Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

MUFRADAAT MADHAB HANABILA

Maana ya mufradaat madhab ni kwamba kauli hio imesemwa na hanabila pekee katika kauli
mashur au riwaya mashur na sio madhab zingine.

1. Katika vigawanyo vya maji ni yale ambayo ni Tuhur lakini haramu kuyatumia kama maji
yaliyoporwa au yameibwa au yale yaliyoweka waqf kwa ajili ya kunywa na kadhalika.

2. Katika vigawanyo vya maji nukta ya maji ambayo ni tuhur lakini haifai ni kutumiwa ni Maji
yanayoondosha hadthi ya mwanamke hayaondoi hadath ya mwanaume au untha Na hapa ni
pale anapwekeka nayo mwanamke aliyebaleghe na mwenye akili kwa ajili ya twahara
kamili kutoka hadath iwe kubwa au ndogo hali ya kuwa ni kidogo. Katika nukta hii
mufradaat madhab ni kusema kwamba mwanamke huyo awe amepwekeka nayo maji basi
hayatafaa kutumiwa.

3. Katika viungo vya maiti mufraadat madhab ni kwamba ngozi haitwahiriki kwa dibagh.

4. Katika mlango wa kustanji mufradaat madhab ni kwamba mawe ambayo yanfaa kustanji
nayo yawe ni halali.

5. Katika sunnah za wudhu mufradaat madhab ni kutamka nia kwa siri isipokuwa amekiradd
al hajawi katika al iqnaa.

6. Katika kupangusa juu ya khofu mbili mufraddat madhab ni kwamba ziwe ni halali na zisiwe
za kuporowa au za kuibiwa.

7. Katika vitenguzi vya wudhu mufradaat madhab ni kwamba kugusa tupu inaharibu wudhu
hata kwa kugusa kwa mgongo wa viganja.

8. Katika vitenguzi vya wudhu mufradaat madhab pia ni kutotenguka kwa kula vilivyobaki
katika viungo vya ngamia kama ini, moyo, wengu, kirsh mafuta, na figo na kichwa, ulimi,
nundu, na kawaria aina ya utumbo, na mchuzi wa nyama na haendi kinyume na kiapo chake
yule mwenye kuapa kwamba hatokula nyama.

9. Katika yanayowajibisha ghusl mufradaat madhab ni kwamba kuhisi kuhama kwa manii
kutoka kwa mgongo wa mwanaume au kifua cha mwanamke kunawajibisha ghusl hata
kama haikutoka

10. Katika fardhi za kuoga mufradaat madhab ni kwamba kwa mwenye hedhi na nifas ni lazima
kufumua nywele.

11. Katika tayamum mufradaat madhab ni kwamba mwenye kuwa na najis katika mwili
anazingatiwa kama mwenye hadath

12. Katika sharti za tayamum mufradaat madhab ni kutumia udongo ambao ni halali.
13. Katika tayamum mufradaat madhab pia ni kwamba mwenye kutopata maji na kutopata
udongo wa kufanya tayamum ataswali fard pekee na hatoirudia.

14. Katika fardh ya tayamum mufradaat madhab ni kwamba udongo unapakwa mpaka mahali
viganja na dhiraa zinawachana na sio mpaka kwa maraafiq.

15. Katika yenye inawajibishwa na hedhi mufradaat madhaab ni kwamba mtu akifanya tendo la
ndoa hali ya kuwa mwanamke yuko kwa hedhi basi ni wajib kutoa kafara.

16. Katika hali ya mustadha na mwenye nifas mufradaat madhab ni kwamba ni haramu
kumwingilia mwanamke aliye katika istihadha.

17. Katika mlango wa shurut za swalah kuhusiana na kufinika awrah mufradaat madhab
kwamba haijuzu kuswali na nguo iliyoporwa hata kama hatapata ingine bali ataswali uchi.

18. Katika arkaan za swalah, Mufradaat madhab ni kwamba anayewacha swala ni kafiri baada
ya kutubishwa kwa siku tatu.

19. Katika swala ya jamaa mufradaat madhab ni kwamba ni fard ayn kuswali katika swala ya
jamaa

20. Katika swala ya iddi mufradaat madhab ni kwamba kuna wakati mbili wa kuiswali na
wakati wa kwanz andio mufradaat nayo ni Kuanzia kunyanyuka jua makadirio ya mkuki
mpaka kabla ya zawaa

You might also like