Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari - Anuai Za Jamii Morogoro

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Nukushi: +255 (026) 2963629 na Utawala Bora,
Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la Taaluma Na. 1,
Tovuti:http://www.utumishi.go.tz Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
18 Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.

TAARIFA KWA UMMA

AFYA ZA WATUMISHI ZIZINGATIWE ILI KUBORESHA UTENDAJI

Waajiri nchini wameelekezwa kuzingatia afya bora za watumishi katika


taasisi zao kwani watumishi ndio nguvu kazi ambayo inawezesha shughuli
kufanyika kwa ufasaha na kuleta tija kwa maendeleo ya taifa.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Anuai za
Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Bi. Leila Mavika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Kitaifa
inayosimamia utekelezaji wa shughuli za VVU, UKIMWI na Magonjwa
Sugu Yasiyoambukizwa (MSY) mahala pa kazi wakati wa kikao kazi cha
kamati hiyo mjini Morogoro.
Bi. Mavika amesema kuwa, kikao kazi hicho kimelenga kubadilishana
taarifa, kutathmini hali halisi ya utekelezaji wa AFUA za UKIMWI mahala
pa kazi, pamoja na kubuni mikakati itakayowezesha Taasisi za
Umma kutekeleza kisheria mwongozo na waraka unaohusu utoaji wa
huduma kwa watumishi wanaoishi na VVU na UKIMWI mahala pa kazi.
Bi. Mavika ameongeza kuwa, Serikali kupitia Ofisi ya Rais-Utumishi, imetoa
miongozo mbalimbali ikiwemo Mwongozo wa Kudhibi VVU, UKIMWI na
Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahala pa kazi katika Utumishi wa
Umma wa mwaka 2014 unaoelekeza utaratibu na usimamizi wa masuala
ya UKIMWI mahala pa kazi.

1
Aidha, Bi. Leila amesema, Serikali imetoa Waraka wa Utumishi Na. 2 wa
mwaka 2014 kuhusu Kudhibiti Virusi vya UKIMWI, UKIMWI na Magonjwa
Sugu Yasiyoambukizwa mahala pa kazi katika Utumishi wa Umma, waraka
huo unawaelekeza waajiri namna ya kutoa huduma kwa watumishi
wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Kwa Upande wake, Katibu wa Kamati hiyo Tendaji ya Kitaifa ambaye pia ni
Afisa Mwitikio wa taasisi za Umma kutoka TACAIDS, Dkt. Ameir Hafidh
amesema kuwa, jukumu lake kubwa ni kuhakikisha suala la
UKIMWI sehemu za kazi katika sekta ya Umma linazingatiwa kwa mujibu
wa Mwongozo na Waraka husika.
Dkt. Hafidh amesisitiza kuwa ni jukumu la mwajiri kuhakikisha anampatia
huduma stahiki mtumishi anayeishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI
mara baada ya kujiweka wazi kwa mwajiri.
Wajumbe wa Kamati Tendaji Kitaifa wanaoshiriki katika kikao hicho ni
kutoka Ofisi ya Rais-Utumishi, Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI
(TACAIDS), Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania (TPSC), Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Tume ya
Utumishi wa Umma Tanzania na Taasisi ya Chakula na Lishe.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 10 MEI, 2018

You might also like