Tamasha Maisara

You might also like

Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

Simu: +255-26-232-2484/232-4560 2 Barabara ya Reli na Mahakama,


Nukushi: +255-26-232-1955, S. L. P. 980,
Barua-pepe: pm@pmo.go.tz Dodoma,
Tovuti: www.pmo.go.tz Tanzania.

11 Januari , 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TUMIENI TAMASHA LA BIASHARA KUKUZA BIASHARA YA UTALII-
MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Biashara, Viwanda na


Masoko ya Zanzibar kuhakikisha inatumia Tamashara la Biashara la Zanzibar
kama chachu ya kukuza biashara ya Utalii kama ilivyo kwa Dubai Shooping
Festival na matamasha mengine Duniani.

“Natambua kwamba kazi ya kulipandisha hadhi zaidi tamasha letu hili si ndogo ,
hata hivyo ninayo imani kubwa kwamba si tu uwezo wa kufikia malengo hayo
mnayo bali pia mnaweza.”

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumatano, Januari 10, 2018) wakati
akifungua Tamasha la Nne la Biashara la Zanzibar lililofanyika kwenye viwanja
vya Maisara katika mkoa wa Mjini Magharib, wilaya ya Mjini.

Tamasha hilo lilifunguliwa jana ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za


kuelekea katika sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar, ambayo yalitokea Januari 12, 1964.

Alisema Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko inatakiwa kutumia fursa ya


uwepo wa tamasha hilo katika kuhakikisha inakuza biashara ya Utalii kwa kuwa
linajumuisha wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali.

Waziri Mkuu alisema Tamasha la Biashara ni nyenzo muhimu ya kukuza


biashara na huduma pamoja na kukuza uchumi wa nchi, pia linatoa fursa ya
kuwakutanisha wafanyabiashara au watoa huduma na wateja wao.

”Hali hii humuwezesha mzalishaji kupata mrejesho kuhusu namna bidhaa yake
inavyokubalika kwenye soko, mapungufu yaliyopo kwenye bidha husika pamoja
na kuelewa maboresho anayotakiwa kuyafanya katika bidhaa au huduma.”

1
Waziri Mkuu alisema kuwa tamasha hilo linaweza kutumika kama nyenzo
muhimu katika kuanzisha mahusiano mazuri ya kibiashara kati ya mteja na
mfanyabiashara, hivyo kuwawezesha wajasiriamali kuwa na masoko ya uhakika.

Pia Waziri Mkuu alisema kufanyika kwa tamasha hilo ni sehemu ya utekelezaji
wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 katika ibara ya 84 (f).

“Ilani imeweka wazi azma ya Serikali ya kuanzisha na kuendeleza ujenzi wa


kiwanja cha maonyesho ya biashara cha kimataifa na kuhakiisha ushiriki wa
wajasiriamali wa Zanzibar katika maonyesho ya biashara ya kimataifa ndani na
nje ya nchi.”

Baada ya kufungua tamasha hilo Waziri Mkuu alitembelea mabanda mbalimbali


katika viwanja yakiwemo ya taasisi za umma pamoja na wajasiriamali ambao
wanatoka Zanzibar, Tanzania Bara, Kenya, Uturuki, Misri, Uganda na Burundi.

Awali, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum


Ali alisema tamasha hilo lenye washiriki zaidi ya 200 limeandaliwa na wizara
yake pamoja na TanTrade.

Balozi Amina aliseka kauli mbiu ya tamasha hilo kwa mwaka 2018 ni ‘wekeza
kwenye viwanda kwa uchumi na ajira’ inalengo la kuhamasisha wadau kuongeza
uelewa kwa wananchi juu ya falsafa na dhima ya ujenzi wa viwanda.

(MWISHO)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
ALHAMISI, JANUARI 11, 2018.

You might also like