Waraka Wa JK Na. 4 Wa 2019 - Kuhusu Matakwa Ya Kuzingatia Sheria

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

OFISI YA JAJI KIONGOZI,

22 Barabara ya Kivukoni,
S.L.P 9004,
DAR ES SALAAM

Kumb. CHA 116/331/01/ 41 19 Julai, 2019

Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wote:


Arusha, Bukoba, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya,
Moshi, Mtwara, Mwanza, Songea, Sumbawanga,
Shinyanga,Tabora, Kigoma, Musoma,Tanga,Divisheni za
Ardhi, Kazi,Biashara na Makosa ya Rushwa na Uhujumu
Uchumi na Kitengo cha Usuluhishi (Dar es Salaam);
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu,
MAHAKAMA YA TANZANIA;
Waheshimiwa Naibu Wasajili Wote,
MAHAKAMA YA TANZANIA;
Waheshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wote,
Mahakama za Hakimu Mkazi, Mahakama za Wilaya na
Mahakama za Mwanzo,
MAHAKAMA YA TANZANIA
YAH: WARAKA WA JAJI KIONGOZI NA.4 WA 2019 KUHUSU
MATAKWA YA KUZINGATIA SHERIA KATIKA UFUNGUAJI NA
USIKILIZAJI WA MASHAURI. YA JINAI MAHAKAMA KUU,
MAHAKAMA ZA MAHAKIMU NA MAHAKAMA ZA MWANZO Ill
KUEPUKANA NA MSONGAMANOWA MAHABUSU USIO WA LAZIMA
Tafadhali rejeeni mada hiyo hapo juu,
Kama mnavyofahamu; Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura
ya 20 R.E.2002 na Sheria zingine zinavyo vifungu vya sheria ambavyo kama
vitazingatiwa magereza yetu hayatalemewa na mahabusu. Sheria hizo zina
vifungu vinavyohusika na:-
a) Wajibu wa kutoa taarifa ya kutendeka kwa jinai au taarifa ya
mpango wa kutendeka jinai;

Page 1 of 4
b) Uandikishaji wa maelezo ya mlalamikaji na haki ya
mtuhumiwa/mshitakiwa kupata maelezo ya mlalamikaji pamoja na
hati ya mashtaka pale kesi inapofunguliwa mahakamani;
c) Uandikishaji wa maelezo ya mashahidi rnballmball wa mashtaka na
yale ya washtakiwa;
d) Utaratibu wa kutolewa kwa dhamana polisi kwa makosa
yanayodhaminika pale ambapo polisi hawajakamilisha upelelezi;
e) Utaratibu wa kutolewa kwa dhamana mahakamani kwa makosa
yanayodhamika kwa kufuata vigezo vya ki-sheria baada ya
mtuhumiwa kufikishwa mahakamani; , I

f) Utaratibu wa kuiomba mahakama isitoe dhamana kwa maslahi ya


umma kwa kufuata misingi ya sheria;
g) Utaratibu wa kuwaweka wahalifu chini ya uangalizi wa polisi au
mahakama bila kuwafungulia mashtaka na kuwafanya wakae
mahabusu;
h) Utaratibu wa kuupa uhuru upande wa mashtaka kuwasilisha
mashahidi wake na kufunga kesi yake ilimradi unayo nia ya dhati ya
kuwaleta mashahidi hao;
i) Utaratibu wa kuupa upande wa utetezi kuwasilisha ushahidi wake;
j) N.k
Aidha, mnafahamu kwamba sheria inamtaka kila Jaji na Hakimu kutoa
hukumu ndani ya siku tisini kuanzia siku alipokamilisha usikilizaji wa kesi
husika.

Kwa upande wa wapelelezi na waendesha mashtaka ni vyema


mfahamu kwamba Tangazo la Serikali Na. 296 la 2012 linatoa mwongozo
kwa kesi nyingi isipokuwa zile zinazohusisha makosa makubwa wa
kukamilishwa kwa upelelezi kabla ya kufunguliwa kwa kesi mahakamani.
Aidha, yapo Maelekezo ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya tarehe 3 Novemba,
2008 ''DPP instructions on Appropriate measures in line with the control of
public prosecutions in the countty"ambayo kupitia kipengele cha 4 yanaitaka
Mamlaka husika kumwajibisha mwendesha mashtaka au mpelelezi ambaye
kwa hila atasababisha haki kutotendeka.

Page 2 of 4
Sambamba na hatua hiyo, vipo vikao vya Jukwaa la Haki -Jinai na vile
vya kusukuma kesi ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa ambavyo ni nyenzo za

.
kuziwezesha Mamlaka zinazohusika na utoaji wa Haki-Jinai kutatua
changamoto zinazojitokeza katika ngazi mbalimbali katika nchi yetu.

Kwa kuwa imebainika kwamba tatizo la msongamano wa mahabusu


kwenye magereza yetu limeendelea kurudlsha nyuma nia ya dhati ya Serikali
kuboresha mifumo ya utoaji haki nchini hatua ambayo ilimlazimu Mhe. Dkt
John Pombe Joseph Magufuri, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
kutembelea Gereza Kuu Butimba Mwanza mnamo tarehe 17/7/2019 na:..
kusikitishwa sana na hali hiyo, Mahakama kwa kutambua kwamba Mhe. Rais
ametoa maelekezo kwa Wizara ya Katiba na Sheria na vyombo
vinavyosimamia utoaji haki nchini kuchukua hatua stahili kuondoa kadhia
hiyo mnaelekezwa kwa nafasi zenu mchukue hatua zifuatazo: -
a) Hakikisheni kesi zinazofikishwa mahakamani zina kidhi matakwa ya
kusajiliwa ki-sheria na zinaposajiliwa hakikisheni mienendo hiyo
inaendeshwa kwa kuzingatia matakwa ya sheria ambayo baadhi
yametajwa hapo juu;
b) Hakikisheni kesi zinasikilizwa na kutolewa hukumu/uamuzi katika
muda uliowekwa na sheria na kwa kuzingatia malengo ya
Mahakama;
c) Hakikisheni fursa za adhabu mbadala ya kifungo cha jela inapewa
kipau-mbele kwa kufuata sheria;
d) Hakikisheni vikao vya kusukuma kesi vinafanyika kadri ya Waraka
wa Mhe. Jaji Mkuu Na.2/1987 kama ulivyorekebishwa. mwaka 2003
na 2011 na mchukue hatua zinazostahili kutekeleza maazimio yake
vikao ambavyo Mahakimu Wafawidhi, Naibu Wasajili na Msajili
Mahakama Kuu ndio wenyeviti;
e) Hakikisheni Mahakama inashiriki kikamilifu kwenye vikao vya
Jukwaa la Haki-Jinai ngazi zote; na
f) Hakikisheni Mwongozo wa Ukaguzi unafuatwa kama ulivyo ikiwa ni
pamoja na kuwafichua watumishi wa mahakama watakaotuhumiwa
kwa vitendo vya Rushwa;
Pamoja na hayo hapo juu, endapo Jaji au Hakimu atajiridhisha kwamba
kuwepo kwa vitendo vya hila vinavyohujumu mwenendo wa kesi iliyo mbele
yake mamlaka-asili ya kuondosha mashtaka (dismissing charge) na
kumwachia huru mshitakiwa ( discharging the accused) itabidi yachukue
Page 3 of 4
mkondo wake kama ilivyoamriwa katika ukurasa wa 13 wa uamuzi wa
Mahakama ya Rufani katika Rufaa ya Jinai Na. 322 ya 2015- Abdallah
Kondo v. Republic, Dar es Salaam. Uamuzi huo umeambatishwa kama
Kiambatisho 'A');
Maelekezo yaliyo katika Waraka huu ambayo yamelenga kukumbusha
wajibu wenu unaoendana na viapo vya Waheshimiwa Majaji na Mahakimu
yafikishwe pia kwa Waheshimiwa Mahakimu wote katika himaya zenu na
kaguzi zijazo zitafuatilia utekelezaji wa Waraka huu.
Nawatakia kazi njema na mafanikio katika utumishi.
I
I

Eli er M. Feleshi (PhD)


All KIONGOZI
Nakala: r"''"=-- ]AJI KIONGOZI
· MAHAKA_MA KUU YA T. ·
Mhe.Prof.lbrahim H. Juma (PhD , - ···-·----~-~------..;_.)
Jaji Mkuu,
Mahakama ya Tanzania,
DAR ES SALAAM

Mhe. Hussein H. Kattanga,


Mtendaji Mkuu,
Mahakama Kuu ya Tanzania,
DAR ES SALAAM-

Mhe. Katarina Revokati,


Msajili,
Mahakama ya Tanzania,
DAR ES SALAAM
Mhe. Msajili,
Mahakama Kuu ya Tanzania,
DAR ES SALAAM

Mtendaji,
Mahakama Kuu ya Tanzania,
DAR ES SALAAM

Page 4 of 4

You might also like