Professional Documents
Culture Documents
FX Swahili
FX Swahili
FX Swahili
unabadili sarafu moja toka sarafu nyingine. Mfano kama ukitoka Tanzania
unatumia TSH ukaenda Kenya ambapo wanatumia KSH itakubidi ubadilishe
sarafu yako ya kitanzania kwenda katika saafu ya kikenya. Kwa zoezi hilo
unakuwa umeshafanya FOREX.
Hapo kinachofanyika ni hiki, TSH/KSH kwamba unauza sarafu ya
kitanzania kwa kununua sarafu ya kikenya. Hili tutaliona katika platform
hii. utakutana na vitu kama USD/CHF GBP/JPY EUR/USD
Hapo kinachofanyika ni hiki, TSH/KSH kwamba unauza sarafu ya
kitanzania kwa kununua sarafu ya kikenya. Hili tutaliona katika platform
hii. utakutana na vitu kama USD/CHF GBP/JPY EUR/USD
Kubadilisha hela huku mtandaoni ni biashara ambayo inazungusha hela
nyingi kupita aina yoyote ya biashara ulimwenguni kwa siku. Kwa siku
biashara hii mzunguko wake wa hela ni zaidi ya $5 TRILLION. Wakati stock
exchange ya New York kwa siku ni $22.4billion, Tokyo ni $18.4 billion na
London ni $7.2 billion kwa siku. Na hizo ni stock exchange kubwa duniani,
hivo FOREX ONLINE ni kubwa kuliko hizi stock exchange.
Biashara hii mara ya kwanza ilikuwa ikifanywa na Institution kubwa za
kifedha kama benki kuu za nchi na mabank ya kibiashara. Lakini
kulingana na mapinduzi ya kiteknolojia hata wewe sasa unaweza kuingia
katika hii biashara kutokana kuwepo na mtu wa kati ambaye unaingia
kwenye soko kupitia yeye. Huyu anaitwa BROKER. Unafungua kaunti kwake
unaingiza kiwango cha mtaji unachotaka kuanza kufanya nacho biashara
(NB- kila broker ana kiwango chake cha chini cha wewe kuweza kuingiza
mtaji hivyo ni chaguo lako umtumie yupi)
Je, hii biashara ina muhimu wowote kwako? Jibu linategemea wewe
unahitaji nini
1. Kama unataka soko ambalo halilali.
2. Kama unataka fursa ya kufanya biashara mda wowote katika siku.
3. Kama unataka kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa.
Basi nadhani FOREX ni mahala sahihi kwa hayo yote
NB: Kama utaweza tengeneza kiasi kikubwa cha pesa ndani ya mda mfupi,
pia unaweza kupoteza kiwango cha fedha ndani ya mda mfupi huohuo
Watu gani wanaokuwepo/wanaoshiriki katika hii biashara?
1. Benki kuu (Central banks)
2. Serikali (Government)
3. Umoja wa wawekezaji(investment coorperation)
4. Wafanyabiashara wa duniani kote(businessies worldwide)
5 Wafanyabiashara wadogo(Retail trader)
Maeneo vitovu katika hii biashara duniani ni:
1. NEW YORK (United States Dollar USD)
2. LONDON (Euro EUR and Pound GBP)
3. FRANKFURT (France franc CHF)
4. TOKYO (Japanese YEN JPY)
5. SYDNEY(Austarlian dollar AUD)
Soko la FOREX hufunguliwa jumapili saa 6 usiku na kufungwa Ijumaa saa
5:59 usiku hivo ndani ya huu mda una uwezo wa kufanya biashara
FAIDA ZA FOREX
1. Una uwezo wa kufanaya biashara sehemu yeyote ulipo
2. Unaweza kutoa faida hela zako mda wowote ndani ya siku za wiki.
3. Sheria rahisi.
4. Inapatikana masaa 24
5. Uwiano mzuri kwa kiasi kidogo unaweza ingiza faida kubwa. (Leverage)
6. Upatikanaji wa FAIDA kubwa na kwa haraka.
HASARA ZA FOREX
1. Upatikanaji wa HASARA kubwa na kwa muda mfupi.
2. Hii sio biashara ambayo kila mtu anaweza kuifanya.
Kwa miaka kadhaa mpaka sasa, kumekuwa na list kubwa ya watu
wakiingia katia hii platform ya forex na ndoto kubwa ni kupata uhurru wa
kifedha na kukua kiuchumi kutokana na hadithi/myths za kutamanishwa
kupitia mitandao au jamaa zao wa karibu.
Ahadi za kutengeneza mamilioni ya fedha ndani ya mwezi na kuacha kazi
kwa week ni vitu vinavyoongelewa sana na waliofanikiwa katika biashara
hii. kwa hio naenda kukushirikisha baadhi ya myths/hadithi kadhaa
ambazo pengine umeshazisikia au utaendelea kuzisikia sana.
Kupata mamilioni ya shillingi ndani ya mwezi mmoja na kuacha maisha ya
ufanyaji wa kazi za kila siku ni mawazo yaliyovichwani mwa watu wengi
yawezekana na wewe mmojawapo.
Sasa hapa naenda kukusimulia baadhi ya hadithi hizo ambazo zipo sana
vichwani mwetu au tunaendelea kuzisikia kupitia platform hii ya forex;
HADITHI YA KWANZA
KUWEPO KWA NJIA(STRATEGY) BORA KUPITA NYINGINE.
Watu wengi wamekuwa wakijikita kutafuta njia ambayo itawetengenezea
hela kwa 100%. Ukimuuliza mtu yeyote mpya anaejifunza forex kama kuna
siri ambayo watu waliofanikiwa katika forex wanatumia, asilimia kubwa ya
majibu yao watakwambia NDIO.
Watu wengi wanafikiri traders waliofanikiwa wanatengeneza hela kila siku
kupitia njia/strategy fulani iliyo tukufu au nzuri kushinda zote. Kitu
ambacho sio kweli.
Hata traders waliofanikiwa huwa wanapoteza 30% ya trades zao kila
mwezi. tatizo ni kuwa trades wapya wanazichukia na kuzitupa trades zao
zilizowaingizia hasara.
Lakini traders waliofanikiwa hukubari kupoteza katika siku tatu na
wanabaki na msimamo katika mpango kazi/plan kwani mara nyingi huwa
ni long term trades na hata wanavokutana na hasara mwanzoni huamini
baada ya ule mda watakuja kupata faida yao.
Hebu jaribu kufikilia jambo hili. unavozungusha sarafu kuna uwezekano
wa kuanguka upande wa mwenge au upande wa kichwa kwa uwiano sawa.
Je, ukizungusha mara 100 utapata 50 kichwa na 50 mwenge? jibu ni
hapana. Lakini kama utazungusha mara 1000 au mara 10000 kuna
uwezekano wa kupata 50 kichwa na 50 mwenge.
Hiki ndicho nachotaka kukwambia kuhusu mpango wako wa kufanya
biashara ya forex. kama njia utayochagua kutumia ina ubora wa 60% basi
ifanye mara kwa mara kufikia au kukaribia hio 60% hata kama utapata
hasara mara kadhaa, lakini mwisho wa siku uwe upande wa faida
HADITHI YA PILI
FOREX NI MCHEZO WA 50-50
Watu wengi wanaamini kuwa forex ni mchezo wa 50-50, wanafikiri kuwa
soko litaenda juu au litaenda chini tu na kusahau kuna mda soko hucheza
katika eneo fulani. (consolidation)
Kwa nadharia hio tu ya kuwepo wa soko kucheza katika eneo moja tayari
sio mchezo wa 50-50, cha kufanya ni kufanya analysis zako kwa usahihi
zaidi.
HADITHI YA TATU
UNAWEZA KUTENGENEZA HELA KWA KUCLICK TU BUTTON
Hili ni jambo tunalolisikia sana kwa wenzetu na kufanya watu wengi
waingie katika forex wakidhani ni kitu rahisi sana kwa kubonyeza tu button
unapata fedha.
Asilimia 80 ya watu wanaojiunga katika forex hupoteza mitaji yao yote
ndani ya miezi mi3 ya mwanzo kwa kukosa maarifa na kutofanya mazoezi
ya vitendo mara kwa mara katika hii biashara.
Forex ni kama fani nyingine. Inahitaji kusoma, kufanya majaribia, kuifatilia
kwa karibu na kw juhudi ndipo uje utengeneze hela. imenichukua zaidi ya
miezi 6 kujifunza kuanzia february mpaka september mpaka kuja kuanza
kutengeneza faida.
HADITHI YA NNE.
UNAHITAJI NJIA/STRATEGY YA KISASA ZAIDI ILI UTENGENEZE FEDHA
KIURAHISI.
Hii ni hadithi ambayo ipo kwa traders walio wengi, wakiamini unahitaji njia
fulani ambayo ni bora kuliko zote, indicators bora au muunganiko wa
indicators nyingi ili uwe accurate.
Hata pale unapokuja kuwapatia njia rahisi wanaona kama ni upuuzi mtupu
na kuidharau. wanaamini njia iliyocomplicated ni njia bora kuupita zote.
lakini kiuhalisia traders wengi waliofanikiwa wanatrade kwa njia rahisi
sana na wengine hawatumii kabisa hata indicators.
Lakini nataka kukambia ubora wa strategy upo mikononi mwa mtu husika
atakaemake commitment na hio strategy. unaweza kuwapa watu wawili
strategy moja kisha mmoja akachoma akaunti na mwingine akafanikiwa
kupitia hio strategy.
Hii ni kwa sababu kila mtu anatrade na kuona vitu tofauti. kwa hio sio njia
gani ni nzuri bali ni jinsi gani utaichukua hio njia na kuiwekea mkazo
ndipo utakapofanikiwa.
2. AINA YA WAFANYABIASHARA KATIKA FOREX.
Hii ni eneo muhimu sana kulijua na wewe kufanya maamuzi unataka uwe
mfanyabiashara wa aina gani. Hivyo kabla hujaanza ni bora kujitathmini
wewe ni mfanyabiashara wa aina gani na utumie njia zipi katika kufanya
biashara yako.
1. SCALPER
Huyu ni mfanyabiashara anaekuwa katika soko kwa mda mfupi sana. Mara
nyingi anaingia na kutoka katika trade na dakika kadhaa tu. Kivutia
kikubwa kwa trader wa aina hii huona faida au hasara ndani ya mda mfupi
tu. Msingi mkubwa wa scalper ni kuwa na uwezo wa kufikiri haraka na
kuweza kumantain pressure. Kulingana na mda mfupi wa fursa scalper
huamua aingie katika hio fursa au aache.
2. DAY TRADER
Huyu ni trader ni yule ambae huingia katika trade siku husika na kutoka
katika trade siku hio hio.Tofauti na scalper, yeye huingia katika trade na
kuisubiri ndani ya dakika 30 au saa. Uzuri wa kuwa day trader ni mda wa
kutosha wa kufanya zako analysis. mara nyingi huwa na mda maalum wa
kuingia katika trades zake. Na mda ukifika wanasubiri fursa ijitengeneze
na kuingiza trades zao, hutumia dakika 30, saa moja mpaka saa 4
timeframe kufanya analysis zao.
3. SWING TRADER
hawa ni traders wanaofanya biashara kila siku.... kwa kua kila siku
kunakuwa na nafasi za mtiririko/swings katika soko. ukitokea mtririko wa
kupanda wanapanda nao.. ukitokea wa kushuka wanashuka nao. Hawa
wanafocus sana katika kuangalia mtiririko wenye asili ya uimara zaidi. na
mara nyingi hutokea katika kufunguliwa kwa soko la london (London open)
na New York open.Hawa wanafanana sana na day trader huwa wanaingia
na kutoka katika soko ndani ya siku husika
4. POSITION TRADER
Hawa huingia katika trade kwa siku kadhaa au week. Hii ni aina nzuri kwa
wale ambao hawana mda wa kuangalia chart kila siku.
Hawa pia tunaambiwa ni traders ambao wanachukua profit sana
ukizingatia wanakua kwenye market kwa mda mrefu hivo kuchukua faida
ya week au mwezi. Hivyo aina hii ni kwa wale wenye mitaji mikubwa
2. ENGULFING.
Hii hutokea pale ambapo candle ya pili imeizidi umbo na pin candlestick ya
nyuma katika eneo la RESISTANCE au SUPPORT. Tazama picha hapo chini
na maelezo yake.
3. HARAMI.
Hii hutokea ambapo candle ya kwanza imezidi umbo na candle inayofuata
mbele yake. Tazama picha hapo chini na maelezo yake
6. SHOOTING STAR.
Hii ni candle inayokuwa peke yake inayoashiria kugeuka soko kwenda
kuuza, hutokea eneo la RESISTANCE. Tazama picha hapo chini na maelezo
yake
7. INVERTED HAMMER.
Hii pia ni candle inayokuwa peke yake inayoashiria kugeuka kwa soko
kwenda kununua inapokuwa imetokea/imejitengeneza eneo la SUPPORT.
Tazama picha hapo chini na maelezo yake
8. HAMMER.
Hii ni candle inayokuwa peke yake ikiashiria kugeuka kwa soko kwenda
kuuza inapokuwa imetokea katika eneo la RESISTANCE. Tazama picha hapo
chini na maelezo yake
9. HANGING MAN.
Hii ni candle inayokuwa peke yake ikiashiria kugeuka kwa soko kwenda
kuuza inapokuwa imetokea katika eneo la RESISTANCE. Tazama picha hapo
chini na maelezo yake