Utaratibu Wa Wajasiriamali Wadogo Na Wa Kati (Smes) Kuwezeshwa Kupata Alama Ya UBORA YA TBS' - Tanzania Bureau of Standards (TBS)

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

UTARATIBU WA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI (SM... about:reader?url=http://www.tbs.go.tz/index.php/services/category/utar...

tbs.go.tz

UTARATIBU WA WAJASIRIAMALI
WADOGO NA WA KATI (SMEs)
KUWEZESHWA KUPATA ALAMA YA
UBORA YA ‘tbs’ — Tanzania Bureau
of Standards (TBS)
3-4 minutes

1.0 UTANGULIZI

Serikali hutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia


wajasiriamali wadogo na wa kati pale wanapoomba bidhaa zao
wanazozizalisha wenyewe zithibitishwe ubora. Katika utaratibu
huu, wapo wajasiriamali ambao husamehewa kulipa ada yoyote
kwa sababu ya mitaji yao kuwa midogo.

Ili kupata msamaha huu, vigezo vifuatavyo huzingatiwa:

• Mjasiriamali hutakiwa kuwa na barua ya utambulisho kutoka


ofisi ya SIDO iliyo karibu. Ni vema kuhakikisha kuwa barua
inafafanua vizuri na kwa kina shughuli zinazofanywa.

• Kwa wale wanaozalisha vyakula huhitajika kuwa na taarifa fupi


kutoka Idara ya Afya iliyo karibu na mahali pa uzalishaji au cheti
cha TFDA.

• Mjasiriamali hupaswa kuwa na leseni ya biashara.

• Wajasiriamali waliokwishapata leseni ya kutumia alama ya


ubora hupaswa kutunza rekodi za uzalishaji na mauzo ambazo
watatakiwa kuzionesha kwa wakaguzi wa TBS pindi

1 of 3 25/03/2020, 00:15
UTARATIBU WA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI (SM... about:reader?url=http://www.tbs.go.tz/index.php/services/category/utar...

zinapohitajika.

2.0 HATUA ZA KUPATA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’

2.1 HATUA YA KWANZA – MAOMBI

• Maombi ya uthibitishaji wa ubora wa bidhaa hufanywa na


mwombaji kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS kwa
maandishi.

• Majibu hutolewa yakielezea taratibu na gharama zote.

• Majibu huambatana na fomu maalum ambayo mwombaji


huijaza na kuirudisha TBS ikiwa na viambatanisho vifuatavyo:

? Mtiririko wa uzalishaji wa bidhaa husika;


? Mfumo wa uongozi ukionyesha kitengo cha udhibiti ubora;
? Orodha ya malighafi anazotumia na mahali zinakotoka kwa kila
bidhaa;
? Ramani inayoelekeza jinsi ya kufika kiwandani kwako;

Baada ya hapo tarehe ya kufanya ukaguzi wa awali hupangwa.

2.2 HATUA YA PILI – UKAGUZI WA AWALI

• Ukaguzi wa awali hufanywa na wakaguzi wa TBS wakati


kiwanda kikiwa katika uzalishaji.

• Sampuli huchukuliwa na kupimwa ili kuona kama zinakidhi


matakwa ya kiwango husika.

• Mkaguzi huandaa taarifa kuhusu hali halisi ya kiwanda na


mambo yanayostahili kurekebishwa.

2.3 HATUA YA TATU – UPIMAJI

• Sampuli zilizochukuliwa hupimwa katika maabara za TBS kwa


kufuata kiwango husika.

• Baada ya kazi ya upimaji kumalizika, ripoti ya maabara

2 of 3 25/03/2020, 00:15
UTARATIBU WA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI (SM... about:reader?url=http://www.tbs.go.tz/index.php/services/category/utar...

hutolewa kwa mwombaji.

2.4 HATUA YA NNE – UTOAJI WA LESENI

• Maamuzi kuhusu kutoa au kutotoa leseni ya kutumia alama ya


ubora hutegemea tu ripoti ya ukaguzi wa awali wa kiwanda
pamoja na ripoti ya maabara.

• Kimsingi ripoti zote mbili zinatakiwa kuonyesha kwamba


mazingira ya uzalishaji kiwandani, mfumo wa uzalishaji na bidhaa
iliyopimwa havina matatizo.

• Ikiwa sivyo basi mzalishaji hutakiwa kufanya marekebisho na


baadaye mkaguzi wa TBS hutumwa tena na kuleta sampuli
nyingine.

3.0 MUDA WA LESENI (VALIDITY OF LICENCE) YA ALAMA YA


UBORA YA ‘tbs’

Leseni ya kutumia alama ya ubora ya ‘tbs’ hudumu kwa mwaka


mmoja na huhuishwa (renewal) baada ya kuhakikisha kwamba
taratibu zilizokubalika (Scheme of Inspection and Test, SIT)
zinafuatwa.

3 of 3 25/03/2020, 00:15

You might also like