Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUNUNUA ARDHI

AU KIWANJA KISICHOPIMWA
Mambo yafuatayo yanatakiwa kuzingatia wakati wa
kununua ardhi au eneo lisilopimwa ili kuepusha
usibomolewe nyumba yako.
Unaweza kununua na kujenga kiwanja ambacho
hakijapimwa katika maeneo ya mjini ili usipate athari
zingatia yafuatayo.
KWANZA wasiliana na Ofisi ya Ardhi ya Halmashauri
husika ili kuulizia mahali ambapo unataka kununua
kiwanja hicho hawajapanga matumizi mengine tofauti ya
makazi,kwa sababu unaweza kununua kiwanja kwenye
eneo ambalo limepangiwa matumizi mengine kama vile
viwanda au dampo,ukalazimika kuhamishwa na kupata
hasara.
Usifanye haraka kununua kiwanja kisa unauziwa kwa bei
nafuu ,jiridhishe kwanza ndipo ununue.
PILI Wasiliana na Uongozi wa Mtaa hasa Mwenyekiti wa
Mtendaji wa Mtaa.Watu wengi wanafanya makosa ya
kutowashirikisha viongozi wa Mtaa wakati wa kununua
kiwanja.Mara kadhaa mtu anafika na fedha zake anamlipa
mwenye kiwanja kisha anaondoka.
Kununua kiwanja bila kuwashirikisha viongozi wa mtaa
unaweza kuuziwa kiwanja kilichouzwa kwa mtu mwingine
na kujikuta kiwanja kimoja kinamilikiwa na watu wawili
au watatu.
Viongozi wa Mtaa ni muhimu kuwashirikisha kwa kuwa
wanaalikwa kwenye mauziano ya viwanja vya watu wao wa
mtaa kwa hiyo viwanja vingi wanavifahamu.
Ili kujiridhisha iwapo utawapata majirani wa kiwanja
unachotaka kununua litakuwa jambo jema zaidi kwa kuwa
watakuhakikishia mipaka ya kiwanja hicho.
Kumbuka kuandika Mkataba wa mauziano na mashahidi
wawepo na watie sahihi kwenye Mkataba huo ili mambo
yakigeuka baadaye usiathirike.
Ukiwa na viongozi wa Mtaa,hakikisha kiwanja chako kina
barabara inayofika kwenye kiwanja hicho au hakikisha
kiwanja hicho hakipo karibu sana na barabara kwa kuwa
baadaye kinaweza kukatwa ili kupisha barabara.
Waulize viongozi wa Mtaa wamependekeza barabara ipite
sehemu gani na itakuwa na upana gani katika barabara ya
Mtaa hakikisha isipungue mita kumi ili ramani ya mipango
itakapochorwa isikuathiri sana.
TATU unapomaliza kununua uanze mara moja
kukiendeleza kiwanja chako kwa kupanda miti,weka fensi
au nguzo kwenye kila kona ya kiwanja ili watu wengine
wasijekukuingilia.
Hakikisha kiwanja chako unakiendeleza mapema kwa
sababu ukichelewa unaweza kukuta mgogoro.Usikiache
kiwanja kitupu kwa muda mrefu kwa kuwa jirani yako
anaweza kukimega au mtu mwingine kukivamia kujenga.
Zingatia vipimo wakati wa kujenga nyumba hasa kiwanja
chako kama kipo pembeni ya barabara,nyumba isiwe
karibu na barabara,isogeze nyuma ya kiwanja.
Unatakiwa uache meta moja na nusu toka kila upande wa
mipaka ya kiwanja chako ili kuacha mpenyo kati ya
kiwanja na kiwanja,pia unashauriwa kuacha angalau meta
tatu hadi tano toka barabarani kutegemeana na ukubwa
wa kiwanja chako.
TAFADHARI FUATA SHERIA KWA MAKAZI BORA.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea

You might also like