Jarida La Nchi Yetu Mwezi Juni

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 23

NCHI YETU Jarida la Mtandaoni

Utamaduni, Sanaa na Michezo

TOLEO NA.5 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO TOLEO LA JUNI 2017

TANZANIA YA VIWANDA HII HAPA


JPM Azindua Viwanda Vitano, Vyaajiri Zaidi ya Watu 900

Kiwanda cha Sharubati Chatoa Soko kwa Wakulima 30,000

www.maelezo.go.tz
i Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Bodi ya Uhariri
Mwenyekiti
Dkt. Hassan Abbasi
Mkurugenzi-Idara ya Habari-MAELEZO

Wajumbe
Rodney Thadeus
John Lukuwi
Elias Malima
Jovina Bujulu
Lilian Lundo
Msanifu Jarida
Hassan Silayo

Huduma zitolewazo MAELEZO


1.Kuuza picha za Viongozi wa Taifa na matukio muhimu
ya Serikali.
2.Kusajili Magazeti pamoja na Majarida
3.Kukodisha ukumbi kwa ajili ya mikutano na Waandishi
wa Habari.
4.Rejea ya Magazeti na Picha za Zamani
5.Kupokea kero mbalimbali za wananchi.

Jarida hili hutolewa na:


Idara ya Habari-MAELEZO
S.L.P 8031
Dar es Salaam-Tanzania
Simu : (+255) 22 -2122771
Baruapepe:maelezo@habari.go.tz
Blogu: blog.maelezo.go.tz
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO ii
TAHARIRI

TANZANIA YA VIWANDA, MKOA WA PWANI UMEONESHA NJIA

Mwezi Juni mwaka huu, karata nyingine ya Mhe. John Pombe Magufuli ilichangwa na kwa wale weledi
wa mchezo wa karata wanaweza kusema alilamba dume. Hii imedhihirika pale alipofanya ziara ya siku
tatu katika mkoa wa Pwani na kuzindua viwanda vikubwa vitano ambapo alisema mkoa huo una zaidi ya
viwanda 127 jambo ambalo kama angevitembelea vyote hata mwaka mmoja usingetosha kuvikagua.

Kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Mhe. Magufuli aliwaomba wananchi
wamchague na wamuamini kwani anadhamiria ya dhati kuitoa nchi katika lindi la umasikini na
kuipeleka katika uchumi wa kati unaojengwa na ukuaji wa viwanda. Jambo hili limeanza kudhihirika.

Mbali na ahadi hiyo, ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM sura ya pili ibara za 32 na 33 zimeweka
bayana mikakati ya kuanzisha viwanda vipya na kushirikiana na wawekezaji kuimarisha viwanda vilivyopo ikiwa
ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa uwekezaji mkubwa wa viwanda ili kuzalisha ajira za kutosha.

Mpango wa maendeleo wa taifa wa Miaka mitano 2016/17-2020/21 pia umeweka bayana mikakati itakayosaidia
kukuza uchumi wa viwanda ikiwemo kushirikiana na Jumuiya za Kikanda katika masoko na uchumi kama Jumuiya
ya Afrika Mashariki pamoja na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kukuza uchumi wa viwanda.

Juhudi zote hizo zinadhihirisha kuwa Tanzania ya viwanda inawezekana chini ya uongozi wa Jemedari
Rais John Pombe Magufuli zimeanza kuzaa matunda. Mkoa wa Pwani ni kioo cha uwekezaji mkubwa
wa viwanda hivyo ni vema kuwakaribisha viongozi wa mikoa mingine ili waweze kujifunza mbinu
walizotumia kufikia mafanikio hayo ambayo yameonekana katika kipindi kifupi kwa ujenzi wa viwanda
vingi ambavyo vitazalisha ajira kwa wingi na hatimaye kuwapunguzia vijana tatizo la ajira kwa vijana.

Sisi NCHI YETU tuna unga mkono jitihada za Mhe. Rais za kuhakikisha kunakuwa na ongezeko
la viwanda, pia tunaunga mkono onyo alilolitoa kwa watumishi wa umma wanaokwamisha
wawekezaji kwa makusudi kwa kuwawekea mlolongo wa taratibu zisizokuwa na tija ambazo mara
nyingi zimewakatisha tamaa na kusababisha wengine kuhamishia uwekezaji katika nchi jirani.

Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali ikiwemo madini, misitu, mbuga za wanyama, hali
nzuri ya hewa na tunu za taifa letu za amani na utulivu, ni vyema tukatumia baraka hizo tulizojaaliwa na
Mungu katika kuhakikisha uchumi unakua kwa sababu mazingira yetu yanaruhusu. Pamoja na mambo
yote mazuri ni vema kila mmoja wetu akatimiza wajibu wake ili tunufaike na ukuaji wa uchumi sambamba
na utetezi wa maslahi ya wanyonge jambo ambalo kila mara Mhe. Rais amekuwa akilitilia mkazo.

Tukiwa watanzania wenye uchungu na uzalendo wa nchi hii, tuendelee kumuunga mkono na kumuombea
Rais wetu katika kuhakikisha azma yake ya kukuza uchumi kwa kuijenga Tanzania ya viwanda inawezekana.
Tuna toa rai kwa viongozi wa mikoa ambayo haina viwanda wakajitathmini na kujitafakari ni kwa namna
gani watamsaidia Mhe. Rais kwa kuanzisha kuweka mazingira wezeshi uanzishwaji wa viwanda. Aidha ni budi
kuhakikisha kwamba wanaiga mfano wa mkoa wa Pwani kwa kuvutia wawekezaji wengi katika sekta ya viwanda
ili kuweza kuongeza ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa Watanzania. Tanzania ya viwanda imeanza
kuonekana, kila mmoja atimize wajibu wake, Mungu ibariki nchi yetu, Mungu ibariki Tanzania ya viwanda.
1 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Inatoka Uk. 1

TANZANIA YA VIWANDA HII HAPA


Na Eliphace Marwa-MAELEZO

H ivi karibuni Rais John Pombe


Magufuli alifanya ziara ya
kikazi ya siku tatu katika Mkoa
wa Pwani na kuzindua viwanda
vitano. Hatua hii inaelekea
kutimiza ahadi yake wakati wa
Uchaguzi Mkuu ya kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Kuwepo kwa ongezeko la


viwanda kunatimiza nia ya
Serikali ya kuwezesha sekta
binafsi kuongoza mendeleo
ya viwanda kwa kuweka
mifumo dhabiti ya usimamizi
na muindombinu wezeshi ili
kuchochea kasi ya maendeleo
ya teknolojia katika viwanda
hivyo. Hii ni pamoja na
kuhakikisha upatikanaji wa ardhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
iliyopimwa na kuweka dira na Magufuli akifungua kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS
mwongozo wa utekelezaji wake. kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Viwanda vitano vilivyozinduliwa tani 1,200,000 kwa mwaka. Serikali katika kuhakikisha
na Rais ni pamoja na kiwanda inawasaidia wawekezaji wa
cha vifungashio cha Global Kiwanda hiki kinamilikiwa viwanda kwa kupitia Shirika
Packaging Tanzania chenye na Mtanzania Bwana la Reli Tanzania (TRL) tayari
uwezo wa kutengeneza mifuko Mohamed Said Kiluwa kwa limejenga njia ya reli ya kilometa
aina ya sandarusi 53, 000 kwa siku. asilimia 51 na mwekezaji 3.5 inayounganisha kiwanda
kutoka China kwa asilimia 49. cha Chuma cha Kiluwa na reli ya
Kiwanda hicho ambacho ujenzi kati ikiwa ni juhudi za kurahisisha
wake umegharimu shilingi bilioni Katika kiwanda cha vinywaji usafirishaji wa malighafi na
nane, kimeajiri wafanyakazi 110. baridi cha Sayona Drinks Ltd vyuma vinavyozalishwa
kinachomilikiwa na Mtanzania kiwandani hapo kwenda
Kiwanda kingine ni cha
Subhash Patel ambapo Rais ndani na nje ya nchi.
kutengeneza matrekta 2,400
Magufuli aliweka jiwe la
aona ya Ursus kiwanda hiki
msingi la ujenzi wa kiwanda Katika ziara hiyo, Rais
kinamilikiwa na Serikali ya
Tanzania kwa asilinia 100.
hicho utakao gharimu shilingi Magufuli pia alizindua
bilioni 120 mpaka kukamilika. Barabara ya Bagamoyo
Kiwanda kingine kilichozinduliwa Makofia - Msata yenye urefu
ni cha chuma cha Kiluwa Aidha kiwanda hicho cha wa kilometa 64 ambayo
Steel Group kilichopo Mlandizi sharubati kitatoa ajira 800 na imejengwa na wakandarasi
ambacho katika awamu ya pia kufungua fursa ya soko la wazawa kwa fedha za ndani.
kwanza kitakuwa na uwezo wa matunda kwa wakulima 30,000
kuzalisha tani 500,000 za nondo ambao watakuwa wanakiuzi Barabara hiyo itasaidia
kwa mwaka na awamu ya pili kiwanda hicho matunda. kupunguza foleni iliyokuwa
kitaongeza uzalishaji hadi kufikia kero katika barabara ya
Inaendelea Uk. 3
Inaendelea Uk. 2
Jarida la Nchi Yetu 2016
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na
Tuimarishe Uchumina
Limeandaliwa wa Viwanda
Idara kwa Maendeleo Yetu
ya Habari-MAELEZO 2
mwaka 2015 wa kuhakikisha
kuwa Tanzania inakuwa nchi
ya viwanda na kupelekea
kuondoa tatizo la ajira nchini na
pia kupunguza bei za bidhaa
kwenye soko la biashara.

Mkoa wa una zaidi ya


viwanda vikubwa na vidogo
85 na ni kielelezo tosha cha
kwamba azma ya Tanzania ya
Viwanda inawezekana, hivyo
watanzania hawanabudi
kuunga mkono juhudi za
Mhe. Rais za kuanzisha na
kufufua viwanda pamoja
na kuhamasisha uwekezaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe nawapongeza


Magufuli akifungua kiwanda cha Sharubati(Juisi) cha Sayona Fruits wawekezaji na pia
kilichopo Mboga Chalinze mkoani Pwani.
naviagiza vyombo
vinavyohusika kutoa
Morogoro toka Dar es kujenga viwanda na kuwataka vibali kwa ajili ya ujenzi
Salaam mpaka Chalinze. wamiliki wa viwanda hivyo
kujali maslahi na usalama
wa viwanda hapa nchini
Aidha Rais Magufuli pia wa wafanyakazi waliowaajiri. viondoe urasimu ambao
amezindua mradi wa upanuzi umekuwa ukiwakatisha
wa mtambo wa maji wa Ruvu Uzinduzi wa viwanda hivyo ni
Juu na ulazaji wa mabomba muendelezo wa kutekeleza tamaa wawekezaji- Rais
makubwa ya maji ya kutoka ahadi yake aliyoitoa wakati wa Magufuli
Mlandizi hadi Dar es Salaam kampeni za Uchaguzi Mkuu wa
uliojengwa na Serikali ya
Tanzania kwa gharama ya
shilingi bilioni 200 ikiwa ni mkopo
nafuu kutoka Serikali ya India.

Rais Magufuli pia ameitaka


Wizara ya Maji na Umwagiliaji
kuhakikisha inajipanga vizuri
kusimamia utekelezaji wa
miradi ya maji inayosuasua,
kudhibiti upotevu na wizi
wa maji na kuwakatia
maji wadaiwa sugu wote.

Akizungumza katika miradi hiyo,


Rais Magufuli amepongeza
uwekezaji huo na ameagiza
vyombo vinavyohusika kutoa
vibali kwa ajili ya ujenzi wa
viwanda hapa nchini viondoe Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka ya Nchini Croatia Olivia Jakupec
akimtembeza Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
urasimu ambao umekuwa katika maeneo mbalimbali ya kiwanda cha utengenezaji wa viungo vya chakula
ukiwakatisha tamaa wawekezaji kilichopo Bagamoyo,Mkoani Pwani.
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na
3 Tuimarishe Uchumi
Limeandaliwa wayaViwanda
na Idara kwa Maendeleo Yetu
Habari-MAELEZO

Uchumi wa Tanzania Waongoza A. Mashariki


Na Said Ameir-MAELEZO

P amoja na Tanzania
kutajwa kuwa ni miongoni
mwa nchi tano zenye
uchumi unaofanya vizuri
barani Afrika, lakini tangu
kuingia utawala wa Awamu
ya Tano kumekuwepo na
dhana miongoni mwa
baadhi ya watu na taasisi
kuwa hali si hivyo ilivyo.

Katika Makala hii Mwandishi


Said Ameir anachambua
kwa kifupi maeneo
yanayopelekea kuwepo
kwa dhana hiyo na kwa nini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani
Kwa mwaka mwingine (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam Mei
tena mwenendo wa hali ya 16,2017.
mafanikio hayo, wako
uchumi nchini umeendelea asilimia 7.1 ikiwa nyuma wanaiona hali ya uchumi wa
kuwa mzuri huku Tanzania ya nchi ya Ivory Coast nchi kuwa si shwari kwa madai
ikitajwa kuwa ni moja kati ya ilioongoza kwa uchumi kuwa kutokana na baadhi
nchi tano barani Afrika zenye wake kukua kwa asilimia 7.9. ya hatua zilizochukuliwa na
uchumi unaofanya vizuri.
serikali bila kushirikisha wadau
Kuendelea kufanya vizuri kumesababisha ukwasi katika
Kwa mujibu wa taarifa za huku kunaelezwa kuwa uchumi, kufungwa kwa
Benki ya Dunia na Shirika ni matokeo ya uboreshaji biashara, na madai kwamba
la Fedha la Kimataifa wa sera uliofanywa na sekta binafsi imepoteza
(IMF) uchumi wa Tanzania unaoendelea kufanywa matumaini na kujiamini.
umeendelea kufanya vizuri na uongozi wa Serikali ya
ukiwa katika orodha ya Awamu ya Tano chini ya Rais Katika hotuba yake ya Bajeti
nchi tano barani Afrika na John Pombe Magufuli, kama Bungeni, Waziri wa Fedha na
nafasi ya kwanza katika alivyosema Naibu Mkurugenzi Mipango Dk. Philip Mpango
ukanda wa Afrika Mashariki. Mkuu wa IMF Bw. Tao Zhang, alieleza kuwa hali ya ukwasi
alipotembelea Tanzania Mei katika kipindi kilichoishia
Kwa mujibu wa takwimu za 2017, hususan katika uthabiti mwezi Machi 2017, kwa hali
Shirika la Fedha la Kimataifa wa maeneo ya ukusanyaji ya baadhi ya vigezo vya
(IMF World Economic wa mapato ya ndani na vita ukwasi inaonyesha kuwa
Outlook Database), uchumi dhidi ya rushwa na ufisadi. ujazo wa fedha kwa tafsiri
wa Tanzania unakuwa kwa
pana zaidi (M3) uliongezeka
Hata hivyo, pamoja na kwa asilimia 4.1 kutoka shilingi
Inaendelea Uk. 4
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
4
maamuzi yasiyotabirika
yanayofanywa na Serikali.

Wanaoeneza dhana hii


potofu ambao baadhi ni
mawakala wa washindani
wa Tanzania katika kuvutia
uwekezaji na biashara
wanafanya hivyo huku
takwimu zikionesha hali tofauti
na kile wanachokieleza.

Serikali imekuwa mara kwa


mara, ikichukua hatua
za kuimarisha mazingira
ya uwekezaji na kufanya
biashara na hata taarifa ya
Benki ya Dunia ya mwaka 2017
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia)
inaonesha matokeo tofauti
akielezea mpango wa Serikali wa kuboresha kilimo ili kukuza uchumi wa viwanda na hiyo dhana inayojengwa
alipofanya Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa na baadhi ya watu.
(IMF), Tao Zhang (wa tatu kushoto), hivi karibuni jijini Dar es salaam

trilioni 21.65 katika kipindi kuwa katika kipindi cha Taarifa hiyo ya Benki ya Dunia
kama hicho mwaka 2016 kuanzia Julai 2016 hadi ya mwaka 2017 inaonesha
hadi shilingi trilioni 22.53. Machi, 2017 ni biashara kuwa, Tanzania imepiga
7,277 tu ndizo zilizofungwa hatua 12 kutoka kuwa nchi
Hotuba hiyo ya Waziri katika mikoa mbalimbali ya 144 hadi nchi ya 132 kwa
ilibainisha pia kuwa kwa sekta nchini ikilinganishwa na urahisi wa kufanya biashara.
ya kibenki nayo iliendelea biashara mpya zipatazo
kuwa imara na himilivu huku 224,738 zilizosajiliwa Kwa upande wa uwekezaji,
uwiano kati ya mali inayoweza katika kipindi hicho hicho. mwaka 2016 Tanzania ilikuwa
kubadilishwa kuwa fedha nchi ya kwanza miongoni
taslim na amana zinazoweza Kufungwa huku kunaweza mwa nchi za Afrika Mashariki
kuhitajika kwa muda mfupi kusababishwa na mambo kwa kuvutia uwekezaji na
ilikuwa asilimia 35.9 mwezi mengi lakini inawezekana ya nane kwa Afrika, ikiwa
Machi 2017 ikilinganishwa na sana kasi hiyo ya kufunga imepiga hatua kutoka
uwiano wa chini unaohitajika biashara inatokana na nafasi ya 19 mwaka 2015.
kisheria wa asilimia 20. wito unaotolewa na
Serikali kuwataka wale Taarfa hii ni kwa mujibu
Imekuwa ikidaiwa pia kuwa wote wanaofunga wa Fahirisi ya Uwekezaji
katika kipindi cha Awamu ya biashara watoe taarifa ili Afrika ya mwaka 2016
Tano kumekuwepo na kasi wasiendelee kutozwa kodi. (Africa Investment Index,
ya wafanyabishara kufunga 2016) iliyotolewa na taasisi
biashara zao likitajwa jiji Ni kweli tumekuwa tukisoma ya Quantum Global
la Dar es Salaam kuwa katika baadhi ya vyombo Research Lab ya Uingereza.
moja miji iliyoathirika sana. vya habari vikiwemo vya
nje vikidai kuwa wawekezaji Katika kuendelea kuweka
Hata hivyo, takwimu rasmi wanasita kuja Tanzania kwa mazingira bora zaidi ya
toka Mamlaka ya Mapato madai kuwa wamepoteza uwekezaji nchini, Kituo cha
Tanzania (TRA) zinaonesha imani kutokana na Uwekezaji Tanzania (TIC)
5 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

wanaojaribu kuujenga
wakosoaji wa hali uchumi
nchini hauna msingi wowote.
Kama alivyoeleza Waziri
Fedha katika hotuba yake
ya bajeti, Serikali imekuwa
ikifanya jitihada za kujenga
mazingira mazuri ya kuvutia
uwekezaji kufanya biashara.

Katika kufanya hivyo,


Serikali imekuwa ikichukua
hatua mbali mbali zikiwemo
kuimarisha utulivu wa uchumi
jumla, kupunguza urasimu,
kuharakisha maamuzi,
kuimarisha ulinzi na usalama
Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini na kuhakikisha upatikanaji
Dar es Salaam wa miundombinu imara
kimetangaza kuanzia Julai vyote ili kutokumfanya na huduma bora zikiwemo
mwaka huu kitaanza kutoa mwekezaji kuzunguka umeme wa uhakika na
kutoa vibali vya uwekeza kwenye mamlaka kutafuta mikopo kwa sekta binafsi.
ndani ya siku tatu tu. vibali, ningependa kuazia Bwana Mwanri aliongeza
Julai mwaka huu tutoe vibali kuwa ni vema Polisi wawe
Taasisi mbalimbali zinazotoa ndani ya siku tatu, anaeleza wanafanyakazi kwa
huduma kwa mwekezaji Mkurugenzi Mtendaji wa kubadilishana ili kuepuka
zinatakiwa zilete ofa na TIC, Godfrey Mwambe. kujenga mazoea ya
kukaa hapa kutoa vibali wachimbaji hao na hivyo
Kwa hivyo, wasiwasi kuathiri utendaji wao.

Bunge Lapitisha Bajeti ya Wananchi


H ivi Karibuni
lilipitisha
Bunge
Bajeti
Serikali kwa Mwaka wa
ya
Waziri wa
Fedha na
Mipango,
Dk Philip
Fedha 2017-2018 ya trilioni Mpango
31.7 Katika Makala hii akionesha
mkoba wenye
Mwandishi Said Ameir bajeti ya
pamoja na kuchambua serikali mjini
Dodoma
kwa ufupi baadhi ya
maeneo anaeleza kuwa
ni bajeti inayoleta unafuu
kwa watu wa kila kipato.
Inaendelea Uk. 6
6
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

dhana ya ushirikishwaji
na pia ni kielelezo kuwa
Serikali imezidi kuwa sikivu.

Serikali haikuamka tu
ikaamua kufuta kodi na
tozo mbali mbali bali ni
matokeo ya kusikiliza maoni
ya wananchi wakiwemo
walipa kodi na watumia
huduma zinazotozwa kodi.
Mwaka huu Serikali, kwa
mfano, imefuta kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT)
kwa magari ya kubebea
wagonjwa, ada ya leseni ya
Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwasilisha Bungeni magari, kodi kwa vifaa va
mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa walemavu, tozo na ada za
mwaka 2017/18. zimamoto kwa shule binafsi.

N i bajeti iliyogusa hisia za


watu wengi tangu wakati
ilipotangazwa kwa mara ya
Hii ni kusema kuwa bajeti
ya mwaka huu imezidi
kuweka mazingira wezeshi
Aidha, serikali imeamua
kutoza asilimia sufuri ya
kwanza tarehe 08 Juni, 2017, kwa uchumi na uwekezaji kodi kwenye usafirishaji wa
wakati wa kujadili wizara kwa kushamiri huku wananchi wa bidhaa au mizigo nje ya nchi
wizara hadi kufikia tamati na kawaida wakipewa unafuu ili kuifanya Tanzania kuwa
kupitishwa tarehe 20 Juni, 2017. katika maeneo mbalimbali njia bora kwa usafirishaji/
kwa kufutwa baadhi ya upitishaji wa mizigo kwenda
Hii ni bajeti ya pili katika kipindi tozo na kodi ambazo nchi nyingine kama vile nchi
cha kwanza cha miaka zimeonekana kuwa kwaza. jirani za Burundi, Rwanda,
mitano ya Rais John Pombe Jamhuri ya Kidemokrasia
Magufuli. Ni bajeti ambayo Fedha nyingi zimeendelea ya Kongo na Malawi.
mchambuzi yeyote wa kutengwa kwa matumizi
masuala ya siasa na uongozi katika sekta muhimu za Hatua hii itasaidia kuongeza
anaweza kusema kuwa maendeleo kama vile ujenzi matumizi ya Bandari
imezingatia sana mwelekeo wa miundombinu ya uchumi, zetu za Dare es Salaam,
na sura halisi ya uongozi wa uimarishaji wa sekta ya Tanga na Mtwara na kwa
Awamu ya Tano chini ya nishati kwa ajili ya uwekezaji kiasi kikubwa kuchangia
Rais John Pombe Magufuli. na wananchi mijini na vijijini ongezeko la ukusanyaji
pamoja na huduma za jamii mapato ya serikali.
Unaliona hilo katika upangaji kama elimu, afya na maji.
wa vipaumbele, mikakati Serikali imeondoa pia Kodi
ya utafutaji wa mapato na Hapana shaka yeyote kuwa ya Ongezeko la Thamani
matumizi pamoja na ari na ushirikishaji wadau mbali (VAT) kwenye bidhaa za
dhamira ya uongozi ya kutaka mbali wakiwemo kutoka mtaji ili kuhamasisha ukuaji
kuondoa kero zisizo za lazima sekta binafsi umesaidia sana wa viwanda, ada ya
zinazowakuta wananchi kuifanya bajeti hii kuwa tathmini ya mazingira kwa
kutokana na baadhi ya bora zaidi kuliko ya mwaka wawekezaji wa viwanda,
maamuzi ya kisera au kisheria. uliopita na unathibitisha tozo ya VAT kwa vyakula vya
kwa vitendo utekelezaji wa mifugo vinavyotengenezwa

Inaendelea Uk. 7
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na
7 Tuimarishe Uchumi
Limeandaliwa na Idarawa
ya Viwanda kwa Maendeleo Yetu
Habari-MAELEZO

hapa nchini chini ya alama


ya HS CODE 2309, tozo ya VAT
kwenye mayai ya kutotolea
vifaranga na imepunguza
ushuru wa mazao.

Hatua hizi zote zinalenga


kuongeza fursa zaidi sio
tu kwa wawekezaji toka
nje bali pia kwa wananchi
kuwekeza katika viwanda
kwa kuazisha vidogo vidogo
na vya ngazi ya kati hatua
ambayo itaongeza uwezo
wao kiuchumi na hatimae
kuinua kiwango cha maisha.
Uchambuzi wa bajeti
unaonesha kuwa mwaka huu Wabunge wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa
wa fedha Serikali imepanga mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma Juni 8 2017.
kutumia jumla ya shilingi
trilioni 31.7 ambapo fedha
kwa ajili ya maendeleo Bajeti hii imezidi kutoa
ni shilingi trioni 11.9 sawa matumaini kwa wananchi Tuna amini pia kuwa uzoefu
asilimia 38 ya bajeti yote. kwa sababu tofauti na bajeti wa upangaji na utekelezaji
Katika fedha hizo matumizi ya ya mwaka uliopita, bajeti ya wa bajeti ya mwaka uliopita
kawaida ni shilingi trilioni 19.7 mwaka huu karibu asilimia umesaidia sana kuimarisha
ikijumuisha shilingi trilioni 7.2 85 inatokana na vyanzo vya utendaji na usimamizi wa
za mishahara na shilingi trilioni ndani hivyo utekelezaji wake bajeti ya mwaka huu.
9.4 kwa ajili ya kulipia deni la unatarajiwa kuanza mara
Taifa na huduma nyinginezo. moja na kwa mafanikio zaidi.

Miswada ya Kihistoria yawasilishwa Bungeni Rais Dkt. John Pombe


Na Mwandishi Wetu-MAELEZO Magufuli akipokea

K
Taarifa ya Kamati
atika kutekeleza agizo ya pili ya Uchunguzi
wa Madini yaliyo
la Mhe. Rais Dkt. John kwenye makontena
Pombe Magufuli lililotokana yenye mchanga
unaosafirishwa
na mapendekezo ya kamati nje ya nchi kutoka
ya pili ya mchanga wa kwa Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Profesa
madini (makinikia) chini Nehemiah Osoro Ikulu
ya Mwenyekiti wake Prof. jijini Dar es Salaam,
kulia ni Waziri Mkuu
Nehemia Osoro, hatimaye Mhe. Kassim Majaliwa
Bunge la Jamhuri ya na Kushoto ni
Makamu wa Rais Mhe.
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
limeanza kujadili miswada

Inaendelea Uk. 8
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na
Tuimarishe Uchumi
Limeandaliwa wayaViwanda
na Idara kwa Maendeleo Yetu
Habari-MAELEZO
8
mitatu ya sheria iliyowasilishwa
na Waziri wa Katiba na Sheria
Prof. Palamagamba kwa ajili
ya kufanyiwa marekebisha.

Miswada iliyowasilishwa
Bungeni ni pamoja na
Muswada wa Sheria ya
Mapitio na Majadiliano
kuhusu Masharti Hasi katika
Mikataba ya Maliasili za Nchi
wa Mwaka 2017, Muswada
wa Sheria ya Mamlaka ya
Nchi kuhusiana na Umiliki wa
Maliasili wa Mwaka 2017 na
Muswada wa kutungwa kwa
Sheria mbalimbali ikiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
sheria ya madini, petrol, kodi akipeana mikono na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada
ya mapato, Kodi ya Ongezeko Profesa John L. Thornton mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es
la Thamani na Sheria ya Bima. salaam Juni 14, 2017. Kulia ni balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles

yataipa Serikali haki na


Sababu za kufanya Muswada huo pia utaanzisha
mamlaka ya umiliki wa
marekebisho hayo ya sheria ni Kamisheni ya Madini na
mazao yote yanayopatikana
kuimarisha mifumo ya udhibiti kuanisha kazi zake ambapo
katika uchimbaji, uchakataji
na uwajibikaji, kupanua ikiwa ni pamoja na kufanyia
na uchenjuaji wa madini
wigo wa makusanyo ya kodi mapitio madaraka ya Waziri
na kuweka utaratibu wa
yanayohusiana na sekta ya na Kamishna wa madini
kuyahifadhi migodini ikiwa
madini na petroli na kuweka kwa lengo la kupunguza
ni pamoja na kuweka ulinzi
masharti yatakayowezesha baadhi ya majukumu
mahsusi wa maeneo yote
Watanzania kunufaika yao na kuyahamishia
ya uchimbaji wa madini.
na maliasili ya madini, katika kamisheni hiyo.
petroli na gesi asilia.

Katika muswada wa
kutungwa kwa Sheria
mbalimbali ikiwemo sheria
ya madini, petrol, kodi ya
mapato, Kodi ya Ongezeko
la Thamani na Sheria ya
Bima, marekebisho ni yale
ya kutambua na kuweka
umiliki wa madini, petroli na
gesi chini ya usimamizi wa
Rais kwa niaba ya wananchi,
tofauti na ilivyokuwa awali
ambapo bidhaa hizo zilikuwa
chini ya wizara yenye
dhamana ya nishati madini.
Malori yakisomba mawe na mchanga wa dhahabu katika mgodi
Marekebisho hayo pia
wa Buzwagi.
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na
9 Tuimarishe Uchumi
Limeandaliwa wa
na Idara yaViwanda kwa Maendeleo Yetu
Habari-MAELEZO

ya madini na rasilimali za taifa


kutokana na udanganyifu
na udhaifu wa baadhi
ya sheria na mikataba.

Upoteaji wa mapato na
udhaifu wa sheria katika sekta
ya madini ulibainika wakati
Mwenyekiti wa Kamati ya Pili
ya kuchunguza mchanga
wa madini uliozuiliwa
kusafirishwa nje nchi, Prof.

Nehemia Osoro alipo bainisha


kuwa makontena 61,320
yalisafirishwa nje ya nchi
katika kipindi cha mwaka
1998-2017 na yalikuwa
Pia serikali itakuwa na na thamani ya shilingi za
uwezo kisheria wa kufanya kwenye shughuli za madini. kitanzania trilioni 183.597 kwa
majadiliano na kupitia upya kiwango cha chini na trilioni
baadhi ya masharti kwenye Akizungumza hivi karibuni, 380.499 kwa kiwango cha juu.
mikataba iliyokwisha fanyika. Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.
Aidha alisema kuwa serikali
Aidha muswada huu pia Job Ndugai amesema kuwa imepoteza mapato kiasi
utaipa serikali uwezo wa Bunge lake linaloendelea cha shilingi trilioni 108.46
kutambua viwango vya kujadili miswada hii,
ambazo ni sawa na bajeti
madini yote yanayotolewa litahakikisha linafanya
ya serikali inayokaribia miaka
kwenye migodi na mabadiliko ya sheria hizo kwa
mitatu kwa kigezo cha
kuanzishwa kwa hifadhi maslahi mapana ya Taifa. makadirio ya matumizi ya
ya dhahabu na vito chini mwaka 2017/2018 pamoja
ya Benki Kuu pamoja na Marekebisho ya sheria hizi na gharama ya kujenga reli
kuanzisha maghala ya serikali yamekuja kufuatia kubainika ya Standard Gauge kutoka
ya kuhifadhi madini nchini. kuwa nchi imekuwa ikipoteza Dar es salaam hadi Mwanza.
mapato mengi katika sekta
Pia Serikali itaanzisha mfumo
mahsusi wa kukusanya
na kuhifadhi taarifa zote
za shughuli za madini.

Kupitia muswada huu baadhi


ya sheria zimependekezwa
kurekebishwa. Sheria hizi ni
pamoja na sheria ya madini
sura ya 123 na sheria ya
petroli ya sura 392, ambazo
zitatambua na kuweka
umiliki wa sekta ya madini
mikononi mwa Watanzania Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akioneshwa maeneo katika mgodi wa
na kuweka utaratibu bora chuma cha liganga uliopo ludewa alipotembelea mgodi huo mapema mwaka
wa kulinda mazingira huu
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
10

KATUNI NA MSAMIATI WA LEO

6
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na
11 Tuimarishe Uchumi
Limeandaliwa na Idarawa Viwanda kwa Maendeleo Yetu
ya Habari-MAELEZO

TANZANIA JUNI HII

Rais Dk. John Pombe Magufuli akisoma ripoti ya


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la
Kamati ya Pili ya kuchunguzi wa mchanga wa Madini
msingi la Kituo cha Kutoa Huduma kwa Waathirika
yaliyo kwenye makontena yaliyozuiwa kusafirishwa nje
wa Dawa za Kulevya mjini Dodoma Juni 29,
ya nchi.Wanaoshuhudia kushoto ni Makamu wa Rais
2017. Kulia ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Mhe. Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
Mhe. Kassim Majaliwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia wakati alipozindua Kamusi Kuu ya Kiswahili
namna samaki anaweza kufugwa vizuri bila
kuharibu mazingira na kuleta manufaa kabla ya
kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma
kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira Juni 19, 2017.
duniani ambapo kilele chake kimefanyika kwenye
viwanja vya Mwenge,Butiama
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
12

NCHI YETU KATIKA HISTORIA

Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage


Nyerere akipata maelekezo kutoka kwa mtaalam Rais wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi
katika moja ya kiwanda alipokitembelea enzi za akiweka mchanga kwenye tofali wakati akizindua
uongozi wake. moja ya jengo enzi za uongozi wake

Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Rais wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Nyerere akiwa anasaidia katika kuponda udongo pamoja na mwakilishi wa Shirika la Misaada la
kwa ajili ya nyumba katika kijiji cha ujamaa Mkoani Ujerumani KFW Bi. Katrin Brandes na aliyekuwa
mkuu wa mkoa wa Lindi Bibi Mwantum Mahiza
Dodoma.
wakifunua kitambaa kuzindua ujenzi wa mradi wa
maji wa mji wa Lindi eneo la Ngapa mjini Lindi
13 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Upanuzi Kina cha Bandari Kugharimu Bilioni 926


Na Benjamin Sawe-MAELEZO

H ivi karibuni Mamlaka ya


Bandari
imesaini
nchini
mkataba
(TPA),
wa
upanuzi na uongezaji wa kina
cha bandari utakaowezesha
bandari ya Dar es Salaam
kupokea meli kubwa za
mizigo na kushindana na
bandari nyingine katika
Pwani ya Bahari ya Hindi.

Upanuzi huo utakaofanywa


na kampuni ya China Harbor
Construction ya China
utagharimu kiasi cha shilingi
bilioni 926 na utadumu kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
miezi 36, ambapo utahusisha
Magufuli akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella
uongezaji wa kina cha lango Bird mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa
la bandari na uongezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
kina cha maji kati ya gati
namba moja hadi saba. kukuza uchumi wa Tanzania,
amesema Prof. Mbarawa. Naye Mkurugenzi Mkuu wa
Akizungumza katika hafla TPA Mhandisi Deusdedit
ya utiaji saini mkataba huo Prof. Mbarawa anasisitiza Kakoko anasema kiasi cha
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na kuwa pamoja na upanuzi dola za Marekani milioni
Mawasiliano Prof. Makame wa bandari ya Dar es 421, kitapatikana kwa ajili ya
Mbarawa amesema hatua Salaam Serikali inaendelea ujenzi huo ambapo kati ya
hiyo inalenga kuifufua upya na ujenzi wa miundombinu fedha hizo Benki ya Dunia
bandari ya Dar es Salaam wezeshi ya reli na barabara itatoa mkopo wa masharti
ili ifanye kazi kwa ushindani ili kuhakikisha mizigo haikai nafuu wa dola milioni 345.
na kuhudumia wateja muda mrefu bandarini.
wengi kuliko ilivyo sasa. Kukamilika kwa ujenzi huo
Ujenzi wa reli ya kisasa ya kutaondoa adha ya baadhi
Kukamilika kwa upanuzi na Standard Gauge toka Dar es ya meli kusubiri kwa muda
uongezaji wa kina cha maji Salaam hadi Kanda ya Ziwa na mrefu kupata nafasi ya kutia
katika gati namba moja Kigoma na ufufuaji wa reli ya nanga na kutaongeza hadhi
(1) hadi saba (7) kutoka Tazara kutawezesha bandari ya bandari ya Dar es salaam
mita 8 hadi 15 kutawezesha ya Dar e s Salaam kufanya na kuvutia wasafirishaji wengi
meli kubwa na za kisasa kazi kwa ufanisi na kuvutia kutoka ndani na nje ya nchi.
zenye uwezo wa kubeba wafanyabiashara wengi
hadi makontena elfu kumi hivyo nawataka wafanyakazi Rais Tayari amezindua ujenzi
na tisa kutia nanga katika wote wa bandari kufanyakazi huo na kutoa maagizo kuwa
bandari ya Dar es Salaam kwa bidii na uadilifu, ukamilike haraka ikiwezekana
na kuongeza ufanisi na amesisitiza Prof. Mbarawa. ndani ya miezi 28 badala ya 36
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO 14

Ukusanyaji Kodi ya Ardhi Kielektroniki


Waongeza Mapato
Wizarani au kituo cha malipo
kulipa kodi bali anaweza kufanya
hivyo akiwa mahali popote kwa
kutumia simu yake ya mkononi
kwa kupitia menyu kuu ya Taifa
ambayo ni *152*00#. Njia hii
itamwondolea usumbufu mlipaji
ikiwemo kupoteza muda mwingi
kutoka anapokaa hadi kufika
Wizarani kwa ajili ya kulipia kodi.

Masami aliongeza kusema kuwa


hadi sasa Wizara imekusanya
shilingi bilioni 90, ukilinganisha
na shilingi bilioni 74 ambazo
Mkuu wa kitengo cha kodi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo zilikusanywa kwa kipindi cha
ya makazi, Denis Masami(kushoto),akizungumza na waandishi wa mwaka 2015/16, na kwamba
habari,katikati ni Mkurugenzi wa mifumo ya kifedha kutoka Wizara bado wana imani kuwa
ya fedha, John Sausi. makusanyo yataongezeka
kwani zoezi linaendelea hadi
kufikia Juni 30, mwaka huu.
wa Kitengo cha Kodi wa Wizara ya
Na Jovina Bujulu-MAELEZO Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Pamoja na kuongezeka kwa
Makazi, Denis Masami amesema
S erikali ya Awamu ya Tano makusanyo, Masami alisema
kuwa tangu kuanza kutumika bado wanakabiliwa na
imeonesha jitihada za
rasmi kwa mfumo huu mwanzoni changamoto za kimtandao na
makusudi katika ukusanyaji
mwa mwezi Juni mwaka huu, uelewa mdogo wa wananchi
wa kodi ambapo mapato
makusanyo yameongezeka katika matumizi ya mtandao.
yameongezeka kwa kipindi
kutoka bilioni mbili hadi bilioni
kifupi kutoka bilioni 8 hadi
2.9 kwa kipindi cha wiki tatu. Ili kutatua changamoto hii
wastani wa trilioni 1.3 kwa mwezi.
elimu inaendelea kutolewa kwa
Kwa mfumo wa kawaida watu maofisa wa Wizara, taasisi na
Katika kutekeleza suala
walikuwa wanalipa kodi ya wananchi wa kawaida ili waweze
la ukusanyaji wa mapato
pango la ardhi kwa siku tano kutumia njia ya kielektoniki
kielektroniki, Wizara ya Ardhi,
tu ambazo ni siku za kazi, lakini kwa wingi na kuongeza
Nyumba na Maendeleo ya
baada ya kuanza kutumia mfumo makusanyo, alisisitiza Masami.
Makazi imezindua Mfumo wa
wa elektroniki watu wanaweza
kukusanya kodi ya pango la
kulipa wakati wowote, muda Naye Mkurugenzi wa Mifumo
ardhi kwa njia ya kielektroniki.
wowote na mahali popote, hivyo ya Kifedha wa Wizara ya
Mfumo huu umeonyesha
ni dhahiri kuwa taratibu za malipoFedha na Mipango John Sausi
kuwa ni bora katika kuongeza
kwa mfumo huu zimekuwa amesema kuwa kwa kutumia
ukusanyaji wa mapato.
ni rafiki anasema Masami. mfumo huo mtu atatumiwa
Katika mahojiano maalumu na ujumbe wa majibu kuonyesha
Aliongeza kuwa kwa mfumo kiasi cha fedha alicholipia
mwandishi wa makala hii, Mkuu
huo, mlipaji kodi hahitaji kwenda ambao utahesabika kama risiti.
15 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

TAKUKURU Inastahili Kongole


Na Mwandishi Wetu-MAELEZO

J umatatu tarehe 19-06-


2017, Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa
nchini (TAKUKURU) ilionyesha
kuwa sasa haitaki mchezo na
suala la wahujumu uchumi
na wanaochezea rasilimali
za taifa kwa kuwafikisha
Mahakamani watuhumiwa
wawili wakuu waliohusika
katika kashfa ya Akaunti
ya Tegeta ESCROW.

Ni dhahiri kuwa taasisi


hiyo inayoongozwa na
Mkurugenzi wake Mkuu,
Kamishna Valentino Mlowola
kuwa sasa imelivalia njuga
suala la wabadhirifu na wala Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Juni 19,
rushwa bila kujali hadhi, vyeo 2017 iliwafikisha mahakamani wafanyabiashara wawili James
wala ushawishi wao katika Rugemalira na Harbinde Seth watuhumiwa wawili wa kesi za
jamii, kama inavyosisitizwa ESCROW na IPTL.
mara kwa mara na kinara
pamoja na ubadhirifu wa Mlowola, lakini pia kwa
wa mapambano hayo
mali za umma na rasilimali taasisi hiyo jinsi ilivyojipanga
ni Rais wa Jamhuri ya
za Watanzania zimeanza kushughulika na watuhumiwa
Muungano wa Tanzania
kuungwa mkono na mbali mbali wa uhujumu
Dkt. John Pombe Magufuli.
taasisi zenye dhamana uchumi, jambo ambalo
ya kumsaidia Mhe. Rais linairudishia heshima Tanzania
Katika hali iliyowashangaza
katika mapambano hayo. iliyojengeka tangu enzi za
mamilioni ya watanzania
Baba wa Taifa hayati Mwl.
Taasisi hiyo ilifanikiwa
Wafanyabiashara hao, Julius Kambarage Nyerere.
kuwafikisha Mahakamani
ambao wanatuhumiwa
wafanyabiashara maarufu
kufanya udanganyifu na TAKUKURU ilikuwa ni
waliowahi kulitikisa Bunge
kuisababishia serikali hasara miongoni mwa taasisi za
katika serikali iliyopita
ya Shilingi bilioni 309, ni umma ambazo zilionekana
aliyekuwa mmiliki wa
miongoni mwa watuhumiwa kushindwa kuwachukulia
Kampuni ya VIP Engineering
ambao walipewa jina la hatua watuhumiwa mbali
and Marketing Limited,
mapapa ikimaanishwa mbali wa kesi za rushwa
James Rugemarila na
kuwa ni wasiogusika. pamoja na ufisadi ambazo
mmiliki wa Kampuni ya
ziliibuliwa na kamati mbali
PAP, Habinder Seth Sigh.
Tunaipongeza Serikali ya Rais mbali za Bunge katika
John Pombe Magufuli kwanza awamu iliyopita na mwanzoni
Ni wazi kuwa juhudi za
kwa kuisuka upya TAKUKURU mwa Awamu ya Tano.
kupambana na ufisadi
chini ya Kamishna Valentino
Inaendelea Uk. 16
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO 16

za kisheria pamoja na
wale wote wanaoliingiza
taifa kwenye umaskini
mkubwa kwa kuhujumu
rasilimali za watanzania.
Katika muktadha huu ni
vyema sasa Mkurugenzi Mkuu
wa TAKUKURU Kamishna
Valentino Mlowola na timu
yake waendelee na moyo
huo wa kuchapa kazi bila
woga na kuhakikisha kuwa
hata wale waliotajwa katika
ripoti ya pili ya mchanga
wa madini maarufu kama
Makinikia, wanachunguzwa
na wakibainika wafikishwe
mbele ya vyombo vya Sheria
ili imani ya Watanzania kwa
aliyeianzisha vita hivi Rais
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli iendelee kuimarika.
Magufuli amepokea toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
Kamishna Valentino Mlowola Taarifa ya Utendaji kazi wa Mapambano haya
TAKUKURU ya mwaka 2015/2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam. yakisimamiwa kwa dhati
na yakiungwa mkono na
Kitendo cha kuwafikisha ni vyema wananchi na wao Watanzania wote, bila
watuhumiwa wa ESCROW kwa upande wao kukataa kujali itikadi za vyama,
Mahakamani sio tu kutoa au kupokea rushwa itawezesha serikali kutekeleza
kimewafurahisha watu wengi lakini pia kusaidia katika majukumu yake ipasavyo
bali hata wakosoaji wa juhudi za kuwafichua wale kwa kujenga mazingira
juhudi za Mh. Rais Magufuli wote wanaojihusisha na mazuri ya kuiwezesha kufikia
za kupambana na ufisadi vitendo hivyo. Kwa kufanya lengo la Tanzania kuwa nchi
wameanza kumkubali hivyo itasaidia kujenga taifa ya uchumi wa kipato cha
na kumuunga mkono. lenye wazalendo wa kweli kati ifikapo mwaka 2025.
watakaosaidia ndoto ya
Kwa mfano, aliyewahi kuwa
Mwenyekiti wa Kamati
Tanzania ya viwanda na
yenye uchumi wa kati kufikiwa.
Viva Magufuli, viva
ya Bunge ya Hesabu za TAKUKURU kila kitu
Serikali (PAC) ambaye Pongezi hizi zisiwafanye
pia ni kiongozi wa Chama Kamishna Mlowola na kinawezekana
cha ACT-Wazalendo, Zito timu yake kulewa sifa na tukiwa na
Kabwe hakuficha hisia zake kuona wameshafanikiwa,
na kumpongeza Mh.Rais wanatakiwa kuhakikiksha nia ya dhati.
na TAKUKURU alipoandika kuwa wale wote walioshiriki
kwenye ukurasa wake wa kwa namna moja ama
mtandao wa kijamii wa Twitter. nyingine katika kashfa ya
Akaunti ya Tegeta ESCROW
Kwa kuwa mwarobaini wa wanachukuliwa hatua
rushwa sio TAKUKURU pekee,
17 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

PPF Yajipanga Kufanikisha Uchumi wa Viwanda


Na Fatma Salum-MAELEZO

M fuko
PPF
wa Pensheni
umejipanga
kuwekeza kwenye viwanda
ili kufanikisha azma ya Serikali
ya Awamu ya Tano ya
kujikita kwenye uchumi wa
viwanda utakaowezesha
Taifa kufikia uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025.

Kauli hiyo imetolewa na


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
huo Bw. William Erio wakati
akizungumza kwenye kipindi
maalum cha TUNATEKELEZA
kinachoratibiwa na Idara Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Dkt. Juma Malewa akisainiana
ya Habari-MAELEZO na mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi wa Muda wa Kampuni ya Mkulazi
Holdings Co. Ltd, Nicander Kileo huku wakishuhudiwa na Wakurugenzi wa NSSF
kutangazwa na Televisheni ya (Prof. Godius Kahyarara) na PPF (William Erio),
Taifa (TBC 1) Jijini Dar es Salaam.
zaidi ya Watanzania laki moja thamani ya mfuko huo
Akifafanua kuhusu uwekezaji hasa vijana. Anasema Erio. inaendelea kukua kila
huo, Erio amesema kuwa mwaka ambapo hadi
PPF kwa kushirikiana na Akieleza kuhusu maeneo mwaka wa fedha 2016/2017
Shirika la Hifadhi ya Jamii mengine ya uwekezaji, imefikia shilingi trilioni 2.5
NSSF wanajenga viwanda Mkurugenzi Mkuu wa PPF na una wanachama zaidi
viwili vya sukari mkoani amesema kuwa Mfuko huo ya laki 3 na elfu 30 kutoka
Morogoro kwenye maeneo pia umewekeza kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi.
ya Mkulazi na Mbigiri na ujenzi wa hoteli, ofisi na
vinatarajiwa kukamilika nyumba za kuishi na kwamba PPF ni Mfuko wa Hifadhi
ifikapo mwaka 2019. kuanzia mwaka 2015 hadi ya Jamii ulioanzishwa
2017 mfuko huo umelipa mwaka 1978 na jukumu lake
Mchakato wa ujenzi wa kodi ya Serikali shilingi bilioni kubwa ni kutoa pensheni
viwanda hivyo umeshaanza 73.9 kutokana na uwekezaji. pamoja na mafao mengine
na vitakapokamilika kwa mujibu wa sheria.
vitaweza kuzalisha tani Aidha amebainisha kuwa
laki 2.5 kwa mwaka na
vitasaidia kupunguza tatizo Mchakato wa ujenzi wa viwanda
la uhaba wa sukari hapa hivyo umeshaanza na vitakapokamilika
nchini. Anasema Erio.
vitaweza kuzalisha tani laki 2.5 kwa mwaka
Uwekezaji kwenye viwanda na vitasaidia kupunguza tatizo la uhaba
hivyo utasaidia kukuza pato wa sukari hapa nchini. William Erio.
la taifa na kutoa ajira kwa
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO 18

Urasimishaji Makazi Holela Dar Wanufaisha Wananchi


Na Jonas Kamaleki-MAELEZO

U kuaji wa makazi yasiyopangwa


ni mojawapo ya changamoto
kubwa ya miji yetu hususan
katika majiji na Manispaa nchini.

Katika utafiti uliofanyika mwaka


2013 ukihusisha majiji na Manispaa
nane, asilimia 66 ya maeneo
yaliyoendelezwa yalikuwa
ni maeneo yasiyopangwa.

Maeneo yaliyojengwa kiholela


hayana huduma muhimu za
kiuchumi na kijamii kama vile
maji safi na maji taka, mitaro
ya maji ya mvua, barabara, Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akionyeshwa
moja ya vifaa vinavyotumika katika upimaji wa Ardhi katika Mkutano mkuu na
umeme huduma za elimu na Kongamano la Wapimaji Ardhi uliofanyika Jijini Dar es Salaam
afya. Ili kukabiliana na hali hiyo,
juhudi mbalimbali zimekuwa ambayo ni Kimara B, Kingongo,
zikifanyika zikiwemo uboreshaji Kwa mujibu wa Mlonda, jumla Matangini, Michungwani,
wa miundombinu kwenye ya viwanja 6,000 vinatarajiwa Saranga, Stopover na Upendo.
maeneo husika (Community kupimwa na kumilikishwa katika jiji
Infrastructure Upgrading) la Dare es Salaam katika zoezi zima Ameongeza kuwa kwa pamoja
urasimishaji (regularization), la urasimishaji wa makazi holela. kata hizo zina wastani wa
utoaji wa leseni za makazi na viwanja 34,000. Mradi umeanzia
ujenzi upya wa maeneo hayo Pamoja na urasimishaji katika kutekelezwa katika Kata ya
hususan yale yaliyoko kwenye Jiji la Dar es Salaam halmashauri Kimara kwenye Mitaa ya
maeneo yaliyoiva kiuendelezaji nyingine sita (6) zimepangwa Kilungule A, Kilungule B na
upya (redevelopment). kutekeleza mradi huo. sasa Mavurunza. Lengo la Mradi
Halmashauri hizo ni; Manispaa ni kutambua, kupanga, kupima
Wizara ya Ardhi, Nyumba na za Musoma, Kigoma-Ujiji, na kumilikisha viwanja 6,000.
Maendeleo ya Makazi imepima Tabora, Singida, Sumbawanga
viwanja 4,333 hadi mwishoni na Lindi, amesema Mlonda. Mkurugenzi Msaidizi huyo
mwa Mei, 2017 na hatua za amesema kuwa baada ya
umilikishaji zimeanza katika Aidha, Mlonda amesema kuwa kukamilisha michoro ya Mipango
utekeleza wa kurasimisha mradi unatekelezwa katika Kata miji na Ramani za Upimaji na
maeneo yaliyojengwa za Kimara na Saranga Manispaa kupata upana wa barabara, kazi
kiholela jijini Dar es Salaam. ya Ubungo ambazo zina ukubwa iliyofuata ni kufungua barabara.
wa hekta 3,960. Kata ya Kimara,
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya inajumuisha mitaa sita (6) ambayo Barabara zenye urefu wa kilomita
Mipango Miji na Vijiji wa Wizara ni Kilungule A, Kilungule B, 9.128 zimechongwa katika Mitaa
ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo Mavurunza, Baruti, Kimara Baruti ya Kilungule A, Kilungule B na
ya Makazi, Bertha Mlonda na Golani. Kata ya Saranga Mavurunza, amesema Mlonda.
anafafanua katika makala hii. ina jumla ya mitaa saba (7)
19 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Katika urasimishaji huo, Mlonda


anaainisha mafanikio ya mradi ni
pamoja na kuboresha mazingira
katika makazi, kuongeza huduma
za jamii na miundombinu katika
maeneo ambayo awali yalikuwa
hayafikiki kwa gari sasa yanafikika
na kuongeza usalama wa miliki ya
ardhi kwa wananchi na kuongeza
fursa ya kutumia ardhi kama
mtaji na kupunguza umasikini.

Ameyataja mafanikio mengine


kuwa kanzi data inajenga uwezo
wa halmashauri kusimamia
na kutoa huduma za ardhi
kwa ufanisi, kuwa na maeneo Mmoja wa wataalamu wa upimaji ardhi akiweka
yaliyopangwa, kupimwa
na kumilikishwa,kupunguza
alama katika eneo lililorasimishwa.
au kupunguza kwa kiasi Urasimishaji huu unatekelezwa kila Halmashauri. Utekelezaji
kikubwa migogoro ya ardhi na kwa mkopo wa Benki ya utatumia uzoefu uliopatikana
kuongeza wigo wa mapato Dunia ambapo viwanja 3,000 wakati wa utekelezaji wa mradi
ya serikali kwa kupitia tozo vinatarajiwa kupimwa katika Jijini Dar es Salaam na Mwanza.
mbalimbali za ya kodi ya ardhi.

Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Waziri Mkuu azindua Wakala wa BarabaraVijijini
W aziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
amezindua Wakala wa Barabara Vijijini
na Mijini (TARURA) ikiwa ni mkakati wa
kuharakisha utatuzi wa changamoto
za usafiri katika maeneo hayo.

Akifanya uzinduzi mapema mwezi huu


mjini Dodoma, Waziri Mkuu amesema
kuwa wakala huo utasaidia kuimarisha
mtandao wa barabara za vijijini na
kuwawezesha wananchi wengi kusafiri
na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi.

Wakala huu tunaouzindua leo utakuwa


na manufaa makubwa kwa ustawi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi kitabu cha Muongozo wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini
nchi yetu kwa kuongeza chachu ya , Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Barabara Vijini na Mijini Mhandisi Victor Seif, katikati ni Waziri wa Nchi
uzalishaji mali mashambani kutokana na Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene . Uzinduzi huo umefanyika July 2, 2017 katika ukumbi wa
mikutano wa Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma
urahisi wa kufika sokoni na pia utasaidia
kushusha bei ya vyakula mijini na vijijini kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.
pamoja na bidhaa za viwandani George Simbachawene amesema
kutokana na gharama za usafirishaji Kwa sasa Tanzania ina zaidi ya
TARURA ni muhimu kwani ujenzi
kupungua, ameeleza Mhe. Majaliwa. kilomita 108,942 za mtandao wa
wa barabara za vijijini zitawagusa
barabara za Mamlaka ya Serikali
wananchi moja kwa moja na ni
Kwa upande wake Waziri wa Nchi za Mitaa ambao ni zaidi ya nusu ya
kichocheo kikubwa cha uchumi
Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na mtandao wa barabara kuu za Kitaifa.
LIMEANDALIWA NA

Idara ya Habari-MAELEZO
S.L.P 8031
Dar es Salaam-Tanzania
Simu : (+255) 22 -2122771
Baruapepe:maelezo@habari.go.tz
Tovuti: www.maelezo.go.tz
Blogu: blog.maelezo.go.tz

@TZ_MsemajiMkuu Msemaji Mkuu wa Serikali MaelezoTv

You might also like