Professional Documents
Culture Documents
Praying God's Word
Praying God's Word
Praying God's Word
0
UTANGULIZI
Ni muhimu tukumbuke kuwa neno la Mungu li hai na tena lina
nguvu. Tunasoma katika (Ebr. 4:12) kwamba; “Maana Neno la neno la
Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote
ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo
na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na
makusudi ya moyo.” Pia soma Isaya 55:11. Maandiko matakatifu yana
uvuvio wa Roho Mtakatifu. Yana pumzi ya kimungu ndani yake na kwa
hiyo ni maneno yaliyo hai. Maneno haya yanatuongoza kumfikia Yesu
mwenyewe ambaye yeye ndiye neno wa Mungu aliyekuwako kwa
Mungu, naye alikuwa mungu, vitu vyote vilifanyika kwake na wala
1
pasipo yeye hakuna lililoweza kufanyika. Ni neno aliyefanyika mwili
akakaa kwetu. (Yoh 1:1…) Katekisimu ya kanisa katoliki inafundisha
kuwa neno la Mungu ni sala ya kikristu.
Bwana wetu Yesu Kristu ni kielelezo chetu katika kutumia maandiko
matakatifu kama sala. Katika (Mt. 27:46 na Mk 15:34) Tunaona kuwa
Yesu alipokuwa msalabani alisali na kusema “Mungu wangu Mungu
wangu mbona umeniacha?” Maneno haya ya sala ya Yesu yanapatikana
katika (Zaburi 22:1) Pia katika (Lk. 23:46) Tunaona kuwa Yesu
alipokuwa msalabani amekaribia kukata roho alimwita baba akisali
maneno ya zaburi na kusema: “mikononi mwako naiweka roho yangu”.
Maneno kama haya yanapatikana katika (Zaburi 31:5). Katika mifano
hii tunapata kujifunza kuwa Yesu alikuwa amejawa na neno la Mungu
ndani yake na alilitumia kama sala yake. Hivyo ndivyo nasi
inavyotupasa. Mtume Paulo anafundisha katika waraka wake kwa
Wakolosai (Kol. 3:16) kwa kuandika kuwa, “Neno la Kristu na likae
kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana
kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu
kwa neema mioyoni mwenu.” Imetupasa kujawa neno la Mungu. Kila
siku tuchukue Muda kusoma neno la Mungu na kulitafakari na kuliweka
katika kumbukumbu za akili zetu. Kiwango cha nguvu ya kiroho tuliyo
nayo hutegemea sana kiwango cha neno la Mungu tulichonacho ndani
mwetu na kiwango cha kutumia hilo neno la Mungu katika sala na
Maisha yetu ya kila siku kwa ujumla.
2
Kuna uhitaji wa kuwa na utajiri wa ufahamu wa neno la Mungu;
kuna uhitaji wa kujua maandiko matakatifu kwa kiasi kikubwa. Kwa
hiyo Chukua muda wako kusoma na kukariri(memorize) neno la Mungu
na kulitumia katika kusali. Kumbuka pia Roho wa Mungu hutumia na
hutusaidia kutumia maandiko haya tunayoyafahamu katika kusali. Aya
hizi zipatazo 200 zimeandikwa ili kukurahisishia wewe uweze kuzisoma
na kuzikariri. Aya hizi pamoja na kuwa zenye manufaa mengi katika
Maisha yetu, ni nzuri hasa katika sala ya kuomba ulinzi wa kimungu
dhidi ya adui mwovu wa maisha mema ya kiroho na ya kimwili. Roho
wa Mungu akujalie paji la akili na elimu, uweze kusoma, kuelewa na
kutumia aya hizi.
27