Tangazo La Ufadhili 2019

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TANGAZO KWA UMMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto


anawatangazia watumishi wote waliopata udahili wa kusoma masomo ya Shahada ya
Uzamili (Masters Degree) katika fani za Afya kwa mwaka 2019/2020, kwamba Wizara
inapokea maombi ya Ufadhili kwa mwaka 2019/2020. Maombi haya yatawasilishwa kwa
njia ya kielektroniki kwa kutumia link iliyotolewa kwenye tangazo hili. Maombi
yatakayofanyiwa kazi ni yale yatakayowasilishwa kwa njia ya mfumo huu tu, hivyo
waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya tangazo hili wanapaswa kufuata utaratibu
huu.

Ufadhili huu ni kwa ajili ya kulipiwa ada ya mafunzo (Tuition fee), pamoja na posho ya
utafiti pindi mwanafunzi anapokuwa kwenye kipindi cha kufanya utafiti kama sehemu ya
mafunzo yake (Dissertation Allowance). Malipo ya posho ya utafiti yatazingatia viwango
vilivyopitishwa na Wizara.

Vigezo vitakavyotumika kuchagua watakaowasilisha maombi yao ni hivi vifuatavyo :

1. Kuwasilishwa kwa maombi rasmi ya ufadhili kwa njia ya mfumo (Post-graduate


Sponsorship Online Application System)

2. Mwombaji awe Raia wa Tanzania.

3. Awe amedahiliwa Chuoni kuanza masomo kwa mwaka wa kwanza 2019/2020

4. Mwombaji awe amefanya kazi kwa muda usiopungua miaka miwili baada ya kuajiriwa
serikalini.

5. Kipaumbele kitatolewa kwa:


a. Watumishi wa Serikali waliomo kwenye sekta ya Afya wanaofanya kazi katika
vituo vilivyoko Wilayani/Mikoanii pamoja na Hospitali za Rufaa za Mikoa
ambao baada ya mafunzo watarudi kuendelea kufanya kazi katika vituo vyao
vya awali, au watapangiwa vituo vya kazi sehemu nyingine yeyote nchini yenye
uhitaji.
b. Waombaji waliodahiliwa katika fani ambazo ni za msingi katika utoaji wa
huduma za rufaa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa. Nyanja hizo ni
Anaesthesiology, Surgery, Obstetrics and Gynaecology, Orthopaedics
Surgery, Emergency Medicine, Paediatrics, Internal Medicine,
Neurosurgery,Radiology, Oncology,Opthalmology, ENT,Psychiatry,
Microbiology, Critical Care in Nursing na Midwifery and Womens Health,
Clinical Pharmacy, Pharmaceutical Management, Epidemiology and
Lab.Management.
c. Waombaji waliodahiliwa katika nyanja za Ubingwa wa Juu (Super-specialities)
zenye umuhimu mkubwa katika Hospitali Maalumu, Kanda na Kitaifa (kama
Cardiology, Nephrology,Haematology,Endocrinology, Neurology, Pulmology,
Gastroentorology, Radiography) ili kujenga uwezo wa ndani ya nchi katika
jitihada za kupunguza wagonjwa wa rufaa wanaotibiwa nje ya nchi.

6. Aidha, mwombaji atatakiwa awe ameambatisha nyaraka zifuatazo wakati wa kufanya


maombi:
a. Barua ya ruhusa ya masomo kutoka kwa mwajiri wake
b. Barua ya udahili kutoka chuoni
c. Cheti cha taaluma
d. Cheti cha kuzaliwa

Maombi yote yawasilishwe kwa kutumia ‘link’ ifuatayo:


esponsorship.moh.go.tz

Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 16/11/2019.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mji wa Serikali Mtumba,
Barabara ya Afya,
S. L. P. 743
40478 DODOMA
18/10/2019

You might also like