Timamu Tea Inawafaa Watu Wote - 4

You might also like

Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 5

TIMAMU TEA INAWAFAA WATU WOTE!

-4

Juma Killaghai

Makala ya leo ni ya nne na ya mwisho, kati ya mfulululizo wa makala tulizodhamiria


kutoa kwa malengo ya kujenga hoja juu ya chai ya Haiiba Timamu kuhitajiwa na kila
mtu. Hoja ya msingi iliyotawala makala zote tatu zilizopita, na ambayo tunaiendeleza
katika makala hii, ni kuwa tiba ya chai hii inatokana na kumrejeshea mhusika viini lishe
mbali mbali muhimu vilivyopungua mwilini mwake. Katika makala zilizotangulia
tulizungumzia makundi matatu ya viini lishe vilivyomo kwenye chai ya Haiiba Timamu.
Tuliyataja makundi haya kuwa ni yale ya vitamini, madini lishe na tindikali za amino, au
vijenzi vya protini. Makala yetu ya leo itataja kundi la nne na la mwisho; hili si lingine
bali ni kundi la vizuia vioksidishaji (anti-oxidants).

VIZUIA VIOKSIDISHAJI

VIZUIA VIOKSIDISHAJI NI NINI?

Vizuia vioksidishaji ni molekuli (molecule) zinazozuia mchakato wa kuoksidisha


molekuli nyingine. Kuokisidisha ni muingiliano wa kikemia (chemical reaction)
unaopelekea molekuli iliyookisidishwa kupoteza chembe yenye/zenye umeme hasi
(electron), au kupoteza kiasili cha hydrogen katika umbile lake, au umbile lake
kuongezewa kiasili cha oxygen.

Mchakato wa uoksidishaji ndani ya mwili hutokea muda wote. Huu ni sehemu ya


mchakato wa ujenzi na uvunjifu wa kemikali ndani ya mwili, yaani metabolism.
Mchakato wa kuoksidisha unaweza kuzaa chembechembe zenye umeme chanya
zinazoitwa free radicals. Kwa upande wake hizi free radicals ni chembe zenye uwezo
mkubwa wa kuoksidisha, na hivyo kuwepo kwake kunaweza kuzaa ‘gharika’ (chain
reaction) ya uoksidishaji ndani ya seli za mwili. Hali hii inaweza kusababisha uharibifu
mkubwa wa seli au hata kifo cha seli husika.

Vizuia vioksidishaji huzuia hizi gharika kutokea ndani ya seli. Badala yake hivi
vioksidishaji huoksidisha hivi vizuia vioksidishaji na kwa hivyo kuacha seli za mwili
zikiwa katika hali ya salama. Kwa kawaida mwili unamiliki na kuendeleza mifumo
kadhaa ya vizuia vioksidishaji mbalimbali. Vizuia vioksidishaji hivi ni pamoja na
glutathione, Vitamini C, Vitamini A, na Vitamini E; pamoja na vimeng’enya mbalimbali
kama catalase, superoxide dismutase na peroxidases mbalimbali. Kuwepo kwa kiwango
kidogo cha vizuia vioksidishaji au kuwepo kwa vimeng’enya ndani ya mwili vinavyozuia
utendaji kazi wa hivi vioksidishaji, kunaweza kusababisha hali inayoiitwa ‘msongo wa
uoksidishaji’ (oxidative stress), hali ambayo husababisha seli za mwili kuharibiwa na hata
kufa. Tafiti zinaonyesha kuwa huu msongo wa uoksidishaji ni chanzo cha magonjwa
mengi ya kimfumo ikiwa ni pamoja na saratani.
VIZUIA VIOKSIDISHAJI VILIVYOMO KATIKA HAIIBA TIMAMU TEA

Baadhi ya vizuia vioksidishaji muhimu vilivyoko kwa wingi katika chai hii ni Curcumin;
Catechines, Flavonoids, Piperine, na Cinnamaldehyde.

Curcumin

Curcumin ni kemikali ya kiorganiki ambayo iko katika kundi pana la kemikali


zinazojulikana kitaalamu kama polyphenols. Polyphenols ni kemikali za kiorganiki
ambazo sehemu fulani katika maumbo yao kuna mkusanyiko wa viasili ulioko katika
mpangilio maalum unaosababisha sehemu kubwa ya tabia za kikemia za kundi hilo
unaoitwa ‘phenol’. Mkusanyiko wa aina hii katika kemikali za kiorganiki zinazounda
kundi lolote huitwa FUNCTIONAL GROUP kwa lugha ya kikemia. FUNCTIONAL
GROUP kwa tafsiri isiyo lazima ni MKUSANYIKO WA VIASILI ambavyo husababisha
tabia ya kikemia ya kundi zima. Faida za curcumin ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni
pamoja na:

i. Kutakasa majeraha dhidi ya bacteria na kuharakisha uponaji wake;

ii. Ina uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa saratani ya tezi dume;

iii. Ina uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa saratani ya matiti;

iv. Ni kizingiti kikubwa dhidi ya (melanoma); ambayo ni aina ya saratani ya ngozi


inayoanzia kwenye chembechembe zinazotia rangi kwenye ngozi (melanine)
kabla ya kusambaa katika maeneo mengine

v. Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya damu kwa watoto;

vi. Ni kitakasaji cha asili cha ini;

vii. Inaweza kuzuia au kusimamisha kukua zaidi kwa ugonjwa wa kupoteza


kumbukumbu (Alzheimer’s disease);

viii. Inazuia aina mbalimbali za saratani kusambaa kutoka eneo moja la mwili hadi
jingine;

ix. Ni kitukiza maumivu cha asili;

x. Inaratibu ujenzi na uvunjifu wa kemikali mwilini na kusaidia katika kuondoa


unene;

xi. Imekuwa ikitumika katika baadhi ya nchi, mathalani China, kama tiba ya
mfadhaiko;

xii. Ni pozo dhidi ya maradhi ya baridi ya yabisi na jongo;


xiii. Inatibu saratani ya tezi ya thyroid;

xiv. Inaharakisha kupona kwa majeraha na kuirejesha ngozi iliyoumizwa katika hali
yake ya kawaida ndani ya muda mfupi; na

xv. Inasaidia katika matibabu ya ugonjwa wa psoriasis (ugonjwa unaosababishwa na


kukua kwa kasi kwa baadhi ya seli za ngozi kupelekea ngozi kuwa na mabaka ya
rangi tofauti tofauti), pamoja na magonjwa mengine ya ngozi yanayotokana na
mfuro (inflammation) wa seli za ngozi.

Catechins

Huu ni mkusanyiko wa vizuia vioksidishaji ambavyo kutokana na maumbo yao kufanana


kwa karibu na tabia zao za kikemia kufanana pia, vimewekwa katika kundi moja la
kemikali za kiorganiki. Hata hivyo kama ilivyo kwa curcumin ambayo tumetangulia
kuitaja, catechins ni sehemu ya kundi kubwa zaidi la kemikali za korganiki
zinazojulikana kama polyphenols. Faida za catechins ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi
ni pamoja na:

i. Huhusishwa na kusaidia sana kuzuia mlundikano wa mafuta mwilini;

ii. Hushusha kiwango cha lehemu katika damu;

iii. Huzuia ongezeko la shinikizo la damu;

iv. Huzuia ongezeko la sukari ya kwenye damu;

v. Husaidia kuzuia kupatwa na ugonjwa wa mafua;

vi. Hupambana dhidi ya maambukizi ya bacteria; na

vii. Huzuia harufu mbaya kutoka katika kinywa.

Flavonids

Flavonoids ni mkusanyiko mwingine wa vizuia vioksidishaji ambavyo kutokana na


maumbo yao kufanana kwa karibu na tabia zao za kikemia kufanana pia, vimewekwa
katika kundi moja la kemikali za kiorganiki. Kama ilivyo kwa curcumin na catechins,
vizuia vioksidishaji hivi pia viko katika kundi pana zaidi la kemikali za kiorganiki za
polyphenols. Faida za flavonoids ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

i. Inaaminika kuwa zina uwezo mkubwa sana wa kupambana na saratani;

ii. Inaaminika kuwa zina uwezo mkubwa sana katika kukabiliana na magonjwa
mbalimbali yanayohusiana na moyo; na

iii. Inaaminika kuwa zina uwezo mkubwa sana wa kukabiliana na mfuro wa seli.
Piperine

Piperine ni miongoni mwa kemikali za kiorganiki zinazoitwa alkaloids. Alkaloid ni


kemikali yoyote ya kiorganiki ambayo umbile lake linajumuisha ‘nyongo’ (base) yenye
kiasili cha nitrogen. Faida za piperine ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

i. Husaidia kuongeza uwezo wa mwili kwa kiasi kikubwa wa kufyonza na kutumia


viini lishe mbalimbali vinavyopatikana kwenye vyakula;

ii. Inaaminika kuwa inachochea ongezeko la kasi ya ujenzi na uvunjifu wa kemikali


ndani ya mwili (accelerates metabolism) na hivyo kusaidia katika harakati za
kudhibiti uzito wa mwili;

iii. Inasaidia kudhibiti mfuro (inflammation) wa seli;

iv. Inapunguza kasi ya ukuaji wa seli za saratani, hususan zile zinazohusiana na


saratani ya mapafu; na

v. Inachagiza mwili kuzalisha homoni ya serotonin ambayo husaidia sana kujenga


hali ya kujisikia furaha na hivyo ni nzuri katika kukabiliana na msongo na
mfadhaiko.

Cinnamaldehyde

Cinnamaldehyde ni miongoni mwa kemikali za kiorganiki zinazoitwa cinnemaldehydes.


cinnemaldehydes ni kemikali za kiorganiki ambazo hutoa harufu (mara nyingi ya
kupendeza) na ambazo FUNCTIONAL GROUP yake ni ile inayokusanya viasili katika
mpangilio unaojulikana kama ALDEHYDE. Cinnamaldehyde ni kemikali ya kiorganiki
ambayo ina faida kubwa mwilini.

i. Inafanya kazi kwa kuzuia kuganda kwa damu kunakoweza kupelekea damu
isitembee mwilini inavyopasa;

ii. Inasaidia sana kupambana na mfuro wa seli na kwa hivyo husaidia sana katika
magonjwa yote yanayosababishwa na mfuro; na

iii. Husaidia ;

iv. Inazuia mlundikano wa mafuta kwenye ini na hivyo kutoa kinga dhidi ya ugonjwa
wa ini bonge (fatty liver disease);

v. Inahitajika katika utengenezaji wa creatine. Creatine ni kiini lishe kinachohitajika


katika uzalishaji wa nishati inayohitajika katika kuifanya misuli ifanye kazi zake
kwa ufanisi;
vi. Inahitajika katika uzalishaji wa protini aina ya collagen ambayo ni muhimu katika
uundaji wa ngozi, kucha na tishu zinazounganisha misuli;

vii. Husaidia kuimarisha siha za watu wanaoishi na virusi vya ukimwi;

viii. Husaidia kupunguza mfuro (inflammation) wa kongosho yaani pancreatitis;

ix. Husaidia kupunguza dalili za ugonjwa wa Parkinson;

x. Husaidia kukabiliana na maambukizi katika njia ya mkojo;

Kama tulivyosema huko nyuma, siku zote kinga ni bora kuliko tiba. Kutokana na faida
nyingi zinazoletwa na viini lishe vilivyoko katika Haiiba Timamu Tea kama
tulivyozielezea hapo juu, ni wazi kabisa kuwa kila mtumiaji wa Haiiba Timamu Tea, bila
kujali hali yake ya kiafya, anaweza kunufaika sana.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA WATENGENEZAJI WA CHAI HII, YAAINI


HERBAL IMPACT, KWA SIMU NAMBA: 0754281131; 0655281131; 0686281131; NA
0779281131 AU WATEMBELEE OFISINI KWAO:

MOSQUE STREET, NO.1574/144, KITUMBINI, DAR ES SALAAM (MKABALA


NA LANGO KUU LA KUINGILIA MSIKITI WA SUNNI)

You might also like