Professional Documents
Culture Documents
Timam Tea Inawafaa Watu Wote
Timam Tea Inawafaa Watu Wote
Timam Tea Inawafaa Watu Wote
-1
Juma Killaghai
Tangu kuingia sokoni kwa chai ya Timamu, baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza iwapo
wanaweza kuitumia hata kama hawana tatizo lolote la kiafya. Ili kupunguza wingi wa
wanaouliza swali hili ni vema tukafikisha kwa wasomaji makala kadhaa fupi zinayolenga
kujibu swali hili. Kila makala itajikita katika kuzungumzia manufaa na faida za kiafya za
kila moja, kati ya makundi mbalimbali ya viini lishe yaliyomo kwenye hii chai ya Haiiba
Timamu. Makala ya leo itazungumzia kundi la vitamini. Hata hivyo, kama utangulizi,
kwa minajili ya kueleweka zaidi, ni vema wasomaji wetu wakatambua kuwa magonjwa
yamegawanyika katika makundi mawili makuu.
MARADHI YA KUAMBUKIZA
MARADHI YA KIMFUMO
Kundi la pili ni lile la maradhi ya kimfumo (metabolic diseases). Haya ni yale magonjwa
yanayozaliwa mwilini kutokana na mifumo ya mwili kushindwa kufanya kazi kwa
utaratibu uliokusudiwa. Kwa mfano kiasi cha sukari kwenye damu ya mtu wa kawaida
(siyo mgonjwa wa kisukari), kinatakiwa kiwe chini ya 7.7 mmol/l (140 mg/dl), kiasi cha
masaa mawili hivi baada ya kula.
Kiasi hiki kikiwa juu ya hapa maana yake ni kwamba mfumo wa mhusika wa kuhamisha
sukari kutoka kwenye damu na kuipeleka huko kwenye seli inakotakiwa iwepo haufanyi
kazi inavyotakiwa. Mfano mwingine. Mtu ambaye siyo mgonjwa anatakiwa kuwa na
kiwango cha juu cha shinikizo la la damu cha kati ya mmHg 110 – 120; na kiwango cha
chini cha mmHg 80.
Nje ya viwango hivi maana yake ni kwamba kuna shida katika eneo fulani la mfumo wa
mzunguko wake wa damu. Shida inaweza kuwa mishipa ya damu imekakamaa na
hainyumbuliki kupanuka pale inapohitajika, na kwa maana hiyo shinikizo la damu
linakuwa kubwa kwenye kuta za mishipa hiyo pale damu inaposukumwa kusambazwa
mwilini. Shida pia inaweza kuwa kasi ndogo ya utaratibu wa uvunjifu na uundaji wa
kemikali mwilini (slow metabolism), hali inayopelekea kasi ndogo ya usukumaji wa
damu wakati wa kuisambaza mwilini na hivyo kuweka shinikizo dogo katika kuwa za
mishipa ya damu.
1. Upungufu wa viini lishe na virutubisho fulani fulani ndani ya mwili. Kwa mfano
maji; madini lishe, vitamini, tindikali mafuta zisizozalishwa mwilini (essential
fatty acids), vizuia vioksidishaji (anti-oxidants), na vijenzi vya protini
visivyozalishwa mwilini (essential amino acids);
f. Nakadhalika.
Msongo endelevu ni tishio kubwa sana kiafya. Sababu kubwa ni kwamba mwili huzalisha
tindikali nyingi sana pale mtu anapokabiliwa na msongo. Msongo endelevu hutumia
nishati nyingi sana ya mwili, na matumizi yoyote ya nishati huzaa tindikali kama zao la
ziada (by product). Aidha homoni mbalimbali zinazozalishwa na mwili ili kukusaidia
kukabiliana na msongo zina kawaida ya kuharibu vinasaba vya seli (DNA) iwapo
zitaachwa mwilini kwa muda mrefu bila kuondolewa. Uharibifu wa vinasaba huzaa
maradhi mengi sana ndani ya mwili, na haswa saratani.
Baada ya utangulizi huu, sasa ni wakati muafaka wa kuingia katika mada yetu ya leo,
ambayo kama tulivyotangulia kuitambulisha hapo awali, inahusu kundi la viini lishe
vilivyomo katika Haiiba Timamu Tea, vinavyojulikana kama vitamini. Huu utakuwa ni
mwanzo wa majibu ya swali tuliloulizwa kuhusiana na ni nani anapaswa kutumia
Timamu Tea.
VITAMINI NI NINI?
Kwa kawaida huwa tunatakiwa tupate vitamini zote tunazohitaji kupitia katika lishe. Hata
hivyo kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyoko katika lishe zetu inatokea tukawa na
upungufu wa baadhi ya vitamini na hivyo kukumbwa na magonjwa yanayohusiana na
huo upungufu.
Baadhi ya vitamini muhimu zilizomo kwa wingi katika chai hii ni B1, B2, B3 na C.
Vitamini B1
ii. Utendaji kazi wa mfumo wa mzunguko wa damu (cardio vascular system). Vita
mini hii inajukumu la kuzalisha kemikali tarishi (neurotransmitter) inayoitwa
acetylcholine. Kazi ya kemikali tarishi hii ni kupeleka taarifa mbalimbali baina ya
misuli na mishipa ya fahamu. Upungufu wa kemikali hii hupelekea mapigo ya
moyo kutokuwa katika mpangilio unaoeleweka (irregular heart-beat). Upungufu
mkubwa unaweza kupelekea kwenye moyo kushindwa kufanya kazi;
iv. Kusaidia ubongo kufanya kazi vizuri. Vitamini hii husaidia kuboresha utunzaji wa
kumbukumbu na umakini, huimarisha mishipa ya fahamu na kukinga dhidi ya
magonjwa mbalimbali yanayohusisha kudhoofika kwa ubongo; na
Vitamini B2
ii. Kufanya kazi kama kizuia kioksidishaji kinachosaidia kukinga dhidi ya magonjwa
ya moyo na saratani;
iii. Kusaidia katika kutibu maradhi ya upungufu wa damu na seli mundu (sickle cell);
Vitamini B3
ii. Husaidia kupunguza kiwango cha lehemu mbaya (bad cholesterol) mwilini;
iii. Husaidia kuongeza kiwango cha lehemu nzuri (good cholesterol) mwilini;
iv. Tafiti pia zinaonyesha kuwa vitamini hii husaidia sana kupambana na ugonjwa wa
kupoteza kumbukumbu; na ugonjwa wa lenzi za macho kufunikwa na ukungu
(cataracts; ugonjwa wa mifupa dhaifu; ugonjwa wa kisukari cha udogoni (Type I
diabetes); na
v. Aidha vitamini hii imehusishwa na kusaidia kuboresha uzalishaji wa nishati
katika ngazi ya seli; kuboresha na kuimarisha mishipa ya fahamu; na kuimarisha
na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula.
Vitamini C
Hii ni vitamini yenye faida nyingi sana muhimu kiafya. Baadhi ya faida hizi ni pamoja
na:
ii. Huzuia mizio (allergies) kwa kusaidia kudhibiti uwepo wa homoni ya Histamine
mwilini;
xi. Inasaidia katika matibabu ya saratani. Tafiti zinaonyesha kwamba dozi kubwa za
vitamini C ni mujarabu sana katika maangamizi ya seli za saratani;
xiv. Huboresha utendaji kazi wa mapafu na hivyo ni msaada mkubwa kwa wagonjwa
wa pumu;
xvi. Inaweza kusaidia katika matibabu ya kifua kikuu. Baadhi ya tafiti zimeonyesha
kuwa vitamini C ina uwezo wa kuua bacteria wanaosababisha maradhi ya kifua
kikuu.
Siku zote kinga ni bora kuliko tiba. Kutokana na mazingira tunayoishi kuwa ni yenye
kufanana sana, kila mmoja wetu ni mgonjwa mtarajiwa. Hata hivyo tukumbuke kuwa
kinga ni bora kuliko tiba, hivyo pale ambapo kuna uwezerkano wa kujikinga ni bora
tukafanya hivyo. Kutokana na faida nyingi zinazoletwa na vitamini zilizoko katika Haiiba
Timamu Tea kama tulivyozielezea hapo juu ni wazi kabisa kuwa kila mtumiaji wa Haiiba
Timamu Tea, bila kujali hali yake ya kiafya anaweza kunufaika sana.