Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, 2116898 OFISI YA RAIS,


IKULU,
Baruapepe: press@ikulu.go.tz
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
Tovuti : www.ikulu.go.tz 11400 DAR ES SALAAM.
Nukushi: 255-22-2113425 Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John


Pombe Magufuli leo tarehe 25 Juni, 2019 amezindua ghala na
mitambo ya gesi ya mitungi inayotumika kupikia (Liquefied
Petroleum Gas – LPG) inayomilikiwa na kampuni ya
Watanzania iitwayo Taifa Gas Tanzania Limited katika Wilaya
ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taifa Gas Tanzania Limited Bw.


Hamisi Ramadhani ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa wa
upanuzi wa ghala na mitambo ya gesi iliyopo Kigamboni
umefanyika kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2018 ambapo
umeongeza uwezo wake kutoka tani 1,650 hadi kufikia tani
7,650.

Uwekezaji huu umekwenda sambamba na ujenzi wa maghala


na mitambo ya gesi katika Mikoa 20 hapa nchini kwa
gharama ya shilingi Bilioni 150 na hivyo kuifanya Taifa Gas
Tanzania Limited kuwa kampuni kubwa zaidi ya uwekezaji
kwa idadi ya mitambo na kwa ukubwa wa ghala lenye
mitambo ya kisasa kuliko yote Mashariki na Kusini mwa
Afrika.

Bw. Hamisi Ramadhani ameongeza kuwa uwekezaji huu


umezalisha ajira za moja kwa moja 260 na zisizo za moja
kwa moja 3,500 na kwamba pamoja na kuuza Tanzania
kampuni hiyo inasambaza gesi katika nchini za Uganda,
Rwanda, Burundi, DRC na Sudani Kusini.

1
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw.
Rostam Azizi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuweka
na kusimamia mazingira yenye usawa kwa wafanyabiashara
na wawekezaji wote na kwamba kutokana na mazingira
mazuri ya kufanyia biashara anatarajia kuongeza uwekezaji
wa miradi mingine yenye thamani ya shilingi Bilioni 500
katika miaka 3 ijayo.

“Msimamo wako thabiti dhidi ya matendo ya zamani


ya ujanjaujanja katika biashara na uwekezaji, na
ukwepaji wa kodi, ndivyo ambavyo leo hii
vimetufanya baadhi yetu ambao kwa miaka tuliamua
kuwekeza mitaji nje ya Tanzania, kupata moyo wa
kuanza tena kurejesha mitaji hapa nyumbani”
amesisitiza Bw. Rostam Azizi huku akitoa wito kwa
wafanyabiashara wenzake kutambua kuwa milango ya
uwekezaji Tanzania iko wazi kwa uwekezaji madhari
wanafuata sheria, taratibu na kanuni za nchi.

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani ameeleza


kuwa kufuatia juhudi mbalimbali zilizofanywa na Serikali
kuanzia mwaka 2015 hadi sasa sekta ya nishati imepata
mafanikio makubwa ikiwemo kuongezeka kwa Watanzania
wanaotumia gesi ya kupikia kutoka Milioni 1 hadi Milioni 2.5,
kuongezeka kwa uwezo wa nchi kupokea gesi kutoka tani
220,000 hadi tani 617,000 (ongezeko la asilimia 240),
kampuni 8 za gesi ya kupikia kuajiri Watanzania 12,000 na
uzalishaji wa umeme kuongezeka kutoka megawati 1,280
hadi kufikia megawati 1,601.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Rais Magufuli


ameipongeza kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited kwa
uwekezaji huo na Wizara ya Nishati kwa kusimamia vizuri
sekta ya nishati nchini ikiwemo kuongeza upatikanaji wa gesi
ya kupikia kwa Watanzania, kuongeza usambazaji wa
umeme kutoka vijiji 2,018 mwaka 2015 hadi kufikia vijiji

2
7,318 hivi sasa na kwa kuhakikisha matatizo ya kukatika
umeme yaliyokuwepo awali yanapungua kwa kiasi kikubwa.

Mhe. Rais Magufuli amewahakikishia Watanzania kuwa


Serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuongeza
uzalishaji wa umeme kupitia miradi mikubwa ikiwemo miradi
ya Mto Rufiji na Mto Ruhuji Mkoani Njombe ili kufikia
megawati 5,000 zitakazowezesha kupunguza bei ya umeme
na kukuza viwanda.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza sekta binafsi kwa


uwekezaji uliofanywa katika sekta ya gesi ulioongeza
uzalishaji wa gesi ya kupikia kutoka tani 17,000 mwaka 2015
hadi kufikia tani 92,500 hivi sasa na amewakaribisha
wafanyabiashara na wawekezaji wengine wa ndani na nje ya
nchi kuja kuwekeza hapa nchi kwa kuwa Serikali ipo tayari
kushirikiana nao.

Ametoa wito kwa Taifa Gas Tanzania Limited na wawekezaji


wengine wa sekta ya gesi kupanua huduma zao hadi vijijini
ili Watanzania waondokane na matumizi ya mkaa na kuni
katika kupikia na badala yake watumie gesi.

“Uwekezaji huu uliofanywa na Taifa Gas Tanzania


Limited ni uthibitisho kuwa Serikali inapenda sekta
binafsi, tunataka wawekezaji wa kweli sio maneno
maneno, na wewe Rostam Azizi kama kuna
wawekezaji huko walete, na umeniambia kiwanda
chako cha ngozi kilichopo Morogoro kitakuwa tayari
baada ya miezi 3, nitakuja” amesisitiza Mhe. Rais
Magufuli.

Kuhusu changamoto mbalimbali za Wilaya ya Kigamboni


ikiwemo mradi mkubwa wa nyumba zilizojengwa na Shirika
la Hifadhi ya Jamii la NSSF uitwao Dege, Mhe. Rais Magufuli
amesema pamoja na kwamba mradi huo umezingirwa na

3
ufisadi, Serikali inasubiri Mamlaka husika ikiwemo NSSF na
wananchi kutoa maoni ya nini kifanyike.

Sherehe za uzinduzi wa ghala na mitambo ya gesi ya Taifa


Gas Tanzania Limited zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo viongozi wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na
Usalama, viongozi wa Dini, viongozi wa vyama vya siasa,
wawekezaji mbalimbali na viongozi wa Mkoa wa Dar es
Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul
Makonda.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
25 Juni, 2019

You might also like