Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 46

Forex inasimama badala ya neno FOREIGN EXCHANGE, Ambapo unakuwa

unabadili sarafu moja toka sarafu nyingine. Mfano kama ukitoka Tanzania
unatumia TSH ukaenda Kenya ambapo wanatumia KSH itakubidi ubadilishe
sarafu yako ya kitanzania kwenda katika saafu ya kikenya. Kwa zoezi hilo
unakuwa umeshafanya FOREX.

Hapo kinachofanyika ni hiki, TSH/KSH kwamba unauza sarafu ya kitanzania kwa


kununua sarafu ya kikenya. Hili tutaliona katika platform hii. utakutana na vitu
kama USD/CHF GBP/JPY EUR/USD

Hapo kinachofanyika ni hiki, TSH/KSH kwamba unauza sarafu ya kitanzania kwa


kununua sarafu ya kikenya. Hili tutaliona katika platform hii. utakutana na vitu
kama USD/CHF GBP/JPY EUR/USD

Kubadilisha hela huku mtandaoni ni biashara ambayo inazungusha hela nyingi


kupita aina yoyote ya biashara ulimwenguni kwa siku. Kwa siku biashara hii
mzunguko wake wa hela ni zaidi ya $5 TRILLION. Wakati stock exchange ya
New York kwa siku ni $22.4billion, Tokyo ni $18.4 billion na London ni $7.2
billion kwa siku. Na hizo ni stock exchange kubwa duniani, hivo FOREX
ONLINE ni kubwa kuliko hizi stock exchange.

Biashara hii mara ya kwanza ilikuwa ikifanywa na Institution kubwa za kifedha


kama benki kuu za nchi na mabank ya kibiashara. Lakini kulingana na mapinduzi
ya kiteknolojia hata wewe sasa unaweza kuingia katika hii biashara kutokana
kuwepo na mtu wa kati ambaye unaingia kwenye soko kupitia yeye. Huyu anaitwa
BROKER. Unafungua kaunti kwake unaingiza kiwango cha mtaji unachotaka
kuanza kufanya nacho biashara (NB- kila broker ana kiwango chake cha chini cha
wewe kuweza kuingiza mtaji hivyo ni chaguo lako umtumie yupi)

Je, hii biashara ina muhimu wowote kwako? Jibu linategemea wewe unahitaji nini
1. Kama unataka soko ambalo halilali.
2. Kama unataka fursa ya kufanya biashara mda wowote katika siku.
3. Kama unataka kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa.
Basi nadhani FOREX ni mahala sahihi kwa hayo yote
NB: Kama utaweza tengeneza kiasi kikubwa cha pesa ndani ya mda mfupi, pia
unaweza kupoteza kiwango cha fedha ndani ya mda mfupi huohuo
Watu gani wanaokuwepo/wanaoshiriki katika hii biashara?
1. Benki kuu (Central banks)
2. Serikali (Government)
3. Umoja wa wawekezaji(investment coorperation)
4. Wafanyabiashara wa duniani kote(businessies worldwide)
5 Wafanyabiashara wadogo(Retail trader)

Maeneo vitovu katika hii biashara duniani ni:


1. NEW YORK (United States Dollar USD)
2. LONDON (Euro EUR and Pound GBP)
3. FRANKFURT (France franc CHF)
4. TOKYO (Japanese YEN JPY)
5. SYDNEY(Austarlian dollar AUD)
Soko la FOREX hufunguliwa jumapili saa 6 usiku na kufungwa Ijumaa saa 5:59
usiku hivo ndani ya huu mda una uwezo wa kufanya biashara

FAIDA ZA FOREX
1. Una uwezo wa kufanaya biashara sehemu yeyote ulipo
2. Unaweza kutoa faida hela zako mda wowote ndani ya siku za wiki.
3. Sheria rahisi.
4. Inapatikana masaa 24
5. Uwiano mzuri kwa kiasi kidogo unaweza ingiza faida kubwa. (Leverage)
6. Upatikanaji wa FAIDA kubwa na kwa haraka.

HASARA ZA FOREX
1. Upatikanaji wa HASARA kubwa na kwa muda mfupi.
2. Hii sio biashara ambayo kila mtu anaweza kuifanya.

Kwa miaka kadhaa mpaka sasa, kumekuwa na list kubwa ya watu wakiingia katia
hii platform ya forex na ndoto kubwa ni kupata uhurru wa kifedha na kukua
kiuchumi kutokana na hadithi/myths za kutamanishwa kupitia mitandao au jamaa
zao wa karibu.

Ahadi za kutengeneza mamilioni ya fedha ndani ya mwezi na kuacha kazi kwa


week ni vitu vinavyoongelewa sana na waliofanikiwa katika biashara hii. kwa hio
naenda kukushirikisha baadhi ya myths/hadithi kadhaa ambazo pengine
umeshazisikia au utaendelea kuzisikia sana.
Kupata mamilioni ya shillingi ndani ya mwezi mmoja na kuacha maisha ya
ufanyaji wa kazi za kila siku ni mawazo yaliyovichwani mwa watu wengi
yawezekana na wewe mmojawapo.

Sasa hapa naenda kukusimulia baadhi ya hadithi hizo ambazo zipo sana vichwani
mwetu au tunaendelea kuzisikia kupitia platform hii ya forex;

HADITHI YA KWANZA
KUWEPO KWA NJIA(STRATEGY) BORA KUPITA NYINGINE.
Watu wengi wamekuwa wakijikita kutafuta njia ambayo itawetengenezea hela kwa
100%. Ukimuuliza mtu yeyote mpya anaejifunza forex kama kuna siri ambayo
watu waliofanikiwa katika forex wanatumia, asilimia kubwa ya majibu yao
watakwambia NDIO.
Watu wengi wanafikiri traders waliofanikiwa wanatengeneza hela kila siku kupitia
njia/strategy fulani iliyo tukufu au nzuri kushinda zote. Kitu ambacho sio kweli.
Hata traders waliofanikiwa huwa wanapoteza 30% ya trades zao kila mwezi. tatizo
ni kuwa trades wapya wanazichukia na kuzitupa trades zao zilizowaingizia hasara.
Lakini traders waliofanikiwa hukubari kupoteza katika siku tatu na wanabaki na
msimamo katika mpango kazi/plan kwani mara nyingi huwa ni long term trades na
hata wanavokutana na hasara mwanzoni huamini baada ya ule mda watakuja
kupata faida yao.

Hebu jaribu kufikilia jambo hili. unavozungusha sarafu kuna uwezekano wa


kuanguka upande wa mwenge au upande wa kichwa kwa uwiano sawa. Je,
ukizungusha mara 100 utapata 50 kichwa na 50 mwenge? jibu ni hapana. Lakini
kama utazungusha mara 1000 au mara 10000 kuna uwezekano wa kupata 50
kichwa na 50 mwenge.

Hiki ndicho nachotaka kukwambia kuhusu mpango wako wa kufanya biashara ya


forex. kama njia utayochagua kutumia ina ubora wa 60% basi ifanye mara kwa
mara kufikia au kukaribia hio 60% hata kama utapata hasara mara kadhaa, lakini
mwisho wa siku uwe upande wa faida
HADITHI YA PILI
FOREX NI MCHEZO WA 50-50
Watu wengi wanaamini kuwa forex ni mchezo wa 50-50, wanafikiri kuwa soko
litaenda juu au litaenda chini tu na kusahau kuna mda soko hucheza katika eneo
fulani. (consolidation)
Kwa nadharia hio tu ya kuwepo wa soko kucheza katika eneo moja tayari sio
mchezo wa 50-50, cha kufanya ni kufanya analysis zako kwa usahihi zaidi.

HADITHI YA TATU
UNAWEZA KUTENGENEZA HELA KWA KUCLICK TU BUTTON
Hili ni jambo tunalolisikia sana kwa wenzetu na kufanya watu wengi waingie
katika forex wakidhani ni kitu rahisi sana kwa kubonyeza tu button unapata fedha.
Asilimia 80 ya watu wanaojiunga katika forex hupoteza mitaji yao yote ndani ya
miezi mi3 ya mwanzo kwa kukosa maarifa na kutofanya mazoezi ya vitendo mara
kwa mara katika hii biashara.

Forex ni kama fani nyingine. Inahitaji kusoma, kufanya majaribia, kuifatilia kwa
karibu na kw juhudi ndipo uje utengeneze hela. imenichukua zaidi ya miezi 6
kujifunza kuanzia february mpaka september mpaka kuja kuanza kutengeneza
faida.

HADITHI YA NNE.
UNAHITAJI NJIA/STRATEGY YA KISASA ZAIDI ILI UTENGENEZE
FEDHA KIURAHISI.
Hii ni hadithi ambayo ipo kwa traders walio wengi, wakiamini unahitaji njia fulani
ambayo ni bora kuliko zote, indicators bora au muunganiko wa indicators nyingi ili
uwe accurate.

Hata pale unapokuja kuwapatia njia rahisi wanaona kama ni upuuzi mtupu na
kuidharau. wanaamini njia iliyocomplicated ni njia bora kuupita zote. lakini
kiuhalisia traders wengi waliofanikiwa wanatrade kwa njia rahisi sana na wengine
hawatumii kabisa hata indicators.
Lakini nataka kukambia ubora wa strategy upo mikononi mwa mtu husika
atakaemake commitment na hio strategy. unaweza kuwapa watu wawili strategy
moja kisha mmoja akachoma akaunti na mwingine akafanikiwa kupitia hio
strategy.
Hii ni kwa sababu kila mtu anatrade na kuona vitu tofauti. kwa hio sio njia gani ni
nzuri bali ni jinsi gani utaichukua hio njia na kuiwekea mkazo ndipo
utakapofanikiwa.

2. AINA YA WAFANYABIASHARA KATIKA FOREX.


Hii ni eneo muhimu sana kulijua na wewe kufanya maamuzi unataka uwe
mfanyabiashara wa aina gani. Hivyo kabla hujaanza ni bora kujitathmini wewe ni
mfanyabiashara wa aina gani na utumie njia zipi katika kufanya biashara yako.

1. SCALPER
Huyu ni mfanyabiashara anaekuwa katika soko kwa mda mfupi sana. Mara nyingi
anaingia na kutoka katika trade na dakika kadhaa tu. Kivutia kikubwa kwa trader
wa aina hii huona faida au hasara ndani ya mda mfupi tu. Msingi mkubwa wa
scalper ni kuwa na uwezo wa kufikiri haraka na kuweza kumantain pressure.
Kulingana na mda mfupi wa fursa scalper huamua aingie katika hio fursa au aache.

2. DAY TRADER
Huyu ni trader ni yule ambae huingia katika trade siku husika na kutoka katika
trade siku hio hio.Tofauti na scalper, yeye huingia katika trade na kuisubiri ndani
ya dakika 30 au saa. Uzuri wa kuwa day trader ni mda wa kutosha wa kufanya
zako analysis. mara nyingi huwa na mda maalum wa kuingia katika trades zake.
Na mda ukifika wanasubiri fursa ijitengeneze na kuingiza trades zao, hutumia
dakika 30, saa moja mpaka saa 4 timeframe kufanya analysis zao.

3. SWING TRADER
hawa ni traders wanaofanya biashara kila siku.... kwa kua kila siku kunakuwa na
nafasi za mtiririko/swings katika soko. ukitokea mtririko wa kupanda wanapanda
nao.. ukitokea wa kushuka wanashuka nao. Hawa wanafocus sana katika kuangalia
mtiririko wenye asili ya uimara zaidi. na mara nyingi hutokea katika kufunguliwa
kwa soko la london (London open) na New York open.Hawa wanafanana sana na
day trader huwa wanaingia na kutoka katika soko ndani ya siku husika

4. POSITION TRADER
Hawa huingia katika trade kwa siku kadhaa au week. Hii ni aina nzuri kwa wale
ambao hawana mda wa kuangalia chart kila siku.
Hawa pia tunaambiwa ni traders ambao wanachukua profit sana ukizingatia
wanakua kwenye market kwa mda mrefu hivo kuchukua faida ya week au mwezi.
Hivyo aina hii ni kwa wale wenye mitaji mikubwa

3.MISAMIATI KATIKA BIASHARA YA FOREX


Kuna misamiati mbalimbali ambayo tutakuwa/utakutana nayo katika hii biashara
ya FX. Misamiati hii kama utaweza kuielewa vizuri basi nina hakika kutakuwa
hakuna shaka ya wewe kuwa katika soko.

1. BASE CURRENCY
Hiki ni kiini msingi katika kununua au kuuza katika forex. kama utabuy USD/JPY
Hii ni kumaanisha unanunua dola ya kimarekani na wakati huohuo unauza yen ya
kijapani.

2. QUOTE CURRENCY
Hii ni ile sarafu ya pili katika pair ya sarafu husika unapofanya trade. Mfano
USD/JPY, JPY ndio quote currency.
3. LONG/BULLISH
Hii ni termonology ambayo unasikia watu wakiiongelea. kama imepatikana
opportunity ya kulong/bullish hapa maana yake NUNUA. Bull ni aina za mnyama
ambae anakula majani hivo candlestick zake nyingi zinakuwa zikiwakilishwa na
rangi ya kijani. Huyu mnyama akitaka kukudhuru huinamisha kichwa chini na
anakunyanyua kwa kukuchota kukupeleka juu. Hivyo katika Forex hapa
inamaanisha soko linatoka chini linapanda juu.
4. SHORT/BEARISH
Kama imepatikana opportunity ya kushort/bearish hapa maana yake UZA.. Bear ni
aina ya mnyama ambae anakula nyama, hivo candlestick yake huwakilishwa na
rangi nyekundu. Huyu mnyama anavyokudhuru huruka juu kisha hukushusha
chini. Hii katika forex inamaanisha soko linatoka juu kushuka chini.
5. PIP (PERCENTAGE IN POINT)
Hiki i kiasi cha thamani kinachocheza kulingana na mzunguko wa sarafu husika
katika biashara. Huanza kuhesabiwa kutoka desimali ya nne katika pair mfano
thamani ya USD/CHF ni 1.1379, thamani hii ikimove toka 1.13*79* mpaka
1.13*80* hapo inakuwa ni 1 pip
Isipokuwa kwa pair inazohusisha sarafu ya YEN nafasi za decimal zitakuwa tatu
na sio nne kama pair nyingine. Mfano USD/JPY=1.137 hivo pip unaanza kuhesabu
kwenye 7
6. LOT SIZE
Hii ni thamani inayotumika kugundua faida au hasara.
standard lot size 1.00=$10 kwa pip moja
min lot size 0.10=$1 kwa pip moja
micro lot size 0.01=10 cent kwa pip moja

7. TAKE PROFIT (TP)


Hili ni eneo ambalo utaamua kutoka nje ya soko baada ya faida. Eneo ambalo
utaona faida uliyopata inakutosha au ni eneo ambali price inaweza kugeuka na
kukuingizia hasara.
Unapoingia kwenye soko analysis zako zinakuonesha sarafu itapanda/kushuka
mpaka eneo Fulani then baada ya hapo itageuka trends Ila haujui itachukua mda
gani mpaka kufika katika hio price. Sasa huwezi kukaa kwenye screen yako mda
wote kuisubiri hio point. Unachokifanya unaset kwamba price ikifika katika hilo
eneo trade yake ijifunge automatically kisha ww ukirudi au ukimaliza mambo yako
kama itakuwa ilifika katika hio point uje ukutane na profit yako. Hapo ndo
panaitwa TAKE PROFIT.
8. STOP LOSS(SL)
Hili ni eneo ambalo utaamua kutoka nje kwa hasara either kwa kuona analysis
yako ilikuw na makosa au unaamini upande wa hasara uliopo utaongezeka zaidi
hivyo badala ya kupata hasara kubwa unaamua kuchukua hasara kidogo.
Wanasema kama hutakubali hasara basi jiandae kupokea mama wa hasara kwa
lazima.
Kwenye market ukishafanya analysis unaona kuna fursa ya kupanda kwa sarafu
hivo unaamua kuinunua ikiwa chini ili ikifika juu uiuze na ile tofauti ya bei
ulonunua na utakayokuja kuuza ndo inakuwa faida Na wewe uliingia sokoni kwa
hio currency labda, Sasa baada ya kufanya hio analysis inatokea news mfano ya
kushuka kwa ajira mfano marekani So kwa namna yoyote currency baada ya
kupanda itashuka... Maana itakuwa weak.Sasa unakuta na wewe ulishaingia so
unagundua itashuka sana hivo unaamua kutoka katika soko katika hasara ndogo ili
usipate hasara zaidi kwani haujui hio currency itashuka mpaka wapi. Hio ndo
inaitwa STOP LOSS

4.AINA ZA ODA KATIKA SOKO


Kuna aina mbalimbali katika soko ambazo unaweza kuzitumia katika kuingiza
trade yako. Hapa nimekuandalia aina tatu tu za msingi japo zipo zaidi ya hizo

1. MARKET ORDER
Hii ni pale unapogundua tu katika soko kuna fursa ya kuuza/kununa kisha
unabonyeza kitufe cha kununa/kuuza wakati huo na kuingia katika soko.

2. BUY STOP
Ukifanya analysis katika soko utagundua kuna fursa fulani inatokea katika soko.
Au imeonesha dalili za kutokea. Lakini sio mda wote utakuwa katika kioo chako
cha kompyuta. Hivo unaweka pending order ya kununua kama price itafika eneo
fulani. Hivo utaweza kuendelea na shughuli zako kisha price ikifika pale itajinunua
na kukuingiza kwenye market.

3. SELL STOP.
Kama maelezo yalivyo katika buy stop hii pia ni hivyo hivyo.. isipokuwa hapa
unaweka oda kama price itashuka basi ijiuze na kukuingiza kwenye market ikifika
point fulaniii.
5.AINA ZA KUFANYA BIASHARA.
Katika forex kuna aina tatu za kufanya biashara, hapa nitazielezea mbili za msingi
ambazo wewe ungependa kuchagua ni ipi itakuwa nzuri kwako. Japo mimi
ningependekeza mtumie aina yangu ambayo kiupande wangu nimeiona anaweza
kumudu mtu yeyote. Siwaaminishi kwamba ni rahisi lakini nina imani mtu yeyote
anaweza kuimudu.

1. Fundamental Analysis
Huu ni ufanyaji wa biashara kwa kuliangalia soko kulingana na shughuli za
kiuchumi,kisiasa na kijamii ambazo hupelekea kuleta madhara katika suala zima la
demand and supply

2. Technical Analysis
Ni somo ya kucheza kwa thamani ya sarafu, kwa lugha nyingine hii ni sawa na
chati.
Katika fundamental kikubwa kinachoangaliwa ni news lakini katika technical
analysis kinachoangaliwa ni historia ya price ilifanya nini na huwa ina tabia ya
kufanya nini. hivyo NEWS pekee ndio kitu ambacho hakiheshimu chart kwani
pindi inavotokea haifuati kanuni za chart.
Hapa chini nimekuwekea NEWS zenye madhara makubwa pia.

6.AINA 11 MUHIMU ZA CANDLESTICK PATTERN


Kuna candlestick 11 za muhimu ambazo tunaziita CANDLESTICK PATTERN,
Candles hizi ni kiashiria kikubwa sana cha kufanya entry kama zitatokea maeneo
ya SUPPORT na RESISTANCE.
1. DOJI.
Hii hutokea pale ambapo bei ya kuuza na kufungua imekuwa ni moja. Tazama
picha hapo chini na maelezo yake.

2. ENGULFING.
Hii hutokea pale ambapo candle ya pili imeizidi umbo na pin candlestick ya nyuma
katika eneo la RESISTANCE au SUPPORT. Tazama picha hapo chini na maelezo
yake.
3. HARAMI.
Hii hutokea ambapo candle ya kwanza imezidi umbo na candle inayofuata mbele
yake. Tazama picha hapo chini na maelezo yake

4. DARK CLOUD COVER.


Hii ni pattern ambayo huashiria kugeuka kwa soko kwenda kuuza mara inapokuwa
imetokea kwenye RESISTANCE. Tazama picha hapo chini na maelezo yake
5. PIERCING.
Hii ni pattern ambayo huashiria kugeuka kwa soko kwenda kununua mara
inapokuwa imetokea katika SUPPORT. Tazama picha hapo chini na maelezo yake

6. SHOOTING STAR.
Hii ni candle inayokuwa peke yake inayoashiria kugeuka soko kwenda kuuza,
hutokea eneo la RESISTANCE. Tazama picha hapo chini na maelezo yake
7. INVERTED HAMMER.
Hii pia ni candle inayokuwa peke yake inayoashiria kugeuka kwa soko kwenda
kununua inapokuwa imetokea/imejitengeneza eneo la SUPPORT. Tazama picha
hapo chini na maelezo yake

8. HAMMER.
Hii ni candle inayokuwa peke yake ikiashiria kugeuka kwa soko kwenda kuuza
inapokuwa imetokea katika eneo la RESISTANCE. Tazama picha hapo chini na
maelezo yake
9. HANGING MAN.
Hii ni candle inayokuwa peke yake ikiashiria kugeuka kwa soko kwenda kuuza
inapokuwa imetokea katika eneo la RESISTANCE. Tazama picha hapo chini na
maelezo yake

10. RAILWAY TRACK


Hii pattern hujumuisha candle mbili ambazo zinakuwa na maumbo
sawa/yaliyolingana katika maeneo ya RESISTANCE na SUPPORT. Tazama picha
hapo chini na maelezo yake

11. SPINING TOP.


Hii ni candle moja ambayo inakuwa ina umbo dogo la pin ndefu juu na chini.
Ikitokea katikati ya eneo la RESISTANCE na SUPPORT huashiria kuendelea kwa
trends, na kama ikitokea eneo la RESISTANCE au SUPPORT huashiria kugeuka
kwa soko. Tazama picha hapo chini na maelezo yake

7. SUPPORT AND RESISTANCE

SUPPORT: Hii ni point ya chini ambapo bei hufika na kugeuza.


RESISTANCE: Hii ni pointi ya juu ambayo bei hufikia na kugeuza.
Mfano: sakafu katika nyumba yako ni support na dari katika nyumba yako
tuichukulie kama resistance.
Haya maeneo ya support na resistance tunayaita kwa jina moja la ZONE.

YAFUATAYO NI MAMBO MUHIMU KUHUSU ZONE


1. Zones ni eneo na sio pointi ya bei.
2. Zones ni madoa katika chati ambapo bei inageuka mara nyingi
3. Zones yaweza kuwa juu au chini kulikokithiri katika chart
4. Zones ni sehemu ambazo wafanyabiashara wa chati tupu(naked traders) hutafuta
fursa za kuingia sokoni
5. Zones za support na resistance zinahitajika kurekebishwa mara kwa mara.
6. Chati ya mistari husaidia naked traders kuweka Zones.
7. Support iliyotobolewa hugeuka kuwa Resistance na Resistance iliyotobolewa
hugeuka kuwa Support
JE, NI KWA NAMNA GANI UNAWEZA KUTAFUTA ZONES ZA SUPPORT
AND RESISTANCE?
1. Tumia chart kubwa kutafuta Zones zenye nguvu(Major zone), Kama unatrade
kwa chati ya saa moja basi tumia chati ya siku au week.
2. Tumia chati ya mistari kutafuta zones.
3. Usitilie maanani zones hafifu(minor zones)
CHANEL
Hii ni njia ambayo bei huifua ta na hujenga kingo ambapo bei haivuki hapo.
Kuna aina 3 za chaneli hizi.

1. UPTREND CHANELI/CHANELI YA KUPANDA


2. DOWNTREND CHANELI/CHANELI YA KUSHUKA
3. SIDEWAY CHANEL/CHANELI MSAMBAMBA
TREND.
Hii ni pale ambapo bei ya sarafu Fulani inapanda juu, inashuka chini au inacheza
katika eneo Fulani(sonsolidation).

Hivyo bei inavyopanda juu inaitwa UPTREND.


Muda ambapo kunakuwa na UPTREND bei huenda JUU JUU (HIGHER HIGH)
NA JUU CHINI (HIGH LOW)
Bei inavyoshuka chini inaitwa DOWNTREND.
Huu ni muda ambapo bei inapungua kwa mtindo wa CHINI CHINI (LOWER
LOW) na CHINI JUU (LOWER HIGH)
Na pale bei inavocheza ndani ya eneo Fulani inaitwa SIDEWAY
TREND/CONSOLIDATION/LAMB/RANGING.
REVERSAL
Hii ni sehemu ambayo hutumika kuelezea sehemu ambapo TREND ya aina moja
hugeuka kuelekea aina nyingine ya TREND. Mfano bei ikiwa inapanda, ikifika
sehemu ikagoma kupanda na kugeuka basi kitendo hiko ndicho tunaita
REVERSAL.

Je REVERSAL hutokea wapi?


1. Eneo la Support.
2. Eneo la Resistance.

CONTINUATION.
Huu ni msamiati unaotumika kuelezea kuwa bei inaendelea na Trend yake lakini
kwa viashiria maalum kama kusita katika eneo Fulani au kurudi nyuma kidogo
kabla haijandelea.

Mfano
1. Kwenye downtrend ikaconsolidate then ikaendelea na kushuka.
2. Kwenye downtrend ikapanda juu kasha ikaendelea tena kushuka.

MARKET SWINGS.
Hii ni pale ambapo market ya inapanda na kushuka bila kujali hio trends ni ya
kushuka au ya kupanda. Pale unapoona price imepanda ile inaitwa UP SWINGS,
Na pale price imeshuka tunaita DOWN SWING. SWING hutokea katika trends
zote, Kwani soko limekaa kwa mtindo wa wave. Linapanda na kushuka bila kujali
trends ni ya wapi kinachotofautiana ni kuwa haishuki na kupanda kwa kiwango
sawa.

TRENDLINES
Hii ni mistari ambayo huchorwa kukutanisha vilele ambavyo vimetengenezwa na
UPSWINGS, au mashimo yaliotengenezwa na DOWNSWINGS, Kukusaidia kujua
hio trends inaenda wapi.
Unahitaji kimo cha chini cha vilele viwili ili kugundua DOWNTREND. Na
unahitaji kima cha chini cha mashimo mawili ili kugundua UPTREND.

Je nini kinamaanisha kama TRENDLINES mbili zikakutana.


Hii humaanisha kuwa trends moja imeisha hivo inafuata trends nyinigine.
THE LAST KISS.
Wafanyabiashara wanapoona bei haipandi juu wala kushuka chini zaidi, hutambua
kuwa bei iinaconsolidate na hakuna anaejua itaenda wapi. Hivyo huchora box
katika lile eneo ili endapo bei ikitoboa upande wowote wanajua ndipo price
inaelekea. Lakini bei inaweza ikatoka ndani ya hilo eneo la consolidation lakini
kumbe ikawa ni BREAKOUT. Matokeo yake unafanya entry kasha price inageuka
na kurudi tofauti na CALL yako.
LAST KISS inakuwa ni break out ambayo inatuhakikishia sasa TREND inaenda
upande sahihi. Baada ya price kutoka katika lile eneo ambalo umelitenga halafu
unaona inarudi tena usawa wa lile eneo kwa kuonesha inaingia lakini
CANDLESICK inafunga kwa kuona ni WICK imeingia katika eneo lile kasha
Price imefunga nje ya eneo la consolidation basi hiko ni kiashiria cha kuwa huo
upande ambao imeenda ndipo price itaelekea. Kwa lugha rahisi ni pale price
ikitoka katika eneo la consolidation kisha ikarudi kugusa lile eneo bila kuingia
(RETEST) hio ndio LAST KISS. Sio kila BREAKOUTS katika eneo la
consolidation ni LAST KISS lakini kila LAST KISS ni BREAKOUTS.
BIG SHADOW
Nadharia ya kivuli kikubwa inazungumziwa kama pindi uonapo kivuli kikubwa
basi kuna mwanga unaosababisha kivuli hicho. Kama umekuwa mfuatiliaji wa
chart utakuwa ushawahi kuona kuna CANDLESTICK ni ndefu sana na hakuna
NEWS au Factor yeyote kubwa. Hii pia lazima itokee katika eneo la
RESISTANCE na SUPPORT. Na inarefer kama REVERSAL. Baadhi ya watu
wanaweza kuifananisha hii na ENGULFING, Lakini nataka kukwambia hii ni zaidi
ya ENGULFING.
Ikitokea katika RESISTANCE tunaiita BEARISH BIG SHADOW.
Ikitokea katika eneo la SUPPORT inaitwa BULLISH BIG SHADOW.
Pale ambapo zikajitengeneza candle mbili zilizofuata hio inaitwa BIG SHADOW
PATTERN.
SHERIA ZA BIG SHADOW.
1. Huu ni muundo wa CANDLESTICK mbili.
2. Candlestick ya pili katika kuundwa huku ndio tunayoiita BIG SHADOW
CANDLESTICK.
3. BIG SHADOW CANDLESTICK lazima iwe kubwa kwa urefu wa juu na chini
kuliko candlestick iliopita
4. BIG SHADOW lazima itokee kwenye ukanda wa SUPPORT na RESISTANCE.
5. BIG SHADOW hutokea kwa kwenda juu na chini kulikokithiri.
6. BEARISH BIG SHADOW CANDLESTICK hujifunga chini ya candle ya
nyuma yake.
7. BULISH BIG SHADOW CANDLESTICK hujifunga juu ya candle ya nyuma.
8. Kwa BULISH BIG SHADOW, Stop loss huwekwa pips chache chini ya ile
BULLISH BIG-SHADOW CANDLESTICK
9. Kwa BEARISH BIG-SHADOW, Stop loss huwekwa pips chache juu ya ile
BEARISH BIG-SHADOW CANDLLESTIICK

You might also like