Kipindi Cha Ukimya (Miaka 400 Kati Ya Ak Na Aj

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 26

P.O.

BOX 1917 MBEYA TANZANIA


Email: Elamseminary@gmail.com. Tel 0762532121

Kuwaandaa Watendakazi Kwaajili Ya Mavuno Ya Nyakati Za Mwisho


LUKA 10:2

MIAKA 400 KATI YA AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA

Msingi wa Kujenga Watendakazi na Viongozi


Watumishi Wanaojizidisha na wenye Maono ya
Kuigusa Dunia Nzima.

Sura ya 1
Kilichotokeo Kati Ya Agano La Kale Na Agano Jipya

1
Dibaji
Miaka mia nne kati ya unabii wa Malaki na majilio ya Kristo huelezewa mara
nyingi kama “ya kimya” lakini ilikuwa imesongwa na shughuli.
Hakuna nabii ambaye maandiko yake umewekwa katika bibila aliyeinuka katika
Israeli wakati wa karne hizo. Agano la Kale lilidhaniwa limekamilika.
Lakini, matukio yaliyotokea ambayo yaliwapa Wayahudi wa wakati wa Kristo
namna yao kipekee ya imani. Kipindi hiki kiliandaa njia ya kuja kwa Kristo na
tangazo la Injili yake.

A. UFALME WA UAJEMI UNATAWALA YUDEA


Miaka kama 100 kabla ya kipindi hiki, Wayahudi walikuwa wamepelekwa
kwenye utumwa wa Babeli (Uajemi) (2 Fal 24:24, Yer 20:6). Uajemi ya
zamani ilijumuisha maeneo ambayo yapo leo katika mataifa ya Iraq na Iran.
Wayahudi walistawi vema wakati wa utumwa wao wa miaka sabini chini ya
utawala wa kiajemi. Mwishoni mwa miaka hii sabini, Koreshi, Mwana wa
Mfalme wa Uajemi, alikuwa amewapa ruhusa ya kurudi Yerusalemu na
kulijenga tena hekalu (linganisha na Yer 29:10 na Dan 9:2).
Ingawa walikutana na upinzani kutoka kwa wenyeji wa Palestina, hekalu
lilimalizika na kuwekwa wakfu wakati wa utawala wa Dario Mkuu
(Ezr 6:1-14).
Mwandishi Ezra na Nehemia, mlei, walitafuta kwa makini kuitia nguvu
jamii ya Wayahudi wa Palestina na kushawishi utii wao kwa sheria za
Mungu (angalia Ezra sura ya 10).
Baada ya wakati wa Nehemia, kwa kama karne moja na nusu, Ufalme wa
Uajemi ulitawala juu ya Yuda, na Wayahudi waliruhusiwa kuangalia
taratibu zao za dini bila kuingiliwa.
Yuda ilitawaliwa na makuhani wakuu ambao waliwajibika kwa serikali ya
Uajemi, jambo ambalo liliwahakikishia Wayahudi kiasi kikubwa cha uhuru
wa kujitawala wenyewe. Hata hivyo, wakati uo huo, ilifanya ofisi ya
ukuhani kuwa ofisi ya kisiasa na kupanda mbegu za shida ya baadaye.
Ushindani kwa ajili ya ofisi ya kuhani mkuu ulileta dalili za wivu, fitini na
hata mauaji.
Yohana, mwana wa Yoyada (Neh w2:22), anaripotiwa kumchinja Yoshua
ndugu yake ndani ya ua wa hekalu.

2
Yohana alifuatiwa kama kuhani mkuu na ndugu yake Yadua, ambaye
Manase ndugu yake, kulingana na maandishi ya mwana-historia Yosefu,
alimwoa binti Sanbalati liwali wa Samaria.
1. Wasamaria Wajenga Hekalu.
Hekalu la Wasamaria juu ya Mlima Gerizimu lilijengwa wakati uo huo.
Hekalu hili, badala yake. Hili lilikuwa limeanzishwa na Yeroboamu
karne nyingi kabla, kufuatia kifo cha Mfalme Sulemani (Fal 12:25).
Hekalu juu ya Mlima Gerizimu liliharibiwa na mtawala wa Hasmonae,
John Hyreamus (134-104 K.K.). Mpaka katikati ya karne ya ishirini
(kama mwaka wa 1950), mabaki ya Wasamaria (kama 300 kwa idadi)
bado huufikiria Mlima huo kuwa wakfu.
Mwanamke Yule kwenye kisima cha Samaria alitaka kubishana na Yesu
kuhusu ustahili wa sehemu zile takatikfu zilizokuwa shindani. Mwokozi
Yesu alichagua kusisitiza nia ya moyo ya kiroho ya anayeabudu kuliko
mahali pa kuabudia (Yon 4:20).
Sanbalati ambaye Yosefu, aliandika juu naye hawezi kuwa mtu yule yule
mwenye jina hilo aliyetajwa na Nehemia (Neh 4:1). Hata hivyo Yosefu
anaelekea kuonyesha desturi thabiti, kwani inaelekea dhahiri kwamba
hekalu lilijengwa juu ya Mlima Gerizimu karibu wakati huu.
Kushindwa kwa Uajemi kutokomeza Uyunani kuliwatia moyo watu
wengi walioshindwa kutafuta uhuru wao. Misri ilikuwa daima ikijitahidi
kuitupilia mbali nira ya Uajemi. Yuda, iliyo kati ya Misri na Uajemi
kijiografia, isingeweza kukwepa kuhusika.
2. Wayahudi Wahamia Pengine
Wakati wa utawala wa Ahasuero III, Wayahudi wengi walitiwa hatiani
katika uasi dhidi ya Uajemi. Uasi uliposhindwa, Waajemi
waliwahamishia Babeli na mwambao wa kusini mwa Bahari ya Kaspiani.
Wayahudi walikuwa wamekimbilia Misri wakati wa Yeremia, karne
moja au zaidi kabla. Kufuatia mauaji ya Gedalia, nabii Yeremia
alilazimika kujiunga na kundi la wakimbizi waliotafuta hifadhi
Tahpenesi, mji, wa Misri, katika mashariki ya maingilio ya mto baharini
(Yer 43:4-13). Bila shaka watu wengine wa Yuda walipata njia yao
kwenda Misri kuepuka kutekwa na Nebukadreza.
Kuhama kuliendelea wakati wa Kipindi cha Uajemi, na kufikia karne ya
tano kabla ya Kristo koloni la askari wa Kiyahudi wa kukodiwa

3
liliwekwa kwenye kisiwa cha Elefantino karibu na Aswani ya leo,
kwenye Maanguko ya kwanza ya Mto wa Naili.
Kinyume na Sheria ya Musa, wakoloni, hawa walijenga hekalu kwa ajili
yao,wenyewe na walichanganya ibada yao kwa Mungu wa baba na
mambo ya kipagani (Yer 44:15-19). Wayahudi wa Elefantino walikuwa
na mwafaka na Wasamaria pamoja na Yuda pia.

B. ISKANDA MKUU
Uajemi haikufanikiwa kamwe katika kuwatiisha Wayunani, lakini mrithi
mwenye mila ya Kiyunani, Iskanda wa Makadonia, hatimaye aliteta mwisho
wa ufalme wa Uajemi.
Iskanda hakuwa tu mtawala fidhuli mwendawazimu wa mamlaka. Akiwa
mwanafunzi wa mfalsafa Aristole, alisadiki kabisa kwamba mila ya
Kiyunani ilikuwa ndiyo nguvu ambayo ingeunganisha ulimwengu.
Mwaka wa 33 K.K. alipita kutoka Makadonia kuingia Asia Ndogo na
akayashinda majeshi ya Uajemi yaliyowekwa pale. Halafu alielekea kusini
kupitia Shamu na Palestina mpaka Misri.
Tiro na Gaza ilitoa upinzani mgumu, lakini vizuio havikumkatisha Iskanda
tamaa; vilitia tu nguvu nia yake ya kushinda tu.
1. Rafiki Wa Wayahudi
Hapakuwepo na haja ya vita virefu dhidi ya Wayahudi na, simulizi
humfanya Iskanda rafiki wa watu wa Kiyahudi. Yadua, kuhani mkuu,
inasemekana alitoka kumlaki Iskanda, kumwambia juu ya unabii wa
Danieli kwamba jeshi la Kiyunani lingekuwa washindi (angalia Daniel
sura ya 8).
Ingawa wana historia hawakichukiulii kisa hiki kwa uzito, kinafafanisha
hisia za kirafiki kati ya Wayahudi na mshindi wa Makadonia.
Iskanda aliruhusu Wayahudi kuadhimisha sheria zao, akiwaruzuku
kuachiliwa ushuru wakati wa Miaka ya Saba (Miaka ya Sabato) .
alipojenga mji wa Iskanda kule Misri (331K.K.), aliwashawishi
Wayahudi kuishi pale na aliwapa heshima zilizolingana na raia wake wa
kiyunani.
2. Aliwashinda Waajemi
Iskanda alikaribishwa Misri kama mkombozi kutokana na uonevu wa
Uajemi.

4
Majeshi yake ya ushindi yalifuatilia tena hatua zao kupitia Shamu na
Palestina, halafu yakaendelea mashariki. Miji ya Babeli (Iraq) na Uajemi
(Iran) ilianguka kwa Iskanda, na alisonga kuelekea mashariki mbali
mpaka jimbo la Punjab, India.
3. Urithi Wa mila Ya Kiyunani
Ingawa alikuwa na nguvu kwenye mapambano ya kivita, urithi wa
Iskanda kwa Mashariki ya Kati ulikuwa ni mila ya ki-Hellenisti
(Kiyunani) zaidi kuliko utawala wa ki-Makadonia.
Alikusudia kuanzisha mji mpya katika kila nchi ya ufalme wake ambao
ungetumika kama mfano kwa ajili ya kuweka upya utaratibu wa maisha
ya nchi kwa ujumla kufuatisha namna ya Kiyunani.
Kusema kuhusu vitu, hii ilimaanisha kujenga nyumba nzuri za umma,
viwanja vya michezo, mahali pa kuonyeshea maigizo hadharani, na
chochote ambacho kingefaa maisha kwenye mji/jimbo la Kiyunani.
Watu binafsi walishawishiwa kuchukua majina ya kiyunani, kutumia
mavazi ya Kiyunani na lugha ya Kiyunani – yaani, kufanyika Mheleni.
Lazima mandhari ya vitu vya Uyunani yalikuwa yanaelekea kuwa ya
kuvutia kwa sehemu kubwa za watu.
Biashara na uchumi vilileta utajiri kwa tabaka jipya la wafanya biashara.
Maktaba na shule zilipokelewa na wataalamu. Nyumba nzuri zaidi na
chakula kizuri zaidi vilisababisha kupanda kwa viwango vya kuishi.
Wengi katika Israeli, kama penginepo, walifurahi kupokea urembo huu
wa mila ya Kiyunani. Kama ibada ya sanamu ilikuwa kizuio cha
kujikwaa kwa Israeli katika kipindi cha kabla ya uhamisho, mila ya
Kiyunani ilikuwa jaribu kubwa la baada ya uhamisho.
Mwandishi wa karne ya tatu K.K. alisema, “Katika nyakati karibu, chini
ya utawala wa kigeni wa Waajemi na halafu wa Wamakedonia, ambao
kwao Ufalme wa Uajemi uliangushwa, kujiliana na mataifa mengine
kumesababisha sheria nyingi za desturi za Kiyahudi kupoteza msimamo
wake.”
Wayahudi wengi walichukua majina ya Kiyunani, waliikubali elimu
fulani ya falsafa ya kiyunani, na walijaribu kuchanganya hekima ya
Uyanani (Uhellenisti) pamoja na imani ya babu zao. Wengine walikataa
mvuto wa Uyunani na wakawa wanajishughulisha zaidi na zaidi katika
kujifunza Sheria yao.
Iskanda alifia Babeli, akiwa na umri wa miaka thelathini na tatu.

5
Kwa miaka kadhaa hatima ya Mashariki ya Karibu ilikuwa haina
uhakika, lakini amiri jeshi walifanikiwa kwenye kuugawa ufalme baina
yao wenyewe na wimbi la Uyunani (Uhellenisti) lililoongezeka.
Wakati Watolemayo wa Misri na Waseleusidi wa Shamu walipopigana
baina yao wenyewe kwa ajili ya ardhi na mamlaka, walikuwa katika
kukubaliana kabisa kuhusu ujumbe wa kijamii na mila.
Mwana historia W.W. Tarn husema kwamba Iskanda “aliubadilisha
ulimwengu kiasi kwamba baada yake hakuna kitu kingeliweza kuwa
kama kilivyokuwa kabla.”

C. WATOLEMAYO
Kufuatika kifo cha Iskanda, Yuda ilikuwa kwanza chini ya Antigoni, mmoja
wa amiri jeshi wake. Lakini iliangukia mikononi mwa amiri jeshi mwingine
kwa haraka, Tolemayo I, ambaye jina lake la ukoo, Sota, ilimaanisha
“Mkombozi”. Alitwaa Yerusalemu kwa nguvu siku ya Sabato mwaka wa
320 K.K.
1. Wayahudi Walistawi
Tolemayo, ambaye ufalme wake ulikuwa na makao yake makuu Misri,
aliwatendea Wayahudi huruma. Wengi wao walikaa katika mji wa
Iskanda – ambao uliendelea kuwa kiini cha wazo la Kiyahudi kwa karne
nyingi.
Chini ya Tolemayo II (Filadelfi) Wayahudi wa Iskanda walitafsiri
Agano la Kale lao la Kiebrania kwa Kiyunani. Tafsiri hii ilijulikana
baadaye kama Septuaginta – Agano la Kale la Kiyunani (neno
“septuaginta” likitafsiriwa humaanisha “sabini”).
Jina hili lilitokana na Wayahudi sabini waliopelekwa toka Yuda kutoka
tafsiri ya kweli walikuwepo sabini na wawili – sita kutoka kila ya
makabila kumi na mawili.
Wayahudi wa Palestina walifurahia kipindi cha mafaniko wakati wa enzi
za utolemayo. Ushuru ulilipwa kwa serikali kule Misri. Lakini mambo ya
mahali pale yalisimamiwa na makuhani wakuu ambao walikwisha kuwa
wakiwajibika na kutawala watu wao tangu nyakati za utawala wa
Uajemi.
Mtu maarufu kuliko wote kati ya Wayahudi wa kipindi cha Talemayo
alikuwa ni Simoni Mwaadilifu, kuhani mkuu. Yeye ni mtu wa sifa ya

6
juu mno katika Kitabu cha Eklesiastika cha Apokrifa, ambacho humwita
yeye, “Mkuu kati ya ndugu zake na utukufu wa watu wake.”
Anaheshimiwa kwa kujenga tena kuta za Yerusalemu ambazo zilikuwa
zimebomolewa na Tolemayo I. ilisemekana alilikarabati Hekalu na
akaelekeza kuchimbwa kwa bwawa kubwa la kuweka maji safi kwa ajili
ya Yerusalemu wakati wa ukame na mazingiwa.
Kwa kuongezea kwenye sifa yake kama kuhani mkuu, vile vile Simoni
aliheshimiwa kama mmoja wa waalimu wakuu wa Yuda wa zamani.
Msemo wake kipenzi wa hekima ulikuwa, “Ulimwengu hutegemea
mambo matatu: Sheria, Utumishi wa ki-Mungu na Huruma.”
Hata hivyo, utambulisho wa Simoni Mwadilifu hutia tatizo la kihistoria.
Kuhani mkuu aliyejulikana kama Simoni I aliishi kipindi cha katikati cha
karne ya tatu, na Simoni II aliishi kama mwaka wa 200 K.K. Bila shaka
mmojawapo wa hawa ni Simoni Mwaadilifu wa desturi na hadithi za
Kiyahudi lakini hatuju ni yupi.
2. Ushindani Kutokea Kati Ya Jamii Za Kikuhani
Wakati wa nyakati za Utolemayo, jamii za kikuhani za Oniasi na Tobia
zilifanyika washindani wakali. Jamaa ya Tobia ilikuwa ikivutia kwao
Misri na iliwakilisha tabaka tajiri la jamii ya Yerusalemu. Familia ya
Tobia inaweza kuwa ilihusiana na Tobia Mwamoni (Neh 2:10; 4:3, 7;
6:1-19) ambaye alimtaabisha mno Nehemia.
Karatasi (mabua ya mafunji yaliyolengwa) kutoka wakati wa Tolemayo
II husema juu ya Myahudi aliyeitwa Tobia ambaye alikuwa mkuu wa
askari wapanda farasi katika jeshi la ki-Tolemayo lililowekwa pale
Ammanisiti, mashariki tu ya Mto Yordani.
Maarifa ya mambo ya kale yamegundua kaburi kubwa zuri kutoka karne
ya tatu K.K. pale Arag el-Emir kule kati ya nchi ya Yordani, likiwa na
jina “Tobia.” Hudhaniwa Watobia walikuwa wakusanya kodi,
walishikilia kazi ile ile kama watoza ushuru wa Agano Jipya.
Yosefu husimulia kwamba Oniasi II alikataa kumlipa Tolemayo IV
talanta ishirini za fedha, ambazo zilikuwa ushuru dhahiri uliodaiwa kwa
makuhani wakuu. Kwa kukataa kulipa inaelekea kwamba Oniasi
alikwisha vunja utii aliopaswa kwa mfalme Tolemayo.
Yusufu mshiriki wa nyumba ya Tobia, basi alifanikiwa kujifanya
mwenyewe ateuliwa “mkulima mtoza kodi” kwa Palestina yote. Ilibidi
mkulima mtoza kodi aende kila mwaka Iskanda kuzabuni upya leseni ya

7
kukusanya kodi. Yusufu alishika nafasi hii yenye ushawishi mkubwa kwa
miaka ishirini, chini ya Tolemayo na chini ya Seleusidi, baada ya ushindi
wa Antioko III.

D. WASELEUSIDI
Watawala wa kipindi hiki wa Shamu huitwa Waleleusidi. Hiki ni kwa
sababu ufalme wao, moja ya majimbo yalifuatia ufalme wa Iskanda Mkuu,
ulianzishwa na Seleusidi I (aliyeitwa pia Nikatori).
Watawala wengi wa kipindi hicho walichukuwa jina la Seleusidi au Antioko
kwenye Mto Oronte.
1. Mila Ya Kiyunani Kulazimishwa Juu Ya Wayahudi.
Mtawala Antioko III mwenye tamaa ya nguvu, aliyepewa jina la ukoo
“Mkuu”, alifanya mfulilizo wa mapambano na Misri. Mwaka wa 199
K.K. alitwaa Palestina kutoka kwa Watolemayo baada ya Pambano la
Panioni, karibu na vyanzo vya Mto Yordani.
Hii iliweka alama ya mwanzo wa kipindi kipya cha historia ya Kiyahudi.
Wakati Watolemayo walikuwa wavumilivu kwa mambo ya Kiyahudi,
Waseleusidi walikusudia kuimarisha Uyunani juu ya wayahudi.
Mzozo ulikuja wakati wa utawala wa Antioko IV, aliyejulikana vema
kama Antioko Epifani. Alipata marafiki katika chama cha Kiyunani
katika Yuda.
Katika siku za mwanzo za utawala wa Antioko IV, Yerusalemu
ulitawaliwa na kuhani mkuu Oniasi III, mjukuu wa Simoni Mwaadilifu,
Myahudi mwenye imani iliyoshika mapokeo ya kisheria sana.
2. Ukuhani Kuenda Kwa Mzabuni Wa Juu Mno
Wayahudi ambao walipendelea mila ya Kiyunani walimpinga Oniasi na
walisaidia hoja ya Yasoni ndugu yake. Kwa kuahidi ushuru mkubwa kwa
Antioko, Yasoni alifanikiwa katika kufanya achaguliwe mwenyewe
kuhani mkuu.
Ingawa Antioko aliuona ukuhani mkuu kama wadhifa wa kisiasa ambao
yeye alikuwa na haki ya kumweka mtu yeyote kwenye nafasi hii kama
apendavyo, Wayahudi wacha Mungu walifaikiri juu ya ukuhani kama
wenye chanzo cha ki-Mungu na walidhani uuzaji wake kwa mzabuni wa
juu mno ulikuwa ni dhambi dhidi ya Mungu.
Yasoni aliwatia moyo Wayahudi wa ki-Yunani waliokuwa wametafuta
uchaguzi wake. Uwanja wa michezo ya mazoezi ya viongo vya mwili

8
ulijengwa Yerusalemu, majina ya Kiyunani yalikuwa jambo la kawaida
na kiustadi katika Yuda kulidhaniwa ni kutiwa giza na kikale tu.
Bado Yasoni alishindana na rafiki yake wa karibu na Mhellisti (Myahudi
wa ki-Yunani) mwenzake, Menelau wa kabila la Benjamini. Kulingana
na Maandiko ya Agano la Kale ni Walawi tu walikuwa wawe makuhani.
Menelau Mbenjamini alitoa ahadi kwamba angelipa ushuru wa juu zaidi
kwa Antioko kuliko ule uliolipwa na Yasoni, na akajisabisha asimikwe
kama kuhani mkuu.

3. Imani Sahihi Ya Kiyahudi Ilishambuliwa


Wayahudi wenye imani, katika mapokeo yao ya kisheria ambao
walikuwa wameaibishwa wakati Yasoni alipowekwa kuhani mkuu,
walisumbuliwa kwa undani zaidi wakati Menelau, Mbenjamini
asiyekuwa na haki ya wadhifa wa kuhani, aliposimikwa.
Yasoni aliunda jeshi kutetea dai lake la kurudia ukuhani mkuu, na
Menelau alipata upendeleo wa Antioko.
Washamu ambao walikuwa wakigombea Misri waliona ni muhimu
kushikilia utawala wa kufaa juu ya Palestina. Hivyo, Antioko Epifani
alifanya shambulio kwa siri juu ya Yerusemu siku moja ya Sabato
(wakati Wayahudi walioendelea kushika mapokeo yao ya kisheria
wasingepigana), na akachinja idadi kubwa ya maadui wa Menelau.
Kuta za mji zilibomolewa na ngome mpya, Akra, alijengwa mahali pa
ngome ile.
Antioko alikusudia kuondoa dalili zote za imani ya dini ya Kiyahudi.
Alitangaza kwamba Yupita, mungu mkuu wa Wayunani aabudiwe kama
kwamba yeye ni sawa kabisa na Mungu wa Israeli.
Antioko aliweka sanamu yenye ndevu ya mungu wa kipagani (pengine
kwa sura Antioko) ikasimamishwa kwenye madhabahu ya Hekalu,
ambapo nguruwe alitolewa kama dhabihu.
Wayahudi walizuiwa, chini ya adhabu ya kifo, kufanya tohara,
kuadhimisha Sabato, au kusherehekea sikukuu tatu za mwaka wa kalenda
ya Kiyahudi. Nakala za Maandiko ziliamriwa kuchomwa.
Sheria hizi ziliwekewa nguvu kwa ukatili kabisa. Mwandishi mzee
aliyeitwa Eliezeri alipigwa mpaka akafa kwa sababu hangekula nyama ya
nguruwe.

9
Maenelau aliendelea kama kuhani mkuu kwa nguvu ya silaha na chama
cha kufanya Uyunani kilipata ushindi. Walakini, wafanya Uyunani
walikuwa wamepitiliza mno, na juhudi yao halisi ya kuangamiza
utaratibu wa zamani ilithibitisha angamizo lao wenyewe.
Waliokuwa wanashika imani ya zamani ya Israeli walikuwa tayari kufa
kwa ajili ya imani yao, lakini wengi walifikiri ni afadhali wafe wangali
wakijitahidi kuwashinda akina Menelau kwa nguvu.

E. UASI WA MAKABAYO
Wayahudi waliogandamizwa hawakuchukua muda mrefu kumpata shujaa
wao.
1. Matathia Aongoza Uasi
Wajumbe wa Antioko walipofika kwenye kijiji cha Modini, kama maili
kumi na tano magharibi ya Yerusalemu, walitarajia kuhani mzee,
Matathia kuonyesha mfano mzuri kwa watu wake kwa kuja mbele kutoa
dhabihu ya kipagani. Matathia alipokataa, Myahudi mwoga alikuja mbele
kutoa hiyo dhabihu.
Kuhani aliyeghadhibika aliisogelea madhabahu na aliwachinja wote
wawili, Myahudi kafiri na mjumbe wa Antioko. Pamoja na wanawe
watano, Matathia aliiharibu madhabahu ya kishenzi na halafu
wakakimbilia vilimani kuepuka kisasi.
Wengine walioshikilia imani ya kidesturi waliungana na familia ya
Matathia katika vita vya msituni kwa Washamu na Wayahudi wa
Uyunani ambao waliwaunga mkono.
Wenye kushikilia imani ya kidesturi hawangepigana siku ya sabato, na
matokeo yake ni kwamba walikuwa kwenye hasara dhahiri ya kijeshi.
Siku moja ya Sabato kikundi cha wenye kushikilia imani ya kidesturi
kilizungukwa na kuchinjwa, kwani hawangejiteka.

Baada ya tukio hili Matathia alipendekeza kanuni ya kwamba kupigana


kwa ajili ya kujitetea binafsi kunaruhusika siku ya Sabato. Ukweli una
njia ya kugeuza theologia zisizo za kimatendo.
2. Yuda “Mmakabayo” Aongoza Kwenye Ushindi
Mara baada ya mwanzo wa uasi, Matathia alikufa. Alikuwa
amewashawishi waufasi wake kuchagua mwanaye wa tatu Yuda

10
aliyejulikana kama “Mmakabayo” – kwa kawaida neno linatofasiriwa
kumaanisha “nyundo”, kama kiongozi wa vita.
Chaguo lilionekana kuwa zuri, kwa kuwa Wayahudi zaidi walikusanyika
kwa ajili ya jambo hilo.
Wamakabayo, kama wafuasi wa Yuda walivyoitwa, waliweza kujitetea
wenyewe dhidi ya mfululizo wa majeshi ya ki-Shamu yaliyotumwa dhidi
yao.
Yuda aliangamiza jeshi la Shamu na Wayahudi wa ki-Uyunani (ki-
Hellenisti) pale Emao kwa shambulio la kushitukiza usiku, na halafu
wakatembea kuelekea Yerusalemu na nyara alizokuwa ameziteka.
Wamakabayo waliuingia mji na kuteka kila kitu isipokuwa Akra.
Waliingia Hekaluni na kuondoa dalili zote za upagani ambazo zilikuwa
zimesimikwa pale. Madhabahu iliyowekwa wakfu kwa Yupita
iliondolewa na madhabahu mpya ikajengwa kwa Mungu wa Israeli.
sanamu ya Yupita ilisagwa ikawa mavumbi.
Kuanzia tarehe ishirini na tano ya mwezi wa Kislev (Desemba)
walisherehekea Sikukuu ya siku nane ya Kuweka Wakfu ijulikanayo
kama Hanukkah, Sikukuu ya Nuru.
(Angalia: Baadaye Wakristo walitwaa siku hii ya sikukuu na
kuiadhimisha kwa makosa kama siku ya kuzaliwa kwa Yesu.)
Kwa njia hii waliweka alama ya mwisho wa kipindi cha miaka mitatu
ambacho hekalu lilikuwa linafanywa najisi.
3. Washamu Kupata Tena Utawala
Hata hivyo, amani ilikuwa ya muda mfupi. Amiri Jeshi Lisia wa Shamu
aliwashinda Wamakabayo kwenye pambano karibu na Yerusalemu na
akauhusuru mji wenyewe. Hata hivyo, wakati wa kuuzingira mji Lisia
alipata habari za shida nyumbani na akafanya amani na Wayahudi.
Sheria dhidi ya kuadhimisha Uyuda zilibatilishwa na Shamu iliacha
kuingilia mambo ya ndani ya Yuda. Menelau alikuwa aondolewe
kwenye wadhifa na ukuhani mkuu upewe myunani mpole aitwaye
Alkimo.
Lisia aliahidi kwamba Yuda na wafuasi wake wasingeadhibiwa. Hata
hivyo, kuta za Yerusalemu zingebomolewa.
Baraza lililofanywa na maafisa wa jeshi la Wamakabayo, waandishi
walioheshimika na wazee wa chama cha wenye kushikilia imani ya
kidesturi ilikutana Yerusalemu kuamua jambo la kuafanya.

11
Patano la amani lilikubaliwa dhidi ya ushauri wa Yuda. Alkimo
alifanywa kuhani mkuu; Menelau aliuawa; na Yuda aliondoka mjini na
wafuasi wachache. Hofu za Yuda zilidhibitika sahihi kwani Alkimo
aliwateka na kuwaua wengi wa chama cha wenye kushikilia imani ya
kidesturi.
4. Vita vya Wenyewe Kwa Wenyewe Kuanzishwa Tena
Wayahudi waaminifu walimgeukia tena Yuda na vita vya wenyewe kwa
wenyewe vikaanza tena. Akiwa na jeshi la watu mia nane ambalo
haliliandaliwa vema, Yuda alikutana na jeshi kubwa la Shamu na akafa
kwenye pambano. Kwa hiyo awamu ya kwanza ya pambano la
Makabayo ilikwisha.
Yonathani, ndugu yake Yuda, alikimbilia ng’ambo ya Mto Yordani na
mamia kadhaa ya askari wa Makabayo. Hawakuwa wameandaliwa vema
kufanya mapambano, lakini ushindi mwingine uliofuata ulikuwa katika
nyanja za upatanishi.
Watu wawili waliokuwa wakidai kiti cha enzi cha Shamu walitafuta, kila
mmoja, kwa makini msaada wa Wayahudi. Waliona kwamba Yohathani
ndiye mtu mzuri mno mwenye kuweza kuliinua na kuliongoza jeshi la
Kiyahudi. Kwa kufanya mbinu ya kuchelewesha, Yonathani aliweza
kumwunnga mkono Yule aliyeshinda kupata kiti cha enzi na wakati uo
huo kufanya mapatano na Sparta na Rumi.
Yonathani alikuwa kuhani mkuu, liwali wa Yuda na mshiriki wa watu
wenye cheo wa Shamu kabla ya vita kumalizika. Ndugu yake Simoni
alikuwa liwali wa eneo la pwani ya Filisti. Yonathani aliweza kuendeleza
mafanikio ya ndani ya Uyahudi, na alipokufa, Simoni ndugu yake
alimfuatia kama kuhani mkuu anayetawala.
Simoni alikuwa mtu wa umri mkubwa alipokuja kwenye kiti. Ushindi
wake mkuu ulikuwa katika nyanja za upatanishi. Kwa kumtambua
Demetrio kama mfalme halali wa Shamu, aliwapatia Wayahudi ruhusa
ya kutokulipa kodi ambayo ilikuwa ni sawasawa na kuwapa Wayahudi
uhuru.
Simoni aliweza kuishindisha ngome ya Shamu njaa pale Akra na kukalia
miji ya Joppa na Betsura. Kwa kutambua utawala wake wa busara
viongozi katika Israeli walimtaja Simoni kuwa “kingozi na kuhani mkuu
daima, mpaka atakapoinuka nabii mwaminifu.”

12
Simoni alikuwa mwana wa mwisho wa Matathia, na jambo hili
lilihalalisha nasaba mpya ya kifalme ambayo iliitwa ya ki-Hasmonae,
pengine ilitokana na babu wa Wamakabayo aliyeitwa Asmonae au, kwa
Kiebrania, Hashmoni.
Mwaka wa 134 K.K. Simomi na wanawe wawili waliuawa na mkwe
wake mwenye tamaa. Mwana wa tatu Yohana Hirkanu, aliweza
kutoroka na kutawala baada ya baba yake kama mtawala wakurithi wa
nchi ya Kiyahudi.

F. WAHASMONAE
Washamu waliitambua Serikali ya Yohana Hirkanu kwa masharti kwamba
angejitambua mwenyewe kuwa chini ya Shamu na kuahidi kusaidia katika
shughuli za kivita za Shamu.
Miji fulani fulani ya pwani iliyotaliwa na Yonathani na Simoni ilikuwa pia
iachwe. Utawala wa Hirkanu wenye kufaa, hata hivyo, uliwezesha kuteka
tena miji hii kwa haraka na nyongeza ya Idumaya (Edomu katika Agano la
Kale) kwenye himaya ya Idumaya.
Ushindi huu wote ulihakikisha matumizi ya njia za zamani za biashara,
lakini ulileta matatizo kwa Wayahudi walioelekezwa kidini.
1. Hirkanu Aongeza Mipaka Ya Nchi Ya Kiyahudi
Hirkanu aliwalazimisha Waidumaya kutahiriwa na kukubali imani ya
Kiyahudi, mazoea ambayo Uyuda uliyaondolea nadhiri baadaye. Ni
dhihaka kumfikiria mjukuu wa Matathia akilazimisha ulinganifu wa
kidini juu ya watu walioshindwa kwa silaha za kiyahudi!
Hirkanu aliendesha vita pia Samaria ambapo aliliharibu hekalu juu ya
Mlima Gerizimu. Kufanikiwa kwa silaha za Kiyahudi kungeweza
kushangiliwa na malimwengu ya kitaifa katika Yuda, lakini ile juhudi ya
kidini ya Wamakabayo wa mwanzo haikuwa dhahiri tena.

a. Kuinuka Kwa Masadukayo.


Wayunan i wa zamani walidharauliwa, lakini mawazo yao
yaliendelezwa katika chama cha Masadukayo. Wenye kushikilia
imani ya kidesturi ya nyakati za Wamakabayo walifanyika Mafarisayo
wa Uyuda wa kabla ya Kristo na wakati wa Agano Jipya.

13
Hirkanu binafsi, alikuwa mtawa na mshika sheria, lakini watoto wake
walikuwa na huruma kidogo na wazo la kidesturi la Kiyahudi.
Walijihesabu wenyewe kwenye tabaka la watu bora na waliwabeza
Wayahudi wenye kushikilia imani ya kidesturi sana. Kama dhihaka,
hawa warithi wa Wamakabayo walifanyika Wayunani hasa!
2. Upanuzi Wa Himaya Ya Yuda Kuendelea
Kifo cha Yohana Hirkanu kilileta mara ushindani wa nasaba ya kifalme
baina ya watoto wake. Mwanaye mkubwa ambaye alipenda jina lake la
Kiyunani Aristobulu kuliko jina lake la Kiebrania , Yuda, alitokeza
kama mshindi. Aliwatupa ndugu zake watatu gerezai – ambao wawili
kati yao inafikiriwa walikufa kwa kukosa chakula. Ndugu mwengine
aliuawa kwenye nyumba ya mfalme.
Katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja tu wa utawala, Aristobulu
alisukuma mipaka ya Yuda kaskazini mpaka Lebanoni akajichukulia
mwenyewe jina la Mfamle. Hata hivyo, maisha yake yalifupishwa na
ulevi, ugonjwa na hofu ya mara kwa mara ya maasi.
Wakati wa kifo cha Aristobulu, alikuwa na kaka mmoja tu hai naye
alikuwa gerezani. Ingawa jina lake la Kiebrania lilikuwa Yonathani,
historia humfahamu kwa jina lake la Kiyunani, Iskanda Yannae. Chini
ya Yannae sera ya kupanua mipaka ya nchi iliendelea. Mipaka ya Yuda
ilipanuliwa kando ya pwani ya Filisti kuelekea mipaka ya Misri na nchi
za ng’ambo ya Yordani.
Kwa wakati huu, nchi ya Kiyahudi ilikaribia nchi iliyotawaliwa na Israeli
katika siku za Daudi na Sulemani. Ilikuwa ni pamoja na Palestina yote na
maeneo yanayopakana nayo kutoka mipaka ya Misri mpaka Ziwa Hulei,
kaskazini mwa Bahari ya Galilaya. Perea ng,ambo ya Yordani ilikuwa
chini ya bonde la Pwani isipokuwa Askaloni.
Nchi zilizounganishwa kwenye ufalme wa Wahasmonae kwa sehemu
kubwa ziliingiziwa Uyuda haraka.
Waidumeya walifanyiza sehemu muhimu katika maisha ya Kiyahudi na
Galilaya ilifanyika kiini muhimu cha Uyuda.
Wasamaria, hata hivyo, walikataa kuchangamana na miji kama vile
Apollonia na Shithopoli (Beth-shani katika Agano la Kale), ikiwa na
sehemu ndogo tu ya Kiyahudi katika watu wake, ilitunza tabia ya
Kiyahudi.

14
a. Uasi Wa Mafarisayo. Hata hivyo, mashindano kati ya wafuasi wa
kidini yalichafua utawala wa Iskanda Yannae, ambaye alionyesha
dharau ya wazi kwa Mafarisayo, iliyoanzisha vita vya ndani.
Mafarisayo walikubali msaada kutoka kwa Washamu katika ugomvi
wao na Yannae na uhuru wa Wayahudi uliogopewa.
Mafarisayo walipojisikia kwamba walikuwa wamepata jambo lao,
waliacha urafiki wao na Shamu na wakatumaini kuwa na nchi ya
Kiyahudi ambayo ingekuwa huru kutokana na utawala wa kigeni na
itakayovumilia msimamo wao. Hata hivyo, Yannae aliwatafuta kwa
makini viongozi wa uasi na aliwasulubisha Mafarisayo mia nane.
3. Salome Iskandra Atawala
Mapokeo husema kwamba Yannae alitubu kwenye kitanda chake cha
kifo, akimwagiza Salome Iskandra, mke wake kufukuza washauri wake
wa ki-Sadukayo na atawale pamoja na Mafarisayo. Mapokeo haya
yanaweza kuwa na msingi mdogo wa kihistoria, lakini Iskandra
aliwageukia Mafarisayo kwa msaada.
Salome Iskandra alikuwa ameolewa kwa mfululizo na Aristobulu na
Iskanda Yannae. Mjane huyo wa watawala wawili wa ki-Hasmonae,
alitawala kwa haki yake mwenyewe kwa miaka saba. Alipokalia kiti cha
utawala alikuwa mwanamke wa miaka sabini, akigawa wajibu wa
kifalme kati ya wanawe wawili Hirkanu (II), mwana mkubwa alkuwa
Kuhani Mkuu, na ndugu yake Aristobulu (II) alipokea utawala wa jeshi.
Ndugu yake Simoni bin Shetah, alikuwa kiongozi kati ya Mafarisayo, na
jambo hili linaweza kuwa lilimwelekeza Iskandra kutafuta amani kati ya
makundi mawili ya Uyuda yaliyokuwa yanapingana.
a. Mafarisayo Wapata Nguvu. Chini ya Iskandra, Mafarisayo
walikuwa na nafasi ya kufanya mchango wa kujenga kwenye maisha
ya Kiyahudi. Katika maeneo mengi, hasa elimu, walifanikiwa kabisa.
Chini ya urais wa Simoni bin Shetah, Sanhedrin (Baraza la Kiyahudi
la Kiyahudi la Nchi) lilitangaza kwamba kila kijana asomeshwe.
Utaratibu kamili wa elimu ya shule ya msingi ulianzishwa ili kwamba
vijiji vilivyokuwa vikubwa zaidi, miji na miji mikuu ya Yuda
ingeweza kutoa watu wasomi, waliofunzwa. Kiini cha elimu hii
kilikwa ni Maandiko ya Kiebrania.
Vidonda vya ugomvi wa zamani havikuponywa wakati wa utawala wa
Iskandra.

15
Ingawa Mafarisayo walifurahi katika kutambuliwa kwao kupya
kulikopatikana, Masadukayo walichukizwa kwamba walikuwa
wamepoteza nguvu yao. Kukuza tatizo, Mafarisayo walitafuta
kulipiza kisasi cha mauaji ya viongozi wao na Iskanda Yannae. Damu
ya Masadukayo ilimwagwa na kuwa ishara ya vita vingine vya
wenyewe kwa wenyewe.
Masadukayo walimpata Aristobulu, mwana mdogo wa Yannae na
Iskandra, kuwa mtu ambaye wangemsaidia kumrithi Iskandara.
Alikuwa askari na alitazamisha kwa chama ambacho kilikuwa na
njozi za upanuzi wa ufalme wote na utawala wa ulimwengu.
Hirkanu, kaka mkubwa na mwenye haki ya urithi wa ufalme
alikubalika kwa Mafarisayo. Pamoja na kifo cha Iskandra, wafuasi
wenye upendeleo tofauti kwa wana hao wawili walikuwa tayari kwa
pambano.
b. Uasi wa Masadukayo. Mama yake alipokufa, Hirkanu (II)
aliyekuwa akitumika kama kuhani mkuu, alifuatia kwenye kiti cha
utawala, lakini Aristobulu ndugu yake aliongoza jeshi la Masadukayo
dhidi ya Yerusalemu.
Hirkanu na Mafarisayo hawakuwa tayari kwa vita hivyo Hirkanu
alisalimisha heshima zake kwa Aristobulu (II) aliyefanyika mfalme
na kuhani mkuu.
Kutoka hapo hirkanu na Aristobulu waliwekeana nadhiri ya urafiki wa
milele na mtoto mkubwa wa Aristobulu, Iskanda alimwoa Iskandra
binti pekee wa Hirkanu.
Hata hivyo, amani kati yao ndugu ilikuwa ya muda mfupi. Ilibidi
Hirkanu akimbie na Antipa liwali wa Idumaya alifuatilia shauri lake.
Likiwepo tishio la vita vya ndani, Pompei alitokea na Majeshi yake
ya Kirumi kuhakikisha amani ya Yuda na kuendeleza makusudi ya
Rumi.

G. WARUMI
Pompei alipomhisi Aristobulu akipanga uasi dhidi ya Rumi, aliuzingira
Yerusalemu na baada ya miezi mitatu, alivunja ngome, akauingia mji, na
inasemekana aliwachinja Wayahudi elfu kumi na mbili.

16
1. Uhuru Wa Kiyahudi Wapotea
Pompei na maafisa wake waliingia Patakatifu pa Patakatifu katika
Hekalu lakini hakugusa mapambo yake ya gharama na aliruhusu ibada ya
hekalu kuendelea. Hata hivyo Yerusalemu, ilifanywa tawi kwa Warumi
na dalili za mwisho wa uhuru wa Kiyahudi ziliondolewa.
Yuda ilichanganywa kwenye jimbo la Kirumi la Shamu na ilipoteza miji
mikuu ya pwani, wilaya ya Samaria na miji isiyo ya Kiyahudi mashariki
mwa Mto wa Yordani.
Hirakanu aliitwa Ethnarki (mtawala) wa Yuda, pamoja na Galilaya,
Idumaya na Perea, na alithibitishwa tena kama kuhani mkuu. Ushuru wa
mwaka ulikuwa ulipwe kwa Rumi.
Aristobulu na idadi ya mateka wengine walipelekwa kwa Rumi
kufaharisha ushindi wa Pompei. Wakati wa safari, hata hivyo, mwana wa
Aristobulu, Iskanda alitoroka na akajaribu kupanga uasi dhidi ya
Hirkanu. Hata hivyo kwa msaada wa Warumi, Hirkanu aliweza kuikidhi
changamoto hiyo kwa mamlaka yake.
2. Antipa: Nguvu Nyuma Ya Kiti Cha Enzi Cha Kiyahudi
Wakati wa miaka ya ugomvi kati ya Aristobulu (II) na Hirkanu (II),
liwali wa Idumaya Antipa (au Antipasi) alijiingiza sana katika siasa za
Yuda.
Antipa alimpinga Aristobulu vikali, kutokana na hofu, na kwa sababu ya
urafiki wake na Hirkanu. Inaelekea kwamba Hirkanu alimtegemea zaidi
Antipa na kwamba kwa kweli Antipa alikuwa nguvu nyuma ya kiti cha
enzi cha Yuda.
Wayahudi walichukizwa na ushawishi wa Antipa karibu kama vile
walivyoumia chini ya mamlaka ya Kirumi. Ingawa Waidumaya
walikuwa wamechanganywa na Yohana Hirkanu kwenye nchi ya
Kiyahudi , walikuwa hawajachangamana kamwe na ushindani wa zamani
ulikuwa haujasahaulika.
Katika shida ambayo ilifuatia mauaji ya Juliasi Kaisari (mfalme mkuu
wa Rumi), Antipa na wanawe walionyesha utiifu kwa serikali mpya. Ya
Kassia kwa kukusanya ushuru kwa bidii. Herode, mwana wa Antipa,
alipewa cheo cha Wakili wa Yuda na ahadi kwamba siku moja angetajwa
mfalme.

17
Antoni aliposhinda Brutu na Kassia pale Filipi, Asia ilianguka tena
kwenye mikono ya serikali mpya. Hata hivyo, Herode alibadilisha utiifu
wake haraka na akahonga kupata upendeleo na Antoni.
Sehemu ya mashariki ya kile kilichokuwa Utawala wenye nguvu wa
Uajemi ilikaliwa na watu wajulikanao kama Wapartha ambao walikuwa
hawajashindwa kamwe mwaka wa 41 K.K. na wakamfanya Antigoni,
mwana wa Aristobulu II, kuwa mfalme na kuhani mkuu.
3. Herode Alitajwa “Mfalme wa Wayahudi”
Herode, mwana wa Antipa, ambaye alikuwa amerithi kiti cha enzi cha
Yuda alikufa Hirkanu, alilazimishwa kukimbilia Rumi. Pale alijipatia
upendeleo wa Antoni na alitajwa rasmi kuwa “Mfalme wa Wayahudi.”
Cheo hicho kingekuwa na maana tu baada ya Wapartha kutolewa nje ya
Yerusalemu. Herode alirudi Yuda na majeshi ya Kirumi na akaingia
Yerusalemu kama mfalme kwa ushindi.
Utawala wa Herode ulikuwa katika miaka ya matukio mengi kutoka
mwaka wa 37 K.K. mpaka mwaka wa 4 K.K. Anajulikana sana kama
mfalme ambye aliogopa kuzaliwa kwa “Mfalme wa Wayahudi”
mshindani na kasababisha mauaji ya watoto wachanga kule
Bethelehemu wakati wa Yesu alipozaliwa.
Ingawa lile tendo la Herode haliwezi kuandikwa kwenye kumbukumbu
za kidunia, mambo yake mengine mabaya mno (ukatili) yanajulikana
vema. Kwa ujumla alikuwa na wake kumi, na inasemekana kwamba
Mfalme Augusto alisema juu ya maisha yake ya familia, “Afadhali niwe
nguruwe wa Herode kuliko kuwa mwanaye.”
a. Alitafuta Kupata Upendo Wa Wayahudi. Ingawa alidhrauliwa na
raia wake wa Kiyahudi, Herode alitafuta kupata upendeleo wao.
Alijenga na kujenga upya miji mikuu nchi nzima. Samaria ilifanyika
Sebaste kwa heshima ya Augusto, Mnara wa Stratoni ulifanyika
Kaisaria ukiwa na bandari iliyolindwa kwa boma la mawe la kuzuia
mawimbi na ukuta wenye minara kumi. Ngome, birika bustani za
maupmziko, sehemu za soko, barabara na starehe nyingine za mila
ya Uyunani zilikuwa sehemu ya mapango wake wa ujenzi.
Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake (20-19 K.K.),
Herode alianza kazi ya kujenga tena Hekalu la Kiyahudi kule
Yerusalemu. Jumba kubwa lilijengwa na makuhani kwa mwaka na
nusu.

18
Lakini kazi ya sehemu nyingine nyingi za nyua na majengo yote
haikukamilika mpaka uliwali wa Albino (mwaka wa 62-64 B.K.). Hii
ilikuwa chini ya miaka kumi kabla ya kuaangamizwa kabisa na
majeshi ya Tito mwaka wa 70 B.K. kama ilivyotabiriwa na Yesu
(Luka 19:41-44).
b. Alikufa Muda Mfupi Baada Ya Kuzaliwa kwa Yesu. Kifo cha
Herode kilifuata haraka kuzaliwa kwake yeye (Yesu) ambaye angetoa
changamoto kwa haki ya Herode kuitwa “Mfalme wa Wayahudi.”
Pamoja na kifo cha Herode – ambacho hakuna mtu aliyeomboleza –
kipindi kati ya Agano la Kale na Agano Jipya hufikia mwisho na
tunaingia kwenye kipindi cha Agano Jipya.

H. MAELEZO YA MADHEHEBU YA KIYAHUDI


Mafarisayo, Masadukayo, Waherode na Wazelote, ambayo hufanya sehemu
kubwa katika kumbukumbu za injili, wote wana mwanzo wao wakati wa
karne mbili kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.
Wanawakilisha urejeo tofauti kwa ungomvi uliokuwa unaendelea kati ya
Uyunani na maisha ya dini ya Kiyunani. Wakati ushindani wa Wamakabayo
ulikuwa umemaliza tatizo la kisiasa la uhusiano kati ya Waseleusidi wa
Shamu na Yuda, ushindani huo ulilazimisha juu ya Uyuda umuhimu wa
kuamua uhusiano wake wenyewe kwa ulimwengu wote wa nchi nyingine.
1. Mafarisayo – Wa Kisheria
Chama chenye jina la Kifarisayo kinatajwa kwanza wakati wa utawala
Yohana Hirkanu (134-104 K.K.), na ni dhahiri kwamba hata wakati huo
kulikuwa na uadui kati ya Ufarisayo wenye “kushikilia imani ya
kidesturi” na Usadukayo wenye mawazo yaliyofunguka zaidi.
Neno Farisayo humaanisha “aliyetengwa.” Pengine mwanzoni jina hili
lilimaanisha mtu aliyejitenga mwenyewe kutokana na ushawishi
uharibuo wa Uyunani katika bidii yake kwa ajili ya Sheria ya ki-Biblia.
Mwana historia Yosefu husema kwamba Mafarisayo “hutokea kuwa
wenye dini zaidi kuliko wengine, na huelekea kutafsiri sheria kwa
usahihi zaidi.”
Mafarisayo walikuwa wanatimiza sheria kuhusu usafi kwa kanuni za
dini kwa uangalifu. Kwa sababu hii hawakuweza kununua vitu vya kula
au kunywa kutoka kwa “wenye dhambi” kwa hofu ya kunajisika.

19
Wala Mfarisayo asingeweza kula kwenye nyumba ya mwenye dhambi,
ingawa angeweza kumkaribisha mwenye dhambi kwenye nyumba yake
mwenyewe.
Katika hali kama hizo Mfarisayo angempatia mwenye dhambi mavazi ya
kuvaa, kwani mavazi ya mwenye dhambi yangeweza kuwa najisi kwa
kanuni za dini.
Wakiwa na nia ya dhati ya kuifanya Sheria ya Musa ifanye kazi katika
ulimwengu wa mila mpya ya Uyunani na Rumi, Mafarisayo walianzisha
utaratibu wa desturi ambazo zilitafuta kutumia Sheria kwa hali mbali
mbali.
a. Vikundi Viwili Vya Wazo La Kisheria. Wakati wa karne ya
kwanza kabla ya Kristo, waalimu wawili wa ki-Farisayo wenye
ushawishi walitoa majina yao kwa vikundi viwili vya wazo la
kisheria.
1) Hilleli alikuwa mtulivu zaidi kati ya hawa wawili, sikuzote
wakifkiria maskini na tayari kukubali kwamba utawala wa Kirumi
ulichukuana na dini halisi ya Kiyahudi.
2) Shammai, kwa upande mwingine, alikuwa mkali zaidi katika
tafsiri yake ya Sheria ya Musa na alikuwa anapingana vikali na
Rumi. Mwishoni mtazamo wake ulipata wonyesho katika dhehebu
la Wazelote ambao upinzani wao kwa Warumi ulileta uharibifu wa
Yerusalemu mwaka wa 70 B. K.
Talmudi imehifadhi kumbukumbu ya mabishano 316 kati ya kikundi
cha Hilleli na cha Shammai.
b. Desturi Kufanyika Sheria. Katika wazo la ki-Farisayo, desturi
ilianza kama fafanusi juu ya Sheria lakini mwishoni ilipandishwa
kwenye ngazi ya Sheria yenyewe.
Kuhalalisha fundisho hili ilishikiliwa kwamba Mungu alitoa “Sheria
ya kunenwa” mwa Musa kwenye Mlima Sinai pamoja na “sheria
iliyoandikwa”, yaani Torah. Sheria ya kunenwa” ambayo alipewa
Musa ilihifadhiwa katika vitabu vya Musa vya Agano la Kale, Torah.
Mwisho katika maendeleo haya ulifikiwa wakati Mishna anaposema
kwamba sheria za mapokeo ya desturi lazima zitimizwe kwa mkazo
zaidi kuliko sheria zilizoandikwa, kwa sababu sheria halali (yaani,
desturi za kunemwa) hugusa maisha ya mtu wa kawaida kwa undani
zaidi kuliko sheria za kikatiba zilizokuwa mbali (Torah iliyoandikwa).

20
Kwa nyongeza kwa dai kwamba Ufarisayo ulihusu kujali mno mambo
ya kawaida ya Sheria, Agano Jipya huthibitisha kwamba desturi
ilipuuza kwa ukubwa kusudi halisi la Sheria (Mt 15:3).
Kama katika milengo mingi inayofaa, utawa wa zamani wa wale
ambao walikuwa wamejitenga wenyewe kutoka uchafu kwa gharama
kubwa, ulibadilishwa na nia ya moyo ya kiburi katika kushika
maagizo ya kisheria.
Watu kama Nikodemu, Yusufu wa Arimathea, Gamalieli na Sauli
wa Tarso (aliyekuwa Mtume Paulo baada ya kumgeukia Kristo),
wanawakilisha mioyo mingine ya kiungwana kutoka desturi za ki-
Farisayo katika Agano Jipya.
Kwa Sauli, Mafarisayo aliwakilisha muhtasari wa ufuasi wa imani ya
kidesturi “madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa” (Mdo 26:5).
Ufarisayo ulianza vizuri, na upotovu wake ni ukumbusho wa daima
kwamba kuridhika binafsi na kiburi cha kiroho ni majaribu ambayo ni
rahisi sana kuwapata watawa.
2. Masadukayo – Wapenda Vitu (Mali)
Ingawa Mafarisayo na Masadukayo wanashutumiwa pamoja wote katika
Agano Jipya, walikuwa na machache ya pamoja ukiacha uadui wao kwa
Yesu. Masadukayo walikuwa wa chama cha jamii iliyo bora ya
Yerusalemu na wa ukuhani mkuu. Walikuwa wamefanya amani yao na
watawala wa kisiasa na walikuwa wamepata nafasi za utajiri na
ushawishi. Utawala wa Hekalu na utaratibu wa ibada ulikuwa wajibu
wao maalum. Masadukayo walijiweka wenyewe mbali na watu na watu
hawakuwapenda.
Jitihada za ki-Farisayo za kutumia Sheria kwa hali mpya zilikataliwa na
Masadukayo ambao waliwekea mipaka dhana yao mamlaka kweye Torah
tu au Sheria ya Musa. Masadukayo hawakuamini katika ufufuo, roho au
malaika (linganisha Mk 12 :18; Lk 20:27; Mdo 23:8). Kwa ujumla imani
yao ilikuwa mfululizo wa kukana na kwa hiyo hawakuacha utaratibu
yakini wa kidini au wa kisiasa.
Wakati Mafarisayo walipowapokea waongofu wa dini (Mt 23:15), chama
cha Usadukayo kilifungwa. Hakuna mtu isipokuwa washirika wa ukuhani
mkuu na jamii zilizo bora za Yerusalemu angeweza kuwa mshirika.

21
Pamoja na uharibifu wa hekalu mwaka wa 70 B.K., chama cha
Usadukayo kilifikia mwisho. Uyuda wa kisasa hufuatisha mizizi yake
kwa Mafarisayo.
3. Waesseni – Watawa Wajinyimao Anasa
Wote, Waesseni na Mafarisayo hufuatisha mizizi yao kwenye uongozi
wa wenye kushikilia imani ya kidesturi wa nyakati za Makabayo ambao
walisimama dhidi ya Uyunani. Mafarisayo walishikilia utunzaji mkali wa
“sheria za mapokeo ya desturi” katika mipaka ya Uyuda wa zamani.
Walishikilia kujitenga kwao na uchafu, lakini si kujitenga na jamii
yenyewe ya Kiyahudi.
Hata kama ibada ya hekalu ilifanywa na Masadukayo, Mafarisayo
waliheshimu ibada hizi kama sehemu ya urithi wao wa kidini. Ingawa
Mafarisayo angejiweka mbali na “wenye dhambi”,

aliishi kati yao na alitaka sana heshima yao.


Urejeo wa upeo zaidi dhidi ya vishawishi ambavyo vilielekea kuharibu
maisha ya Kiyahudi ulichukuliwa na dhehebu ambalo waandishi wa
zamani filo, Yosefu na Pline huita Waesseni.
Waesseni huelekea kuwa wengi wao walijitenga kuishi kwenye jamii za
watawa, kama vile ile iliyoshikilia makao yake makuu pale Qumran
karibu na ncha ya kaskazini magharibi ya Bahari Mfu. (Fahamu: Qumran
ni pale “Hati za Kuviringisha za Bahari Mfu [Maandiko Matakatifu Ya
Zamani Sana]” maarufu zilipopatikana kwenye pango katikati ya karne
ya ishirini. Inawezekana Waesseni waliyaweka pale katika kipindi cha
kabla ya Ukristo.)
Kwa kutafuta kuulezea Uyuda kwa ulimwengu uliozungumza Kiyunani,
Yosefu alizungumza juu ya “falsafa” tatu – zile za Mafarisayo,
Masadukayo na Waesseni.
Neno “Esseni” huelekea lilitumika katika njia nyingi tofauti. Makundi
tofauti ya Wayahudi wenye mawazo ya utawa walishikilia na walitenda
mazoea mbali mbali ya kidini. Bado wote walikuwa wakijulikana kama
Waesseni.
Pline husema kwamba Waesseni waliwaepuka wanawake na hawakuoa,
lakini Yosefu husema juu ya kundi la Waesseni ambao waliruhusiwa
kuoa. Machimbo ya Qumran huonyesha kwamba wanawake
waliandikishwa katika jamii ya Qumrani.

22
Waandishi wa zamani hunena vema juu ya Waesseni, ambao waliishi
maisha magumu na ya vivi hivi tu. Washirika wa jamii walijifunza
Maandiko na vitabu vingine vya kidini. Kila Messeni alitakiwa kufanya
kazi za mikono ili kuifanya jamii ijitegemee.
Mali na vifaa vya kila mmoja vilikuwa kwa msaada wa wote na nidhamu
kali iliwekewa nguvu na mwangalizi. Yale makundi ambayo yalikataa
ndoa yaliwalea vijana katika umri mdogo na kuwafanya wana ili
kuwafundisha na kuendeleza fikra za Uesseni. Utumwa na vita
vilikataliwa.
Waesseni waliwapokea waongofu wa dini, lakini mwanafunzi wa dini
yao alitakiwa kupitia kipindi cha majaribio makali kabla hajafanyika
mshirika kamili.
Kiidadi, Waesseni hawakuwa wengi kamwe. Filo husema kwamba
walikuwepo elfu nne, na Pline huzungumzia juu ya jamii kaskazini mwa
Engedi inayopakana na eneo la Qumran. Ni wazi kwamba kulikuwa na
maskani mengine, kwani tunaambiwa kwamba washirika wote wa
dhehebu walikaribishwa katika makoloni yoyote ya Waesseni.
Hakuna kitu kinachojulikana hakika kuhusu historia ya mwanzoni ya
dhehebu, kwani kama vile milengo yote ya matengenezo hufuatisha
vyanzo vyake kwamba Musa alianzisha desturi ya Uesseni , na Yosefu
husema kwamba ilikuwepo “hata tangu nyakati za zamani za mababa.”
Ni hakika kwamba mwamba mwanzoni mlengo wa Esseni ulikuwa
unapinga vikali ubovu uliokuwa wazi katika Yuda kabla ya Ukristo, na
kwamba hatimaye washirika wengi walijitoa kutoka kwenye maisha ya
jamii ya ki-Plestina na kutafuta usafi wa kiroho katika mahali kama eneo
la Qumran.
Kwa wale walio wanafunzi wa historia ya Kanisa, ingeelekea dhahiri
kwamba ushawishi wa Esseni uliendelea wenyewe mpaka kufikia karne
hii ya ishirini. Mazoea yao mengi yalichanganywa kwenye “taratibu”
mbali mbali za matawi ya ki-Orthodox na ki-Katoliki ya Ukristo.
Inawezekana kwamba Paulo alikuwa anarejea ushwishi fulani wa
mafundisho ya ki-Esseni alipoonya juu wengine ambao walishikilia “…
mafundisho ya mashetani … wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru
wajiepushe na vyakula …” (Tim 4:1-3).
Wakijidhania wenyewe kama Waisraeli wa kweli au wasafi peke yao
tu, Waesseni walikataa kushirikiana na kile walichoamini kuwa

23
maadhimisho maovu ya kidini kwenye Hekalu la Yerusalemu. Maisha
yaliyoratibishwa kwa ungalifu kwenye kituo cha Esseni huelekea
kutumika kama badili ya hekalu machoni pa Waesseni wacha Mungu.
Ukali wa nidhamu ya Waesseni na ugumu ambao kwao Sheria iliwekewa
nguvu vinasisitizwa na wote ambao wameandika juu yao. Yosefu husema
kwamba walikuwa wakali kuacha kufanya kazi siku ya Sabato.
Kifungu cha maneno katika Maandiko Ya Dameski (ambayo huelekea
kuwa na chanzo cha ki-Esseni) husema kwamba si halali kumtoa
mnyama shimoni siku ya Sabato. Maoni kama hayo yalidhaniwa kuwa ya
upeo mno hata na Mafarisayo wa kisheria (linganisha na Mt 12:11).
Kutokuwepo kwa Waesseni kwenye mkondo mkuu wa maisha ya
Kiyahudi bila shaka ni sababu kwa nini hawakutajwa katika Agano Jipya
au katika Kitabu Cha Mafundisho Ya Wayahudi (Talmudi). Ingawa
maadili ya hali ya juu ya Waesseni husifiwa kweli, mafundisho na
utendaji wa Yesu ulikuwa kinyume kabisa na uhalali na utawala wa
mafundisho ya ki-Esseni.
Ingawa Waesseni walidhani kwamba kugusana na mashirika wa kundi
lao wenyewe la ngazi ya chini ilikuwa ni najisi kwa kanuni za dini, Yesu
hakusita kula na kunywa na “…watoza ushuru na wenye dhambi…”
(Mt 11:19; Lk7:34).
Ingawa aliitii sheria ya Musa, Yesu hakuwa na huruma kwa wale
walioifanya Sheria kuwa mzigo badala ya Baraka. Kulingana na Yesu,
Sabato iliwekwa kwa manufaa ya mwanadamu. Ni kisheria kufanya jema
siku ya Sabato (Mt 12:1-12; Mk 2:23-28; Lk 6:6-11; 14:1-6).
Yesu alishutumu matumizi mabaya ya hekalu na litabiri juu ya
kuharibiwa kwake. Lakini hakukataza huduma za Hekalu. Alikuja
Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu za Wayahudi, na baada ya ufufuko
wake, bado wanafunzi wake walishika njia yao kwenda hekaluni wakati
wa saa ya maombi (linganisha na Matendo sura ya 3).
Ingawa kujinyima anasa na utawa kulijiingiza katika kufikiri ki-Kristo,
Ukristo katika kipindi cha mwanzoni sana haukuwa kwa maana yoyote
mlengo wa kujinyima anasa. Huduma ya Yesu ilikuwa zaidi kwa “watu
wa kawaida” ambao walikataliwa na Mafarisayo na Waesseni pia. Kwa
sababu Yesu alijihusisha na watu wa kizazi chake kwa uhuru,
waliojihesabia haki walimwita mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye
dhambi (Mt 11:19).

24
Hakufanana na namna ya kisheria ya Wafarisayo, mazoea ya kujinyima
anasa na utawa wa Waesseni au mambo ya kisasi na tamaa ya mali ya
ulimwengu huu ya Wasadukayo. Juu yake ilisemwa, “mkutano mkubwa
walikuwa wakimsikiliza kwa furaha” (Mk 12:37).
4. Vikundi Vingine
Agano Jipya hutaja Maherodi (Mk 3:6; Mt 22:16) na Zelote (Lk 6:15),
makundi ya Wayahudi waliokaa pande mbili tofauti kabisa katika mambo
ya kisiasa.
Maherode yaelekea walikuwa Wayahudi wa ushawishi na msimamo
ambao ulikuwa umeandaliwa vema kwa utawala wa Maherode na,
kutokana na hili, kwa Warumi waliowaunga mkono Maherode.
Zelote, kwa upande mwingine, walipenda taifa lao sana na walikusudia
kupinga Rumi kwa hali na mali.
Ushupavu wao wa dini ulileta vita ambayo katika hiyo jeshi la Tito
liliharibu Yerusalemu na Hekalu lake (70 B.K.).
Kwa taarifa zaidi juu ya kipindi kati ya Agano la Kale na Agano Jipya
angalia sura ya pili ya Sehemu Ya C1. Angalia pia Elimu Ya Miaka
Na Mambo Yafuatanavyo Kati Ya Agano La Kale Na Agano
Jipya hapo chini.
Elimu Ya Miaka Na Mambo Yafuatavyo Kati Ya Agano La Kale Na Agano
Jipya
Tarehe K.K.
612 Ninawi ilihaibiwa na Wamedi na Wababeli
587 Yerusalemu iliharibiwa na Nebukadreza
559 Koreshi alirithi ufalme wa anshani; mwanzo wa ufalme wa Uajemi
539 Babeli iliangukia kwa Koreshi; mwisho wa Ufalme mpya wa Babeli
530-522 Kambyse amfuatia Koreshi; ushindi wa Misri
522-486 Dario I mtawal wa Ufalme wa Uajemi
515 Hekalu la Pili lilimaliziwa kujengwa na Wayahudi kule Yerusalemu
486-465 Ahasuero I ajaribu kushinda Uyunani; wakati wa Esta
480 Ushindani wa manoari ya Kiyunani pale Salami, Ahasuero akimbia
464-424 Artashasta I atawala Uajemi, kipindi cha Nehemia
334-323 Iskanda wa Makedonia ashinda Mashariki
311 Seleusidi ashinda Babeli; mwanzo wa nasaba ya ufalme wa Seleusidi
223-187 Antioko (III) Mkuu, mtawala wa ki-Seleisidi wa Shamu
198 Antioko III ashinda Misri, apata utawala wa Palestina
175-163 Antioko (IV) Epifani atawala Shamu; Uyuda wakatazwa
167 Matathia na wanawe waasi dhidi ya Antioko; mwanzo wa uasi wa Makabayo
166-160 Yuda, Kiongozi wa Makabayo

25
160-142 Yonathani ni kuhani mkuu
142-135 Simoni ni kuhani mkuu; aanzisha nasaba ya ufalme wa Hasmonea
134-104 Yohana Hirkanu apanua eneo ya utawala wan chi huru ya Kiyahudi
103 Utawala wa Aristobulu
102- 76 Iskanda Yannae atawala
75- 67 Salome Iskanda atawala;
Hirkanu II kuhani mkuu
66- 63 Kupigania ufalme: Aristobulu II na Hirkanu II
63 Pompei ahusuru Palestina; utawala wa Kirumi waanza
63- 40 Hirkanu II atawala, chini ya Rumi; Antipa afanya kuongeza nguvu
40- 37 Waparthiani washinda Yerusalemu; wamweka Aristobulu II kama kuhani mkuu na
Mfalme
37- 4 Herode Mkuu, mwana wa Antipa, atawala kama mfalme; chini ya Rumi

26

You might also like