Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

Habib ibn Mohammad al-'Ajami al-Basri, raia wa Uajemi aliyeishi Basra, alikuwa ni

sufi mkubwa alikua ni murid wa al-Hasan al-Basri, Ibn Sirin, na viongozi wengine.
Kubadilika kwake kutoka kwa maisha ya raha na ubinafsi ililetwa na ufasaha wa
Hasan al Basri; alikuwa mhudumu wa mara kwa mara kwenye mihadhara yake, na
kuwa mmoja wa washirika wake wa karibu. Kazi yake kabla ya kutubu na kua
mchamungu ni mkopeshaji kwa riba. Aliishi Basra, na kila siku alifanya raundi
kuwapitia wateja wake.

Ikiwa hatapata pesa, alidai malipo yake kwa thamani ya ngozi ya kiatu. Kwa njia hii
alikusanya matumizi yake ya kila siku. Siku moja alikua amekwenda kumfuata
mdaiwa fulani. Mtu huyo hakua nyumbani; hivyo akashindwa kumpata, alidai malipo
ya ngozi ya viatu. "Mume wangu hayupo," mke wa mdaiwa alimwambia. "Mimi
mwenyewe sina chochote cha kukupa. Tulikuwa tumemchinja kondoo, lakini imebaki
shingo tu. Ikiwa unapenda nitakupa hiyo iwe ndio kama malipo ya mkopo wake "Hilo
ni jambo," habib akajibu, akidhani kwamba angeondoka na shingo ya kondoo na
kwenda nayo nyumbani. Kakini akaona hasara kuipikia nyumbani kwake
akamwambia yule mama "Weka sufuria jikoni, "Sina mkate wala mafuta,"
mwanamke huyo akajibu."Vizuri," Habib alisema. "Nitaenda kuchukua mafuta na
mkate, lakini nitakutoza kama ngozi ya kiatu ( yaani kama riba ya ziada)."Basi,
akaenda akachukua vitu hivi, na yule mwanamke akaiweka sufuria. Ile nyama
ilichemka na yule Mwanamke alikuwa karibu kumimina mchuzi kwenye bakuli
wakati huo huo ombaomba aligonga mlangoni . Habib akajibu "Ikiwa tutakupa kile
tulichokuwa nacho, hautakua tajiri, na sisi wenyewe tutakua maskini."Mwombaj
hakukata tamaa, alimsihi mwanamke huyo kuweka kitu chochote kwenye bakuli.
Akainua kifuniko cha sufuria, na kugundua kuwa yaliyomo ndani yake yote
yamegeuka kuwa damu nyeusi. Alibadilika rangi haraka akarudi nyuma na kumshika
Habib kwa mkono, akamwongoza kuelekea kwenye sufuria."Angalia ni nini
kimetupata kwa sababu ya malipo yako ya laana ya riba, na kelele zako kwa huyo
ombaomba!"alilia. "Ni nini kitakachokua kwetu sasa katika ulimwengu huu" Alipoona
hii, Habib alihisi moto ndani yake ambao baadaye haukudorora."Mwanamke,"
alisema, "ninatubu kwa yote nimefanya."

Siku iliyofuata akatoka kwenda kutafuta wateja wake. Ilikuwa Ijumaa, na watoto
walikuwa wakicheza barabarani. Walipomuona Habib walianza kupiga kelele."Hapa
anakuja Habib mla riba. Kimbieni, kabla hatujalaaniwa kama yeye! "Maneno haya
yalimuumiza sana Habib. Alichukua njia ya kwenda kwenye mawaidha ya Sheikh
Hasan al Basri yale mawaidha yalimgusa Habib moyoni, hata akashindwa kuvumilia.
Kisha akatubu.Kugundua kilichokuwa kimetokea, Hasan wa Basra alimshika mkono
na kumtuliza.Aliporudi kutoka kwenye mkutano aligunduliwa na mmoja wa mdaiwa
wake, ambaye alifanya kukimbia."Usikimbilie," Habib alimwita. “Mpaka sasa ilikuwa
nyie ndio mnanikimbia; sasa lazima mimi ndio niwakimbie. "Akaendelea. Watoto
walikuwa bado wanacheza. Walipomuona Habib walipiga kelele tena."Anakuja Habib
mwenye toba. Kimbieni, labda vumbi letu limguse, kwa sababu sisi ni wenye dhambi
dhidi ya Mungu. ​Akalia Habib. "Kwa sababu ya siku hii moja ambayo nimerejea
kwako,umeibadilisha mioyo ya watu kwa ajili yangu na umefanya jina langu
lijulikane kwa wema. "Kisha akatoa tangazo. "Yeyote anayetaka chochote kutoka
kwa Habib, njoo uchukue!"Watu walikusanyika pamoja, naye akatoa mali zake
zote.Mtu mwingine alikuja na mahitaji. Hakuwa na chochote kilichobaki, Habib
akampa kilemba cha mke wake). Kwa mdai mwingine alimpa shati lake mwenyewe,
akabaki uchi.Baaada ya hapo Habib alihamia nje ya mji pempeni ni mto euphrates,
na hapo akajitoa kwa ibada ya Mungu. Kila usiku na mchana alihudhrua darasa kwa
Hasan al Basri, lakini hakuweza kujifunza Korani, kwa sababu hiyo aliitwa jina la
muajemi ( Al ajam).Wakati ulipita, naye alikuwa mnyonge kabisa.

Mke wako alikua akimuomba pesa za matumizi mara kwa mara. Lakini yeye kila
akiamka alikua anaondoka kwenda kufanya ibada zake huku akimwambia mke wake
anaenda kazini.Usiku ulipofika alirudi kwa mkewe.Mkewe akauliza, "Umekuwa
ukifanya kazi wapi, mbona hauleti chochote nyumbani?""Yule ambaye nimekuwa
nikifanya kazi kwake ni mkarimu sana," Habib akajibu. "Yeye ni mkarimu san ahata
naona aibun kumuomba chochote.Wakati ukifika atatoa tu. Kwa maana anasema,
'Kila siku kumi mimi hulipa mshahara.' ”Basi Habib akaendelea na ibada za huko
shambani kwake , hata siku kumi zilikuwa zimeisha. Siku ya kumi wakati wa sala ya
adhuhuri, wazo liliingia akilini mwake."Nitarudi vipi nyumabi sina kitu, na
nitamwambia nini mke wangu?"Na alitafakari haya kwa undani. Moja kwa moja
Mungu Mwenyezi mbeba mizigo mlangoni wa nyumba yake na akiwa na punda
mwende unga, mwingine na kondoo, na mwingine na mafuta, asali, mimea na
vitunguu. Wasindikizaji walipakia hii yote. Kijana ambaye alikua na umbile la ajabu
aliandamana nao na begi la fedhakiasi cha dinar mia tatu. Kufika nyumbani kwa
Habib, aligonga mlango."Unataka nini?" Aliuliza mke wa Habib, akifungua
mlango."Tajiri wake Habib ametutuma” Anasema aongeze bidii kwenye kazi na
malipo yake yatakua Zaidi.”

You might also like