HESLB - Kuongezwa Muda Wa Kuomba Mkopo Hadi Agosti 23 - Final - 15082019

You might also like

Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 1

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HESLB YAONGEZA MUDA WA KUOMBA MKOPO HADI AGOSTI 23

Alhamisi, Agosti 15, 2019

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza kuongeza muda wa kuomba
mkopo kwa njia ya mtandao kwa siku tano hadi Ijumaa, Agosti 23, 2019 ili kuwapa fursa waombaji
ambao hawajakamilisha maombi yao kutumia muda ulioongezwa kufanya hivyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema jijini Dar es salaam leo (Alhamisi,
Agosti 15, 2019) kuwa HESLB ilianza kupokea maombi ya mkopo kwa mwaka wa masomo
2019/2020 tarehe 1 Julai mwaka huu na tarehe ya mwisho ilipaswa kuwa leo, Agosti 15, 2019.

Kwa mujibu wa Badru, HESLB imepokea maombi kutoka kwa baadhi ya waombaji mikopo ambao
hawajakamilisha maombi yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa nyaraka muhimu.

“Ingawa hadi leo asubuhi (Agosti 15, 2019) tumeshapokea maombi zaidi 74,821 yaliyokamilika
kwa njia ya mtandao, tumepokea pia maombi kutoka kwa wateja wetu wakitaka kuongezewa muda ili
wakamilishe nyaraka muhimu kama nakala za vyeti vya vifo vya wazazi wao, barua kutoka kwa
wadhamini wao na nyaraka nyinginezo … tumewasikiliza na kuongeza muda,” amesema Badru.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amewataka waombaji mkopo ambao hawajakamilisha maombi yao kutumia
muda ulioongezwa kukamilisha maombi yao kwa kuwa HESLB haitaongeza muda zaidi baada ya
tarehe 23 Agosti mwaka huu.

“Tunasihi waombaji wetu watumie muda huu ulioongezwa kukamilisha maombi yao kwa kuwa
hatutaongeza tena. Baada ya Agosti 23, tutaanza kufanya uchambuzi wa maombi tuliyopokea ili
tuwapangie mikopo wenye sifa kwa wakati na tupeleke fedha za mikopo vyuoni kabla vyuo
havijafunguliwa,” amesema Badru na kuongeza:

“Tunawaomba wadau wetu kama Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Wakala wa Usajili wa
Matukio ya Kijamii Zanzibar na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kuendelea kuwahudumia wanafunzi
katika kipindi hicho,” amesema.

Katika kipindi kilichoongezwa cha hadi Agosti 23, Badru amesema dawati la huduma kwa wateja la
HESLB klitakuwa wazi ili kutoa ufafanuzi kwa waombaji mkopo pale utakapohitajika. Dawati hilo
linapatikana kuanzia saa 2:30 asubuhi – saa 11:30 jioni kupitia:

Simu: 0736 665533 au 0738 66 55 33 au 022 5507910


Barua pepe: adcp@heslb.go.tz au info@heslb.go.tz

Taarifa hii pia inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz

Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
DAR ES SALAAM

You might also like