Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

KUBADILI CHUO AU KOZI KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA NA


OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OR-
TAMISEMI) KWA MWAKA WA MASOMO 2020/2021

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), lilikasimiwa na Ofisi ya Rais Tawala


za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kuratibu uthibitishaji na baadae
kubadili kozi au Chuo kwa wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne mwaka
2019. Waziri wa OR-TAMISEMI alielekeza kuthibisha, kubadili kozi/programu
na Vyuo kufanyika kupitia tovuti ya NACTE.

Mpaka 27 Julai, 2020 wanafunzi 28,668 wamethibitisha kati ya 45,593


waliopangiwa kozi mbalimbali katika vyuo vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa
la Elimu ya Ufundi. Hata hivyo, jumla ya wanafunzi 16,925 hawajathibitisha nafasi
hizo mpaka sasa.

Aidha, Baraza, linapenda kuwafahamisha wanafunzi wote waliochaguliwa na OR-


TAMISEMI kwamba:
(i) Wanapaswa wathibitishe kuchaguliwa kwao hata kama wanahitaji
kubadili kozi au vyuo walivyopangiwa;
(ii) Hakuna mwanafunzi atakayeweza kubadili kozi au chuo kama hatakuwa
amethibitisha kupitia tovuti ya NACTE;
(iii) Uhamisho/kubadili chuo au kozi kunamanisha kujaza nafasi zilizowazi
kutokana na kutothibitisha; na
(iv) Waombaji ambao hawajathibitisha hadi tarehe 15 Agosti, 2020
watapoteza nafasi zao walizochaguliwa na OR-TAMISEMI.

Hivyo, Baraza linawafahamisha waombaji kuwa zoezi la kuomba kubadilisha kozi


au kuhama chuo litaanza tarehe 16 hadi 31 Agosti, 2020.

Baraza linawashauri wanafunzi waliopangiwa vyuo kuthibitisha kupitia tovuti ya


Baraza (www.nacte.go.tz) kabla ya tarehe 15/08/2020 kama ilivyopangwa hapo
awali. Baada ya tarehe hiyo hakutokuwa na nafasi nyengine ya kuthibitisha.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 27/07/2020

You might also like