Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 64

Sauti ya Ilala

TAHARIRI
Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini Tanzania zipo kwa mujibu wa Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 145. Kwa
kutambua umuhimu wa vyombo hivi Serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua
hatua mbalimbali za kuziboresha. Hata hivyo maboresho yaliyochukuliwa na
Serikali ya Awamu ya Tano nchini yameendelea kuzipa nguvu zaidi Mamlaka
hizi kujiendesha.
Sote kwa pamoja tumeshuhudia ufanisi wa utekelezaji wa maagizo mbalimbali
yaliyotolewa. Toleo hili linaanisha baadhi ya maeneo kati ya mengi ambayo
yamefanyika Katika Manispaa ya Ilala kwa kipindi cha takribani miaka miwili
na nusu 2015 hadi Juni 2018 katika Sekta za huduma za Jamii ikiwemo
ongezeko la uandikishaji wa Wanafunzi katika shule za msingi sambamba na
kuboresha miundombinu ya Elimu, Huduma za Mama na Mtoto, Afya,
Uanzishaji wa Viwanda vidogovidogo, Ujenzi wa Barabara katikati ya Mji,
Matumizi ya Mifumo ya Kielektroniki katika kukusanya maduhuli ya Serikali
Uboreshaji wa miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam unaojumuisha
upendezeshaji wa mandhari pamoja na Usafi wa Mazingira.
Agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Hassan Suluhu kuhusiana na mazoezi ya viungo kwa Watumishi limetekelezwa
kikamilifu katika Manispaa ya Ilala. Badala ya kufanyika Jumammosi ya Pili ya
kila mwezi Watumishi wameamua kufanya mazoezi hayo mara tatu kwa kila
wiki hii inatokana na manufaa yatokanayo na mazoezi hayo. Si wao tu utaratibu
huo umeweza kuvuta Watumishi wengine kutoka Taasisi za Serikali zilizopo
karibu na Ofisi za Mnispaa ya Ilala. Hongera Makamu wa Rais kwa kuliona hili
la afya za Watumishi.
Pongezi pia zinaelekezwa kwa Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
(Madiwani) ambao wamekuwa wakishirikiana na Watendaji kuhakikisha
maelekezo na maagizo ya Serikali yanatekelezwa.

Bodi ya Uhariri
Bibi Tabu F. Shaibu Wajumbe Mhariri Mshauri
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Neema Njau Said Mwishehe
Habari, Mawasiliano, Habari na Hashim Jumbe Msanifu Kurasa
George Mwakyembe NPC - KIUTA
Uhusiano
Mchapishaji
(Mwenyekiti) NPC - KIUTA

1
Sauti ya Ilala

Meya Kuyeko:Tumefanikiwa kudhibiti mapato ya Manispaa

Tumeboresha huduma.

Mhe. Charles Kuyeko - Mstahiki Meya Halmashauri ya Manispaa


ya Ilala

Na Simon Nyalobi

Manispaa ya Ilala, ni miongoni mwa Manispaa tano za Jiji la Dar es Salaam,


ambayo inategemewa kuwa ni kitovu cha uchumi wa jiji hilo na nchi kwa
ujumla.

Kwa sasa Baraza la Madiwani wa Manispa ya Ilala, limetimiza takribani miaka


miwili na nusu tangu madiwani hao waingie madarakani mwaka 2015.

2
Sauti ya Ilala

Moja ya Kikao cha Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Katika kipindi hicho baraza la madiwani la Manispaa hiyo, linajivunia kuleta


maendeleo.

MEYA wa Manispaa ya Ilala, Mhe Charles Kuyeko, anaeleza katika kipindi cha
takribani miaka miwili na nusu, Manispaa hiyo imefanikiwa kusimamia katika
maeneo tofauti ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

Kuyeko anasema matumizi ya mashine za kieletroniki (EFD), katika ukusanyaji


wa mapato kumesaidia kudhibiti ubadhirifu na upotevu wa fedha za Manispaa
hiyo.

Anaeleza Manispaa hiyo iliamua kutumia mashine hizo, baada ya kujua faida
zake katika udhibiti wa mapato katika taasisi za umma na binafsi.

“Kupitia mashine za kieletroniki, tumehakikisha kila mapato yetu yanayoingia


katika Manispaa tunayaona na mashine hizi zimeongeza uwazi katika
makusanyo yetu.

3
Sauti ya Ilala
“Tunahakikisha hakuna fedha yoyote inayotumika bila ya kupitishwa na kamati
ya Fedha na Utawala na hatimaye katika Baraza la Madiwani,”anasema.

Meya huyo wa Manispaa ya Ilala, anatolea mfano makusanyo ya mapato ya


machinjio ya Vingunguti, ambayo yameongezeka baada ya kuanza kutumika
kwa mashine hizo.

Anafafanua kuwa, baada ya kuanza kutumiwa kwa mashine hizo kwa kipindi
cha mwaka wa fedha 2015/16 mapato yalipanda kufikia milioni 80 hadi 85,
ambapo kabla ya matumizi ya mashine yalikuwa milioni 15 hadi 20.

Akizungumzia mwenendo wa ukusanyaji wa mapato katika Manispaa hiyo,


anasema Manispaa imekuwa ikiongeza malengo ya ukusanyaji kila mwezi
ambapo kipindi cha bajeti ya mwaka 2015/16 na mwaka 2016/17.

Kwa mujibu wa Kuyeko, Manispaa ya Ilala, imepata hati safi kutoka kwa Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa kipindi cha mwaka 2016/17, baada
ya kufanikiwa kupata hati hiyo kwa kipindi cha mwaka 2015/16.

Anaeleza matarajio ya kupata hati safi hiyo, ni kutokana na matumizi mazuri


na usimamizi wa mapato yanayoingia katika Manispaa hiyo.

Huduma za Kijamii
Akizungumzia utoaji wa huduma za jamii, alisema kuwa katika Manispaa hiyo
umeboreka na kurahisishwa zaidi.

Kulingana na maelezo yake, kwa sasa wako katika mchakato wa kuanzisha


vituo vya huduma kwa wakazi hao, ili kuwarahishia kupata huduma za malipo
bila matatizo.

4
Sauti ya Ilala
“Vituo hivi vitakuwa na ofisi zote, kutakuwa na ofisi ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), benki mbalimbali na ofisi zetu za Manispaa, hii itampungizia
gharama za muda na fedha mfanyabiashara kufika Manispaa.

“Pia kwa utaratibu huu, tutaondoa wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa


kukwepa usumbufu wa mizunguko isiyokwisha kulipia huduma katika ofisi za
serikali,”anasema.

Anaeleza hatua hiyo, itasaidia kupunguza msururu wa wananchi kuja katika


ofisi ya meya kuwasilisha malalamiko yao.

Miundombinu
Kuhusu ujenzi wa miundombinu, anasema manispaa imefanikiwa kujenga
barabara za lami zenye urefu wa Kilomita 4.6 kutoka Segerea hadi Bonyokwa
na Mombasa hadi Moshi Bar.

Pia, anasema inaendelea kujenga barabara za ndani za kiwango cha udongo


Katika Kata ya Gongo la Mboto na Ukonga, barabara ya Majichumvi
inayounganisha hadi Kimara, katika Manispaa ya Ubungo, huku barabara za
changarawe zikijengwa katika kata zote 36 za manispaa hiyo.

Katika elimu, anasema wamefanikiwa kulitekeleza agizo la Rais Dk. Dk. John
Magufuli, la kutaka shule ziwe madawati ya kutosha na kuongeza ujenzi wa
vyumba vya madarasa.

“Sisi tulienda mbali zaidi ya agizo la Rais Magufuli, tuliona hatuwezi kutengeneza
madawati pekee yake bali kujenga na madarasa, tulijua kutakuwa na ongezeko
la wanafunzi kutokana na elimu kuwa bure,”anasema.

Ni dhahiri uongozi wa Manispaa ya Ilala umedhamiria kutatua kero za wananchi


pamoja na kuboresha huduma za jamii, kupitia makusanyo kutoka katika
vyanzo vyake vya mapato.

5
Sauti ya Ilala
Hivyo, wananchi wa manispaa hiyo, ni budi kuwaunga mkono viongozi wao
katika dhamira hiyo, ili kuipaisha manispaa hiyo kiuchumi.

SERA YA ELIMU BILA MALIPO NI DARAJA LA MAFANIKIO KWA


MTOTO MNYONGE, JAMII ISHIRIKI KUMVUSHA

Na: Hashim Jumbe

Katika kipindi cha takribani miaka miwili na nusu cha Serikali ya Awamu ya
Tano, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, mambo
mbalimbali ya kimaendeleo yameendelea kutekelezwa kama yalivyoainishwa
kwenye Mkakati wa Taifa wa kuinua Uchumi, huku Sekta ya Elimu ikiwa ni
moja ya Sekta zilizopewa kipaumbele katika ustawi wa Taifa la Tanzania.

Katika hilo, ipo Miongozo na Nyaraka za Elimu inayoelekeza utoaji wa Elimu


bila malipo kama moja ya ahadi ya Mheshimiwa Rais Magufuli wakati wa
kampeni mwaka 2015, kwa maana hiyo Elimu bila malipo ilianza rasmi
mwaka 2016 ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya
mwaka 2014 na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015

Sera hiyo ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 imetamka kuwa Serikali


itahakikisha Elimu msingi (Elimu ya Awali hadi Kidato cha Nne) inakuwa ya
lazima na bure kwenye Shule za Umma.

Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Ufundi ilitoa
Waraka wa Elimu namba 5 wa Mwaka 2015 ambao unafuta ada kwa Elimu ya
Sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne kwa Shule za Umma na
michango yote katika Elimu msingi, hivyo basi, Waraka huu unafuta Waraka
namba 8 wa Mwaka 2011 kuhusu michango Shuleni.

Aidha, Waraka huo wa Elimu namba 5 unafafanua kuwa “Serikali imeamua


kutoa Elimu msingi (kuanzia Elimu ya Awali hadi Kidato cha Nne) bila malipo.
Azma hii ya Serikali ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya
Mwaka 2014 ambayo ina lengo la kuhakikisha kwamba Watoto wa Kitanzania
wenye rika lengwa la Elimu msingi wanapata elimu bila kikwazo chochote
ikiwemo ada au michango”

6
Sauti ya Ilala
Kuanza kwa utekelezaji wa Elimu msingi bila malipo, Manispaa ya Ilala kupitia
Idara ya Elimu Msingi imefanya jitihada mbalimbali za kuboresha Sekta hiyo
ili kutoa wigo mpana wa upatikanaji wa Elimu iliyo bora kwa kuboresha
Mazingira ya kujifunzia kwa Wanafunzi kwa maana ya kuongeza nyenzo muhimu
katika Miundombinu na Samani, mfano: vyumba vya Madarasa, matundu ya
vyoo, Ofisi na Madawati.

Aidha, maboresho hayo yameenda sambamba na ongezeko kubwa la


Wanafunzi kutokana na muitikio wa Sera ya Elimu bila malipo ambapo
uandikishaji wa Wanafunzi wa darasa la kwanza umeongezeka kutoka
Wanafunzi 21,798 walioandikishwa mwaka 2015 hadi Wanafunzi 28,838
waliondikishwa mwaka 2016 ikiwa ni tofauti ya Wanafunzi 7,040 sawa na
ongezeko la 24.4%, huku idadi ya Wanafunzi kwa ujumla ikiongezeka kutoka
150,826 waliokuwepo mwaka 2015 hadi 163,946 kwa mwaka 2016 sawa na
ongezeko la 8% .

Ongezeko hilo la Wanafunzi limeleta chachu kwa Idara ya Elimu Msingi


Manispaa ya Ilala na kupelekea kufanyika jitihada mbalimbali ili kukabiliana
na hali hiyo, jitihada hizo ni pamoja na kuanzisha kampeni maalum za kuchangia
elimu kwa kushirikisha Wadau mbalimbali wa elimu, huku kampeni hizo zikianzia
ngazi ya Wilaya, Mkoa na Kitaifa.

Mpango wa ugawaji wa Madawati uliozinduliwa na Mheshimiwa Rais Julai 13,


2016 kutoka kwenye fedha iliyobanwa matumizi ya Bunge ulizidisha hamasa
ya kampeni ya uchangiaji Madawati kwa Manispaa ya Ilala hivyo kufanikisha
upatikaji wa Madawati 22,403 kati ya hayo Madawati 1,694 yalitoka katika
Mfuko wa Jimbo (Majimbo matatu ya Ilala, Ukonga na Segerea).

Isitoshe Madawati 2,282 yalitoka kwa Wafadhili ambao ni PEPSI, EWURA,


TRA, CRDB, NMB, Jamani Foundation na wengineo. Madawati 1,611
yamepatikana kutoka Serikali Kuu na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
imetengeneza Madawati

7
Sauti ya Ilala

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mbunge
wa Jimbo la Ilala Mh. M.A. Zungu Madawati yaliyotolewa na Ofisi ya Bunge kwa niaba ya
Wabunge waliopata mgao huo katika awamu ya kwanza.

Idadi hiyo ya Madawati ni ongezeko la 38.2% kutoka kwenye idadai ya


Madawati 36,196 yaliyokuwepo kabla ya Novemba 2015, hivyo kufanya idadi
ya Madawati kufikia 58,599 ambapo kwa uwiano wa dawati moja kwa
Wanafunzi watatu.

8
Sauti ya Ilala

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo
na baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge wakati wa hafla ya utoaji Madawati
kwa Waheshimiwa Wabunge kwa ajili ya Shule zilizopo kwenye Majimbo yao.

Jitihada nyengine zilizofanyika ni Ujenzi wa Shule mpya, Jumla ya Shule mpya


Kumi (10) zilijengwa kama ifuatavyo:- Shule ya Msingi Gogo, Mzinga II, Misitu,
Serengeti, Kinyerezi Jica, Mafanikio, Yangeyange, Mgeule, Kichangani na
Pugu Bombani.

Aidha, hadi kufikia mwaka 2018 Shule mpya mbili zilijengwa kutokana na
fedha za Ruzuku zilizotolewa na Mhe. Rais Magufuli, Shule hizo ni Shule ya
Msingi Maghorofani na Lubakaya, nazo zimesaidia sana kupunguza
msongamano wa Wanafunzi darasani na kupunguza Wanafunzi kutembea
muda mrefu kufuata Shule.

9
Sauti ya Ilala

Shule ya Msingi Maghorofani ni moja kati ya Shule mpya zilizojengwa kutokana na fedha
za Ruzuku zilizotolewa na Mhe. Rais John Magufuli.

Kwa Mwaka 2018, bado ongezeko la uandikishaji Wanafunzi limekuwa kubwa


zaidi tofauti na makadirio ya awali. Aidha kumekuwa na wimbi kubwa la
Wanafunzi wanaohamia kutoka Shule zisizokuwa za Serikali, hali hiyo
imepelekea Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuendelea kujenga Shule mpya
nne (4) katika Kata za Chanika-Kidugalo, Buyuni-Zavala, Pugu-Kinyamwezi
na Majohe-Uamuzi, lengo kubwa likiwa ni kupunguza msongamano wa
Wanafunzi katika Shule za Serikali.

Sambamba na hilo, vyumba vya Madarasa 28 vimejengwa kupunguza


msongamano wa Wanafunzi darasani, matundu 176 ya vyoo yamejengwa ili
kuboresha Afya za Wanafunzi Shuleni.

Ukarabati wa vyumba vya Madarasani umefanyika ili kuboresha mazingira ya


kujifunzia kwa Shule za Mchikichini na Kinyerezi, ukarabati unaendelea Shule
za Ilala na Msimbazi.

10
Sauti ya Ilala
Nini maaana ya Elimu msingi bila malipo?

Utoaji wa Elimu msingi bila malipo una maana ya kwamba Mwanafunzi atasoma
bila Mzazi/ Mlezi kulipa ada wala michango ya fedha iliyokuwa ikitozwa Shuleni
kabla ya kotolewa kwa Waraka wa Elimu namba 5 wa mwaka 2015. Serikali
itagharamia ada ya Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya kutwa na bweni
iliyokuwa inatolewa na Mzazi au Mlezi kwa Shule za Serikali.

Majukumu katika utaratibu wa Elimu msingi bila malipo:

Katika kutekeleza Sera ya Elimu bila malipo, Serikali kupitia Waraka wa Elimu
namba 5 wa mwaka 2015 umeelezea nini wajibu wake na majukumu ya Mzazi/
Mlezi katika utekelezaji wake sambamba na majukumu ya Wakuu wa Shule
na Kamati/Bodi za Shule na Jamii kwa ujumla.

Serikali imefafanua kuwa ina wajibu wa kununua Vitabu, Kemikali na Vifaa


vya Maabara, Samani, yakiwemo Madawati, Vifaa vya Michezo, matengenezo
ya mashine na mitambo, kujenga na kukarabati miundombinu ya Shule, kutoa
chakula kwa Wanafunzi wa bweni pamoja na kutoa ruzuku kwa kila Mwanafunzi.

Kwa upande wa Wazazi/Walezi, Waraka umeeleza kuwa wana wajibu wa


kununua sare za shule na michezo, madaftari na kalamu, kugharimia chakula
kwa Wanafunzi wa kutwa, pamoja na matibabu ya Watoto wao, kulipia nauli
ya kwenda na kurudi shuleni, kununua magodoro, shuka na vifaa vya usafi
kwa Wanafunzi wa bweni.

Je, Elimu bila malipo imewakumbuka Wanafunzi wenye mahitaji


maalum?

Katika kuhakikisha kuwa kila Mtoto anapata elimu bila kujali mapungufu yake,
Serikali imenunua vifaa vya kujifunzia kwa Wanafunzi wenye uhitaji maalum
sambamba na vifaa vya kufundishia kwa Walimu wanaofundisha Watoto wenye
mahitaji maalum ikiwa ni kielelezo cha kutimiza ahadi za Mhe. Rais Dkt. John
Pombe Magufuli.

Akikabidhi vifaa vya kufundishia kwa Wanafaunzi wenye mahitaji maalum


vilivyotolewa na Shirika la Global Partnership vyenye thamani ya Shilingi Bilioni
6, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
(Mb) alisema “Vifaa hivi vitakwenda katika Mikoa yote 26 iliyopo Nchini kwa

11
Sauti ya Ilala
ajili ya Wanafunzi wenye mahitaji maalum ambapo itanufaisha Shule za Msingi
213 kati ya Shule 408 na Shule 22 za Sekondari kati ya Shule 43 zenye
Wanafunzi wenye mahitaji maalum”.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Ndugu Msongela Nitu Palela moja ya vifaa vya kujifunzia
kwa Wanafunzi wenye uhitaji maalum kwa Shule ya Uhuru Mchanganyiko.

12
Sauti ya Ilala

Tumeiwezesha Jamii na kuipunguzia Serikali mzigo

NA MWANDISHI WETU

ILALA

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam kupitia Idara ya Ustawi


na Maendeleo ya Jamii imetekeleza jukumu lake la Msingi la kuhakikisha
makundi ya Kijamii yanayopewa kipaumbele na Serikali yanasaidiwa kuweza
kujikwamua katika changamoto zinazowakabili. Makundi hayo yanayojumuisha
Wanawake, Vijana, Watoto na watu wenye ulemavu na Wazee yanamekuwa
yakihudumiwa kwa kufuata miongozo iliyopo.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ustawi wa Jamii na Vijana wa Manispaa


ya Ilala, Bibi Fransisca Makoye katika makala haya anaelezea mikakati
iliyofanywa na Idara yake kuhakikisha wanawakomboa wanawake, vijana na
wazee.

Majukumu ya Idara ya Ustawi wa Jamii

Fransisca anasema idara yake inakazi ya kuiwezesha jamii kupata huduma


kwa kuzingatia mahitaji maalum hasa makundi ya watoto wanaoshi mazingira
hatarishi, wazee, vijana na wanawake.

Anasema katika kutoa huduma hizo wanazingatia umri, jinsia, jinsi ambapo
kazi hiyo inafanywa bila kuzingatia umri, dini, kabila, utaifa wala itikadi yoyote.

Fransisca anasema anashukuru Mungu katika kipindi cha takribani miaka


miwili cha uongozi wa Rais, Dk.John Magufuli (CCM), Idara yake imefanikiwa
kuhudumia wananchi zaidi ya 20,000.

Anasema huduma zilizotolewa ziliwalenga, watoto wanaoishi mazigira hatarishi


ambao 400 walipata vifaa mbalimbali vya shule. Anavitaja vifaa hivyo kuwa ni
begi, karamu ya risasi, peni, madaftari na mkebe.

13
Sauti ya Ilala
Anasema katika mpango huo pia walifanikiwa kutoa elimu ya kisaikolojia kwa
watoto 500 walioathirika na ukatili wa kijinsia, mfano ngoni, kimwili na
kutelekezwa.

” Tunajivunia katika awamu hii tumefanikiwa pia kuwapatia msaada wa kisheria


watoto 200 na kupata mahitaji yao ya msingi,”anasema Fransisca.

Anasema kwa upande wa Wazee wamefanikiwa kuwatambua wazee 10,000


waliopo katika Kata 36 za manispaa hiyo na mpaka sasa wazee 6,200 wamepata
vitambulisho vya huduma mbalimbali ikiwamo afya.

” Wazee hawa wamepatikana ndani ya kata 36 na tunaendelea kuwatafuta


wazee wengine ili waingie katika mpango huu maalum ambao ni utekelezaji
wa Ilani ya CCM,”anasema Fransisca.

Fransisca anasema kwa upande wa watu wenye ulemavu wamefanikiwa


kuwapa elimu ili waweze kutumia fursa na kujikwamua kiuchumi ambapo
albino 50 wamepatiwa vifaa mbalimbali.

” Tumejitahidi kuwashirikisha watu wenye ulemavu kwa kuwapa zabuni


ndogondogo zinazotolewa na Manispaa ikiwamo usimamizi wa Vyoo vya Umma,
mitaji midogomidogo,vifaa vya kujimudu kama kiti cha kukalia,mafuta ya ngozi
ya kupaka watu wenye ualbino na shime ya sikio ya kumuongezea
usikivu,”anasema Fransisca.

Anasema pia vikundi vitatu vyua walemavu vyenye wanachama 15 wamepata


tenda ya vyoo vya umma.

Fransisca anasema pia wanaendelea kutoa elimu na mafunzo kwa kundi hilo
ili waweze kutambua fursa mbalimbali zinazotolewa hapa nchini na Serikali ya
awamu ya tano pamoja na asasi nyinginezo binafsi na za kiserikali.

Bajeti

Anasema katika mwaka wa fedha 2018/2019 Manispaa hiyo imetenga jumla


ya Sh.Bilioni mbili ikiwa ni asilimia mbili ya mapato yake kwa ajili ya
kuwawezesha walemavu kiuchumi ili waweze kuibua viwanda vidogo na
hatimaye waweze kufikia uchumi wa viwanda.

14
Sauti ya Ilala
”Tumelenga kama Idara kulikomboa kundi hili kwa kuhakikisha wanaacha
uchuuzi na badala yake wanakuwa wazalishaji wa bidhaa kubwa wenye viwanda
vidogo vidogo,”anasema Fransisca,
Vijana
Fransisca anasema zaidi ya vijana 1,500 wa manispaa hiyo wamenufaika na
mafunzo ya ujasiriamali na kupata vifaa vya cherehani, fundi uashi na umeme
ambapo mafunzo hayo yametolewa kwa ushirikiano na Shirika la Plan
International.
Pia anasema idara yake imefanikiwa kuzifunga kambi 15 zilizokuwa za dawa
za kulevya na kuunda vikundi vidogo vidogo ambavyo vinajihusisha na shughuli
za manispaa.
Mafanikio
Anasema wamefanikiwa kutoa mikopo kwa vijana zaidi ya 400 kupitia asilimia
10 ya mapato ya ndani ya manispaa hiyo kwa ushirikiano wa benki ya DCB.
Pia wamefanikiwa kuwashirikisha Vijana na Wanawake katika maonyesho
mbalimbali ya Kitaifa.

Vyombo mbalimbali vya Habari vikiwahoji Wajasiriamali katika maonesho ya wajasiriamali


wanawake na vijana yaliyoratibiwa na Manispaa ya Ilala katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

15
Sauti ya Ilala
Mkurugenzi Ilala: Nidhamu ya Kazi imeongezeka
Na mwandishi wetu Ilala

Bw.. Msongela Nitu Palela Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Mageuzi mbalimbali yaliyofanywa katika kipindi cha miaka miwili na nusu ya


Awamu ya tano hayakuacha nyuma eneo la Rasimali watu kutokana na kuwa
ni kiungo muhimu katika kufikia malengo ya Taasisi au Serikali yoyote Duniani.
Kiwango cha mafanikio katika eneo hili hutegemea mambo yafuatayo;
Kujituma, Ubunifu, Uaminifu na Uadilifu Serikali ya Awamu ya Tano ilitoa
maagizo katika eneo hilo Manispaa ya Ilala iliweza kutekeleza kama inaelezwa
katika makala haya.
Je ni kwa vipi agizo la Uhakiki wa Watumishi lilitekelezwa?

Akizungumza na mwandishi wa makala hii Mkurugenzi wa Halmashauri ya


Manispaa ya Ilala Msongela Palela anaeleza yafuatayo; Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala ilifanya zoezi la uhakiki watumishi wake na kubaini watumishi
ambao hawakuwa na sifa za kuwa Watumishi wa Umma katika maeneo ambayo
walikuwa wanatoa huduma. Katika uhakiki huo Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala ilibaini uwepo wa watumishi 357 ambao hawakuwa na sifa zinazohitajika
na tayari walikuwa wameipotezea serikali fedha nyingi, hivyo watumishi hao
waliondolewa kazini.

16
Sauti ya Ilala
Anazungumziaje utoaji wa huduma kwa Wateja/Wananchi?
Mkurugenzi Palela anaeleza kuwa katika kipindi hiki cha takribani miaka miwili
ya Serikali ya awamu ya tano kumekuwa na mabadiliko ya kiutendaji ya namna
watumishi wanavyowahudumia wateja/Wananchi katika sekta zao. Malalamiko
ya wananchi wengi yamepungua wamekuwa wakiridhika na jinsi
wanavyopokelewa na kuhudumiwa. Kila mtumishi amekuwa akijituma katika
eneo lake na kupunguza misururu mirefu ya watu wanaosubiri kuhudumiwa.
Aidha kiwango cha mahudhurio kimeongezeka. Katika kuhakikisha hakuna
udanganyifu wa mahudhurio kwa Watumishi, Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala kwa makusudi kabisa iliamua kufunga mashine za Kielektroniki (Bio-
Metric attendance Register) ambapo mtumishi atasaini wakati anaingia ofisini
na wakati wa kutoka. Hivyo imekuwa viguni mtumishi kudanganya muda ambao
alifika na kuondoka kazini. Aidha uvaaji wa vitambulisho vya Watumishi
unazingatiwa.

Mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw Laurent William Matto akijisajili katika


mashine za Kielektroniki ( Bio-Metric Attendance Register)

17
Sauti ya Ilala
Stahiki za Watumishi
Katika kipindi cha takribani miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya awamu ya
Tano ya Mheshimiwa John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeweza kuboresha stahiki
mbalimbali za Watumishi wake kama vile kulipa nauli za likizo kwa watumishi
wake kwa wakati, kulipa gharama za kuwasafirisha watumishi wake waliostaafu
katika utumishi wa umma kwa wakati. Kiasi cha Sh 917,329,200 zimelipwa
kwa watumishi 474 katika kipindi cha miaka miwili.

Baadhi ya wajumbe wa timu ya Menejimenti wakiwa katika moja ya vikao.

18
Sauti ya Ilala

MRADI WA TASAF WAZIKOMBOA KAYA MASIKINI ILALA


Na George Mwakyembe
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dar es Salaam ni moja kati ya manispaa hapa
nchini ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuzikomboa kaya masikini
kupitia mradi wa TASAF.
Ukweli ni kwamba TASAF imekuwa nguzo ya mafanikio hasa kwenye kuzisaidia
kaya hizo kupitia mradi huo ambao umeleta mabadiliko makubwa kwenye
kaya hizo.
Manispaa ya Ilala ina jumlaya kaya masikini 4670 ambazo hunufaika na
mradi huo. Baadhi ya wanufaika na mradi wamepiga hatua kimaendeleo ikiwa
ni pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo kutokana na kupata
fedha kutokaTASAF.
Fedha ambazo zimekuwa chachu ya kuanzisha maendeleo.Mfano nikuanzishwa
kwa miradi ya ufugaji wa kuku, Ufugaji wa mbuzi, Kilimo cha mboga mboga
na matunda. Fedha hizo hutolewa kila baada ya miezi miwili na zimekuwa na
mafanikio makubwa kutokana na usimamizi unaofanywa na maofisa wa TASAF
kwa kuwasimamia walengwa kwa ukaribu ili wanafaika kutimiza malengo.
Mbali ya kuwepo na changamoto nyingi lakini maofisa wa TASAF wamekuwa
wakifanya juhudi za kuhakikisha kila anayestahili na mwenye vigezo basi
anaingizwa na kunufaika na mradi huu.
Kulingana na kuendelea kwa haraka kwa sayansi na teknolojia wanufaika
wamekuwa wakipokea fedha zao kupitia huduma ya fedha za simu za mkononi
yaani kwa njia ya M-pesa, Tigopesa, Airtel Money na mitandao mingine ya
aina hiyo.

19
Sauti ya Ilala

Wakazi wa Buguruni Kisiwani wakiwa wanasubiri kupatiwa fedha kutoka kwa maofisa
wa Kwa Manispaa ya Ilala ambapo fedha hutolewa kwa kaya masikini kila baada ya miezi
miwili ili wajikimu na kujikwamua kimaisha.

Mradi huo wa TASAF umeweza kuwainua wanufaika kutoka hatua moja hadi
nyingine hasa kimaendeleo.

Juhudi za TASAF kwenye Manispaa ya Ilala imewafikia idadi kubwa ya wananchi


walio kwenye kaya masikini.

Miongoni mwa wanufaika wa fedha za TASAF kwenye Manispaa ya Ilala ni Bi.


Asha Salumu Mbaruku ambaye nimkazi wa Mtaa wa Markaz Kata ya Ukonga
Manispaa ya Ilala.

Kaya ya Bi. Asha Salumu ina jumla ya watu nane (8) kati ya hao wajukuu ni
watatu (3) ambao wanasoma, mjukuu mmoja anasoma darasa la pili (2), wa
pili anasoma darasa la nne (4) na watatu anasoma darasa la kwanza (1).

Hivyo Kaya ya Bi Ashani ni moja kati ya kaya ambazo zinapokea ruzuku ya


Mpango wa kunusuru Kaya Maskini unaoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (TASAF).

20
Sauti ya Ilala
Asha anapokea Sh.36000 kila baada yamiezi miwili ikiwa ni ruzuku ya msingi,
Sh.10,000) ni ruzuku ya kuwa na wajukuu na Sh.12000 niruzuku ya watoto
wanaosoma Shule ya msingi.

Hakika unapoamua kuisikiliza historia ya Mama huyu toka alivyoingia kwenye


Mpangowa TASAF niya kusisimua naunatamani awe anakusimulia kila wakati.Ni
simulizi ambayo ukiisikiliza unapata funzo kwenye maisha ya kila siku na
mchango wa TASAF kwenye kuleta maendeleo ya watu walio kuwa kwenye
kaya maskini.

Kabla ya kuingizwa kwenye mradi wa TASAF, ulifanyika mchakato wa


kumchambua kama anastahili nakutokana na aina ya maisha aliyokuwa anaishi
alikidhi vigezovya Kaya maskini.

Aliishi kwenye nyumba mbovu ambayo ukuta wake napaa hazikufaa hali
iliyosababisha Serikali kumuamuru ahame kwani alikuwa kwenye eneo hatarishi
kwa maisha yake.

21
Sauti ya Ilala
“Maisha ya wajukuu wake kwenda Shule ni mtihani kwa upande wa mahitaji
kama vile viatu, daftari na sare za shule. Nyumba yangu kipindi hicho ilikuwa
mbovu, ukuta mbovu, paa mbovu hata iliamuriwa nihame.

“Mlo wangu ulikua washida, mavazi ya shida” kiasi kwamba nilikuwa najisikia
vibaya hapa mtaani, nilijiona ni mwenye bahati mbaya kwani hakuna
ambacho kwake kilikwenda vema kwenye maisha yake ya kila siku,”
anasimulia Mama huyo.

Hata hivyo Maofisa wa TASAF wa Manispaa ya Ilala walipomtembelea nyumbani


kwake Desemba mwaka 2017 walimkuta amekarabati nyumba yake upande
mmoja umeisha na kuezeka bati, na upande mwingine bado anaendelea na
ujenzi kwaruzuku ya TASAF anayoendelea kupokea.

Bi. Asha akiwa amesimama pembeni mwa nyumba yake ambayo ameikarabati kwa fedha
za ruzuku kutoka TASAF.

22
Sauti ya Ilala
Muhimu kwa Mama huyo ni kwamba alikuwa na mipango thabiti ya kujikomboa
kutokana na ruzuku anayopokea na haonishida kusema ya moyoni mwake.

Kwa maisha aliyoishi hapo awali mambo yalikuwa hayaendi maana alikuwa
anakula mlo mmoja kwasiku. Hiyo ilinipelekea kukata tama siku zote. Sasa
TASAF imemsaidia kuboresha maisha yake baada ya kufika kwenye mtaa
wake.

MWAKA 2017 ULIVYOBEBA MAFANIKIO IDARA YA ELIMU MSINGI


MANISPAA YA ILALA

 SHULE ZA ILALA MJINI ZASHIKA NAFASI YA NNE KITAIFA KWA


UBORA WA UFAULU

 SHULE ZA ILALA VIJIJINI NAZO ZAPANDISHA UFAULU KUTOKA


NAFASI YA 77 KWA MWAKA 2016 HADI NAFASI YA 31

 WANAFUNZI WOTE WALIOFAULU WAINGIA KIDATO CHA


KWANZA MWAKA 2018

Na: Hashim Jumbe

Shule za Msingi za Manispaa ya Ilala, zimeibuka kidedea kwenye matokeo ya


Mtihani wa Taifa wa darasa la Saba uliofanyika Nchini kote kuanzia tarehe 06
hadi 07 Septemba, 2017, Shule hizo zilizogawanywa kwenye Wilaya mbili za
Mitihani ambazo ni Wilaya ya Ilala Mjini na Wilaya ya Ilala Vijijini, zimefanya
vizuri kwa kupandisha ufaulu ukilinganisha na Matokeo yalivyokuwa kwa
mwaka 2016.

Matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)


yameonesha Shule za Msingi Wilaya ya Ilala Mjini kushika Nafasi ya nne (4)
Kitaifa kwa ubora wa ufaulu kwa kufuata mpangilio wa Halmashauri, ambazo
Jumla yake ni 186, ambapo Wilaya ya Ilala Mjini imepanda juu kwa Nafasi 13
za Ufaulu kutoka Nafasi ya 17 waliyokuwa kwenye Matokeo yaliyopita, huku
ikiwa ndiyo Wilaya yenye idadi kubwa ya Watahiniwa ukilinganisha na
Halmashauri nyengine.

23
Sauti ya Ilala
Aidha, Shule zilizoshiriki kwenye Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi kwa
mwaka 2017 kwa Wilaya ya Ilala Mjini, Jumla yake ni 112 zilizokuwa na idadi
ya Watahiniwa 12,841 waliosajiliwa kufanya Mtihani huo, kati yao Wavulana
wakiwa 6,181 na Wasichana ni 6,660, huku waliofanya Mtihani huo Jumla
yake ni 12,778 kati yao Wavulana wakiwa ni 6,145 na Wasichana ni 6,633

Wakati wa kutangazwa kwa Matokeo hayo, Watahiniwa waliofaulu Mtihani


Jumla yake walikuwa ni 11,815 sawa na 92.46% ikiwa ni ongezeko la 5.44%
kutoka 87.02% ya ufaulu wa mwaka 2016, ambapo kwa mwaka 2017 Wavulana
waliofaulu ni 5,725 sawa na 93.17% na Wasichana 6,090 sawa na 91.81%.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Eng Stella Manyanya akiongea
na Wanafunzi wa shule ya Msingi Olympio katika kuwahamasisha kufanya kusoma kwa
bidii

24
Sauti ya Ilala
Kwa upande wa Wilaya ya Ilala Vijijini, Shule zilizoshiriki kwenye Mtihani wa
kumaliza Elimu ya Msingi kwa mwaka 2017 Jumla yake ni 72, zilizokuwa na
idadi ya Watahiniwa 8,863 waliosajiliwa kufanya Mtihani, kati yao Wavulana
wakiwa 4,097 na Wasichana ni 4,766, huku waliofanya Mtihani huo wakiwa ni
8,791 kati yao Wavulana ni 4,059 na Wasichana ni 4,732.

Pamoja na changamoto mbalimbali zinazozikabili Shule zilizopo Wilaya ya


Ilala Vijijini ikiwa ni pamoja na muitikio hafifu kutoka kwa Wazazi hususani
kwenye ufatiliaji wa Maendeleo ya Wanafunzi, lakini bado kumekuwa na jitihada
mbalimbali kutoka kwa Walimu pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa
ya Ilala zilizopelekea kupanda kwa ufaulu kutoka Nafasi ya 77 waliyokuwa
mwaka 2016 hadi Nafasi ya 31 kwa mwaka 2017.

Jitihada zilizowekwa zimepelekea Wanafunzi 7,421 kufaulu Mtihani huo ikiwa


ni sawa na 84.42% ambapo Wavulana waliofaulu ni 3,474 sawa na 85.59%
na Wasichana ni 3,947 sawa na 83.41% ufaulu huo ukiwa ni ongezeko la
jumla la 11.31% tofauti na matokeo yaliyopita ambayo yalikuwa ni 73.11%

Kwa kuzingatia utaratibu uliopo, jumla ya Wanafunzi 19,236 wamechaguliwa


kujiunga katika shule za Sekondari za Serikali na hakuna Mwanafunzi hata
mmoja aliyefaulu ambaye hakupangiwa shule, ambapo kwa Manispaa ya Ilala;
Ilala Vijijini 7,421 na Ilala Mjini 11,815

Aidha, pamoja na uwepo wa Wilaya mbili za Mtihani kwa Shule za Manispaa


ya Ilala, lakini pia utolewaji wa Matokeo umegawanywa kwenye makundi
mawili ya Watahiniwa ambayo ni Kundi lenye Wanafunzi zaidi ya Arobaini
(+40) na kundi lenye Wanafunzi chini ya Arobaini (-40)

Kwa Wilaya ya Ilala Mjini, Shule zilizokuwa na Watahiniwa zaidi ya Arobaini


(+40) zilikuwa Shule Tisini (90) Kwenye Kundi hilo, Shule Kumi (10) bora
zilizofanya vizuri ni hizi zifuatazo;

25
Sauti ya Ilala
Nafasi Shule Nafasi Shule
1 Tusiime 6 Kipawa Liberman
2 St. Joseph Millenium 7 Mtendeni
3 Genius King 8 Zanaki
4 Heritage 9 St. Therese
5 Havard 10 St. Mary’s
Aidha, zipo Shule ambazo zilikuwa na Watahiniwa chini ya Arobaini (-40) kwa
Wilaya ya Ilala Mjini, Shule hizo Jumla yake ni Ishirini na mbili (22), hivyo
Shule Kumi (10) bora zilizofanya vizuri ni hizi zifuatazo;
Nafasi Shule Nafasi Shule
1 Fontain Gate 6 Bariadi
2 Lusasaro 7 ACCT
3 ABC-Capital 8 Montesori Msimbazi
4 Agnes Michael 9 Patmo
5 Sabisa 10 Andrews
Kwa upande wa Wilaya ya Ilala Vijijini Shule zilizokuwa na Watahiniwa zaidi
ya Arobaini (40+) zilikuwa Hamsini na Moja (51) Katika kundi hilo, Shule
Kumi (10) bora zilizofanya vizuri kwenye kundi hilo ni hizi zifuatazo;
Nafasi Shule Nafasi Shule
1 Macedonia 6 Zabikha
2 Bati valley 7 Michael Mausa
3 Green hill 8 Daddy
4 Masaka 9 Nyamata
5 Benedict 10 Blessed Hill
Shule zilizokuwa na Watahiniwa chini ya Arobaini (-40) kwa Ilala Vijijini zilikuwa
Ishirini na Moja (21) Kwenye shule hizo, Shule Kumi (10) bora zilizofanya
vizuri kwenye kundi hilo ni hizi zifuatazo;
Nafasi Shule Nafasi Shule
1 Nyiw a 6 G i se la
2 Full Gospel 7 Erimelinda
3 Upendo Montessori 8 Heroes
4 Rosalia 9 Kwila
5 Holy Family 10 Trinity
Ukiondoa Matokeo ya Jumla kwa Shule za Manispaa ya Ilala, ndani yake zipo
Shule za Serikali zilizofanya vizuri ambazo zipo katika kundi lililohusisha
Watahiniwa zaidi ya (+40) kwa Shule Kumi (10) za Wilaya ya Ilala Mjini
zilizofanya vizuri ni hizi zifuatazo;
26
Sauti ya Ilala
Nafasi Shule Nafasi Shule
1 Mtendeni 6 Msimbazi
2 Zanaki 7 Mkoani
3 Kiwalani 8 Maktaba
4 Msimbazi Mseto 9 Hekima
5 Lumumba 10 Ukonga Jica
Shule nyengine za Serikali zilizofanya vizuri ambazo zipo katika kundi
lililohusisha Watahiniwa chini ya (-40) kwa Shule za Ilala Vijijini ni hizi zifuatazo;
Nafasi Shule Nafasi Shule
1 Kiyombo 6 Kinyerezi Jica
2 Kig e z i 7 K in yerezi
3 Kibog a 8 K iv u le
4 Mafanikio 9 Kilimani
5 G ogo 10 B u yu ni

TAARIFA ZA WALIPA KODI ZABORESHWA


Na: Mwandishi wetu Ilala
Mweka Hazina wa Manispaa ya Ilala Tulusubya Kamalamo anaeleza kuwa
katika kipindi cha kuanzia 2015 hadi 2018 Manispaa imehakikisha makusanyo
ya mapato ya ndani yanakusanywa ipasavyo na kutumika kwa mujibu wa
kanuni na taratibu za fedha. Anaendelea kueleza kuwa Manispaa ya Ilala
imeendelea kuhuisha taarifa za walipa Kodi ili kuweza kuwafikia kwa urahisi.
Anaongeza kuwa matumizi ya Mifumo ya Kielektroniki yanasaidia kuwa na
taarifa za walipa kodi kwa usahihihali inayowezesha kuwasiliana kwa karibu
zaidi na walipa kodi hao. Kwasasa Manispaa ya Ilala imeanzisha Kitengo maalum
kinachowajibika na uingizaji wa taarifa zote za walipa kodi.

Bw Tulusubya Kamalamo Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara

27
Sauti ya Ilala

Usahihi wa Taarifa za Walipa Kodi


Akifafanua usahihi wa taarifa za walipa kodi Kamalamo anasema siku za
nyuma walipa kodi wengi walikuwa wakitoa taarifa zisizo sahihi wakilenga
kukwepa kodi. Anaendelea kueleza kwamba mfumo umesaidia katika uwekaji
wa kumbukumbu sahihi wa walipa kodi na mapato yanayokusanywa kila siku
yaani (Data Base). “Kwa kuwa na kumbukumbu sahihi kunasaidia kufuatilia
kwa karibu zaidi mwenendo wa mlipa kodi husika tofauti na siku zilizopita
mbapo wahusika washindikana kupatikana kutokana na taarifa zilizokuwa si
sahihi hususan eneo la anuani.Tumelenga kuwafikia walipa kodi wote katika
Manispaa ya Ilala” anasema
Ili kupunguza utegemezi wa Ruzuku kutoka Serikali Kuu Manispaa imebuni
vyanzo vipya ikiwemo miradi ya uwekezaji. Akitaja vyanzo hivy amesema
miradi ya ujenzi wa masoko ya Kisutu, Ilala, Buguruni na Machinjio ya
Vingunguti itakapokamilika mapato ya Manispaa yataongezeka kwa asilimia
50.
Akizungumzia kanuni na taratibu za fedha anasema Manispaa imechukua
hatua ya kuboresha sheria ndogo za Halmashauri zinazohusu ukusanyaji wa
mapato. “Tunaboresha sheria ndogo za mapato ili ziendane na hali halisi
lakini pia ziwe zinazotekelezeka” anasema Kamalamo.
Elimu kwa Mlipa Kodi
Kamalamo anasema eneo lingine lililopewa kipaumbele katika kipindi hiki cha
2015 hadi 2018 ni elimu ya mlipa kodi ambapo vipindi mbalimbali vya redio
vimefanyika kwa lengo la kutoa ufafanuzi kwa walipa kodi. Sambamba na
vipeperushi njia nyingine iliyotumika ni gari la matangazo kwa ajili ya
kuwakumbusha walipa kodi vipindi vya ulipaji wa kodi.

28
Sauti ya Ilala

HABARI KATIKA PICHA

Rais wa shirika la KOICA Mi-Kyung Lee (katikati) ,akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Mhe Paul Makonda, na Viongozi wengine wakiwa katika hafla ya kukata utepe
kuashiria kuzinduliwa kwa Hospitali ya mama na mtoto Chanika iliyopo katika Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala.

Hospitali ya mama na mtoto Chanika iliyojengwa kwa ufadhili wa shirika la KOICA

29
Sauti ya Ilala

Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Selemani Said Jaffo akiwa katika Ziara ya ukaguzi wa athari
zilizosababishwa na mvua zilizonyesha Jijini Dar es Salaam katika picha ni moja ya eneo
lililoathiriwa eneo la Pugu Mnadani katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Chanika katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakipanda


Mti katika siku ya Uzinduzi wa Upandaji miti iliyofanyika katika eneo la Hospitali ya mama
na Mtoto Chanika.

30
Sauti ya Ilala

Picha ya Pamoja ya Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala


baada ya kumaliza mafunzo ya Uongozi na Utawala Bora yaliyofanyika katika Chuo cha Serikali za
Mitaa Hombolo jijini Dodoma .

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko akizindua rasmi jengo la Ofisi
ya Mtaa wa Mtakuja katika Kata ya Vingunguti.

31
Sauti ya Ilala

Jengo la kutolea huduma ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya Msongola baada ya ukarabati

Barabara ya Segerea Bonyokwa iliyojengwa kwa fedha za ndani (Own Source) kwa
kiwango cha Lami yenye urefu wa Km 2.0

32
Sauti ya Ilala

Madarasa 6 katika Shule ya Sekondari Kasulu yaliyofanyiwa ukarabatiwa na Programu ya


P4R (Program for Result) kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Madarasa matatu yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Karakata kwa ufadhili wa “ Education
Program for Result” (P4R) progamu iliyopo katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

33
Sauti ya Ilala

Madarasa manne yaliyojengwa kwa fedha za mapato ya ndani (own source)


katika Shule ya Msingi Kidugalo iliyopo Kata ya Chanika

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akuzindua huduma ya matibabu bure kwa
Wazee wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, sambamba na mmoja kati ya
wazee waliopatiwa kadi ya huduma ya afya bure akionesha kadi yake

34
Sauti ya Ilala

Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko inavyoonekana kwa sasa baada ya kufanyiwa ukarabati
kwa fedha kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufaundi.

Mradi wa tanki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji yenye ujazo wa lita 150,000 ambalo
litaunganishwa na Miundombinu ya DAWASCO kwa ajili ya kutoa huduma ya maji kwa
Wananchi wa Kata ya Kisukuru.

35
Sauti ya Ilala

Diwani wa Kata ya Ilala, Mhe. Saady Khimji akizindua Mradi wa Maji katika Mtaa wa
Sharifu Shamba, mradi uliojengwa kwa fedha za miradi ya maendeleo LGCDG.

Jengo la Utawala la Mradi wa DMDP katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

36
Sauti ya Ilala

Wenyeviti Kamati za Mitaa wakiwa katika kiapo cha Utii na Uadilifu mara baada ya kuchaguliwa.

Pichani ni viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo (maarufu kwa jina la Wamachinga)


wakiwa katika ofisi yao iliyopo Kariakoo. Huu ni utekelezaji wa kuunga mkono jitihada za
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli za kuinua wananchi
kiuchumi ( hususani vijana) kwa mazingira wezeshi.

37
Sauti ya Ilala

Pichani ni moja ya wafanya biashara ndogondogo waliosajiliwa na kupangwa katika vizimba


wakiendelea na biashara zao katika mitaa ya Kariakoo.

Vijana wakiwa katika jitihada za kujikwamua kiuchumi , wakifanya biashara katika maeneo
yaliyorasimishwa katika mitaa ya Kariakoo.

38
Sauti ya Ilala
WATUMISHI WA MANISPAA YA ILALA WAHAMASIKA NA UTALII WA
NDANI, WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI NA SAADANI
Na: Mwandishi wetu Ilala
Tanzania ni moja kati ya Nchi chache Duniani zilizobarikiwa kwa kuwa na wingi wa
vivutio vinavyowavuta Wageni kuona, kuburudika na kujifunza mambo mbalimbali
yanayoifaharisha Nchi yetu, kama vile uoto wa asili, Milima, Mito, Mabonde pamoja
na hifadhi za Mbuga za Wanyama zinazochagiza ukuaji wa Sekta ya Utalii Nchini.
Lakini pamoja na uwepo wa vivutio vyote hivyo, bado kumekuwa na muitikio hafifu
wa Watanzania wanaotembelea maeneo hayo, ingawaje Serikali imekuwa ikitenga
bajeti kubwa kutangaza maeneo yenye vivutio na kuyaboresha kwa kuweka
Miundombinu bora na ya kisasa ili kuweza kufikika kwa kipindi chote cha mwaka.

Kwa kutambua umuhimu wa maeneo yenye vivutio Nchini mwetu na kuunga mkono
jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kukuza Sekta ya Utalii, ndipo Watumishi
wa Manispaa ya Ilala waliposukumwa na nia ya kutembelea maeneo hayo yenye
vivutio kwa lengo la kujifunza na kujionea ufahari wa Nchi yao ya Tanzania.

Iliwalazimu kusafiri mwendo wa Kilomita 295 kutokea upande wa Magharibi mwa


Jiji la Dar es Salaam huku ikiwachukua wastani wa masaa Matano hadi Sita ndipo
walipoweza kufika kwenye Mbuga ya Mikumi, ambayo ni hifadhi ya Nne kwa ukubwa
wa eneo Nchini Tanzania.

Baadhi ya Watumishi wa Manispaa ya Ilala waliotembelea Mbuga ya Mikumi wakifurahia


picha wakati wa ziara hiyo.

39
Sauti ya Ilala
Kihistoria Mbuga ya Mikumi ilianzishwa mwaka 1964 iliitwa jina hilo kutokea
katika jina la asili la eneo ilipo Mbuga hiyo, ambalo ni ‘Mikumi’ huku Mbuga
hiyo ikiwa na vivutio mbalimbali vya Wanyamapori kama vile; Tembo, Twiga,
Simba, Swala, Nyati na Wanyama wengineo mbalimbali, huku Mbuga hiyo
ikikadiriwa kuwa na ukubwa wa Kilomita za Mraba 3,230.

Katika ziara hiyo, Watumishi kutoka Manispaa ya Ilala walitembelea maeneo


mbalimbali wakiwa kwenye hifadhi ya Mbuga ya Mikumi, huku wakipata pia
fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yaliyowajengea uwezo wa kufahamu
maisha ya viumbe mbalimbali vinavyoishi kwenye Mbuga hiyo, hivyo ziara
hiyo imewazidishia pia ari ya kujivunia Nchi yao na Rasilimali zilizopo

Watumishi wa Manispaa ya Ilala waliotembelea Mbuga ya Mikumi wakiwa kwenye picha ya


pamoja baada ya kufurahia Utalii Mbugani hapo

Azma ya kufanya Utalii wa ndani haikuishia tu kutembelea Mbuga ya Mikumi,


Aidha Watumishi wa Manispaa ya Ilala walipata pia fursa ya kutembelea Hifadhi
ya Taifa pekee Nchini Tanzania na Afrika Mashariki yenye fukwe za bahari
zinazokutana na uoto wa asili wa nchi kavu, nayo ni hifadhi ya Taifa ya Saadani
inayopatikana baina ya Mkoa wa Tanga na Pwani.

40
Sauti ya Ilala
Hifadhi hiyo ya Saaadani imepandishwa hadhi na kuwa hifadhi kamili mwaka
2005 kutoka kuwa pori la akiba, ni ya upekee kwa sababu inapakana na
bahari ya Hindi na unapotembelea unaweza kufanya utalii wa nchi kavu, majini
na kwenye maeneo ya historia ya mambo ya kale.

Pamoja na Watumishi wa Manispaa ya Ilala kufanya utalii kwenye hifadhi ya


Saadani na kujionea vivutio mbalimbali, lakini pia waliitumia hifadhi hiyo kama
sehemu ya kufanyia mafunzo na tathmini ya utendaji kazi kwa kipindi cha
mwaka 2017 na kupanga mikakati ya mwaka 2018.

Pia katika hifadhi ya Saadani unaweza kufanya utalii wa kutumia boti kwenye
Mto Wami kwenda umbali mrefu na kuna Ndege wengi na Wanyama aina ya
Viboko na Mamba ndani na nje ya maji na kwenda hadi sehemu ya Bahari na
Mto vinapokutana huku kukiwa na miti aina ya mikoko kwa uwanda wa pwani.

Afisa Utumishi Bwana Robert Muna wa kwanza kushoto akifurahia mchezo wa kuvuta
kamba sambamba na Watumishi wengine wa Manispaa ya Ilala kwenye fukwe za bahari
Hindi walipofanya ziara kwenye hifadhi ya Saadani.

Kwenye hifadhi hiyo kati ya wanyama watano mashuhuri wanaopatika kwenye


Mbuga kubwa za hifadhi za Taifa na Ulimwenguni (Big five) wanne
wanapatikana kwenye hifadhi ya Saadani ambao ni Tembo, Simba, Nyati, na
Chui isipokuwa Faru pekeee ndio hapatikani.

41
Sauti ya Ilala

Watumishi wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa ziara ya kutembelea hifadhi ya


Saadani

Hii ndio hifadhi ya Taifa ya Saadani, ukifika utajionea vitu vingi vinavyotia
raha kwa kiasi kikubwa mno, pia utajifunza na mila za Watu wa Pwani kwani
sehemu ya hifadhi hii kuna makazi ya Watu wanaoishi kwenye kijiji chenye
asili ya jina la Saadani.

42
Sauti ya Ilala

SERIKALI YA AWAMU YA TANO YARUDISHA MUONEKANO WA


SHULE KONGWE ZILIZOPO HALMASHAURI YA MANISPAA YA
ILALA
Na Neema Njau

Serikali ya awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe Dr John Pombe Magufuli


katika azma ya kuiboresha Sekta ya Elimu pamoja na Elimu bure imejidhatiti
katika kufanya mazingira ya elimu kuwa bora zaidi kwa kujenga na kukarabati
miundombinu ya shule kongwe ambazo kwa ujumla zilijengwa zaidi ya miaka
50 iliyopita.
Kwa upande wa Elimu Sekondari Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina Jumla
ya Shule za Sekondari 101 ambapo shule 52 ni shule za Serikali, 49 ni shule
zinazomilikiwa na watu pamoja na mashirika binafsi. Shule za serikali zina
jumla ya wanafunzi 48430, wavulana 23326 na wasichana 25104 wakati
shule zinazomilikiwa na watu binafsi zikiwa na wanafunzi 13548 ikiwa ni
wavulana 6994 na wasichana 6554.

Halmashauri ina shule 6 kongwe za Serikali ambazo ni Shule ya Sekondari


Pugu, Azania, Jangwani, Kisutu, Zanaki pamoja na Tambaza Sekondari. Serikali
katika kuboresha na kurudisha heshima ya shule kongwe imekarabati shule
hizi katika awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza zilikarabatiwa shule ya
Sekondari Tambaza, Zanaki na Kisutu na awamu ya pili ukarabati unafanyika
katika shule ya Sekondari Pugu, Jangwani pamoja na Azania. Pamoja na
ukarabati uliofanyika awali kwa shule za Sekondari Tambaza, Zanaki na Kisutu
Serikali katika azma yake ya kurudisha heshima na hadhi ya shule kongwe
imepeleka fedha za ukarabati katika kila shule iliyokarabatiwa awamu ya
kwanza ili kukarabati maeneo madogomadogo ambayo yanahitaji ukarabati.

Ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu

Shule ya Sekondari Pugu ni miongoni mwa shule kongwe iliyojengwa mwaka


1948 . Shule hii ni shule ya kihistoria ambayo Baba wa Taifa Hayati Julius K.
Nyerere alifundisha miaka michache kabla ya kuanza harakati za kupigania
uhuru ambayo pia imewafundisha viongozi wengi wa kitaifa. Shule hii kwa
sasa ina jumla ya wanafunzi 841 , kati ya wanafunzi hao kidato cha kwanza
hadi cha nne ni wanafunzi 373 na wanafunzi wa kidato cha tano na sita 468.
Shule hii ni moja ya shule yenye wanafunzi 83 wenye mahitaji maalum ambao
ni wanafunzi wenye ulemavu.

43
Sauti ya Ilala

Jengo la Utawala katika shule ya sekondari Pugu.

Serikali inategemea kufanya ukarabati kwa awamu tatu katika shule ya


Sekondari Pugu,ambapo katika awamu ya kwanza umefanyika ukarabati wenye
thamani ya Tsh 984,934,257.00 . Ukarabati uliofanyika ni kuondoa mabati ya
Asbestoes ambayo yalikuwa hatari kwa afya za walimu na wanafunzi na
kuweka mabati mapya kwenye madarasa 10, jingo la utawala, mabweni 27
na maktaba.

44
Sauti ya Ilala

Muonekano wa shule ya Sekondari Pugu baada ya kubadilishwa kwa vigae vya asbestos
na kuezekwa upya kwa kutumia mabati.

Ukarabati mwingine uliofanyika ni ukarabati wa vyoo na mifumo ya maji safi


na maji taka, ambapo vyoo 34 vilikarabatiwa,vyoo 5 vya walemavu, ujenzi wa
septic tank na sock pit 3, chemba ,mabomba,mabafu 12,sehemu za kufulia 3,
pamoja na choo kipya chenye matundu 6 ,bafu mpya 9,sehemu mpya ya
kufulia 1 na vyoo 2 vipya vya walemavu.

Muonekano wa vyoo vipya na bafu vilivyojengwa katika shule ya sekondari Pugu.

Vyumba vya madarasa na mabweni ambayo madarasa 15 yalikarabatiwa,


mabweni 27 kuweka mfumo mpya wa umeme , pamoja na kujenga eneo la
kufunga mashine ya kusukuma maji kuingia kwenye matanki.
45
Sauti ya Ilala

Moja ya Maabara iliyokarabatiwa katika shule ya sekondari Pugu.

Ukarabati wa shule ya Sekondari Jangwani.


Shule ya Sekondari Jangwani iliwekwa jiwe ya msingi tarehe 28 Mei, 1928
ikiwa ni takribani miaka 90 iliyopita, shule hii ina jumla ya wanafunzi 1414 kati
ya wanafunzi hao kidato cha kwanza hadi cha nne wanafunzi 1154 pamoja na
wanafuzi wa kidato cha tano na sita ambao ni 260 miongoni mwa wanafunzi
hao 88 ni wenye mahitaji maalumu ambao ni wanafunzi walemavu.

Jengo la Utawala katika shule ya Sekondari Jangwani.

46
Sauti ya Ilala
Ukarabati uliofanyika katika shule ya Sekondari Jangwani umegharimu jumla
ya Tsh Millioni 900 zimetumika kukarabati miundombinu ya shule hii, kwa
upande wa madarasa ukarabati uliofanyika ni pamoja na ofisi ya mkuu wa
shule, ofisi kuu ya walimu, ofisi ndogo ya walimu, ofisi ya taaluma, ofisi ya
mhasibu, madarasa 24,vyoo 15 vya walimu, maabara, vyoo vya wanafunzi 13
, ujenzi wa vyoo vipya 17 na mabafu 4 pamoja na ujenzi wa vyoo vitatau vya
matundu ambavyo vitatumika kwa matumizi ya dharura wakati maji
yanapokuwa yamekatika.

Wanafunzi wakijisomea katika moja ya darasa lililokarabatiwa katika shule ya


Sekondari Jangwani

Aidha maabara zimefanyiwa ukarabati ikiwa ni pamoja na maabara ya Biolojia,


maabara ya Fizikia, maabara ya cookery, maabara ya lishe “nutrition”, maabara
ya kemia, stoo ya kemikali na vifaa, maabara za kompyuta, pamoja na chumba
cha ushonaji.

47
Sauti ya Ilala

Moja ya Maabara iliyokarabatiwa katika shule ya Sekondari Jangwani

Kwa upande wa hosteli ukarabati uliofanyika ni wa vyumba vitano vya hosteli,


vyoo 3 na mabafu 3 kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu, pamoja
na vyoo 10 na mabafu 10 kwa wanafunzi wa kawaida.

Pichani ni muonekano wa ukarabati wa bweni

Ukarabati mwingine ni wa bwalo, jiko na ujenzi wa jiko jipya la kuni


unaoendelea, dispensary pamoja na nyumba ya matroni.

48
Sauti ya Ilala
Ukarabati wa shule ya Sekondari Azania.

Shule ya Sekondari Azania ilianzishwa mwaka 1934 wakati huo ikiwa katika
mtaa wa Mtendeni ikijulikana kwa jina la Shule ya Msingi “Mtendeni Indian
Primary School”. Mwaka 1939 shule hii ilitaifishwa na kuwa shule ya Sekondari
ya Serikali ya mchanganyiko wa wavulana na wasichana. Mwaka 1965
wanafunzi wa kike walihamishiwa katika shule ya Serikali “Indian Secondary
School “ ambayo kwa sasa inajulikana kwa jina la Shule ya Sekondari Jangwani
na wavulana walihamishiwa kwenye majengo mapya yaliyokuwa katika
barabara ya Umoja wa Mataifa ambayo kwa sasa yanajulikana kwa jina na
Shule ya Sekondari Azania ambapo mwanafunzi wa kwanza mwenye asili ya
Kiafrika aliweza kusajiliwa.

Jina la Shule ya Sekondari Azania lilianza kutumika rasmi mwaka 1967 ikiwa
imesajiliwa kwa usajili namba 08.

Shule hii ina jumla ya wanafunzi 1787 ambapo kidato cha kwanza hadi cha
nne ina jumla ya wanafunzi 1403 pamoja na 384 ni wanafunzi wa kidato cha
tano na cha sita.
u

49
50
51
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA

UTARATIBU UNAOTUMIKA KUTOA VIBALI VYA UJENZI WA  Urefu wa jengo (height)


MAJENGO
 Matumizi yanayokusudiwa Idadi ya maegesho yatakayokuwepo
1. KIBALI CHA UJENZI
 Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks) na
 Kulingana na Sheria ya Serikali za Mitaa Na. 8 ya mwaka 1982.  Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo. Barabara
 Sheria ya Mipango Miji na Majengo Mijini si ruhusa kwa mtu inayopitia mbele ya kiwanja na mshale unaoonyesha Kaskazini.
yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila:
5. VIAMBATANISHO
i. Kutuma maombi kwa mamlaka ya Mji kwa kupata ridhaa ya awali
(Planning Consent)  Fomu moja ya maombi iliyojazwa kwa usahihi.

ii. Majengo makubwa kuwe na ramani (Outline scheme designs)  Hati ya kumiliki kiwanja au barua ya toleo au leseni ya Makazi

iii Kuwasilisha michoro ya jengo na kumbukumbu husika za  Kumbukumbu nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za
kiwanja mauzo,makabidhiano n.k.
iv. Kupata kibali kwa maandishi kinachitwa “Kibali cha Ujenzi”.  Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo

2. KIBALI CHA AWALI  Mabadiliko ya matumizi ya ardhi.


(Planning Consent); 6. HATUA ZINAZOFUATWA KATIKA KUSHUGHULIKIA
Inashauriwa kupata kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi. MAOMBI YA KIBALI

Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (Outline plan) kwa Zifuatazo ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuchunguza michoro hiyo:
utaratibu unaotakiwa ukionyesha aina ya ujenzi atakaokusudia kufanya ili
 Kuwasilisha michoro na kulipa gharama za uchunguzi
aweze kupata ridhaa ya kuendelea na hatua za kuandaa michoro ya mwisho. (scrutiny fee).

FAIDA:  Uhakiki wa miliki

 Kuokoa muda na gharama, iwapo michoro ya mwisho itaonekana  Kukaguliwa usanifu wa michoro
kuwa na dosari za kitaalam ambazo zitahitaji kufanyiwa
marekebisho.  Kukaguliwa kiwanja kinachokusudiwa kuendelezwa

 Kuwa na uhakika kuhusu mahitaji muhimu ya kuzingatiwa wakati  Uchunguzi wa upimaji kiwanja
michoro inaandaliwa.
 Uchunguzi wa matumizi ya jengo na uwiano
3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA
UJENZI  Uchunguzi wa Maafisa Afya

 Uchunguzi wa Mipango ya uondoaji majitaka


Baada ya michoro kukamilika, iwasilishwe ikiwa kwenye majadala kwa
namna ambayo inaweza  Uchunguzi wa tahadhali za moto

kufunguliwa na kusomeka. Michoro hiyo iwasilishwe kama ifuatavyo:  Uchunguzi wa athari za mazingira (EIA)

 Seti tatu za michoro ya jengo (Architectural drawings)  Uchunguzi wa uimara wa jengo (Structural Drawings)
 Seti mbili za michoro ya vyuma) structural drawings) kwa  Kuandaliwa kwa maombi yaliokamilisha taratibu hizi na
majengo ya ghorofa.
kupele kwa kwenye Kamati ya Ujenzi ambayo wajumbe
4. MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI wake ni Madiwani
 Hatimaye kuandika na kutoa kibali
Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:
7. FAIDA ZA KUJENGA NYUMBA IKIWA NA KIBALI CHA UJENZI
 Jengo litakavyokuwa (Plan) Sections, elevations, Foundation and
roof Plan). Kuishi kwenye nyumbayo imethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama

 Namba ya eneo la kiwanja kilipo,Jina la Kampuni na anwani ya  Kuwa na mazingira bora kwa kuwa na mji ulipangwa

Kampuni iliosanifu jengo husika.  Kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kutokea iwapo ujenzi

 Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba umefanyika bila kibali kiwa ni pamoja na kushitakiwa mahakakani
kuvunjiwa na kulipa gharama za uvunjaji.
 Ujazo wa kiwanja (Plot coverage)

 Uwiano(Plot ratio)
Sauti ya Ilala

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda aliyepo upande wa kulia akiweka
tofali pamoja na Makamu wa Rais wa Shirika la KOICA kutoka Nchini Korea Kusini, Taemyon
Kwon, uwekaji wa tofali hilo uliashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa Hospitali ya Mama na
Mtoto Chanika

Aidha, ujenzi wa Hospitali hii ya Chanika umejumuisha wodi mbili zenye vitanda
120, (60 kwa kila moja) ambazo ni kwa ajili ya akina Mama ambao
hawajajifungua na waliojifungua, ICU mbili zenye vitanda 10 kila moja,Wodi
ya kujifungulia, Wodi ya Watoto njiti yenye vitanda 10, Vyumba vitatu vya
upasuaji, viwili vya upasuaji mkubwa na kimoja upasuaji mdogo, Maabara,
Idara ya uchunguzi wa mionzi, Idara ya ufuaji na utakasaji vyote hivi vina
vifaa vya kisasa.

52
Sauti ya Ilala

Moja kati ya nyumba za kuishi Watumishi waliopo Hospitali ya Mama na Mtoto Chanika,
nyumba hizi zimesaidia kuwapata Watumishi muhimu muda wote wanapohitajika hivyo
kurahisha huduma hasa za dharura

UTOAJI HUDUMA:
Ujenzi wa majengo haya umewezesha kuanza kutoa huduma za ndani (IPD
Services) ambazo zilianza tarehe 9 Oktoba 2017 kwa huduma za sehemu ya
wodi ya akina Mama wanaosubiria kujifungua (antenatal ward), wodi ya
Kujifungulia (Labour ward) na Wodi baada ya kujifungua (postnatal ward).

Pamoja na Hospitali ya Mama na Mtoto Chanika kupunguza msongamano


katika vituo vingine hasa Amana na kwengineko, lakini pia Hospitali hii
imewezesha kuwepo kwa maboresho katika vituo vyote. Maboresho yote
kwa ujumla yatasaidia kupunguza vifo na maumivu kwa Mama wajawazito na
Watoto
“Nchi yetu kupitia Shirika la KOICA imeamua kujitolea kujenga Hospitali hii ili
kuwasaidia Wananchi wa Tanzania kupata huduma bora ya Afya ya Mama na
Mtoto wakati wa kujifungua kwani hatupendi kuona wanapoteza maisha wakati
wa kujifungua” alisema Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Geum-young
Song.

53
Sauti ya Ilala

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bibi Theresia Mmbando akikagua vifaa
vilivyopo kwenye Hospitali ya Mama na Mtoto Chanika

Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mama na Mtoto Chanika Dr. Richard M. Andrea (wa kwanza kulia)
akitoa maelezo kwa viongozi waliofika katika Hafla ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Hospitali
katika moja ya wodi ya wamama ambao tayari wamekwisha jifungua.

54
Sauti ya Ilala
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YAUNGA MKONO NA
KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA KWA KUTUMIA VIUADUDU

Na Neema Njau.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya


Muungano wa Tanzania Dr John Joseph Pombe Magufuli la vita dhidi ya malaria
kwa kununua viuadudu toka kiwanda cha Kibaha cha serikali ya Tanzania
ambacho ndiyo kiwanda pekee kinachozalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi
wa mbu hapa nchini . Halmashauri imenunua jumla ya lita 5,900 za viuadudu
aina ya Bacillus thuringiensis var isralensis (Bti) na Bacillus sphaericus (Bs).

Shughuli ya kuua viluwiluwi wa mbu ilisimama Januari 2016 kutokana na


ukosefu wa viuadudu. Baada ya serikali kujenga kiwanda cha kuzalisha
viuadudu hivyo, Halmashauri imeanza kutekeleza shughuli ya kuua viluwiluwi
wa mbu kwenye Kata 17 kati ya Kata 36 za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Aidha Kata 7 ziko katika hatua ya maandalizi ya kukusanya takwimu za awali
kama vile idadi, ukubwa na aina ya mazalio yaliyopo.

Viuadudu vinavyotumika kuua viluwiluwi wa mbu kwenye mazalio

Viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu

55
Sauti ya Ilala
Elimu kwa Jamii

Pamoja na huduma ya kupuliza Viuadudu, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala


imeendelea kutoa elimu katika jamii, juu ya matumizi sahihi ya viuadudu kwa
wana jamii pamoja na kuweka mazingira yao katika hali ya usafi ili kutoruhusu
mazingira ya mazalio ya mbu. Ikiwa ni pamoja na kuwafundisha wanajamii
watanaofanya shughuli ya kupuliza viuadudu kwa kuwa havina madhara
kwa binadamu wala viumbe wengine isipokuwa viluwiluwi wa mbu.

Pichani ni moja ya wanajamii wakipuliza viuadudu na kuangalia uwepo wa viluwiluwi

Ugawaji wa vyandarua ngazi ya kaya

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Wizara ya Afya


Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imeendelea na kampeni ya ugawaji
wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu ngazi ya Kaya. Jumla ya
vyandarua 725,866 vimegawiwa katika kaya 480,823 na wananchi
kuelimishwa na kusisitizwa kuvitunza na kuvitumia ipasavyo ili kuweza kupiga
vita ugonjwa wa Malaria.

56
Sauti ya Ilala

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akigawa vyandarua katika kata
ya Gerezani

Halmashauri katika jitihada zake za kupiga Vita Ugonjwa wa Malaria imejidhatiti


katika kuzingatia kampeni ya kufanya usafi kila Jumamosi na kuua mazalia ya
mbu pamoja na utoaji wa elimu juu ya matumizi sahihi ya vyandarua
kumewezesha ugonjwa wa Malaria kupungua kutoka asilimia 9.8 mwaka
2015 , asilimia 7.1 kwa mwaka 2016 mpaka kufikia asilimia 5.6.

Malaria inasambazwa kwa binadamu kwa kung’atwa na mbu wanaobeba


vimelea vya malaria ,inayosababisha dalili zinazofanana na mafua, na
ikishakuwa malaria kali husababisha vifo.Walio katika hatari zaidi ni
watoto,wanawake wajawazito na walio maeneo ya mbali yasiyofikika kiurahisi
ambapo upatikanaji wa vifaa vya kinga na tiba ni mdogo.

Maleria inaweza kuzuilika na kutibika kwa vitendea kazi rahisi kama vyandarua,
matumizi sahihi ya dawa sahihi ya malaria, upuliziaji wa dawa za mbu pamoja
kuuwa viluilui wa mbu kwa kutumia viua dudu.

57
Sauti ya Ilala
MANISPAA YA ILALA YAIMARISHA USAFI WA MAZINGIRA
Na Neema Njau
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeongeza uwezo wake wa uondoshaji wa
taka ngumu kutoka 36%-50% ya mwaka 2015/2016 na kufikia 50%-55% ya
tani 110 zinazozalishwa kwa siku. Hali ya usafi kwa ujumla inaridhisha. Kupitia
gari maalum la matangazo ambalo limekuwa likitoa maelekezo mbalimbali
kuhusiana na usafi wa mazingira pamoja na vipindi katika vyombo vya habari
jamii imehamasika kwa kufanya kampeni shirikishi za usafi kwa kila Jumamosi
na Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kwa kata zote 36.
Katika utekelezaji wa dhana ya ushirikishaji wa sekta binafsi katika utoaji wa
huduma Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeingia mkataba na makampuni
binafsi 7 yanayotoa huduma katika kata za katikati ya mji na vikundi vya
kijamii 26 vinavyotoa huduma ya kukusanya na kusafirisha taka kuzipeleka
dampo katika kata za pembezoni. Uthibitisho wa moja kwa moja unaweza
kupatikana katika eneo la kariakoo ambapo awali kulikuwa na changamoto ya
malundo ya takataka. Lakini kutokana na kuwepo kwa kampuni yenye uwezo
hali hiyo imeweza kudhibitiwa.

Watumishi wa Manispaa ya Ilala wakiwa katika usafi wa Jumamosi ya mwisho wa mwezi


katika eneo Daraja la Salenda

58
Sauti ya Ilala

Baadhi ya magari ya Kampuni ya Usafi ya Green Waste PRO inayoshirikiana na


Manispaa ya Ilala katika hali ya usafi na uboreshaji wa mazingira.

Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanikiwa sana katika


kutunza na kuhifadhi wa mazingira, aidha katika kuboresha mandhari ya mji
(city beautification) Halmashauri imefanikiwa kupanda miti 7,640 katika
barabara kuu zote,mitaa,shule za msingi na sekondari, taasisi za Umma pamoja
na kufanya jitihada za kupata wadau mbalimbali wa uboresha bustani na
maeneo ya wazi ikiwemo bustani ya Askari Monument, Mnara wa saa, pamoja
na eneo la wazi lililopo Samora avenue (kaburi moja).

59
Sauti ya Ilala

Bustani ya Mnara wa Askari

Halmashauri katika kutimiza azma ya uzafi wa mazingira kwa wananchi wake,


katika eneo la katikati ya mji (CBD), Jamii imehamasika kulipa ada ya taka
kwa mwitikio mkubwa. Pamoja na hilo, Halmashaui imefanikiwa kununua
bajaji tano zinazotumika kwa ajili ya uhamasihaji wa elimu ya mazingira na
ufuatiliaji wa kazi za kila siku.

Utoaji wa elimu ni moja ya nyenzo muhimu katika kufikia malengo katika


suala la usafi wa mazingira, hivyo Halmashauri imefanikiwa kuelimisha Umma
juu ya masuala ya usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na usimamizi wa
Sheria katika maswala ya usafi na uhifadhi wa Mazingira, (Environmental
Extension Service and Law Enforcement), kwa kutumia gari la matangazo
kuendelea kufanyika, ambapo katika kipindi cha Julai 2016-Juni 2017 Kata
36 na mitaa 119 imefikiwa na huduma hiyo.

Katika Usimamizi wa sheria, wachafuzi wa mazingira wameendelea kuchukuliwa


hatua, ambapo kwa kipindi cha Julai 2016-Juni 2017, Jumla ya wachafuzi 411
walichukuliwa hatua mbalimbali ikiwemo kutozwa faini, kupewa onyo na
wengine kufikishwa mahakamani.

60
Sauti ya Ilala
Halmashauri inaendelea kukagua na kuhakikisha kuwa miradi yote
inayotekelezwa ndani ya Halmashauri, inayohofiwa kuleta athari kwa mazingira
inatekeleza matakwa hayo ya kisheria kabla ya kutekelezwa. Kwa kipindi cha
Julai 2016-Juni 2018, jumla ya miradi 108 imekaguliwa kwa kushirikiana na
Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira.

WATUMISHI WA MANISPAA YA ILALA WAZIDI KUHAMASIKA NA


MAZOEZI

Na: Hashim Jumbe

Watumishi wa Manispaa ya Ilala wameendelea kuhamasika na ufanyaji wa


mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya zao ikiwa ni njia moja wapo ya kujiepusha
na magonjwa yasiyoambukiza kama vile Kisukari na Presha.

Ratiba ya ufanyaji wa mazoezi kwa Watumishi wa Manispaa ya Ilala ni ya kila


siku za Jumatatau, Jumatano na Ijumaa kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa
11:30 jioni na Jumamosi ya pili ya kila mwezi Watumishi wa Manispaa ya Ilala
hushiriki kwenye ufanyaji wa mazoezi kuanzia saa 12:00 asubuhi ikiwa ni
kutekeleza agizo la Makamu wa Rais linaloagiza Watumishi wote wa Umma
kushiriki kwenye mazoezi kila Jumamosi ya pili ya mwezi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Bwana Msongela Palela wa pili kuanzia kushoto akishiriki
katika mazoezi sambamba na Watumishi wengine wa Manispaa ya Ilala.

61
Sauti ya Ilala

Katibu Tawala Wilaya ya Ilala, Bwana Edward Mpogolo aliyepo upande wa kulia, akifanya
mazoezi ya kukimbia pamoja na Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala, Wakili Bonaventure
Mwambaja.

Watumishi wa Manispaa ya Ilala wakiwa kwenye mazoezi ya pamoja viwanja vya Mnazi
Mmoja kama ilivyo kawaida ya siku ya Jumatatu, Jumatano na Ijumaa ambapo mazoezi
huanza baada ya masaa ya kazi.

62
Sauti ya Ilala

Jumamosi ya pili ya kila mwezi, Watumishi wa Manispaa ya Ilala hutekeleza agizo la Makamu
wa Rais kwa kufanya mazoezi asubuhi kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete-Kidongo
Chekundu

Baada ya mazoezi, Watumishi wa Manispaa ya Ilala hukaa pamoja na kukumbushana


mambo mbalimbali hususan afya ya mwili

63

You might also like