Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

HIJAMA RAMADHAN

Je hijama inafaa wakati wa kufunga au la? Kuna hadithi tatu ambazo zinafaa kuangaziwa ili kupata
uwiano na kupata hitimisho katika masala haya

Hadithi ya kwanza

Amesimulia Ibn Abbas kwamba Mtume alifanya hijama mara moja alipokuwa kwenye Ihraam na
alifanyiwa hijama mara moja kama amefunga.1

Hadithi ya pili

Amesimulia Shadad Ibn Aws kwamba wakati mmoja Mtume alipatana na mtu karibu na Baaqi
katika mchana wa Ramadhan na huyu mtu alikuwa anafanyiwa Hijama. Mtume akasema: ‘Mwenye
kufanya Hijama na mwenye kufanyiwa Hijama wote hawa saum zao zimevunjika’ 2

Hadithi ya tatu

Amesimulia Anas Ibn Malik alisema: Kwamba mwanzo kufanya Hijama haikuwa halali kufanya
hijama mchana wa ramadhan na wakati huo ndio Jaffar ibn Abu Talib alifanya hijama na huku
amefunga, na Mtume akampita na akasema nyote saum imefunguka, kisha baadaye Mtume
alikubalisha aliyefunga kufanyiwa hijama na amefunga na wakati huo ndio Anas ibn Malik alikuwa
anafanyiwa hijama wakati amefunga’

Hadithi ya kwanza inaonyesha kwamba kufanya hijama wakati wa saum yafaa kinyume na hicho
hadithi ya pili yaonyesha haifai kufanya hijama wakati wa saum na mwenye kufanya na kufanyiwa
wanavunja saum, na hadithi ya tatu inaonyesha mwanzo haikuwa inafaa kufanyiwa hijama wakati
wa saum lakini baadaye ikakubalishwa.

Kutokana na hayo kuna kauli mbili zinajitokeza:

1. Hijama haivunji saum


2. Hijama inavunja saum

Hijama haivunji saum:

Kauli hii imejengwa juu ya hadithi ya kwanza ya Ibn Abbas kwamba Mtume alifanyiwa hijama na
hadith ya tatu ya Anas kwamba mwanzo ilikuwa haifai na baadaye ikakubaliwa na pia swahaba
Anas alikuwa anafanyiwa wakati anafnga. Na wakajibu hadithi ya pili kirahisi kwa kusema kwamba
hio hadithi ilikuwa ni mwanzo wa wakati ambapo ilikuwa imekataliwa na baadaye ikakubaliwa.

Na hii kauli ni kauli ya jumhur ya wanachuoni na miongoni mwao ni Abu Hanifa, Malik ibn Anas,
Shafii na wengineo.

Hijama inavunja saum:

Kauli hii imejengwa kwa hadithi ya pili ya Shadad Ibn Aws kwamba funga ya mwenye kufanya
hijama na mwenye kufanyiwa imevunjika. Na mwenye anafanya hijama saum yake inavunjika kwa
sababu zamani hawakuwa wanfanya hijama na vikombe kama siku hizi bali wakati wa kufanya
hijama walikuwa wananyonya na mdomo na huenda damu hio ikaingia ndani sana kwa mdomo.

1
Imepokelewa na Bukhari
2
Wameipokea watano yaani Bukhari, Muslim, Abu Daud, Ibn Majah, Nasai na Tirmidhi hakuipokea na
imesahihishwa na Ahmad, Ibn Khuzaimah na Ibn Hibban
Wanajibu hadithi ya kwanza ya Ibn Abbas kwamba ina vipande mbili, kwamba hijama kwa ihram
na hijama katika saum. Wanasema kwamba sentensi ya pili ‘na alifanya hijama wakati yuko kwa
saum’ haijathibiti kwa riwaya zingine. Imam Muslim anaileta hio riwaya pia lakini bila sentensi hio
ya pili na wanachuoni wengine pia wanaileta hio hio hadithi lakini bila hio sentensi ya pili.
Wakasema hio sentensi ya pili ni makosa. Na hawa pia ni wanachuoni wa hadithi.

Wanajibu hadithi ya tatu ya Anas kwamba ili kusema kwamba hadithi fulani inaifuta hadithi ingine
basi lazima ulete dalili kwamba hadithi hio ilikuja baada ya nyingine. Na katika hadithi hii
haithibitiki kwamba gani ilitangulia gani. Kwa mfano hadithi ya kwanza inaweza semwa kwamba
ilikuwa katika hajj ya mwisho lakini pia inaweza kusemwa kwamba ilifanywa katika miongoni mwa
umrah zilizopita hata kabla Makkah kurudi kwa mikono mwa waislamu. Na pia wanasema kwamba
hadithi ya pili huenda ikafuta ya kwanza. Na pia wanasema kwamba hata wakiweza kuthibitisha
kwamba hadithi yao ilikuja baadaye, basi hadithi ya Shadad ina nguvu sana kuliko hadithi ya Anas
katika kuwa na nguvu na usahihi wake. Na wanachuoni wa hadithi wanasema kwamba hadithi ilio
na nguvu kidogo haiwezi kufuta hadithi iliyo na nguvu zaidi. Ilikuonyesha kufuta basi hadithi inafaa
na nguvu ilio sawa na inayofutwa au iko na nguvu zaidi. Basi tunapatia hadithi ilio na nguvu zaidi
hujjah nayo ni Shadad Ibn Aws.

Sheikh Fawzaan anasema hadithi ya Shadad ibn Aws imesimuliwa na maswahaba kumi na ziada. Na
kusema kwamba hadithi imefutwa ni katika ngazi za mwisho sana. Kama yawezekana kuzikusanya
au kuipa moja nguvu kulingana na nguvu zake basi hio inafanywa kwanza kabla ya kuleta hoja ya
kufutwa. Na katika hili hadithi ya Shadad ina nguvu kuliko hadithi ya Anas.

Na hii ni kauli ya Ahmad, Ishaq ibn Rahuwayh mwalimu wa Bukhari, Ibn Khuzaimah, Ibn
Taimiyyah, Ibn Qayyim na wanachuoni wengine. Na Sheikh Ibn Baaz amesema kwamba hii masaala
ni daqiiq sana na kila kauli ina hoja zake ambazo zina nguvu. Na Ibn Baaz katika moja ya kauli yake
anasema sio lazima kufanya Hijama wakati wa saum na kwa sababu masaala ina kauli mbili na kila
kauli ina dalili zake basi ni vyema kuiwacha hata kama unaamini kwamba haivunji saum. Na lau
ukifanya hijama basi wanachuoni wanaoona kwamba saum yako imevunjika watasema kwamba
imevunjika lakini kama mtu hatafanya hijama wakati amefunga basi wanachuoni wote
watakubaliana kwamba saum yake iko sawa.

Miongoni mwa sababu walizotoa wale wenye kusema inavunja saum naye ni Sheikh Fauzaan
anasema kwamba wakati wa kufunga mtu hafai kufanya kitu ambacho kitamfanya awe dhaifu na
wanachuoni wa salaf wamesema ukifanyiwa hijama inakufanya uwe na udhaifu na wakati
mwingine hata kuendesha gari inakatazwa kama umefanyiwa hijama. Na hijama inakufanya dhaifu
wakati wa saum kwa sababu mtu hajakula na tena anatolewa damu nyingi inayomfanya dhaifu.

You might also like