Professional Documents
Culture Documents
Unabii Wa Daniel
Unabii Wa Daniel
Daniel Nabii.
Katika sura ya pili ya kitabu cha Danieli tunasoma juu ya tukio muhimu.
Nebukadineza aliota ndoto ambayo ilitibua sana akili yake. Aliona taswira ya
mwanaume mkubwa ambaye kichwa chake kilikuwa dhahabu, kifua na mikono ya
fedha, tumbo na mapaja ya mchanganyiko wa shaba na zinki, miguu ya chuma, nyayo
zake zikiwa za mchanganyiko wa chuma na udongo. Halafu akaona jiwe likiiponda
tawira hiyo miguuni kwa nguvu kiasi cha kuiangusha chini na kuvunjika vipande
vipande. Jiwe lilikua na kuwa mlima mkubwa wa kujaza dunia nzima. Ndoto hiyo
ilikuwa inaonekana wazi na taswira iling’aa na kutisha kwamba Nebukadineza
alilazimika kutafuta tafsiri yake. Aliwaita wachawi na wataalamu wake wa nyota
wamwambie ndoto ilikuwaje na maana yake, lakini pasipo shaka hawakuweza. Habari
hiyo ilipomfikia Danieli alimwomba Mungu wake ambaye alimfunulia kuwa alikuwa
ndoto yenyewe ilikuwa inaeleza mambo ambayo yangetokea “siku za baadaye”
(Danieli 2:28). Huu ni mmoja tu kati ya nabii kadhaa katika Biblia ambazo zinaeleza
mambo ya “siku za baadaye.”
Danieli alianza kuieleza ile ndoto kwa usahili na tafsiri yake kama Mungu alivyokuwa
amemfunulia. Picha ya kisanii ya taswira hiyo inaonyeshwa katika ukurasa ufuatao,
pamoja na tafsiri ya Danieli na jinsi historia ilivyothibitisha undani wake.
Nguvu ya ile jiwe na kazi yake imeelezwa wazi wazi katika aya ya 44 na Danieli
anaposema: “katika siku za hawa wafalme Mungu wa mbinguni atasimika ufalme
ambao hautavunjwa kamwe: na ufalme na huo ufalme hautaachwa mikononi mwa
watu wengine ila utavunja na kumaliza kabisa falme zote hizi na utasimama milele.
Kwa hiyo katika ndoto hii ya kushangaza pamoja na tafsiri yake tunapata historia ya
dunia tangu enzi za Nebukadineza hadi wakati yesu Kristo atakapotumwa na Mungu
kusimika ufalme wake hapa duniani.
Huu ndiyo ufalme ambao Yesu aliwafundisha wafuasi wake kuomba aliposema
“ufalme wako uje. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni” (Mathayo 6:10).
Pia tunasoma kuhusu wakati huu ambapo Yesu atatawala dunia: “Falme za dunia hii
zimekuwa falme za bwana wetu na za Kristo wake na atatawala milele na milele”
(Ufunuo 11:15).
Nabii Danieli mwenyewe alipewa maono kadhaa ambayo pia yanaonyesha historia ya
dunia tangu mwaka 606 kabla ya Kristo hadi Ufalme wa Mungu utakapoanzishwa
hapa duniani.
Danieli mwenyewe alipewa ndoto ya ajabu ambayo pia alitabiri urithisho wa himaya
za dunia tangu wakati wake hadi hapo ufalme wa Mungu utakaposimikwa duniani.
Ndoto na tafsiri yake ziko katika kitabu cha Danieli sura ya 7. Katika ndoto hii
himaya nne za dunia zinazofuatana zinaonyeshwa kama ni wanyama. Hatujaachwa
kushangaa hawa wanyama wanawakilisha kitu gani kwani Danieli aliuliza na kupewa
jibu “Hawa wanyama wakuu ambao ni wanne, ni wafalme wanne ambao watainuka
hapa duniani. Lakini watakatifu wa aliye juu zaidi watachukuwa ufalme na kumiliki
ufalme milele na milele yote (Danieli 7:17-18). Tafsiri pana yatuambia kwa mara
nyingine juu ya himaya nne za dunia ambazo nafasi zake zitachukuliwa na ufalme wa
Mungu. Watakatifu ni wale watumishi waaminifu wa Mungu ambao watakuwa hai
wakati Yesu anaporudi au watakaofufuliwa na kufanywa wasife tena. Kazi yao
itakuwa ni kutawala na Yesu katika ufalme wa Mungu.
Wanyama wanne waliotajwa ni:-
Simba – akiwakilisha himaya ya Babiloni
Dubu – akiwakilisha himaya ya Mede ya Kiajemi
Chui – akiwakilisha himaya ya Kigiriki
Mnyama wa kutisha – akiwakilisha himaya ya Kirumi
Kila mnyama ana vitu vinavyomtofautisha ambavyo wanafunzi wa Biblia kwa muda
wa miaka 1500 na zaidi wamevitambua kama za hizi himaya nne za dunia.
Mfano wa hili ni chui ambaye alikuwa na vichwa vinne na mbawa nne.
Historia inakumbusha kuwa baada ya kifo cha Aleksanda mkuu himaya ya Kigiriki
iligawanyika katika sehemu nne kila mmoja akipewa mmojawapo wa majenerali
wake wanne. Hili ni jibu la vichwa vine na mbawa nne. Kwa kuhusishwa na Mungu,
Danieli alitabiri haya miaka 300 kabla hayajatukia.
Mnyama wa nne.
Swali linalofuata ambalo linakuja akilini mwetu ni: “Kama himaya ya Kirumi
ilivunjwa mwaka 400 baada ya Kristo, tutapata wapi maelezo ya kuanzia wakati huo
hadi sasa?” Kwa kweli Mungu ameisha yaonyesha kiwazi hasa.
Utaona kwamba mnyama alikuwa na mapembe manne, Danieli aliuliza haya yalikuwa
na maana gani na aliambiwa: “Mapembe manne katika ufalme huu ni wafalme 10
watakaoinuliwa” (Danieli 7:24). Hapa pia tunatambulishwa kuvunjika kwa himaya ya
Kirumi katika falme mbalimbali, na hicho ndicho historia inatuambia kilitukia Ulaya.
Tuliliona hilo katika kitabu cha Danieli sura ya 2.
Halafu Danieli aliona “pembe lingine dogo” likitokeza miongoni mwa yale 10 na
likawa kuu zaidi. Pembe hili lilikuwa na macho kama binadamu na mdomo ulionena
maneno makuu” (aya ya 8). Pia tunapewa ishara za kutambua pembe hili ambalo
lilijitokeza kwenye mnyama wa Kirumi. Ni utawala “uliopigana vita na watakatifu”
(Wafuasi waaminifu wa Injili ya kweli ya Yesu Kristo na kuwashinda (aya ya 21)
ikiwatesa wale wote waliokataa kukubali mamlaka na mafunzo yake. Pembe hili
linawakilisha mfumo wa ki-dini unaodai kuwa na mamlaka ya kutoa amri za ki-dini,
hata hivyo amri zake zinapinga ukweli wa neno la Mungu. Tunasoma: “Na atasema
maneno makuu dhidi ya Aliye Juu zaidi na atawachosha watakatifu wa Aliye Juu zaidi
na kuwaza kugeuza nyakati na sheria” (aya ya 25). Historia inazo kumbukumbu za
dini hii iliyochoka ambayo imejitwalia maguvu ya kidini na kisiasa hasa katika eneo
la himaya ya Ki-rumi ya zamani. Maelezo ya kina zaidi ya dini hii ya uongo ya
Kikristo ambayo ilizuka yamo katika nabii za baadaye katika 2 Wathesalonike 2 na
Ufunuo 13-19.
Kwa hiyo Mungu alimfunulia danieli mambo makuu ya kisiasa na ki-dini ambayo
yamekuwepo tangu nyakati hizo hadi nyakati zetu, kwa mara nyingine tena historia
inathibitisha unabii huu wa kushangaza.
danieli alimalizia unabii huu pia na ahadi kwamba Mungu ataingilia kati mambo ya
dunia na kuweka ufalme wake hapa duniani.
Tunasoma:
“Watakatifu wa aliye juu zaidi watachukua ufalme na kuumiliki milele na
milele.” (aya ya 18)
“Mzee wa siku alikuja na hukumu ikatolewa kwa watakatifu wa aliye juu
zaidi,na wakati ukafika ambapo watakatifu waliumiliki ufalme.” (aya ya 22)
“Na ufalme na utawala na ukuu wa falme zote chini ya mbingu yote watapewa
watu wa watakatifu wa aliye juu zaidi ambaye ufalme wake ni ufalme
usiokuwa na mwisho na tawala zote zitamtumikia na kumtii yeye. (aya ya 27)
hivyo katika nabii mbili hizi (Danieli 2 na 7) Danieli ametabiri kuwa kila mfumo wa
kisiasa na mfumo wa dini ya uongo itafagiliwa mbali Yesu atakapokuja kuanzisha
ufalme wa Mungu duniani. Tunapofikilia miaka 6000 ya giza la mateso iliyopita
katika utawala wa mwanadamu tunashukuru kiasi gani kwamba Mungu ana udhibiti
wa hali hiyo na karibuni atamtuma Yesu Kristo kuitawala dunia hii kwa haki (Mat-
17:31)
Danieli siyo tu kwamba alitoa mtazamo mpana wa historia ya dunia hadi ufalme wa
Mungu utakaposimikwa duniani bali pia alizungumzia matukio yatakayotokea karibu
na kuanzishwa kwa ufalme huo. Alifunua kuwa “wakati wa mwisho” (aya ya 40)
mamlaka ya kijeshi inayoitwa “mfalme wa kaskazini” atavamia mashariki ya kati
kupitia Israel hadi Misri. Huu utawala wa kaskazini umetambuliwa na wasomi wengi
kuwa ni shirikisho la mataifa likiongozwa na Urusi.
Angalia madokezo makuu:-
Matukio yatatokea wakati wa mwisho
Taifa lenye nguvu la kaskazini linaingia kijeshi mashariki ya kati likiwa na nia
ya kuitawala Israeli na Misri (Danieli 11:40;43)
Taifa hili la kaskazini lenye nguvu linateketezwa Israeli (Danieli 11:44-45)
Yesu Kristo anarudi na wafu wanafufuliwa (Dan. 12:1-2)
Wenye haki wanapewa uzima wa milele ili kutawala pamoja na Kristo (Dan.
12:3)
Danieli 12:1-3 inaonyesha kuwa wakati ule ule uvamizi wa Israeli kutoka kaskazini
unapofanyika (“yaani wakati wa mwisho”). Ufufuo wa wafu utakuwa unafanyika pia.
“Kutakuwa na wakati wa matata ambao haukupata kutokea tangu liwepo taifa
hadi wakati huo.”
“Wakati huo watu wako watakombolewa , kila mmoja atakayekuwa
ameandikwa kitabuni.”
“Wengi wanaolala ardhini wataamka.”
“Baadhi watapata uzima wa milele.”
“na baadhi watapata aibu na dharau ya milele.”
“Wale wneye busara watang’ara kama anga.”
“Wale wanaowaongoza wenzao katika haki, wataangaza kama nyota milele na
milele.”
Mashariki ya kati sasa hivi ikiwa katika hali ya mvutano usiokwisha na mataifa mengi
ya ulimwengu katika vurugu hakuna shaka kwamba tumo katika zile siku ambazo
kwa wazi kabisa zinatangaza kuwa Yesu Kristo karibu atarudi kuja kuanzisha ufalme
wa Mungu.
Muhtasari wa Ezekieli38.
Muhtasari
Jiwe
Jiwe linagonga na kuvunja sanamu hii na sehemu zake ‘pamoja’ danieli aliona kuwa
katika “siku za baadaye” serikali zitakazokuwa zinatawala katika himaya hizi kongwe
zitaungana katika muungano au ushirika na kwamba Mungu atavunjilia mbali
muungano wao akibadili na ufalme wake utakaotawaliwa na Yesu Kristo. Jiwe
litatanuka na kujaa katika dunia nzima.