Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 2

1

STATE HOUSE ZANZIBAR


OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE
Zanzibar 1.12.2017

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali


Mohamed Shein jana aliwaongoza Waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na
wananchi mbali mbali katika Maulidi ya kuadhimisha Kuzaliwa Mtume Muhammad
(SAW) kitaifa yaliofanyika katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.

Sherehe hizo za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambazo hufanyika kila
mwaka Kitaifa hapa Zanzibar ni miongoni mwa kawaida na mila ya Waislamu wa
Zanzibar.

Alhaj Dk. Shein aliungana na Waislamu na wananchi hao wakiwemo viongozi mbali
mbali wa Dini na Serikali pamoja na wananchi ambapo pia, Mama Mwanamwema Shein
nae alihudhuria Maulid hayo akiwa pamoja na viongozi wengine wanawake wa Kitaifa.

Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji alitumia fursa hiyo kuwakaribishwa
wananchi wote pamoja na viongozi mbali mbali akiwemo Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein
katika sherehe hizo za Maulid.

Katika Sherehe hizo, Waislamu walisisitizwa suala zima la amani, umoja na


mshikamano miongoni mwao na kutakiwa kufuata nyayo za Mtume Muhammad
(S.A.W) ili wapate kuongoka hapa duniani na kesho akhera.

Akisoma khutba Sheikh Muhammed Kassim Said kutoka Kamisheni ya Wakfu na Mali
ya Amana aliwataka Waislamu kuwa kitu kimoja huku akiwasisitiza umuhimu wa
kusaidiana na kuhurumiana kwa lengo la kupata rehema za Allah.

Sheikh Muhammed pia, alitumia fursa hiyo kukemea mambo maovu katika jamii hasa
suala la unyanyasaji wa wanawake na watoto ikiwa ni pamoja na suala zima la ubakaji
jambo ambalo limeanza kushamiri hivi sasa katika jamii na kueleza athari zake na
kutaka mashirikiano ya pamoja katika kulipiga vita.
2

Aidha, alieleza kuwa ni jukumu la Waislamu kusherehekea siku hii adhimu pamoja na
kufuata mafunzo ya Mtume Muhammad (S.A.W) aliyokuja nayo.

Sherehe hizo za Maulid ambazo husherehekewa duniani kote, zilianza kufunguliwa na


Qur-an tukufu iliyosomwa na Ustadhi Hamdan Juma Hamdan kutoka Magogoni Mkoa
wa Mjini Magharibi, ambapo tafsiri yake ilitolewa na Sheikh Ali Muobwa Hassan
kutoka Chuo cha Kislamu Zanzibar.

Milango ya Maulid Barzanji iliyoenda sambamba na Qasweeda ilisomwa na Maustadhi


kutoka vyuo mbali mbali vya Qur-an kutoka Unguja na Pemba yakiwemo Maulid ya
Hom kutoka Jumuiya ya Maulid ya Hom Mtendeni, Mkoa wa Mjini Magharibi ambayo
nayo yalikuwa kivutio kikubwa katika sherehe hizo adhimu.

Katika sherehe hizo za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Madressa


Qamaria ya Kibandamaiti, Mjini Unguja walisoma Qiyam Talaa, kilichotanguliwa na
Mlango wa nne uliosomwa na Ustadhi Abdalla Mjomba Daawa kutoka Madressa
Qaqmaria ya Kibandamaiti, Mjini Unguja.

Qasweeda ya mwaka 1439 Alhijra, ilisomwa na wanafunzi kutoka Madrassa Ihsan


Islamia kutoka Tumbatu Gomani, Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya Maulid hayo Sheikh Sherali Chapsi alitumia fursa hiyo kama
ilivyokaida kwa kila mwaka kumkabidhi Rais, Qasweda hiyo maalum.

Maulid hayo yalimalizika kwa Mlango wa dua uliosomwa na Sheikh Wazir Hassan
Choum, kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi na hatimae kufungwa kwa fatha iliyosomwa
na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Qabih chini ya mshereheshaji
Sheikh Hamza Zubeir Rijal.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar


Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

You might also like