Professional Documents
Culture Documents
Somo La Kutengeneza Tambi Za Dengu
Somo La Kutengeneza Tambi Za Dengu
Somo La Kutengeneza Tambi Za Dengu
MAHITAJI
Unga wa dengu ½ kilo
Binzari nyembamba ½ kijiko cha mezani
Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai
Unga wa mchele ¼ kilo
Chumvi kiasi
Mafuta ya alizezi ½ lita
Baking powder
JINSI YA KUTENGENEZA
Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu kasha chukua nyunyuza baking powder na
baadae chumvi.
Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga
Changanya vizuri na kasha weka maji kidogo kidogo huku ukikanda hadi liwe donge gumu kama
unavyofanya kwenye maandazi.
Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika.Acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa
moja.
Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni hadi mafuta yapate moto kabisa.Kisha
chukuwa mashini ya kupikia tambi[spaghetti] na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku
ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yako yaliyo jikoni.
Weka kiasi kiasi huku ukikaanga.acha mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri.Ipua na
weka pembeni.
Weka kwenye sahani safi na kavu.tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Tafuta fingushio vizuri funga kasha peleka sokoni.
ANZA NA ULICHONACHO,ANZA SASA.