Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 23

ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

MJADALA ULIOFANYIKA KATIKA FACEBOOK BAINA YA ABEL


SULEIMAN SHIRIWA NA ABU RASHIDA AKIWAKILISHWA NA
AKASHA OPATO DAAWAH

Abel Suleiman Shiriwa VS ABU RASHIDA

1|Page
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

Contents
1..POST YA ABEL SULEIMAN SHIRIWA...........................................................3

1..JIBU YA ABU RASHIDA.................................................................................. 4

2..JIBU YA ABEL SULEIMAN SHIRIWA........................................................... 7

2..JIBU YA ABU RASHIDA...................................................................................9

3..JIBU YA ABEL SULEIMAN SHIRIWA.......................................................... 13

3..JIBU YA ABU RASHIDA..................................................................................14

4..GODPHREY SWITI MFUATILIAJI WA MIJADALA.....................................16

4..JIBU YA ABU RASHIDA..................................................................................17

5..GODPHREY SWITI MFUATILIAJI WA MIJADALA.....................................19

5..JIBU YA ABU RASHIDA..................................................................................20

6..NATIJA NA MWISHO WA MJADALA...........................................................22

7..MAREJEO...........................................................................................................23

2|Page
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

1.POST YA ABEL SULEIMAN SHIRIWA:


Abel Suleiman Shiriwa

March 4 at 2:42pm · Edited

HIVI WATUKUTU WAISLAMU, HUYU IMAMU MALIK ALIYEKUWAA


ANAMFIRA MKEWE..

Imepokewa kwa Abu Sulayman Aljarjaaniyy akisema, "Nilimuuliza Malik bin Anas
kuhusu Kumuingili mke katika Tupu ya nyuma, akajipiga kichwani na kusema, sasa
hivi natoka kukoga kwa ajili hiyo" Maana yake Imamu Malik bin Anas alikuwa
ametoka kumwingili Mkewe katika tupu ya nyuma, kisha akaenda kukoga!

Naye Imam Shafii anasema, "Halikusihi Jambo lolote kwa Mtume (s.a.w) kuwa ni halali
wala haramu kumwingilia mke katika tupu ya nyuma, na kwa kutumia Qiyas, jambo
hilo ni halali. (Umtadul Qaary J. 18, uk. 155
Irshadus Saary J. 10, uk 61-61)

NA KISHA KUENDELEA KUSALISHA WAISLAMU WA ZAMA HIZO


WALIMCHUKULIA HATUA GANI?

3|Page
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

1.JIBU KUTOKA KWA ABU RASHIDA


bwana abel asema imam malik na imam shafii wanakubali mume kumwingilia mke
wake kwa tupu ya nyuma na ushahid wake ni UMTADUL QAARI J 18 UK 155 na
ISHADUUS SAARY j10 uk 60-61

MAJIBU

Kila sifa njema ni za Allah Muumba Mbingu pasina nguzo ambaye hana wake wale
waume wala watoto, hazai wala hazaliwi, hana mshirika, halali wala hasinzi na sala na
salamu zimfikie kipenzi chetu Mtume Muhammad aliekuja kutoa watu kutoka giza
kuwaleta katika nuru ya kumwabudu Mungu Moja, pia ahli zake na.masahaba wake na
wote waliowafuata katika uongofu mpaka siku ya qiyama

Ama baada ya kumhimidi Allah na.kumtakia rehma na amani mtume wetu muhammad
twasikitika tena masikitiko makubwa kwa maneno alioleta abel akijidai msomi na.kutoa
hoja ya kuwa imam malik na imam shafii wanakubali mume kumwingilia mke kwa
tupu ya nyuma. Hoja zifuatazo zitathibitisha udhaifu wa hoja zake na alivyojawa na
chuki na uislamu na waislamu mpaka kuchukua riwaya na kuzisinanga tafsiri zake ndio
azushe uongo

1. Kwa insafu na.bila chuki ningependa kumwuliza abel.kama kasoma kweli hata
angalau line ya kwanza ya UMDATUL QARI wacha juzuu ya 18 na kama hata
anajua mtunzi.wa IRSHADUS SAARY wacha hata kukiona hicho kitabu? Jibu
lenyewe ni hapana na sababu inafuata kwa hoja ya pili

2. Bwana mkubwa kama ambavyo alikuwa anapelekwa na chuki yake na wala si


hoja AMECOPY PASTE akanukuu na.kusema UMTADUL QAARI badala ya
UMDATUL QAARI. Hamna katika ulimwengu wa kiislamu.kitabu kwa jina la
UMTADUL ikianza na T na.kufuadiwa na D na ni challenge kwa abel.kutuletea
kitabu hicho na.mtunzi.wake kama mkweli. zaidi ya hapo ni.copy.paste kutoka
vitabu vya kishia na kupelekwa na.uadui.wake na.uislamu.

3. Zifuatazo ni hadithi chache miongoni mwa nyingi ambazo zinaharamisha


kumwingilia mwanamke kwa nyuma mpaka mwanaume analaaniwa akifanya
kitendo hicho

 Hadithi ya kwanza: Anasimulia Abu Hurayrah kwamba Mtume Rehman na


Amani ziwe juu yake amesema "Allah hatomwangalia mwanaume ambaye
anamwingilia mke wake kwa tupu la nyuma"(1)

 Hadithi ya pili: Anasimulia Ibn Abbas kwamba Mtume Rehma na Amani ziwe
juu yake amesema " Allah hatomwangalia mwanamume ambaye anamwingilia
mwanamume mwenzake au mwanamke kwa tupu ya nyuma"(2)

 Hadithi ya tatu: Amesimulia Abu Hurayrah kutoka kwa Mtume Rehma na


Amani ziwe juu yake kuwa" Atakamwingilia mke wake kupitia kwa tupu ya
nyuma amelaaniwa"(3)

4|Page
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

Hizo hadithi tatu zatosha kuonyesha msimamo wa Uislamu na waislamu kuhusu


kumwingilia mwanamke kwa tupu ya nyuma na hayahijtaji tafsiri maana yanajieleza
ama hadithi za kuharamisha kitendo hicho ni nyingi lakini tumeona tusiweke nyingi
huenda tukachosha watu

4.Zifuatazo ni kauli za maswahaba wa mtume, wanachuoni wakubwa na.maimamu


wakubwa.

 Kauli ya kwanza: Tafsiri ya Ibn Abbas ambaye ni swahaba alipokuwa akitafsiri


ayah ya 223 ya suratul baqarah akasema : Tupu za mbele za wake zenu ni kama
mashamba kwa sababu ya watoto wenu kwa hivo endeni katika mashamba zenu
vile mutakavyo, kutoka nyuma au mbele maadamu mutawaingilia katika tupu za
mbele na muogope Allah kuwaingilia wake zenu kwa tupu ya nyuma........"(4)

 Kauli ya Pili: Ibn Kathir alipokuwa akitafsiri ayah ya 222 ya surah baqarah
alipofika "...... kama vile Allah alivyowawekea" akasema ibn Abbas, Mujahid na
wanachuoni wengine wamesema kuwa ina maanisha Al Fajr(Tupu ya Mbele)
kwa hivyo kumwingilia kwa tupu ya nyuma ni haramu(5)

 Kauli ya tatu: Imam Jalal al din al Mahali na Jalal al Din al Suyuti katika tafsiri
ya ayah ya 223 ya surah baqarah wanasema "wanawake wenu ni mashamba
zenu bimaana mahali ambapo mutaweka mbegu za watoto wenu, kwa hivo ijieni
shamba lenu yaani tupu ya mbele ya mwanamke kwa njia yoyote mutakayo, kwa
kusimama, au kwa kukaa, au kwa kulala, kutoka mbele au nyuma. na ayah hii
iliteremshwa kwa sababu wayahudi walikuwa wanasema ukimwingilia mkeo kwa
tupu ya mbele lakini kwa njia ya nyuma mtoto atazaliwa akiwa na macho
kengeza......."(6)

Hayo kauli tatu pia zatosha kueleza hukmu ya kumwingilia mkeo.kwa tupu ya nyuma

5. Sasa tuje kwa hao maimamu wawili waliosingiziwa kuwa wamekubali mume
kumwingilia mkeo kwa tupu ya.nyuma. Je ni kweli

Ibn.Kathir anatoa majibu anasema "Abu bakr bin ziyad Naysaburi anasimulia
kuwa Ismail bin Ruh alisema kwamba alimuuliza imam Malik bin Anas(ndiye huyo
ambaye abel amemsingizia) "Je wasemaje kuhusu kumwingilia mwanamke kwa tupu ya
nyuma" akasema imam malik "Wewe si mwarabu je kumwingilia mke hupatikana ila
mahali.pa uzalishaji. Mwingilie mkeo katika Farj(Tupu ya mbele). Nikasema "Ewe abu
abdullah(akimaanisha imam malik), wanasema kuwa wewe unakubalisha kumwingilia
mkeo kwa tupu ya nyuma. akasema imam malik "wananizulia uongo, wananizulia
uongo" na hii ndio msimamo wa Imam Malik katika hilo na msimamo wa said
ibn.musayib, Abu salamah, ikrimah, Tawus, Ata, Said ibn.jubair, Urwah bin az zubayr,
Mujahid bin.jabr, Al Hasan na wanavyuoni wengine kutoka maswahaba na
waliowafuata (akiwemo imam shafii). Hawa wote na wengi katika wanachuoni
walikataza kumwingilia mkeo.kwa tupu ya nyuma mpaka wengi wao wakauita
hicho.kitendo ni Kufru(Ukafiri) (7)

5|Page
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

Ewe abel Imam Malik ashakujibu zamani ulichomsingizia yeye na ima shafii hata kabla
uzaliwe. Usiropokwe ovyo ovyo bila dalili.

6. Sasa natujibu hizo kauli ulizonukuu. Kama tulivyosema kauli ya imam malik
ni.kuwa ni haramu kumwingilia mkeo.kwa tupu ya nyuma basi hizi kauli mbili
alizozinukuu abel zamaanisha kuwa hicho kitendo alichokihalalisha imam malik
na imam shafii ni kumwingilia mkeo kwa tupu ya mbele lakini kwa njia ya
nyuma(Yaani Style). na sio kuwa kahalalisha kumwingilia mkeo kwa tupu ya
nyuma. Twasema hio alichofanya abel amecopy paste tafsiri mbovu ya maneno
ya imam malik na imam shafii ambayo ni kawaida ya watu waliofilisika hoja.

7. Na tujalie kuwa ni kweli imam malik na imam shafii wamekubali kumwingia


mkeo kwa tupu ya nyuma bado haimaanishi kuwa huo ni msimamo wa Uislamu
bal huwo ni.msimamo wao. Msimamo wa Uislamu.unapatikana kwa Quran na
Hadithi za bwana Mtume kwa muelewo wa Masahaba na wema waliotangulia.
Ikikwenda kauli ya mmoja wao kando na Quran.na sunnah tunawacha
kauli.yao.na.kuchukua kauli ya Quran na Sunnah na nimethitibisha kutoka
Quran na Sunnah kuwa hicho kitendo ni haramu tena ya kulaaniwa

8. La.mwisho kama ambavyo.nimethibitisha msimamo wa uislamu kuhusu


kumwingilia mwanamke kwa tupu ya nyuma na sasa nataka.abel atupe ayah
hata mmoja kwenye bibilia nzima iliyo na hoja safi ambayo haihitaji kigugumizi
yeyote wapi mwanamume amekatazwa kumwingilia mkewe kwa tupu ya nyuma.
Kama iko tupewe na kama hakuna tuambiwe kama kumwingilia mkeo kwa tupu
ya nyuma ni halali? Na kama hakuna lakini kitendo hicho ni haramu kwa
mujibu wa ukristo tuambiwe alieharamisha nani?

Hatutaki watu kupayuka na kuropokwa ovyo twataka majibu ya kielimu kwa hoja nane
tulizotoa. Hatutaki ubabaishaji kama ulivyofanywa baal hoja zijengwe na dalili. Post
yetu ikijibiwa ijibiwe kihoja na kidalili sio matukano na ubabaishaji usiokuwa na
maana yeyote

NA ALLAH ANAJUA ZAIDI

6|Page
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

2.JIBU KUTOKA KWA ABEL


SULEIMAN:
Unajua bwana Akasha Opato Daawah umenichekesha sana, sasa kukopy na kupaste
kuna madhara gani? kwani wewe hizo hadithi ambazo umezinukuu hapo umezitunga
wewe au umezicopy na kutupestia hapa?

Me nilitegemea labda utarejea kunukuu vitabu ambavyo nimeviweka hapa useme ni


sehemu gani nimenuku tofauti? badala yake unakuja na kuanza kunishambulia, uongo
ni wangu mimi au hawa waandishi?

Imepokewa na Husein bin Said kutoka kwa Ibn Abi Umeir, kutoka kwa Hafs bin
Suuqih, kutoka "Aliyemweleza" amesema, Nilimuuliza Abu Abdillah (a.s) kuhusu
Muislamu aliyemwingilia mkewe katika tupu yake ya nyuma, akasema, Hiyo ni moja ya
sehemu, inayoingiliwa, kunahitaji kukoga." (Al-Istibasaa J. 1 uk. 112)

Naye Imamu Shafii anasema: "Halikusihi Jambo lolote kwa Mtume (s.a.w) kuwa ni
halali wala haramu, kumwingilia mke katika tupu ya nyuma, kwa kutumia Qiyas,
jambo hilo ni halali." (Umdatul Qaary J. 18, uk. 155)

Imepokewa kwa Naafii. Anasema, "Aliniuliza Abdullah bin Umar bin Khattab;
"Unajua Aya hii (223, sura ya 2) ilishuka kwa ajili gani? NIKAJIBU, la, sijui, Akasema:
Imeshuka kwa ajili ya kuwaingilia wanawake katika Tupu zao za nyuma. (Addurul
Manthur J. 1 uk. 474
Fat'hul Baary J. 8 uk. 38-39
Irshadus Saary J. 10, uk. 61-63
Allubab fyi Ulumil kitabi J. 4 uk. 80)

Imepokewa kwa Abu Sulayman Aljarjaaniyy akisema, "Nilimuuliza Malik bin Anas
kuhusu Kumuingili mke katika Tupu ya nyuma, akajipiga kichwani na kusema, sasa
hivi natoka kukoga kwa ajili hiyo" Maana yake Imamu Malik bin Anas alikuwa
ametoka kumwingili Mkewe katika tupu ya nyuma, kisha akaenda kukoga!

Naye Imam Shafii anasema, "Halikusihi Jambo lolote kwa Mtume (s.a.w) kuwa ni halali
wala haramu kumwingilia mke katika tupu ya nyuma, na kwa kutumia Qiyas, jambo
hilo ni halali. (Umtadul Qaary J. 18, uk. 155
Irshadus Saary J. 10, uk 61-61)

Hebu vinukuu vitabu hivyo wewe ambae umeshaviona kwa macho tuone ni sehemu gani
nimeweka uongo?

Katika maelezo yako umekiri kweli vitabu hivyo vipo ila mimi nimeteleza na kuandika
Umtadul badala Umdatul, hapa umedhihirisha habari za Imamu malik kumfira mkewe
zimeandikwa kwenye kitabu cha Umdatul ndiyo maana katika maelezo yako umesema
walienda kumuuliza akasema anasingiziwa..

Sasa kama hizi habari zisingekuwa nimeandikwa Wangemuulizaje wakati hakuna kitu

7|Page
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

kama hicho?

Me nawasubiri wewe pamoja na Farid Hassan na Humpty Humpty mvinukuu hivyo


vitabu ambavyo nimeweka hapo halafu mniambie ni wapi nimesema uongo?

Issue ya kuona kitabu kizima wala siyo hoja ta msingi, waislamu madrasa
wanafundishwa hadithi za Bukhari, Muslimu, Ibn Majah, At-rimidh, bila bila vitabu
hivyo vilivyokamilika kuwepo isipokuwa vinanukuliwa kwa sehemu katika vitabu
vingine.

8|Page
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

2.JIBU TOKA KWA ABU RASHIDA:


Majibu ya bwana Abel Suleiman Shiriwa na ubabaishaji alionukuu kusema imam malik
na imam shafii na swahaba ibn umar wamekubali kuingilia mwanamke na tupu ya
nyuma na ubabaishaji alioufanya ya kudai kujibu majibu yangu

MAJIBU

Kila sifa njema ni za Allah Muumba Mbingu pasina nguzoambaye hana mke wala
mume wala mtoto, hazai wala hazaliwi,hana mshirika, halali wala hasinzi na sala na
salami zimfikie kipenzi chetu Mtume Muhammad aliekuja kutoa watu kutoka giza ya
ujahiliya na ushirikina na kuwaleta katika nuru ya kumwabudu Muumba Mbingu na
Ardhi Allah, pia ahli zake na.masahaa wake na wote waliowafuata katika uongofu
mpaka siku ya qiyama.

Ama baada ya kumhimidi Allah na kumtakia rehma na amani kipenzi chetu mtume
muhammad twasikitika tena twasikitika sana kwa majibu ya bwana abel sasa ndio
kathibitisha kinachompeleka kusema anavyosema ni chuki kwa uislamu na waislamu
ndio anadandia gari kwa mbele hali yaelekea kisimani. chunga bwana abel utaanguka
kwa kisima nagari juu yako na hautaonekana mwisho wako pamoja na udhaifu wa hoja
zake bado tutamjibu ili wanaofuatilia wafaidike na wajue wazushi na wanavyozua na
ifuatayo twaangalia majibu yetu tukilinganisha na yake tuone kama kajibu kweli ama
kababaisha na kurudia hoja zile zile zilizojiwa zamani.

(1) Hoja yetu ya kwanza ilikuwa kumwuliza abel kama amesoma hizo vitabu
angalau alizozinukuu na kama anajua hata mtunzi wa irshadus saary. Nilikuwa
natarajia msomi atatujibu maswali yetu baal kakubali kuwa amecopy paste na
twamshukuru katika kukubali hilo maana labda ameuliza mwalimu wake mkubwa
"google" na hakupata majibu ikabidi akubali tu kuwa kuwa ame copy paste ila kaleta
ubabaishaji kuwa hata mimi nimecopy paste hizo hadithi na namwambia sijacopy paste
bali nimefungua vitabu vyenyewe nikatafsiri kutoka kwa lugha yenyewe na kuweka.
kwahivo kuna tofauti kubwa baina yangu na yako. wewe umecopy paste bila
kuhakikisha tena kwa vitabu vya kishia na tutathibitisha hilo hapo mbele na sisi
tumerudi kwa vitabu vya asili na kukuwekea yalivyo. kwa hivo hio hoja hujajibu na hilo
hoja bado yangoja majibu yako sio ubabaishaji.

(2) Hoja yetu ya pili ya kuonyesha amecopy paste na hajahakikisha anachosema ni


pale tulimkosoa aliposema UMTADUL QAARI na tukasem ni UMDATUL QAARI. na
tukamwambia atulete hicho kitabu UMTADUL....... bwana mkubwa kumwuliza pastor
mkubwa "google" akaona hapo pia hakuna majibu akajitetea na kusema
yanayoangaliwa ni maneno yaliyonukuliwa na sio spelling mistake. Lakini twamwambia
tutaangalia yaliyonukuliwa na kutoka yanayonukuliwa ni jina la kitabu ambacho
hukukinukuu vizuri na.msiba uliojee katika majibu yako tena umenukuu hivo hivo
UMTADUL. sasa tukueleweje bwana abel? yaani waonyeshwa huku.ni shimo usiingie
wadai kusema naam ni shimo lakini wazidi kuingia. Hio hoja pia hujajibu bali
umeonyesha kutumbukia katika shimo zaidi.tena katika majibu yake akanukuu kutoka
AL ISTIBASAA. hamna kitabu kama hicho babu baal ile iko ni AL ISTIBSAR. tena
kasema ALLUBAAB......... na sahihi ni AL LUBAB.........

9|Page
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

(3) Hoja yetu ya tatu ilikuwa ni hadithi tulizozileta na twashukuru kwamba abel
hakuzikanusha hizi hadithi bi maana kakubali Allah amekataza tendo hilo mpaka
kumlaani mwenye kufanya. Jamani.si mjadala umekwisha basi. twajadiliana nini zaidi
ya hapo

Lakini sasa twaongeza hadithi zingine katika mada huo na ni challenge kwa abel
kuzikanusha kama anaweza.

- Hadithi ya nne: Anasimulia Kuzaimah bin Thabit kuwa Mtume wa Allah rehma
na amani ziwe juu yake amesema "Allah haoni haya kusema kweli" mara
tatu."Msiwaingilie wake zenu kwa Tupu ya nyuma"(8)

- Hadithi ya Tano: Ali anasimulia kutoka kwa mtume rehma na amani ziwe juu
yake amesema " Wakati mmoja wenu anapotoa hewa basi afanye wudhu, na
musiwaingilie wake zenu kwa tupu za nyuma" (9)

- Hadithi ya sita: Jabir anasimulia: Mayahudi walikuwa wakisema kuwa mume


anapomwingilia mke wake kwa tupu ya mbele lakini kupitia nyuma basi mtoto
atazaliwa akiwa na kengeza. kwa hilo Allah akateremsha (ayah hii) "wanawake wenu ni
mashamba zenu kwa hivo zijieni mashamba zenu vile na wakati munayopenda." (10)

Kazi kwako bwana abel ima ukubali hizi hadithi sita ambapo zipo zingine bado na
ukubali Allah na Mtume wake wamekataza hili tendo au ukanushe hadithi hizi kwa
hoja na dalili. sio kukurupukwa tu. Hoj baado iko pale pale.

(4) Hoja yetu ya nne ilikuwa kauli za masahaba wanavyuoni wakubwa na maimamu
wakubwa ambayo bwana abel hakukanusha hata mmoja yaamanisha aliyakubali
kwamba waliharamisha.

Lakini tutaongeza na kauli zingine hapa

- Kauli ya nne: Anasimulia Abu Muhammad Abdullah bin Abdul Rahman Darimi
katika musnad yake kuwa Said ibn Yasar Abu Hubab amesema: Nilimwambia Ibn
Umar "wasemaje kuhusu kumwingilia mwanamke kwa nyuma" akasema "nini maana
yake?" nikasema " kumwingilia kwa tupu ya nyuma" akasema "kwani Muislamu
hufanya kitendo kama hicho?" (11)

- Kauli ya tano: Ali ibn Ahmad al Wahidi akielezea kwa nini ayah ya 223 ya surah
baqarah iliteremka ananukuu maswaba na wanavyuoni wengi akiwemo Jabir ibn
Abdallah, Mujahid, ibn abbas, Said ibn Musayib ambao wamesema kuwa ayah hii
iliteremshwa kwa sababu mayahudi walikuwa wanadai kuwa akiingiliwa mwanamke
kwa tupu ya mbele kupitia nyuma mtoto atakayepatikana atakuwa na macho kengeza
kwa hivo Allah akateremsha hii ayah. (12)

- Kauli ya sita: ansema sheikhul Islam Ahmad ibn Taimiyah “Kumwingilia mke
kwa tupu ya nyuma ni haramu kwa mujibu wa Quran na Sunnah na hii ndio kauli ya
wanavyuoni wa zamani na wa sasa ...... ama katika uislamu mwanamume
amekubalishwa kumwingilia mke wake kutoka pande yeyote maadamu ni kwa tupu ya
mbele. Mume akifanya kitendo cha kumwingilia katika tupu ya nyuma na mke

10 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

akakubali wote wanafaa kupatika adabu na lau wakikazana na kitendo hicho basi
watenganishwe. (13)

Abel bado ana kibarua ya kujibu kauli hizo sita badala ya kukazana na kubabaisha
hoja. Twasema hoja bado haijajibiwa

(5) Hoja ya tano tuliyotoa ni kuwa Imam Malik amesingiziwa kuwa kahalalisha
hicho kitendo na ukweli ni kuwa yeye kaharamisha kama walivyoharamisha
wanavyuoni wengine. Bwana abel hakutosheka na hilo akanukuu na copy paste zake na
kumzulia ibn Umar swahaba wa Mtume kwamba kahalilisha kitendo hicho na hilo
limejibiwa katika hoja ya nne kauli ya nne hapo juu alipouliza ibn umar. “Je muislamu
hufanya kitendo kama hicho?” na maneno kama hayo hutumiwa kama mshangao yaani
swali lililoulizwa ni la kushangaza sana mpaka ibn umar anapata na mshtuko na
mshangao. Na twamzidishia na nyingine mahali yakanushwa kuwa ibn Umar
kahalalisha

Kab bin Alqamah amesema kuwa Abu an Nadr amesema aliuliza Nafi “Watu wanasema
kuwa wewe umesimulia kutoka kwa Ibn Umar kuwa yeye amekubali wanawake
kuingiliwa kwa tupu ya nyuma” akasema “wamenizulia uongo. Wacha nikuambie
yaliyotokea. Ibn Umar alikuwa anasoma Qurani wakati mmoja na mimi nilikuwa
pamoja naye na akafika katika ayah....”na wanawake wenu ni mashamba zenu.......”
akasema “Ewe Nafi wajua yaliotokea mpaka ayah hii iteremshwe . Nikasema “La!!!’
aksema “sisi watu wa Quraish tulikuwa tukiingilia wake zetu kupitia nyuma(kwa tupu
ya mbele). Tulipohama Madina na tukaoa wanawake wa kiansari tulikuwa twataka
kufanya vivyo hivyo. Walichukia hilo na wakalifanya kuwa ni jambo kubwa. Wanawake
wa Ansari walikuwa wanafuata mila ya wahayudiambao wanawaingia wake zao wakiwa
wamelala katika ubavu wao.na Allah akateremsha “wanawake wenu ni mashamba
zenu..........”(14)

Kwa hivo hata ibn umar aliharamisha kitendo hicho na sio kama alivyosinanga abel na
kumzulia. Na tena Nafi mwanafunzi wa Ibn Umar ashakujibu zamani.

(6) Hoja ya Sita tulijibu hizo kauli alizozileta bwana abel na tukasema kuwa kauli
hizo zilikuwa na maana ya kumwingilia mwanamke kwa tupu ya mbele lakini ni kama
bwana abel haoni akadai hatujamjibu na sisi twasema MWENYE MACHO
HAAMBIWI TAZAMA. Afadhali kipofu kuliko mtu anayo macho na haoni na anadai
anaona, na ushahidi wa hilo ni hadithi nyingi tulizozinukuu pamoja na nukuu za
maswahaba na wanavyuoni wakisema ayah ya 2:223 iliteremshwa ili kukubalisha
kumwingia mkeo kwa njia yeyote maadamu wamwingilia kwa tupu ya mbele. Kwa hivo
yaliosemwa na ibn umar na imam malik na kadhalika ni kuwa ni sawa kumwingilia
mkeo kwa njia ya nyuma lakini kwa tupu ya mbele na sio tupu ya nyuma(style)

(7) Hoja yetu ya saba tulisema hata kama hao aliowanukuu abel ndivyo basi
haimaanishi huo ni msimamo wa Uislamu maana uislamu unapatikana kwa Qurani na
hadithi sahihi kwa walivyoelewa maswahaba na tumekunukulia hadithi sahihi na kauli
za maswahaba na wanavyuoni wakiwemo ibn umar na imam malik uliowasinanga kwa
uchafu na kuwazulia.

11 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

(8) Hoja yetu ya nane ilikuwa abel kuleta anagalau ayah moja katika bibilia nzima
inayokataza kitendo hicho ambayo haihitaji kigugumizi wala kubabaisha ambacho
hajafanya mpaka saa hii.kwa hivo hoja iko palepale

(9) Twaongeza hoja ya tisa kama tulivyoahidi kuwa tutaonyesha kuwa amecopy
paste kutoka kwa vitabu au website vya kishia ni pale alipoleta hadithi kutoka kwa
vitabu cha AL ISTIBSAR ambacho ni cha kishia akakiita AL ISTIBASAA na hadithi
hio imesemwa Abu Abdullah Alaihi Salam(A.S) ambacho ni kawaida cha mashia kwa
maimamu wao na sio watu wa kufuata Quran na Sunnah yaani Ahlu Sunnah wal
Jamaah. Yaani mtu anaulizwa nyanya analeta pilipili. Ni kama kujadiliana na mkristo
msabato na kuleta hoja za jehovah witness.

(10) Hoja ya kumi ni kuwa bwana mkubwa anasema tumemsingizia kuwa amesema
uongo na akadai tusahihishe mahali kanukuu vibaya. Twasema abel wewe ndio ulioleta
hizo copy paste kwa hivo wewe ndio uteletee ushahidi kwamba ni ukweli ulisemwa hivo,
ama wewe kudai kuwa umenukuu pia ni uongo maana haujanukku umecopypaste.
Naam vitabu vipo lakini umecopy paste uzushi usiokuwa na ushahidi nalo. Hapa
hatujadili kama vitabu vipo ama havipo wala sijasema maneno ya imamu malik
kumwingialia mkewe kwa tupu ya nyuma yapo kwa UMDATUL bali nimenukuu ibn
kathir anayesimulia kuwa zama za imam malik walienda wakamwuliza akakanusha.
Tuna umezusha kuwa ilikuwa imeandikwa ndio maana walimwuliza yaonyesha hata
hujui historia hali “maulana google” yupo hai. Imam Malik amefariki hapo karibu na
795AD na Imam Ayni mtunzi wa Umdatul Qari amezaliwa 1360CE sasa ilikuwaje
iandikwe miaka ya baadaye baada ya imam malik kufa ndio aulizwe imam malik?
Mbona hujielewi ewe kiumbe cha Allah? Ama wewe kudai mambo ya madrasa basi
walimu wananukuu hizo vitabu vya hadithi sio kucopy paste bila kuthibitisha na
wengine wakifunzwa huwa bukhari iko hapo na walimu na wanafunzi wanazo(their is
no blid following)

Ama kauli yako kusema “Uongo ni wangu ama waandishi” nasema ni wako na
mwandishi uliecopy paste kutoka kwake na sio watunzi wa vitabu vya asili maana
umecopy paste wewe na kutaka kuthibitisha kitu na ukawanukuu watunzi asli vibaya,
umezusha na kudanganya na hoja ambazo hazijathibiti tena kutoka kwa vitabu vya
mashiaambao wamewanukuu wanavyuoni vibaya bila wewe kuthibitisha. Haiwezekani
wewe kushirikiana na mwizi kuiba alafu udai wewe si mwizi. Bwana abel afadhali
hungejibu maana umejidhalilisha zaidi kuliko mwanzo.na ndio kawaida ya waliofilisika
hoja.

Maji yalishamwagika na hayazoleki. Out of the frying fan into the fire and this is your
state.

Mwisho: Hatutaki watu kupayuka na kuropokwa ovyo , twataka majibu ya kielimu kwa
hoja zetu 10 tulizotoa. Hatutaki ubabaishaji kama ulivyofanywa bali hoja za msingi
zikiambatana na dalili. Majibu yetu yakijibiwa yajibiwe kihoja na kidalili sio matukano
wala ubabaishaji usiokuwa na maana yeyote wala uongo na ulaghai wa watu wasiokuwa
na hoja isipokuwa kugeuza maneno.

ALLAH ANAJUA ZAIDI

12 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

3.ABEL SULEIMAN ANAJIBU:


Akasha Opato Daawah
Katika maelezo yako hayo marefu sijaona sehemu hata moja ambayo umenukuu
Hadithi ambazo mimi nimezinukuu.

Badala yake unaleta stori na hadithi zingine, rejea kwenye post yangu kuna sehemu
nimesema kuwa waislamu wameruhusiwa kuwafira wake zao?

Hebu nukuu hadithi hizo Umdatul ... na Irshadul... unionyeshe ni sehemu gani
nimeongea uongo?

Halafu unakomalia copy na paste hahahaha.... hivi Mwandishi wa Alu lu Walmarjan


ambaye amechukua hadithi za Bukhar na muslim, mimi nikinukuu humo nitakuwa na
makosa mpaka nikatafute BUKHARI NA MUSLIM NZIMA?

Madrasa wanafunzi wafundiswapo hadithi hupelekewa BUKHARI juzuu 9? mbona


unakuwa na hoja za kitoto kaka?

Nasubiri uzinukuu hizo hadithi ambazo mimi nimeziweka unionyeshe wapi


nimeongopa?

13 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

3.JIBU KUTOKA KWA ABU RASHIDA


Sifa njema ni za Allah Muumba Mbingu pasina nguzo na sala na salamu zimwendee
kipenzi chetu mtume muhammad na ahli zake na masahaba wake na kila anayewafuata
juu ya ongofu mpaka siku ya Qiyama.

Ama baada ya kumhidi Allah na kumtakia rehma na amani kipenzi chake twashukuru
tena sana kwa majibu ya bwana abel maana hakuweza kujibu hoja zetu kumi bali
kafikia hatua akauliza

"rejea kwenye post yangu kuna sehemu nimesema kuwa waislamu wameruhusiwa
kuwafira wake zao?"

kumbe kakubali waislamu hawajaruhusiwa kuwafira wake zao na jamaa IBN UMAR ni
muislamu tena Swahaba, imam Malik na Imam Shafii pia waislamu tena maimamu
itakuwaje wao wafanye kitendo hicho hali asiekuwa muislamu kama abel anajua
haijaruhusiwa. Hivi abel huoni umeingia mtego na umejijibu mwenyewe?
Pili kama wakubali waislamu hawajaruhusiwa post yako na kuquote kauli za
wanachuoni kwamba walifanya kitendo hicho ilikuwa na maana gani? Huku ndio
tunasema "Preaching water and drinking wine"

"katika sehemu hata moja ambayo umenukuu hadithi ambazo mimi nimezinukuu"

Naam sikuzinukuu maana wewe mwenyewe hukuzinukuu pia na umetoa kwa vitabu vya
kishia kama tulivyoelezea katika hoja yetu ya kumi. Yaani wewe usinukuu alafu wataka
nipa kibarua ya kukunukulia. unilete chakula mbovu ukisema ni safi. ukionyeshwa
uchafu wake wataka nikusafishie ndio ule. Msiba mkubwa. tena hizo SI HADITHI
ulizonukuu ni maneno ya wanachuoni. Kumbe hata maanya hadithi hujui. wacha
nikufunze
"Hadithi ni kauli ya mtume,au vitendo vyake au vitu vilivyofanywa mbele yake na
hakukataza au description yake" na hio hata mtoto mdogo anajua nashangaa abel hajui
sio maneno ya imam malik au imam shafii. kaa chini usomeshwe sio kukurupukwa
ovyo.

"badala yake unaleta story n hadithi zingine"


Mfa maji haachi kutapatapa ndivo walivyosema wahenga. hamna mahali nimenukuu
story ewe abel. nimenukuu kauli za wanachuoni wakiwemo uliowasingizia na wakasema
hawajahalilisha zaidi ya hapo wataka nini? Ama hadithi nilizonukuu ndio zilikupelekea
ukasema kwamba hujasema mahali waislamu wamekubaliwa hicho kitendo na
ubarikiwe.

"Hebu nukuu hadithi hizo umadatul na irshadul unionyeshe ni sehemu gani nimeongea
uongo"
Mwenye macho haambiwi tazama. Hoja yetu ya tano sita na saba zimeongelea kauli hizo
n tukakupa majibu yenye kukinaisha, sasa kama huoni hatuwezi kukusaidia. waambie
waliona macho wakusaidie kusoma.
wataka tukunukulie hizo kauli na mwenye wadai ushanukuu. sasa sisi tutakufundisha
maana ya maneno hayo ama tuanze kunukuu tena?

14 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

"halafu unakwamilia copy paste hahaha"


Hio lugha ni ya watu waliofilisika hoja na hawana la kusemandio hufanya mzaha za
kisampuli hizo kwa mambo ya dini

umesema mambo ya lulu wal marjan


Mwenyewe umesema NIKINUKUU kutoka kwa lulu wal marjan. kumbe utafungua lulu
wal marjan ukifungue uhakikishe sio KUCOPY PASTE kutoka maadui wakubwa na
mtunxi walulu wal marjan ukadai umenukuu. labda sasa tukufunze lugha na huu ni
msiba

"Madrasa wanafunzi wafundshwapo hadithi hupelekewa BUkHARI juzuu 9? mbona


unakuwa na hoja za kitoto kaka?"

sasa wakifunzwa juzuu ya kwanza wataka wapelekewe juzuu hizo nane zingine ewe mja
wa Allah? sasa hoja za kitoto ni nani anazo? na wanaosomeshwa vitabu vya hadithi
husomeshwa kama vitabu vimefunguliwa sio copy paste za adui wa vitabu hizo.

Kimsingi bado kibarua cha kujibu hoja zangu kumi ziko pale pale. na kama huna jibu
sema huna. umedai malik amekubali kitendo hicho imam malik ansema umemzulia
uongo na mimi nasema naam umemzulia uongo

Lete hoja na dalili kwa post zangu kumi

15 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

4.Godphrey Switi Mfuatiliaji wa Mjadala


Tunafuatilia sana hoja zenu wewe na Abel hongereni kwa hilo kwanza.

Katika maelezo yako ya hii comment yako ya mwisho umedai Abel kanukuu hadithi
hizo toka ktk vitabu vya Kishia.

Shia ni waisilam au wapagani?

Sunni ni waisilamu au wapagani?

Unapoandika ameukuu toka ktk vitabu vya Kishia unamaanisha alivyoandika Abel
kweli vipo ila vimetoka kwa Shia sio Kwa Sunni.

Ndugu yangu Humpty Humpty alijieleza Ukweli jinsi jinsi alivyofindishwa maandiko na
akayaelewa.

Kaeleza jinsi ya kutumia njia ya kumuingilia mwanamke ktk tupu ya mbele ikiwa
kakupa mgongo sio kumuingilia ktk tupu ya Nyuma.
Katoa maelezo ambayo mtu unaelewa kuwa amefunzwa ukweli huo toka ktk roho yake.

Hivyo vitabu Imam Malik anasema katoka kikoga kwa ajili hiyo ana maanisha nini
Okasha?

Halafu hao walioenda lkumuuliza kama kweli alimfiwa mkewe akakataa walipata wapi
hizo taarifa za Imam kumfira mkewe?

Tusaidieni kiandika kwa kuirudia hadithi moja moja na unaitolea maelezo kuwa
aliyeandika alikuwa na lengo gani na nyinyi sunni?

Ukisema Wakristo wanaabudu sanamu unawajumuisha wote kitu ambacho sio


kweli,mpaka ufundishwe kuwa kuna madhehebu mengi ndani ya Ukristo.
Pia ktk up uislam mna madhebu mengi lakini mnadai uislam ndio dini ya kweli wakati
mnakataana ninyi kwa ninyi.

Tuelezeni kwann mnayakataa aliyoandika Abel neno kwa neno,hadith hizo hatasimulia
Abel yeye kapaste kama wewe ulivyopaste hizo ulizotolea maelezo.

Asanteni kwa mjadala mzuri wenye ustaarabu na hekima!

.
16 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

Godphrey Switi > Kwanza shukran kwa hongera zako na twatumaini wasoma hio
mjadala kwa utulivu bila ushabiki na natumai mwishowe utafungukiwa na kuona nuru
mahali ilipo na giza ilipo.

Abel bado anakibarua ya kunijibu hoja zangu kumi na natumai atazijibu kwa hoja na
dalili

"Umedai kuwa abel kanukuu hadithi hizo kutoka vitabu vya shia"

Naam nimedai hivo na ni kweli kwa ushahidi niliotoa

"Shia ni waislamu au wapagani? Sunni ni waislamu au wapagani?"

Hio ni mada refu kaka ila kwa ufupi kuna itikadi zingine ambazo ni za kikafiri mashia
WENGINE wanaamini kwa hivo twasema huo ni itikadi ya kikafiri ama kumkufurisha
mmoja mmoja hio ni kazi ya wanachuoni baada ya kujua kwa yule jamaa
amesimamishiwa hoja ameelewa lakini bado ameshikana na itikadi hio ya kikafiri
baada ya kujua ni ukafiri. ama sunni ni mwenye kufuata Quran na Sunnah

"unapoandika amenukuu toka katika vitabu vya kkshia unamaanisha alivyoandika abel
kweli vipo ila vimetoka kwa shia sio kwa sunni"

Naam kuna hadithi moja amenukuu kutoka kwa vitabu vya kishia na hadithi hio ni
mbovu haina mashiko.
ama hivo vingine alinukuu ni kauli za maulamaa lakini kutoka kwa vitabu vya kishia
ambao wamegeuza maana kama tulivyoeleza mimi na ndugu yangu humpty humpty.

Ama hio maelezo uliotoa alivyoeleza humpty humpty ndivyo nilivyoeleza mimi
na.nikaeleza mashia wamegeuza tafsiri na nikaeleza pia hata kama ni sahihi si hoja
maana Quran na Hadithi za mtume ni kinyume na hayo

"Imam malik anasema katoka kukoga kwa ajili hio ina maana gani"

Ina maana imam malik alimwingilia mke wake kwa tupu ya mbele lakini kupitia nyuma
na baada ya kutenda hicho kitendo ameenda kukoga ambayo yaitwa kuoga janaba. hili
nalo mada ingine

"halafu walioenda kumuuliza kama kamwingilia mkewe kwa tupu ya nyuma akakataa
walipata wapi hizo taarifa za imam kumfanyia mkewe kitendo hicho"

Hawakuemda kumwuliza kama kamfanyia kitendo hicho bali kama alihalalisha hicho
kktendo maana kivumi kilikuwa kimeenea kwa wale waliom "MISQUOTE" ndio
akakataa kuhalilisha na akasema ameharamisha.

Ama maelezo tushayatoa na kaka humpty pia ashatoa na hio ndio ilikuwa maana ya
imam malik na ibn.umar

Ama hilo mada la wakristo kuabudu miungu mingi ni mada ya siku ingine

17 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

"pia katika uislamu mna madhehebu mengi lakini mnadai uislamu ndio dini ya kweli
wakati mnakataana nyinyi kwa nyinyi"

Hilo pia mada ya siku ingine lakini kwa ufupi uislamu ni Quran na Hadithi
walivyoelewa maswahaba na wwma.waliotangulia. Ama madhehebu mengi ama watu
wakihitafiana wanarudi kwa Quran na Hadithi. ama kukataana hilo ni uislamu ni
wanaoitwa waislamu na hio ni wao watakujibu kwa nini wanafanya hivo.

Ama wewe kusema mimi nimecopy paste huo nadhani nishajibu. mimi nimenukuu
maana vitabu vyenyewe mahali nimenukuu ila abel amecopy paste kutoka kwa vitabu
vya kishia

Ama kama ulivyoona ukitumia lugha ya heshima nasi pia twatumia lugha ya heshima.
ukidandia gari kwa mbele sisi pia tutaidandia na humo humo alafu asije mtu akasema
sisi ni wakali.

Twashukuru wewe kufuatilia mjadala na twaomba uone nuru na uifuate na uone giza
na uiepuke.

ALLAH ANAJUA ZAIDI

5.ABEL SULEIMAN ANAJIBU:


18 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

Nikupongeze kwa kukubali kuwa ni kweli HIVYO vitabu ambavyo nimevinukuu ni


kweli vimeandikwa hivyo na Mashia, (Ambao pia ni Waislamu) Kwa maana hiyo mimi
sina kosa, maana umethinitisha kuwa hayo sijayatunga mimi, wala kubadili tafsiri kama
alivyoongopa Humpty Humpty kuwa mimi ndiye nimetunga.

Sasa huo ugomvi wenu wa SUNI VS SHIA mimi haunihusu, kipondo nawapa nyote
maana ni nyote mnaojiita Waislamu, kama ambavyo ninyi mnavyotuuita Wakristo
Makafiri, bila kubagua dhehebu...

Ikifika kwenu msitake tuwatenge wakati nyote ni wale wale, SHIA wanakubali kuwafira
wanawake zenu katika uislamu ni ruksa.... sijui kama wewe nawe huwa unamfira mkeo
(‫ )ملعا هللا‬Kwa hivyo siku nyingine usirudie kunishutumu kwa Hadithi ambazo
sijaziandika mimi.

Hamuwezi kunipangia eti nisitumie Hadithi za mashia nitumie Hadithi za Suni.. yaani
kwangu mimi Suni na Shia wote ni wamoja, wote ni makafiri kwangu.... kwa hivyo
hakuna hata mmoja ambae ana unafuu kwangu.

Kiwe ni kitabu cha Kishia, Kisuni, Ki Answar.... Ki Ahmadia, maana nyote


mnajitangaza kuwa ni waislamu basi nyote mpo kundi moja.

Labda tu kama mtaamua kuvichoma vitabu vyote vya KISHIA na kutangazw kuwa vya
Kisuni ndo sahihi, hapo sasa nitadili na vitabu vya kisuni tu.

.
“Nikupongeze kwa kukubali kuwa ni kweli HIVYO vitabu ambavyo nimevinukuu ni
kweli vimeandikwa hivyo na Mashia, (Ambao pia ni Waislamu) Kwa maana hiyo mimi

19 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

sina kosa, maana umethinitisha kuwa hayo sijayatunga mimi, wala kubadili tafsiri kama
alivyoongopa Humpty Humpty kuwa mimi ndiye nimetunga.”

Ni wapi nimesema hivyo ndivyo ilivyoandikwa katika VITABU VYA ASILI? Mbona
huelweki ewe mja wa Allah?sijui wataka kujihalalishia hicho kitendo ukidai kwa jina la
waislamu wakati mtume ashasema kuwa Allah amemlaani mwanamume mwenye
kufanya kitendo hicho. au una maslahi na mashia. Mbona sikuelewi? Husemezi
hueleweki. Mimi nimedai umecopy paste kwa vitabu vya mashia ambao ni maadui wa
masunni na hapo haliitwi kunukuu maana ungenukuu basi ungenukuu kutoka kwa
vitabu vya masunni ambao wanafuata Quran na Hadithi sio mashia. Tena
tumethibitisha kuwa hio tafsiri hio bali Imam Malik na Nafi wanasema kuwa
wamezuliwa na ni uongo.

“Sasa huo ugomvi wenu wa SUNI VS SHIA mimi haunihusu:


Ndio maana ukacopy paste kutoka kwa vitabu vya mashia maadui wakubwa wa
masunni(hatuzungumzi maamuma wa kawaida bali wanachuoni miongoni mwa mashia)
maana haikhusu maadama uponde uislamu sio kwa watu ambao hawajui?

“kipondo nawapa nyote maana ni nyote mnaojiita Waislamu”


Kwa msingi mimi nasema hata jehova witness wanadai yesu si mungu kwa maana hio
wakristo wote wanaofuatilia wajue Yesu si mungu katika ukristo maana hata jehova
witness wanajiitwa wakristo. Kama wataka twende hivo basi na twende hivo.

“kama ambavyo ninyi mnavyotuuita Wakristo Makafiri, bila kubagua dhehebu...”


Hilo mada la wakati mwingine na kama walitaka fungua hio mada kwa post ingine –
isipokuwa wakristo wenyewe hawaelewani hata Mungu wao ni nani? Allah anasema
kuna waislamu na makafiri. Sasa ili wewe usiwe kafiri wafaa uwe..................? Jijazie

“Ikifika kwenu msitake tuwatenge wakati nyote ni wale wale”


Msiba ulioje basi hata jehovah witness na nyinyi ni wale wale si hata sisi tuseme
WAKRISTO HAWAMJUI MUNGU WAO NI NANI. Sio sisi tunatenga, ni Quran na
Hadithi za bwana mtume ndizo zinawatenga . na uislamu ni Quran na Sunnah
walivyoelewa maswahaba.

“SHIA wanakubali kuwafira wanawake zenu katika uislamu ni ruksa.... sijui kama
wewe nawe huwa unamfira mkeo (‫م(”لعا هللا‬
Naona ni kama screw za akili sasa zimepotea. Hapo mbeleni uliuliza ni wapi umesema
kuwa waislamu wameruhusiwa vitendo hivo ukiwa na maana hujasema na hapa
unasema katika uislamu ni rukhsa. Sasa wewe tukueleweje? Tuseme umekuwa kipofu
hukuona hizo dalili zote tulizotoa ama ni mkaidi tu?Mtume anasema atakaefanya
kitendo hicho ana laana sasa mimi nitafanyaje kitendo hicho ama ukisema mashia
wanakubali kitendo basi ni wao tena wana............ ya Allah. Jijazie mwenyewe. Na huo si
uislamu bali ni ushia na uwaulize wao walikotoa.

“Kwa hivyo siku nyingine usirudie kunishutumu kwa Hadithi ambazo sijaziandika
mimi”
Sisi twasema siku ingine usijaribu kupost vitu ukidai ni uislamu na kumbe ni ushia na
ukome katika hilo. Bado narudia wewe ni mwongo, umezua, umefanya ubabaishaji na
ukome katika hilo. Ukimsaidia mwizi pia wewe ni mwizi. Ukiwasaidia mashia kuzua na
kusema uongo kuzua na kubabaisha hoja na wewe pia umo humo.

20 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

“Hamuwezi kunipangia eti nisitumie Hadithi za mashia nitumie Hadithi za Suni”


Ni kweli hatuwezi ila hio yapangwa na akili yako mwenyewe ukijua wajadiliana na nani.
Labda tuseme akili imepiga shot ndio maana hata hujui unayejadiliana naye ni nani na
ana amini nini? Ni kama kujadiliana na watu ambao hawaamini mungu ukiwaletea
vitabu vya wanaoabudu moto. Utaonekana akili kidogo ina matatizo kaka. Jirekebishe.

“yaani kwangu mimi Suni na Shia wote ni wamoja, wote ni makafiri kwangu.... kwa
hivyo hakuna hata mmoja ambae ana unafuu kwangu.”
Kwanza ungetupa taarifa ya kafiri ni nani ndio utuite makafiri ingekuwa umefanya la
maana. Ndio tujue nani kweli kafiri na nani sie. Ila Quran imeweka wazi. Kuna
waislamu na makafiri...... sasa wewe jijazie uko wapi.

“Kiwe ni kitabu cha Kishia, Kisuni, Ki Answar.... Ki Ahmadia, maana nyote


mnajitangaza kuwa ni waislamu basi nyote mpo kundi moja.”
Ahmadia ni makafiri hakuna pingamizi katika hilo. Mormon, Wasabato, Wakatoliki na
Jehova Witnes wote wakristo na hawajui Mungu wao ni nani?

“Labda tu kama mtaamua kuvichoma vitabu vyote vya KISHIA na kutangazw kuwa
vya Kisuni ndo sahihi, hapo sasa nitadili na vitabu vya kisuni tu.”
Ukiawa akili maji usitaraji wengine wapo hivo. Ukitaka kujadiliana ushia MIMI NIKO
TAYARI KUKUTHIBITISHIA UKAFIRI UNAYOPATIKANA KUTOKA KWA
VITABU VYA WANACHUONI WAO. Ila naona watutoa mada.

NATIJA NA MWISHO WA MJADALA


1) Tumethibitisha kuwa kumwingilia mwanamke katika tupu ya nyuma ni haramu
kwa mujibu wa Allah na Mtume Muhammad mpaka anayefanya akalaaniwa na
pia kutoangaliwa na tukatoa marejeo (1), (2), (3), (8), (9), (10)

21 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

2) Tumethibitisha kwa maneno ya maswahaba na wanavyuoni wakubwa kuwa


kitendo hicho ni haramu na tukatoa marejeo (4), (5), (6), (11), (12), (13)

3) Tumethibitisha pia kuwa maswahaba na maulamaa waliosinangwa kuwa


wamekubalisha kitendo hicho wamesema ni uongo na wamezuliwa na tukatoa
marejeo (7), (11), (14)

4) Pia tumesema hata kama ni kweli basi huo haiwi uislamu bali unakuwa ni
msimamo wao

5) Pia tumethibitisha kuwa maneno ya abel ni ya kuzua na ni uwongo wa wazi


kutoka kwa vitabu vya kishia ambao wamewanukuu wanavyuoni vibaya na hata
ni kweli haiwi hoja

6) Pia tulimtaka abel alete ayah moja kutoka bibilia iliyoharamisha kitendo hicho
na hakuleta wala hakugusa hata sijui ina maana hicho kitendo halali kwa
wakristo au nini...... Hio mtajijazia wenyewe

Mwisho ni kusema ukitaka kujua kitu wafaa kuenda kwa asili yake na ukitaka kujua
Uislamu rudi katika Quran na Hadithi sahih walivyoelewa maswahaba.
Twatarajia kuwa wasomaji watasoma mjadala huu kwa uso wa insafu na kufanya
juhudi kusoma na kuelewa bila ushabiki na huenda Allah akawaongoza Ameen

MAREJEO
(1)Sunan Ibn Majah Juzuu ya 3. Sura ya 29 katika mlango wa Nikah uk wa 101 Hadithi
Nambari 1923

(2)Jami at Tirmidhi Juzuu ya pili Sura ya 12 katika mlango wa Kunyonyesha uk wa 533


hadithi nambari 1165
22 | P a g e
ULIWATI WA WANAWAKE KWA MUJIBU WA UISLAMU NA UKRISTO

(3)Sunan Abu Dawud Juzuu ya pili Surah ya 44/45 Katika mlango wa Nikah uk wa 559
hadithi nambari 2162

(4)Tanwir al Miqbas min Tafsir Ibn Abbas Tafsiri ya 2:223 Uk wa 48

(5)Tafsir ibn Kathir. Mukhtasari Juzuu 1-10 uk wa 553

(6)Tafsir al jalalain uk wa 58

(7)Tafsir ibn Kathir. Mukhtasari Juzuu ya 1-10 Uk wa 557

(8)Sunan Ibn Majah Juzuu wa 3 Sura ya 29 katika mlango wa Nikah uk wa 101 Hadithi
nambari 1924

(9)Jami al Tirmidhi Juzuu ya 2 Sura ya 12 katika mlango wa kunyonyesha uk wa 534


Hadithi nambari 1166

(10)Sunan Abu Dawud Juzuu ya 2 Sura ya 44/45 katika mlango wa Nikah uk wa 559
Hadithi nambari 2163

(11)Tafsir Ibn Kathir Mukhtasari Juzuu 1-10 uk wa 557

(12)Asbab Al Nuzul Tafsiri ya Ayah 2:223 uk wa 38

(13)Fatawa za wanawake waislamu ya Ibn taimiyah uk wa 177-178

(14)Tafsir Ibn Kathir Mukhtasari Juzuu 1-10 uk wa 556

23 | P a g e

You might also like