Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 84

~i~

JIKOMBOE KIUCHUMI
&
UJASIRIAMALI

Linus .S. Siwiti

~ ii ~
©July 2018

Linus .S. Siwiti


+255766466209, +255652303709
Email: linussiwiti12@gmail.com
Tabora Tanzania
East Africa.

TOLEO LA KWANZA

Hakuna sehemu yoyote ya kitabu hiki ambayo


inaruhusiwa kutolewa upya au kuhamishwa
kielektroniki au ufundi wowote wa kurekodi au
kufungua na kutoa nakala upya na kurudishia tena
bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mwandishi

Kimechapishwa na:
KAS PRINTERS
Dar es Salaam
Contacts: 0653 409 946
kassolutionstz@gmail.com

~ iii ~
YALIYOMO
TABARUKU ..............................................................................vi
DIBAJI .....................................................................................vii
SHUKRANI ............................................................................. viii
*SURA O1* ............................................................................ 1
UTANGULIZI .......................................................................... 1
Kanuni 12 Za Kuwa Mjasiriamali: ........................................ 2
Kwa Nini Uwe Mjasiriamali? ............................................. 14
*SURA YA 02* ..................................................................... 16
KANUNI ZA KUPATA MTAJI .................................................. 17
Kanuni nane (7) bora za kupata mtaji: .............................. 20
Namna Ya Kuona Fursa Na Kutumia Hiyo FursA ............... 27
Kanuni Tano (5) Ya Namna Ya Kuiona Fursa ..................... 29
*SURA YA 03* ..................................................................... 34
KANUNI ZA KUTENGENEZA SABUNI .................................... 34
Sabuni Ya Majivu: .............................................................. 34
Sabuni Ya Urembo: ........................................................... 35
Sabuni Ya Manukato: ........................................................ 37
Sabuni Ya Asali Au Cream ................................................. 37
Sabuni Ya Kipande/ Mche ................................................. 39
Sabuni Ya Magadi (Gwanji) ............................................... 40
Sabuni Ya Kusafishia Vyoo, Masinki, Na Tiles: .................. 41

~ iv ~
Sabuni Ya Maji ................................................................... 43
Sabuni Ya Unga ................................................................. 45
Sabuni Ngumu: .................................................................. 47
Sabuni Ya Rangi Kwa Kutumia Vitu Asilia:......................... 48
Cream Ya Kunyolewa ........................................................ 49
*SURA 04* ........................................................................... 50
UTENGENEZAJI WA MISHUMAA/SHAMPOO ...................... 50
Utengenezaji Wa Mishumaa ............................................. 50
Utengenezaji Wa Shapooo:............................................... 53
*SURA YA 05* ..................................................................... 56
JINSI KUTENGENEZA UBUYU WA ZANZIBAR ...................... 56
Jinsi Ya Kutengeneza Karanga Za Mayai ........................... 57
*SURA YA 06* ..................................................................... 59
MPANGO BIASHARA NA UJASIRIMALI (BUSSNES
PLANNING) .......................................................................... 60
SURA YA 07 ........................................................................... 69
*HITIMISHO* ........................................................................ 69
USHAURI KUTOKA KWA MWANDISHI:.............................. 69
MAANA YA MANENO YALIYOTUMIKA: ............................. 72
REJEA MBALIMBALI: .......................................................... 75

~v~
TABARUKU
Maalumu kwa wenye nia na shauku ya kubadilika
kimtazamo na fikra na kuondokana na maisha ya kuwa
tengemezi. Katika ajira kwa kuajiriwa pekee bali
unaweza kujiari kwa ujasiriamali. Inawahusu watu wote,
wanaotamani kuyabadili maisha yaokwa kujiunga na
ulimwengu wa ujasiriamali, au kuongeza ujuzi na
maarifa katika ujasiriamali.
“Maisha haya jitoshelezi kwa kitu kimoja mpaka
yatoshelezwe”
(Shughuli zote afanyazo mwanadamu ni biashara,
lakini siyo kila shughuli ni ujasiriamali")
Peter a. Paul mwandishi, kitabu, mifereji 7 ya pesa.

~ vi ~
DIBAJI

Moja wapo ya njia ambazo mtu anaweza kujikomboa


kiuchumi ni ujasiriamali. Kama unataka kuleta mapinduzi
mbalimbali kwenye jamii yako unapaswa kuwa na fikra kama
za mjasiriamali. Nchi yeyote yenye watu wenye watu wengi
wenye mafanikio ukiangalia kwa makini utagudua watu
wengi waliamua kuwekeza katika ujasiririamali.

Lile wazo la biashara ulilonalo linaweza kukupa mafanikio


makubwa endapo tu utaamua kuchukua hatua na kuanza
kulitekeleza. Ufunguo wa kwanza wa mafanikio ni kuchukua
hatua hatua, yaani kuweka kwenye vitendo yale ambayo
unajifunza. Ili uweze kufanikiwa katika ujasiriamali. Lazima
uweke uoga pembeni, usiogope kukosea, kukosolewa,
kukatishwa tamaa, kupata hasara na mengine mengi
utakayokutana nayo. Unapaswa:

 Kujiamini,
 Kujifunza,
 Kujituma,
 Kuwa mvumilivu.

Rafiki yangu Linus S. Siwiti kwenye kitabu hiki


amekuelekeza njia mbalimbali za kuweza kujikomboa
kiuchumi katika ujasiriamali. Unaweza kujifunza kwa aina
mbalimbali za bidhaa alizokufundisha namna ya
kuzitengeneza na ukaanza kuchukua hatua.

Maisha hayatakuwa kama yalivyokuwa endapo utaweka


kwenye vitendo lile ambalo umepata katika kitabu hiki.
Endelea mbele, ndoto yako inawezekana.

@ Jacob Mushi
Mwandishi namjasiriamali.
Mwanzilishi wa Usiishie Njiani.

~ vii ~
SHUKRANI

N
amshukuru Mungu kwa mafunzo ya
MJASIRIAMALI KWANZA na Dr. Didas
Lunyungu niliyo udhuria na kujifunza mwaka
2012 katika ukumbi wa Dar Live Mbagala
Temeke jijini Dar es salaam. Namshukuru Mungu
kwa kunipa ufahamu kwa kujifunza kutoka kwa watu
mbalimbali ambao wanafanya maswala ya ujasiriliamali, na
wamefanikiwa kwa hali ya viwango. Pia kwa nafasi ya pekee
napenda kuwashukuru watu wote ambao wamefanya kazi ya
maandalizi yote hadi kufanikisha kitabu hiki kukamilika.

Niwashukuru marafiki zangu wa karibu kwa mchango wao


mkubwa na ushauri ambao ni:

Violeth Bura, Daud Kazinja, mwl Emmanuel Makwaya,


Kasian Rwechungura.Bna Team nzima ya huduma T.M.T
(Tabora Mission Team).

Shukrani Kwa mhariri wa kitabu hiki,Jacobo Mushi.


Shukrani zangu za pekee ziwaendee pia wazazi wangu wa
kiroho nikiwa Tabora wananilea na kuahakikisha nakuwa.
Rev Paul Mwavikie na Mama chungaji Agnes Mwavikie
(TAG KITETE CHRISTIAN CENTER).

Wazazi Wanguwote wa kimwili na ndugu zangu kwa kunitia


moyo kwa kazi hii.

Ahsante Sana pia kwa wewe ambae umepata na kala hii na


kuwa na nia ya dhati kabisa ya kutaka kujifunza na kuchukua
hatua yakulete mabadiliko na Mungu akubariki.

“Mabadiliko hayaitaji mtu mwingine kuyabadili hila ni


wewe wa kuyabadili”……. Linus Siwiti

~ viii ~
*SURA O1*

UTANGULIZI

M
jasiriamali ni mtu yeyote ambaye yupo
kwa ajili ya kutatua matatizo ya watu
wengine kwa nia ya kukidhi na kuweza
kujipatia kipato. Mfano muuza mkaa wa
mafungu mtaani yupo kwa lengo la kumtatulia tatizo
Yule ambaye hana kipato cha kununua mkaa wa
magunia.
Ujasiriamaliniuwezo wakukubali kuingia katika biashara,
kumiliki na kusimamia jambo kwa ujasiri.Ujasiriamali
unahusu utafutaji, ushawishina uendeshaji wa shughuli
yako, kibiashara kwalengo la kupata faida. (By Mwalimu
Ngunda).

Mjasiriliamali ni muunganiko wa maneno mawili kuleta


maana moja yenye usahahi na uhalisia ndani yake

Mjasiri + Mali= Mjasiriamali

Ili uweze kufanikiwa na kuchuma matunda ya mali na


kutajirika kupitia ujasiriamali ni lazima uwe jasiri.

“Hakuna mwenye mkono wa ulegevu akapata kuwa na


mafanikio” mwenye mkono wa bidiii ndiye atakaye pata
utajiri.”

~1~
“Huwezi kuvuka bahari kama huna ujasiri wa kuacha kuona
ufukwe.”….Christopher Columbus

Huwezi kuwa mjasiriamali kama huna ujasiri wa kuacha


kuyaona mafanikio. Pamoja na changamoto, kwani palipo na
changamoto pana mafanikio na palipo na mafanikio hapakosi
kuwa na changamoto.

KANUNI 12 ZA KUWA MJASIRIAMALI:

“Omba msaada kujifunza mbinu na ujuzi wa


kukuwezesha kupata mahitaji yako na sio kuomba
mahitaji yenyewe bila kujua jinsi ya kutafuta
itakukufanya kuwa mwombaji na tegemezi kila mara.”…..
(Bruce Lee)

01 Kuwa Mtatuzi wa matatizo:

Ujasiriamalini zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue


changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa
mtu husika, watu, jamii na Taifa kwa ujumla wake. Ni
muhimu ukafahamu kanuni hii kama mjasiriamali kwani
hutojikita kutafuta pesa bali utajikita

Kutatua matatizo ya watu.

Kwa mfano kama kuna tatizo la upatikanaji wa mboga katika


mji au eneo unalokaa, ikiwa wewe utaleta mboga katika eneo
hilo ni wazi kuwa watu watakupa pesa ili uwape mboga.
Hivyo ni muhimu kila mara ukatafuta changamoto ukaitatua,
nawe bila shaka utapata pesa za uhakika.

“Pesa ni matokeo ya kutatua shida ya mtu”

~2~
02. Kuwa na maono na malengo:

Huwezi kufanikiwa kwa jambo lolote unalotaka kufanikiwa


kama huna maono na malengo juu ya kile unachotaka
kufanikiwa au kukifanya ili ufanikiwe kupitia hicho unacho
kifikiria. Huwezi kuwa mjasiriamali kama huna malengo na
wala hujawahi kuona kama unaweza kuwa mjasiriamali.
Weka maono na malengo ya nia ya dhati ukiwa unataka au ni
mjasiriamali. Weka maono yako na malengo yako katika
vitendo zaidi na sio maneno zaidi.

“Wajasiriamali waliofanikiwa ni wale walioweza kubadili


maono yao kuwa uhalisia”

3. Tafuta soko/ masoko ya bidhaa yako:

Hakuna kitu ambacho ni kipya hapa duniani, vitu vingi


ambavyo utawaza kufanya au utavifanya wapo watu ambao
tayari wanafanya vituambavyo unataka kuvifanya wewe.
Nawakati mwingine umejikuta kwako inakuwa changamoto
kuanzisha biashara. Hapana sikuzote soko la biashara nila
ushindani na ubora wa bidhaa yako ndio soko lako lilipo.
“Mfano dhairi kwamba sehemu moja kunaweza
kukawanawafanyabiashara ya nyanya, ndizi viazi, nk zaidi ya
mmoja lakini chaajabu wateja wengi wakawa wanakimbilia
sehemu moja kwa nini?

Kile ambacho unakiona na kukiamini ndicho kinakuwa


sahihi kwako”….Linus Siwiti

Ubora wa bidhaa yako nikipimo tosha watu kuona huduma


yako ni ya kufaa zaidi kuliko zawengine.

“Vipimovikilegeauboraunapungua”….. (Mwl
Emmanuel Makwaya)

Wewe ni mfanyabiashara au unataka kuwa vipimo ya ubora


wa bidhaa yako ndio soko lako. Vipimo vikilegea maana yake

~3~
ubora wa bidhaa yako inapungua. Ukijikuta huna wateja na
kuanza lalamika jibu hapo ni rahisi kwa sababu bidhaa yako
haina ubora.

“Ikiwani mara ya kwanza unataka kufanya kitu unachotaka


kukifanya kifanyekatika hali ya ubora zaidi”

Sitosahau nakumbuka niliwai kupata mteja akanipa tenda ya


kumtengenezea ubuyu wenye asili ya Zanzibar. Lakini
sikutengeneza katika kiwango ambacho anakitaka mteja
wangu,

Maoni yake yalikuwa ni haya:

 Sukari umepunja
 Viungo ulivyoweka havisikiki
 Pakeji yako ni ndogo

Haya yalinipa fundisho kubwa katika ujasiriamali.


Igawanilimpoteza mteja niliyempata kwa sababu ya
bidhaayangu kutokuwa katika hali ya ubora.

Kabla ujafanya chochote angalia kwanza soko lako liko wapi.

Utawauzia watu gani bidhaa yako?

Na unawapataje watu hao?

Wataipokeaje bidhaa yako?

Ni vitu ambavyo unatakiwa kujiuliza kabla ya kufanya


chochote juu ya biashara yako.

Kabla ya kuwapelekea watuwengine bidhaa yako ijaribu


kwanza wewe mwenyewe.

NB: Mambo muhimu ya kukumbukaukiwa unataka kuboresha


soko la biashara yako:

~4~
 Fanya katika hali ya ubora, kama ni vifungashio
tafuta vya viwango vya ushawishi.
 Usiangaliye kupata faida kubwa sana na ikakupelekea
kuiandaa bidhaa yakokatika viwango hafifu.
 Siku zote fikiria Ubora, usipofanya hivyo itaku
gharimu. (Think quality it pay not quality it
cost)ikiwa na maana kufikiria ubora inalipa la!
Usipofikiri itakugharimu.

4. Chagua washirika au timu sahihi.

Moja kati ya mambo muhimu niliyo wai kupata kutoka kwa


walimu wangu ni juu ya usia wao.

Walimu wangu (wazazi) walikuwa wakiniambia“Linus sio


kila mwanafunzi anaweza kuwa rafiki yako huko shuleni
tafuta marafiki sahihi.

Sio kila mtu unaweza kuambatananae lazima ujue nani


wa kuambatana nae au wakina nani wakuambatana
nao”.(Mwalimu Emanuel Makwanya)

Wakati mwingine utahitaji kufanya kazi na watu au mtu


fulani. Ni muhimu kuwa makini wakati wa kuchagua
washirika au timu ya kufanya nayo kazi ili kuhakikisha
maono yako hayakwamishwi. Kamwe usichukue mtu tu kwa
kigezo kuwa ni rafiki au ndugu yako, bali chukua mtu ambaye
unaamini anaweza kufanya kitu chenye tija kwa ajili ya
kufanikisha malengo yako kama mjasiriamali.Chukua muda
kidogo kumfahamu kwa kina mtu unayetaka kufanyanaekazi

Watu wengi wamejikuta wakipata hasara na kupoteza mali


kwa kuibiwa fedha katika shughulizao kwa nini? Kutokumjua
unayetenda naye kazi kwa kina. Mwaminifu kwa mwonekano
wa sura ya nje, anafanya kazi vizuri, sio mtu mbaya.
Mshangao pale anapo kufanyia mambo usiyo yatalajia. Jipe
muda wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi ya nani wa
kufanyanae kazi. Ili asije kukuaribia kazi. Hapa pia nimuhimu

~5~
kuzingatia vipo vikundi mbalimbali katika maswala yanayo
husu ujasiriamali. Mfano TUMAIN JIPYA
GROUP.(NewHope Interpreurship Group (NEHI).
Inawezekana likawepo au lisiwepo, lakini nimetolea mfano.
Katika Group (kikundi) lazima wana kikundi wawe na
mawazo yanayoendana. (Mlandano wa mawazo). Huku
wakinena maoja na kukubaliana kwa kilajambo. Akiwepo
hata mmoja ambaye mawazo yake, na utendaji kazi wake ni
tofauti na kundi zima huyo siyo wakuendelea kuwepo kwenye
kundi. Otherwise (vinginevyo) atakuwa mrudishanyuma
malengo ya kikundi. Kama mawazo yake ni ya msingi na
utendajikazi wake ni watofautilakinini katika hali ya kuleta
utoauti chanya wenye mafanikio huyo anafaa zaidi, pengine
kuliko kundi nzima.

5. Fahamu na jali wateja

Ikiwa wewe ni mjasiriamali, au unataka kuwa


mjasiriamalibasi futa mawazo kuwa wateja wanakuhitaji
wewe. Fahamu kuwa wewe kama mjasiriamali, ndiye unaye
wahitaji wateja ili ukuze biashara au huduma yako. Hakikisha
mambo haya kuhusu wateja unayazingatia:

 Fahamu wanataka nini.


 Sikiliza maoni na ushauri wao.
 Hakikisha unakamilisha mahitaji yao.
 Tumia lugha nzuri na rafiki kwa wateja.(Lugha ni
pesa ongea, ishi na wachukulie watu vizuri uache
alama)
 Mfanye mteja aone unamthamini.
 Mfanye mteja aone kuwa umetanguliza huduma kabla
ya pesa. Siyo pesa kabla ya huduma.
 Mfanye mteja arudi tena au akutafute tena.
Iiwezekana siku anarudi akuletee na wateja wengine.

Naamini kwa kufanya hivi utaweza kujijengea msingi mzuri


wa wateja kwa ajili ya huduma au bidhaa zako kila siku.

~6~
6. Weka vipaumbele

“Sio kila kitu unaweza kukifanya kwa wakati mmoja


tambua mambo muhimu”.

Huwezi kufanya kila kitu kwa wakati moja kuna mengine


yatakwama au yasifanyike kwa ukamilifu. Hivyo ni muhimu
kugawa mipango yako na kuyapa yaliyo ya msingi sana
vipaombele kuliko mambo mengine.Kwa
siku,wiki,Mwezi/miezi namwaka.

Wewe kama mjasiriamali, ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya


kujiwekea vipaumbele; vipaumbele vitakuwezesha kubaini ni
kipi kianze na ni kipi kifuate kutokana na umuhimu wake.

Kwa mfano ikiwa kuna wateja walipata shida kupata huduma


au bidhaa yako, maliza kwanza swala hili kabla ya kuendelea
kuweka jitihada za kuuza bidhaa mpya. Kwa kufanya hivi
utaweza kufanya mambo kutokana na umuhimu wake, jambo
ambalo litakuwezesha kukua. Kama unataka kuanzisha
biashara anza kufikiri swala la mtaji, soko la biashara kama
kipaumbele chako.

7.Jifunze kujifunza kutokana na makosa:

Moja ya kanuni inayozingatiwa na wajasiriamali


waliofanikiwa ni kujifunza kutokana na makosa. Makosa ni
shule nzuri sana kwa kila mtu hasa wajasiriamali. Ikiwa
uliwekeza ukapata hasara, basi jifunze nini hasa kilikuwa
chanzo cha hasara ili mbeleni iweze kukusaidia. Usikubali
kukwamishwa na makosa, bali yawe ni hamasa kwako ya
kuendelea mbele zaidi. Wengi ukatishwa tamaa katika
biashara au ujasirimali kwa sababu ya changamoto za hasara,
kwa kukosa soko nk.

~7~
“Uzoefu ni kufanya makosa na kujifunza kutokana na
makosa hayo”Bill Ackman

8. Jifunze kwa watu liofanikiwa:


“Ukitaka kujua unakokwenda mulize aliyetoka unatokwenda”

Ukitaka kufanya au kuthubutu kitu fulani chukua muda


kujifunza kwanza kwa waliofanikiwa wao watakupa mambo
mbalimbali ambayo kwako yatakupa picha nzuri ya safari
yako ambayo unataka kuianza au ulishaianza lakini
ikakwamia njiani. Watu wengi wameshindwa kufanikiwa
kwenye maisha yao kwa sababu wanajifunza kwa
walioshindwa. Walioshindwa wana maneno mengi, hasa ya
kukatisha tamaa kama vile hili haliwezekani, hili linahitaji
pesa nyingi sana, mimi lilinishinda, utaweza wewe?
Linachosha, lina faida ndogo, kuna wengi wanaolifanya,
Fulani alishindwa, unapoteza muda wako tu tafuta mambo
mengine ya kufanya, Mama nani siunamwona, jamaa yule
yuko wapi alikuwa anafanya unachotaka kukifanya n.k.

Wewe kama mjasiriamali, epuka watu hawa kwani ni sumu


sana (toxic people) na ujifunze kwa waliofanikiwa, fahamu
walitatua vipi changamoto walizo pitia kukabiliana nazo
pamoja na mipango waliyoitumia hadi wakafika hapo walipo.
Ambatana nao ukitaka kujua mengi kutoka kwao.

“Kelele za watu sumu zisikukatishe tamaa bali mafanikioyako


na yakapige kelele kwenye masikioyao” Just be Foccus(
kuwa na mtazamo wako, simamia unacho kiamini hadi
kukifanikisha).

Kujifunza ni gharama: “Huwezi kujua pasipo kutaka


kujuaa”. Kuna uhusiano mkubwa kati ya kujua na kufahamu,
vyote hivi viwili vinatofautiana pia.

~8~
“Unaweza ukawa unajua lakini hufahamu, na ukawa
unafahamu, lakini hujui” mambo mengi amabyo wakati
mwingine unatamani kuyajua yahusuyo biashara na
ujasiriamali ingawaje unayafahamu vizuri. Kuna haja ya
kujifunza. Ndio maana kunawakati mtu ujitoa kwa namna ya
yoyote hili mradi hayapate mafunzo ili yakapate kumsaidi na
kumfaaa katika kujikomboa kimaisha. Ufahamu ni pale
kujiona kila kitu unakijua. Unaweza ukawa na stashahada au
shahada, ya maswala yanayohusu uchumi na ujasiriamali hapa
unaweza ukawa na maarifa ya maandishilakini siyo vya
vitendo. Chukua nafasi yakujifunza sasa kwavitendo.

Kujifunza kunahitaji nini?

 Utayari wa mtu
 Gharama ya kifedha
 Kujitoa katika muda,
 Bidii na uwajibikaji,
 Shauku na nia ya dhati kutaka kujua,

Bado nilikuwa na zungumzia kipengele cha kujifunza.


Ninakumbuka kauli mmoja zito kutoka kwa Baba wa Taifa
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Aliwai kusema
ya kuwa

“Ukiona elimu ni gharama basi jaribu ujinga”

Hakuwa na maana ya kuwatukana wa Tanzania hapana

Ujinga: Nikutokuwa na ufahamu na maarifa juu ya kitu


chochote. Na ujinga uondolewa kwa kujifunza.

Kujifunza:ni kufuta ujinga, na kuwekeza maarifa na


ufahamu. Hata mwandishi wa kitabu hiki kabla hajawa na
ufahamu na maarifa juu ya ujasiriliamali alichukua muda wa
kujifunza.

~9~
“Unaweza ukawa na elimu na usiwe na maarifa na
unaweza kuwa na maarifa na usiwe na elimu”…. Mwalimu
Christopher Mwakasege

9. Weka mipangona Tumia muda vizuri.

“Muda ni sasa wala sio ujao ukishindwa kutumia muda


wako vizuri muda utakutumia wewe vizuri”. Kuna
wanao lalamika muda ndo unamfanya ashindwe mudu
mambo mengine kwa wakati mmoja. Ni kweli yupo
sahihi kutokana na mipango yake, bali kama utaamua
kuweka mipango yako vizuri na kila kitu ukifanya kwa
ratiba yake unaweza kufanya vitu vingi na vya msingi
vyakuweza kukuingizia kipato chako. Usiwe mpuuziaji
wa muda. Badili mfumo wa ratiba zako na kuweka
katika namna inayofaa zaidi kukuwezesha kumudu
mambo yako yote kwa wakati sahihi, bila shida yoyote.
Anza siku yako mapema, ukifatilia ratiba za Watu
wakubwa waliofanikiwa. Mara nyingi wana amka alfajili
sana na kuianza siku yao mpya kwa namna ya tofauti.

Tujifunze kitu kutoka kwa Mohamed Enterprises (MO)

Wakati siku moja napitia pitia makala za maandishi na


video kuhusu namna yakufanikiwa katika kutunza muda.
Nilijifunza kitu kutoka kwa Mohamed.
Mohamed Enterprises (MO) ukiwataja wajasiriamali
wakubwa ambao wanazalisha bidhaa mbalimbali hapa
nchini na nje ya nchi basi ni miongoni mwao.
Anafanikiwaje na kuwa Bilionea Afrika Mashariki,
Afrika na Dunia?

~ 10 ~
Moja kati ya kitu muhimu nikufanikiwa kufanya kilakitu
katika muda. Ratiba ya siku nzima, mpangilio wa vitu
vya kufanya nk. Tuone ratiba yake ikoje:
 Ana amka saa kumi na moja kamili,
 Anasali,
 Saa kumi na mbili kasoro anakwenda ofisini,
sababu kubwa kuepuka foleni za barabarani na
kumwezesha kufika mapema.
 Saa kumi na mbili kamili hadi saa moja na
nusu,anapitia email mbalimbali zaidi ya 500-
600, kupata kujua kinacho endelea kutokana kile
anachofanya (processing products) uzalishaji
bidhaa, mfano mahidi, sukari, kokoa, mafuta
mbolea, nk.
 Saa moja na nusu anamaliza kusoma email, na
saa moja na nusu – saa saba anafanya mikutano
na bodi zake, kupanga bajeti, faida, hasara na
kufunga mahesabu.
 Saa saba anapanda gari kwenda Gymu (mazoezi)
kwenye gari anasoma magazeti takribani 10 ya
siasa sababu yeye pia ni mwanasiasa.
 Saa nane kamili hadi na robo anapata chakula
chamchana.
 Saa nane na robo anarudi ofisini hadi usiku saa
tatu saa nne kulingana na siku hiyo.
Vipi wewe ratiba yako ikoje kwa siku? Unasoma kurasa
ngapi kutokana na unachofanya, unachotaka kukifanya
(vitabu, magazeti, email nk)? Jichunguze kisha anza leo
kufanya kila kitu katika muda.
Kwenda na muda + Unachofanya = Mafanikio makubwa

“Lango la mafanikio yako yapo ndani ya muda”

~ 11 ~
“Muda mzuri wa kupanda mti ni miaka 20 iliyopita.
Lakini muda mwingine mzuri wa pili ni sasa.”

Chinese Proverb.

Pia sio kila jambo unaweza kulifanya katika muda


ambao unaona kwako ni sahihi, kunavitu utaanzisha au
umeanzisha kama ni biashara n.k lakini kumbe sio
msimu wake au wakati wake. Tambua njisi ya kwendana
na muda.

10. Usikate tamaa:


Unaweza ukijiona kama vile kila jambo kwako ni
changamoto, hivyo utamani hata kusikia au kufanya tena.
Pengine hii ilikuwa nikutokana na kushindwa kwako kwa
mara ya kwanza. Huko tunaita kwako ni dalili ya kuwa
umekata tamaa.

Ni wazi kuwa katika safari ya ujasiriamali utakutana na


changamoto mbalimbali. Jambo la msingi ni kukumbuka
kanuni hii kuwa usikate tamaa. Tumia changamoto kama
fursa na mtaji kwako wakufanya vizuri zaidi.

Changamoto zipo leo na kesho lakini keshokutwa


hazitakuwepo tena; jambo unalotakiwa kufanya ni
kutazama mbele na kusimamia lengo lako na kufanya
bidii kila leo kuzikabili changamoto husika ili ufikie
lengo lako.

“Siri ya mafanikio yetu ni kutokukata tamaa”


(Wilma Mankiller)

Matatizo sio ishara ya kuacha, bali ni miongozo.


(Robert H. Schuller).

~ 12 ~
Kuna watu wamevikatia tamaa vitufulani kwa kutovifanya
tena kutokana na matatizo waliyo kumbana nayo kipindi cha
nyuma. Ukiwa utaka kuwa mjasiriamali au kuendelea katika
ujasiriamali futa dhana ya kukata tamaa maishani mwako
kwanza.

11. kuwa na njia mbadala:

Katika safari ya maisha ya uangaikaji kutafuta mafanikio kuna


wakati plan (mipango) yako inagoma na unashindwa ufanyeje
ili kuweza kujinasua. Kikubwa na cha msingi kabla
ujaanzisha safari yako yeyote ya ujasiriamali n.k jua mbele
yako kunaweza kutokea lolote ni lazima uwe na njia mbadala
endapo changamoto itajitokeza uwe na njia nyingine ya
kutokea kupitia changamoto hiyo hiyo.

“Mlango mmoja wa furaha ukifungwa, mwingine


unafunguliwa, lakini mara nyingi tunautazama sana ule
uliofungwa na kushindwa kuona ule uliofunguliwa kwa ajili
yetu.”

(Helen Keller)

12. Uthubutu:
“Unashindwa kufanya vitu, kuanzisha, kutekeleza sio
Kama huwezi au kinashindikana”. Kwa vile hujaamua
tukuchukua hatua na kuthubutu. Ukitaka kuwa mjasiriamali
au kufanikiwa katika kila ulifanyalo kwa kupitia kanunina za
mafanikio na hii ni muhimu zaidi ya uthubutu. Acha kuwa
mtu wa kuongea tu bali kuwa mtu wa vitendo zaidi.

Kuna rafiki yangu mmoja alinifurahisha sana na nilivutiwa na


kanuni yake yeye alikuwa akuambii nini anataka akifanye bali
akisha kifanya ndipo anakuambia. Nikamuuliza siku
mojanikwa nini anafanya hivyo? Alinijibu kwamba yeye
hataki kuwa mtu mwongeaji sana hila anataka kuwa mtu wa

~ 13 ~
vitendo zaidi. Nilivutia sana na hiki kitu. Mwandishi wa
kitabu cha NGUVU YA UTHUBUTU. (AminaSanga) yeye
anaamini kuwa kwa kila jambo ili ulifanikishe ujasiriamali,
elimu, nk cha kwanza ni kuthubu. Nilijifunza na kupata
kuongeza kitu ndani yangu.

“Sipendi ni shindwe na jambo bali nilishinde jambo kwa


wema”.

“Siogopi kushindwa kwa sababu kunakushinda”. Linus S.

“Yale ambayo unayona kwako hayawezekani hayo ndiyo


fursa kwako ya kukufanikisha”.

KWA NINI UWE MJASIRIAMALI?

Maisha ya kuwa tegemezi hayo ni maisha ya utumwa,ajira ni


Maisha tegemezi. Nini na manisha? Kwani ili mtu aweze
kuenendesha maisha yake kwa ujumla kitu pekee
anachokitegemea ni mshahara/posho ya ajira yake. Hapana
sina nia ya kumpiga yule ambaye ameajiriliwa na tegemeo
lake ni ajiri bali nikujaribu kuleta njia yenye nuru zaidi pia.
Maelfu ya vijana walioko mtaani hali si njema kutokana na
ukosefu wa ajira. Na kauli mbiu wanayo tumia ni kwa madai
(Vyuma vimekaza). Hizi ni fikra zilizo kufa halihali
zinatembea.Mwalimu Julis kambarage Nyerere aliwahi
kusema kwamba
(Nibora kuishia na fikra hai, kuliko kuishia fikra
zilizokufa).

Maisha hayajitoshelezi kwa kile ambacho unakifanya pekee.


Unaweza ukajikomboa kimaisha kwa namna nyingine kuliko
kubaki katika tegemezi moja tu.

Kuna umuhimu wa kuwamjasiriamali:

~ 14 ~
(1) Utakusaidia kuepukana na maisha ya kuwa
tegemezi:
Kuliko kutegemea wazazi kama ni kijana binti, kaka,
kuliko kutegemea kila mwisho wa mwezi upange
foleni, mikopo, kuombaomba msaada kwa ndungu
(ndugu nao watakuchoka).
Unaweza ukayaendesha maisha yako bila stress
(mawazo) na kufanikiwa kwa viwago kupita kile
unachofanya (ujasiriamali).

(2)Utakuletea maendeleo katika familia, jamii na Taifa

Mshahara pekee hauwezi kukidhi kila kitu, usomeshe,


ujenge, uweke mazingira sawa ya malazi,mavazi na
chakula na wakati huhuo ujenge, uboreshe maisha
yako nk. kwa kutengemea mshahara au posho ambayo
nayo itaishia kwenye makato na madeni.Kwa hiyo
mambo mengine utaweza kuyakomboa kwa kupitia
ujasiriamali fedha ambayo utapata itakuwa na
mchango mkubwa katika kukupahatua yamaendeleo.
Wengi waliofanikiwa na kuletamaendeleo ya familia
na taifa ni wajasiriamali. Haijalishini wafanya
biashara wa kubwa au wadogo.

(3)Kufanya maisha yaendelee:

Shughuli hizi za ujasiriamali zitafanya maisha mengine


yaweze kusonga mbele pasipo shakayeyote. Na manisha nini
mwajiriwa anayetegemea mshahara, pindi atakapoishiwa
maisha kwake hayawezi kuendelea kwani hana njia mbadalaa.
Mwisho hujikuta anaingia kwenye utumwa wa madeni.

~ 15 ~
*********************

~ 16 ~
*SURA YA 02*

KANUNI ZA KUPATA MTAJI

M
taji siyo kigezo cha kukufanya kushidwa
kutimiza malengo ya kufanya biashara yako. Hila
ninamna ya kufanya (kanuni) ili upate mtaji.
Moja kati ya changamoto kubwa iliyopo katika
swala zima la kuanzisha biashara au ujasiriamali
wowote ule nimtaji. Pengine hata wewe ambae unaendelea
kusoma kitabu hiki, usijali habari jema ni kwamba “Nothing
is impossible if you make it to be impossible will be” ikiwa na
maana hakuna kinachoshindikana hila ukikifanya
kishindikane kitashindikana tu.

Nilipata wasaa wa kufanya utafiti na kupata maoni


mbalimbali kutoka kwenye vikundi kadha ya vijana Amabao
wapo vyuo na wamtaani. Niligundua mengi watu wana
malengo makubwa sana juu ya biashara wanawaza mazuri
sana kiasi kwaba ukiwasikiliza utaona dhairi kuna mafanikio
makubwa kupitia yale ambayo wana yawaza au
kuyafikiriendapo tu watabadili na kuwa mchakato watawezaje
na changamoto mtaji?.

“Siyokila biashara ni mtaji na sikila mtaji ni biashara”


(Linus siwiti).

Ninachokimaanisha sio kila biashara au ujasiriamali unaitaji


mtaji, hapana kuna biashara zingine zinakuitaji akili yako tu.
Mfano:
 Biashara ya boda boda
 Udalali mfano wa nyumba/chumba, viwanja,simu, nk

~ 17 ~
 Biashara ya kutafuta masoko kwa njia ya mtandao, na
kutumia pesa ya mteja (network bussines) kufanyanae
biashara (pressing order) kwa kuweka bili.
Ukikaa na kutulia utagudua biashara zingine nyingi ambazo
eidha zikawa zinaitaji mtaji mdogo sana au zisihitaji hata
mtaji (lakini isiwe biashara ambayo siyo ya halali).
Swala la mtaji limekuwa kilio kwa kila mwenye nia ya
kuendesha biashara na wenye malengo na mipango mingi
lakini tatizo ni mtaji.

Tatizo kubwa ambalo lipo pia imani iliyojengeka ni kwamba


swalakuanzisha biashara ni mpaka eti uwe na mtaji mkubwa.
Na ikiwa hata biashara ya mtaji mdogo hujaiwazia. Mtu
anafikiria ili aweze kufanya anachotaka kufanya basi awe na
kiasi labda cha kuanzia 10000, 100000, 500000, 1000000/=
fedha za kitanzania. Unaweza kuanzisha biashara kwa mtaji
mdogo tu 2000/=, 3000/= hadi 10000/=na mwisho
kukuwezesha kufikia viwango vya kuwa na mtaji mkubwa
zaidi. Kumbuka ya kuwa “kila kitu uanza kwa vilivyo
kidogo hili kuleta vilivyovikubwa”.

“Unaweza ukawa na mtaji na bado ukala mtaji, na


kuendelea kulalamika huna mtaji.”

Angalia jendwali hili la mfano wa watu waliyo anzisha


biashara wakiwa na mtaji tofauti tofuti.
Mtaji Iliyozaa Faida kwa
wiki
Mtu 01 10000 20000 10000
Mtu 02 5000 10000 5000
Mtu 03 1000 1000 00

~ 18 ~
Unajifunza nini?

Kuwa na mtaji siotatizo, swala ni kwamba namna


utakavyotumia mtaji ambao utaupata katika kuzalisha faida.
Watu watatu hapo juu kila mmoja alikuwa na mtaji wake
Mtu 01:
Alikuwa na mtaji wa shilingi elfu 10000/= akaamua
kuhufanyia biashara /ujasiriamali na ukamzalishia faida ya
shilingi elfu 10000/=

Mtu wa 02:
Naye hakusita kwa shilingi 5000/= ya mtaji aliokuwa nao
aliamua kuufanyia biashara ambaye anaijua mhusika na
ikamzalishia faida ya shilingi 5000/=
Mtu 03:
Hakuona thamani ya mtaji aliokuwa nao, mosi pepingine
aliuona ni mdogo sana. Pili inawezekana hakuona shilingi
1000/= hafanyie kitu gani? Maamuzi ambayo uenda
aliyafanya
 Alifukia shilingi shimoni kwa akili kwamba
itajizaa.
 Alinunulia vocha
 Au kufanyia matumizi yeyote mengine
 Aliigawa nakadharika (n.k)

Tathimini baada ya miaka mitatu:


Mtaji Iliyozaa Faida kwa
Miaka 02 miaka 2
Mtu 01 10000/= 6120000/= 3560000/=
Mtu 02 5000/= 1560000/= 780000/=
Mtu 03 1000/= 1000/= 00

Kuna utofauti katika uanzishaji na umaliziaji wa jambo au


mambo kuna ambae anaanza na kidogo na anamaliza na vingi
na kuna ambae anaanza na vingi na kumalinza na vingi au
kidogo tofauti.

~ 19 ~
Kila mfanya biashara kubwa ambae unamwona kuna namna
ambavyo yeye alianza. Daktari nguli na bigwa wamaswala
ya Biashara na uchumi Dr. David J. Schwartzaliwahi
kusema safari ndefu inaanzishwa na hatua moja (The longest
journey begins with one step).Hatua ya kwanza katika
biashara nikuwa na wazo la biashara, pili namna ya kupata
mtaji na namna ya kukuza huo mtaji.

Kanuninane (7) bora za kupata mtaji:

Huwezi kuangaikia kitu ambacho ukijui, wala hakina


umuhimu kwako. Chenye muhimu lazimakitaitesa nafsi
kukiangaikia kukipata, mtaji ni kitu ambacho ni rahisi kupata
na wakati mwingine ni viguu kuupata. Je imekuumiza,
imekutesa, imekusumbua, namna ya kupata mtaji? Zifuatazo
ni kanuni kuu 7 bora za kukuwezesha namna ya kupata mtaji
na kuanzisha unachotaka kuanzisha. Hakika kwa kuzingatia
kanuni hizi haitatokea ukawa na stress (mawazo) ya namna ya
kupata mtaji wako.

Pia kabla hata ya kufikiria juu ya namna ya kupata mtaji


kwanza fikiria mambo makuu manne (4) ya fuatayo:
1. Aina ya biashara mfano (kuzalisha,
kuchuuza, huduma)
2. Aina ya soko (walengwa wa bidhaa yako
ni kina nani, watoto, vijana, watu wazima,
kijiji,au mtaaa nk.)
3. Ukubwa wa mtaji ( mdogo, wa kati au
mkubwa sana)
4. Ufahamu wako kwenye biashara yako
 Elimu
 Ujuzi
 Maarifa

~ 20 ~
Majibu yote ya maswali hayo juu yatakupa picha ya namna
gani ya kufikirisha AKILI kupata mtaji. Twende kwenye
kanuni za namna ya kupata mtaji.

01 WATU:
Kuna biashara hazitaji kuumiza akili sana bali zinahitaji tu
kufahamiana na watu.
“Watu ndio mtaji wako wa kwanza”. Walengwa wako wa
kwanza katika bidhaa yako ni watu, pia walengwa wa kwanza
kukufanikisha kupata mtaji ni watu.Kivipiau kwa namna ipi?
Kuna namna mbayo unaweza kujipatia mtaji kupitia mtu.
Mfanokama ni kijana na lengo lako ni kuja kumiliki pikipiki
nyingi kwa ajili ya biashara ya bodaboda. Kule kufamihana
nammiliki wa pikipiki (Tajiri) na kuweza kuwekeana mkataba
au maafikiano (Sign of agreement). Kwa fedha ambayo
utalipwa ndani ya mwaka mmoja au miwili unauwezo
kumiliki pikipiki yako.
Pia kule kuishi na watu vizuri na kufamihana nao kwa ukaribu
(build the strong relationship with others). “Ikiwa na maana
moja kati ya vitu muhimu katika kuhusiana na watu ni
kujenga uhusiano imara na watu wengine,” pindi uendapo na
wazo la biashara na ukionyesha hali ya uhitaji na kwa
kuwashirikisha kukusuport (yani wa kusaidie) ni rahisi pia
wao kuonyesha moyo wa mwitikio.
Hapa ndipo ule msemo wa“Watu ni azina ya kila kitu”
utapotimia. Ishi na watu uvae viatu.
“Ulipoleo nikutokana na watu ambao walikubeba walioko
nyuma kukufikisha hadi hapo” kiwango cha ulivyo ni
kutokana na matokeo yaliyokubeba na wewe mbebwaji. Kuna
wakati pengine ulibebwa lakini hukubebeka, fikiri kwa upya.”

Kwa nini? ni kwa sababu karibu kila kitu ambachoutakifanya


lazima pia kihusishe watu. Biashara utakayofanya wahusika ni
watu. Kuna kitu kinaitwa udhamini, kuna wakati unaitaji
kufanya biashara lakini pesa huna. Hapa unaweza kutafuta
udhamini (sponsors) kutoka kwa watu au mtu, inaweza ikawa
pesa, au chochote kitakacho kuwezesha kupata mtaji wako.

~ 21 ~
NB: Siyo kila mtu au watu wanaweza kukusaidia (supportors)
waleambao kiuhalisia hata ukiwaendea hawezi kuacha
kukusaidia hao chunga usijewapoteza. Pia wakati mwingine
uwezi jua nani wakukusaidia jaribu kwa kila unayeweza.
Kikubwa usichoke, kukata tamaa nk.

02 FEDHA BINAFSI UNAZOZIPATA:


Kati ya kanuni hii ni bora zaidi, ukweli ni kwamba fedha
ambambazo zina pita mikoni mwako ni nyingi sana. Nakama
mikono ya mwanadamu ingekuwa na uwezo wa kunukuu
(record) kiasi cha kila fedha inayopita kwenye mikono.Ni
fedha nyingi sana,Mabilioni kuna wakati unakuwa na fedha
na inakwisha pasipo kujua, au kuelewa umeifanyia nini?
 Fedha kutokakwa ndugu
 Marafiki
 Vibarua ulivyo fanya
 Msaada
 Na vyanzo vingi (chanya) vinavyo sababisha kupata
fedha.
Ukitaka kufanya biashara yeyote au kununua chochote kwa
pesa yako. Unaweza kujichanga kidogo kidogo yani kwa
kujiwekea AKIBA kwa malengo mahususi juu ya kitu
unachotaka kufanyia, wazungu wanasema “Bootstrapping”.
Unajichanga kidogo kidogo hadi kupata mtaji unaotaka. Hii
kanuni inaonekana kama ngumu sana, kwani mtu kujiwekea
akiba anakiona kitu ambacho hakiwezekani au pindi
inapotokea dharua au changamoto akiba ambayo ilikuwa kwa
dhumuni kwa lengo husika, inahamishwa na kutumiwa katika
kutatulia changamoto. “Ni bora kutafuta njia nyingine
kutatulia changamoto yako lakini siyo AKIBA”.
Ambayo umeiweka kwa ajili ya kutatulia shida yako ya mtaji.
Ndiyo maana katika mapato unayopata unatakiwa kuigawa
fedha yako mfano kanuni nzuri ni hii:
 Tenga fedha kwa ajili ya Muumba wako
aliyekufanikisha, kumtolea sehemu yako ya mapato
na kusaidia wengine kama sadaka,
~ 22 ~
 Tenge fedha kwa ajili ya maendeleo ya
unachokifanya
 Weka akiba ya Kodi, maji, nyumba na bili ya
umeme,
 Weka akiba ya dharula, Safari, kuugua ghafla, nk
 Weka akiba ya maswala ya watoto shule, nk kama
Unao.
Na mengine mengi.
“Mwingine atasema mimi kipato changu kidogo siwezi
kuweka akiba, bado kupitia hichohicho unaweza kufanya kitu.
Tafuta kujifunza zaidi juu ya shule ya kuweka akiba. Kama
unashida katika eneo hila la juu ya matumizi na namna ya
kuweka Akiba, tafuta vitabu ambavyo vinazungumzia
maswala ya Akiba na maamuzi ya matumizi ya pesa. Muhimu
itakusaidia kama unashida na unataka kuitibu hiyo shida.

03KUAZISHA BIASHARA KWA FEDHA ZA MTEJA:


Unaweza ukaumiza akili nyingi sana na ukawaza juu ya swala
la utafanyaje biashara na hauna mtaji, njia hii ni zuri na
inauwezo wa kukufanya ukapata mtaji wako. Niliwai kufanya
biasharaya nguo,(mashart), viatu, mikoba ya kina mama
pasipo mtaji hadi kupata mtaji, nilifanyaje? Nilikuwa tatafuta
picha zuri kwenye moja ya duka kariakoo Jijini Dar es Salaam
hali hali mimi nikiwa Tabora. (kupitia dada yangu) nilitafuta
wateja kwa kukuziweka picha kwenye mtandao wa simu
(what’sapp). Nilikuwa na pokea order na mteja kunipa pesa
nusu kisha kuangizi bidhaa na kumfikia mteja popote alipo.
Kwenye simu yako una majina mangapi au namba ngapi? Hao
nao ni wateja wako wakwanza, washirikishe unacho fanya
kama huna mtaji?
Mfano unawatumia picha au ujumbe wa kawaida juu ya
biashara ya order unayofanya. Wanakupa pesa ndipo nawe
unawapelekea bidhaa au anakupa pesa unampa bidhaa.
Wakati huu pengine wewe umeichukua kwa udhamini,
utarudisha deni sehemu husika ulipo chukulia bidhaa, %
(asilimia) iliyobaki hiyo itakuwa inakuhusu wewe.

~ 23 ~
04 MICHANGO KUTOKA KWA NDUGU AU JAMAA:
Je una mahusiano mazuri na ndugu na jamaa ambao
wanakuzunguka? Kwani mahusiano ndiyo msingi wa mambo
mengine yote kuendelea kutokea na kutendeka. Wazo lako la
biashara unaweza kulifanikisha kupitia (support) msaada
kutoka kwa ndugu au marafiki. Hakuna ndugu asiyependa
maendelea labda yule tu asiyetaka maendeleo yako.
Washirikishe wazo lako au malengo yako ya juu ya kile
unachotaka kukifanya, washirikishe changamoto yako ya juu
ya kupata mtaji, na wakiwa waelewa wataonyesha ushirikiano
wao pamoja na wewe. Kingine ambacho wengi ukosea ni kule
kuto jenga mahusiano na ndugu na jamaa mapema, ndio
maana nilianza kwa kukuuliza swali, je ni vyema
kumkumbuka mtu wakati wa shida au uhitaji? Nijambo
ambalo siojema. Pia kumbuka ya kuwa sio kila ndugu au
jamaa wanaweza kukusaidia, wapo ambao wao hawependi
kuona unasonga mbele au kufanikiwa kama wao. Mwombe
Mungu akuonyeshe ndugu na jamaa sahihi ambao
watakusaidia, kulifanikisha kusudi lako.

05: KUUZA KITU AMBACHO KITAKUPA THAMANI YA MTAJI.


Ni jambo ambalo gumu sana lakini kutokana na uhitaji na
ugumu inakulazimu kufanya hivyo. Kuuza kitu au vitu kwa
maslahi yenye maana siyo kosa, kosa ni kuuza kwa maslahi
ya siyo stahiki (yasiyo fahaa). Uza lakini ukiwa na malengo
ya kukirejesha kama hicho au zaidi. Mfano mzuri ni kutoka
kwa rafiki yangu, tukiwa chuoni sikumoja aliniletea wazo la
biashara ya ASALI,wazo hili lilikuwa jema sana. Swali
ambalo nilimuliza ni juu ya upatikanaji wa mtaji binafsi
nilikuwa na akiba kidogo kwa upande wake akaniabia hana
kitu hila anaweza kufanya kitu. Nikamuliza tenani kipi hicho?
akaniambia nina hii smart phone yangu naweza nipo tayari
kuuza nipate mtaji, tufanye pamoja biashara kama simu zipo
tu nitapata nyingine tena uenda bomba zaidi ya hii. Haya
yalikuwa maamuzi magumu sana yenye mamufaa. Sikwabii
wewe kama unataka kufanya biashara au ujasiriamali ufanye
kama alivyofanya huyu ndugu hila ukiwa na nia ya dhati na

~ 24 ~
kuona kanuni za kupata mtaji zote zimeshindikana unaweza
kufanya hivyo ukiwa na malengo ndani yake.
“Kuuza kitu chochote na ukiwa huna lengo la kukirudisha,
utakuwa wajiona unaenda mbele kumbe huko palepale”
(unapiga marktime).linus s.

Kama ulikinunua hapo awali hili mradi uwe nacho tu


kama wengine lakini hakikuwa na maana kwako, kwa
wakati huo kukiuza kwa manufaa ya mpango mwingine
siyo sumu.

06 FANYA VIBARAUA KWA MUDA:


Kibarua, maana yake nini?
*Ni kazi dogodogo za mikonoanazoweza kuzifanya mtu
kwa ajili ya kujipatia Ujira (kipato) baada ya kumfanyia
mtu kazi yake.

Kibaru,ni kazi isiyomaalumu au ya kudumu (not


permanent business/job).

Vibarua,ni watenda kazi mbalimbali ambo wameajiriwa


na mwajiri kufanya kazi iliyo kusudiwa kwa muda
mahususi na kujipatia kipatao.
Ni kanuni nzuri ya kuweza kujipatia mtaji wako wa
kuanzisha biashara yako binafsi tafuta vibarua mbali
mbali ambavyo unajua unaweza kuvifanya kwa muda
Fulani kisha ukishapata fedha kama sehemu ya kianzio
cha shughuli unayotaka kufanya haina haja kuendelea na
vibarua. Nenda kaazishe utachotaka,
Chenye kuleta mafanikio.

~ 25 ~
07FEDHA ZA MKOPO KUTOKA TASISI/ SHIRIKA LA
BANK:
Kuna Bank na mashirika mbalimbali (Micro finance),
ambayo yana toa mikopo, dhana kubwa ya watu
kushindwa kuchukua mikopo ni juu ya mashariti
yaliyopo katika upatikanaji wa mkopo. Kingine kuogopa
kuja kushidwa kurejesha, mkopo ni kanuni kuu ya
kukuwezesha kutatua tatizolako la mtaji, ikiwa kanuni
zingine zote zimeshindikana. Chukua mkopo ukiwa na
lengo la kufanyia biashara kweli na plans (mipango)
mikakati ya namna ya kuzalisha faida na kurejesha
mkopo uliochukua. Tatizo linakuja mtu anachukua
mkopo akiwa bado hana mpango mkakati wowote
kuhusu anachotaka kukifanyia na namna atakavyofanya
kukuza na kuzalisha faida kubwa. Mwisho anajikuta
anafanya biashara ambayo mosi inaweza kuwa na faida
kubwa lakini mzunguko wake wa pesa ni wa taratibu, au
akachukua mkopo na kuanzisha biashara katika eneo au
mazingira ambayo bidhaa hiyo inafanywa na wengi au
wahitaji ni wa chache na mwisho wa siku hujikuta
anapata hasara kubwa na kushindwa kurejesha fedha
aliyokopa na kubakiwa anadaiwa. Kila kitu kina faida
yake na hasara yake, hivyo swala la mkopo linafaida
yake na hasara yake pia. Kuwa na malengo mapana na
mahususi kabla ya kuchukua mkopo,

NB: Kuna mtu anaweza kuchua mkopo kwa lengo la


kufanyia biashara kweli, lakini anapo kutana na
changamoto au fedha zinapokuwa mikononi mwake
anakosa msimamo na kushidwa kuya heshimu mawazo
ya awali na kubadili mawazo au fedha aliyochukua
anatatulia shida nyingine ambazo zimejitokeza. Hili ni
kosa kwa mtu yeyote anayetaka kufanya biashara /
ujasiriamali. Mtu huyu ni sawa na anayekwenda mbele

~ 26 ~
huku hajui aendako ni wapi. Hawezi kuleta maendeleo,
binafsi, jamii, na Taifa. Na akitaka kupona katika eneo
hili cha kwanza:
 Awe mtu wa kuheshimu wazo la kwanza,
 Awe na msimamo na malengo yake,
 Asiwe mtu wa kuiishia njiani,
 Awe na mipango na mikakati
 Aheshimu kila fedha inayopita mkoni mwake,

*NAMNA YA KUONA FURSA NA KUTUMIA


HIYO FURSA*

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kauli hii “If


opportunity doesn’t knock,build a door” akiwa na
maana ya kuwa “- Ukiona fursa hazigongi mlango
(kubisha hodi) kwako, ujue pengine huna mlango,
jenga mlango.”
Ukweli ni kwamba kwa hali ya kawaidi tumezungukwa
na fursa ambazo ni nyingi sana za kuweza kutengeneza
mamilioni ya fedha. Sehemu uliyopo, iwe mtaani kwako,
eneo lako la kazi, shuleni, chuo, mkoa uliyopona hata
hapo ulipo sasa hivi nyuma yako mbele yako na pembeni
kote umezungukwa na fursa.Tatizo ni moja hujaiona? Au
umeiona lakini wajanja wameshakuwai, nauenda
umeiona lakini bado hujaitumia hiyo fursa. Hakuna mtu
yeyote ambaye atakuja kushikisha mkononi, kukuletea ni
wewe wakuinuka na kuishika. (Hold careful opportunity)
ikiwana maana fursa ukipata ishikiliye kwa makini. Kila
mfanya biashara, mjasirimali, ambaye unamwona
leomafanikio yake yametokana na kugudua fursa na
kutumia kubaini tatizo na kulifanyia ufafanuzi na
~ 27 ~
kuweza kujipatia kipato kwa kumtatulia mtu mwingine
changamoto:
Nini maana ya fursa?
Neno fursa lina maana tofauti tofauti lenye kulenga
kubaini mbadala wa kuweza kujipatia kipato kwa
kutatua shida au changamoto ya wengine.

* Fursani uwezo wa kugundua tatizo na kulifanyia


ufumbuzi kwa ajili ya kujipatia kipato.
* Fursani jinsi mtu anavyoweza kutazama jambo, au
kitu na kubuni mbinu mbalimbali za namna ya kuweza
kufanikiwa kwa faida yake, jamii, na taifa.

*Fursani tatizo ambalo linahitaji suluhisho na kupitia


suluhisho hilo hilo mtoa suluhisho atafanikiwa kwa
kuingiza kipato. Mfano mtani kwako kuna tatizo la
upatikanaji wa mboga mboga, vitunguu, nyanya nk
maana kupatikana kwakwe mpaka mtu atembee umbali
kidogo, wewe unaweza kutatua tatizo hili kwa kwa kutoa
suluhisho la kufungua genge.
*fursa ni kituchochote chanya ambacho ugundulia
(vumbuliwa) na kufanywa kwa manufaa, tija (husika) ili
kutoa matokeo mahususi yakuweza kutengeneza kipato.

“Fursa hazitafutwi, hazitengenezwi, daima zipo ni


jinsi ya kuiona au kuigundua tu”

~ 28 ~
*KANUNI TANO (5) YA NAMNA YA KUIONA
FURSA*

Mwenyezi Mungu na akupe macho ya kuona vyema.


“Sikila fursa unayoiona au inayopita kwako ni fursa bali
pima kila fursa zingine ni bandia (mtego). Ni nacho
jaribu kulenga hapa kwako msomajina unatamani kujua
namna ya kuiona fursa chukua hatua ya kuwa mchunguzi
na kufatilia zaidi.

 Soma vitabu, hudhuri mafunzo:


Katika kujifunza, na kupitia kusoma kuna mambo mengi
ambayo ya mejificha ndani yake (madini). Walio
migodiniiliwaweze kujipatia dhahabu, na madini
mbalimbali uwa wanalazimikakwenda chini maili ndefu
sana hadi kuyafikia. Nini maana yake, katika swala zima
la fursa, ili kupata na kuviona vingi, inakulazimu
uchukue muda wa kusoma na kuhudhuria mafunzo, na
kujifunza kutoka kwa watu wengine kwaundani wake
zaidi ili nawe upate kufahamu ni kwa namna gani, wao
walivyoweza kufanikiwa kupitia kuigudua fursa. Elimu
na maarifa utakayo ya pata kupitiakusoma na kuijifunza
vichanganye kwa pamoja wekakatika mchakato au
vitendo zaidi.

Maarifa + Mchakato= Matokeo makubwa


Hii kanuni ni nzuri sana ukitumia itakupa hatua kila
itwapo leo tumia na ujionee matokeo. Msiwe msomaji,
msikilizaji, mwongeaji pasipo vitendo zaidi
 Kusoma vitabu,
 Mafunzo,

~ 29 ~
Muhimu yafanyie kazi yatakutengenezea mianya
mikubwa katika kufanikiwa na kukipata ambacho
haukuwa nacho, na kukiongeza ubora zaidi ulichokuwa
nacho. Kumbuka kuwa kila umwonae anafanya kitu
fulani jua ya kuwa lazima awe amejifunza au kupitia
kujifunza ndio maana akitenda kwa ufanisi kile
akitenacho.

 Kupitia changamoto:
Ukiona kile ambacho wengi wanakisumbukia kukipata
kiurahisi, yawezekana ikawa mtaa unao kaa, shuleni,
chuoni, ofisi au mahali popote ulipo. Jua hii ni
changamoto na ukiweza kuipatia suluhisho kwa
kurahisisha huo upatikanaji wa uhitaji wawengi wa watu.
Mfano upatikana wa maji, utapochukua hatua ya na
kuamua kutafuta yafuatayo:
 Sim tank na kulijaza na kuanza kuuza maji,
 Kutafuta magurudumu na kuajili vijana wa
kusambaza maji mtaani,
 Kuchiba kisima na kufunga mota ya kuvutia
maji,
Kwa kuona tatizo hili utakuwa umetatua lakini kubwa
utakuwa umejitengenezea kipato.

 Uwezo ulionao:
Mungu ni mgawa talanta na vipawa mbalimbali ndani ya
kila mwanadau, ndani yako kuna kitu ngani ambacho
unaweza kukifanya?
 Kipaji ulicho nacho,
 Ujuzi uliojifunza au kuzaliwa nao,
 Maarifa ndani yako,
Ukiona ndani yako kuna kitu cha ziada na cha kipekee
mbali na elimu ya darasani anza na hicho kwanza.
Tumiakwa juhudi, na manufaa chanya tunu uliyonayo

~ 30 ~
ilikuyafanya maisha yaendelee. Kuna mtu moja anaitwa
Arthur yeye anasea hivi:

“Start where your, use what you have, do what you can”
akiwa na maana ya kuwa anzia hapo ulipo, tumia
ulivyonavyo, fanya unachoweza au uwezavyo.
Hapa tunajifunza kitu muhimu sana kutoka kwa Bwana
Athur, kuna ambao wanavyo vitu lakini hawaoni kama
kwa vichache walivyo navyo na sehemu walipo
wanaweza kuvitumia na kuleta badiliko. Leo fanya hivyo
na wewe usisubiri mpaka iwe hali shwari, uwe eneo,
mkoa fulani ndipo uweze kufanya ambacho unatamani
kukifanya.

 Mkusanyiko wa watu:

Popote penye mkusanyiko wa watu jua yakuwa kuna


fursa nyingi sana ambazo wazionazo huwa awafanyi
uzembe kuzikimbilia na kuzitumia vyema. Lakini bado
unakuta mtu kila siku anakumbia haoni fursa hata
kwenye ili. Mwingine anaweze kukumbia kati ya haya:
 Nitafanya kitu gani sasa,
 Mbona kila mtu anafanya ninacho taka kufanya,
 Nanzia wapi mbona mtaji nao sina.
Mambo mengi sana ambayo mwenye upofu wa kuziona
fursa anajiuliza. Kwako wewe ambae unataka,
unatamani siku zote kufanya kitu katika maisha hususani
katika biashara ujasiriamali pakuanzia ni hapa.
Mikusanyiko hiyo inaweza kuwa ni ipi?
1. Kwenye makutano ya watu mfano maeneo ya
panda njia,
2. Mikutano na mihadhara mbalimbali,
3. Matamasha na washa ,

~ 31 ~
4. Shughuli mbalimbali za wanafunzi, mfano
mahafari ya kuhitimu, makongamano, na
kambi mbalimbali za wanafunzi.

 Kuboresha wazo la mwingine:


Kuchukua kila kitu (Copy and pasting) anachofanya mtu
mwingineni kitu ambacho kitazidi kukufanya ushindwe
kuiona milango ya mafanikio. Hapa fursa ni ya kwamba
ukiona akifanyacho mtu mwingine kina mapungufu
(Mapengo mapengo) na kwake kuna ambacho hakipo,
wewe chukua hatua ya kuboresha na kuanza kufanyia
kazi, juhudi, nidhamu, na uvumilivu na uaminifu
vitakupamatokeo makubwa sana ambayo pengine
uliyechukua wazo kwake hajayafikia.
 Kuonyeshwa:
Kipofu uhitaji msaada mkubwa sana ili kuonyeshwa njia
na kuweza kufika mahala ambapo anatamani kufika.
Hata kwenye swala zima la fursa kuna ambao ni vipofu,
yani hawaoni kabisa kabisa. Wewe ambae umepata
uwezo wa kuona fursa lakini waiona kwako haifai,
hakidhi, huna muda wa kuifanyia kazi. Mshilikishe,
mwabiena mwingine ikimfaa aifanyie kazi, kwa kufanya
hivi kwako wewe unajitengenezea hazina kubwa ya
mafanikio.

Ukifanyacho + Kujitoa kwa ajili yawengine =


Mafanikio yako zaidi.

*Kudharau kitu, watu au kila wazo linalopita kwenye


masiko hadi kwenye ufahamu wa akili, huku ni
kujitengenezea mazingira ya kuwa hivyo hivyo ulivyo.
Na kutokuwana badiliko katika eneo uliyopo (changes in
your cariers). Nini cha kufanya?

~ 32 ~
 Pima kila wazo na ambalo la muhimu lifanyie
kazi kwa haraka,
 Fanyia mchakato kile ambacho unaonyeshwa
ukiona chakufaa.

~ 33 ~
*SURA YA 03*

KANUNI ZA KUTENGENEZA SABUNI


abuni ni bidhaa za vidwani kamazilivyo bidhaa zingine.

S lakini bidhaa hizi za aina mbalimmbali za sabuni


unaweza ukajifunza na ukatengeneza mwenyewe ukiwa
nyumbani kwako, unaweza kufungua hata kiwanda kidogo
ukawa unazalisha bidhaa ya sabuni.Ni rahisi na nyepesi
kujifunza ukiwa tu na nia ya dhati kutoka moyonu yakutaka
kujifunza. Twende tukaangaliye Sabuni mbalimbali
zinazotumika kwa 99% katika maisha ya kila siku,na naamna
ya kutengeneza. Kufulia kuoshea vyombo, kuogea, kusafishia
vyoo, nyumba, magari, nk.

SABUNI YA MAJIVU:
Utengenezaji wa sabuni hii inahitaji juhudi na umakini
mkubwa kwa mtengenezaji.
Jinsi ya kutengeneza:

Hatua ya 1
Kusanya maganda ya ndizi, magogo ya mipapai, maganda ya
mbegu za kakao, kausha vitu hivi kwenye jiko la jua hadi
vikauke, kama huna jiko la jua vikaushe juani.

Hatua ya 2
 Vichome hadi kupata jivu, pia unaweza kutumia jivu
la kuni au karatasi ambazo hazijaandikwa na sii jivu
la plastiki au vitu visivyo vya asili.
 Kusanya majivu na uyapima kwenye ndoo ya lita 10.
 Tumia ndoo yenye ujazo wa lita 20, ongeza lita 15 za
maji ya moto na Korogavizuri, baada ya dakika 10,
chuja kwa kutumia kitambaa, Kumbuka wakati wote
kutumia ndoo ya plastiki au chombo cha mfinyanzi.

~ 34 ~
 Ongeza maji ya moto lita 5 kwenye majivu yaliyobaki
endelea kukoroga kwa dakika 10 halafu chuja tena.
 Weka pamoja vile vyote ulivyochuja kwenye chombo
cha mfinyanzi kama utatumia chombo cha metali
kitaharibika.
Hatua ya 3
Chemsha majivu ya kuni vizuri kilo sita na uchanganye na
maji lita 4. Korogakwa pamoja kwa dakika kumi kisha
yarudishe tena kwenye moto. Chemshakwa muda wa dakika
thelathini na uepue ili yapoe.

Hatua ya 4;

Chukua magadi soda kilo 6 na uloweke kwenye maji lita 14.


Viache pamoja kwa siku 4 ukiwa unakoroga asubuhi na jioni
kwa kutumia chombo cha bati au alminium unapokoroga.

Hatua ya 5

Changanya majivu lita tatu na maji ya magadi soda lita 3 na


ukoroge kwa muda wa dakika10.Endelea kukoroga na
tumbukiza chumvi vijiko6 vya chakula, mafuta lita mbili huku
ukikoroga baada ya muda huo unaweza kuweka kwenye umbo
kwa ajili ya kutengenezea miche.

SABUNI YA UREMBO:

Sabuni hizi zinatengenezwa na mafuta safi na ni nzuri


sana kwa ngozi ya mwili.Unapotumia sabuni hizi ngozi
yako hungara kwa sababu ya tabia yake ya kuufanya
mwili kama umepakwa mafuta kila wakati.

Mahitaji :
i. Mafuta ya mbogamboga/ mawese lita 8
ii. Maji lita 5.
iii. Sodium hydroxide {NaOH}lita 1
~ 35 ~
Jinsi ya kuchanganya
Hatua ya 1
Pima maji lita 5, ongeza sodium hydroxide {NaOH} lita 1,
koroga mchanganyiko huo na uache hadi joto lake lipungue.
Hatua ya 2
Ongeza mafuta lita 8 kwenye mchanganyiko wako huku
ukikoroga bila kusita kwa muda usiopungua dakika 60, ili
kuutambua kama mchanganyiko wako umekuwa tayari utaona
umekuwa laini.

Hatua ya 3
 Mimina kwenye trea au vifyatulio, kabla sabuni
haijawa ngumu unaweza kukata kwa maumbo
unayotaka au kutia urembo, jina kwenye sabuni huu
ndio wakati muafaka.

 hifadhi sabuni mahali penye mwanga na penye kivuli,


ni lazima sabuni ikaae majuma (siku) 8 hadi 12 au
ianikwe kwenye jiko la jua kwa majuma 3 hadi 4
kabla ya kutumika.
Kuharakisha kuitumia ni hatari kwa sababu sodium hydroxide
itakuwa haijamaliza utaratibu wa utengenezaji hivyo kuharibu
ngozi ya mtumiaji.

 Maji lita5
 Sodium
Hydroxide (NaoH)
 Mafuta lita 8

~ 36 ~
SABUNI YA MANUKATO:
Sabuni hii inakuwa imesheheni manukato ya aina mbalimbali
ambayo mtengenezaji anakuwa ametumia katika utengenezaji.
Mahitaji
 Unga wa sabuni iliyotengenezwa na kuwa tayari
zaidi ya majuma (wiki) 8
 Maji

Jinsi ya kutengeneza
Hatua ya 1
Saga sabuni iliyotengenezwa muda mrefu kupata unga.
Pima kg (kipimo) 8 vya unga wa sabuni, ongeza maji lita 2 na
yeyusha kwenye joto la kadiri ukikoroga hadi utakapo
changanyika vizuri.
Hatua ya 2
 Ongeza matone mawili ama matatu ya marashi halafu
mimina kwenye vifyatulio.

 Usiwe na haraka unapotengeneza sabuni za manukato


kama hutotumia njia niliyokuonyesha hapo juu
sodium hydroxide itaharibu manukato uliyoweka.
.

4. SABUNI YA ASALI AU CREAM

Sabuni hii ni ya asili ni mahususi kwa ngozi zenye mafuta na


madoa madoa.
 Mafuta lita 8.
 Maji lita 5.
 Sodium hydroxide lita1.
 Asali lita 1.

jinsi ya kuchanganya
Hatua ya 1
Pima maji lita 5, ongeza sodium hydroxide {NaOH} lita 1,
koroga mchanganyiko huo na uache hadi joto lake lipungue.

~ 37 ~
Hatua ya 2
Ongeza mafuta lita 8 kwenye mchanganyiko wako huku
ukikoroga bila kusita kwa muda usiopungua dakika 60, ili
kuutambua kama mchanganyiko wako umekuwa tayari utaona
umekuwa laini.
Hatua ya 3
Weka asali lita 1 kwenye mchanganyiko wako hapo juu na
kisha koronga ili asali ichanganyike
Hatua ya 4
 Mimina kwenye trea au vifyatulio, kabla sabuni
haijawa ngumu unaweza kukata kwa maumbo
unayotaka au kutia urembo, jina kwenye sabuni huu
ndio wakati muafaka.
 hifadhi sabuni mahali penye mwanga na penye kivuli,
ni lazima sabuni ikae majuma (siku)8 hadi 12 au
ianikwe kwenye jiko la jua kwa majuma(wiki) 3 hadi
4 kabla ya kutumika.

Kuharakisha kuitumia ni hatari kwa sababu sodium hydroxide


itakuwa haijamaliza utaratibu wa utengenezaji hivyo kuharibu
ngozi ya mtumiaji.

 Maji lita 5
 Sodium hydroxide
Lita 1
 Mafuta lita 8
 Koroga dk 60
 Asali lita

~ 38 ~
5. SABUNI YA KIPANDE/ MCHE
Sabuni hii inaitaji vitu vifuatavyo wakati wa utengenezaji
wake
Mahitaji
 Caustic soda kg1
 Mafuta lita 5 au 10
 Mawese
 Nazi
 Nyonyo
 Mbosa
 Glycerin 1 4
 Chumvi 1 4 kg
 Rangi 1 kijiko cha chai
 Maji 5lita
 Slesi vijiko 5
 Sodium silicate vijiko 4-5 vya chakula

Jinsi ya kutengeneza
Hatua 1.
Chukua Caustic soda kg 1 changanya na maji lita 5
(koroga kwa daki 3) acha siku 3ili ipoe vizuri.
N.B chombo kisiwe cha plastic.
Hatua 2
 Chemsha mafuta hadi yaivehii unaweza kutambua
kwa kutumbukiza karatasi nyeupe ikitoka nyeupe
kama ilivyo basi mafuta yako yapo tayari. Pia
unaweza kutumia hydrogen peroxide kuondoa
rangi ya mafuta.
 Acha yapoe
Hatua 3
Chukua mchanganyiko wako wa caustic soda ulioifadhi
kwa siku 4 changanya na mafuta uliochemsha. Mafuta
yanayotumika ni moja wapo kati ya yale yaliyo
oredheshwa hapo juu.
Hatua 4
Changanya mchanyiko wako hapo juu pamoja na hivi:

~ 39 ~
 Glycerin 1 4
 Chumvi 1 4Kg
 Rangi 1kijiko cha cha chakula
 Perfume 1kijiko cha chakula
 Sodium silicate vijiko4-5 vya chakula

Hatua 5
Baada ya kukoroga utapata uji mzito ambao utapelekea
kwenye mould.

SABUNI YA MAGADI (GWANJI)


Sabuni ya magadi au gwanji ni sabuni yenye uasili wa tofauti
kutokana na jinsi ilivyotengenezwa na matuizi yake.
Chimbuko la bidhaa hii ni maeneo ya ukanda ambao zao la
mchikichi inapatikana kwa wingi kwa ajili ya mafuta ya
mawese. Mfano ni KIGOMA. Sabuni ya Gwanji
inatengenezwe kwa wingi sana na halimaarufu wake ni sabuni
ya kigoma.

Mahitaji:
 Caustic soda 450g
 Mafuta lita 1na nusu (1 ½)
 Korie,
 Nazi,
 Mawese
 Sodium silicate
 Gelcerine

~ 40 ~
 Cd E
 Perfumu
 Soda ash.

JINSI YA KUTENGENEZA:

HATUA 01
Changanya Caustic soda na maji kisha acha kwa masaa
24maji chupa nne (4) za soda zenye ujazo 350 lita.

NB: Usichukue maji na kuweka kwenye Caustic soda, bali


chukua Caustic soda weka kwenye maji. Ukifanya kinyume
na hapo utakuwa umejitengenezea hatari.

Hatua ya 02
Utachukua sodium silicatena kumiminia kwenye
mchanganyiko wako hatua namba 01 hapo juuna kukoroga.

Hatua 03
Chukua mchanganyiko wako tena wa hatua namba 2 weka
kwenye ndoo yenye mafuta na kisha ukoroge.

Hatua 04
Weka rangi ya blue, perfume na baada ya hapo peleka
mchanganyikowako kwenye Mould (UMBO) , weka juani na
uache baada ya muda kidogo. Sabuni yako itakuwa tayari

SABUNI YA KUSAFISHIA VYOO, MASINKI, NA


TILES:
Utengenezaji wa sababuni ya kusafishia vyoo, masinki na tiles
hauna tofauti na sabuni ya kawaida ya maji. Hatua pia ni zile
zile huku unaweza kutumia marighafi za kuvutia kwa harufu
safi ya manukato (perfume) pia unaweza kutumia rangi ya
utofauti na rangi inayopendwa hapa ni rangi ya kijani

~ 41 ~
Mahitaji:
 Formaline 1 2 lita
 Slesi 1 2
 Perfume
 Rangi
 Chumvi yamawe 2kg
 Maji 40lita
 Beseni
 mwiko
Jinsi ya kutengeneza
Hatua01
Weka maji kwenye beseni 40lita
Hatua 02
 Weka formaline
 Slesi 16 vijiko vya chakula
 Rangi
 Perfume 5 vijiko au kifuniko 100ml
Hatua 03
Koroga mchanganyiko wakowote kwa mda wa daika 15
Hatua 04
Sabuni yako itakuwa tayari kwa kupakiwa kwenye vyombo
maalum na kwenda sokoni
Mwonekano wa sabuni yako ukiwa umepaki kwenye
vifungashio.

 Maji lita 40
 Formaline chupa
500ml
 Slesi vijiko 16
 Koroga
 Rangi
 Perfume vikio 5
 Chumvi 2kg

~ 42 ~
SABUNI YA MAJI
Sabuni hii ni ya maji inafaa kwa kufulia, kuonyeshea vyombo
kusafishia vyumba, vyoo na matumizi mengine mengi.
Mahitaji:
 Beseni
 Maji 20 lita
 Mwiko
 Sulphonic acid 1 lita
 Soda ash
 Rangi
 Glycerine
 Perfume
 chumvi
Jinsi ya kutengenza
Hatua 1
Weka maji 20lita kwenye beseni lako
Hatua 2
 Weka sulphonic acid
 Soda ash
Hatua 3
Koroga hadi mchanganyikowako uchanganyikane vizuri
Hatua 4
 Weka chumvi ya mawe au kiwandani 1kg
 Rangi 2 vijiko vya chakula
 Glceline 2 vijiko vya chakula
 Perfume yoyote mfano, rose, orange, pineaple n.k
Hatua 5
Koroga mchanganyiko wako kwa mda wa dakika 15
Hatua 6
Sabuni yako tayari kwakuhifadhiwakwenye vyombo maalum
na kwenda sokoni.

~ 43 ~
Mwiko

 Maji 20 lita
 Sulphonic acid 1 lita
 Soda ash
 Rangi
 Glycerine
 Perfume
 chumvi

Njia nyingine/ Mbadala yepesi ya utengenezaji wa sabuni


ya maji 25 lita
Andaa marighafi zako zote kama vile
 Sulphonic acidi lita 1
 Soda ash ½
 Sles mfuto glass( 250ml)
 Chumvi
 Rangi
 Perfume
 Glceline
Hatua 01
Pima maji lita 5 kutoka kwenye lita 25 changanya na soda
asha kisha acha kwa mda kidogo

Hatua ya 02
Pima maji 1lita kutoka kwenye lita 20 changanya na chumvi
250-300 gram, kama chumvi ni ya mawe acha kwa mda
kidogo hili iwezekuyeyuka vizuri.

~ 44 ~
Hatua ya 03
Andaa Beseni lako au chombo chochote kikubwa kisiwe cha
chuma. Weka sulphonic acid lita moja kwenye beseni na kisha
ikorogo kwa mwiko mrefu au mti.
Hatua ya 04
Weka sles yako kwenye sulphonic acid kisha koroga kwa
haraka haraka.
Hatua ya 05
Weka maji lita 15 kwenye mchanganyiko wako hatua namba
04, weka tena changanyiko wako wa soda ash na maji lita 5.
Jumla itakuwa lita 20.
Hatua ya 06
Weka mchanganyiko wako wa chumvi na maji(lita 01)
kwenye hatua 05. Na kisha pima maji lita 4 zilizo baki. Weka
hatua 06. Kumbuka kwa hatua zote usiache kukoroga.
Hatua 07
weka vitu vilivyobakia ikiwepo rangi, gyceline na marashi
(perfumu). Koroga na mwisho sabuni yako itakuwa tayari
kwa kwenda sokoni.

SABUNI YA UGA
Mahitaji
 Sulphonic acid 1 lita
 Sodium carbonate ( Naco3) 3kg
 Optical Bright 6 vijiko vya chakula
 Nasa vijiko 5 vijiko vya chakula
 Perfume
 Beseni
 Mwiko mrefu
Jinsi ya kutengeneza
Hatua 1
Vaa glofusi, chakuziba pua

Hatua 2
 Pima sulphonic acid 1lita
 Weka kwenye beseni

~ 45 ~
Hatua 3
Weka sodium carbonate lita 3/ kg kwenye mchanganyiko
hapo juu kisha koronga
Hatua 4
 Weka optical brighty 6vijiko
 Nasa 16 vijiko
 Soda ash
 Perfume
 Koroga
Hatua 5
Sabuni yako itakuwa tayari kwa matumizi
Beseni
 Sulphonic acid
1 lita
 Sodium carbonate
(Naco3) 3kg
 Optical Bright 6 vijiko
vya chakula
 Nasa vijiko 5 vijiko
 vya chakula
 Perfume

Kanuni ya pili ya kutengeneza sabuni ya unga


Kilo si chini ya 8kg
Mahitaji:
 Maji 500ml
 Sulphonic acid 1lita
 Optical bright
 Nasa 10gram
 Soda ash 6gram
 Sodium metasilicate vijiko 12-15 vya chakula
Jinsi ya kutengeneza:
Hatua 01
Andaa kifaa chako chakukuwezesha kutengeneza kiwango
cha sabuni unayotaka kutengeneza, kiwe katika hali ya ukavu.

~ 46 ~
Weka maji kiasi 500ml.
 Weka Sulphonic Acid `1 lita kwa hali ya taratibu
kwenye maji huku ukikoroga. Rangi itabadilika
kutoka kahawiya na kuwa uji mzito mweupe
Caution/ Tadhari: Always add acid to water and not water to
acid “ikiwa na maana siku zote ongeza kemikali kwenye maji
na siyo maji kwenye kemikali. Kinyume na hapo utakuwa
unajitafutia hatari na kusababisha jina lako kubadilika,
nakutakia hali ya umakinihapa.

Hatua 02:
 Weka Optical Bright vijiko 16 vya chakula
 Nasa vijiko 5 vya chakula
 Weka perfume hadi kupata nakshi unayotaka.
Hakikisha unaendeleakukoroga hili
mchanganyiko wako uwe sawia.
Hatua 03
 Weka soda ash kilo 6kg
 Sodium metasilicate vijiko 12-15 changanya kwa
pamoja.
Hatua 04:
Acha sabuni yako ipo kwa muda na kisha ifunge kwenye
vifaa ambavyo utakuwa umeandaa. Sabuni yako itakuwa
tayari kwa kwenda sokoni.

9. SABUNI NGUMU:
Sabuni hii inatumika kuondoa uchafu mgumu pamoja na
madoa sugu.
Jinsi ya kuchanganya
 Pima maji lita 5
 weka sodium hydroxide lita 1
 acha mchanganyiko uchanganyike vizuri hadi uanze
kupoa. Ongeza mafuta vipimo (lita) 6 kwenye
mchanganyiko wako huku ukikoroga bila kukoma
hadi dakika 60.

~ 47 ~
Kabla sabuni haijawa ngumu sana, ongeza vipimo 2 vya
kaolin iliyochekechwa vizuri kama kaolini haipatikani
unaweza kutumia majivu ya kuni yaliyochekechwa vizuri
mimina sabuni kwenye kifyatulio na baada ya kuganda ikate
vipande kisha iweke sehemu safi ikauke taratibu hadi ndani ya
siku 12 sabuni itakuwa tayari kutumika.

Sabuni hii ni ile inayotumiwa na watu kwa ajili ya kufulia hii


inafaa sana hasa katika maeneo yaliyo na maji ya chumvi.

Utengenezaji wake hautofautiani sana na sabuni nyingine


lakini sabuni hii ina mawese au mafuta kidogo kuliko zile za
kuogea au za kipande.

 Maji lita 4
 Sodium hydroxide {NaOH} lita1
 Mafuta lita 5

Baada ya kuchanganya na kuikoroga kwa muda wa dakika 60


acha ikauke kama sabuni nyingine muda usiopungua majuma
8 hadi 12, isage na kuichekecha na chekecheo ili kupata unga
laini wenye ukubwa ulio sawasawa hapo sabuni yetu iko
tayari kuifungasha na kuiingiza sokoni ama kuitumia wewe
mwenyewe.

11. SABUNI YA RANGI KWA KUTUMIA VITU


ASILIA:
Sabuni hizi ni zile ambazo zinatengenezwa na rangi asilia
ambazo hazina mazara yoyote kwenye ngozi ya binadamu
Unaweza kujiuliza ni kwa jinsi gaini nitapata rangi ya sabuni
huku sina fedha ya kununua hii sitatizo tumia rangi za viungo
kama:
 manjano,
 zingifuri,
 karafuu, unga wa miti ya dawa kama mwarubaini,
 na hata mafuta ya mawese.

~ 48 ~
Kitendo cha kuweka rangi kwenye sabuni unaamua uweke
wakati gani wakati unaanza au wakati wa kumalizia hii haina
tatizo ila inategemea.Mafuta ya mawese huwa na rangi ya
njano,nyekundu kutokana na carotene iliyomo.
Kwa sababu hii ukitumia mawese bila kuharibu carotene
iliyopo unapata sabuni ya njano na hii ni rangi halisi na ya
asili isiyo na madhara yoyote.

Mawese pamoja na mbegu za bixa hupata sabuni nyekundu.


Utengenezi wake unafuata hatua kama tulivyokwisha kuona
kwenye sabauni zilizopita. Isipokuwa mwishoni utakuwa
unaweka unga wa miti ya dawa pamoja na rangi.

11. CREAM YA KUNYOLEWA

Mahitaji
 Majani mabichi yanayo nukia mfano mkaratusi,
limau, michaichai, lavenda
 kipimo 1
 Maji Lita 1
 Unga wa sabuni iliyotengenezwa zaidiya wiki 8 kilo 5
Asali vijiko 3
Jinsi ya kuchanganya
Changanya vitu hivyo kwa pamoja taratibu chemsha
mchanganyiko huu hadi uwe kitu kimoja, hii ni nzuri
ikifanyika kwenye jiko la jua itasaidia kupunguza kiwango
cha mvuke utakao toweka wakati wa kuchemsha.
Kama huna jiko la jua basi lazima uongeze maji ili kurudisha
katika ujazo wa awali, baada ya kuepua koroga hivyo hivyo
wakati inaendelea kupoa, ikisha poa kabisa hifadhi katika
chombo kisichopitisha hewa ili kuzuia isikauke.
chombo kizuri ni cha kioo, plastiki au ka

~ 49 ~
*SURA 04*

UTENGENEZAJI WA
MISHUMAA/SHAMPOO
UTENGENEZAJI WA MISHUMAA

M shumaa, ni nishati mbadala inayotumika kwa


matumizi mbalimbali, na utengenezaji wake siyo
mgumu zao kuu la mshumaa nia Paraffine Wax.
Yapo mahitaji makuu katika utengenezaji wake nayo ni haya:

Mahitaji:1Paraffin Wax
2.Utambi
3.Mould (Umbo)
4. Stearine au mixture
5.Rangi
6.Jiko la mafuta ya taa au mkaa.
7.Sufuria.
8. Boric acid.

MAELEZO YA MUHIMU JUU YA MAHITAJI YETU:

1. Paraffin Wax :
Hii inatokana na nta na sega ya nyuki iliyo
changanywa na mafuta ya taa. Ina rangi nyeupe na
katika utengenezaji wa mishumaa ina ubora kuliko bee
wax.

Bee Wax:
Inatokana na masega ya nyuki yaliyo changanywa na
mafuta ya petroli na diesel na rangi yake ni ya njano.

~ 50 ~
STEARINE
Hii dawa maalumu inayo fanya mishumaa iungane ama
ishikamane vizuri na kuwa imara zadi

Mould (Umbo) . Mfano wa umbo linalo weza kutumika


kutengeneza mishumaa. Hata hivyo, unaweza kutengeneza
umbo lolote kwa kadri unavyo taka " shape " ya
mishumaa yako iwe. Yako maumbo mbali mbali ambayo
unaweza kutumia katika utengenezaji wa mishumaa yako
mfano.

~ 51 ~
BORIC ACID:

Hii ni maalumu kwa ajili ya kuufanya utambi usiishe


mapema na uwake bila kutoa moshi.

4. RANGI:

Rangi nzuri zinazo tumika katika utengenezaji mishumaa


ni rangi maalumu (siyo rangiza chakula) na nyingi huwa
ni za maji.Kuna rangi yeupe,nyekundu, blue, njano nk
unawezakutumiarangi yeyete.

JINSI YA KUTENGENEZA:

Hatua 01
 Andaa maumbo (mould) ya mshumaa kwa jinsi
upendavyo kwa ubunifu unaouhitaji

Hatu,02,kuandaa,Utambi
Chukua Boric Acid vijiko 5 vya chakula,changanya na maji
vijiko 4 vya chakula,Koroga kwa mdaa wa dakika 5,na kisha
tumbukiza utambi wako ukae kwa mdaa wa dakika 5,Anika
ukauke.Sababu ya kufanya hivi ni kutengeneza UTAMBI
wako usiishe haraka na usitoe Moshi,na ndio kazi ya Boric
Acid.

Hatua 03
Ukiwa umeshaandaa maumbo yako ya mshumaa (mould)
chukua utambiwako weka katikati ya chombo chako kwa
kushikiza na ute wa mshumaa,funga utambi wako juu ya
chombo kwa kijiti hii itakusaidia utambi wako usikae
pembeni.

Hatua,04
Washa jiko lako na,weka sufuria jikoni chukua Paraffin wax
kilo 1,sterin vijko 4, rangi na ikifuatiwa Perfume kijiko
1(rangi na perfume kama ukipenda)wakati mchanganyiko
~ 52 ~
wako unayeyuka koroga taratibu kuhakikisha mchanganyiko
wako umechanganyika vizuri,epua na anza kumimina
mchanganyiko wako kwenye maumbo yako,weka sehemu
yenye kivuli na baada ya kuwa mchanganyiko wako
umeganda,ondoa mshumaa taratibu kutoka kwenye maumbo
yake.Hivyo mshumaa wako utakuwa tayari kwa kutumia na
tayari kwa kwenda Sokoni.SIMPRONELA ;hii ni perfume na
pia ni dawa ya kuua mbu,waweza kuweka kwenye
mchanganyiko wako wa mshumaa ili kuboresha bidhaa yako
na kuwavutia watumiaji/wateja wengi.

UTENGENEZAJI WA SHAPOOO:
Ni sabuni maalumu kwa ajili ya kuonyeshea au
kusafishia nywele, kwa asilimia kubwa wadada, mabinti
na wakina mama ndio watumiaji sana wa bidhaa hii. Pia
hata wakaka na wababa ambao wanapenda nywele zao
kuwa safi nanadhifu.
Jinsi ya kutengeneza shapoo kuanzia 10lita

Mahitaji

 Maji
 Sulphonic acid lita 1
 Slesi 1kg
 Chumvi ya mawe 2kg au sodium sulphate
 Glycerine 1 4 kilo
 Formaline 1 4 lita
 Rangi 1 kijiko cha chai
 Perfume 1kijiko cha chakula
 Maji lita 10

Jinsi ya kutengeneza
Hatua 1
 Chukua maji 10 lita
 Weka slesi
 Chumvi au Naso4 (sodium sulphate) 2kg
~ 53 ~
Hatua 2

 Koroga hadi iwe nzito


 Maji yawe katika ndoo, beseni au chocho kipana
chenye ujazo unohitaji na chenye uwezo kuruhusu
kukoroga mchanganyiko.

Hatua 3

Weka

 Glycerine 1 4kilo
 Formalin 1 4 lita
 Perfume 1kijiko cha chai

Hatua 5

Koroga kwa daki 10 na kasha shapoo yako itakuwa tayarii.

 Sulphonic acid (usiweke


Maji kwenye sulphonic
Bali weka sulphonic
Kwenye maji.
Chukua
 maji 10 lita
 Weka slesi
 Chumvi au Na2So4
(sodium sulphate) 2kg
 Koroga hadi iwe nzito
 Glycerine 1 4kilo
 Formalin 1 4 lita
 Perfume 1kijiko cha chai

~ 54 ~
******

~ 55 ~
******

*SURA YA 05*

JINSI KUTENGENEZA UBUYU WA


ZANZIBAR (2kg)
Namna ya kutengeneza ubuyu wa Zanzibar usio zidi 2kg

Mahitaji

 Ubuyu 2kg
 Maji vikombe 2 vya chai 200ml
 Rangi ya chakula vijio 2 vya chakula
 Sukari 2kg
 Radha ya chakula/ vanilla
 Pili pili manga
 Iriki

Jinsi ya kutayarisha

Hatua 1

Chemsha maji yako hadi ya chemke

Hatua 2

Chukua sufuria nyingine na upime maji yakovikombe 2


na nusu/robo

Hatua 3

 Chukua sukari 2kg weka kwenye maji uliyopima


~ 56 ~
 Hakikisha sukari imeiva na kuyeyuka yote
 Acha viendele kuchemka kwa mda huku
ukikoroga kwa mda dk5
 Weka pili pili manga 21 4 vijko vya chakula
 Iriki
 Koroga mchanganyiko wako
 Weka rangi

Hatua 4

Chukua radha ya chakula /vanilla 2vijiko vya chakula na


kisha koroga kwa mda kidogo

Hatua 5

 Ukiwa tayari umeshachambua ubuyu wako


chukua mchanganyiko wako mimina kwenye
ubuyu wako taratibu huku unakoroga.
 Koroga hadi uchanganyikane vizuri

Hatua ya 6

Na mwisho uwache ubuyu wako upoe na kisha uanze kuifadhi


kwenye vyombo maaluma utavyopendelea

JINSI YA KUTENGENEZA KARANGA ZA MAYAI


Mahitaji:

 Karanga kg 1
 Sukari 1 4 robo
 Mayai 3
 Mafuta ya kupikia
 Chumvi 1 kijiko cha chakula.

~ 57 ~
Jinsi ya kutengeneza
Hatua 01

Andaa sufuria yako kavu, chukua sukari yako robo kilo


weka kwenye sufuruia.

Hatua 02

 Chukua chumvi vijiko 1 vya chakula changanya


kwenye sufurua wenye sukari.
 Vunja mayai yako 3 na kisha changanya
mchanganyiko wako hadi uwe kama uji.

Hatua 04

Chukua karanga zako changanya pamoja na mkorogo


wako hadi mchanganyiko uchanganyikane pamoja

Hatua 05

 Bandika mafuta yako acha ya chemke


 Chukua karangazako weka kwenye mafuta
koroga zisishikamane.
 Ipua karanga zako ukiona zimebadika rangi.
 Ziache mahali pasafi zipoe na kuchuja
mafuta.
 Na mwisho karanga zako zitakuwa za
kupakiwa NA KWENDA sokoni.

~ 58 ~
******

~ 59 ~
*SURA YA 06*

MPANGO BIASHARA NA UJASIRIMALI


(BUSSNES PLANNING)

H akuna kitu ambacho ni muhimu kama hiki, huwezi


kufanikiwa katika jambo lolote liwe ambalo unahitaji
kufanikiwa, usipokuwa na malengo na mipambo
mathubuti au mikakati ambayo itakuongoza katika namna ya
kukuwezesha kufanikisha kila kitu ambacho unataka
kufankiwa nacho. Kila unaemwona leo sio kwamba
alikurupuka na kujikuta tu ameanza biashara ambayo
anafanya, hapana ayo uyaonayo ni matokeo yake ya malengo
na mipango ambayo alijiwekea awali kabla ya kuanza
mchakato wa utekelezaji wake. Wengi ambao wananzisha
biashara na kujikuta wanaishia njiani, na shughuli zao kufa
kabisa sababu ni nini hasa?

 Kutokuwa na malengo na mipango kabla ya


kuanzisha chochote,
 Kukatisha tama ( Kushindwa kusimamia malengo),
 Kukosa soko baada ya kuanzisha biashara (alianzisha
biashara kabla yakujua soko lake liko wapi,
anawauzia watu gani nk).
 Aliona fulani anafanya (kufanya kitu kwa kuiga).

MPANGO:

Kutoka kwenye “investor words searching” mpango maana


yake (The process of setting goals, developing strategies, and
outlining tasks and schedules to accomplish the goals). Ikiwa
Na maana “Mpango= nimchakato wa kuweka malengo,
kuendeleza mbinu na kuorodhesha mambo ya kufanya na
kuweka ratiba ya namna ya kutimizaji malengo”.

~ 60 ~
Mipangoni mchakato wa namna ya kutimiza malengo, kwa
kubuni na kubaini kanuni na njia mbalimbali ya namna ya ya
kuyafikiahayo malengo.

 Kuyaorodhesha,
 Kubuni kanuni,
 Kuweka ukomo wa kuyatimiza,
 Matarajio au matokeo,

Nini maana ya mpango biashara (business planning):

Wakati siku moja nimeketi kupitianakutafuta kujua jinsi ya


kuanda mpango biashara nilikutana na maana kutoka the
www. balancesmb.com (Suzan, Ward). Walieleza ya kuwa,
“A business plan is the document that summarizes the
operational and financial objectives of a business and
contains the detailed plans and budgets showing how the
object are to be realized.”

“MpangoBiashara,ni nyalaka ambayo urahisisha uendeshaji


na malengo ya fedha za biashara na pia inakuwa na taarifa za
mipango na bajeti (mgawanyo wa matumizi) kunyesha ni
namnaza gani lengo linaweza kutendeka.

Kwa nini uwe na mpango Biashara?

“Mtu hajengi kwanza ndipo akaketi chini na kuanza kutafuta


ramani ya nyumba aliyo jenga, ni vyema kuweka mpango
kabla ya mchakato wenyewe”..... Linus Siwiti

Nini maana yake? Ikitokea amejenga bili kutumia ramani


katika ujenzi, chunguza ubora na ufanisi wa jengo. Vile vile
na kwenye biashara. Kama unafanya tu biashara hila hukuwa
na mpango wowote uliokuongoza katika namna mbalimbali
za kukufanisha. Usishagae kwako ukiona matokeo ya biashara
yako, kuwa kama haya:

 Unafanya biashara lakini mapato ni madogo,


 Unafanya biashara lakini kila siku kwako hasara,
~ 61 ~
 Kuto kuona maendeleo katika biashara yako,
 Kila biashara unayo anzisha inakufa,

Habari njema ni kwamba ukiona mtu amesimama basi tambua


yakuwa kuna siri ambayo imemfanya asimame pasipo
kuanguka katika shughuli mbalimbali zauzalishaji mali. Kitu
kikubwa ambacho kitakusaidia leo ni kuwa na malengo na
mipango. Tuangaliye nini faida yake,

Faida kuu Tatu (3) ya kuwa na malengo na mipango


katika Biashara:

Kuishia kuwa mwongeaji sana kuliko vitendo unajitengenezea


mazingira mafanikio katika maneno kuliko vitendo. Kipimo
cha mafanikio nikuwa na malengo na mipango na kisha
kuiweka katika vitendo zaidi.

01 kukuonyesha wapi unataka kufika:

“Planning and goals its indictors on which ways want to


pass, cross and tell you what is destiny point to reach... Linus
Siwiti”

Ikiwa na maana ya uwa mipango na malengo ni viashilia njia


gani wataka kuvuka, kukatisha na kukuambia nini hatima ya
mwisho wako utafikia. Ukiwa na biashara, kampuni, nk, kitu
ambacho ulimwengu wa mafanikio wanataka kukiona kutoka
kwako ni.

 Nini malengo ya biashara yako?


 Kwanini ufanya hiyo biashara na sizingine?
 Unaifanya kwa manufaa yapi?

“Unaona nini ndani yako? Baada ya mwezi, mwaka na


miaka. Ukiwa na nyalaka ambayo umeandika maswali haya
niliyokuorodheshea. Itakusaidia ni wapi unatoka na wapi
unakwenda katika kila kitu chanya na manufaa ukifanyacho.
Usishangae miaka 10 umefanya biashara lakini kwako bado
hakuna hatua yeyote ya mabadiliko kutokana na kile
~ 62 ~
unachofanya. Nikuakishiye kwamba bado ujachelewa keti
chini anza kuweka upya mipango na malengo yako leo,
namna ya kuleta matokeo mapya ndani yako.

Muda mzuri wa kupanda mti ni miaka 20 iliyopita. Lakini


muda mwingine mzuri wa pili ni sasa.”

Chinese Proverb.

*nampenda sana Chinese proverb anatufundisha kitu


kikubwa sana katika maisha ya leo, tunalinganishaje
msemowake na upande wetu, muda zuri wa kuweka
malengo yetu ya mafanikio ni miaka kenda iliyopita
lakini mda mwingine ni sasa. Anza kuweka malengo,
mipango, na kwako yasiwe mapambo tu bali
yatekelezwe kilasiku.

02. Kukuweka kwenye mstari:

“Gari moshi hata siku moja haliwezi likatoka na


kutembelea katika barabara ya lami au yeyote, bali isipo
kuwa ni katika reli yake”. Nini na maanisha malengo na
mipango itakufanya usitoke nje ya kile ambacho
unapaswa kukifanya, ulichokipanga. Hii ni shule nzuri
kwa mwenye shauku ya kufanikiwa, ukiyazingatia
yatakupa nidhamu. Mashuleni walimu wanatumia
Andalio la somo (scheme of work) na mpango kazi
wakufundishia (lesson plan) kwanini? Ili iwasaidiye
wasije kutoka nje ya kile anacho paswa kufundisha.
Kwako pia itakusadia leo. Panga malengo yako ya siku,
wiki, mwezi, mwaka na miaka na tembea katika hayo.

Malengo + Mchakato= Matokeo makubwa

~ 63 ~
03. Kufanikiwa:

“Watu waliofanikiwa ni ambao wao asilimia 99% ya maisha


wanaishi ndani ya malengo” tofauti na mtu ambaye anaishi
mradi bora siku ziende, liwalo na liwe, maisha yenyewe
hayahaya, wa kufanikiwa nitakuwa miye, Mama nani mwenye
kashindwa biashara yake imekufa. Hizi ni baadhi ya kauli zao.
Yawatu ambao ni vipofu lakini watatembea. Kwa nini nawaita
vipofu kwa sababu ndani yao hawana mafaniki, na hawaoni
kama wanayo.

Mipango na malengo ukiyazingati na kuyafuta nayo


yatakufuata na utafanikiwa katika kila utakacho fanya, na
utakachokifanya.

NAMNA YA KUANDIKA MPANGO BIASHARA (BUSINESS


PLANI):

Kuna mambo ya muhimu au (dondoo) unazo takiwa


kuzingatia kabla huja ya kuandika mpango biashara wako,
yakupa uwe na umakini wa hali ya juu ili ikusaidie usiweze
kukosea au kusahau mahala popote. Mpango biashara
unaweza kuugawa katika sehemu mbili yani:

1. Utangulizi wa mpango biashara wako,


2. Kiini kikuu cha mpango biashara yako,
3. Hitimisho,

01 Utangulizi wa mpango biashara:

Mpango biashara lazima uwe na utangulizi, lengo lake kuonye


mhusika wa biashara, aina ya biashara.

~ 64 ~
Mfano:

(i)Jina:

Kipengele ambacho kinafafanua mhusika wa biashara ni nani


katika, kuandika mpango biashara jina ni kitu muhimu, ili
kuwa na uhalali na uhakika kwa kile utakachokifanya.

(ii)Aina ya Biashara:

Mahususi kwa ajili ya kuelezea au kubainisha ni biashara gani


inayofanyika au itakayo fanyika mfano Biashara ya Cafteria,
(uuzaji wa chakula na vinywaji baridi), Duka, Genge,
Sambusa nk.

02 Kiini kikuu cha mpango biashara:

Kina jumuhisha mambo yote yaliyobeba mpango biashara


wako mzima, inakuwa na vipengele vifuatavyo:

(iii) Historia ya biashara na maendeleo yake:

Kama tayari unaendelea na biashara hapa utaonyesha historia


kwa ufipi wapi ulipo anzia na sasa upo hatua gani
(maendeleo) kama huja anza biashara yeyote tafuta kujua kwa
kina historia ya hiyo biashara katika eneo uliyopo kabla ya
kuifanya.

(iv) Huduma au bidhaa:

Kipengele hiki unatakiwa kueleza au kufafanua bidhaa au


huduma ambazo vinavutia kutoka katika biashara yako, kwa
kuzingatia uzalishaji wako, soko. Hatua ya uboreshaji wa
huduma/ bidhaa pengine ukikutana na maoni ya changamoto
ya biashara yako, uzalishaji, vitendea kazi (wafanyakazi na
rasiliamali), Fedha (mtaji), mzungu wa fedha katika biashara
yakoulivyo au utakavyokuwa.

~ 65 ~
(v) Tathimini ya soko:

Utaelezea bidhaa/ huduma ambayo unazalisha au utazalisha


soko lake katika mahali ulipo likoje? Je mzunguko wa fedha
upo juu ya biashara hiyo, unao walenga kuwauzia
wanapatikana, yote haya yakupasa kuyafahamu na
kuyabainisha.

(vi) Ushindani:

Utaonyeka ni kwa namna gani bidhaa/huduma yako ina


ushindani zidi ya bidhaa/huduma zinazo zalishwa na watu
wengine mfano unaweza kubuni kufanya biashara ya aina
fulani ukajikuta takribani zaidi ya watu kadhaa nao wanafanya
ambacho unafanya wewe, hiki ndicho tunaita ushindani wa
biashara yako, Mfano unampango wa kufungua huduma ya
Stationary (kwa ajilia ya kutoa kopi na kuuza vitu
mbalimbali). Tuna inaita duka la kuuza vifaa vya mashuleni
na kopi. Mkajikuta eneo moja mpo zaidi ya wawili. Hapa
ndipo pakupima ushindani wa bidhaa/huduma yako.

(vii) Ufanyaji kazi:

Ni vyema ukajua utendaji kazi wako ulivyo, utakavyo kuwa,


ni muda gani utaifanya biashara hivyo onesha muda (masaa
utayo fungua na kufunga) kwa siku za kazi.

(viii) Usimamizi na utawala:

Ni nani ambaye atahusika na kusimamia biashara yako


(mradi) wewe mwenyewe, mtu uliyemwajili, binti au kijana
wako au aidha mtu yeyote yule unayemwanini? Sheria na
kanuni ulizojiwekea au utakazojiwekea, na kuwawekea.

(ix) Uwezo wa wafanyakazi:

Kama biashara inahusisha watenda kazi ambao umewapa


ajira, pengine una miliki kampununi, biashara ya hoteli,

~ 66 ~
mgahawa, cafeteria, au unampango wakumiliki ainisha namna
ambavyo utatumia mbinu kujua uwezo wa wafanyakazi wako.

(x) Matatizo na utatuzi:

Orodhesha namna ambavyo unaweza kukabiliana na


changamoto ambazo unakutananazo au utakazo kutananazo
katika biashara uitendayo (utakayoitenda pengine bado uja
anzisha).

03.Hitimisho:

Mwisho kabisa unaweza kuonyesha mipango mbadala


ambayo unatalajia kufanya, na plan B (Njia mbadala endapo
mambo yatakukwamia njiani nini utafanya). Utaweka sahihi
yako na msimamizi mkuu wa biashara yako.

NB: wakati mwingine siyo muhimu kila mtu ajue huu mpango
biashara wako, wanaweza wakafahamu watendakazi wako tu,
au mtu wakaribu yako zaidi na siwatu baki. Kwa nini kwa ajili
ya usalama wa wazolako.

~ 67 ~
Mfano wa Fomu ya mpango biashara (Business plani):

MPANGO BIASHARA (BUSINESS PLAN) 2018:

Jina............................................................................................................................

Aina ya biashara..........................................................................................................

Historia ya biashara na
maendeleo.......................................................................................................................
.........................................................................................................................................

Huduma/bidhaa.............................................................................................................
.........................................................................................................................................

Tathiini ya
soko.................................................................................................................................
.........................................................................................................................................

Ushindani........................................................................................................................

Ufanyajikazi.................................................................................................................

Usimamizi na utawala.................................................................................................

Uwezo wa wafanyakazi................................................................................................

Matatizo na utatuzi......................................................................................................

Hitimisho.......................................................................................................................

Sahihi ya Miliki na jina Sahihi ya Msimamizi mkuu na jina

.................................... .................................................

~ 68 ~
SURA YA 07

*HITIMISHO*
01 USHAURI KUTOKA KWA MWANDISHI:
* Hatu wezi kufanikiwa kwa lolote kasipo kuweka tegemeo
sehemu ambapo tunapata msaada katika mambo yote.
Mwenyezi Mungu ni tegemeo na kimbilio kwa kila mtu. Yeye
ndiye aliyeziumba mbingu na nchi na vitu vyote, Uhai, afya
yeye ndiye atujaliaye. Kama unaumwa unaweza kufanya kazi
ya kuzalisha Mali? Kwa hiyo tunaitaji afya na uzima na
Mungu ndiye mtoaji.

* Mungu ndiye mwasisi wa mafanikio, inua tegemeo lako


kwake, wanadamu wanamsada wa muda yeye anao msaada
wa milele, napenda kuna sehemu anasema:

“Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye


akupaye nguvu za kupata utajiri, ili alifanye imara agano lake
alilowapa baba zako, kama hivi leo”... Swahili Biblia offline
Kumb 8:18.

* Muombe mwenye Mungu dua, sala na maombezi kwa kile


unachotaka kukifanya, unachofanya, na utakachofanya
iliakuweze kukufanisha.

Katika safari ya mafanikio, kila mmoja ana namna yake


ambayo ufanya ili kuyafikia mafikio. Ukitaka kuwa
kamamwingine, ukitaka kufanya afanyavyo mwengine,
ukitaka kufanikiwa kama yule, utakuwa unachicheleweshea
binafsi kusonga mbele.

“Usiyatamani mafanikio yake bali tamani kujua namna alivyo


ya pata mafaniko yake”... Linus Siwiti

~ 69 ~
*Nampenda sana mtu aitwaye Maya Angelous anaoushauri
mzuri kwa ajili yako wewe ambaye unatamani kuyasogeza
maisha yako kutoka hatua uliyopo hadi hatua nyingine yenye
mafanikio. Katika mafanikio Maya Angelous anachokiamini
ni ya kuwa.

“Success is liking yourself, liking what you do, and liking how
you do it” akiwa na maana ya kuwa – “Mafanikio ni
kujipenda wewe, kupenda unachokifanya tena kwa namna
unavyofanya”

Chakujifunzakutokakwa Maya Angelous:

01 Kundi kubwa la watu wafanyao yale ambayo siyo


machaguoyao, au wanachokipenda asilimia 100% watafanya
tu ilimradi mambo yaenda au waweze kujikimu. Mfano mtu
anafanya biashara ya kuchoma vitumbua, mandazi, nk kama
atakuwa anafanya tu hila siyo kama ni kitu ambacho
anakipenda, hawezi kufanikiwa.

02 Ukikifanya kitu ambacho unakipenda, na kuzidi


kuelendelea kukifanya utafanikiwa nacho katika hicho.
Nasiyo kukifanya tu bali kujitoa, kujituma, na kukiwekea
bidii ya hali ya juu.

* Mshauri mwingine niColin Powell ambaye naye amelezea


kitu cha muhimu sana kama wewe unashauku na kiu ya
kufanikiwa katika kila unachofanya, Bishara, ujasiriliamali
mdogo mdogo, shuleni nk. Ameleze ya kuwa:

“Hakuna siri ya mafanikio, ni matokeo ya maandalizi,


kufanya kazi kwa bidii, na kujifunza kutokana na makosa”

Kwa hiyo mafanikio siyo kitu cha muujiza bali ni mchakato


(Sucess is not something that is miracle, but its process)

 Maandalizi yako,
 Kufanya kazi kwako kwa bidii,
 Kujifunza kutokana na makosa.

~ 70 ~
Mambo haya matatu kwa wewe unayetaka kufanikiwa ya
nukuu (ya andike) yatakusaidia mbele ya safari yako.

* Usiwe mtu wa kutafuta visingizio, ya kwamba umeshindwa


kwa sababu ya kitu fulani, mtaji, ukufanya kwasababu hali
ngumu, maisha magumu serikali nayo haieleweki, chanzo ni
wazazi, marafiki, nk

*Kutoka kwaJim Rohn, ambaye alikuwa Mmarekani na


mjasiriamali, mwandishi na mnenaji mwamasishaji. Siku
moja nilikuwa nikisoma habari zake alinivutia na kunitia
moyo katika swala zima la mafanikio kupitia ujasiriamali,

“Kama unataka kufanya kitu, utatafuta njia. Kama hutafanya


hivyo, utatafuta kisingizio”

Unalaumu hali ngumu, mambo ayaendi, je wewe umetumia


njia gani kuyatatu, kuyakabili?

****************

~ 71 ~
MAANA YA MANENO YALIYOTUMIKA:
Yapo maneno na chemikali ambazo kiuhalisia yakupasa
uzijue pia kwa undani wake kidogo maana nawakati
mwingine matumizi yake msomaji ili ikurahisishie katika
ujifunzaji na kujifunza karibia kila kitu kina maana yake.
Caustic soda:Kaustiki soda, ni kemikali poda inauwezo wa
kuchangayika kwenye maji na kutengeneza mchanganyiko
kamili (dissolving substance, it soluble in water). Utumika
kutengenezea sabuni ya mche (kipande) kazi yake,ni chanzo
cha kuwezesha povu kutokea, kuondoa uchafu, kuunganisha
maji + mafuta kuwa kitu kimoja. Caustic Soda ndio chanzo
kikuu kupata sabuni ya mche au kipande.
Cd E:Kirefu chake ni coconut die emide, (imetengeneza na
zao kubwa la nazi. Kazi yake ni kulainisha mikono utumiapo
sabuni, pia isichumbue mikono. Haina tofauti na matumizi ya
glycerini,

Glycerine:Kimiminika kisichokuwa na kemikali kabisa, kazi


yape inapo tumiwe kwenye utengenezaji wa sabuni kusaidia
mtumiaji anapotumia isiweze kumsababishia kuchubuka
mikono, (kilainishi).

Malengo:mawazo ambayo ubainishwa katika nyalaka au la!


Namna mtu ambayo utamani kufanikiwa katika hayo, baada
ya mdafulani. Mfano kufungua duka kubwa la uzaji wa vitu
(supermarket) baada ya miaka miwili.( huu ni mfano moja
wapo wa malengo),
Mipango:ni mchakato wa namna ya kutimiza malengo,
hatuakwa hatua.
Formalini:Ni chemikali ambayo utunza vitu kwa mda mrefu
visinuke, kuchacha na kuaribika mapema, utumiwa katika
sabuni ilikufanya sabuni ikae muda mrefu.

Nasa: malighafi mahususi pia kwenye sabuni ya unga kazi


yake ni kuipanga sabuni na kuongezea uzito.

Perfume:Marashi, kazi yake inafahamika, kuleta harufu


nzuri, utumiwa katika utengenezaji wa sabuni ili sabuni iwe
~ 72 ~
na manukato ya kuvutia na kupendeza Mfano Rose,
kasalacka, pine Perfume nk

Slesi:Ni aina ya malighafi ambayo ipo kama mafuta fulani


mazito sana maeupe, kazi yake katika sabuni ni kuleta povu,
kug’arisha na kuondoa uchafu sehemu yenye uchafu.

Simpronela;hii ni perfume(marashi) pia ni dawa ya mbu.


Utumika mara nyingikatika utengenezaji wa mishumaa ya
dawa ya Mbu.

Sodium hydroxide: Chemikali kimiminika (inaunguza sana)


(NaOH) ni hatari sana, hushambulia ngozi, katika u
kutengenezea sabuni za urembo (Cream soap or loation)

Sodium peroxide: chemikali kwa ajili ya kuondoa rangi ya


mafuta mfano, mise nyonyo na mawese.

Soda ash:Ni kemikali ambayo ipokwenye mfumo wa unga


unga mweupe, kazi yake katika sabuni ni kuongeza ujazo wa
sabuni, mara nyingi utumika kwenye sabuni ya unga.

Sodium silicate:ni kemikali kwa ajili ya kuondoa muwasho


wa caustic soda.
Sodium metasilicate: Ni kemikali ambayo kiu halisia iko
tofauti kabisa na hiyo hapo juu. Hii kazi yake ni kusaidia
sabuni uliyotengeneza iweze kukauka kwa haraka kabisa bila
hata kuianika,

Sulphonic acid:Salphonik aside, ndiyo sabuni yenyewe kwa


ajili ya kutoa povu, mara sote upendelea kutumika
kutengenezea sabuni ya maji naUnga.

Uthubutu:kujaribu kufanya au kutenda pasipo kujali hali.

Vipaumbele:Ni kuyapa mbambo yalio muhimu nafsi ya


kwanza kuliko mengine.

~ 73 ~
Optic bright: Ni chemikali ambayo ipo katika hali ya chenga
chenga nyeupe, blue na wakati wingine nyekundu kazi yake
nikuleta nakshi na mwonekano mzuri katika sabuni ya unga.

~ 74 ~
Rejea mbalimbali:
Dr. Didas Lunyungu, (2012).MJASIRIAMALI KWANZA.
Mbagala Dr Live, Jijini Dar es salaam. Tanzania

Elisha Chuma (February 16, 2014). Jinsi ya kutengeneza


mpangobiashara (businessplan).Elishachua.blog spot.com

www. balancesmb.com (Suzan, Ward). Nini maana ya


mpango biashara (business plan),

Rafiki elimu faoundation, (Nov 11, 2012). Utengenezaji


wasabuni aina zote. rafikielimu.blogspot.com,

Sanga, Amina (2017). Nguvu ya Uthubutu. Grecious printing


solution. Dar es Salaam.Tanzania,

Swahili Biblia offline Kumbubu la Torati 8:18,

*Vitabu mbalimbali vinavyo husu Ujasiriamali.

~ 75 ~
VITABU VINGINE AMBAVYO
AMEANDIKA MWANDISHI:

1. Ijue njia iliyo sahihi (wapi unakwenda


naunataka kufika).
2. Jikomboe kichumi na ujasiriliamali,
3. nguvu iliyoo ndani ya jina asili yake na
maanayake, kwa nini uitwe ilo jina, (kipo
kinakuja kutoka)

Mawasiliano:
Email: linussiwiti12@gmail.com,

Phone: +255652303709/ +255766466209

Location: Tabora Tanzania East Africa

Facebook:linussiwiti,

*Tukutane ukurasa mpya wa


mafanikio*

~ 76 ~

You might also like