Chagua herufi ya jibu sahihi katika sentensi zifuatazo;
1. Samaki wa maji chumvi wana__________ nzuri (mabaka, ladha, chumvi, rangi)
2. Vitabu __________ juu ya meza (viko, vimo, zipo, vimekaa) 3. Pili alimuua mbwa wake kwa____________ (bomu, risasi,, bunduki) 4. Hawa watu ni chanda na pete______________ (marafiki, majirani, wanaishi karibu karibu) 5. Ni vizuri kufuata___________- ya shule (haki, ratiba, nidhamu, kazi) 6. Rehema ni hodari wa_____________ mashairi (kughairi, kughani, kukubali, kuchapa) 7. Hapo ___________ za kale binadamu alifanana na Sokwe (mwanzoni, zamani, mwishoni, katikati) 8. Mchwa huishi kwa kuzaliana kwenye____________ (mzinga, zizi, kichuguu, kichukuu) 9. Huyu ni___________ wa hapa kijijini kwetu (mkungu, mkunga, mkonge, mkenge) 10. Jose alipigwa_________ kuonekana eneo la shule kwa sababu ya wizi (tetemeko, marufuku, nadra) 11. Jua huchomoza asubuhi upande wa__________ (chini, juu, magharibi, mashariki) 12. Wagonjwa hulazwa_________ (chumbani, wodini, chumbani, nyumbani) 13. Baba___________ mama ni wazazi wangu (na, ni, wa, ya) 14. Ili tufaulu mitihani yetu____________ kusoma kwa bidii (ni budi, hatuna budi, si lazima, tuwahi) 15. Aghalabu maana yake ni____________ (maranyingi, mara moja, nadra, marachache) 16. Shangazi aliweka fedha na funguo_________ ndani ya pochi (yake, zake, wake, lake) 17. _______ ya ng’ombe ipo mgongoni (pembe, nundu, kwato, kinga) 18. ___________ mvua zikanyesha na watu wakapanda mbegu za kila aina (fukuto, hatimaye, maarufu) 19. Ali___________ pesa katika kiganja cha mkono na kukimbia hadi dukani (adhimisha, hamaki, fumbata, tabasamu, shuhudia) 20. _________ ya shule yetu ni shati jeupe na siketi bluu (sare, vazi, rangi) 21. Kila siku nina amka____________ ili kufanya usafi ( alasiri, alfajiri, jioni, adhuhuri) 22. Sakafu ya nyumba imetengenezwa kwa____________ (saruji, sarufi, majivu, theluji) 23. Kabla ya kuanza biashara ni lazima uwe na______ (faida, fidia, kiasi, mtaji) 24. Usifanye________ kwenye biashara (zaidi, kero, mzaha, salio) 25. Wakatafakari maana yake ni___________________ (wakasahau, wakakariri, wakafikiri) 26. Pigia msitari neon lililo tofauti na mengine kati ya haya yafuatayo 27. Nyumba, kibanda, ghorofa, mti 28. Maji, maziwa, soda, ugali 29. Meli, jahazi, mtumbwi, mlima
Jaza nafasi zilizoachwa kwa ajili yako 70. Keti maana yake ni_______________ 71. Mtu ambaye hasikii huitwa ___________________ 72. Mtu ambaye hawezi kutembea huitwa___________________ 73. Mtu asiye na pua huitwa_____________________ 74. Mtu asiyeona huitwa__________________ 75. Mtu asiyeongea huitwa_______________________ 76. Mtu asiye na meno huitwa_______________ 77. Mtu anayeendesha treni huitwa_____________ 78. Waislamu daima_____________ kwenye msikiti. 79. Nyumba ya nyuki huitwa__________________ 80. Mtoto wa ndege huitwa__________________ wakati huo motto wa ng’ombe ni____________ 81. Mtu anayefanya kazi ya kufua na kupiga pasi nguo huitwa _________________ 82. Mtu anayefanya kazi ya kusafisha vyoo huitwa___________ 83. Mtu anayejenga nyumba kwa kutumia tofali na mawe huitwa__________ 84. Mtu anayetengeneza vitu vya thamani kama shanga na heleni huitwa____________
Kamilisha methali, jibu vitendawili au toa maana ya nahau
85. Haraka haraka _____________________
86. _____________________- mati nyuma 87. Usiache mbachao __________________________ 88. Mvumilivu__________________________ 89. Kila mtu humwabudu apitapo _____________________ 90. Fikiri kabla ya__________________ 91. Kila niendapo hunifuata _________________ 92. Haba na haba____________________ 93. Kula chumvi nyingi__________________________ 94. Chapa mguu_____________________________ 95. Nyumba yangu ina mlango juu ___________________ 96. Pruu! Mpaka Maka ___________________ 97. Hesabu yake haina faida_____________ 98. Bwana afya wa porini _________________ 99. Pita huko nipite huku tuonane katikati _________________ 100. Mwamvuli upo msituni __________________ 101. Mama hachoki kunibeba_________________ Jaza sehemu zilizoachwa wazi kwa kutumia maneno; kabla ya, baada ya, kwa ajili ya, bila shaka, huna budi, mara kwa mara 102. Wingu jeusi limetanda angani kote____________ mvua itanyesha sasa hivi 103. Ukitaka kufaulu ____________ kusoma kwa bidii 104. _____________ kumsubiri muda mrefu, hatimaye mgeni aliwasili 105. ______________ kuanza kujibu swali lolote lile ni vizuri kulisoma tena na tena 106. Anafaulu kwa sababu hupitia masomo yake_______________ 107. Wageni wote tayari wamewasili_____________ kikao Chagua nahau zifuatazo kukamilisha maana katika sentensi zinazofuata
Usingizi ulipaa, fedha lukuki, walikaa chonjo, waliangua kicheko, walipigwa butwaa, walitega sikio, kufuja mali 108. Watu wote_______________ waliposikia Juma ameuawa na majambazi 109. Wanafunzi wote___________________ walipomwona mwalimu wao anacheza dansi. 110. Alikuwa na________ lakini hakuwa na mippango mizuri ya matumizi. 111. Baada ya kuota ndoto ya kutisha ____________ usiku wote. 112. Wanakijiji ____________ kumsikiliza mgombea wa ubunge wake alipofanya kampeni yake. Andika katika wakati mbalimbali kama ulivyo elekezwa 113. Anacheza vizuri (uliopita) 114. Watakula wali wa Kyela (uliopo timilifu) 115. Ameangua vibaya sana (uliopita) 116. Watoto wamefaulu mitihani yao vizuri (ujao) 117. Kila mmoja aliandika barua ya kujieleza (uliopo) 118. Wanafunzi watacheza uwanjani (hali ya mazoea) Weka alama sahihi za uandishi katika sentensi zifuatazo 119. Kwanini umechelewa kufika shule 120. mwalimu amemwambia serina kuwa aondoke 121. mama aliniagiza kuwa ninunue vitu vifuatavyo kisu kijiko sahani kikombe 122. Lo wameadhibiwa tena 123. Wanafunzi wote walifika jumatatu na alhamisi 124. Rais wa kenya anaitwa uhuru Kenyatta 125. Dada alisema nina hasira sana na wewe Tumia herufi zifuatazo kuunda maneno ya Kiswahili 126. Luemi- 127. Mulimwa- 128. Sehul- 129. Lumii- 130. Mobak- 131. Suuki- 132. Ragi- 133. Sadara- 134. Dogoro- 135. Komno-