Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

ISMAIL NA ISHAQ

Mwanzo kabisa tunamshukuru Allah na baada ya hapo tunamtakia sala na salamu kipenzi chake na
si mwingine ni Mtume Muhammad.

Mada ya nani aliyekusudiwa kuchinjwa kati ya Ismail na Ishaq ndio imefanya watu kugawanyika
madhehebu madhehebu. Ama waislamu na wakristo wote wanaamini kwamba Ibrahimu ni baba wa
Imani lakini wakaja kutafautiana kati ya watoto wawili nani kati yao aliyekusudiwa kuchinjwa, Pia
wakatafautiana je hajra alikuwa mke wa Nabii Ibrahim au Ibrahim alizini naye? Je Ismail ni mtu wa
halali au haramu? Na haya ni baadhi ya wakristo kushikilia kwamba hajra hakuwa mke wa Ibrahim
bali Ibrahim alizini naye na akapata mtoto wa haramu ambaye ni Ismail ili tu waporomoshe sifa na
hadhi ya Ismail. Basi tutaweza kuangalia maandiko katika vitabu na tutadadisi. Ni yapi ya kweli na
yapi ya kusingiziwa?

IBRAHIM ALIKUWA MUISLAMU

Kwa mujibu wa kiislamu Ibrahim alikuwa muislamu na wala hakuwa mkristo wala myahudi. Allah
anasema:

“Ibrahimu hakuwa myahudi wala mkristo lakini alikuwa muongofu, mtii kamili wala hakuwa katika
washikirikina” 1

HAJRA KAMA MKE WA SARAH

Baadhi ya watu wanatoa dosari kwamba hajra alikuwa ni mfanyikazi baadaye Sarah akamchukua
na kumpa Ibrahimu awe mkewe. Hivi kweli kuwa mfanyikazi ni dosari au ni kazi kama kazi zingine?
Tujuavyo ni kwamba mfanyakazi huyo pia alikuwa mwanamke kama wanawake wengine na
ilipoonekana anaweza kuwa mke basi Ibrahim akamuoa na kumfanya mke wake. Na lau ikawa
shida ni kuhusu mtu kuwa mke basi Sarah kuwa mke wa Ibrahim ndio ingelikuwa na shida zaidi

“Ibrahim akasema, kwa sababu naliona yakini hapana hofia Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa
ajili ya mke wangu, naye kweli ni ndugu yangu, binti wa baba yangu ila sie mama wa mama yangu
ndipo akawa mke wangu”2

Maana Ibrahimu anasema Sarah ni dadake na akawa mke wake. Hivi kati ya mfanyikazi kuwa mke
na dada kuwa mke gani baya?

Ama Hajra alipewa na Sarah kwa Ibrahimu awe mkewe3 na siokwamba azini naye. Na hilo twaona
halina tatizo kabisa

WATOTO WA IBRAHIMU

Qurani inasema kwamba Ibrahimu alikuwa na watoto wawili nao ni Ismail na Ishaqa na Bibilia pia
inakubaliana nayo isipokuwa katika bibilia Ibrahimu alikuwa na mke mwingine Ketura ambaye
alimzalia watoto wengine. Lakini hawa watoto wawili ndio waliopewa kipaumbele ndipo hata Paulo
anasema kwamba Ismaili na Ishaqa ndio kama maagano mawili ambaye huyo ismail kwa kujibu
wa baadhi ya wakristo ni kwamba ni mwana haramu aliyezaliwa nje ya ndoa.

1
Quran 3:67
2
Mwanzo 20:11-12
3
Mwanzo 16
“Niambieni nyinyi mnaotaka kuwa chini ya sheriah, Je, hamuiskii sheriah? Kwa maana imeandikwa
ya kuwa Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja kwa mjakaazi na mmoja kwa muungwana lakini
yule wa mjakaazi alizaliwa kwa mwili, yule wa muungwana kwa ahadi, mambo haya husemwa kwa
mfano kwa maana haya ni sawa na maagano mawili, mmoja kutoka mlima Sinai ambao ni Hajra
maana Hajra ni kama mlima Sinai uliopo Arabuni” 4

KUADHIMISHA SIKU YA KUCHINJWA KWA MWANA WA IBRAHIMU

Hakuna watu wengine wanaoadhimisha siku ambayo alikusudiwa kuchinjwa mwana mmoja wa
Ibrahimu isipokuwa ni waislamu katika Eid ul Adha. Lakini kwa sababu yule mwana alikombolewa
kwa kondoo wa sadaka na waislamu pia wanachinja mnyama siku hio.

MTOTO WA KWANZA WA IBRAHIMU

Ibrahimu baada ya kupewa hajra kama mke wake na akamuingilia, katika umri wa miaka 86 ndio
anapata mtoto wa kwanza ambaye ni Ismaili na baada ya miaka 14 akiwa na miaka 100 ndio
anapata mtoto wa pili ambaye ni Ishaqa.

Kwa miaka 14 Ismaili ndio aliyekuwa mtoto wa pekee wa Ibrahimu kabla aje Ishaqa.

URITHI KWA IBRAHIMU NA ISMAILI

Mungu alimpa urithi na sio urithi wa mapanga na visu bali alimpa baraka Ibrahimu akisema:

“Bwana akanena, Je nimfiche Ibrahimu jambo nifanyalo? Akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu” 5

Na hivo hivo alimbariki Ismail akisema:

“Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ismaili angeishi mbele yako, Mungu akasema: Sivyo,
Lakini Sarah mkeo atakuzalia mwana, atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishaqa,
name nitafanya agano lake kwangu kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake ama
kwa habari za Ismaili nimekusikia nimembariki, nitamzidisha name nitamuongeza sana sana atazaa
masayyid 12 nami nitamfanya awe taifa kuu” 6

Kando na kuwa Ishaqa alibarikiwa na Mungu kwa sababu ya uzao wake lakini Ismaili ambaye
baadhi ya watu wanasema ni mtoto wa zinaa alibarikiwa pia kwa sababu ya dua ya babake
Ibrahimu na akapewa Baraka ya kuwa taifa kuu kama alivypopewa Baraka hizo babake Ibrahimu. Je
baba aliyezaa nje ya ndoa awe kuridhiwa na kubarikiwa kiasi hio na je dua yake yaweza kusika na
Mungu mpaka na mwana huyu aliyepewa nje ya ndoa pia akabarikiwa kiasi hicho? Bali hapa
tunapata sivyo bali Ismaili alikuwa mwana wa halali na Hajra alikuwa mke wa Ibrahimu wa halali.

KUZALIWA KWA ISMAILI NA ISHAQA

Ibrahimu analalamika kwamba amekuwa mzee lakini hana mtoto na atakayemrithi ni Eliazari
Mdameski. Basi Mungu akamwambia huyu hatakurithi bali atakayekurithi atatoka katika viuno
vyako.7

4
Wagalatia 4:21
5
Mwanzo 18:17
6
Mwanzo 17:18-20
7
Mwanzo 15:1-4
Maana ya viuno vyako ni kwamba Ibrahimu atashirikiana na mke wake na watazaa mtoto kama
ambavyo watoto wengine wanapatika duniani. Na kwa mujibu wa bibilia mtoto aliyepatikana
kutoka kwa viuno vyake ni Ismaili baada ya Sarah kupeana Hajra kwa Ibrahimu awe mkewe. 8 Ama
kwa habari ya Ishaqa Mungu akamjia kama alivyonena 9 Sarah akapata mimba akazaa mtoto kama
Mungu alivyonena. Hapa hatuoni kwamba sarah kazaa kwa nguvu za viuno vyake bali kazaliwa kwa
ahadi.

“Niambieni nyinyi mnaotaka kuwa chini ya sheriah, Je, hamuiskii sheriah? Kwa maana imeandikwa
ya kuwa Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja kwa mjakaazi na mmoja kwa muungwana lakini
yule wa mjakaazi alizaliwa kwa mwili, yule wa muungwana kwa ahadi, mambo haya husemwa kwa
mfano kwa maana haya ni sawa na maagano mawili…….”10

TUKIO LA KUCHINJWA

Tukio hilo la kuchinjwa lilitokea wapi na lilitokea vipi? Ibrahimu alikuwa beer sheba. Bibilia
inasema:

“Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer Sheba akaliita huko jina la Bwana Mungu wa milele” 11

Je ni nani kati ya watoto wa Ibrahimu alikuwa Beer Sheba?

“Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akachukua mkate na kirimba cha maji akampa Hajra
akimtwika begani mwake na kijana akamruhusu naye akatoka akapotea katika jangwa la Beer
Sheba”12

Kumbe ni Ismaili ndie aliekuwa anaishi Beer Sheba na babake alikuwa anapanda mkwaju hapo Beer
Sheba kama tulivyoona.

“Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu akamwambia Ewe Ibrahimu, naye
akasema mimi hapa. Akasema, umchukue mwanao, mwana wako wa pekee,umpendaye Ishaqa” 13

Hapa jina la ishaqa limepachikw. Mwana wa pekee kwa miaka 14 ni Ismaili. Tukio linatokea Beer
Sheba. Aliekuwa Beer Sheba ni Ismaili lakini jina linapachikwa la Ishaqa.

Baada ya tukio la kuchinja Ibrahimu alirudi wapi?

“basi Ibrahimu akawarudia vijana wake wakaondoka wakaenda zao mpaka Beer Sheba” 14

Kumbe walitoka Beer Sheba wakiwa na Ismaili wakaenda kwa nchi ya Moria ambapo tukio lilikuwa
linafaa kutokea na baada ya Ismaili kukombolewa wakarudi zao Beer Sheba.

“Basi umri wa Sarah ulikuwa miaka 127 hio ndio iliokuwa miaka yake, sarah akafa katika nchi ya
kiajarth arba katika nchi ya kanaan, Ibrahim akaja”15

Kumbe baada ya tukio na baada ya muda Ibrahim alitoka Beer Sheba mahali walipo Hajra na Ismaili
na kuenda kwa Sarah na hapo ni pale alipofariki Sarah.

8
Mwanzo 16
9
Mwanzo 21
10
Wagalatia 4:21
11
Mwanzo 21:33
12
Mwanzo 21:14
13
Mwanzo 22:1-3
14
Mwanzo 22:19
15
Mwanzo 23:1
“Na itakuwa katika siku za mwisho, Mlima wa nyumba ya bwana utakuwa imara juu yam lima, na
utainuliwa juu ya milima na mataifa yote watauendea makundi makundi” 16

Hapa inasema kwamba katika mlima huo ambapo alikuwa anafaa kuchinjwa huyo mtoto katika siku
za mwisho watakwenda watu makundi makundi kutoka mataifa yote. Na yajulikana wazi ni
kwamba ni waislamu wanakwenda Makkah kwa makundi makundi kutoka mataifa yote na
wakiadhimisha hio siku ya kuchinjwa.

Katika Quran hili liko wazi na halihitaji ziada yoyote. Allah anasema:

“Ee Mola wangu17, nipe mtoto awe miongoni mwa watenda mema, ndipo tukampa habari njema ya
kuwa atampata mtoto mpole basi akapata (naye ndiye Ismaili) basi alipofika makamu ya kwenda na
kurudi akamwambia mwanawe “Ee Mwanangu hakika nimeona katika ndoto kwamba nakuchinja
na ndoto za mitume ni wahyi basi fikiri waonaje? Akasema “Ee Baba yangu fanya ulioamrishwa
utanikuta Insha Allah miongoni mwa wanaosubiri. Basi wote wawili walipojisalimisha kwa
Mwenyezi Mungu akamlaza kifudifudi ili amchinje. Pale pale alimuita “Ewe Ibrahimu umekwisha
sadikisha ndoto usimchinje mwanao kwa yakini hivi ndivo tunawalipa watendao mema ” 18

Je ishaqa hapo alikuwa amezaliwa au bado? Jawabu bado bali alikuja baadaye. Allah anasema:

“Tena tukambashiria kumzaa ishaqa”19

16
Isaya 2:2
17
Nabii Ibrahimu ndie anayeomba dua hio.
18
Quran 37: 100-105
19
Quran 37:102

You might also like