ramani kutegemeana
na mada husika.Pia kama somo ni la Kiswahili katika mada ya aina za maneno,mwalimu
anaweza kuandaa chati inayoonesha aina za maneno.
Umri au kiwango cha elimu cha wanafunzi, mwalimu anapaswa kuandaa zana zinazoendana na
umri pamoja na kiwango cha elimu cha wanafunzi wake,kwa kufanya hivyo itawarahisishia
wanafunzi kuelewa mada husika kwa urahisi zaidi,pia itamsaidia mwalimu kufundisha kwa
wepesi zaidi.
Zana inapaswa ibebeke, mwalimu anapaswa atumie zana ambayo ni rahisi kubebeka na
kuhamishika ili iwe rahisi kwa wanafunzi kuiona kwa makini na kwa urahisi zaidi,kwani zana
isiyobebeka wala kuhamishika kwa urahisi inakua ni kikwazokikubwa kwa wanafunzi katika
kujifunza.Hivyo zana itakayo tumika inatakiwa iwe nyepesi na yenye kuhamishika kutoka
sehemu moja hadi sehemu nyingine.
Zana haipaswi kuwa inayotisha, mwalimu anatakiwa kuandaa zana isiyotisha hasa kwa
wanaojifunza.Baadhi ya zana hazipaswi kutumika kwa wanafunzi wenye umri mdogo kwani
zinaweza kuwaogopesha hata na kuwahamisha darasani kisaikolojia , kwa mfano ; matumizi ya
picha za wanyama wakali kama vile simba na nyoka.
Zana inatakiwa iwe yenye kuonekana, mwalimu anatakiwa atumie zana zinazoonekana ili
wanafunzi waweze kuelewa kitu husika kinachoelekezwa kwa kuangalia picha yake au kitu
halisi ambapo mwnafunzi anaweza kudadisi ,kuchunguza na kugundua nini
kinachomaanishwa,kwa mfano; mtumizi ya chati,picha za vitu,mabango,grafu na ramani.
Kukosekana kwa ujuzi na ubunifu, mwalimu anatakiwa kuwa mbunifu na awe na ujuzi wa
kutengeneza na kuandaa zana zinazoendana na somo pamoja na mada husika ambazo zitamsaidia
mwalimu kufundisha vizuri na kwa urahisi na kuwawezesha wanafunzi kumuelewa mwalimu
kwa urahisi zaidi.
Ukosefu wa vifaa vya kutengenezea zana, katika uandaaji wa zana ,mwalimu anaweza kukosa
vifaa vya kutengenezea zana husika.Changamoto hii inaweza kusababishwa na utofauti wa
mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa, kwa mfano; mwalimu anayetaka kutumia mimea au
wadudu kama zana zake katika ufundishaji wa somo husika ni vigumu kuwapata wadudu au
mimea hiyo hasa wakati wa kipindi cha kiangazi ,mwalimu anaweza kukosa vifaa vingine katika
mazingira ya karibu ,mfano wa vifaa hivyo ni kama gundi,karatasi ngumu na hata rangi.
Uandaaji wa zana unagharimu muda, katika uandaaji wa zana hizo ,mwalimu anatakiwa kutenga
muda wake wa ziada wa kuzitafuta na kuziandaa zana hizo,hivyo suala hili humpa changamoto
kubwa mwalimu katika utengaji wake wa muda ,suala ambalo linaweza kusababisha mwalimu
kufundisha pasipo kutumia zana pale tu atakapokosa muda wa kuzitafuta na kuziandaa zana hizo.
Kunahitajika umakini wa hali ya juu wakati wa utumizi wa zana ,mwalimu hana budi kutoa
maelezo ya kina kwa wanafunzi wake katika kutumia zana hizo,kwa mifano baadhi ya zana
zimetengenezwa kwa vioo hasa katika masomo ya sayansi ,hivyo mwalimu na wanafunzi
wanatakiwa kuwa makini wanapotumia zana hizo ili zisiweze kuvunjika hata kuwadhuru
wnafunzi.
Kwa ujumla ,zana za ufundishaji na ujifunzaji ni muhimu sana katika suala zima la ufundishaji
na ujifunzaji kwani humsaidia mwalimu kuongeza ustadi na ujuzi zaidi juu ya mada husika,pia
humsaidia mwanafunzi kutumia milango yake ya fahamu zaidi ya mmoja kitu ambacho
humfanya mwanafunzi huyo kuielewa mada kwa undani zaidi na kuihifadhi kichwani kupitia
utumizi huo wa zana moja kwa moja.Kama vile utumizi wa zana masikizi,zana maono na zana
maono-masikizi.
MAREJELEO
KITIVO : ELIMU.
IDARA :ISIMU NA LUGHA.
JINA LA KOZI : MBINU ZA KUFUNDISHIA KISWAHILI
MSIMBO : CT126.
JINA LA MHADHIRI : KILAVE Y.
MWAKA WA MASOMO : MWAKA WA KWANZA, 2016/2017.
AINA YA KAZI : KAZI YA KIKUNDI.
MKONDO : BAED 1 A.
KUNDI : NAMBA 04
NAMBA MAJINA NAMBA ZA USAJILI SAHIHI