Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Nukushi: +255 (026) 2963629 na Utawala Bora,
Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la Taaluma Na. 1,
Tovuti:http://www.utumishi.go.tz Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
18 Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI YATOA HATI ZA HAKIMILIKI ZA KIMILA 275 KWA WANANCHI WA MSALALA WILAYANI KAHAMA

Serikali kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) mkoani
Shinyanga imepima mashamba 2158 na kutoa Hati za Hakimiliki za Kimila 275 kwa wananchi wa vijiji vya Lunguya na
Segese wilayani Msalala.

Takwimu hizo za urasimishaji zimetolewa Bw.Leonard M. Mabula kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na
Serikali za Mitaa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Msalala Bw. Simon Berege.

Akikabidhi Hati za Hakimiliki za Kimila kwa baadhi ya wananchi, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala
na Serikali za Mitaa Mhe. Jason Rweikiza (Mb) amewata wananchi hao kuzitumia vizuri hati hizo ili waweze kujiondoa
katika umasikini, kuboresha familia zao na wilaya yao.

Miongoni mwa wananchi waliopata fursa ya kukabidhiwa hati na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala
na Serikali za Mitaa ni Bw. Kimbuya Shija, Bw. Daudi Steven Ntowe, Bw. Christopher Malajo, Bw. James Shija na Bi.
Sabina Migayo.

Akizungumza na wananchi katika kijiji cha Lunguya, Waziri mwenye dhamana ya usimazi wa Mpango wa Kurasimisha
Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) nchini wa Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora,
Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema Serikali inarasimisha ardhi za wananchi wa vijijini kuwa mali
na kutoa hati za kimila zinazotambulika kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi wananchi wake.

Kapteni (Mstaafu) Mhe. Mkuchika, amewahikishia wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe.
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ina dhamira ya dhati ya kuboresha maisha ya wananchi wenye kipato cha chini kupitia
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

Naye, Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi. Seraphia
Mgembe amewata wananchi kutumia hati za kimila kupata mitaji, ameongeza kuwa Serikali inatoa hati hizo ili
kuwawezesha wananchi wapate maendeleo kwa kutumia fursa hiyo kupata mitaji kutoka katika taasisi za kifedha.

Akiwasilisha taarifa fupi ya utekelezaji kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga Mhe. Zainab R. Telack amefafanua kuwa, mradi umetekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
katika vijiji viwili (2) vya Lunguya na Segese vilivyokuwa katika Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambapo jumla ya hati
za kimila 275 zimetolewa na MKURABITA.

Aidha, urasimishaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kama ilivyo katika Halmashauri nyingine nchini, umetoa
matokeo chanya kwa kupunguza migogoro ya ardhi iliyokuwepo na kuongeza usalama wa milki za ardhi za wakulima
waliorasimisha ardhi zao.

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI


OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 16 MACHI, 2018

You might also like