Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 19

SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.

P.O.Box 248, Songea


Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

MWONGOZO WA KILIMO CHA MAPAPAI


SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

KILIMO BORA CHA MIPAPAI

Utangulizi:
Mipapai ni moja ya miti ya matunda inayolimwa ulimwenguni kote na hapa
Tanzania, miti hiyo inalimwa karibu kila mahali. Mipapai au kwa jina la kitaalam
Carica papaya, ni miongoni mwa spishi 22 zinazokubalika katika jenasi ya Carica
na familia ya Caricaceae.
Asili ya mipapai ni katika maeneo ya tropiki huko Amerika, pengine kusini mwa
Mexico na nchi kadhaa za Amerika ya Kati. Kwa mara ya kwanza miti hii ililimwa
nchini Mexico karne kabla ya kuibuka kwa ustaarabu wa Mesoamerican.
songea businesss clinic inafahamu kwamba, tunda la papai lina sukari, Vitamini A
na C kwa wingi na huweza kuliwa kama tunda. Pia huweza kutengenezwa saladi,
jamu na kukamuliwa kupata juisi.
Utomvu wa papai bichi hutumika kulainisha nyama na kutengeneza dawa
mbalimbali.
Nchini Tanzania, wastani wa uzalishaji ni tani 2,582 tu kwa mwaka.
Hata hivyo, India na Brazil ndizo nchi zinazoongoza kwa uzalishajji wa mapapai
ulimwenguni, ambapo kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la
Chakula na Kilimo (FAO) za mwaka 2013, nchi hizo kwa pamoja zilizalisha 57%
ya tani milioni 12.4 zilizozalishwa mwaka huo.
Takwimu hizo, ambazo songea businesss clinic imeziona, zinaonyesha kwamba,
kwa mwaka 2013, India ilizalisha tani milioni 5.5, Brazil tani milioni 1.6,
Indonesia tani milioni 0.9, Nigeria tani milioni 0.8 na Mexico tani milioni 0.8.
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Zao hili ambalo llimepata umaarufu mkubwa duniani miongoni mwa mazao
yanayozalishwa katika nchi za tropiki kwa sasa linashika nafasi ya nne nyuma ya
migomba, machungwa na maembe.
Kidunia, uzalishaji umeongezeka kwa kasi katika miaka michache iliyopita, hasa
kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji nchini India. Mapapai yamekuwa
miongoni mwa mazao ya kilimo yanayosafirishwa nje ya nchi katika nchi
zinazoendelea, ambako mapato ya usafirishaji wa zao hilo yameongeza ustawi wa
maelfu ya watu, hususan katika nchi za barani Asia na Amerika ya Kati.

Mapapai yakiwa shambani


SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Mazingira:
Ingawa asili ya zao hili ni kusini mwa Mexico (hasa maeneo ya Chiapas na
Veracruz), Amerika ya Kati, na kaskazini mwa Bara la Amerika ya Kaskazini, kwa
sasa mipapai inazalishwa kwa wingi katika nchi za kitropiki duniani.
Songea business clinic inatambua kwamba, Papai ni moja ya matunda ambayo
huchukua muda mfupi hadi kufikia mavuno. Huchukua muda wa miezi 8-9 kufikia
mavuno Mipapai huhitaji joto la wastani kati ya nyzi 22 na 26 za Sentigredi na
mvua kiasi cha milimeta 1,000 na 1,800 kwa mwaka. Zao hili linastawi vizuri
kwenye udongo usiotuamisha maji kwani yakisimama kwa saa 48 tu mpapai
unaweza kufa, wenye rutuba ya kutosha kwani mipapai haina mzizi mrefu,
haihitaji udongo wenye kina kirefu na lazima udongo uwe na uchachu kati ya pH 6
na pH 7.
Upepo mkali huangusha mipapai, hivyo inashauriwa kupanda miti pembeni mwa
shamba la mipapai. Inashauriwa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka
shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena Spp) na
miembe pia inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi
mipapai kwa mita 10 mpaka 20 juu zaidi.
Kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama
hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii
huongeza ubora wa papai ikiwemo kutooza mapema sokoni.

Usipande mipapai mfululizo kwenye shamba moja kwa zaidi ya miaka mitano kwa
sababu hiyo inaweza kusababisha usugu wa magonjwa. Unahitaji kubadilisha
mazao japo kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa.
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya michungwa,


pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta, alizeti na mboga mboga
yanaweza kulimwa.
Kuna aina mbili za mbegu
 red royal F1
 MALAIKA F1
Megu hizi Uvumiliasana magonjwa na ukomaa kwa muda wa miezi 8 hadi
9 pia huvunwa kwa muda wa miaka 5mfululizo.

Aina za mipapai:
Kwa kawaida kwenye mipapai kuna mipapai ya jinsia tatu: midume, majike na
yenye jinsia zote (hermaphrodite) ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia
kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai mafupi sana. 
Papai dume hutoa poleni peke yake, siyo matunda. 
Papai jike linaweza kuzaa matunda madogo, yasiyolika ikiwa halikuchavushwa. 
 
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Mpapai wenye jinsia zote mbili unaweza kujichavusha wenyewe kwa sababu maua
yake yana stamens za kiume na mayai ya kike. Kwa kawaida bustani nyingi za
mapapai ya bishara zina miti yenye jinsia zote, yaani hermaphrodite. 
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

MAPAPAI YAKIWA SHAMBANI

songea business clinic inafahamu kwamba, kuna aina nyingi za mipapai lakini
zinazolimwa zaidi nchini Tanzania ni aina ya Solo, Hortus Gold na aina za
kienyeji.
Solo ni aina ya mipapai ambayo maua yake yana mbegu za kike na kiume katika
ua moja. Mapapai ya Solo yana umbo lililochongoka kidogo mfano wa yai au
kama tunda la peasi na nyama yake ni nyekundu. Matunda yake hukua hadi kufikia
uzito wa nusu kilo.

 Hortus Gold ni aina ambayo mbegu za kiume na kike zinapatikana katika maua
tofauti lakini katika mmea mmoja. Rangi ya nyama yake ni ya dhahabu na
matunda yake hukua hadi kufikia uzito wa kilo moja na nusu mpaka kilo mbili.
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Mapapai ya Solo ni matamu zaidi kuliko ya Hortus Gold na ndiyo yenye soko
kubwa.

Utayarishaji wa shamba:
Shamba litayarishwe mwezi mmoja kabla ya kupanda. Wakati wa kutayarisha
shamba punguza miti, ng’oa visiki na fyeka majani, halafu yakusanye pamoja na
yachome.
Chimba mashimo yenye ukubwa wa sentimeta 40 upana, urefu na kina. Nafasi kati
ya shimo na shimo iwe meta mbili au tatu na mstari na mstari iwe meta mbili na
nusu hadi tatu. Baada ya kuchimba mashimo jaza mbolea ya samadi au takataka
zilizooza vizuri (mata mahuluku) kiasi cha debe mbili kwa kila shimo.
Upandaji:
Mbegu za mipapai zinaweza kupandwa moja kwa moja shambani au kuoteshwa
kwanza kitaluni na baadaye miche kuhamishiwa na kupandikizwa shambani.
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Kama zitaoteshwa kitaluni zipande katika nafasi ya sentimeta mbili na nusu kutoka
shimo hadi shimo na sentimeta 10 kutoka mstari hadi mstari.
Mbegu za mipapai zinaweza kupandwa kwenye viriba vilivyojazwa mchanganyiko
wa udongo na mbole za asili. Kwenye kila pakiti weka mbegu 2 – 3.
Kwa kawaida, mbegu huota baada ya wiki mbili na miche huwa tayari
kupandikizwa shambani kuanzia wiki sita hadi nane ambapo wakati huo miche
huwa na urefu wa sentimeta 20-40. Kama udongo unatuamisha maji panda kwenye
matuta yenye urefu wa sentimeta 40 – 60.
yaliyokwishatayarishwa mapema. Mbegu nane zipandwe katika kila shimo maana
miche mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume.
Katika kuandaa mbegu, kusanya mbegu kutoka kwenye mapapai makubwa na
yaliyokomaa na kuiva, kausha mbegu vizuri kabla ya kupanda. Kama utapata
mbegu za kununua ni vizuri zaidi. Baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani
ya wiki moja.

Utunzaji wa shamba la mipapai:


Kupunguza miche
Baada ya mbegu kuota, miche ipunguzwe na kuacha miche minne katika kila
shimo. Maua yakishatoka mipapai isiyotakiwa. Baada ya miezi 3 – 5 tangu
kupandwa shambani mipapai itatoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana na
mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume, mipapai yenye jinsi zote inatakiwa
isizidi asilimia 10 – 20 na midume ibaki mmoja katika kila mijike 25. Kama
umepanda aina ya mipapai ambayo maua yake yana mbegu za kiume na kike,
ondoa mipapai yote ya kiume. Mimea yenye magonjwa pia inabidi ing’olewe.
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Urutubishaji wa udongo
Ili mimea iweze kukua haraka, inashauriwa kuweka mbolea za kukuzia kama vile
SA au Urea. Kiasi kinachotakiwa ni kilo 200 za SA au kilo 100 za Urea kwa hekta
moja. Mbolea za asili kama vile samadi na mbolea vunde ziwekwe kila mwaka
kiasi cha kilo debe moja hadi mbili kwenye kila mpapai ili kuongeza ukuaji na
uzazi. Mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama matandazo na h ii ni
muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.

PALIZI
Palizi katika shamba la mipapai ni muhimu hasa wakati wa mwanzo. Mipapai
inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa
magugu. Magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua chini sana
maana mizizi ya mipapai huwa juu juu. Njia nzuri ni kuweka matandazo kwenye
shamba lote ili kuzuia uotaji wa magugu.
Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini
ikiwa itabainika kuwa na magonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na
virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji na kipato chako.

 Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii


ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.
 Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale
yenye afya tu

 Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati
wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

 Mipapai ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya mazao bora
ondoa mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3) kwani
mpapai unapo kuwa mkubwa basi rutuba yote huishia kwenye mti wenyewe

Magonjwa na wadudu waharibifu:


a)  Magonjwa
Mipapai hushambuliwa zaidi na magonjwa ya ukungu na virusi.
Magonjwa ya ukungu

Magonjwa ya ukungu huababisha majani na matunda kuwa na uyoga mweupe na


madoa mesui ya mviringo. Mizizi huoza kutokana na athari za magonjwa hayo na
mmea hufa.
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Kuzuia
-         Kupanda mipapai katika sehemu isiyotuamisha maji
-         Kuweka shamba safi wakati wote
-         Kuepuka kujeruhi mizizi wakati wa kupalilia
-         Kubadlisha mazao
-         Kunyunyiza dawa za ukungu kama vile Dithane M 45.

Magonjwa ya virusi

Magonjwa ya virusi husababisha mmea kudumaa, majani kukunjamana na kilele


kuwa na kitita cha majani. Magonjwa hayo huenezwa na panzi na vijidudu aina ya
vidukari.
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Kuzuia
-         Kutumia dawa kama vile Sumithion au Killpest ili kuangamiza wadudu
wanaoeneza magonjwa hayo.

b)  Wadudu waharibifu


Wadudu wanaoshambulia zaidi zao hili la mipapai ni vidukari na minyoofundo.

Vidukari
Vidukari hivi hufyonza utomvu wa majani.

Dalili
Mmea hudumaa.
Kuzuia
Nyunyizia mojawapo ya dawa kati ya Sumithion au Dimethoate.

Minyoofundo
Minyoofundo hushambulia mizizi na kuifanye iwe na nundunundu.

Kuzuia
Kubadliha mazao. Baada ya kung’oa mipapai panda aina nyingine ya mazao
ambayo haishambiliwi na minyoofundo kama vile mahindi na mazao jamii ya
mikunde.

Wadudu na wanyama wengine waharibifu ni ndege na panya.


SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Uvunaji:
Mipapai huanza kuzaa katika kipindi cha miezi NANE had TISA
Mapapai kwa ajili ya matumizi ya nyumbani yavunwe wakati yanaanza kubadilika
rangi kutoka kijani kibichi na kuwa njano. Mapapai kwa ajili ya kusafirishwa
yachumwe yakiwa yamekomaa lakini bado yakiwa na rangi ya kijani.
Uvunaji wa mapapai ni wa kutumia mikono au kutumia vichumio maalum. Vuna
mapapai na vikonyo vyake ili kurahisisha ubebaji na kuzuia kuingia kwa vimelea
vya magonjwa. Weka mapapai kivulini baada ya kuvuna.
Mipapai iliyotunzwa vizuri inaweza kutoa tani 40 kwa hekta kwa mwaka kwa
mzao wa kwanza na tani 25 kwa hekta kwa mzao wa pili. Mavuno hupungua
katika mzao wa tatu na kuendelea.

WAKINAMAMA WAJASILIAMALI WAKILANGUA MAPAPAI


SHAMBANI
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

MCHANGANUO WA KIPATO CHA MAPAPAI KWA UFUPI

Vitu vya kuzingatia:


 Hekta 1 = Square meter 10,000
 Ekali 1 = Square meter 4000
 Hekta 1 = Ekali 2.5
GHARAMA ZA UZALISHAJI NA MAPATO GHARAMA YA HEKTA
MOJA:

S/NO HUDUMA @EKALI KIWANGO THAMANI


1 KUKODI SHAMBA 1 100,000
2 MBEGU 1 375 GRAMS 375,000
3 VIBARUA 1 300,000
4 MBOLEA 1 MIFUKO 2 140,000
5 MAJI 1 100,000
6 SAMADI 1 50,000
7 DAWA YA WADUDU 1 110,000
8 DAWA YA UKUNGU 1 40,000
9 KUVUNA 1 50,000
JUMLA 1,265,000

Mapato kwa ekari moja kwa kipindi cha miezi 8-9 JUMLA
Eka moja hutoa Mapapai sawa na 40,000x Bei 1000 40,000,000
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

KWA HESABU HIYO NI RAHISI KUTHIBITISHA KUWA MAPAPAI NI


MOJA YA ZAO PEKEE AMBALO LINA FAIDA KWA MKULIMA

FAIDA ZA KIAFYA ZA TUNDA LA PAPAI


Tunda la mpapai lina faida nyingi katika mwili wa binadamu ,pamoja hivyo
nipamoja na kuwa na uwezo wa:
1. Kutibu tatizo la shida la kusaga chakula tumboni
2. Kutibu udhaifu watumbo
3. Kutibu kikohoz kitokacho mapafuni
4. Hutmika kutibu kifua kikuu
MBEGU ZA MPAPAI

5. Tunda hili huleta afya nzuri ukila kila siku


6. Maziwa yatokanayo katika jani lake huponya vidonda
7. Husaida kutibu sehemu palipoungua ,moto mwilini
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

8. Kama hiyo aitoshi maziwa yatokanayo katika jani la mpapai hutmika


kuondoa kiungulia na ugonjwa wakoloni(njia ya haja kubwa ndani)
9. Pia yanasaidia kutofunga choo
10..Maganda ya tunda la mpapai yanasaidia kutibu tatizo la kuungua,vipele na
saratani ya ngozi
11..Mbegu zake zinatibu ini zikitafunwa 10-12 kwa siku tano

Mizizi ya mpapai

12..Majani yake yakaushie ndani yanatibu pumu,inapoanza kubana yachome


majani yaliyokaushwa,kasha jifukize kule kubana kutakwisha
SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

13. Majani yake yanasaidia katika kutibu shinikizo la damu


14..Papai likipondwa vizuri huweza kutumika kama urembo likitumiwa kama
lotion

Majani ya mpapai

15.Mbegu za papai hutumika kutibu homa meza kijiko cha chakula mara tatu
kwaajili ya kutibu homa
16.Mbegu za mapapai zilizokaushwa ndani kasha zikasagwa kuwa unga
zinatibu maralia,tumia kijiko kimoja cha chai changanya na uji kunywa mara
tatu kwa siku tano,mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda
mrefu atapona bila kutumia dawa nyingine
17.Mizizi yake ikipondwa na kuchemshwa katika maji lita mbili na nusu kwa
dakika kumi na tano yanatibu figo,bladder,yanazuia kutapika,Nusu kikombe
cha chai kutwa mara tatu kwa siku tano

FURAHIA TUNDA LA PAPAI NA JUISI YA PAPAI


SONGEA BUSINESS CLINIC COMPANY LTD.
P.O.Box 248, Songea
Reg. N0: 128839
Mobile phone: +255756096291,+255742346961,+255712421264
Email: songeabusinessclinic@gmail.com, ladslausbigambo@gmail.com

Copy right

Songea Business Clinic Co. Ltd 2017

You might also like