Zana Za Kufundishia Na Kujifunzia Ni Vifaa Anavyotumia Mwalimu Wakati Wa Mchakato Wa Ufundishaji Na Ujifunzaji Ili Zimrahisishie Ufundishaji Wake Na Kuwafanya Wanafunzi Waelewe Somo Kiurahisi Zaidi

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

Zana za kufundishia na kujifunzia ni vifaa anavyotumia mwalimu wakati wa

mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji ili zimrahisishie ufundishaji wake na


kuwafanya wanafunzi waelewe somo kiurahisi zaidi.Kwa hiyo zana za kufundishia na
kujifunzia ni vifaa vinavyotumika katika mchakato mzima wa ufundishaji na
ujifunzaji.

AINA ZA ZANA

Zana za kujifunzia na kufundishia zipo za aina mbalimbali kama ifuatavyo;-

I. Zana maono, hizi ni zana ambazo hutumuka katika mchakato wa kufundishia


na kujifunzia ambapo vitu halisi huhusishwa,kwa kutumia viyu halisi
mwanafunzi anajifunza kwa udadisi,kuchunguza na kupindua,pia vitu halisi
vinampa mwanafunzi nafasi kubwa ya kujifunza kwa vitendo an kutumia
milango mingi ya fahamukwa wakati mmoja.Kwa ukosefu wa vitu halisi
mambo au vitu bandia huchukua nafasi ya pili,mwanafunzi anapata
kuona,kusikia,kuhisi kana kwamba antumuia vitu halisi.Bandia ni igizo la vitu
halisi, hivyo huchangia kiasi fulan cha ukweli, mfano;
chati,picha,mabango,grafu na ramani.
II. Zana masikizi, zana hizi humsaidia mwanfunzi kujifunza kwa kusikia.Vipindi
maalumu hutayarishwa kwa ajili ya shule au wanafunzi wanaosoma kwa
masafa, mfano;redio,tepu-rekoda,santuri.
III. Zana masikizi maono, zana hizi zinachangia kuonesha vitu kama vilivyo,hali
hii kuna ukweli ndani ya zana hizi.Zana hizi zinamuwezesha mwanafunzi
kusikia na kuona matendo wakati ule ule yanapofanyika.Kwa mfano;
luninga,sinema,ngamizi na vifaa vingine vinavyohusisha kuona na kusikiliza.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UANDAAJI WA ZANA ZA KUJIFUNZIA AN KUFUNDISHIA

Katika uandaaji na utumiaji wa zana ,kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kama


ifuatavyo;

Somo na mada, mwalimu anapaswa kuandaa zana zinazosadifu somo na mada


husika , kwa mfano; kama somo ni historia ,mwalimu anapaswa kuandaa zana kama
vile nramani kutegemeana na mada husika.Pia kama somo ni la Kiswahili katika
mada ya aina za mmaneno,mwalimu anaweza kuandaa chati inayoonesha aina za
maneno.

Umri au kiwango cha elimu cha wanafunzi, mwalimu anapaswa kuandaa zana
zinazoendana na umri pamoja na kiwango cha elimu ya wnafunzi wake,kwa kufanya
hivyo itawarahisishia wanafunzi kuelewa mada husika kwa urahisi zaidi,pia
itamsaidia mwalimu kufundisha kwa wepesi zaidi.

Zana inapaswa ibebeke, mwalimu anapaswa atumie zana ambayo ni rahisi


kubebeka na kuhamishika ili iwe rahisi kwa wanafunzi kuiona kwa makini an kwa
urahisi zaidi,kwani zana isiyobebeka wala kuhamishika kwa urahisi zinakua ni
kikwazokikubwa kwa wanafunzi katika kujifunza.Hivyo zana itakayo tumika intakiwa
iwe nyepesi na yenye kuhamishika kutoka sehemu moja adi sehemu nyingine.

Zana haipaswi kua inayotisha, mwalimu anatakiwa kuandaa zana isiyotisha hasa
kwa wanaojifunza.Baadhi ya zana hazipaswi kutumika kwa wanafunzi kwa
wanafunzi wenye umri mdogo kwani zinaweza kuwaogopesha hata an kuwahamisha
darasani kisaikolojia , kwa mfano ; matumizi ya picha za wanyama wakali kama vile
samba na nyoka.

Zana inatakiwa iwe yenye kuonekana, mwalimu anatakiwa atumie zana


zinazoonekana ili wanafunzi waweze kuelewa kitu huhsika kinachoelekezwa kwa
kuangalia picha yake au kitu halisi ambapo mwnafunzi anaweza kudadisi
,kuchunguza na kugundua nini kinachomaanishwa,kwa mfano; mtumizi ya
chati,picha za vitu,mabango,grafu na ramani.

CHANGAMOTO WAKATI WA UANDAAJI W A ZANA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA

Katika mchakato wa kuandaa zana za kufundishia na kujifunzia ,changamoto


zifuatazo zinaweza kujitokeza;

Gharama ya zana husika, katika mchakato wa uandaaji wa zana za kufundishia na


kujifunzia ,kuna baadhi ya zana ambazo hugharimu kisi kikubwa cha fedha n a hivyo
kumfanya mwalimu ashindwe kuzipztz zana hizo,hivyo basi hulazimika kufundisha
bila kutumia zana.

Kukosekana kwa ujuzi na ubunifu, mwalimu anatakiwa kuwa mbunifu na awe na


ujuzi wa kutengeneza an kuandaa zana zinazoendana na somo pamoja na mada
husika ambazo zitamsaidia mwalimu kufundisha vizuri na kwa urahisi an
kuwawezesha wanafunzi kumuelewa mwalimu kwa urahisi zaidi.

Ukosefu wa vifaa vya kutengenezea zana, katika uandaaji wa zana ,mwalimu


anaweza kukosa vifaa vya kutengenezea zana husika.Changamoto hii inaweza
kusababishwa an utofauti wa mazingira an mabadiliko ya hali ya hewa, kwa mfano;
mwalimu anayetaka kutumia mimea au wadudu kama zana zake katika ufundishaji
wa somo husikani vigumu kuwapata wadudu au mimea hiyo hasa wakati wa kipindi
cha kiangazi ,mwalimu anaweza kukosa vifaa vingine katika mazingira ya karibu
,mfano wa vifaa hivyo ni kama gundi,karatasi ngumu na hata rangi.

Uandaaji wa zana unagharimu muda, katika uandaaji wa zana hizo ,mwalimu


anatakiwa kutenga muda wake wa ziada wa kuzitafuta na kuziandaa zana hizo,hivyo
swala hili humpa changamoto kubwa mwalimu katika utengaji wake wa muda ,swala
ambalo linaweza kusababisha mwalimu kufundisha pasipo kutumia zana pale tu
atakapokosa muda wa kuzitafuta na kuziandaa zana hizo.

CHANGAMOTO WAKATI WA UTUMIAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA


Kukosekana kwa maarifa katika kutumia zana hizo, hapa tunamaanisha kuwa,zana
zinakuwepo tayari ,pengine zimenunuliwa,zimefaraguliwa au zimetengenezwa na
mwalimu mwingine wa somo hio,lakini katika utumiaji inaweza kutokea baadhi ya
walimu kukosa maarifa ya kutosha katika uelezeaji ili kurahisisha ujifunzaji.Hii
inaweza kupelekea hasa kutoeleweka kwa maada lengwa au kumsumbua mwalimu
katika kutafsiri.mfano; matumizi ya jedwaliau chati ya aina za maneno
isipotafsiriwa vizuri inaweza kumfanya mwalimu asieleweke.

Kunahitajika umakini wa hali ya juu wakati wa utumizi wa zana ,mwalimu hana budi
kutoa maelezo ya kina kwa wanafunzi wake katika kutumia zana hizo,kwa mifano
baadhi ya dhana zimetengenezwa kwa vioo hasa katika masomo ya sayansi ,hivyo
mwalimu na wanafunzi wanatakiwa kuwa makini wanapotumia zana hizo ili zisiweze
kuvunjika hata kuwadhuru wnafunzi.

Kwa ujumla ,zana za ufundishaji na ujifunzaji ni muhimu sana katika suala zima la
ufundishaji na ujifunzaji kwani humsaidia mwalimu kuongeza ustadi na ujuzi zaidi
juu ya mada husika,pia humsaidia mwanafunzi kutumia milango yake ya fahamu
zaidi ya mmoja kitu ambacho humfanya mwanafunzi huyo kuielewa maada kwa
undani zaidi na kuihifadhi kichwani kupitia utumizi huo wa zana moja kwa
moja.Kama vile utumizi wa zana masikizi,zana maono na zana maono-masikizi.
MAREJELEO

1. Wanjara S.F. na J.M.Kavoi (2012).Stadi za mawasiliano na mbinu za


kufundishia kswahili.Mwama :Serengeti Educatinal publishers(T) Ltd.
2. Syambo .B. na wengine (1987).Jinsi ya kufundisha Kiswahili katika shule za
msingi.Nairobi:Heineman Kenya.
3. Ndunguru S. (1986). Kanuni na mbinu za kufundishia ,Dar es salaam:Mbogo
International Graphic Arts.
4. Tuntufie,N.D (1972). Jinsi ya kufundisha Kiswahili. Dar es salaam: Tanzania
publishing.

You might also like