Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

KODI KWENYE MAKAMPUNI

Kodi ni 30% ya faida ya kikodi inayopatikana katika mwaka mzima wa mapato.


ISIPOKUWA
1. Makampuni yaliyopo soko la hisa la Dar es salaam (DSE) na umma kuwa na umiliki
wa 30% au zaidi kwa miaka 3 mfululizo. Kodi yake inakuwa 25% ya faida ya kikodi.
2.Makampuni yanayopata hasara kwa miaka mitatu mfululizo kodi yake ni 0.5% ya
mauzo kwa mwaka huo wa mapato.
3. Makampuni mapya kwa ajili ya utengenezaji wa dawa za binadamu na ngozi zenye
makubaliano na serikali, zitalipa kodi ya 20% ya faida za kikodi kwa miaka mitano ya
mwanzo.
4. Makampuni mapya yaliyoanzishwa kwa ajili ya mitambo na mashine ya kuunganisha
magari, matrekta, boti za uvuvi na injini za nje zenye makubaliano na serikali, zitalipa
kodi ya 10% ya faida za kikodi kwa miaka mitano mfululizo.
kampuni inajikadiria mapato kabla au mnamo tarehe 31 mwezi wa 3 kila mwaka. Na
kulipa kodi hiyo kwa awamu 4 yaani mwezi wa 3,6,9,12.
Kampuni inatakiwa kuleta taarifa ya mapato kabla au mnamo tarehe 30 mwezi wa sita
ya mwaka unaofuata zilizothibitishwa na mhasibu anayesajiliwa na bodi ya uhasibu na
ukaguzi (NBAA).
WAJIBU WA MAKAMPUNI
1. Kutumia mashine za EFD kwa usahihi
2. Kulipa kodi ya SDL ndani ya siku saba ya mwezi unaofuata (ikiwa inawafanyakazi
kuanzia wanne)
3. kukusanya na kuleta kodi za waajiriwa wao (PAYE) ndani ya siku 7 ya mwezi
unaofuata.
4. Kutunza kumbukumbu za biashara kwa kipindi kisichopungua miaka mitano.
KALENDA
Mwaka wa mapato unaanza tarehe 1/1 kila mwaka na kuisha 31/12 kila mwaka.
Ikiwa unataka uwe na mwaka wa mapato tofauti unatakiwa kuleta barua katika ofisi
unayohudumiwa ili wa kubadilishie endapo maelezo yako yatakuwa na mantiki.
ADHABU
1.Kuchelewa kufanya makadirio au kutokuleta taarifa za mapato, adhabu yake ni Tsh
225,000 kila mwezi uliochelewesha.
2. kutokutumia mashine ya EFD kwa usahihi, adhabu yake ni Tsh 3000,000 mpaka Tsh
4,500,000.
MUHIMU
Huwa tunawatumia meseji kwenye simu zenu kuwapa taarifa mbalimbali ukiona
imetoka TRA HUDUMA ni ya kwetu zikija kutoka vyanzo vingine tupigie 0800780078 au
0800750075 ili tukuthibitishie usahihi wa jambo hilo EPUKA MATAPELI.
PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU
Nini maana ya kodi ya makampuni?

Kodi ya makampuni ni kodi inayotozwa katika mapato yanayotozwa kodi (Faida) ya asasi kama
vile makampuni yenye dhima ya ukomo na makampuni mengine ikiwa ni pamoja vilabu, vyama,
jumuiya na vikundi vingine visivyo shirikishi.
Mwongozo huu unatoa mtazamo wa msingi wa kodi ya Makampuni. Unaelezea maana ya “kodi
ya makampuni” nani anawajibika na anapaswa kufanya nini na lini ikiwa atatakiwa kutimiza
masharti ya Kodi ya makampuni. Unabainisha namna kodi inavyokokotolewa, viwango vya kodi
vinavyohusika na muda wa kulipa.
Unaelezea pia dhana za msingi zinazohusiana na kodi ya mapato kama vile “makadirio binafsi”, “
muda wa kufanya mahesabu” na “ Faida inayolipiwa kodi”
Kodi ya makampuni ni kodi inayotozwa katika mapato yanayotozwa kodi (faida) ya asasi kama
vile makampuni yenye dhima ya ukomo, taasisi, au makampuni ikiwa ni pamoja na klabu, vyama,
jumuiya, ushirika, mashirika ya wahisani na vikundi vingine visivyo shirikishi.
Mapato yanayotozwa kodi (faida) katika kodi ya makampuni yanahusisha:

 Faida inayotokana na shughuli za biashara


 Faida kutokana na uwekezaji (isipokuwa migawanyo ya faida ambayo imetozwa kodi tofauti
kama kodi ya mwisho)
 Kodi inayotokana na mapato ya makampuni yenye hasara za muda mrefu ambazo
hazijasamehewa kwa miaka mitatu mfululizo

Ni nani wanapaswa kulipa kodi ya Makampuni?


a) Makampuni yenye dhima ya ukomo
b) Amana
c) klabu
d) Asasi zisizo za Kiserikali
e) vyama vya ushirika
f) Mashirika ya Wahisani
g) Makampuni ya ndani ya kudumu (Matawi ya makampuni ya nje)
h) Vyama vya siasa
i) Wakala wa serikali
j) Kampuni mpya iliyoanzishwa na ambayo inajihusisha na utengenezaji wa madawa ya binadamu
na bidhaa za ngozi na ina mkataba wa makubaliano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania itatozwa kodi kwa kiwango cha 20% kwa kipindi cha miaka mitano mfulizo kutoka mwaka
walipoanza uzalishaji.
Je Wabia wanapaswa kulipa kodi ya Makampuni ?
Wabia hawalazimiki kulipa kodi ya mapato. Hata hivyo, wabia wanatozwa kodi ya mapato katika
faida zinazosambazwa kutoka kwenye ubia kwa kuzingatia uwiano wa uchangiaji uliokubalika.
Nini maana ya mwaka wa mapato?
Katika muktadha wa kodi ya mapato, mwaka wa mapato una maana ya kalenda ya mwaka wa
miezi kumi na miwili (kwa maana ya kipindi kinachoanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31
Desemba). Hata hivyo, Asasi inaweza kuomba kwa maandishi kwa Kamishna kibali cha kubadili
mwaka wake wa mapato kutoka mwaka unaoanzia Januari kwenda mwaka unaoanzia wakati
mwingine unaopendekezwa na asasi. Mwaka wa mapato ni muhimu katika utunzaji wa hesabu za
kodi.
Nini maana ya taarifa ya mapato ya kodi?
Taarifa ya mapato ni maelezo yanayowasilishwa Mamlaka ya Mapato Tanzania yanayoonesha
makadirio ya mapato na kodi inayolipwa au mapato ya mwisho na kodi inayolipwa kwa kila
mwaka wa mapato.
Chini ya sheria ya kodi ya mapato, kampuni inatakiwa kuwasilisha taarifa ya mapato hata kama
hakuna mapato yanayotozwa kodi.
Maelezo kuhusu makadirio ya kodi inayolipwa
Kila kampuni iliyosajiliwa na watu binafsi ambao wanapaswa kuandaa hesabu za mizania na
kuwasilisha taarifa inayoonesha makadirio ya kodi inayolipwa katika kila mwaka wa mapato.
Fomu
Inayotumiwa na kampuni: ITX 202.01.E MAKADIRIO – fomu ya Kampuni
Maelezo ya makadirio/makadirio yaliyopitiwa upya ya kodi inayolipwa kwa awamu kwa niaba ya
kampuni.
Inayotumiwa na watu binafsi: ITX 200.01.E Makadirio – watu binafsi
Maelezo ya makadirio/makadirio yaliyopitiwa upya ya kodi inayolipwa kwa awamu na mtu
binafsi
Tarehe ya mwisho (makataa) ya kulipa kodi
Taarifa ya makadirio ya kodi inayolipwa yanapaswa kuwasilishwa ofisi za TRA katika tarehe
zifuatazo kutegemeana na muda wa mahesabu:
i. Ifikapo au kabla ya tarehe 31 Machi
ii. Ifikapo au kabla ya tarehe 30 Juni
iii. Ifikapo au kabla ya tarehe 30 Septemba
iv. Ifikapo au kabla ya tarehe 31 Desemba
Malipo ya awamu ya kwanza ya kodi yanaishia wakati taarifa ya makadirio ya kodi inayolipwa
(taarifa ya awali ya mapato) inapowasilishwa na kisha awamu nyingine zitalipwa kwa kuzingatia
tarehe za makataa zilizoainishwa hapo juu.
Taarifa ya mwisho ya mapato:
Taarifa ya mwisho ya mapato inapaswa kuwasilishwa ndani ya miezi sita kuanzia mwisho wa
tarehe ya hesabu. Taarifa hii inapaswa kuandaliwa au kuthibitishwa na Mhasibu ambaye
amethibitishwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu
Tarehe za mwisho za kulipa kodi uliyojikadiria
Tarehe za mwisho kwa malipo ya kodi (makadirio binafsi ya kodi ya mwisho) ni tarehe za
mwisho za kuwasilisha taarifa ya mapato.
Fomu:
 ITX 203.01.E – Fomu ya kampuni ya Taarifa mapato
 ITX 202.01.E – Fomu ya makadirio ya kampuni

What are the due dates for payment of duties and taxes?
Income Taxes
 Withholding taxes are payable within seven (7) days after the end of calendar month
 Taxes payable in installments (Provisional assessed tax) payable on quarterly basis e.g in
case of taxpayers whose accounting periods ends on 30th December the installments shall
be due by the end of March, June, September and December.
 Self-assessed tax is payable on the date of filling the final return of income ( 6 months
after the end of the year of income
 Jeopardy assessed tax is payable on the date specified on the notice of assessment
 Adjusted assessed tax is payable within 30 days from the date of assessment
Value Added Tax (VAT)
VAT is payable on 20th day of the following month of the business that is a due date of
submitting the return. If the 20th day follows on the Saturdays, Sunday, or public holiday the
return shall be lodge on the first working day following the Saturdays, Sunday or Public day.
Customs taxes
Duties and Taxes on importation of goods are payable within 30 days from the date of
assessment
Guidance for paying taxes
This page contains guidance and codes which will assist you to make proper payment of the
intended taxes. The page provides codes used for payments by indicating specific type of taxes,
forms used to specific banks and payments made through mobile phones.
1. GFS Code
This is a special number which is used by the taxpayers when make payment by filling it on the
deposit paying slip.
2. TISS
TISS stand for Tanzania Interbank Settlement System. This is a simplest way used by the
taxpayers to order the commercial bank to transfer payments to BOT, and the contents which
are found in the TISS form are: Name of Account holder (s), Account number, Name of
commercial Bank, Amount in TSHS, Amount in words and value date.
3. Payment of Tax Manually
The following are the procedures which Taxpayers are required to follow during making tax
payment.
1. Visit the nearest TRA office/Centre.
2. Obtain the tax assessment/charge together with control number.
3. Collects a payment notice and Deposit slip and fill in the appropriate particulars (Name of
Taxpayer, type of tax, TIN, GFS code Number, Amount of tax to be paid, Date of payment
and Signature of the person making payment.
4. Submit the same to the Bank/Teller and make payment.
5. Obtain the copy of Bank payment notice and Deposit slip for his/her record

You might also like