RATIBA MIEZI 8 MPAKA MWAKA NA MIEZI 11 (Week 1&2-2020)

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 33

HII NI RATIBA YA WIKI MBILI KWA

MTOTO MWENYE UMRI WA MIEZI NANE


MPAKA MWAKA NA MIEZI 11….
TUMEWEKA RATIBA HII NDEFU KWA
SABABU VYAKULA NI VILEVILE NA
WAZAZI WENGI WANASAGA VYAKULA
MPAKA MTOTO ANAFIKA MIAKA MIWILI

MTOTO ANATAKIWA AANZE KUZOESHWA


VYAKULA VYA KUPONDA PINDI TU
ANAPOFIKA MIEZI 9 UKIMCHELEWESHA
HAPA UTAJIKUTA UNASAGA MPAKA
ANAFIKA MIAKA 3
KAMA MTOTO ANAMIEZI 8-9
UNASAGA CHAKULA BAADA YA
KUMALIZA KUPIKA

KAMA MTOTO NI MIEZI 9-12 ANZA


KUMUIBIA IBIA CHAKULA CHA KUPONDA
NA MKONO TU (KAMA ATASUMBUA
CHAKULA CHA KUPONDA BASI MILO
MIKUU UTASAGA ILA MIDOGO
UNAMPONDEA)
Siyo lazima kufuata saa nilizoweka ila
anza RATIBA pale tu mtoto
anapoamka
KABLA YA KUANZA RATIBA HAKIKISHA
MTOTO AMENYONYA VIZURI NDO
RATIBA IANZE HII ITAMSAIDIA SANA
Kumbuka asilimia 70 ya lishe ya mtoto
ni maziwa ya mama chakula ni asilimia
30 tu hvyo nyonyesha mtoto kadri
uwezavyo ili asitetereke kwenye uzito

DAY 1
🕒8:00-uji walishe wenye butter
( Tunaunga wa lishe mzuri sana
tunauza 8000 kg 1 ni mzuri sana
kwa MTOTO asiyependa kula au
asieongezeka uzito)

Kama tayari unao unga basi tumia huo


na ongeza butter DAKIKA tano kabla ya
kuipua

🕒11:00 smoothie parachichi+ndizi+mtindi


Weka vitu vyote ktk blender kisha saga
vilainike mimina mpe mtoto

🕒13:00 Ndizi+njegere+Nyama+tui la
nazi MAHITAJI
▪ndizi bukoba mbili
▪njegere kikombe kimoja
▪carrot Nusu
▪kitunguu kidogo kimoja
▪kitunguu swaumu punje mbili
▪mafuta vijiko viwili
▪nyanya ndogooo 1
▪spinachi kikombe 1
PISHI
▪Menya ndizi mbili na ukate vipande
(tumia ndizi bukoba)
▪chemsha njege kidogo ili zilainike
▪bandika chombo jikoni utakachotumia
kupikia
▪weka mafuta Kisha ongeza vitunguu
maji na swaumu
▪pika mpaka vibadili rangi kidogo kisha
ongeza carrot na nyanya iliyosagwa
koroga viive kidogo kisha ongeza ndizi
njegere na supu ya Nyama yenye
minofu miwili pika mpaka viive kisha
ongeza tui zito la nazi na spinach
▪pika mpaka tui liive
▪ipua acha kipoe andaa mpe mtoto

🕒 15:00 apewe tunda

🕒17:00 uji wa lishe


Andaa kama alivyokunywa asubuhi
🕒19:00-20:00 tambi+carrot+iliki+maziwa
MAHITAJI
▪tambi kikombe kimoja
▪carrot nusu
▪maziwa
▪hiliki

PISHI
▪chemsha tambi na carrot Pamoja
mpaka viive
▪vikiiva ongeza Unga wa hiliki nusu
kijiko cha chai na maziwa ( kama ni
ya ng’ombe changanya wakati wa
kupika Ila kama ni ya formula basi
utatumia kusagia)
Saga au pondaponda na andaa mpe
mtoto

DAY 2
🕒8:00 mtori
▪ndizi bukoba 2
▪kiazi 1
▪carrot 1
▪kitunguu kidogo 1
▪supu ya kuku au ng’ombe

PISHI
▪menya ndizi na kiazi Kisha katakata
na uchemshe
▪bandika jikoni na ukatie kitunguu
▪sagia karoti kisha ongeza mafuta
vijiko viwili,Maji kisha funika na
upike mpaka vilainike
▪vikilainika vizuri ongeza supu na acha
ichemke kidogo kisha ipua na usage
▪hakikisha chakula kinakua chepesi
cyo kizito sana

🕒11:00 smoothie
Embe+carrot +juice ya chungwa
▪embe ½
▪carrot 1
▪juice ya chungwa glass 1
Menya embe na carrot Kisha weka
kwenye blender na usage vyote kwa
juice ya chungwa
▪mimina mpatie mtoto

🕒13:00 VIAZI
MVIRINGO+HOHO+KAROTI+KUKU+MCHIC
HA
▪viazi mviringo kikombe 1
▪hoho kipande kidogo
▪karoti kikombe ½
▪kuku kikombe ¼
▪mchicha ½ kikombe

PISHI
▪chemsha kuku wako upate supu ya
kutosha
▪menya viazi carrot na kitunguu Kisha
bandika na upike kwa supu ya kuku
mpaka vilainike
▪vikikaribia kuiva ongeza hoho na
mchicha
na pika kwa dakika tano mpaka 10
▪Ipua na usage au kuponda kisha
mpatie mtoto

🕒15:00 APATIWE TUNDA


ANALOPENDA
🕒17:00 MAZIWA

🕒19:00-20:00 NDIZI
▪ndizi mbili
▪green beans kikombe 1
▪supu ya ng’ombe
▪butter kijiko 1
▪hiliki ½ kijiko cha chai
PISHI
▪menya ndizi na ukate vipande
▪osha maharage yako na ukate vipande
▪bandika jikoni Kisha chemsha kwa
supu mpaka vilainike
▪hakikisha supu inabaki ya kumpondea
au
kumsagia
▪baada ya kukaribia kuiva ongeza Unga
wa hiliki Kisha koroga na uipue
▪andaa kisha mpe mtoto

DAY 3
8:00 UJI WA MTAMA
{tunauza Unga mzuri sana ikiwemo
wa mtama kwaajili ya watoto bei ni
8000 tu Waweza pia kuandaa
mwenyewe)

PISHI
▪koroga uji wako kama kawaida na
ukikaribia kuiva ongeza maziwa na
butter vijiko viwili hakikisha unapika
kwa moto mdogo ili usishike chini au
kuungua
▪hakikisha uji wako unapika kwa dakika
35-
40
🕒11:00 KIAZI
▪kiazi lishe kikombe 1
▪tangawizi 1/4 kijiko
▪Tui zito kikombe 1
▪embe kikombe 1

PISHI
▪menya na chemsha kiazi mpaka kiive
▪pika tui lako kwa mvuke
▪pika embe kwa mvuke
▪weka kiazi embe na tangawizi ktk
blender kisha saga na tui la Nazi

🕒13:00 MAHARAGE+KABICHI
▪maharage kikombe 1
▪kabichi kikombe 1
▪kitunguu kidogo 1
▪tui la nazi kikombe 1
▪viazi kikombe 1

PISHI
▪loweka maharage masaa 6 kabla ya
kupika ili kupunguza gesi na pia tumia
maharage ya njano
▪chemsha maharage mpka yalainike
▪menya viazi mviringo na kata
vipande vidogovidogo
▪bandika jikoni na upike mpaka vikaribie
kuiva
▪ongeza maharage na kabichi kisha
endelea kupika kidogo
▪weka tui lako na upike kwa dakika tano
▪ipua andaa mpe mtoto kulingana
na mahitaji yake

🕒15:00 UJI WA MTAMA


{andaa kama nilivyoelekeza juu}

🕒17:00 maziwa apewe

🕒19:00-20:00 {ale kama


alivyokula mchana}

DAY 4
🕒 8:00 UJI WA LISHE
{pika kama tukivyoelekeza kwenye uji
wa mtama, kama wahitaji unga huu
pia tunauza mzuri sana kwa
WATOTO be ni ileile 8000 kg 1}

🕒11:00 SMOOTHIE
▪beetroot 1
▪embe ½
▪passion 1
▪tangawizi kipande kidogo sana

MAANDALIZI
Menya vyote na ukatekate kisha weka
ktk blender na usage kwa maziwa ya
kawaida Au mtindi

🕒13:00 BUTTERNUT
▪butternut kikombe 1
▪apple 1
▪mchicha kikombe 1
▪supu ya kutosha
▪carrot ½

PISHI
▪menya butternut na ukate
vipande vidogovidogo
▪menya Apple na ukate vipande
vidogovidogo
▪osha mchicha a ukate kidogokidogo
▪menya caroti na ukate
vipande vidogovidogo
▪weka butternut apple na karoti jikoni
kisha ongeza Maji kisha funika na pika
mpka viive
▪ongeza mchicha na supu kisha funika
na pika kwa dakika 10 kisha ipua
tayari kwa matumizi

🕒15:00 JUICE YA TIKITI

🕒17:00 MAZIWA

🕒19:00-20:00 UJI WA DONA


▪unga wa dona
▪butter
▪unga wa mbegu za maboga

PISHI
▪maji kikombe kimoja
▪koroga vijiko vitatu vya Unga wa dona
▪pika mpaka uive ( waweza ongeza
Unga kulingana na uzito unaohitaji au
kiasi cha UJI unachohitaji)
▪UJI ukiiva ongeza butter vijiko viwili
PAMOJA na unga wa mbegu za
maboga kijiko kimoja
▪pika kwa dakika 3 na ipua tayari
kwa matumizi

DAY 5
🕒8:00 BOKOBOKO
▪almond punje 8
▪Apple 1
▪mchele kikombe 1/2
▪maziwa kikombe 1
▪hiliki kijiko kidogo ¼

PISHI
▪Loweka mchele nusu saa ili ulainike
▪ukilainika bandika na katika
apple ulilomenya vizuri
▪pika mpaka viive vizuri ongeza hiliki
na acha kwa DAKIKA tano kisha
ipua Andaa kwaajili ya mtoto (saga
au pondaponda)

🕒11:00 MAZIWA

🕒13:00 NDIZI+ DENGU


▪ndizi bukoba 2
▪dengu ½ kikombe
▪swaum punje 2
▪tui vikombe 2

PISHI
▪menya ndizi na ukate vipande
▪chemsha dengu mpaka ziive vizuri
▪menya vitunguu swaum na pondaponda
▪bandika ndizi na funika ziive
▪zikiiva ongeza dengu na kitunguu
swaum ulichoponda kisha acha viive
kwa dakika kadhaa
▪ongeza tui la nazi na acha viive
Ipua andaa mpe mtoto

🕒15:00 APEWE TUNDA

🕒17:00 APEWE MAZIWA

🕒19:00-20:00
ALE KAMA ALIVYOKULA MCHANA

DAY 6
🕒 8:00 oats+rojo ya embe
▪Maji kikombe kimoja
▪oats vijiko vitatu
▪bandika na uchemshe kwa dakika 5
▪ipua na tayari kumpa mtoto

ROJO YA EMBE
▪menya embe nusu kisha katakata
vipande na saga kwa maziwa
Ile utakayopata ndo rojo yako
▪mimina oats uliyokwishapika ktk sahani
kisha ongeza rojo ya embe na koroga
kisha mpe mtoto

🕒11:00 SMOOTHIE
▪embe nusu
▪karoti kipande
▪spinach kiganja kimoja
▪tikiti kipande

Pika embe,spinach na karoti kwa


mvuke mpaka vilainike kisha weka
kwenye blender ongeza tikiti kisha saga
kwa mtindi

🕒13:00 kiazi lishe+ dengu


▪kiazi lishe kikombe ½
▪dengu kikombe ½
▪apple ½
▪mdalasini wa unga ¼ kijiko cha chai

PISHI
▪chemsha dengu mpaka ziive
▪chemsha kiazi mpaka kiive
▪pika Apple kwa mvuke(waweza
changanya na kiazi ukachemsha
PAMOJA)
▪changanya vyote ktk blender kisha saga
kwa maziwa
▪mimina mpe mtoto

🕒15:00 UJI WA DONA WENYE ROJO


YA
NDIZI {pika uji na andaa rojo
kama tulivyoelekeza siku za
nyuma}

🕒17:00 APEWE MAZIWA

🕒19:00-20:00 ALE KAMA ALIVYOKULA


MCHANA

DAY 7
🕒 8:00 UJI WA KIAZI LISHE
(nitaelekeza ktk PDF)
🕒11:00 MAZIWA
🕒13:00 BOKOBOKO
▪mchele ½ kikombe
▪choroko ¼ kikombe
▪tui la nazi vikombe 2
▪kitunguu swaum punje moja kubwa au
2 ndogo

PISHI
▪loweka mchele nusu saa
▪chemsha choroko ziive ongeza
swaumu iliyosagwa
▪bandika mchele na pika mpaka ulainike
kisha ongeza choroko na tui zito la nazi
pika mpaka tui liive
Ipua tayari kwa matumizi

🕒15:00 JUICE YA TIKITI NA YAI


▪chemsha yai na umpe kiini tu pamoja
na juice ya tikiti

🕒17:00 APATIWE MAZIWA


🕒19:00-20:00ALE KAMA MCHANA

DAY 8
🕒8:00 UJI WA TAMBI
{Unaweza kutumia macaroni au tambi
za kawaida}
• Chemsha tambi sagia
carrot funika ziive
• zikiiva weka butter kidogo acha ziive
• ipua kisha saga na na maziwa au tui
la nazi
{kama utatumia tui basi pika tui
kwa mvuke}
•Ukishasaga rudisha jikoni tia sukari na
vichumvi kidogo kama kafika mwaka
chini ya mwaka wakati wa kusaga
ongeza tende punje 8 ulizozitoa mbegu
na hiliki ya unga nusu kijiko cha chai
▪acha uchemke kwa dakika kadhaa
ipua pooza mpe mtoto

🕒11:00 JUICE YA TIKITI


🕒13:00 ugali+mtindi+mlenda

🕒15:00 SMOOTHIE
• embe ½{pika kwa mvuke}
•ndizi ½
•mtindi kikombe 1
•saga kwa pamoja kisha mpe mtoto

🕒17:00 UJI WA MTAMA MWEKUNDU

🕒19:00-20:00 KIAZI+SUPU+MCHICHA
• kuku eneo la paja
•viazi mviringo kikombe 1
•mchicha kikombe 1

PISHI
• chemsha kuku upate supu yako
•ongeza viazi ulivyokata vipande
kishafunika viive
•vikiiva ongeza mchicha na funika
kisha upike kwa dakika 5 ipua na
tayari kwa
matumizi {unaweza pika mchicha
kwa mvuke}

DAY 9
🕒8:00 UJI WA LISHE

🕒11:00 MAZIWA

🕒13:00 MAHARAGE+KABICHI+MCHELE
Pika kama tulivyoelekeza siku za
nyuma

🕒15:00 JUICE YA MUWA NA CHUNGWA

UANDAAJI wa JUICE YA MUWA


• chukua muwa menya na kata
vipande vidogo vidogo
• weka kwenye blender ongeza maji
kidogo kisha saga
• ikilainika toa na chuja upate ile juice
• andaa juice ya chungwa kulingana na
juice ya muwa uliyopata (
mchanganyiko uwe
nusu kwa nusu kulingana na
size utakayompatia mwanao)
Changanya huo mchanganyiko kisha
mpatie mtoto

🕒17:00 smoothie
• papai kikombe 1
•ndizi 1
• mtindi kikombe 1
•changanya vyote na saga kisha
mimina kisha mpe mtoto

🕒19:00-20:00
CHAGUA CHAKULA CHOCHOTE
ALICHOPENDA MTOTO KATIKA SIKU
ZA NYUMA KISHA MPIKIE ALE

DAY 10
🕒8:00 MTORI
{pika kama tulivyoelekeza nyuma}

🕒11:00 MAZIWA
🕒13:00 BOKO
• supu ya kuku na minofu kidogo
•njegere nusu kikombe
• karoti ½
•swaum punje mbili zisage
• TUI ukipenda

PISHI
• chemsha kuku na upate supu ya
kutosha
• loweka mchele nusu saa kabla ya
kupika
• chemsha njegere
•bandika mchele katia au sagia karoti
na vitunguu swaumu
ulivyosaga(vitunguu swaumu waweza
chemsha ktk supu)
•pika mpaka vilainike
•vikishalainika ongeza njegere na supu
kisha pika vilainike vizuri
Waweza ongeza tui la nazi ukipenda
• Acha viive kisha ipua tayari kwa
kumpa mtoto
🕒15:00
Juice tikiti na kiini cha yai

🕒17:00 UJI

🕒19:00-20:00
Ale kama alivyokula mchana

DAY 11
RUDIA RATIBA YA SIKU YA 1

DAY 12
🕒 8:00 mchele+apple+almond
• mchele ½ kikombe
• almond punje 8
•maziwa kikombe 1
PISHI
• loweka mchele nusu saa
• saga almond ktk blender ya vitu
vigumu upate unga
•bandika na pika mpka uive
•ipua saga kwa maziwa ongeza na unga
wa almond
🕒11:00 smoothie
• beetroot 1
• nanasi kipande1
•tangawizi kidogo sana
•maziwa/mtindi
•Pika beetroot na nanasi kwa mvuke
Kisha saga vitu vyote kwa maziwa au
mtindi
•mimina mpe mtoto

🕒13:00
Ugali na mtindi au mlenda

🕒15:00 MAZIWA

🕒17:00 UJI WA MTAMA

🕒19:00-20:00 NDIZI
• ndizi bukoba 2
• tui zito la nazi
•nyanya 1
•Nyama ya kusaga kikombe 1
•karoti nusu
•kitunguu 1 kidogo
•njegere robo kikombe

PISHI
• chemsha nyama na ubakize
supu ya kutosha
•chemsha njegere weka pembeni
•unga kama unavyounga Nyama kawaida
•chemsha ndizi zikikaribia kuiva wekatui
la nazi pika mpaka ziive kabsa
• baada ya ndizi kuiva miminia njegere
na ile rost ya nyama yenye supu kidogo
• ipua saga na supu hakikisha siyo vizito
sana

DAY 13
RUDIA RATIBA YA SIKU
YOYOTE ALIYOPENDA
MTOTO

DAY 14
🕒8:00 boko
• mchele nusu kikombe
•maziwa au tui la nazi
•mayai 2
•tende kabu punje tano

PISHI
• loweka mchele kama kawaida
• kisha bandika na uchemshe mpaka
ulainike
•ongeza tui la nazi au maziwa na unga
wa hiliki
•ongeza viini vya yai na tende zako
kisha koroga haraka haraka hakikisha
unakua kama uji na MAYAI
yavurugike vizuri
•ipua tayari kwa matumizi
🕒11:00 SMOOTHIE
• embe
•karoti
•chungwa
ANDAA KAMA TULIVYOELEKEZA JUU

🕒13:00 ndizi

▪ndizi mbili
▪green beans kikombe 1
▪supu ya ng’ombe
▪butter kijiko 1
▪hiliki ½ kijiko cha chai
PISHI
▪menya ndizi na ukate vipande
▪osha maharage yako na ukate vipande
▪bandika jikoni Kisha chemsha kwa
supu mpaka vilainike
▪hakikisha supu inabaki ya kumpondea
au kumsagia
▪baada ya kukaribia kuiva ongeza Unga
wa hiliki Kisha koroga na uipue
▪andaa kisha mpe mtoto

🕒15:00
APEWE TUNDA

🕒17:00
APEWE MAZIWA

🕒19:00-20:00
ALE KAMA ALIVYOKULA MCHANA

You might also like