Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 22

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

(THBUB)

THBUB
Majukumu, Mafanikio na Changamoto

Ujumbe: ‘Miaka 60 ya Kulinda na Kukuza Upatikanaji wa Haki’


YALIYOMO

UTANGULIZI...........................................................................................................................3

SEHEMU YA KWANZA: TUME YA KUDUMU YA UCHUNGUZI (1966 – 2001)...........4


1.1 Utangulizi...................................................................................................................5
1.2 Kazi za TKU...............................................................................................................5
1.3 Muundo wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi...........................................................5
1.4 Viongozi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi..........................................................6
1.5 Mafanikio ya TKU.....................................................................................................7
1.6 Changamoto...............................................................................................................8

SEHEMU YA PILI: TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA


BORA (2001 – 2011)........................................................................................10
2.1 Utangulizi.................................................................................................................11
2.2 Dira ya Tume............................................................................................................12
2.3 Dhamira ya Tume.....................................................................................................12
2.4 Majukumu ya Tume.................................................................................................12
2.5 Muundo wa Tume....................................................................................................13
2.6 Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora....................................16
2.7 Kanda na matawi ya THBUB...................................................................................18
2.8 Mafanikio.................................................................................................................18
2.9 Changamoto.............................................................................................................23
2.10 Mipango ya baadaye.................................................................................................25

2
UTANGULIZI

Historia ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaanzia mwaka 1966
ilipoundwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) ambayo ilivunjwa mnamo mwaka 2001.

Sehemu ya kwanza ya kijitabu hiki inaelezea juu ya Tume ya Kudumu ya Uchunguzi na


sehemu ya pili inazungumzia juu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

3
SEHEMU YA KWANZA

TUME YA KUDUMU YA UCHUNGUZI


(1966 2001)

4
1.1 Utangulizi
Tume ya Kudumu ya Uchunguzi ni chombo kilichoundwa kikatiba chini ya kifungu
cha Sheria Na. 67-(1) ya mwaka 1965 ambacho kinasema kwamba ni lazima kuwepo
kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi ambayo ina mamlaka ya kuchunguza tabia na
mwenendo wa kila mtu katika mamlaka yake au sehemu binafsi.

Chombo hiki kilianza kufanya kazi kisheria kwa sheria (Sheria Na. 25/1966) ambayo
inaipa Tume mamlaka ya kuchunguza malalamiko yote yanayohusiana na matumizi
mabaya ya ofisi kwa watumishi wa umma.

1.2 Kazi za TKU


 Kufanya uchunguzi juu ya malalamiko yote yanayohusiana na utumiaji wa ofisi
na madaraka vibaya.

 Kutoa elimu kwa umma juu ya mfumo mzima wa mgawanyo wa madaraka na njia
muhimu za kufuata kabla ya kuleta malalamiko Tume ya Kudumu ya Uchunguzi.

 Kupokea malalamiko.

1.3 Muundo wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi


Chini ya ibara ya 68 ya Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Rais ana
mamlaka ya kuteua Makamishna watatu wenye sifa tofauti, na mmoja kati ya hawa
Makamishna anateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume.

Mbali na Makamishna, Tume inaundwa na Katibu Mtendaji pamoja na maafisa


uchunguzi. Muundo wa TKU ni kama ufuatao:
 Mwenyekiti
 Makamishna
 Katibu Mtendaji
 Wakurugenzi na Wakuu wa vitengo
 Maafisa Uchunguzi.

1.4 Viongozi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi

Wenyeviti 1966 – 2002


JINA MWAKA
1. Chifu Erasto A. M. Mang’enya 1965 - 1970
2. Jaji Mark P. K. Kimicha 1970 – 1972
3. Chifu Erasto A. M. Mang’enya 1972 – 1973
4. Col. S.J. Kitundu 1974 – 1978
5. Nd. Ackland L.S. Mhina 1978 – 1983
6. Nd. Anthony R. Mbelwa 1984 – 1989
7. Nd. Abdallah M.R. Nungu 1989 – 1995
8. Nd. Ibrahim S.A. Kajembo 1995 – 1997
9. Prof. Joseph Mbwiliza 1998 – 2002

Makamishna 1966 – 2002


JINA MWAKA
1. Nd. Samson Kishosha Gabba 1966 - 1967
2. Sheikh M. Ramiyah 1967 - 1968

5
3. Nd. K.M. Kikwete 1967 - 1971
4. Sheikh Abdallah Iddi Chaurembo 1969 - 1973
5. Nd. Wilson Nkeno Bizuru 1972 - 1976
6. Nd. Alhaji Mharami Mfaume 1973 - 1977
7. Nd. John Rwemigira Kibogoyo 1976 - 1978
8. Bibi Thekla Grace Mchauru 1976 - 1978
9. Nd. John Baptist Mwenda 1976 - 1978
10. Nd. Samson Kishosha Gabba 1978 - 1983
11. Nd. Ali Ame Chum 1978 - 1983
12. Nd. Rabia Mohamed Hamdani 1978 - 1983
13. Nd. Ephraim Kulwa Mvanga 1978 - 1984
14. Nd. Vincent Magoma Dimiso 1983 - 1984
15. Nd. Asia Amour Hassan 1983 - 1989
16. Nd. Mohamed Khatibu Suleiman Reja 1984 - 1990
17. Nd. Crispin Tungaraza 1985 - 1991
18. Bibi Margreth Lilian Ngude 1985 - 1991
19. Nd. Mwinyiwesa Idarous 1989 - 1993
20. Nd. Haji M. Haji 1990 - 1996
21. Nd. I.S.A. Kasembo 1991 - 1995
22. Nd. A.S. Kabongo 1993 - 1999
23. Nd. Halima Hamisi 1994 - 2000
24. Nd. Ramadhani Shabani 1997 - 2002

Makatibu Watendaji 1966 – 2002


JINA MWAKA
1. Nd. Herbert Katua 1966 – 1973
2. Nd. Anthony R. Mbelwa 1973 – 1977
3. Nd. Fredrick P.S Malika 1978 – 1993
4. Nd. Q.J. Mlama 1993 – 1998
5. Nd. Anastas P. Guvette 1998 – 2002

Wakurugenzi 1996 – 2001


Jina Idara Kipindi
1. Sabath B. Tetti Uchunguzi 1996 - 2001

1.5 Mafanikio ya TKU


 Ilifanikiwa kujitangaza na kutembelea wilaya zote za Tanzania bara na Visiwani
vikiwemo vijiji mbalimbali na kupokea malalamiko kutoka kwa Wananchi.

 Ilitoa mchango muhimu katika mfumo mzima wa siasa ya ujamaa na kujitegemea.


 Kuhusu haki za binadamu, Tume ilitoa mchango muhimu katika kuhakikisha
kwamba haki za kila raia zinalindwa na kuhifadhiwa, hii ilisaidia sana kuwafanya
Wananchi kutovunja Sheria, ingawa kwa kipindi hicho hadi kufikia 1984 haki za
binadamu (bill of rights) zilikuwa bado hazijaingizwa kwenye Katiba ya nchi.

 Tume ya Kudumu ya Uchunguzi ilikuwa sehemu pekee kwa wakati huo ambako
raia waliweza kupeleka malalamiko yao kuhusiana na matumizi mabaya ya
madaraka na ofisi yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wa umma dhidi ya
wananchi na kufanyiwa uchunguzi.

6
 Kwa kipindi cha miaka 20 Tume ilikuwa ikipokea wastani wa malalamiko 3,000
kwa mwaka, haya ni yale yaliyoletwa kwa maandishi na kufunguliwa majalada.
Mengi ya malalamiko hayo yalielekezwa kwenye mamlaka husika na mengine
yalishughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi. Aidha, mengine yaliachwa kwa sababu
mbalimbali baada ya kufanyiwa uchunguzi na mengine yalionekana hayana
msingi.

1.6 Changamoto
 Watu kukosa imani na utendaji wa Tume kwa kuwa ushahidi ulionyesha kuwa
kulikuwa na ongezeko la utumiaji mbaya wa madaraka miongoni mwa Watumishi
na viongozi wa umma.

 Kukosekana kwa ushirikiano wa dhati kutoka kwa viongozi wa serikali wakati wa


kufanya uchunguzi, hii ilitokana na viongozi wengi kutojua umuhimu wa Tume na
mamlaka yake. Kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, uvunjwaji wa
Sheria na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka vilifanya Tume iwe na wakati
mgumu wa kufanya kazi zake kwa uwazi zaidi.

 Urasimu katika mfumo mzima wa utendaji kazi serikalini ulifanya utoaji huduma
kwa Wananchi kuwa wa taratibu na kufanya wale waliokuwa wanadai haki zao
kuendelea kusubiri kwa muda mrefu bila mafanikio. Hii ilisababisha kutokuwa na
mahusiano mazuri kati ya Tume ya Kudumu ya Uchunguzi, taasisi za serikali na
Wananchi.
 Uhaba wa vitendea kazi, mfano magari na ukosefu wa fedha za kutosha kwa ajili
ya kufanikisha malengo ya Tume, hali hii ilisababisha kazi nyingi kutofanyika
kwa wakati na nyingine kutofanyika kabisa.

Hatua zilizochukuliwa kukabiliana na changamoto tajwa


 Tume ilianzisha na kuendesha kampeni ya kuelimisha viongozi wa umma
majukumu ya Tume kwa njia ya mikutano ili kuwapa uelewa kuhusu Tume na
kazi zake ikiwa ni pamoja na kuwasisitizia umuhimu wa kushugulikia barua
kutoka Tume kwa wakati.

 Tume ilitumia rasilimali chache zilizokuepo kipindi hicho kuhakikisha kuwa kazi
za Tume zinaendelea kufanyika kwa ufanisi bila kuathiri kwa kiasi kikubwa
jitihada za kuwahudumia Wananchi.

 Tume ilijitahidi kujenga na kudumisha mahusiano mazuri baina yake na


serikali,Wananchi na vyombo vingingine vya kimataifa kwa nia ya kufanikisha
malengo yake ya kuhudumia Wananchi.

Mabadiliko ya hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ulimwenguni kote katika miaka ya


1990 yalipelekea kuwepo kwa mabadiliko hayo hapa nchini pia. Kati ya mabadiliko
yaliyofanyika ni kuvunjwa kwa TKU mwaka 2000 na kuanzishwa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora mwaka 2001.

7
SEHEMU YA PILI

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA


(2001 - 2019)

8
2.1 Utangulizi
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni chombo huru cha Serikali
kinachojitegemea ambacho kinahusika na kulinda, kuhifadhi na kutetea haki za
binadamu na misingi ya utawala bora hapa Tanzania.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni idara inayojitegemea kwa mujibu wa


Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toleo la mwaka 1997 sura ya sita (6),
sehemu ya kwanza (1) ibara ya 129 (1) ikisomwa pamoja na ibara 130-(2). (Sheria na.
3/2000 ibara 17).

Kuanzishwa kwa Tume hii kulitokana na mchakato wa mapendekezo ya Tume na


Kamati mbalimbali, kama vile Tume ya Nyalali, Kamati ya Bomani, Kamati ya
Kisanga na mapendekezo ya mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali.

Moja ya mapendekezo ya Kamati ya Nyalali ilikuwa kuanzishwa kwa chombo huru


cha kusimamia haki za binadamu. Mapendekezo ya Kamati ya Bomani ya
Kurekebisha mfumo wa sheria (Legal Task Force) chini ya mpango wa kurekebisha
mfumo wa kitaasisi na kisheria (FILMUP) kwenye ripoti ya mwaka 1996, moja ya
mapendekezo yake ilikuwa ni kuanzishwa kwa Tume huru ya haki za binadamu na
usimamizi wa utawala (Commission for Human Rights and Administrative Justice).

Kamati ya Kisanga ya kutafuta maoni ya wananchi kwa kutumia waraka wa Serikali


Na. 1 wa mwaka 1998 (white paper Na.1) kwa ajili ya kufanyia marekebisho Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, moja ya mapendekezo
ilikuwa kuanzishwa kwa Tume huru ya kushughulikia haki za binadamu.

THBUB ilianzishwa kupitia mabadiliko ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa


Tanzania ya mwaka 1977, mabadiliko haya yalibadilisha sura ya sita (6) sehemu ya
kwanza (1) ya Katiba iliyokuwa imeanzisha na kuelezea kazi za Tume ya Kudumu ya
Uchunguzi, na kuunda Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Majukumu na
kazi za Tume yamefafanuliwa zaidi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977 Sura ya Sita Sehemu ya Kwanza Ibara ya 130 (1) na
Kifungu Na. 6 (1) cha sheria ya bunge ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora Na.7 ya mwaka 2001.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kama Idara inayojitegemea ilianzishwa
mnamo tarehe 01 Julai 2001 kwa taarifa ya kawaida Na. 311 kwenye gazeti la Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na. 23 la tarehe 08 Juni 2001. Imeanza na
watumishi wa serikali 76 (63 Tanzania Bara, 13 Zanzibar) ambao walikuwa katika
Tume ya Kudumu iliyofutwa kwa sheria Na. 7 ya mwaka 2001.

Aidha, Tume ilizinduliwa rasmi tarehe 15 Machi, 2002 baada ya kuteuliwa na


kuapishwa Makamishna wake.

2.2 Dira ya Tume


Kuwa na jamii yenye utamaduni ambao unaheshimu, unakuza na kulinda haki za
binadamu na misingi ya utawala bora.

2.3 Dhamira ya Tume


Kukuza na kulinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa ushirikiano na
wadau.

9
2.4 Majukumu ya Tume
Ibara ya 130 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kifungu cha 6(1)
cha sheria Na.7/2001 zinafafanua majukumu ya Tume. Majukumu hayo ni haya
yafuatayo:
 Kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za binadamu na wajibu kwa jamii kwa mujibu
wa Katiba na sheria za nchi.

 Kupokea na kuchunguza malalamiko yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu


na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

 Kutoa ushauri kwa Serikali na vyombo vingine vya umma na vya sekta binafsi
kuhusu haki za binadamu na utawala bora.

 Kufanya utafiti, kutoa na kueneza elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na
misingi ya utawala bora.

 Kuchukua hatua zipasazo kwa ajili ya kukuza na kuendeleza usuluhishi na suluhu


miongoni mwa taasisi na watu mbalimbali wanaofika au kufikishwa mbele ya
Tume.

 Kama ikibidi, kufungua mashauri mahakamani kuzuia vitendo vya uvunjwaji wa


haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

 Kuishauri Serikali kuridhia au kuingia kwenye mikataba ya kimataifa ya kulinda


haki za binadamu.

 Kupendekeza marekebisho katika sheria za nchi, miswaada au taratibu za


kiutawala ili kuhakikisha kuwa zinakidhi matakwa ya kanuni za haki za
binadamu.

 Kushirikiana na mashirika ya kimataifa, kikanda na mashirika mengine ya kitaifa


yenye uzoefu na umahiri katika ukuzaji na utetezi wa haki za binadamu na
utawala bora.

 Kutembelea magereza na sehemu nyingine ambazo watu wanazuiliwa au


kufungwa, kwa nia ya kukagua hali halisi ya sehemu hizo na watu waliozuiliwa au
waliofungiwa, na kutoa mapendekezo yenye lengo la kuboresha hali ya maisha
katika sehemu hizo.

2.5 Muundo wa Tume


 Tume inaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Makamishna watano na
Makamishna Wasaidizi ambao idadi yao haikutajwa kwenye Sheria ambao ndio
mamlaka ya usimamizi wa Tume.
 Makamishna wanateuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya Kamati ya Uteuzi
ambayo inapokea maoni kutoka kwa wananchi.

 Makamishna wanafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu, na wanaweza


kuteuliwa tena siyo zaidi ya kipindi cha pili kisichozidi miaka mitatu.

10
 Tume ina Katibu Mtendaji ambaye huteuliwa na Rais baada ya mashauriano na
Tume. Huyu ndiye msimamizi mkuu wa kazi za siku hadi siku kuhusu masuala ya
kiutawala na utekelezaji wa maamuzi ya kisera ya Tume.

Utendaji kazi wa Tume umegawanywa katika Divisheni na Vitengo. Kila Divisheni


inaongozwa na Mkurugenzi, na kila Divisheni imegawanywa katika seksheni chini ya
Wakurugenzi Wasaidizi. Divisheni hizo ni kama zifuatazo:
1. Divisheni ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu.
2. Divisheni ya Malalamiko na Uchunguzi
3. Divisheni ya Elimu kwa Umma, Mawasiliano, Utafiti na Nyaraka.
4. Divisheni ya Huduma za Kisheria

11
12
Aidha, kuna vitengo vifuatavyo katika Tume:
1. Kitengo cha Uhasibu na Fedha
2. Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Hesabu
3. Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
4. Kitengo cha Ununuzi na Ugavi.
5. Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini
Pia kuna Ofisi ya Zanzibar na Ofisi za Matawi za Tume kama ifuatavyo:
1. Ofisi ya Zanzibar
2. Ofisi ya Tawi Mwanza
3. Ofisi ya Tawi Lindi
4. Ofisi ya Tawi Pemba
5. Ofisi ya Tawi Dar Es Salaam
2.6 Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Wenyeviti 2002 – 2019


JINA MWAKA
1. Mhe. Jaji Robert Habesh Kisanga 2002 - 2008
2. Mhe. Jaji Ramadhani Amiri Manento 2008 - 2011
2015 - 2018
3. Mhe. Bahame Tom Mukirya Nyanduga
4. Mhe. Jaji Mathew Pauwa Mhina Mwaimu 2019 - hadi sasa

Makamu Wenyeviti 2002 – 2019


JINA MWAKA
1. Mhe. Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa 2002 - 2008
2. Mhe. Mahfoudha Alley Hamid 2008 - 2011
3. Mhe. Idd Ramadhani Mapuri 2015 - 2018
4. Mhe. Mohamed Khamis Hamad 2019 - hadi sasa

Makamishna 2002 – 2019


JINA MWAKA
1. Mhe. Catherine Herieth Mbelwa Kivanda 2002 - 2008
2. Mhe. Stephen Zakaria Mwaduma 2002 - 2008
3. Mhe. Jecha Salim Jecha 2002 - 2008
4. Mhe. Robert Vincent Makaramba 2002 - 2006
5. Mhe. Safia Masoud Khamis 2002 - 2008
6. Mhe. George Francis Mlawa 2007 - 2010
7. Mhe. Joaquine Antoinette De-Mello 2008 - 2011
8. Mhe. Zahor Juma Khamis 2008 - 2011
9. Mhe. Bernadeta Gambishi 2008 - 2011
10. Mhe. Ali Hassan Rajabu 2010 - 2013
11. Mhe. Mohamed Khamis Hamad 2015 - 2018
12. Mhe. Dkt. Kevin Mandopi 2015 - 2018
13. Mhe. Rehema Msabila Ntimizi 2015 - 2018
14. Mhe. Salma Ali Hassan 2015 - 2018
15. Mhe. Dkt. Fatma Rashid Khalfan 2019 - hadi sasa
16. Mhe. Thomas Masanja 2019 - hadi sasa
17. Mhe. Amina Talib Ali 2019 - hadi sasa
18. Mhe. Khatib Mwinyi Chande 2019 - hadi sasa

13
19. Mhe. Nyanda Josiah Shuli 2019 - hadi sasa

14
Makamishna Wasaidizi 2002 – 2019
JINA MWAKA
1. Mhe. Costantine Biseko Luguli Mugusi 2007 - 2010
2. Mhe. Fahamu Hamidu Mtulya 2007 - 2010

Makatibu Watendaji 2002 – 2019


JINA MWAKA
1. Bw. Anastas Pius Guvette 2002 - 2003
2. Bw. Gad John Kimweri Mjemas 2004 - 2006
3. Bibi Upendo Msuya 2007 - 2008
4. Bibi Mary C. Massay 2010 - 2019
5. Bibi Fatuma I. Muya (Kaimu Katibu)1 2019 – hadi sasa

Wakurugenzi 2004 – 2019


Kufuatia mabadiliko ya muundo ya mwaka 2004/2005 wakurugenzi wa Divisioni
zifuatazo waliteuliwa na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Oktoba 2004, tarehe 15 Julai
2005 na tarehe 12 Oktoba 2005. Wakurugenzi hao na Idara zao ni kama ifuatavyo:

Jina Idara Kipindi


1. Bw. Issa A. Nchasi Utawala na Utumishi 2004 - 2009
2. Bibi Mary C. Massay Huduma za Sheria 2004 - 2010
3. Bw. Hamisi J. Mvamba Utawala Bora 2004 hadi sasa
4. Bibi Epiphania H. Mfundo Utafiti na Nyaraka 2004 hadi 2011
5. Bibi Rosemary C. Jairo Elimu na Mafunzo 2004 hadi 2016
6. Bw. Francis K. Nzuki Haki za Binadamu 2004 hadi sasa
7. Bw. Augustine M. Mudogo Utawala na Utumishi 2009 hadi 2012
8. Bw. Nabor Assay Huduma za Sheria 2010 hadi sasa
9. BW. Alexander S. Hassan Elimu na Mafunzo 2017 hadi sasa
10. Fatuma I. Muya Utawala Bora 2012 hadi sasa
11. Godlisten H. Nyange Utafiti na Nyaraka 2012 hadi 2019
12. Florida Kazora Utumishi na Utumishi 2013 hadi 2014
13. Tabu Aron Utumishi na Utumishi 2015 hadi 2016
14. Benard Marceline Utumishi na Utumishi 2017 hadi 2018
15. Orest Mushi Utumishi na Utumishi 2019 hadi sasa

15
Watumishi
Tangu mwaka 2003/2004 Tume imekuwa ikiajiri watumishi wapya ili kukidhi
mahitaji ya rasilimali watu. Hadi hivi sasa Tume inao jumla ya watumishi 154 katika
nafasi mbalimbali. Hivyo kuna upungufu wa watumishi 65. Idadi hiyo ni pungufu
kidogo kufikia idadi ya watumishi wanaohitajika yaani 219 kwa mwaka wa fedha
2020/2021.

2.7 Kanda na matawi ya THBUB


Hivi sasa Tume ina ofisi nne (6) nchini kote. Ofisi hizo ni kama zifuatazo:
 Dodoma (Makao Makuu), ipo Kilimani, mtaa wa Nyerere, Kitalu Na. 339.

 Dar es Salaam (Kanda ya Mashariki), ipo mtaa wa Luthuli Kitalu na. 8 katika
jengo lijulikanalo kama “Haki House”. Tarehe 28 Januari, 2003 Tume
ilikabidhiwa jengo hilo jipya. Jengo hili lilijengwa kwa ufadhili wa serikali ya
Denmark. Jengo hilo lilifunguliwa rasmi Aprili 30, 2003 na makamu wa rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein kwa niaba ya
aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini William Mkapa.

 Zanzíbar (ofisi ya tawi yenye hadhi ya kitaifa), ipo katika jengo la Kamisheni ya
Wakfu na Mali za Amana, eneo la Mbweni.

 Mwanza (Kanda ya Ziwa), ipo mtaa wa Liberty, ndani ya jengo la Benki ya Taifa
ya Biashara, Ghorofa ya tatu (3).

 Lindi (Kanda ya Kusini), ipo mtaa wa Wailesi, Barabara iendayo kwa Mkuu wa
Mkoa, ndani ya jengo la zamani la TTCL.

 Pemba (Tawi), ipo Wete Pemba, mtaa wa Kitutia, mkabala na ofisi za posta wete.

 Aidha, kwa Dodoma, Tume ina ofisi nyingine mbili katika majengo ya Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyopo katika Kitivo cha Sayansi ya Jamii.

2.8 Mafanikio
Tangu Tume ianze kufanyakazi mwaka 2001 hadi hii leo imepata mafanikio mengi.
Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na yafuatayo:
 Hadi Desemba 31, 2019 Tume ilikuwa imeshughulikia na kuhitimisha mashauri
19,622 kati ya 27,346 yaliyopokelewa ambayo ni sawa na asilimia 72 ya mashauri
yote. Baadhi ya malalamiko hayo yameelekezwa kwenye mamlaka husika kwa
hatua zaidi. Aidha, zaidi ya asilimia 90 ya malalamiko yaliyopokelewa na
kushughulikiwa yanahusu ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na chini ya
asilimia 10 yanahusu uvunjwaji wa haki za binadamu.

 Tume imefanikiwa kufanya utafiti na uchunguzi juu ya matukio yanayojirudia ya


uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala wa haki.
Utaratibu huu wa utafiti na uchunguzi unalenga katika kutafuta vyanzo vya
uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala wa haki.
Tangu ilipoanzishwa, Tume imefanya utafiti na uchunguzi wa wazi mara kadhaa.

Miongoni mwa tafiti muhimu ni pamoja na:

16
- Utafiti juu ya Unyanyasaji wa Watoto Tanzania Bara mwaka 2005
- Utafiti juu ya Mateso na Unyanyasaji unaofanywa na Vyombo vya Kutekeleza
Sheria Tanzania mwaka 2007
- Utafiti na Uchunguzi juu ya Utekelezaji wa Haki za Watoto Zanzibar mwaka
2008 na
- Utafiti juu ya Mauaji ya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi (albino) na
Vikongwe wenye Macho Mekundu Tanzania Bara mwaka 2009.

Aidha, kutokana na utafiti na uchunguzi huo, Tume iliweza kupokea malalamiko


kutoka kwa jamii, kuelewa ukubwa wa matatizo na jinsi ya kushiriki kwa namna
inayofaa ili kutatua matatizo hayo. Kadhalika, baada ya utafiti na uchunguzi wa
wazi, Tume huwaalika wadau wa haki za binadamu kutoka katika sekta binafsi na
umma na kushauri jinsi ya kutatua matatizo yaliyogunduliwa.

 Tume imefanikiwa kuweka mfumo wa kisasa wa elektroniki wa kushughulikia


malalamiko. Kwa ufupi mfumo huu unaisaidia Tume kushughulikia malalamiko
ya wananchi kwa ufanisi na haraka zaidi ya ilivyokuwa hapo awali.

 Tume ilipata nafasi ya kupitia na kutoa maoni juu ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi na
Sheria ya Kuzuia na Kudhibiti Kuenea kwa VVU na UKIMWI. Pia Tume ilishiriki
kwa sehemu kubwa katika mchakato wa maandalizi na utungaji wa Sheria ya
Mtoto.

 Tume imeweza kutembelea magereza, vituo vya mafunzo na polisi mara kwa
mara kwa lengo la kufanya ukaguzi na kutoa elimu ya haki za binadamu na
misingi ya utawala bora kwa wafungwa, mahabusu, maafisa wa jeshi la magereza
na polisi. Ifuatayo ni adadi ya taasisi zilizotembelewa kila mwaka:

Mwaka Magereza Vituo vya polisi


2002/03 46 -

2003/04 21 36

2004/05 16 42

2005/06 37 75

2006/07 - -

2007/081 132 313

2008/09 75 -

2009/10 62 -

2010/11 29 51
1
Takwimu hizi ni kwa kipindi cha July 1, 2007 hadi Machi 31, 2008
2
Ikiwa ni magereza matatu (3) Tanzania Bara na Vyuo 10 vya mafunzo visiwani Zanzibar
3
Ikiwa ni vituo vya polisi sita (6) Tanzania Bara na vituo vya polisi 25 Zanzibar.

17
2011/12 - -

2012/13 46 48

2013/14 - -

2014/15 - -

2015/16 37 32

2016/17 32 32

2017/18 9 6

2018/19 22 13

Tume imekuwa ikitoa taarifa za ukaguzi wa magereza na vituo vya polisi na


kuziwasilisha kwa mamlaka husika na wadau kwa hatua zaidi. Inatia moyo
kutambua kuwa baadhi ya mapendekezo hayo yameshughulikiwa au kutekelezwa.
Mapendekezo hayo yanajumuisha:
- Kuondolewa kwa matumizi ya ndoo au “mitondoo” zilizokuwa zikitumika
kama vyoo magerezani kwa kujenga vyoo bora katika baadhi ya magereza.

- Matumizi ya magodoro badala ya “virago” ambavyo vilikuwa vinatumika


katika magereza mengi kama vifaa vya kulalia.

- Kutolewa kwa mavazi bora (suruali) yenye kuheshimu utu wa wafungwa.

- Kuanza kutolewa kwa huduma za kijamii kama burudani, michezo, taarifa


kupitia magazeti, luninga na radio katika baadhi ya magereza.

- Kufuatia kuwepo kwa uhuru wa kupata habari na elimu katika magereza


Novemba 2007 Tanzania iliingia katika vitabu vya historia. Kwa mara ya
kwanza mfungwa aliyekuwa akitumikia kifungo chake katika gereza la
Ukonga, Bwana Haruna Pembe Mgombela (57) kupata shahada ya Sheria
kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

 Imetayarisha machapisho mbalimbali, yakiwemo majarida, taarifa, vipeperushi,


vipindi vya radio na luninga na kugawa kwa wananchi na wadau machapisho
mbalimbali bure.

 Imefanya ziara na kutoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora katika Wilaya
zaidi ya 130 zilizoko katika Mikoa 26 ya Tanzania bara. Vilevile imetembelea
Mikoa yote mitano na Wilaya zake 10 visiwani Zanzibar.

 Imefanya mikutano ya hadhara vijijini, katika shule za sekondari na taasisi


mbalimbali. Kupitia mikutano hii ya hadhara wananchi wamepata fursa ya
kuwasilisha kero na malalamiko yao na Tume imeyashughulikia na kuyapatia

18
ufumbuzi na mengine kuyaelekeza kwenye mamlaka husika kwa hatua zaidi.
Matokeo ya ziara hizo ni kuongezeka kwa idadi ya malalamiko yanayowasilishwa
Tume kila mwaka.
 Imeweza kuandaa semina kwa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa
habari, Asasi Zisizo za Kiserikali, watu wenye ulemavu, wabunge wa Bunge la
Muungano na wajumbe wa baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

 Pia, Tume katika mwaka wa 2009 iliandaa Kongamano la Kitaifa lililokusudia


kuzingatia, kujadili na kupitisha vipaumbele vya Taifa na changamoto kuhusiana
na suala zima la haki za binadamu nchini Tanzania. Tume kwa kushirikiana na
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu walialika
wadau kuchangia katika uundaji wa mfumo mpya wa kitaasisi na kimkakati wa
kulinda na kukuza haki za binadamu nchini. Mapendekezo ya kongamano hilo
yalikusudiwa kutengeneza Mpango wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Haki za
Binadamu na kuingiza katika sera za nchi. Tume kama ilivyo ada iliishauri
Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kupitisha mpango huo kama njia bora
ya kulinda na kukuza haki za binadamu.

 Imeshiriki katika mikutano na makongamano mbalimbali ndani na nje ya nchi na


kutoa mada zinazohusu haki za binadamu na utawala bora.

 Wananchi wamekuwa na mtazamo chanya kwa Tume. Katika wiki ya maonyesho


ya Taasisi za Umma yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam, Juni 2009, Tume ilishinda tuzo ya juu katika utoaji huduma bora kwa
jamii na moja ya sababu ilikuwa ni kufikika kwake kwa urahisi.

Tena katika maonesho hayo hayo yaliyofanyika katika viwanja vya CCM
Kirumba jijini Juni 2010, Tume ilishinda nafasi ya tatu katika tuzo ya utoaji
huduma bora. Kadhalika, katika ngazi ya kimataifa, Tume imepewa daraja ‘A’
miongoni mwa Taasisi za kitaifa za haki za binadamu. Tume imepangwa daraja
hilo la ‘A’ na Kamati ya Kimataifa ya Kuratibu Ukuzaji na Utetezi wa Haki za
Binadamu (The International Coordinating Committee on the Promotion and
Protection of Human Rights).

 Tume imeweza kutiliana saini mkataba wa ushirikiano na AZAKI 31 na kuanzisha


zaidi ya klabu za haki za binadamu 121 katika shule za msingi, sekondarina Vyuo
vya Ualimu nchini katika kutoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora kwa
umma. Na vilevile Tume ina mahusiano mazuri na taasisi na jumuiya mbalimbali
za kitaifa na kimataifa zinazojihusisha na masuala ya haki za binadamu.

 Imeweza kuandaa taarifa za kazi za mwaka na kuziwasilisha Bungeni na mamlaka


mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na taarifa za ukaguzi wa magereza na sehemu
wanazoshikiliwa mahabusu na ziara mbalimbali.

 Kwa miaka yote imeweza kuratibu maadhimisho ya kitaifa ya siku ya Haki za


Binadamu Duniani kwa kushirikiana na wadau wengine na imeweza kushiriki
katika matukio mbalimbali ya kitaifa ikiwa ni pamoja na maonesho ya kibiashara
ya Sabasaba, Wiki ya Utumishi wa Umma, wiki ya sheria, maonesho ya nanene
n.k na kutoa elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa umma.

19
2.9 Changamoto
Tume inakabiliwa na changamoto zifuatazo katika kutekeleza majukumu yake:
 Watanzania wengi kutokuwa na uelewa wa kutosha wa haki za binadamu na
misingi ya utawala bora.

 Ukosefu wa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa baadhi ya taasisi za umma


hususan katika kutekeleza maamuzi na mapendekezo ya Tume, jambo
linalochelewesha upatikanaji wa haki kwa wakati. Kwa upande mwingine
ushirikiano mdogo husababisha mchakato wa uchunguzi wa malalamiko
kuchukua muda mrefu isivyo stahili.

 Mfumo wa sheria za Tanzania bado unakumbatia sheria zilizopitwa na wakati


ambazo zilibainishwa na Tume ya Jaji Nyalali mapema miaka ya 1990. Sheria hizi
ni kikwazo kwa upatikanaji wa haki za binadamu za wananchi. Mfano wa sheria
hizi ni Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, Kifungu Na 13 na 17, na Sheria ya
Uchaguzi ya mwaka 1985 na sheria zingine za Uchaguzi, kwa mfano kifungu cha
39(1)(f) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kifungu cha 7(1) cha Sheria
ya Taifa ya Uchaguzi na Kifungu (3)(a) cha Sheria ya Gharama za Uchaguzi
2010.
 Ufinyu wa bajeti unakwamisha utekelezaji wa majukumu ya Tume. Mara nyingi
Tume imekuwa ikitengewa bajeti ndogo kinyume na matakwa ya Kanuni za Paris
zinazotaka Serikali kutenga bajeti ya kutosha kwa taasisi za kitaifa za haki za
binadamu ili kuzihakikishia uhuru wake kiutendaji. Na hili linaikwamisha Tume
kuchukua hatua za haraka mara tu tukio la uvunjwaji wa haki za binadamu
linapotokea, mfano mauaji ya watu, albino katika sehemu mbalimbali nchini.
Vilevile kuwa na vitendea kazi na watumishi wa kutosha na kufungua ofisi nyingi
zaidi za matawi.

 Kukosekana kwa nguvu ya kisheria kuhusu utekelezwaji wa mapendekezo na


maamuzi ya Tume.

 Mgongano kati ya sheria za haki za binadamu na mila na desturi na mawazo


potofu ya baadhi ya wanasiasa na maafisa wa Serikali ya kuwa THBUB
inachochea mizozo kati ya Serikali na wananchi.

 Kutojadiliwa kwa taarifa za mwaka za Tume Bungeni. Tangu kuundwa kwa


Tume, ni mara moja tu taarifa zake ziliwasilishwa na kujadiliwa na bunge, ingawa
sheria iliyounda Tume awali ilitaka taarifa hizo ziwasilishwe na kujadiliwa
bungeni. Lakini baada ya mabadiliko ya mwaka 2004 ya sheria iliyounda Tume,
taarifa za Tume sasa zinaweza kuwasilishwa bungeni, lakini hakuna msukumo wa
kisheria wa taarifa hizo kujadiliwa. Mpaka sasa, mapendekezo mengi ya Tume
kwa Serikali yanatekelezwa, lakini kukosekana kwa mijadala juu ya taarifa zake
bungeni ni mapungufu. Mapendekezo ya Tume ya Rais juu ya mfumo wa kisiasa
unaofaa kati ya chama kimoja au vyama vingi (Tume ya Nyalali) yalitaka Tume
iwajibike kwa Bunge.

 Kutofikika kirahisi kwa Tume kutokana na huduma zake kuwa mbali na wananchi
walio wengi. Nchi inayokadiriwa kuwa na watu milioni 50 inatarajiwa

20
kuhudumiwa na Tume yenye ofisi sita tu zilizopo Dodoma, Dar es Salaam,
Zanzibar, Mwanza, Lindi na Pemba.

2.10 Mipango ya baadaye


Ili kuondokana na changamoto zilizobainishwa hapo juu na hivyo kufikia ndoto yake
ya kuwa na jamii yenye utamaduni ambao unakuza na kulinda haki za binadamu na
misingi ya utawala bora, Tume inayo mipango mingi. Baadhi ya mipango hiyo ni
ifuatayo:
 Kuongeza matumizi ya vyombo vya habari katika utoaji wa elimu kwa umma.
Kuwa na programu ya mafunzo juu ya haki za binadamu na utawala bora kwa
waandishi wa habari ili kuwajengea uwezo katika nyanja hizo. Vilevile kuandaa
na kurusha vipindi vingi zaidi vya Runinga na Radio vya elimu ya haki za
binadamu na utawala bora.

 Kuendelea na mchakato wa kuhakikisha kuwa elimu ya haki za binadamu na


utawala bora inaingizwa katika mitaala ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya
elimu ya juu. Hili litafanywa kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia na wadau wengine. Aidha, Tume itaendelea na mpango wake wa
kuanzisha klabu za haki za binadamu na utawala bora katika shule na vyuo na
kushirikiana na AZAKI katika kutoa elimu ya haki za binadamu na misingi ya
utawala bora kwa umma.

 Kuhusu sheria zinazovunja haki za binadamu na kukiuka misingi ya utawala bora,


Tume inatarajia kufanya tafiti zitakazosaidia kuzijua, kuzifanyia mapitio na
hatimaye kutoa mapendekezo kwa Serikali ili iweze kuzirekebisha au kuzifuta
kabisa.

 Tume inatarajia kutengeneza mkakati na mwongozo wa kufuatilia na kutathimini


masuala ya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala
bora.

 Pia tume inatarajia kufungua ofisi zaidi katika ngazi ya kanda na baadaye mikoa
kwa lengo la kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

 Kuongeza idadi ya watumishi na vitendea kazi kwa lengo la kuongeza ufanisi.

 Kuendelea na utekelezaji wa mkakati wa ushirikiano na wadau wa ndani na nje ya


nchi. Katika kulitekeleza hili Tume inatarajia kuwa na mawasiliano ya mara kwa
mara na wadau wake, kuwa na semina na mikutano ya uhamasishaji na vilevile
kuonana na kuongea na viongozi mbalimbali wa taasisi za umma.

 Kufanya utafiti utakaosaidia kuipitia upya sheria ya Tume ya Haki za Binadamu


na Utawala Bora kwa lengo la kuiongezea Tume nguvu za kisheria na
kushughulikia vikwazo vilivyopo.

 Kuishawishi serikali na bunge waweze kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya


Tume ili iweze kutekeleza majukumu yake kadiri ya matarajio ya wananchi.
Aidha, Tume itafanya ushawishi zaidi kwa wadau wa maendeleo kwa ajili ya
kupata misaada zaidi ya kifedha na kiufundi.

21
22

You might also like