Katiba Ya Kikundi

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 13

KATIBA

2020

SEHEMU YA KWANZA

MAMBO YA AWALI
1
KATIBA

Jina la Katiba 1. Katiba hii itajulikana kama “Katiba ya Kikundi cha Umoja Wa
Wanaisimani”
Tafsiri ya Maneno 2 (1) Katika katiba hii, isipokuwa kama imefafanuliwa vinginevyo
katika sharti husika, maneno yafuatayo yatakuwa na maana kama
ifuatavyo:
“Kikundi” maana ya Kikundi cha Umoja Wa Wanaisimani;
“Mwanachama” maana yake ni mwanaisimani yeyote aishiye Mbeya na
Songwe na ambaye amekidhi masharti ya kuwa mwanachama wa kikundi
kwa mujibu wa Ibara ya 6 ya Katiba hii ;
(2) Katika katiba hii maneno yaliyotumika katika umoja yatakuwa na
maana ile ile yakitumika katika wingi na hivyo hivyo maneno
yaliyotumika katika wingi yatakuwa na maana ile ile yakitumika katika
umoja.
Jina, Anuani na 3. (1) Jina la Kikundi litakuwa “Kikundi cha Umoja Wa Wanaisimani”
Makao Makuu ya (2) Anuani ya Kikundi itakuwa xxx
(3) Ofisi na Makao Makuu ya Kikundi itakuwa xxx
Kikundi

SEHEMU YA PILI
DIRA, DHIMA NA MADHUMUNI YA KIKUNDI

Dira na Dhima ya 4. (1) Dira ya Kikundi ni “Kuwa Kikundi chenye faida na maslahi kwa
Kikundi ustawi wa wanachama kijamii na kiuchumi’’
(2) Dhima ya Kikundi ni “ Kuwawezesha wanachama kushirikiana na
kusaidia kuleta ustawi wa kijamii na kiuchumi kwa wanachama wake”

Lengo na Madhumuni ya 5. (1) Lengo kuu la Kikundi ni kuwa jukwaa la wanachama kujadili na
Kikundi kubadilishana mawazo na uzoefu na kusaidiana kutatua changamoto
mbalimbali za maisha.
(2) Bila kuathiri lengo tajwa hapo juu, madhumuni ya Kikundi
yatakuwa ni pamoja na:-
a) Kuwezesha wanachama kubadilishana taarifa mbalimbali
zinazoweza kusaidia maendeleo na ustawi wa wanachama;
b) Kuanzisha mfuko wa fedha utakaochangiwa na wanachama na
kutumika kutatua changamoto mbalimbali za wanachama kwa

2
KATIBA

kuzingatia matakwa ya Katiba hii;


c) Kuhamasisha wanachama kushirikiana na kusaidiana katika
shughuli za sherehe, misiba, nk;
d) Kuwezesha kikundi kuanzisha miradi au kushiriki katika
shughuli za uwekezaji wa pamoja kwa maslahi ya wanachama;
e) Kujihusisha na shughuli yoyote kwa lengo la kufanikisha lengo
na madhumuni ya Kikundi.

SEHEMU YA TATU
MASUALA YANAYOHUSU UANACHAMA
Uanachama na sifa ya 6. (1) Uanachama wa kikundi utakuwa wazi kwa mtu yeyote ambaye
kuwa mwanachama anaishi Mbeya na Songwe na ni mwenyeji wa Isimani.
(2) Bila kuathiri matakwa ya Katiba hii, mtu yeyote anaetaka
kuwa mwanachama ni lazima:-
a) Awe anaishi Mikoa ya Mbeya na Songwe.
b) Awe na uwezo wa kulipa kiingilio, ada na michango mbalimbali
ya kikundi itakayokubalika na wanachama kwa mujibu wa Katiba
hii;
c) Awe tayari kushirikiana na wanachama wengine katika
kufanikisha lengo na madhumuni ya Kikundi; na
d) Awe tayari kusimamia na kutekeleza matakwa ya Katiba hii.
Utaratibu wa kujiunga 7. (a) Mtu yeyeto anayetaka kujiunga Uanachama atapaswa kutuma
Uanachama maombi kimaandishi kwa viongozi.
(b) Maombi ya uanachama yatajadiliwa endapo zaidi ya nusu ya
wanachama watamkubali, Mwenyekiti au Katibu wa Kikundi
. atamjulisha mhusika kuwa amekubaliwa kuwa mwanachama
kimaandishi.
(c) Mwombaji atapaswa kulipa kiingilio, ada na michango ambayo
kila mwanachama anatakiwa kulipa kwa mujibu wa katiba hii.
(d) Iwapo maombi ya Uanachama yatakataliwa, mwombaji atakuwa
na haki ya kuelezwa sababu ya kukataliwa kwake uanachama na
Mwenyekiti au Katibu kimaandishi
Haki za Mwanachama 8. Bila kuathiri matakwa ya Katiba, Mwanachama atakuwa na haki
zifuatazo:-
a) Kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Kikundi;

3
KATIBA

b) Kuhudhuria na kushiriki katika Mikutano ya Kikundi;


c) Kuitisha Mkutano Mkuu Maalum wa Kikundi iwapo ataungwa
mkono na wanachama wengine wasiopungua robo tatu ya
wanachama kwa kufuata taratibu zilizoainishwa na katiba hii;
d) Kuteua wawakilishi na kuwabadilisha kwa mujibu wa katiba hii;
e) Kupatiwa huduma stahiki za Kikundi baada ya kukidhi vigezo
vinavyotakiwa;
f) Kushiriki katika kufanya maamuzi ya Kikundi;
g) Kupatiwa taarifa zinazokihusu Kikundi;
h) Kupatiwa Mgao wa ziada au mafao mengine yatokanayo na
uendeshaji wa shughuli za Kikundi;
i) Kushiriki katika kufanya marekebisho ya Katiba ya Kikundi;
j) Kujitoa katika Kikundi;
k) Kuanzisha uchunguzi wa mwenendo wa Kikundi chake kwa
kuzingatia matakwa ya Katiba;
l) Kukata rufaa dhidi ya maamuzi yaliyopitishwa kwa kuzingatia
Katiba ya Kikundi;
m) Haki nyingine zozote zitakazotolewa kwa wanachama wengine
kwa kuzingatia vigezo na Katiba yaliyokubaliwa.

Mwanachama 9. Bila kuathiri matakwa ya Katiba, mwanachama ana paswa kupewa


anayestahili Kupewa Pole pole baada ya tatizo kutokea ikiwa ni;-
a) Mwanachama hai anayeshiriki vikao, anachangia ada ya
uanachama kila mwezi na aliyekamilisha ada ya kiingilio.
b) Mwanachama ambaye hajachangia kwa miezi minne au zaidi bila
taarifa rasmi iliyokubalika na uongozi pamoja na wanachama
hatapewa pole.
c) Mwanachama ambaye hajachangia kuanzia mwezi mmoja hadi
mitatu ataonwa, ila atakatwa madeni yote anayodaiwa.
d) Mwanachama asipochangia ndani ya miezi mitatu atatozwa faini
ya Tshs 15,000/= yaani ni sawa na 5,000/= kwa kila mwezi.
Wajibu wa Mwanachama 10. Bila kuathiri matakwa ya Katiba, Mwanachama atakuwa na wajibu
ufuatao:-
a) Kutii matakwa ya Katiba, maadili na taratibu zote zinazotumika
kuendesha shughuli za Kikundi;

4
KATIBA

b) Kulipa kiingilio, Ada na Michango ya kikundi kwa mujibu wa


Katiba hii;
c) Kushiriki katika kutekeleza shughuli zote zilizokubaliwa
kutekelezwa na Kikundi hiki;
d) Kuhudhuria Mikutano na vikao vya Kikundi kwa mujibu wa
Katiba hii;
e) Kulipa madeni yote anayodaiwa na Kikundi kwa mujibu wa
katiba hii au makubaliano mengine ya Kikundi;
f) Kutekeleza maazimio ya Mikutano au vikao vya Kikundi;
g) Kulinda na kutetea maslahi na mali za Kikundi;
h) Kulinda hadhi na mwonekano wa Kikundi;
i) Kuwa tayari kujifunza, kukosolewa na kukanywa na uongozi wa
kikundi au mwanachama mwingine; na
j) Kufanya jambo lolote litakalo hitajika kulingana Katiba hii.
Kukoma kwa Uanachama 11. (1) Mwanachama atakoma kuwa mwanachama kwa:
a) Kujiondoa kwa hiari yake mwenyewe.
b) Mwanachama hai anaweza kujitoa katika kikundi mwisho wa
mwaka tu.
c) Mwanachama atakaye jitoa bila kufuata utaratibu uliowekwa
atapoteza haki zake zote.
d) Mwanachama ambaye ataacha kuchangia katika mfuko kwa
muda wa miezi minne bila taarifa rasmi na iliyokubalika
atakuwa amejitoa mwenyewe na hivyo atapoteza haki zake
zote.
e) Mwanachama atakayejitoa mwisho wa mwaka atapata robo
tatu ya hisa zake.
(2). Bila kuathiri matakwa ya Katiba, wanachama watakuwa na mamlaka
ya kumfukuza mwanachama kupitia mkutano au kikao chochote cha
kikundi iwapo mwanachama:-
a) Atahusika, kutuhumiwa na kuhukumiwa kwa kosa lolote
la jinai kwa mujibu wa Sheria za nchi na kufungwa kwa
kipindi kisichopungua miezi sita (6);
b) Atakiuka matakwa ya katiba ya Kikundi na sheria za
Udhibiti wa matumizi ya mitandao;

5
KATIBA

c) Atakiuka mikataba au makubaliano halali iliyoingiwa na


Kikundi kwa maslahi ya wanachama; na
d) Atathibitika kuwa na matendo yanayoathiri amani,
upendo, maslahi au maadili ya kikundi.
(3) Mwanachama yeyote hataweza kufukuzwa uanachama isipokuwa
baada ya kupata haki ya kusikilizwa, kujitetea na kujadiliwa na
wanachama na atakuwa na haki ya kukata rufaa kwa mlezi wa kikundi
kuzingatia matakwa ya Katiba hii.
(4) Mwanachama aliyekoma uanachama anaweza kurejeshewa
uanachama wake akiomba kwa maandishi na kurekebisha dosari
zilizosababisha Uanachama kukoma na iwapo robo tatu ya wanachama
wataridhia na ataanza kama mwanachama mpya.
Stahili baada ya kukoma 12. Mwanachama yeyote mwenye deni na ambaye Uanachama wake
Uanachama umekoma atapaswa kurudisha deni lake lote analodaiwa mara moja.
Ada na Michango ya 13. (1) Kwa lengo la kuwa mwanachama halali, kila mwanachama
Kikundi atawajibika kuchangia mtaji wa Kikundi kwa kulipa kiingilio, ada na
michango ya kikundi kwa kiwango na kiasi kitakachoamuliwa na
Mkutano Mkuu wa wanachama kama ifuatavyo:-
a) kulipa ada ya kiingilio ya kiasi cha shilingi elfu
hamsini(50,000/=) ambacho hakitarejeshwa kwa mwanachama
endapo uanachama wake utakoma;
b) Kulipa ada ya mwezi ya shilingi elfu tano(5,000/=) kila jumapili
ya mwanzo wa kila mwezi;
c) Kulipa michango kwa ajili ya matukio mbalimbali kwa kiwango
ambacho kitakubaliwa na wanachama kwa kuzingatia tukio
husika;
(2) Wanachama wanaweza kukubaliana kubadili viwango vya ada na
michango mbalimbali ya Kikundi iwapo watakubaliana kwa maamuzi ya
robo tatu ya wanachama.

SEHEMU YA NNE
MAPATO NA MATUMIZI YA KIKUNDI

Mapato na Mali za 14. (1) Bila kutahiri matakwa ya Katiba, Kikundi kitakuwa na vyanzo
Kikundi mbalimbali vya mapato ikiwa ni pamoja na:-

6
KATIBA

a) Viingilio vya wanachama;


b) Ada za wanachama;
c) Michango mbalimbali ya wanachama kama itakavyoamuliwa na
wanachama;
d) Mapato kutokana na uwekezaji utakaofanywa na Kikundi;na
e) Mapato mengineyo yatakayopatikana kutokana na shughuli na
vyanzo mbalimbali.
(2) Kikundi kitakuwa na Daftari la Mali za Kikundi ambamo
kutaorodheshwa mali zote za Kikundi ikiwa ni pamoja na:
a) Fedha taslimu;
b) Fedha zilizoko Benki au katika taasisi nyingine za fedha;
c) Uwekezaji katika taasisi nyingine; na
d) Mali nyingine kwa kadri ya daftari la mali za Kikundi.

Matumizi ya fedha na 15. (1) Kikundi kitatumia fedha zake kama ifuatavyo:-
utoaji msaada a) Kumsaidia mwanachama atakayepata tatizo la msiba kwa kufiwa
na mke au mume; mtoto wake wa kumzaa; mama au baba mzazi;
na Mlezi wake. (Mwanachama iwapo atafiwa na wazazi (Baba au
Mama) au Walezi wake atapewa 200,000/= (Kikindi kitatoa Tsh
100,000/= na Kila Mwanachama atatakiwa kuchangia Tshs
5,000/= ili kutimiza 200,000/=.
NB: Pesa itakayo zidi itaingizwa katika mfuko wa kikundi.
b) Kumsaidia mwanachama atakaye ugua na kulazwa hospitali kwa
kipindi kisichopungua siku saba (7) (Mwanachama akiugua kwa
muda wa juma moja kila mwanachama atawajibika kuchangia
Tshs 2,000/= kwa ajili ya kwenda kumpa pole).
c) Iwapo mwanachama atafariki (Kikundi kitatoa pole ya Tshs
200,000/= kwa ndugu zake siku ya msiba);
d) Kuchangia shughuli za ndoa iwapo mwanachama anaoa au
kuolewa(Mwanachama akiwa na sherehe ya kuolewa/kuoa
atachangiwa kiasi cha Tshs 200,000/=(100,000/= itatoka katika
mfuko wa kikundi na 100,000/= itachangishwa kutoka kwa
wanachama) ambayo itawasilishwa na wawakilishi au
wanachama wote siku tukio Ukumbini); na

7
KATIBA

e) Kuwekeza katika miradi au shughuli za uwekezaji kwa ridhaa ya


wanachama.
(2) Bila kuathiri matakwa ya ibara hii, Nje na wategemezi iwapo
mwanachama atafiwa na ndugu yake aliyekuwa anaishi naye nyumbani
kwake, kila mwanachama atawajibika kuchangia kiasi cha Tshs 2,000/=
kwa ajili ya kuhani msiba.
(3) Bila kuathiri matakwa ya katiba hii, kiwango cha fedha
kitakachotumika kumsaidia mwanachama kitahusisha fedha za mfuko wa
kikundi na michango kwa viwango vilivyokubaliwa na wanachama.
Uwekezaji 16. Kikundi kitafanya uwekezaji katika vitega uchumi mbalimbali
ikiwemo kununua hisa katika taasisi mbalimbali kwa ridhaa ya
wanachama lakini kiasi kitakachowekezwa kutozidi asilimia 20% ya
fedha za mfuko au mali zote za Kikundi.
SEHEMU YA TANO
UONGOZI NA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA KIKUNDI
Mikutano na vikao 17. (1) Uongozi na usimamizi wa shughuli zote za Kikundi utafanywa

vya Kikundi kwa kuzingatia Katiba ya Kikundi kwa maslahi ya wanachama ambapo
mamlaka ya juu ya Uongozi na Usimamizi wa shughuli zote za Kikundi
yatakuwa mikononi mwa wanachama kupitia mikutano na vikao halali ya
Kikundi.
(2) Bila kuathiri matakwa ya Katiba hii, Kikundi kitakuwa na aina mbili
ya mikutano ambayo ni mkutano mkuu na mkutano maalum na kutakuwa
vikao vya kila mwezi.
Mkutano Mkuu wa 18. (1) Mkutano Mkuu wa Kikundi utafanyika mara moja kwa mwaka na

Kikundi utakuwa na majukumu yafuatayo:-


a) Kutathmini na kujadili utekelezaji wa lengo na madhumuni ya
kikundi kwa mwaka;
b) Kupokea na kupitia taarifa za fedha za mwaka pamoja na
taarifa nyingine muhimu kwa maendeleo ya Kikundi;
c) Kupokea, kujadili na kuidhinisha makisio ya mapato na
matumizi ya mwaka unaofuata;
d) Kupokea, kujadili na kupitisha mpango mkakati na mpango
kazi wa Kikundi;
e) Kuamua matumizi au uwekezaji wa ziada, halisi iliyopatikana
kwa kuzingatia matakwa ya katiba;
8
KATIBA

f) Kujadili na kuidhinisha marekebisho ya katiba ya Kikundi;


g) Kuchagua wajumbe wa Bodi wakiwemo mwenyekiti,
Makamo Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mhazini na
wajumbe wawili ambao ni wawakilishi wa wanachama;
h) Kusikiliza na kuamua malalamiko yaliyowasilishwa na
wanachama kutokana na maamuzi au matendo ya viongozi au
watendaji; na
i) Kushughulikia jambo lolote lenye maslahi kwa Kikundi
lililowasilishwa mkutanoni kwa utaratibu unaokubalika.
(2) Taratibu zote za uitishwaji, uendeshwaji na ufanywaji maamuzi
katika mkutano mkuu utapaswa kuzingatia matakwa ya Katiba na
maelekezo na miongozo husika itakayotolewa na uongozi wa kikundi.
Mkutano Mkuu 19. (1) Kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Mkutano Mkuu Maalum wa

Maalum Kikundi unaweza kuitishwa kwa maombi maalum yaangalau nusu ya


wanachama, au kwa maombi ya uongozi.
(2) Mkutano Mkuu Maalum ulioitishwa kwa mujibu wa ibara hii
utapaswa kuwa na ajenda maalum.
Akidi ya mikutano 20. Mikutano yote halali ya Kikundi itakuwa halali ikiwa utahudhuriwa
na zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya wajumbe au wanachama wote.
Uitishwaji na 21. Uitishwaji na maamuzi ya mikutano utakuwa kama

maamuzi ya mikutano ifuatavyo;


a) Kila baada ya mwezi mmoja kutakuwa na kikao cha wanachama
b) Kikao cha dharula kitaitishwa na viongozi, iwapo kutakuwa na jambo
la dharula.
c) Wanachama wanaweza kuitisha kikao iwapo wataomba na lazima
watimie robo tatu (3/4) ya wanachama.
d) Bila kuathiri matakwa ya katiba hii, katika mikutano yote ya kikundi
wajumbe watajulishwa si chini ya siku saba kabla ya siku ya mkutano.
e) Taarifa kwa wajumbe inaweza kutolewa katika njia ya mitandao au
kwa ujumbe wa simu ya mkononi, barua pepe, au njia nyingine
itakayokuwa muafaka kwa mujibu wa teknolojia ya mawasiliano.
f) Tangazo la mkutano kwa uchache litaonyesha tarehe, mahali pa
mkutano, maelezo ya maudhui ya mkutano na ajenda za mkutano mkuu
huo.

9
KATIBA

g) Maamuzi yoyote yatakayofikiwa katika mikutano ya kikundi itakuwa


halali iwapo yafanywa kwa makubaliano ya wengi.
h) Iwapo katika mkutano wa kikundi kutatokea jambo lolote
litakaloshindikana kuamuliwa kwa njia za muafaka au kura, jambo hilo
litapaswa kuahirishwa au kufutwa.
Bodi ya Kikundi 22. Kutakuwa na Bodi ya uongozi wa kikundi ambayo itakuwa na
jukumu la kusimamia shughuli, mali na uendeshaji wa Kikundi kwa
niaba ya wanachama.
a) Idadi ya wajumbe wa Bodi itakuwa ni wajumbe watano ambao ni;
Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti, Katibu, Katibu msaidizi, Mweka
hazina na wajumbe wawili watakaochaguliwa na Mwenyekiti kwa
mamlaka yake na kuthibitiswa na theluthi mbili ya wanachama wote.
b) Wajumbe wa Bodi watakaa madarakani kwa kipindi cha mwaka
mmoja na baada ya hapo wajumbe wanaweza kuchaguliwa tena kwa
muda mwingine iwapo wataonekana wanafaa.
Vikao vya kikundi 23. Bila kuathiri majukumu ya mikutano ya kikundi, kikundi kitakuwa na
vikao vya kila mwezi ambavyo vitafanyika kwa lengo la kujadili masuala
mbalimbali yatakayojitokeza na maazimio ya vikao hivyo yatapaswa
kutekelezwa na uongozi.
Mwenyekiti wa 24. (1) Mwenyekiti wa Kikundi atakuwa ni kiongozi mkuu na

Kikundi mwakilishi wa Kikundi na wanachama wote na atakuwa na majukumu


ya:-
a) Kuongoza mikutano au vikao vya Kikundi;
b) Kuwa Msemaji mkuu wa Kikundi;
c) Kutoa taarifa za maendeleo ya Kikundi katika Mkutano Mkuu
wa Kikundi;
d) Kuwakilisha Kikundi katika mikutano na vikao vinavyohusu
Kikundi;
e) Kuteua kamati mbalimbali za kikundi iwapo kuna ulazima wa
kufanya hivyo; na
f) Kutekeleza shughuli na majukumu mengine kwa maelekezo ya
wanachama na kwa mujibu wa Katiba
(2) Mwenyekiti atachaguliwa na wanachama kwa kupigiwa kura na
ataongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja isipokuwa anaweza
kuachishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu kabla ya kipindi hicho na
10
KATIBA

uchaguzi mwingine kufanyika endapo atakuwa na makosa au


anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, uadilifu au kushindwa kutekeleza
majukumu yake.
Katibu wa kikundi 25. (1) Katibu wa kikundi atachaguliwa na wanachama atashika
madaraka kwa mwaka mmoja, isipokuwa anaweza kusimamishwa au
kuachishwa wadhifa wake na wanachama kabla ya kipindi hicho.
(2) Katibu atakuwa msaidizi mkuu wa Mwenyekiti na atakuwa na
jukumu la kumsaidia Mwenyekiti na kutekeleza majukumu ya
Mwenyekiti iwapo Mwenyekiti hatakuwepo au kwa ridhaa ya
Mwenyekiti.
Mhazini wa Kikundi 26. (1) Mhazini wa kikundi atachaguliwa na wanachama atashika
madaraka kwa mwaka mmoja, isipokuwa anaweza kusimamishwa au
kuachishwa wadhifa wake na wanachama kabla ya kipindi hicho.
(2) Atakuwa ndiye mtunzaji wa fedha za kikundi.
(3) Ataandaa na kutoa taarifa ya fedha za kikundi katika
Mkutano/Kikao.
(4) Ataandaa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za kikundi.
WATIA SAHIHI 27. Kikundi kitakuwa na makundi mawili ya watia sahihi ambayo ni;-
(A)1. Mwenyekiti (B) 1. Mhazini
2. Katibu 2. Mjumbe

Vikao vya Bodi 28. Bodi ya Kikundi itakuwa na vikao vifuatavyo;


a) Itafanya kikao angalau kimoja kila robo mwaka na vikao hivyo
vitakuwa na jukumu la pamoja na mambo mengine kupokea na kujadili
taarifa za hali ya fedha, utekelezaji wa kamati mbalimbali na taarifa ya
uwekezaji katika vitega uchumi vya Kikundi.
b) Katika vikao vyote vya Bodi akidi ya vikao ni mahudhurio ya asilimia
50% au zaidi ya wajumbe halali wa vikao.
c) Bodi kwa ridhaa ya wanachama inaweza kuandaa Kanuni na Taratibu
za uendeshaji wa kikundi na shughuli za kikundi ikiwa ni pamoja na
taratibu za kusaidiana miongoni mwa wanachama.
Kukoma kwa uongozi 29.(1) Bila kuathiri matakwa ya Katiba hii, uongozi wa kikundi ni wa

wa kikundi mwaka mmoja :


(2) Kiongozi atakoma uongozi baada ya muda wake kumalizika lakini
anaweza kuchaguliwa tena endapo ataonekana anafaa.

11
KATIBA

(2) Kiongozi wa kikundi ataweza kuondolewa madaraka yake iwapo


itaibainika kwamba Mjumbe huyo:-
a) Atahusika katika wizi au ubadhirifu wa mali za Kikundi
au kutuhumiwa na kuhukumiwa kwa kosa lolote la jinai
kwa mujibu wa Sheria;
b) Atavunja au kukiuka Katiba ya Kikundi na sheria zingine
husika;
c) Atakiuka mikataba au makubaliano halali iliyoingiwa na
Kikundi kwa maslahi ya wanachama;
d) Atakiuka maadili na miiko ya uongozi kwa kuzingatia
Katiba na Misingi ya Maadili ya kikundi; na
e) Atajihusisha katika shughuli ambazo zinaathiri maslahi ya
Kikundi au wanachama au iwapo atakuwa na mgongano
wa maslahi na Kikundi au wanachama wenzie na hayupo
tayari kuachana na shughuli husika.
(3) Kiongozi wa kikundi hataweza kuondolewa madarakani na
wanachama isipokuwa baada ya kupata haki ya kusikilizwa, kujitetea na
kujadiliwa katika Mkutano Mkuu na atakuwa na haki ya kukata rufaa
dhidi ya maamuzi yoyote kwa bodi ya kikundi

SEHEMU YA TANO
MAMBO YA JUMLA

Kukata rufaa 30. Kiongozi au mwanachama yeyote ana haki ya kukata rufaa dhidi ya
maamuzi yoyote kwa bodi ya kikundi ambaye maamuzi yake yatakuwa
ni ya mwisho.
Kuvunjika kwa 31. a) Kikundi kinaweza kuvunjika iwapo wanachama wataazimia

Kikundi na Hatima Kikundi kuvunjwa kwa Azimio la robo tatu (3/4) ya Wajumbe wote
katika Mkutano Mkuu;
ya Mali za kikundi
b) Kikundi kikivunjwa fedha au mali za kikundi zitagawanywa kwa
wanachama wote walio hai kwa kuzingatia hisa za kila mwanachama;
c) Iwapo kikundi kitakuwa kinadaiwa wakati wa kuvunja, basi kila
mwanachama atawajibika kulipa deni hilo kabla ya kuvunjwa kikundi.
Kushindwa kufanyika Endapo uchaguzi utashindwa kufanyika kwa sababu yoyote ile, Bodi ya

12
KATIBA

uchaguzi kwa mujibu kikundi itaongozi kikundi kwa muda wa mpito (muda usiozidi miezi

wa Katiba mitatu) na kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa Katiba hii.

Kurekebisha Katiba 32. Katiba hii inaweza kufanyiwa marekebisho kwa maamuzi ya robo
tatu ya Wanachama katika Mkutano
Kuidhinishwa na 33. Katiba hii itakuwa halali na kuanza kutumika baada ya kupitishwa na

kuanza kutumika kwa kuungwa mkono na wanachama wasiopungua robo tatu ya wanachama
wote.
Katiba

MAJINA YA WANACHAMA
No JINA KAMILI NAMBA YA SIMU
:
1. TAUSI MSIGALA 0782470136
2. THOMAS MHONGOLE 0756200639
3 GENORTH SANGA 0754614632
4. JOSEPHAT MSAMBWA 0768036094
5. ADELINA JOSHUA 0675797608
6. SOPHIA KAMBILI 0755538347
7. GODFREY MSAMBWA 0769848217
8. GASPALINA SAMBALA 0758247409
9. JULIANA MAYEMBA 0756632873
10. JULIANA NYALUSI 0763465462
11. MICHAEL SHONI 0742038945
12. ANJELO KAVINDI 0754660202
12. VAILETI MWILASI 0752327144
14. MARY KIKOTI 0755059973
15. ANJELINA KASTORY
16. RAHEL LUOGA
17. EVER MSIGWA
18. SHUKURU WANDELAGE
19. JUSTINE SENGELE
20. SAMWELI SENGELE
21.
22.
23.
24.
25.

13

You might also like