Professional Documents
Culture Documents
Media History
Media History
(1)
Na Rwambogo Edson.
Mawasiliano ya umma tunaweza kuita ni kitendo cha kundi la watu kuzalisha taarifa
ambayo itawafikia kundi kubwa zaidi la watu wenye tabia tofauti na mitazamo tofauti
bila kuzingatia mipaka yao ya upeo.
Pia tunaweza kusema mawasiliano ya umma yanatumika kufikisha ujumbe tofauti kwa jamii
husika yenye tamaduni na mapokeo tofauti kwa wakati mmoja. Panapokua na mawasiliano kati
ya watu wawili tunaita mawasiliano binafsi, mwalimu anapofundisha darasani au mwana siasa
anapotoa hotuba huo unakua ni mfano wa mawasiliano ya kundi la watu lakini pia kuna hatua
nyingine ya mawasiliano pale mtu anapokua anasoma maandiko ya vitabu au taarifa yoyote
kupitia maandiko mbalimbali.
Kuna hatua nyingine ambayo tunasoma magazeti, majarida, kusikiliza Radio au kutazama Tv.
Hii inaweza kuitwa mawasiliano ya umma kwa kuwa ujumbe huwafikia watu wengi kupitia njia
tofauti ambapo mala nyingi chanzo kinaweza kua mtu mmoja na wafikwa wa huo ujumbe
wakawa watu wengi ambapo huwa ni ngumu kujua Idadi yake.
Mawasiliano ya umma yana upekee wake na yana utofauti kutoka katika mawasiliano binafsi
kutokana na asili ya mawasiliano kujikita katika kutumia vyombo vya ziada kuwafikia watu
wengi zaidi na ata mapokeo na urudishaji wa taarifa au mapokeo ya ujumbe kuwa tofauti. Hii
tunaweza kuita ni taaluma ya masomo yanayomaanisha mtu mmoja kutuma ujumbe mmoja ulio
na uzani sawa kwa kundi kubwa la watu na wakati mwingine inaweza kua ni kwa muda mmoja.
Mamilioni ya miaka yamepita kabla ya kugundulika binadamu ambae alikua na viungo kamili na
miguu iliyosahihi katika kuamua na kufanya mabadiliko katika mazingira yanayomzunguka.
Miaka zaidi ya milioni moja mpaka milioni tano iliyopita ziligundulika taarifa za kuwepo
binadamu katika bara la Africa binadamu huyo alikua akiishi mapangoni na mavazi yake yalikua
yakitumika na familia nzima na ilipokua inatokea kutembea umbali mrefu alilazimika kutumia
miguu na mikono.
Katika zama zilizofuata binadamu huyu alipiga hatua kubwa sana katika muonekano na
kimaendeleo kutokana na mazingira yaliyomzunguka kubadilika pia. Katika zama hizi binadamu
aliweza kugundua moto kwa matumizi yake mbalimbali, Binadamu hawa walianza kuishi katika
kundi kubwa sehemu moja kutokana na kuzaliana hivyo kuongezeka kwa Idadi na mahitaji yake
binafsi.
Kisha zama zikabadilika katika zama za tatu, ambapo binadamu huyu alianza
kugundua zana tofauti zilizoweza kumsaidia kupunguza ugumu wa kazi zake za kila
siku. Katika zama hizi binadamu aligundua chuma kwa ajili ya kukatia vitu
mbalimbali lakini pia kwa ajili ya ulinzi na kuwinda. Binadamu huyu aliweza
kutengeneza makazi ya muda wa kati kwa ajili ya kujihifadhi na maadui na hali
ngumu ya hewa.
Kwa kuwa binadamu huyu aliishi katika mapango alianza kupamba na kuweka
michoro katika mapango alimokua akiishi. Lakini pia alianza kutengeneza zana za
Kilimo kwa ajili ya kulima na kupanda baadhi ya mimea ili kujipatia Chakula na
kuandaa nyama ya kuchoma kwa kutumia zama za mawe na chuma lakini pia
alitengeneza mavazi ya kuvaa,pia alianza kufuga wanyama kwa ajili ya kitoweo.
Katika zama hizi binadamu alibadilika kimuonekano na kiupeo kwa kugundua njia
rahisi zilizompunguzia ugumu wa kazi, kutokana na ugumu wa kazi kupungua pia
aliboresha makazi yaliyomsaidia kudhibiti hali ngumu ya hewa.
Mfano ni katika zama hizi ambapo binadamu huyu aliweza kukopa ujuzi na kujifunza
kutatua matatizo mbalimbali kwa kushirikiana na jamii zilizomzunguka na zilizomabli
na mazinigra yake. Hii ilileta maana hasa katika kukusanya taaluma na ujuzi kutoka
sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuvumbua mambo mbalimbali.
mapinduzi ya mawasiliano(3)
1) Zama za alama na ishara (3)
Kwa hiyo mawasiliano yalikuwa mepesi kidogo. Ni katika zama hizi Binadamu hawa
walianza kutumia moshi na moto kuwasiliana japo haikurahisisha pia ugumu wa
mawasiliano.
Ni katika zama hizi binadamu aliweza kuchora picha za binadamu na wanyama kwa
kutumia mawe, pembe, mifupa na michoro mbalimbali wenye kuta za mapango
walimokua wakiishi. Miongoni mwa michoro hiyo iliweza kupatikana katika nchi za
dunia ikiwemo ufaransa na Hispania.
Katika kipindi hiki binadamu aliweza kutengeneza nguo zake kwa kutumia ngozi za
wanyama mbalimbali. Lakini pia walitengeneza vyungu kwa kutumia udongo na kwa
kuvikaza kwa kutumia moto. Pamoja na hayo yote jambo kubwa la uvumbuzi katika
zama hizi ilikua uchoraji na upakaji wa rangi katika mapango yao.
Binadamu wa zama hizi alikua na fuvu la kichwa, ulimi na kibox cha sauti kama
alivyo binadamu wa leo. Kwa hiyo matamshi uwezo wa kuongea katika lugha fasaha
kama ilivyo leo inakadiliwa kuwa ni miaka 35,000 mpaka 40,000 iliyopita. Masalia
baadhi yamekutwa katika nchi ya uhoranzi . binadamu wa zama hizi masalia
yanaonyesha alikua na nguvu na ujasiri wa kupambana na hali yake.
Wakati haya yote yakitokea lugha iliendlea kukua na kustawi zaidi. Binadamu alianza
kwenda maeneo mbalimbali kujifunza lugha tofauti na kukuza lugha zao kupitia
muingiliano wa jamii tofauti.
Walizalisha maneno na tarakimu lakini pia walianza kujiwekea utaratibu wa namna ya
kuishi katika makundi yao hii ilikuza sana lugha zao. Kupitia sheria walizojiwekea
ilipunguza sana binadamu hawa kuzunguka badala yake walianza kujenga makao ya
kudumu katika maneo yao. Kitu cha muhimu katika zama hizi lugha ilikua muhimu na
ilisaidia kubadili namna ya kuishi kutoka katika uwindaji na maisha ya kuzumguka
kutafuta Chakula na kufikia katika hatua kubwa ya kujitambua.
Wakati lugha haipo haikua rahisi ata kidogo kudhibiti mienendo na maisha ya watu
katika mazingira walimokua wak,iishi.
Faida kubwa yah ii teknologia ni kwamba michoro hii ilikuwa ya kudumu kwa kua
haikua rahisi kuharibu na kubomoa vipande hivyo vya udongo na mawe kwa kuwa
vilitengenezwa vikiwa imara sana. Pamoja na kujitahidi kuviweka katika hali ya
udogo lakini kubeba vipande vya mawe vilivyo andikwa na kuchorwa haikua kazi
rahisi kwa binadamu wa wakati huo.
Ili kuepuka hilo jambo Wamisri wakagundua magome ya miti aina ya papyrus ambayo
ilikua imara na bora kwa ajili ya kubebea maandishi hayo hiyo ilikua miaka 2500 BK.
Pia ilikua rahisi sana kuandika katika karatasi zile kwa kua walitumia manyoya na
wino na iliokoa muda kwa kua kuandika katika karatasi/gome ilikuwa ni rahisi zaidi
kwa kua mwandishi angeweza kulinyoosha na kuandika kwa urahisi.
Utengenezaji wa karatasi kwa mala ya kwanza ulifanyika katika ghuba yam to Nile
baada ya kukutwa miti mingi sana aina ya PAPYRUS. Gome safi lilichunwa kutoka
katika shina la mti huuo na kasha kulazwa chini yakiwa magome mengi kupondwa ili
kuondoa takataka mpaka kutengenezwa moja katika magome mengi.